google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 31, 2017

Toka Kwenye Vifungo Hivi,..Utengeneze Zaidi Mafanikio.

No comments :
Vipo vifungo vingi ambavyo vinaweza kukufunga na kukupotezea mafanikio yako. Vifungo vingine unavijua na vingine unaweza ukawa huvijui. Kwa mfano;-
Acha kujiweka kwenye vifungo vya kidini na kuamini utajiri mkubwa ni dhambi. Kumbuka, mafanikio hayana uhusiano moja kwa moja na kutenda mabaya.
Acha kuamini umaskini ndio ni kitu kizuri kwako. Hivyo ukashindwa kuweka juhudi zako zote kwa kisingizio cha kwamba ukiwa maskini ni sawa kwako.
Acha kuamini ukiwa na pesa nyingi ndio ushetani. Utajikwamisha sana wewe mwenyewe kufikia mafanikio yako bila kujijua ukiwa upo kwenye kifungo cha dini.

Acha kuamini kwamba Mungu atakusaidia kila kitu, hata kama umebweteka na wala hujitumi sana yaani huweki juhudi sana, ndio maana amekupa akili ufikirie na vingine.
Acha kutumia uvivu wako kutumia kama kisingizo ukiamini hio ndiyo imani sahihi.. Kama kuna kazi unayotakiwa kufanya, fanya kweli. acha kuendekeza uvivu unaomba kazi kwenye kampuni moja halafu unamlaumu Mungu. Ukiona uko hivyo ujue kabisa upo kwenye kifungo..
Toka kwenye kila aina ya vifungo ambavyo unaona vinakukwamisha kufanikiwa sana kwenye maisha yako, kuwa huru ili utengeneze mafanikio yako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com



Mar 30, 2017

Nufaika Na Kilimo Bora Cha Matango.

2 comments :
Habari rafiki na karibu sana katika safu hii ya makala za kilimo. Katika somo liliopita tuliangalia juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora na faida zake. Sasa leo tutaangalia kilimo cha matango kwa kutumia mbegu bora inayoitwa Hybrid Cucumber YETU F1 ambayo utaanza kuvuna baada ya siku 45-50 kutoka kupandwa kwake.
YETU F1 ni mbegu chotara ambayo ina umbo zuri na hupendwa sana na walaji. Kiasi cha mbegu 300g(Gramu 300) huweza kutosha ekari moja ambayo utainununua kwa shilingi laki tatu(300,000/=) za kitanzania.
 UANDAAJI WA SHAMBA.
Chagua sehemu iliyo nzuri,na ukipata sehumu ya tifutifu iliyo changanyikana na mchanga itakuwa vizuri zaidi.
Pia ukipata sehemu yenye udongo mzito lakini usiwe una tuamisha maji.
Lima shamba na hakikisha umelisawazisha vizuri(yaani hallowing),baada yapo panga matuta yako.
KIASI CHA MBEGU.
Gramu 300 zenye kiasi ya YETU F1 kinatosha kupanda eneo la ekari moja(100m×40m).
Na hii aina ya mbegu 1g ina mbegu 30-40.

