google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 6, 2021

Njia mbili ziletazo mafanikio maishani.

No comments :

 

Katika kufikia mafanikio yoyote yale, huwa zipo njia za kuweza kufikia mafanikio hayo. Hakuna mafanikio ambayo yanapatikana nje ya njia husika za mafanikio.

Na kwa kawaida, zipo njia mbili bora za kuufikia mafanikio. Hizi ni njia halali ambazo zinatumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kweli na halali duniani.

Njia ya kwanza; Njia ya kawaida.

Hii ni njia ambayo mtu anafikia mafanikio makubwa kutokana na malengo anayoyafatilia kila siku. Hapa lazima uwe na malengo ya kuyafatilia kila siku.

Katika njia hii unakuwa na malengo yako, lakini wakati huo huo unakuwa unaenda nayo mdogo mdogo hadi kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Hii ni njia bora, inayoaminika, kwa sababu kuna kujifunza mengi ndani yake, ingawa inataka muda na uvumilivu, lakini mwisho wa siku utafika.

Njia ya pili; Njia isiyo ya kawaida.

Hii ni njia isiyo ya kawaida kwa sababu ndani yake kuna kuwa na hali hatarishi nyingi. Kwa mfano, kuna kuweka mtaji mkubwa ndani yake au kuchukua hatua kubwa kabisa.

Katika kutekeleza njia hii iko hivi, unakuwa unafata njia ile ya kawaida kama kawaida, isipokuwa katika njia hii kuna vitu ambavyo vinaongezeka.

Katika njia hii lazima utenge kiasi fulani cha pesa, ili kuingiza katika 'dili' ambazo zinajitokeza kati kati lakini wakati huo ukiendelea na njia ya kwanza.

Kufata njia ya pili hatumaanishi njia ya kwanza umeiacha, hapana unakuwa nayo,  isipokuwa hii unaitumia kama ziada kutengenezea pesa ndefu.

Hizi ndio njia kubwa mbili, ambazo zinatumiwa na watu wengi wenye mafanikio kuweza kufanikiwa. Ni muhimu kutumia njia zote mbili ili kujihakikishia mafanikio.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Oct 5, 2021

Zingatia Jambo Hili Sana, Litakusaidia Kufanikiwa.

No comments :

Inapotokea kuna kitu hukijui, kuwa mtu wa shukrani, kwa sababu umepata fursa nzuri ya kujifunza juu ya kitu hicho.

Inapotokea unapitia magumu katika maisha yako, shukuru pia, kwani magumu hayo yanakufanya uwe bora na imara.

Ikiwa pia unapitia changamoto sana, huo sio wakati wa kukimbia, bali ni wakati wako wa kujiboresha kimaisha.

Unapokuwa umechoka kwa sababu ya kazi, basi pia huo ni muda wa kushukuru, kwa sababu kuna mabadiliko umefanya.

Kama umefanya makosa, pia shukuru, kwa sababu hiyo inakukumbusha ni kipi ambacho hutakiwi tena kukifanya.

Ni rahisi sana kuwa na shukrani na mambo mazuri, lakini pia jifunze kuwa na shukrani hata kwenye changamoto.

Watu wengi si wepesi sana wa kushukuru pale wanapokutana na magumu. Ni watu ambao wanakuwa hawaoni zuri lolote.

Kipo kitu chanya au kizuri unaweza kukiona pia kwenye changamoto. Usilalamike, jifunze kupitia changamoto yako.

Yapo mafanikio na  baraka ambazo zimejificha kwenye changamoto. Unatakiwa uyaone mafanikio hayo.

Changamoto unazopitia zina uwezo wa kukufanya, ujifunze, ukue na kuwa jasiri wa kufikia mafanikio yako.

Zingatia, mafanikio yako utaendelea kuyapata kama utakuwa mtu wa shukrani katika kila eneo la maisha yako. 

Kuwa na shukrani ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Anza leo kuwa mtu wa shukrani, utafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Oct 4, 2021

Mawazo Kumi (10) Yatakayokupa Nguvu Kubwa Yakufikia Mafanikio Yako.

