google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 23, 2022

Ushauri Kwa Kijana Aliye Mtaani, Hana Ajira, Haoni Cha Kufanya.

No comments :

Kuna watu hawajui cha kufanya, yaani ni watu ambao hawajui wafanye nini ili walau waingize kipato. Kwa bahati mbaya watu hawa huwa ni wahitimu wa chuo kikuu na wengine ni watu wa kawaida. 

Hebu fikiria, inakuwaje kwa mhitimu wa chuo kikuu anakuwa hajui cha kufanya? Lakini hali hiyo ndio huwa ipo mtaani na ndio uhalisia wenyewe unakuwa uko hivyo. 

Angalia kile unachopenda, unajua kuchora, kuimba, kuigiza, kuchekesha, fanya hivyo na kisha waonyeshe watu kile ulichonacho na uachane na kulala.

Jifunze kutengeneza tovuti, jifunze kuendesha mitandao ya kijamii kibiashara, jifunze graphics na vitu vingine vingi vitakavyokulipa baadae.

Tumia simu yako kuuza vitu vya watu wengine. Unaweza kuongea na mtu mwenye duka ukawa unauza vitu mtandaoni kisha unapata asilimia kadhaa.

Ukiweza fanya udalali wa viwanja, nyumba, vyumba, vyombo na bidhaa zingine ila fanya kwa weledi mkubwa.

Kama unapitia hali hiyo usipate shida sana, ndio maana dirayamafanikio.blogspot.com ipo kwa ajili yako kukupa mwelekeo wa maisha. Kwa kuwa huna kazi, usilale mpaka saa tatu, badala yake fanya haya:-

Kipindi ambacho huna ajira na huna labda smartphone, unaweza kujifunza ujuzi mpya utakaokulipa zaidi kwa baadae.

Jifunze ufundi, namna ya kutenengeneza simu zilizoharibika, kutengeneza friji, pasi, tv au redio. Unaweza ukajifunza vyote au kimoja unachopenda.

Ongea na wafanyabiashara wenye maduka, ili hata uweke pesa kidogo rehani, kama laki moja, ili uwe unachukua vitu dukani kwao na kuviuza kwa mali kauli, visiponunuliwa unawarudishia vitu vyao.

Nenda sokoni toa uvivu na aibu, tafuta kitu kimoja uza, iwe ni mboga za majani, dagaa na hii itakuondolea uvivu na kukuonyesha fursa mpya.

Fanya umachinga, uza bidhaa ndogo ndogo, kama chaji, cover, protector, hapa mtaji unaweza kuanza na laki moja tu.

Kumbuka watu ni mtaji, hakikisha unafahamiana na watu muhimu. Hawa watakusaidia kupata wazo, mtaji au kushirikiana na wewe.

Wakati mwingine katika makala zinazokuja tutaangalia biashara unazoweza kuzifanya kwa mtaji mdogo. Kitu kikubwa na cha msingi, endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza kwa kina.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 22, 2022

WAZO LA KUJIAJIRI: Biashara Ya Vikombe Vya Chai Vyenye kubadili Rangi Vikiwekwa Chai Au Maji Ya Moto.

No comments :