KUPANDA.
Kabla ya kupanda hakikisha una mbolea ya kupandia kama DAP ikichanganywa na Agrigrow starter yenye madini mengi ya phosphorus.
Panda mbegu kwa nafasi 150cm×45cm mbegu mbili mbili kila shimo.
Na hii mbegu huota baada ya siku tatu hadi tano,hivyo huchukua muda mfupi kuota.
Mara baada ya kuota tumia mbolea ya majani Agrigrow starter ambayo itaimarisha mizizi hivyo kurahisisha mmea kupata chakula kutoka kwenye udongo.
Huu mmea huchukua muda mfupi kukua hivyo hivyo mara baada ya kuota baada ya siku chache tumia mbolea ya yara mila winner kukuzia.
Pia yatakavyo anza kutambaa tumia mbolea ya majani Agrigrow vegetative hii itafanya yawe na matawi mengi hivyo kuongeza uzalishaji.
Maua yakianza kuonekana tuu,tumia mbolea ya majani Agrigrow flowering and fruiting,hii itasaidia maua kuto pukutika,pia itaboresha muonekano wa tunda,itafanya maua yawe mengi hivyo na kupatikana kwa matunda mengi.
Epuka kumwagilia maji jioni sana kwa kuwa unaweza ukasababisha magonjwa kama ya fangasi kwa mmea.
Pia epuka kupulizia dawa pale wadudu wa muhimu wawapo shambani(kama nyuki)kwani kutafanya kupunguza kwa mazao shambani.
DAWA ZA WADUDU
Ukiwa ni mkulima unayelima kitaalamu na unayetaka mafanikio kupitia kilimo yakufaa kuwa na dawa za wadudu zifuatazo.
1. Prosper 720EC yenye mchanganyiko wa sumu mbili(Profenofos 600g/L +Cypermethrin 120g/L),hii ni dawa ambayo ina ua wadudu katika wigo mpana(yaani ni broad spectrum). Na mchanganyiko wake ni 2mls au 2cc kwa maji lita 1.
2. Avirmec 1.8EC (Yenye sumu ya Abamectin) hii itauwa utitili shambani wa aina yote,na mchanganyiko wake ni 7mls kwa lita 20 za maji.
3. Dawa ya ukungu Agrilax 72WP,hasa kwa nyakati za baridi,hii ni dawa ambayo ina mchanganyiko ya wa sumu mbili yaani Mancozeb na Metalaxyl,ambayo mancozeb kwa ajiri ya kukinga(Preventive)  na metalaxyl kwa kutibu(Curative).
Hivyo Agrilax hukinga na kutibu magonjwa yote yatokanayo na fangasi(yaani fungicide diseases).
 MAVUNO.
Matango(YETU F1) huwa tayari baada ya siku 45-50 kutoka siku ya kupandwa.
Je utakuwa na miche mingapi kwa ekari moja? Kwa kawaida miche hufikia 11850.
Tuliangalia katika somo la matikiti kanuni ya kutafuta idadi ya miche yaani Plant population(I.e PP)
Plant population(PP) =(Area/Spacing) ×no of seeds per hole.
 Kwa mfano:-Area(A)=1acre=4000m square.
-Spacing (SP)=150cm×45cm or 1.5m×0.45m.
-No of seeds to be sown per hole=2seeds.
-Required: Plant population (PP)
Then,from the formula;-
 PP=((A/SP))×no of seeds per hole.
 PP=((4000)÷(1.5×0.45))×2.
 PP=(4000÷0.675)×2
 PP=5925×2
 PP=11,850Plants/acre
Therefore, there will be 11,850plants per acre.
Na haya matango kwa matunzo mazuri, huwa na matunda mengi sana ambayo yataweza kufikisha viroba 150 kwa makadilio ya chini kabisa  ambayo utauza kwa sh 70,000/= kwa kiroba kimoja kwa bei ya chini kabisa.
Viroba 150@sh 70,000 ni sh 10,500,000/= kwa makadilio ya chini na hyo pesa ni kwa ekari moja tu.
Na hayo mapato ni kwa wale ambao wamepanda bila kuwekea nguzo(Non trellised)
Kwa wale watakao wekea nguzo(Trellised) wataweza kutumia eneo dogo na kupata mavuno mengi zaidi.
Na hivi ndivyo kilimo biashara kinavyotakiwa kuendeshwa(lima eneo dogo vuna mazao mengi)
Hebu tuangalie kwa wale watakao wekea nguzo(Trellised Cucumber)
Shamba la ekari moja(4000m square), Spacing =80cm×40cm(0,8m×0.4m),number of seeds per hole =1seed,Plant population (PP)=?
    Therefore:-
PP=(Area/spacing) × no of seeds per hole.
PP=((4000)÷(0.8×0.4))×1.
PP=4000÷0.32
PP=12,500Plants/acre
-Na kwa kuiwekekea nguzo(Trellised cucumber) huweza kuzaa matunda mengi zaidi kuliko bila kuyawekea nguzo.
-Kwa kuyawekea nguzo mche mmoja huweza kuzaa matunda 15-30 kwa mche mmoja.
-Tuchukulie kwa makadilio madogo kabisa mche mmoja umezaa matunda 15
   Kwa hiyo basi;-
   1plant=15fruits
 12500plants=x?
        By crossing:
x=12500×15
x=187,500fruits/plants
-Kwa hiyo utakuwa na jumla ya matunda 187,500 kwa ekari moja
-Kwa kuuza kwa bei ndogo kabisa ya sh 50 kwa tunda moja,utakuwa na jumla ya fedha =187,500×50= Tzs 9,375,000/=
-Kwa watakao uza kwa sh 100 kwa tunda moja,basi utakuwa na jumla ya pesa 187,500×100=18,750,000/=.
Kazi kwako kwa wewe mkulima unaye taka mafanikio,tumia mbegu bora (Hybrid seeds) zikuletee mafanikio.
Wako mtaalamu wa kilimo.
Boniface L Pwele,
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0762567628 au tuma ujumbe kwa barua pepe blugahno95@gmail.com

Mar 29, 2017

Hawa Ndio Wanawake Waliofanikiwa Sana Kwenye Ujasiriamali.