No comments :
Mafanikio siku zote yanaanza na mawazo. Kama hakuna wazo sahihi ieleweke pia hakuna mafanikio sahihi ambayo yataweza kuchipua kwa nje, sana sana  utakuwa ni mtu wa kushindwa kila wakati. Kupitia makala haya utajifunza mawazo muhimu yatakusaidia kuweza kufikia mafanikio yako. Karibu na twende tujifunze;-
1. Usifanye maamuzi kwa muhemko kwani utaahirisha tu, ni wachache wanaofanikiwa na maamuzi ya muhemko. Kwa mfano, utakuta mtu kasikia habari kwamba biashara ya aina fulani inalipa, mtu huyo utakuta anakurupuka na kujikuta kwenye wakati mgumu sana wa kuweza kushindwa. Kabla hujafanya maamuzi, tafakari kwanza.
2. Usitake mafanikio kama unavyotaka wewe. Mafanikio yana njia yake na misingi yake pia. Kama unataka mafanikio kwa jinsi unavyotaka wewe na unategemea utayapata huo ni uongo hutaweza kuyapata. Futa njia, kanuni na miiko ya mafanikio inasema nini utafanikiwa. Ulikilazimisha kufanikiwa kama unavyotaka wewe, haitawezekana.
3. Usikae tu na kusubiri mambo yatokee, utajichelewesha sana. Amua kupambana kufanya mambo yaweze kutokea na hiyo itakusaidia sana kuweza kufanikiwa. Kuwa mtu wa kulazimisha matokeo uyatakayo na uyapate. Kusubiri subiri tu mambo yajiendee, utajikuta unasubiri sana na mambo hayawi kama utakavyo, komaa.

4. Kama unaona maisha yako ni magumu sana, rudi kwenye mawazo yako, rudi na uende ukaanze kufikiri upya tena, maana ugumu wa kila kitu unaanzia kwenye akili na si kwingine tena. Inawezekana maisha yako ni magumu kwa sababu umeshindwa kuifikirisha akili yako vya kutosha, fikiri hili na chukua hatua.                                                                               
5. Kuwa tayari kwa wakati ufaao na wakati usiofaa kwenye maisha. Kuna wakati maisha yanakutaka uwe tayari hata wakati wewe unajiona hauko tayari iwe hivyo. Unatakiwqa uwe kama mwanajeshi kwa kuamua kufanya chochote kile na wakayi wowote ule ilimradi tu kuyafanya maisha yako yasogee mbele  na kuleta mafanikio yatakiwayo.
6. Fanya ufanyalo kwenye maisha yako, lakini hakikisha uwe una kitu cha watu kujifunza kwako. Usiishie kujifunza kwa wengine ila hakikisha watu nao wajifunze kwako kupitia wewe kama wewe. Fanya vitu ambavyo watu watakuiga na wakuone kwamba wewe ni mfano wa kuigwa na wakufate nakufanya maisha yao kuwa bora.
7. Ukiwa unafanya kazi, hakikisha uwe una kitu cha kuuza yaani una bidhaa ambayo unaweza ukawauzia watu na wakanunua kwako. Fanya ufanyalo lakini hakikisha uwe na pesa ya ziada, pesa hiyo ya ziada au akiba itakusaidia. Anza kuuza kitu ambacho kitakusaidia sana kuweza kukuza uchumi wako nje ya kazi uifanyao.
8. Kila mtu anaweza akawa na wasiwasi na wewe, lakini ukijitoa na kuamua basi kila kitu kinawezekana kwako na utafanya maajabu makubwa kwako. Jiamini kwamba unaweza ukafanya mambo makubwa maishani mwako hata kama hakuna mtu anayekuamini. Jiamini wewe kama wewe na utatoboa na kufikia mafanikio makubwa.
9. Weka juhudi sana kwa kila unachokifanya pasipo kuyumbishwa na wakati unaweka juhudi ili uweze kwenda mbele zaidi kubali kujifunza kwa kukosolewa. Bila ya juhudi, kukubali kukosolewa au kuelekezwa kwa usivyojua, hauwezi kwenda. Kukosolewa si dhambi, wewe kosolewa na kubali kujifunza na utafanikiwa pa kubwa.
10. Kila jambo lifanye kwa wakati wake. Kama kwako upo kwenye muda wa kuwekeza, nikwambie tu wekeza sana na mtu asikutanie katika hilo. Usipoteze muda mwingi sana kwa kuwaza kwamba muda upo pale pale au unakusubiri, utapotea. Utumie muda wako kufanya yale yaliyo ya msingi na yale ambayo yatakusaidia kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Oct 3, 2021

Weka Umakini Wako Wote Kwenye Vitu Hivi Na Utafanikiwa.

1 comment :
Kila wakati zingatia kile kinacholeta mabadiliko sana kwenye maisha na unatakiwa kuachana na kile ambacho hakileti mabadiliko kwenye maisha yako. Kama unaendelea kufanya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwako huko ni kujipoteza.
Kwa maana hiyo, kama kuna kitu unataka kukifanya unatakiwa ujiulize je, kitu hiki kina mchango kiasi gani katika kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kama unaona kitu hicho hakina machango wowote ni jukumu lako kuweza kuachana nacho mara moja.
Kila wakati weka nguvu zako, muda wako na umakini wako wote kwenye vile vitu ambavyo vinaleta matokeo kwako ya mafanikio tu. Haina maana kupoteza nguvu zako nyingi kwa kufanya kitu ambacho hakina msaada kwako, utakuwa unapotea sana.
Kila wakati ijaze akili yako  mawazo chanya yatakayokusaidia wewe kuweza kufikia ndoto zako. Kila wakati weka juhudi sahihi za kukusaidia kuweza kufanikiwa kwa kufanya vitu vinavyoendana na ndoto yako unayoitaka kuifanikisha.

