google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 30, 2019

Ongeza Uwezo Wako Wa Kupata Pesa Kwa Kufanya Mambo Haya.

No comments :
Upo uwezekano mkubwa wa wewe kuongeza uwezo wako wa kupata pesa zaidi ya hapo ulipo ikiwa utafuata misingi sahihi ya pesa jinsi inavyotaka. Kila kitu kina kanuni zake ikiwamo hata kanuni za kupata pesa.
Kama bado unashangaa kwa nini wengine wana pesa nyingi na wewe huna, hiyo yote ni kwa sababu wanazifanyia kazi kanuni za pesa bila kujali wanazitumia kwa bahati mbaya au kwa kujua.
Huna haja ya kuendelea kukosa pesa kila wakati. Umefika wakati wa kukubali kujifunza na kutumia kanuni za pesa ili zikusaidie kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kufanikiwa maishani mwako.
Kupitia makala haya, naomba nikuachie dondoo kadhaa zitakazoweza kukusaidia moja kwa moja kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kuwa mtu wa mafanikio. Karibu tujifunze kwa pamoja;-
1. Jifunze mambo ya pesa kila siku. Jifunze kwenye vitabu, pia jifunze kwenye semina. Huwezi kufanikiwa kipesa kama hujachukua hatua za kujifunza jinsi pesa inavyofanya kazi.
Unalazimika kujua jinsi pesa inavyoweza ikawekezwa na kudumu katika maisha yako. Yote haya hayawezi kuja kwenye upande wako kama uchawi bali ni kwa wewe kuweza kujifunza.

Ongeza uwezo wako wa kupata pesa kila siku.
2. Tafuta mshauri (Mentors) atakayekuwa anakuongoza kwenye mambo yako ya pesa pale unapokwama au unataka kusonga mbele zaidi. Hili linaweza kuwa jambo ni dogo kwako lakini ni muhimu kwako.
Watu karibu wote ambao wana mafanikio kila siku wana watu ambao wanawafuata au wanawashauri kila mara katika mambo ya pesa. Hali hiyo hupelekea kuwaweka juu kimafanikio.
3. Kama upo kwenye madeni, tafuta namna ya kuondoka huko. Madeni  ni sumu kubwa ya mafanikio kama utakuwa nayo kwa muda mrefu. Kama una madeni mengi, upo uwezekano wa nidhamu yako ya kipesa ikawa mbovu.
Weka mpango imara ambayo itaweza kukutoa kwenye madeni na kuanza kuishi kwa uhuru wa kifedha. Hutaweza kufika mbali kimafanikio ikiwa kila wakati ni mtu wa kudaiwa, hutaweza kufanya kitu chochote.
4. Jilipe wewe kwanza kila ukipata pesa yoyote ile. Kila aina ya pesa unayoipata, tenga kiasi kidogo na ujilipe kama mtafutaji wake. Usiache kujilipa hata kama pesa uliyopata ni kidogo.
Pesa ile ambayo utakuwa unajilipa wewe kwanza, huna haja ya kuwa nayo na haraka kuitumia. Kama ambavyo tumekuwa tukisema iache iwe nyingi baada ya hapo iwekeze.
5. Tafuta namna pesa zako zitakavyoweza kukulinda pale unapokuwa umeumia au kufa na kuacha watoto wadogo. Kuwa na ulinzi wako kama bima vile, lakini wewe bima yako inaweza ikawa  pia vitega uchumi vyako mbalimbali.
Hapa unatakiwa ujifunze kuwekeza mapema wakati bado ukijana mwenye nguvu. Kwa kadri jinsi unavyozidi kuwekeza pesa zako zitakulinda hata pale utakopokuwa umeshazeeka au kupatwa na matatizo yoyote.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuongeza uwezo wako wa kupata pesa kama utazingatia mambo hayo matano kama yalivyowekwa wazi kupitia makala haya. Naamini umejifunza kitu na chukua hatua.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa na tupo pamoja.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Jan 28, 2019

Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kukuongoza Kwenye Safari Ya Ujasiriamali Na Kukupa Mafanikio Makubwa.

No comments :
Kila mtu anatamani biashara anayoifanya ifanikiwe, kila mtu anatamani akiingia kwenye ujasiriamali mambo yake yanyooke sana na yawe ya mafanikio makubwa. Hiki ndicho kitu ambacho watu wengi sana wanapenda kiwe kwenye maisha yao.
Hata hivyo uelewe hivi, unapochagua kuingia kwenye biashara, ujue kabisa umechagua  kabisa kuingia kwenye ulimwengu wa wapambanaji haswa, yaani ulimwengu wa ujasiriamali. Hivyo, unapoingia kwenye dunia ya  ujasiriamali kuna mambo lazima uyajue kwanza.
Pasipo kuyajua mambo haya, nakuhahakikishia kabisa, utakwama sana na itafika mahali utajiona wewe si kitu na si lolote. Pengine jiulize, mambo hayo ni mambo gani ambayo yatakusaidia kukuongoza kwenye safari ya ujasiriamali na kukupa mafanikio?