No comments :
Siku zote tunasema na tutaendelea kusema  kwamba mafanikio hayana rangi, kabila, umri wala jinsia, ukiamua kufanikiwa kwa vyovyote vile ulivyo hata uwe katika kona gani ya dunia utafanikiwa tu, kwa sababu umeamua iwe hivyo kwako na itakuwa.
Nasema hivyo kwa sababu, mara nyingi watu wengi linapokuja suala la mafanikio huwa kuna bagua bagua nyingi sana kwa upande wao. Kwa mfano, mtu anakwambia kabisa huwezi kufanikiwa kwa sababu wewe umri wako ni mdogo au huwezi kufanikiwa sana kwa sababu wewe ni mwanamke.
Ukiangalia ukweli wa mambo ulivyo kwenye mafanikio hauko hivyo, kwa vyovyote vile ulivyo unaweza ukafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa bila kujali unaishi nchi gani au bila kujali wewe ni mtu wa jinsia gani yaani mwanaume au mwanamke.
Kutilia mkazo katika hilo na ili unielewe vizuri ninachosema hapa, leo kupitia makala haya tuangalie baadhi ya wanawake ambao wamepata mafanikio makubwa sana duniani kupitia ujasiriamali, ingawa kuna wakati pengine walibezwa na kukejeliwa sana kwamba hawawezi kufika popote.
1. Oprah Winfrey
Pamoja na kwamba Oprah kwa sasa ameshaacha mambo ya utangazaji kwenye televisheni lakini ni moja ya wanawake ambao wamefanikiwa sana na kuwa na pesa nyingi kutokana na kujituma na kuwekeza kadri alivyoweza hadi kufikia mafanikio aliyonayo sasa.
Yeye kama yeye kupitia kituo chake cha Oprah Winfrey leadership academyamefanikiwa kuwasaidia watoto wengi wa kike, pia ni jambo ambalo limekuwa llikimuungizia pesa za kutosha. Ameidhirihishia dunia kwamba mafanikio hayana jinsia ni kujituma tu.

2. Folorunsho Alakija
Alakija ni moja pia ya wanawake wenye pesa na tajiri sana nchini Nigeria. Biashara zake zilizompa utajiri ni biashara ya mapambo na mafuta. Kwa sasa Alikija anakadiriwa kufikia utajiri wa dola za kimarekani billion 1. 6.
Mpaka hapo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo naye amejitahidi kuweka juhudi nyingi za kufikia mafanikio yake aliyonayo katika kile anachokifanya. Hiyo yote inaonyesha juhudi ikiwekwa popote hakuna kinachoshindikana.

3. Wang Laichun
Laichun pia inasemekana ni moja ya mabillionea wa kichina ambapo utajiri wake alionao ambao kwa sasa unafikia dola za kimarekai bilini 1.67, umetokana na juhudi zake binafsi na sio kurithi.
Biashara iliyompaisha hadi kufika huko aliko sasa ni biashara ya vifaa vya umeme ambavyo anavisambaza na amekuwa mojawapo ya wanawake matajiri sana duniani.

4. Debbie Fields
Pia katika wanawake wajasiriamali na wenye pesa huwezi kumsahau mwanadada huyu Debbie fields katika ulimwengu wa mafanikio. Ni moja ya wanawake kweli waliofanikiwa haswaa.
Utajiri wake hasa ni wa nini? Huu ni mwandada anayejihusisha na kutengeneza vyakula vya aina tofauti tofauti vyenye mfumo kama wa keki. Ambapo kwa sasa anasambaza vyakula vyake zaidi ya nchi kumi duniani. 
Mafanikio katika maisha yako yanawezekana. Huna haja ya kuwa na sababu kwamba mimi sina hiki au kile au mimi kwa sababu ni jinsia hii siwezi kufanikiwa, weka juhudi, matokeo utayaona.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspt.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

Mar 27, 2017

Namna Unavyoweza Kugeuza Makosa Yako Na Kuwa Mafanikio.

No comments :
Makosa katika safari yoyote ya mafanikio  ni kitu ambacho hakikwepeki. Bila shaka wewe na mimi tumeshawahi kukosea katika maeneo kadhaa ya maisha yetu. Kukosea huko kulitufanya pengine tujute au kuumia kabisa na kujiona kama vile hatufai.
Je, kitu cha kujiuliza hivi ndivyo tulivyotakiwa kuyachukulia makosa haya na kujihukumu vya kutosha. Jibu rahisi hapa ni hapana. Hatukuwa na sababu ya kujihukumu sana kutokana na makosa yetu, zaidi ya kugeuza makosa hayo na kuwa ushindi.
Na ni kwa namna gani tunaweza kugeuza makosa yetu kuwa ushindi?
1. Jifunze kutokana na makosa hayo.
Ili uweze kuwa mshindi na kugeuza makosa yako kuwa ushindi, ni lazima kujifunza kutokana na makosa ambayo unayafanya. Kama hujifunzi, hakuna utachokuwa unafanya, zaidi utaendelea kukosea na kubaki hapo. Wanaojifunza na kuchukua hatua ndio wanaofanikiwa.
Kukosea kwako hakuna shida sana, shida inakuja pale unaposhindwa kujifunza. Ni muhimu kujifunza kutokana na makosa yako na kurekebisha pale ulipokosea. Kwa kadri utakavozidi kujifunza utajikuta makosa yako yanageuka kuwa ngazi ya kukufanikisha badala ya vizuizi.