Usijaribu kupoteza nguvu zako kwa kufanya mambo ambayo hayakusaidii kuweza kutimiza ndoto zako. Ishi kwa faida kwa kufanya mambo ambayo yanakusaidia kuweza kutimiza ndoto zako, kinyume cha hapo hutaweza kufikia ndoto zako.
Tatizo la watu wengi wanapoelekea kwenye kufikia ndoto zao, wanakuwa wanaweka umakini wao kwenye vitu ambavyo hata haviwasaidii. Kwa kufanya vitu hivyo watu hao ndio hujikuta wakipotea karibu kila wakati kwenye kufanikisha ndoto zao.
Ili uweze kufikia ndoto zako, fanya ufanyalo, lakini hakikisha unaweka umakini wako wote kwenye vitu vya msingi vinavyokusaidia kutimiza ndoto zako. Kwa kufanya vitu hivyo ni kweli ndoto zako utaweza kuzifikia hata kama unakutana na changamoto nyingi.
Usiendelee kusita, usiendelee kusubiri, kama unataka kufanikiwa weka nguvu zako zote kwenye mambo yanayoweza kukupa mafanikio. Kama nilivyosema watu wengi hawaweki sana nguvu zao kwenye mambo yaletayo mafanikio yao, zingatia hilo.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.


Oct 2, 2021

Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.

No comments :
Najua kila wakati tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali ambazo kimsingi zimekuwa zikikusaidia kwa namna moja ama nyingine katika kuulisha ubongo chakula ya akili. Au kwa maneno mengine elimu ambayo umekuwa ukiipata hapa imekuwa ikikusaidia kuzaliwa upya kifikra hatimaye kutimiza kusudio lako hapa duniani.

Lakini katika makala ya leo nataka tujikite katika masuala mazima ya mapishi. Najua utakuwa unashangaa vipi leo afisa mipango kuleta somo hili. Wala usishangae kila kitu ambacho unakiona katika dunia hii ni fursa.  Inawezekana kabisa ukawa hauna lengo la kupika aina hii cha chakula. 

Ila kutokana na ulichojifunza hapa kukusaidia kutoa elimu kwa watu wengine na wao wakalipa pesa au chakula hiki unaweza ukakipika katika sehemu mbalimbali kama katika sherehe mbalimbali na wageni waalikwa na wasio waalikwa wakafurahia aina hii cha chakula. 


Au unaweza ukapika aina hii ya chakula kwa ajili ya biashara kama vile kwenye mahoteli, migahawa na sehemu nyinginezo.

Hebu tuangalie mahitaji kwa ajili ya kupika aina hii cha chakula. 

1. Tambi 1/2 paket
2. Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
3. Vitunguu swaumu kijiko 1 cha chakula
4. Carry powder kijiko 1 cha chai
pilipili hoho 1
5. Njegere zilizo chemshwa 1/2 kikombe
6. Mafuta ya kupikia kiasi
7. Chumvi kwa ladha upendayo

MAANDALIZI YA CHAKULA HIKI

a) Chemsha maji yachemke haswaa, tia chumvi na mafuta kiasi, weka tambi katika maji yaliyo chemka ziache ziive kiasi; kisha chuja maji na uziache kavu.

b) Chukua bakuli pasua mayai kisha weka pembeni.

c) Chukua kikaango kilicho safi weka jikoni tia mafuta kiasi na utaendelelea kuweka vitunguu maji,vitunguu swaumu,hoho ,karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo mdogo na havitakiwi kuiva sana.

d) Kisha tia tambi na njegere katika mchanganyiko wako na uendelee kukaanga kwa dakika kadhaa.

e) Chukua mayai tia katika tambi ongeza moto kiasi, ili tambi zako zichambuke ,moto hautakiwi kuwa mdogo sana ikiwa moto ni mdogo tambi zako zitashikana na kutia mabonge , mayai ya kiiva hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mpaka kufikia hapa chakula chako kitakuwa tayari kwa ajili ya kuliwa, chakula hiki wakati wa kula unaweza ukawa unashushia na juisi ambayo unayopendelea kunywa. 

"Mwili hujengwi kwa mawe bali hujengwa kwa kula"
 Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya. 