Naam, wala usishangae najua tumezoea kunywa chai kwa kutumia vikombe hivi vya kawaida ambavyo havina kitu cha kushangaza pindi utuamiapo. Sasa katika wazo letu la kujiajiri tunakuleta wazo jipya ambalo kwa baadhi ya watu huenda likawa ni geni kabisa. Wazo hili si jingine bali ni vikombe vya udongo ambavyo hubadili mwonekano hasa pale vinapowekwa maji ya moto au chai.
Vikombe hivi ni vizuri sana ndugu yangu kwa sababu ya uimara wake lakini najua pindi utakapoamua kuifanya biashara ya vikombe hivi utawashangaza wengi sana na kiukweli utapata wateja wengi sana. Chukua sekunde chache wawaze mamantile waliopo mtaani kwako, usiishie hapo endelea kuwaza mahotel ambayo upo nayo karibu.
Endelea kuwaza wale watoto ambao hawapendi kunywa chai, vipi ukimpa mtoto huyo chai kwenye kikombe ambacho kitaonesha sura yake pamoja na jina lake bila shaka mtoto huyo hata kusumbua tena kwenye suala la kunywa chai na uji pia, kwa sababu mtoto huyo atashangaa majabu ya kikombe hicho pia hivyo atakunywa tu.
Endelea kuwaza kwa sauti ya chini, Vipi mumeo anaamka asubuhi kabla ya kwenda kazini anakuta umemuwekea maziwa kwenye kikombe kimeandikwa “ I love you Benson” na hilo ndilo jina la mumeo na akimaliza kunywa chai hiyo hayo maandishi yanatopea hadi kesho tena kikombe hicho kikiwekewa chai, bila shaka mumeo huyo atafarijika na michepuko haitakuwa  nafasi tena na utafurahia ndoa yako.
Kwa mifano hiyo michache utaona ni kwa namna gani vikombe hivo jinsi vitakavyokupa hela nyingi kwa sababu kwa hapa nchini kwetu havipo kwa wingi, hivyo bado ni fursa ambayo ni mbichi kabisa. Hivyo ni nafasi yako mwafaka wa kukamatia fursa hii na kuanza kuifanyia kazi ili uanze pia kujitengenezea pesa.
Kumbuka; Vikombe hivi  hubadilisha rangi, picha, maneno  kila vinapowekwa chai au maji ya moto hivyo ni fursa sana kama utaifikiria  kwa jicho la tatu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
MUHIMU: Kama utakuwa  upo tayari na unahitaji kufanya biashara hii wasiliana na uongozi wa DIRA YA MAFANIKIO kwa nambari 0757 909 942 au bofya namba hii tuwasiliane kupigia whatsapp wa.me/+255757909942  hii au email yetu ya dirayamafanikio@gmail.com
------------------------------------------------------------------------------------------------
Makala hii  imeandikwa; Benson Chonya
------------------------------------------------------------------------------------------------

Nov 21, 2022

Umaskini Wako Unasababishwa Na Kitu Hiki Tu,...

No comments :

Watu sio maskini eti kwa sababu hawana pesa, watu ni maskini ni kwa sababu ya mawazo yao. Unaweza ukawa unapato zuri sana lakini ukabaki kuwa maskini katika maisha. Kitakachokufanya uwe maskini ni matumizi ya mawazo yako katika kukufanikisha.

Wapo watu wengi sana ambao wana kipato kikubwa lakini wanashindwa kufikia utajiri. Hapo hakuna uchawi wowote ni matokeo ya matumizi ya mawazo. Wataalamu wa mambo ya mafanikio wanatuambia hivi, asilimia 90 ya matatizo yote ya pesa yana sababishwa na matumizi ya mawazo au akili zako.

Hivyo, ni muhimu sana kila wakati kuangalia, je mawazo yako yana uwezo wa kukufikisha kule unakotaka kufika kimafanikio? Ukiona una mashaka hata kidogo, ongeza juhudi ya kujifunza na kutamani kujua kila kitu kinachohusiana na pesa na mafanikio maishani mwako.

Wewe ni tajiri mkubwa sana, ikiwa utajiamini na kukubali kutumia nguvu kubwa ya mawazo uliyo ndani mwako kukufanikisha. Miaka kadhaa mbele naamini utakuja kunitafuta na kuniambia aisee ni kweli ulichosema Imani. Yote hayo yanawezekana kwako, hakuna uchawi zaidi kuchukua hatua na kujituma.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428 hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app 0687449428,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Nov 20, 2022

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuweka Jitihada Usikose Pesa.

No comments :

Kukosa pesa ni kilema kikubwa sana katika huu ulimwengu tuliopo. Ukiwa huna pesa changamoto kwako ni nyingi na unakuwa upo kwenye ukilema mkubwa usioujua.

Maskini wa kipato kidogo hata akiwa na mawazo mazuri bado hatapewa kipaumbele katika jamii yake kama vile pumba za tajiri zinavyopewa kipaumbele kikubwa zaidi.

Mungu mwenyewe analijua hilo ndio maana baada ya mfalme sulemani kumuomba hekima, Mungu akaamua kumpatia na utajiri kama ziada ya maombi yake.

Maana alijua kuwa hekima ya maskini inadharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.

Binafsi nawapongeza wote ambao wanahamasisha wengine kutafuta pesa, maana wakizipata wataheshimiwa.

Umaskini ni mbaya sana, na unapaswa kuchukiwa kwa nguvu zote, nami nasema hakuna mpumbavu duniani zaidi ya anae ona ufahari kuwa juu ya umaskini.