USHINDI NI LAZIMA
2. Chukua jukumu la kuwajibika.
Hautaweza kwenda popote wala kupata mafanikio, ikiwa utakuwa ni mtu wa kulaumu wengine kwamba ndio waliosababisha ukakosea. Mtu wa kwanza kuwajibika kwa makosa uliyofanya ni wewe. Acha kulaumu wengine, utakuwa unapoteza wako bure. Wajibika kwanza wewe.
Unapochukua jukumu la kuwajibika elewa wewe ndiye kiongozi wa maisha yako, hivyo kama kuna makosa yamefanyika kwa sehemu una mchngo wa kusababisha makosa hayo kujitokeza. Badala ya kulaumu, tafuta nini kilichokufanya ukakosea, kirekebishe baada ya hapo endelea na safari yko.
3. Jifunze kutokana na uzoefu.
Linaweza likawa ni jambo linalokuuma sana, hasa pale unapokosea. Lakini nina uhakika pamoja na maumivu hayo kuna kitu ambacho unaweza ukajifunza hapo. Kujifunza huko, huo ndio uzoefu ninaotaka uuchukue hapo na kuugeuza kuwa ushindi pengine yanapotokea makosa kama hayo kwa baadae.
Acha kuishia kuumia na kulalamika na ukabaki hivyo, utakuwa hufanyi kitu. Utumie uzoefu kukusaidia kufika kwenye kilele cha mafanikio. Mara nyingi kwenye kipindi cha kukosea unaweza ukakiona ni cha mateso na maumivu. Lakini , kumbuka siku zote uzoefu ni mwalimu mzuri w mafanikio yako.
4. Badili tabia zako.
Inawezekana ukawa unashindwa na unaendelea kufanya makosa kwa sababu ya tabia ulizonazo. Ili uweze kutoka hapo na kuepuka makosa huna namna nyingine zaidi ya wewe kuweza kubadili tabia zako mara moja. Ukiweza kubadili tabia zako hizo zinazokurudisha nyuma, basi yapo makosa ambayo unayarudia kuyafanya utayaepuka moja kwa moja na kuwa mshindi.
Hivi ndivyo unavyoweza kugeuza kushindwa kwako na kuwa ushindi wa mafanikio. Acha kuhuzunika na kusononeka sana. Fanyia kazi mambo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwako sana.
Endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO na kumbuka tupo pamoja.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,



Mar 25, 2017

Habari Njema Kwa Wafugaji Wote Wa Kuku.

No comments :
Habari njema kwa wafugaji wote wa kuku.  Dezhou Runde Metal Products, Ltd tuliopo Tanga, Tanzania ni wauzaji  wa mashine za kuangulia vifaranga (Incubators) kwa  bei nafuu sawa na kiwandani.
Pia hio haitoshi tunauza na vifaa vingine ambavyo vinatumika kwenye ufugaji wa kuku kama Drinker, Nipple drinker, Auto drinker, chick auto drinker, cages na vinginevyo vingi kulingana na mahitaji yako.


Kama una hitaji mashine bora za kuangulia vifaranga kwa muda mfupi na bei nafuu, tafadhari wasiliana nasi kwa kutupigia simu moja kwa moja kwenda 0767 04 80 35.
Hata hivyo pia ukiona Tangazo hili, mwambie na mwingine, asiikose fursa hii.  
WOTE MNAKARIBISHWA NA TUPO KWA AJILI YAKO KWA KUKUPA HUDUMA BORA NA YA FAIDA.

Mar 24, 2017

Kinachokupotezea Mafanikio Yako Sana Ni Hiki Hapa.

No comments :
Acha kujidanganya kwamba unatafuta mafanikio wakati hata unashindwa kubadili tabia ndogo ndogo za kukupeleka kwenye mafanikio yako, huo utakuwa ni uongo mkubwa.
Acha kuendelea kujidanganya kwamba kesho yako itakuwa bora wakati hata leo hii hufanyi kitu cha uhakika cha kubadilisha maisha yako. Maisha yako kiukweli hayataweza kubadilika.
Acha kuendelea kulaumu watu wengine kwa maisha yako kuendelea kuwa mabaya. Mtu wa kwanza unayetakiwa kumlaumu ni wewe mwenyewe hasa kutokana na mienendo na tabia zako.
Sio kwa sababu maisha ni magumu kwa sasa, basi unachanganyikiwa na kuona kila kitu hakifai kwako na kwa wengine. Maisha yanahitaji sana utulivu wa hali ya juu ili ufanikiwe, unatakiwa ujue hili.