Oct 1, 2021

Hiki Ndicho Kitu Kinachokuzuia Kufanya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Ikiwa kila wakati unajaribu kufanya mabadiliko ya kitu fulani na unashindwa kuleta mabadiliko hayo, basi tambua maumivu ya kushindwa hayajawa makubwa sana ndani yako hadi uweze kuleta mabadiliko hayo.
Kwa mfano, unataka kuwa na mtaji na unashindwa kila mara, basi elewa kabisa maumivu ya kushindwa kupata mtaji hayajawa makubwa vya kutosha. Tuchukulie leo hii, ukaambiwa usipokuwa na mtaji hadi mwaka huu unaisha, utapigwa risasi.
Jiulize utakubali kufa kwa sababu ya kukosa mtaji huo unaoutaka? Bila shaka haitawezekana, utafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo. Hivyo, wakati mwingine mabadiliko yanakuja kwenye maisha yako kwa sababu ya kule kuumia sana.

Wakati ulipokuwa shule ulisoma sana na kuhakikisha unafaulu ili kukwepa maumivu ya kufeli. Pia kuna wakati umeweka juhudi nyingi sana ili kukwepa maumivu ya aina fulani na kutafuta mahala sahihi kwako.  

Tunaambiwa kitu chenye nguvu ya kubadili tabia yako na mafanikio ni maumivu. Waulize wote ambao wamefanikiwa na ambao wanafikiri chanya kuhusu mafanikio, watakwambia maumivu yamewasaidia sana kubadilika na kuweza kufika hapo walipo mpaka leo.
Kitu kinachokuzuia wewe kufanya mabadiliko kwenye maisha yako ni maumivu, hujawa na maumivu ya kutosha kuweza kubadilisha maisha yako. Ikiwa utakuwa na maumivu hayo, hutakubali, utafanya kila njia kubadilisha maisha yako.
Tunajua sote maumivu yanauma, kama maumivu yanauma, huwezi kukubali ukabaki na maumivu hayo kwako, lazima utatafuta njia ya kubadilisha maumivu hayo. Hivyo, kila wakati pambana kuweza kuleta mabadiliko juu ya maisha yako.
Mwisho kabisa niseme kwako hivi, utabadili maisha yako, ikiwa utakuwa una uchungu na maumivu ya kutosha, maumivu ya kuchoshwa na hali mbaya uliyonayo na kutaka kubadili maisha yako kabisa, hapo mabadiliko utayaona.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE.


Sep 30, 2021

Njia Pekee Itakayokufanya Ukawa Hodari Ni Hii…

No comments :
Kuna watu ambao huwa wanatamani sana, wawe hodari katika jambo fulani. Watu hao hufika mahali hata kuwatamani watu ambao ni mahodari katika maisha yao na kujiuliza wamefikaje huko kwenye uhodari huo.
Nikwambie, ipo njia moja kubwa ya kukufanya ukawa hodari kwa kile unachokifanya, njia hiyo si nyingine bali ni kufanya kitu hicho kila siku bila kuacha. Kama utafanya jambo hilo kila siku na kwa njia tofauti za kujifunza basi utakuwa hodari.
Unapofanya jambo hilo kila siku, unatengeneza uhodari mkubwa sana ndani yako na mwisho wa siku unajikuta ni mshindi katika hilo eneo. Ukiwa unafanya jambo na kuliacha, huo uhodari utaupoteza tu.


Jiulize unataka kuwa hodari katika jambo lipi? Ukishapata jambo hili ambalo unataka kuwa hodari, anza utekelezaji wa kulifanya jambo hilo kila siku na kwa juhudi zote. Usijaribu kufanya na halafu ukaacha, hautaweza kuujenga uhodari kwa namna hiyo.
Watu wenye mafanikio, watu ambao unawaona wamefanikiwa, wamekazana kujenga uhodari kwa kuchagua kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu na si kugusa gusa na kuacha halafu ukategemea ukawa hodari.
Angalia maisha ya wanamichezo walio hodari ni kipi wanachokifanya, angalia maisha ya wajasiriamali wakubwa ni kipi wanafanya, utagundua ni watu ambao wameamua kuweka nguvu zao kwenye jambo moja kwa muda mrefu na kutengeneza uhodari.
Acha kuwa na ndoto za kukurupuka na kusema kwamba unataka kuwa hodari, unataka kufanikiwa sana na halafu kitu hicho unachotaka kukifanya hukifanyi kila siku. Kama haufanyi kila siku sahau mafanikio hayo unayoyataka.
Kama wewe ni mwimbaji, hebu imba kila siku. Kama wewe ni mwandishi, hebu andika kila siku, kama wewe mchoraji, chora kila siku na fanya hivyo kwa miaka kumi, na huku ukijifunza tuone kama hujawa hodari.
Ukiona vya elewa ujue vimeumbwa, hivyo ndivyo wahengfa walivyosema na hawakukosea hata kidogo. Na vivyo hivyo ukitaka uhodari, acha kujidanganya, kaza buti na fanya kila siku jambo lako litakupa mafanikio tu.
Hakuna uchawi wala muujiza kwenye kutafuta uhodari. Ule uhodari unaoutafuta kila wakati upo kwenye kufanya kila siku na tena ikiwezekana unaamua kufanya maisha yako yote pasipo hata kukwama mara moja, ukifanya hivyo nakwambia utafanikiwa.
Kumbuka, uhodari unakuja kwa wewe kuamua kufanya jambo unalolitaka kila siku. Amua leo kuutafuta uhodari wako mpaka watu washangae, kumbe siri kubwa ya uhodari huo inakuwa imejificha kwa wewe kuamua kufanya kila siku.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNERS, kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,


Sep 29, 2021

Sababu Nne (4) Kwa Nini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine.