Umaskini sio baraka ni laana, ndani ya umaskini kuna ujinga mwingi, maradhi sugu, pamoja na kuonewa, nenda kwenye magereza au vituo vya polisi utakuta 90% ya walioshikiliwa ni maskini.

Nenda kwenye hizi hospital za kawaida, utakuta wanaoteseka wengi ni maskini, hata anaetumiwa mgambo waende kumkamata huyo ni maskini kwa sababu, wenye pesa hutumiwa barua ya wito na atajisalimisha mwenyewe maana utajiri unampa ujasiri wa kutokuogopa hovyo.

Ndugu yangu unaesoma ujumbe huu, anza kuuchukia umaskini kama unavyochukia harufu mbaya na uogope kama vile unavyoogopa magonjwa yasiyotibika, hiyo itakusaidia upate hamasa ya kutafuta pesa na kuwa tajiri katika siku zote za maisha yako.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 19, 2022

Mambo Ambayo Mungu Hawezi Kufanya..

No comments :

Ni muhimu kujua yapo mambo ambayo Mungu anaweza kufanya kwa ajili yako na yapo baadhi ya mambo ambayo Mungu hawezi kufanya. Hebu, tuangalie mambo ambayo Mungu hawezi kufanya.

1. Mungu hawezi kudanganya.

2. Mungu hawezi kubariki uongo.

3. Mungu hawezi kubadilika.

4. Mungu hawezi kuwa mdogo kuliko changamoto yako.

5. Mungu hakumbushii makosa yaliyopita, akikusamehe amesamehe.

6. Mungu hana upendeleo.

7. Mungu hawezi kukuacha.

8. Mungu hawezi kubariki hali ya mashaka.

9. Mungu hawezi kuvunja agano lake.

10. Mungu hawezi kuwa dhaifu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo Mungu hawezi kufanya kabisa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 18, 2022

Hawa Ndio Marafiki Wa Kuwa Nao.

No comments :

Ni muhimu kuzungukwa na marafiki wazuri, ambao watatupa imani na kujiamini hata kwenye nyakati ngumu. Ukiwa na marafiki wa aina hiyo ni rahisi kuwa mshindi kimafanikio wakati wote.

Tatizo la watu wengi wana marafiki ambao hawana msaada. Ukitaka kujua hilo ngoja itokee changamoto, ndio utaona. Wengi wataanza kukimbia kama Yesu alivyokimbiwa na wanafunzi wake.

Ukiona una marafiki hao waweke pembeni haraka, kwa sababu hawatakusaidia kufikia ndoto zako. Hawa ni marafiki ambao wanataka mcheke na mfurahi wakati wa raha tu, ila wakati wa shida huwaoni tena.

Ni kheri kubaki ukiwa mwenyewe kuliko ukajikuta ukawa na kundi kubwa la marafiki ambao ni wanafiki, marafiki kupe. Marafiki wanafiki wote watupe huko, watakusaidia nini, ni sawa na utakuwa unajichosha.

Kaa na watu wenye akili. Kaa na marafiki wenye akili, watakaokupa moyo, hamasa, kujiamini kwenye harakati za kuelekea mafanikio yako. Wengine waliobakia basi iishie kujuana tu, inatosha.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 17, 2022

Hivi Ndivyo Njia Ya Mafanikio Ilivyo...

No comments :

Njia ya mafanikio ni ndefu. Hakuna njia ya mafanikio iliyo fupi. Njia ya mafanikio ni ndefu kwa sababu, katika urefu huo huo, ndimo kuna kujifunza kwingi.

Ikiwa unatafuta njia ya mkato, basi wewe unatafuta kuwa na msongo wa mawazo na kijichanganya zaidi. Njia za mkato hazina kujifunza zaidi utaumia tu wewe.

Mafanikio ni sawa na mbio za muda mrefu. Mafanikio sio mbio za muda mfupi, hivyo inakubidi ukubali kujifunza kwa namna yeyote ile. Ili ujifunze lazima ufuate njia ndefu.

Kuna hadithi moja, inayoeleza kwa ufasaha juu ya hili kuwa ni muhimu kufuata njia ndefu iliyoko kwenye mpango wa Mungu ili kufanikiwa na kujifunza mengi zaidi.