Kama unaona maisha yako yamekweda hovyo, jichunguze, panga mipango yako upya kwa umakini na utulivu na hata wala usikurupuke katika hilo. Utulivu ni kitu cha msingi sana ambacho kinaweza kukupa mafanikio.
Tabia mbaya na mienendo mibovu ulionayo hiyo ndiyo inaokufanya au naweza kusema inaharibu maisha yako moja kwa moja. Angalia hilo halafu utaujua ukweli ambao ninakwambia.
Kila wakati jiulize, unaendelea kukua kimafanikio, au unarudi nyuma? Kama unarudi nyuma, kama nilivyosema kuwa makini sana na tabia na mienendo yako, hiyo ndiyo inayokukwamisha.
Kama umefika wakati kwako wa kusema uko 'serious' na mafanikio yako, basi hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kubadilisha tabia zako na kujenga tabia zitakazokuwezesha kufanikiwa.
Kumbuka pia kinachokupotezea mafanikio yako, ni tabia ambazo unazo na unazibeba kila wakati, hicho ndicho kitu kikubwa kinachokupotezea mafanikio yako ya leo na kesho.
Nikutakie siku njema na kila kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

Mar 23, 2017

Hatua Nne Za Kufikia Malengo Yako Kwa Uhakika Mkubwa.

No comments :
Kila mtu katika maisha yake ana malengo maalumu ambayo anakuwa amejiwekea na anakuwa ana waza kwamba kwa namna yoyote ni lazima baada ya muda fulani malengo yake yatatimia.
Pia sina shaka na wewe, naamini umejifunza kwa sehemu namna au mbinu ambazo mtu anaweza akazitumia kuweza kufikia malengo yake. Lakini leo hii, si vibaya kama nitakung’ata sikio kukumbushia tena jinsi unavyoweza kufikia malengo yako kwa uhakika mkubwa.
Najua kila mtu ana njia zake na mbinu ambazo anazitumia kuweza kufikia malengo yoyote katika maisha. Leo hii, naomba nikuonyeshe mbinu ambazo zinatumiwa karibu na watu wote wenye mafanikio makubwa kufikia malengo yao kila wakati.
Andika malengo yako chini.
Yaweke malengo yako kwenye karatasii ili yawe rahisi kuyaona. Yawe ni malengo mahsusi ambayo utekelezaji wake unafikika na uwe tayari umejiwekea tarehe maalumu ya kuyafikia. Hio ndiyo sifa ya malengo unayotakiwa kuwa nayo.

Anza kuweka mipango.
Umesha andika malengo yako tayari. Hatua inayofuata ni kwa wewe sasa, kuweka mipango ya kufanya. Kumbuka unapofanya jambo unapata nguvu zaidi ya kuweza kulifanikisha kuliko ukitulia. Hivyo ni lazima mipango yako iwe hai na ya kiutekelezaji.
Lipa gharama.
Kubali kulipia kila gharama inayohitajika ili kufikia malengo yako. Gharama hizo zinaweza zikawa ni muda au nidhamu binafsi. Lakini gharama yoyote fanya kila ufanyalo hakikisha unailipa. Kama utakwepa kulipa gharama yoyote ile naomba nikwambie sahau mafanikio.
Yapitie malengo yako kila siku.
Hakuna namna ya nyingine ya kuwa mshindi zaidi ya wewe kukomaa kupitia malengo yako kila siku. Unapopitia malengo yako kila siku yanakupa nguvu na hamasa kubwa ya kuona ni jinsi gani yanawezekana na unaweza kuyafikia.
Hivyo ndivyo, unaweza kutimiza malengo kwa kufuata hizo hatua rahisi kabisa.
Nikutakie siku njema na kila kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,


Mar 22, 2017

Haya Ndiyo Mahusiano Yaliyopo Kati Ya Mafanikio Na Afya Yako.