No comments :
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la watu linalalamika kwamba maisha yamekewa magumu. Kwa sababu hii pia watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kuona maisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradi siku ziende.
Malalamiko ya maisha kuzidi kuwa magumu yamekuwa yakisikika sana karibu ulimwenguni kote. Na kwa hili  hiyo imekuwa ikipunguza raha ya kuona ‘utamu’ wa maisha halisi. Si vijana wala wazee kila mtu amekuwa akisema lake juu ya ugumu wa maisha.
Lakini pamoja na malalamiko hayo, kitu ambacho tunatakiwa tujiulize nini kinachopelekea kuwe na ugumu wa maisha kila kukicha? Makala haya ya leo inakwenda kukupa majibu kwa nini  maisha yanakuwa magumu kwa wengi zaidi.

1. Kutegemea chanzo kimoja cha mapato.
Kutokana na maisha kubadilika na gharama za maisha kupanda karibu kila siku, suala la kutegemea kipato kimoja, ni moja ya chanzo cha maisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemea kipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.
Kwa bahati mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo ya maisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tu ugumu wa maisha uonekane. Hata siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kama bado una kipato kimoja.
2. Watu wengi wanafanya vitu wasivyovipenda.
Maisha ni magumu pia kwa watu wengi chini ya jua kwa sababu wamekuwa ni watu ambao kila siku wanafanya kazi ambazo wasizozipenda. Kama unafanya kazi usiyoipenda, unategemea nini, lazima maisha yatakuwa magumu tu.
Kufanya kazi usiyoipenda, kwa kawaida kunakuwa kunakuchosha sana na unakuwa unaifanya tu, kwa sababu eti upate pesa ya kula. Kama umechagua maisha hayo, ujue kabisa maisha hayo yatazidi kukufanya wewe uyaone magumu kila kukicha.
3. Watu wengi wanaishi juu ya matumizi.
Ugumu wa maisha pia kwa namna moja au nyingine unachangizwa na watu kuishi juu ya matumizi au vipato vyao halali. Unatakiwa kuelewa watu wengi, wanaishi juu ya matumizi kwa sababu ni watu ambao wanataka waonekane wamefanikiwa.
Watu hawa wanakuwa wapo tayari wakope au wafanye lolote lile ili waonekane mambo yao yako safi. Kwa msingi huo wanakuwa wanajitengenezea maisha magumu ambayo wanashindwa kuyamudu kwa urahisi na matokeo yake kuongeza ugumu usio na sababu.
4. Hakuna anayejali sana maisha ya wengine.
Maisha ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa, ukilinganisha na zamani. Kwa sasa ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae nayo hadi utoke.
Kutokana na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumu wa maisha.
Mwisho, pengine ujiulize, je, maisha yanaendelea kuwa magumu kwako kila kukicha? Jibu unalo wewe, nimekupa walau sababu chache zinazoonyesha kwa nini maisha yanazidi kuwa magumu. Wewe unaamini nini, niwekee maoni hapo chini.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.






Sep 28, 2021

Mambo Ya kuzingatia Ukitaka Kufanikiwa Katika Masuala Ya Kifedha.

No comments :
Somo la fedha ni la muhimu sana kwa kila mmoja wetu, hii ni kwa sababu tunashindwa kupata au kudumu katika mafanikio yetu kifedha hii ni kwasababu wengi wetu hutuna uelewa wa kutosha katika suala la kipesa.

Wengi hatuelewi namna ya kupata pesa na namna ya kuzifanya pesa hizo ziendelee kuwa upande wetu, Ila ukweli unabaki palepale siku zote kwamba, ukitaka kufanikiwa kifedha na kufika mbali, unalazimika kujua mambo haya yafutayo;-


 1. Jinsi ya kutawala pesa zako.

Katika maisha yako yote unatakiwa kuwa mtalawa wa fedha zako na sio fedha zikutawale wewe. Wapo wengi wetu wanashindwa kufanikiwa kimaisha  hii ni kwa sababu fedha zimewatawala wao, yaani unaweza ukaona mtu kapata fedha lakini atataka kila kitu nachoikiona akinunue, huku ndiko kunakoitwa kutwaliwa na fedha.

Nini kifanyeke?