Kulikuwa na ndege mmoja ambayo alikuwa mzuri sana. Ndege huyo kila ilipokuwa ikifika jioni alikuwa anatua kwenye mti na kuanza kuimba nyimbo nzuri sana za kuvutia.

Siku moja wakati anaimba, mara alitokea mtu akiwa ameshikilia boksi, yule ndege akauliza, vipi mbona umebeba boksi kama zito hivi humo ndani lina nini? yule mtu akamwambia lina minyoo.

Yule ndege akafikiria akamwambia basi, naomba mmoja. Yule mtu akamwambia nipe na wewe nyoa moja na mimi nakupa mnyoo mmoja. Basi ndege akakubali akawa anatoa nyoa, anapewa mnyoo, mwisho wa siku ndege akajikuta hana manyoa karibu yote.

Ule uzuri aliokuwa nao ukawa umetoweka. Akawa hawezi kuruka tena. Kitu kikubwa kilichomwathiri ni kutaka kutafuta njia ya mkato ya kutafuta chakula wakati njia nzuri alikuwa nayo.

Hivyo, ndivyo athari za kutafuta njia za mkato zinavyojitokeza. Ni vyema na ni bora ukafata njia ndefu ikawa na manufaa kuliko njia fupi yenye majanga makubwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 16, 2022

Hizi Ndizo Faida Za Msamaha.

No comments :

Ipo haja ya wewe kujifunza msamaha hata kama kuna waliokukosea kwa kiasi kikubwa sana.

Ipo faida ya kusamehe. Msamaha unaweza kusababisha: 

1. Mahusiano yenye afya.

2. Kuboresha afya ya akili. 

3. Kupunguza uadui. 

4. Kutengeneza mfumo wa kinga wenye nguvu zaidi. 

5. Uboreshaji wa afya ya moyo. 

6. Kuboresha kujithamini zaidi. 

7. Mungu pia anakuwa anakusamehe, kwa sababu umesamehe.

8. Moyo wako unakuwa hauna maumivu, tofauti na ambavyo ukishindwa kusamehe utaumia.

Hizo ni faida chache za kuwa na msamaha, ukizingatia zitakusaidia kuishi maisha yenye amani na furaha.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Nov 15, 2022

Usitishwe Na Watu Wa Aina Hii...

No comments :

Katika maisha yako unatakiwa usitishwe na watu wa aina mbili, wakosoaji na watu wasio na shukrani. Hawa watu inatakiwa wasikutishe kwa lolote lile, maana ni watu ambao wapo na hawawezi kuisha. 

Wewe jiruhusu kufanya mambo yako kama kuna ambao watakukosoa acha wakukosoe kwa jinsi wanavyotaka, kama kuna utakaowasaidia kisha wakashindwa kuwa na shukrani achana nao pia.

Inatakiwa ujue wakosoaji na watu wasio shukrani ndio watu pekee wanaweza wakakufanya uhisi huwezi kufanikiwa tena. Lakini elewa, hakuna mtu atakayekufanya ujihisi wa kawaida au kuacha ndoto zako bila ya ruhusa yako. 

Watu wanaweza kusema sana kuwa huwezi hicho unachokifanya, lakini hiyo sio sababu ya wewe kujiona hutaweza. Mpaka ifike mahali ya kuwa huwezi inakutaka wewe ujiruhusu kuwa kweli sasa huwezi.

Unaweza kukosolewa sana, lakini hicho kisikutishe. Kama kile unachokifanya kipo kwa ajili ya kusudi la Mungu, acha wanaoendelea kusema waseme mpaka kesho, ila utafanikiwa. 

Acha kuweka nguvu zako kwenye kukosolewa, zingatia kile unachofanya. Wakosoaji juu ya maisha yako hawawezi kuisha, ni wapo tu, leo watasema hiki na kesho watasema kile.

Si wakosoaji tu pia unaweza ukawa na watu wasio na shukrani lakini usipigwe na mshangao hata wakati wa Yesu katika wale wakoma kumi walioponywa ni mkoma mmoja aliyerudi na kushukuru.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

Aug 7, 2022

Jinsi Ya Kukabiliana Na Kukatishwa Tamaa.

No comments :

Ili kuishi maisha yako bora, unatakiwa ujifunze JINSI YA KUKABILIANA NA KUKATISHWA TAMAA, Kimsingi, hakuna mtu ambae hakatishwi tamaa, kila mtu kwenye maisha yake anakatishwa tamaa kwa namna moja au nyingine.