No comments :
Je kuna mtu ambaye hapendi mafanikio katika maisha yake? Kila mtu ukimuuliza atakwambia ana taka mafanikio, maendeleo na maisha bora.
Lakini ulisha wahi kujiuliza afya yako ina husiana vipi na mafanikio unayoyahitaji? Je una weza kufanikiwa bila kuwa na afya bora na imara? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi unayopaswa kuji uliza kabla huja endelea kusoma makala hii.
Tabia zetu zimekua zikiathiri moja kwa moja afya yetu hivyo kupelekea kushindwa kutimiza malengo tunayo jiwekea katika maisha yetu. Tabia hizo ni vitu ambavyo tunaviendekeza na kuvichukulia kama sehemu ya maisha yetu bila kujua madhara yake baadae.
Tofauti kati ya bustani na msitu ni matunzo, bustani hutunzwa hivyo hustawi na kupendeza na kuifanya izae matunda mazuri yapendezayo. Hivyo mwili nao unahitaji matunzo ili uweze kukupa matunda unayo tamani.
TABIA ZINAZO ATHIRI AFYA ZETU
1. Ulaji Mbaya Wa Chakula.
Hapa ndipo watu wengi wana angukia, kuna makundi mawili ya ulaji mbaya
Ratiba mbaya ya kula
Watu wengi hawana ratiba nzuri ya kula na wengi huchelewa kula kwa madai kazi zina watinga. Lakini ukweli ni kuwa ukichelewa kula una ua mwili wako taratibu, magonjwa kama vidonda vya tumbo yamekua yaki wasumbua watu wengi kutokana na kushindwa kula kwa wakati.
Kula usiku sana hupelekea mwili kutunza mafuta na kuongezeka uzito. Kupoteza uwezo wa kufikiri,na kusinyaa kwa ubongo kutokana na kukosa cha nguvu kwa muda mrefu.
Kula vyakula hatarishi
Ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi,chumvi na kahawa hupelekea magonjwa kama shinikizo la damu na kusukari pia kuongezeka uzito kupunguza uwezo wa moyo kufanya kazi na kuathiri uwezo wa kufikiri.
CHAKULA BORA NI MAFUTA YA UBONGO.
Kula chakula bora kwa afya yako.
2. Msongo wa mawazo.
Ndio msongo wa mawazo, kuwaza ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu. Lakini kuwaza kupitiliza husababisha matatizo makubwa bila kujijua.
Vitu kama kufanya kazi kupitiliza, majibizano,kukosa muda wa kutosha kupumzika, kukataliwa huweza kusabisha msongo wa mawazo.nakuleta madhara kama kupoteza mwelekeo, kushindwa kufanya maamuzi,kupoteza umakini,kushindwa kuhusiana na watu vizuri.
3. Kukosa Muda mzuri wa Kulala.
Uta shangaa kulala? lakini ukweli unabaki pale pale, kulala kwa wakati. Una lala saa kumi na kuamka saa kumi na moja hii ni moja kati ya tabia hatarishi sana kwa afya zetu. Wanasayansi wana shauri kulala kwa afya ni masaa 6-7.
Magonjwa ya figo,moyo,uzito ulio pitiliza,kisukari na shinikizo la damu yana weza kusababishwa na kukosa muda wa kutosha kulala.
4. Tabia binafsi.
Hizi ni zile tabia ambazo mtu huzi anzisha na baadae kushidwa kuzi himili na huanza kumuendesha, tabia kama ulevi,kuvuta sigara,madawa ya kulevya,ngono zembe,huanza taratibu na baadae hugharimu afya yako.
Watu wotewalio fanikiwa hujali afya zao kuliko mali walizo nazo, lakini maskini hutumia kidogo alicho nacho kuharibu afya yake bila kujua, na huku aki hitaji kufanikiwa.
HUWEZI KUPATA MAENDELEO KAMA HUTA ITUNZA AFYA YAKO.
ITUNZE AFYA YAKO KWA MAENDELEO YAKO.
Makala imeandikwa na Dr.Julius Kimaro, 0745524031.

Mar 21, 2017

Utajiri Na Umaskini Unatokana Na Nini?

No comments :
Kila mmoja ninaamini anao uwezo wa kuwa tajiri, isipokuwa binadamu huwa na fikra tofauti juu ya mambo yale yale. Kitu kilichoko akilini mwako ndicho kinacho leta tofauti ya hali ya maisha unayoishi kwa sasa .
Maana yake ni kwamba, jinsi ulivyo wewe ni zao la yale yote unayofikiri kila siku. Watu waliofanikiwa kuwa matajiri, wana mambo kama 5 ambayo wameyafanya kuwa kama kanuni zao za kudumu na kwakuwa ni kanuni, wao huzitekeleza na kuziishi kila siku.
Kanuni zenyewe ni....
Namba moja: Matajiri wana fikra vichwani mwao kwamba kila kitu duniani kipo kwa wingi. Lakini maskini wao hufikiri kwamba kila kitu duniani hakitoshi. Kwa maneno mengine ni kwamba, masikini kila wakati anafikiria uhaba, jambo ambalo umletea wasiwasi na kumnyima uwezo na moyo wa kusubiri mambo makubwa yatokee kwake. 
Watu wote tuko duniani hapa hapa, lakini tunatofautiana sana utajiri tulionao. Kitu kimojawapo kinachosababisha utofauti huu mkubwa ni jinsi tunavyofikiri na mtazamo tulionao juu ya ukweli wa rasilimali zilizopo hapa duniani. 

Matajiri wao uamini katika ukweli kwamba fikra za binadamu ndizo uzaa vitendo na vitendo uzaa matokeo, ambayo ni pamoja na pesa. Kwa vyovyote vile ukifikiria kupata pesa kiasi fulani lazima ufikirie kitu cha kufanya ambacho ukikifanya kitakuletea pesa zaidi ya ile uliyokuwa unahitaji.
Uzuri wa matajiri ni kwamba, wao hufikiria na kuiona pesa kwenye akili yao tayari kabla ya kuishika au kuipata. Maskini wao hufikiria na kuona uhaba ndani ya akili yao kabla ya kupata pesa. 