Jambo muhimu la kuzingatie ni kila mmoja wetu ahakikishe hatawaliwi na pesa ila yeye ndio anayezitawala pesa hizo. Wewe ndiye unayekuwa na maamuzi sahihi juu ya kuzitumia pesa hizo na si vinginevyo.

2. Jinsi ya kutoka kwenye madeni.

Wakati mwingine madeni ni njia nambari moja imfanyayo mtu awe maskini kama hatakuwa makini mtu huyo, japo wapo baadhi ya watu, wao huamini ya kwamba mfanyabiashara wa kweli haogopi madeni, huko ni kujidanya. Kama una mkopo au madeni ni bora ukawa nayo yale ya biashara zaidi lakini si kwa ajili ya matumizi.

Nini kifanyike?

Hivyo ndugu yangu unatakiwa kuelewa ya kwamba madeni ni mabaya sana hasa ukiwa na hulka ya kujiendekeza katika michezo hii, hivyo kila wakati ili uweze kuwa na uhuru wako binafsi hususani katika uhuru wa kipesa unatakiwa kuondokana na madeni hayo mara moja, kwani madeni ni mabaya sana.

3. Jinsi ya kuongeza kipato.

Mara zote ukitegemea mfereji mmoja kama chanzo chako cha kipato basi fahamu fika maisha yako yatakuwa ni yale yale kila wakati. Ni lazima uwe na njia nyingi za wewe kuweza kukuingizia kipato ili njia hizo zikusaidie kuweza kupiga hatua. Kama una njia moja tu ya kipato, sahau kuwa huru kifedha.

Nini kifanyike?

Jambo la muhimu unalotakiwa kulikumbuka hapa ni kwamba kila wakati ni lazima uwaze kuongeza njia mbadala ya kuongeza kipato chako, na miongoni mwa njia zitakazokusaidia kuwa hivyo ni kuongeza wigo wako wa kutafuta pesa.

4. Jinsi ya kuweka akiba na jinsi ya kuwekeza kwa ajili ya baadae.

Wakati mwingine hatufahamu lile litakalojitokeza siku ya kesho hii ni kwa sababu kesho si rafiki kwetu ila tunaamini siku hiyo ipo, kama tunaamini hivyo basi tunatakiwa kujifunza kuweka akiba kwa ajili ya uwekezaji wa kesho.

Uwekaji wa akiba ni mzuri hii ni kwa sababu miongoni mwa faida itokanayo na kuweka akiba ni kwamba inasadia kutatua changamoto husika kwa muda muafaka hasa unapokuwa haupo vizuri katika suala la kifedha.

Unachotakiwa kufanya?

Ni kuhakikisha kwa kila kipato unachopata unatenga asilimia kadhaa kwa ajili ya akiba hii ni kwa sababu hatujui  likalotokea siku ya kwesho na pia ni faida kuweka akiba kwa sababu itakusaidia kuwekeza.

Hayo ndiyo mambo ya msingi unayaopaswa kufahamu kuhusu fedha.

Ndimi Benson Chonya.

Sep 27, 2021

Silaha Kubwa Ya kufikia Mafanikio Yako Ni Hii.

No comments :

Kati ya kitu muhimu sana cha kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Kati ya silaha kubwa ya kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Unapokuwa na akili ya utulivu inakusaidia kuona mambo mengi, na kufanikisha mambo mengi pia. 

Si rahisi sana kuweza kufanikiwa sana kama akili yako haijatulia. Unatakiwa ujue, silaha yako kubwa ya mafanikio ni matumizi ya akili yako na wala si bahati au muujiza kama uwazavyo.

Akili yako ina uwezo wa kukupa matokeo makubwa sana kama imetulia, hapa inaweza ikakupa majibu mazuri na ikaleta matokeo ya kushangaza ambayo huwezi kuyaamini.

Hivyo, unatakiwa kila wakati kuchagua mazingira tulivu yatakayoifanya akili yako ifanye kazi kwa utulivu. Unatakiwa kuishi na watu sahihi, wasio na makelele kwako.

Lakini si hivyo tu, unatakiwa kuishi na mke au mume sahihi kwako asiye na makelele. Unatakiwa kuishi na mwenzi wako ambae anaifanya akili yako itulie na isiwe ya vurugu.

Amani ya akili, utulivu wa akili, ndio chanzo cha mafanikio makubwa yote na yakutisha. Hakuna ambae aliyefanikiwa huku akili yake ikiwa haijatulia, mtu huyo hayupo.

Waangalie vizuri watu waliofanikiwa, utajifunza kitu kimoja kwao ni watu ambao akili zao zimetulia. Unasema nimejuaje, angalia jinsi wanavyoongea, wanaongea kwa utulivu mkubwa sana, hiyo ni ishara akili zao zimetulia.