1. Tambua jinsi ya kukabiliana na hali yoyote ile.
Unapoinguia kwenye biashatra na huku ukaingia na mawazo ya aina moja tu kwamba mimi naenda kupata, basi utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu sana. Kwa kuwa umechagua kuingia kwenye biashara ujie kabisa kuna kupata na kukosa.
Inapotokea umepata unashukuru Mungu, lakini inapotokea umekosa pia unashukuru Mungu kwa matokeo hayo na kuchukua uamuzi wa kusonga mbele.  Usiingie kwa akili ya kupata moja kwa moja utapotea.
2. Tambua kuna hali hatarishi.
Zipo hali hatarishi nyingi sana au ‘risk’ hasa pale unapochagua kuingia kwenye ulimwengu wa biashara. Hali hizi hatarishi unatakiuwa kupambana na kukabiliana pasipo na hofu yoyote kwani kwa kuzishinda huko ndiko unafanikiwa.
Kama umeamua kuingia kwenye biashara  au ujasiriamali na ukawa mwoga na hali hiz hatarishi basi utakuwa unapotea. Kwa kujua kuna hali hatarishi basi itakuwa ni njia sahihi ya namna ya wewe kuongozwa kwentye njia ya mafanikio ya ujasiriamali wako.
3. Tambua kukabiliana na hofu.
Wale wanaofanikiwa si kwamba ni watu ambao hawana hofu kabisa, ni watu ambao wana hofui kama wewe ila wanaamua kukabiliana na hofu zao hivyo hivyo pasipo kujali nini kinaendelea ndani mwao juu ya hofu hizo.
Hata wewe unaweza kukabiliana na hofu hizo hivyo hivyo kila siku. Kuna wakati utakutana na mambo yatakayokuwa  magumu kwako lakini unatakiwa kujifunza jinsi ya kukabaliana nayo na uatafika wakati utakuwa mshindi kweli.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,



Jan 1, 2019

Acha Kuishia Hapa Tu, Fanya Mabadiliko Ya Kudumu Ya Maisha Yako.

No comments :
Leo ni siku ambayo watu wengi wanaamini wakati wa kufanya mabadiliko mapya umewadia. Kwani nini wanaamini iko hivyo ni kwa sabbau leo ni mwaka mpya, kwa hiyo imani ile ya kubadilisha mambo leo iko juu sana.
Kama unaamini hivyo kwamba kuna sehemu ulishindwa na huu ndio wakati wa kufanya mabadiliko kwako, tafadhari, fanya mabadiliko hayo na acha hata kidogo kuishia kati, kama ni mabadiliko hayo endelea kuyafanya maishani mwako kote na yasiwe ya kitambo.
Mabadiliko ya kweli katika maisha yako hayaji tu kwa sababu leo ni mwaka mpya, bali yanakuja kwa sababu unatakiwa kubadlili maisha yako haswaa na kila siku pasipo kusubiri kitu chochote cha nje ikiwa pamoja na msukumo wa nje.
Leo hii kama wewe mwenyewe umeamua kweli iwe siku yako ya mabadiliko, naomba uzaliwe upya kweli. Acha kuishia tu kusheherekea mwaka mpya na kusahau kufanya mabadiliko ya kweli na ya kudumu katika maisha yako.

Usiwe mtu ambae umejipa ‘ubatizo’ wa kuzaliwa upya na halafu kesho nikukute unarudia maisha yale yale ya zamani yanayokurudisha nyuma. Weka mikakati mizito ya kuamua kubadilisha maisha yako kweli na acha lelemama.
Kama umeamua kufanya mabadiliko ya kweli fanya kweli, acha utoto na acha kujirudisha nyuma kwa namna yoyote ile ambayo ni hatari kwa afya ya mafanikio yako. Jambo la kuzingatia sana kwako ni kuhakikisha lazima unasonga mbele .
Najau kwa miaka mingi umepitia makubwa ya kupanda na kushuka, lakini hiyo nikwambie tu inatosha, sasa ni wakati wako wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika maisha yako na mabadiliko hayo unaweza ukayaanza leo.
Asikuzuie mtu, kisikuzuie kitu, amua kufanya mabadiko ya kweli katika maisha yako na mabadiliko hayo yasiishie tu katika siku za mwanzo za mwaka bali yawe endelevu kizazi na kizazi hadi iwe kumbukumbu kwako kubwa na kudumu.
Ngoja leo nikupe baraka zote za kukutakia heri ya mwaka mpya, lakini mwaka huu uwe kweli wa mabadiko ya kudumu kwako na usiwe mwako ambao uwe wa majuto kwako tena kama ambavyo imekuwa pengine ikitokea.
Naamini hilo litafanikiwa kwako na Mungu atakubariki ikiwa utachukua hatua sahihi. Kama nilivyosema, acha kuishia kusheherekea mwaka mpya tu, bali amua kufanya mabadiliko ya kweli ya maisha yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,