Kwakuwa maskini wao hufikiria uhaba kwanza kabla ya kitu kingine, ndiyo maana uishia kufanya kazi ndogo ndogo na vitu vidogo vidogo, ambavyo mwisho wake umpatia pesa kidogo (haba) zinazolingana na uhaba alioufikiria mwanzoni kwenye akili yake. Kwa maana nyingine watu maskini pesa kidogo wapatayo, huifikiria mapema kabla hata ya kuanza kazi ya kuitafuta. 

Namba mbili: Matajiri wao huona fursa mbele yao, wakati maskini wao uona matatizo tu mbele yao. 

Mfano mwalimu mmoja alifundisha wanafunzi darasani, lakini mwisho wake wanafunzi wengi wakashindwa vibaya sana wakalazimika kukaririri darasa. Mwalimu huyu alianza kulalamika na kusononeka. Mara akafikiria kuwa darasa hilo yawezekana lina wanafunzi ambao hawana uelewa wowote ni wabovu wa kufikiri. Mwalimu mwingine aliposikia na kujionea hali halisi ya kushindwa kwa wanafunzi hawa, akaona fursa. 

Baada ya kuona fursa hiyo, akatunga kitabu cha mwongozo wa “jinsi ya kufauru mtihani na akatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kulipia na kupata masomo ya ziada. Kitabu pamoja na masomo ya ziada kwa wanafunzi ni vitu vilivyompatia pesa nyingi wakati mwalimu huyo mwingine aliendelea kulalamika huku akiandamwa na umaskini wake kama kawaida. Walimu hawa wawili wanawakilisha makundi mawili ya watu—maskini na tajiri ambao tofauti zao ni fikra tofauti kwa kitu kile kile. 

Namba tatu: Matajiri wao hununua vitegauchumi ambavyo baadae uwatengenezea faida na faida hii wao huiwekeza tena na tena. Kitendo hiki cha kurudisha faida kwenye vitegauchumi kila mara, uwapa fursa ya kuifanya faida waliyoipata kuzaa pesa nyingine zaidi. 

Namba nne: Matajiri wao hujali sana kuwa na mtandao wa watu waliofanikiwa. Maskini wao upenda kukaa peke yao, kufanya kazi peke yao Matajiri huona umuhimu sana wa kuwa na watu waliofanikiwa.
Unapokuwa na mtandao wa watu waliofanikiwa unapata nafasi ya kusikiliza simulizi zao za mafanikio, na wakati mwingine wanapata kukwambia njia sahihi walizotumia kufanikiwa. Mambo yote mazuri unayojifunza kutoka kwao, ukufanya na wewe upende na kuanza kufanya kama wao. 

Namba tano: Matajiri wao pesa huwafanyia kazi wakati watu maskini hufanyia kazi pesa. Maana yake ni kwamba, maskini wanafanya kazi kwa niaba ya pesa na kwa upande wa pili pesa inafanya kazi kwa niaba ya tajiri. Kinacholeta tofauti hapa ni kwamba kwakuwa tajiri pesa inamfanyia kazi, anakuwa na muda wa kufanya vitu vingine vingi ndani ya masaa 24. 

Maskini yeye anafanya kila kitu mwenyewe, kwasababu anaogopa kutumia pesa isije ikaisha—muda wote anajihami pesa isiishe, ingawaje mara zote imekuwa ikiisha bila kujali ubahili wake.
Tatizo la kufanya kazi mwenyewe, ni kwamba unatakiwa kufanya kazi muda wote wa Maisha yako, kwani siku ukiacha pesa nayo inakatika. Ndiyo, maana inakuwa vigumu kusafiri au kufanya kitu chochote kile nje ya hiyo kazi.
Maisha ya namna hii si mazuri hata kidogo. Tunahitaji kufanya kazi ambazo mwisho wake zinatupatia mazingira ya kuwa na uhuru wa kuchagua mambo mbalimbali tunayoyapenda. 

Jaribu kutafakari baada ya kusoma makala hii, vuta picha ya maisha yako binafsi na uone kati ya makundi hayo mawili—maskini na tajiri wewe uko wapi na unaelekea wapi hata kama ni miaka 10 ijayo usijali, ilimradi tu una malengo mahususi.
Ukisha pata picha amua unataka kukaa katika kundi lipi. Maamuzi yoyote utakayokuwa umeamua yasimamie na usilalamike hata siku moja. Ikitokea ukaona upande uliochagua kuishi haukufuraishi tena, basi fahamu kwamba wewe unao uamuzi wa kuhamia upande ambao unakidhi matarajio yako, kwani kikubwa katika maisha ni Amani na furaha. 

Makala hii imeandikwa na Cpyridion Mushongi wa MAARIFA SHOP.

Mar 20, 2017

Tumia Mbinu Hizi Kubuni Jina La Biashara Yako.