Ili kufukia mafanikio yako makubwa, haina haja na maana kuishi na watu au katika eneo ambalo linakunyima utulivu wa akili. Jiulize, ya nini kuishi na mpenzi ambaye anaifanya akili yako isitulie na kuanza kumwaza yeye. Tafuta utulivu wa akili utaona matokeo yake makubwa jinsi utakavyo yapata.

Unapokuwa na utulivu wa akili inakusaidia sana wewe kupangilia mambo na mikakati yako kwa ukamilifu, tofauti na ambavyo ukikosa utulivu akili yako haiwezi kuwaza kitu cha maana na kukupa matokeo makubwa. 

Zingatia sana, utulivu wa akili, ni silaha ya kwanza katika kufikia mafanikio yako. Kila siku, jitahidi, utafute eneo lilotulia na tafakari maisha yako, na utaona matokeo mazuri yakija kwa upande wako. 

Unatakiwa ujue, silaha kubwa katika kufikia mafanikio yako ni utulivu wa akili. Ukituliza akili zako, utafanya mambo makubwa sana na ya kushangaza wengi na pia wengi hawataamini je, kweli ni wewe. Kumbe siri, ipo kwenye kutuliza akili, basi.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Sep 26, 2021

Chagua Mwendo Upi Unakusaidia Kufanikiwa.

No comments :

Kuna wakati unaweza ukakamilisha mambo mengi sana, kama utaamua kwenda kwa taratibu. Unatakiwa usikimbize mambo yako, ila unatakiwa kwenda taratibu na kufanya kwa uhakika na ufanisi mkubwa wenye faida. 

Kwa mfano, kama kuna majukumu ambayo unayafanya kila siku, basi, majukumu hayo yafanye kwa utaratibu, kwa utulivu mkubwa na utajikuta unakamilisha mambo mengi ambayo hukutegemea.

Kuna watu wanafikiri ili kukamilisha mambo mengi unatakiwa kwenda kwa haraka zaidi, kitu ambacho si kweli. Unaweza kwenda taratibu na ukakamilisha mambo mengi, unaweza kwenda haraka halafu ukaharibu.

Ni wajibu wako unatakiwa ujue ni wakati upi unatakiwa uende taratibu na wakati upi unatakiwa uende haraka. Si kila wakati wa kwenda kwa haraka ikiwa utafanya hivyo huwezi kukamilisha mambo mengi zaidi unajiharibia wewe.

Kama nilivyosema, kwenda haraka hakuwezi kukusaidia kukamilisha mambo mengi kwa sababu, akili yako inakuwa haijatulia yaani inayumba yumba. Kama akili yako inayumba hivyo, kufanikisha mambo mengi ni ndoto.

Unatakiwa kila wakati kujiuliza, hapo ulipo ni wakati wa kwenda haraka au wakati wa kwenda kwa kasi. Kisha ukishapata majibu, fanya uamuzi sahihi. Maisha sio mashindano na wengine, angalia mwendo wako.

Hapa ndio upo ule umuhimu wa kuchagua mwendo upi unakusaidia kukamilisha mambo mengi. Je, mwendo wa kasi au mwendo wa taratibu, lakini kaa ukijua kila mwendo una sehemu yake.

Suala hili, lipo kama vile unavyoendesha gari. Si kila wakati unatakiwa kukimbiza gari, yapo mazingira yake. Na kwenye maisha iko hivyo hivyo, kuna wakati wa kwenda kwa haraka na wakati wa kwenda taratibu.

Kufanikiwa kwako kunategemea sana uchaguzi wako wa mwendo upi uutumie na katika eneo lipi. Fanyia kazi hili, na utaona matokeo makubwa kwa upande wako.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Sep 25, 2021

Mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kufanya uwekezaji.

No comments :

Ipo hivi unapofanya uwekezaji katika jambo lolote unatakiwa kuelewa kwamba hakuna faida utakayoipata papo hapo. Bali uwekezaji huchukua muda fulani mpaka uje uone uwekezaji wa jambo hilo.

Wengi wanapoambia wawekeze katika jambo fulani hukurupuka katika kuwekeza mwisho wa siku hujikuta wanapata hasara au kutokuona faida ya uwekezaji waliofanya.

Kitu pekee ninachopaswa kukumbusha ni kwamba unapotaka kuwekeza katika jambo fulani, unatakiwa kuzingatia mambo haya machache;

·        Uwekezaji unakutaka uweze kulielewa jambo unalotaka kuliwekeza kwa undani zaidi.

·        Faida ya uwekezaji  huchelewa sana kuonekana.

·        Uwekezaji huitaji uvumilivu mkubwa ndani yake.

·        Uwekezaji unahitaji umakini wa hali ya juu ili kuepukana kupata hasara ya jambo husika.

Hivyo ni vyema ukayazingatia hayo machache kati ya mengi kabla hujaamua kuwekeza katika jambo lolote lile ulitakalo.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.