Kuna wanaokatishwa tamaa na mambo madogo madogo kama kukosa karo ya shule, kushindwa kupata mkopo, biashara kushindwa kwenda vizuri au kuchelewa usafiri, kushindwa kuongezewa mshahara na kushindwa kuvuna unavyotaka.

Kuna wanaokatishwa na mambo makubwa kama kufiwa na umpendae, kupoteza kazi, kuambiwa una ugonjwa ambao huwezi kupona, nyumba au biashara kuungua, ajali, kuachishwa kazi, ndoa kuvunjika, ajali inayokupa ulemavu na mengineyo.

Kwa vyovyote vile iwavyo,  unapokatishwa tamaa na jambo lolote lile, kitu kikubwa kinachotokea kwako, IMANI YAKO INAKWENDA KUTIKISWA, Utaanza kuona kila kitu hakifai, hata kama ulikuwa na imani kubwa inashuka chini na kujikuta kushindwa kuchukua hatua.

Kitu cha kufanya hali ya kukatishwa tamaa inavyoingia ndani mwako, jitahidi sana kusahau yote yaliyokukatisha tamaa. Unatakiwa jiambie, YALIYOPITA YAMEPITA na sasa ni wakati wa kusonga mbele.

Usiruhusu YALIYOPITA yaharibu kesho yako. Usikae kwa kuendelea kuvunjika moyo kwa sababu ya matukio ambayo tayari YAMEPITA. Weka nguvu za uzingativu kwa yale unayoweza kubadilisha tu. Anzia hapo ulipo na hapo utaweza kukabiliana na kukatishwa tamaa.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno  WINNER'S FAMILY kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Feb 20, 2022

WAZO LA KUJIAJIRI: Biashara Ya Kupaka Kucha Rangi Kwa Kutumia Mashine bora.

No comments :

Leo katika wazo letu kujiajiri, tunakuletea wazo la kuanzisha biashara ya kupaka rangi kucha kwa kutumia mashine ya kisasa. Ndio nimesema kupaka rangi kucha, usiwe na papara tulia. 

Kama unavyojua mjini, wadada wengi mjini wanapenda kupendeza na wengi hujiremba kwa mengi ikiwa pamoja na kupaka rangi kucha.

Lakini kwa ilivyozoeleka na inavyojulikana, kucha nyingi hupakaliwa kwa kutumia mkono. Ajabu katika nyakati hizi kwa sasa, ipo mashine ya kufanya hivyo yaani kupaka kucha rangi.

Kama nilivyokwambia kwa sasa ipo mashine ya kupaka kucha rangi. Hii ni mashine ya kupaka kucha rangi. Huhitaji kutumia mkono ili rangi ipakaliwe kwenye vidole vyako vya mkono. Unatumia mashine maalumu. 

Ni machine ambayo  inapaka rangi za maumbile tofauti tofauti zaidi ya 500, lakini pia hata ukijipiga picha wewe ukataka ihamie kwenye kucha inawezekana.

Vitu unavyotakiwa uwe navyo ili mashine ifanye kazi vizuri ni smart phone na rangi zake. Gharama za rangi si nyingi ni Tsh.35000/= inapaka kucha 1000, ambapo hapo ni sawa na watu 100.

Ni mashine ambayo inapaka kucha kwa ubora wa hali ya juu sana, na kucha zinakuwa za viwango. Huwezi kulinganisha na kucha zinazopakaliwa na mkono.

Mashine hii inafaa kwa MJASIRIAMALI anayetaka kwenda ki digital, hapa ukiiweka mjini, ndo habari ya mjini, nani apakaliwe kucha zake kwa mkono, wakati mashine ipo ni dakika tano tu, kazi imeisha.

Jaribu kuwaza kwa sauti, jinsi utakavyoteka wakina dada, pindi wakijua kwenye mtaa fulani au saluni fulani kuna mashine ya kupaka rangi kucha kwa dakika tano tu.

Uzuri wa mashine hii kama nilivyosema hata ukimpiga picha mpenzi wako au ukijipiga wewe, unaweza kuihamisha, kwenye kucha.

Kwa leo katika wazo letu la KUJIAJIRI, tuishie hapa. Kama una swali karibu na kama pia umeipenda na unaitaka mashine hii, karibu tuwasiliane. 

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.