0757-909942

 

Sep 24, 2021

Jinsi Ya Kupata Wazo Bora La Biashara.

4 comments :
Kisaikolojia kila mtu ana mawazo bila kujali ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine binadamu huwa na mawazo mazuri ambayo kama atayaendeleza na kuyafanyia kazi yanaweza kubadili kabisa maisha yake.

Mawazo humfanya mtu awe alivyo, aonekane vile anavyoonekana. Mwenye akili, mpole, mkorofi,mwema au mkatili. Haya yote ni matokeo ya mawazo aliyonayo mtu kichwani mwake.

Kila siku tunasikia watu wanasema nina pesa ila sijajua nifanye biashara au mradi gani. Wakati mwingine utasikia mtu akisema nina wazo zuri la kufungua biashara au mradi tatizo langu mtaji sina.

Katika kuwaza kwao watu hawa mwisho hujikuta muda umeenda, umri umesonga bila hata kutekeleza wazo moja alilopanga. Mwenye pesa amekaa na pesa hadi  imekwisha kwa kutatua matatizo ya aina mbalimbali.


Mwenye wazo kawaza mpaka kawazua mtaji hana na wazo limechina mwisho anakata tamaa na kuamua kufanya kazi asiyotaraji kuifanya ili kujikimu na mahitaji ya kila Siku katika maisha.

Ni Kitu gani kifanyike ili watu hawa waweze kufanikiwa? Mwenye wazo na mwenye pesa? usiumize kichwa Kisuda nitakupa siri yake leo. Kabla sijaeleza namna gani ufanye nikudokezee siri moja muhimu katika mafanikio.

Tafuta wazo sahihi la kukufanikisha.
Ili mtu yeyote iwe mimi au wewe uweze kufanikiwa unahitaji vitu vinne.

1. MAARIFA/UJUZI juu ya jambo unalotaka kufanya.

2. WAZO BORA NA  ZURI la kukuongoza hatua kwa hatua lenye taarifa sahihi juu ya mradi au biashara husika.

3. WATU WAZURI wa kushirikiana nao. Hakuna kazi au mradi unaoweza kuufanya peke yako ila kushirikiana na watu. Hivyo ni lazima upate watu makini na sahihi wa kushirikiana nao.

4. MTAJI /PESA ya kuanzishia mradi lakini zingatia kuwa pesa si chochote katika mradi au biashara hata uwe na mamilioni ya shilingi kama huna hivyo vitu vingine wazo,maarifa na watu sahihi sahau kuhusu MAFANIKIO utaangukia pua tu.
Kisaikolojia  pesa haileti mawazo, bali mawazo ndiyo huleta PESA. Na hii ndio Imani yangu na falsafa yangu Kisuda  katika maisha yangu ya mafanikio.


Sasa nitoe njia 5 za kuweza kukusaidia wewe rafiki yangu katika kupata wazo la biashara ili uweze kufanikiwa kirahisi kwa wewe mwenye pesa na mwenye wazo:-

1.Tafuta uhitaji wa watu/ tatizo linalowasibu watu kisha tafuta namna ya kuwatatulia shida /tatizo lao utapata pesa nyingi sana.

2. Boresha wazo la mwingine. Hapa ni kuangalia tu mapungufu ya mtu katika kazi au biashara halafu una boresha utendaji kazi na utaona mabadiliko makubwa katika kazi au biadhara yako. Kamwe usiige wafanyavyo wengine utapata matokeo yaleyale wapatao wao badili njia.

3. Hamisha wazo kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hapa na maanisha ukiona mradi au biashara sehemu si lazima nawe ukafanyie pale unaweza anzisha wazo kama hilo sehemu tofauti na ukafanikiwa sana.

4. Rahisisha mchakato au upatikanaji wa huduma au bidhaa fulani badala ya watu kuifuata sokoni au mjini wapelekee wewe nyumbani kwao watakulipa pesa nyingi na gharama ya usafiri kwa nini wakulipe? Umewaokolea muda wao ili wafanye mambo mengine na pia wamepata wanachotaka kwa wakati.

5. Tengeneza uhitaji kwa watu. Hapa ni kubuni Kitu cha ziada ambacho watu wanakihitaji lakini kutokana na muda au umbali wanaona kama hakina umuhimu sana kwao. Mfano simu za mkononi zimekuja baada ya barua kuonekana kuchelewa kuwafikia wahusika leo hii taarifa ya dakika 10 imeshasambaa nchi nzima.

Haya sisi wataalamu tunaita ni kutengeneza mahitaji ya ziada kwa watu ili wakulipe pesa. UWEZO WAKO WA KUJA NA MBINU AU WAZO JIPYA TOFAUTI NA MAZOEA YA WATU NDIO CHANZO CHA MAFANIKIO YAKO.

Ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO na endelea kujifunza hapa bila kuchoka.