No comments :
Roho kubwa katika biashara ni jina la biashara yako. Watu wengi wamekuwa wakikurupuka katika kuanza kufanya biashara ila wamekuwa wakisahau ya kwamba kitu ambacho kinaibeba biashara kwa asilimia kubwa ni jina la biashara. 

Wengi wao wamekuwa wakishirikiana jina la biashara kama ni sehemu ya kawaida sana.  Lakini ninachotaka kukwambia haijalishi ni biashara ya aina gani ambayo unafanya hakikisha ya kwamba jina la biashara linachukua kipaumbele. 

Hivyo ili kuonyesha ya kwamba unaipenda biashara yako hakikisha inaendana nami siku ya leo kwani nitakueleza kiundani kuhusu mbinu itakapotimia katika kubuni jina la biashara yako.

Bila kupoteza wakati zifuatazo ndizo mbinu za kupata jina la biashara yako.

1.Jina ni lazima liwe fupi.

Imeshauriwa ya kwamba katika kubuni jina la biashara ni lazima uhakikishe unapata jina ambalo ni fupi.  Kwani kuwa na jina refu katika biashara yako huwafanya wateja wako waweze kulishau kwa urahisi.

Pia ni vyema jina hilo ambalo utalitumia liwe ni rahisi kutamkika. Na kwa kuongezea tu ni kwamba katika kubuni jina la biashara yako ni vyema ukahakikisha jina unalolitumia lisizidi maneno matano. Kwa mfano kuna mama mmoja yeye huwa anauza mkaa hivyo banda lake ameamua kuliita " mkaa plaza" hivyo hata wewe  jaribu kuchagua jina ambalo ni fupi pia ni rahisi kutamkika.

2. Hakikisha ni jina linalo akisi kile unachokifanya.

Katika kitu ambacho unatakiwa kuweza kukifahamu kila wakati ni kuhakikisha unachagua jina ambalo linaendena na kile ambacho unakifanya.  Kama unauza nguo basi hata jina liwe katika maahadhi ya biashara hiyo, hata pale mtu anapolisikia iwe rahisi kujua ni biashara gani ya biashara ambayo unaifanya.

Jina linalogusa hisia za watu

Moja kati ya njia bora ya kupata wateja katika biashara yako, ni kuipa biashara hiyo jina ambalo litagusa hisia za wateja wako. Kufanya hivyo kunamfanya mteja wako ajihisi ni sehemu ya biashara yako. Kwa mfano hivi hajawahi kuona mteja fulani akikosa kinywaji fulani ambacho amezoea kunywa hughairisha kabisa?  Bila shaka umewahi kuona aina hii ya mteja. Hapa ndipo ninapozungumzia ya kwamba mfanye mteja kuwa sehemu ya biashara yako kwa kutoa huduma bora na kwa wakati sahihi ili kugusa hisia zake.

Jina la kipekee

Hupaswi kunakiri majina ya biashara nyingine.Chagua jina la kipekee ambalo litakutambulisha wewe na biashara yako.Kuipa biashara yako jina la biashara nyingine inaweza kuleta athari kwa biashara yako kwani unaweza kuwa unaitangaza biashara ya mtu mwingine bila kujifahamu hususani kama biashara ya mtu huyo imekuwa kubwa kuliko yako. Kwani hata huyu mwenye biashara yake Atasema wewe ni tawi lake.  Hivyo epuka mfanano wa majina.

Lakini nimalize kwa Kusema ya kwamba biashara bora huenda sambamba upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati sahihi na uwepo jina lililo thabiti la kibiashara.

Ndimi afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com

Mar 17, 2017

Tumia Mbegu Bora Ukuze Kipato Chako.

No comments :
Leo tunaendelea na umuhimu wa kutumia mbegu bora kwa mkulima yoyote anayetaka mafanikio ni lazima atumie mbegu bora ili kuyaendea mafanikio. Mbegu bora ndio msingi wa mafanikio kwa mkulima.
Naomba bila kupoteza muda tuangalie utofauti uliopo kati ya mbegu ya kawaida (Open pollinated varieties OPV) na mbegu chotora (Yaani Hybrids seeds) na ni nini faida yake kwa mkulima akishajua tofauti hizo.
Kwanza katika uotaji,mbegu ya kawaida ina husua sua katika uotaji yaani uotaji wake ni shida lakini mbegu chotora zina uhakika mkubwa sana wa kuota na mkulimahupotezi pesa yako ukinunua.
Ukichunguza kwa kina utagundua ndiyo maana mbegu nyingi chotara ukiuziwa uliza kabisa kuna mbegu ngapi humu ingawa zingine zimeandikwa idadi ya mbegu. Hiyo yote inaonyesha uhakika wa mbegu hizo.


Ustahimilivu wa magonjwa,Mbegu chotara huwa zina vumilia magonjwa yaani hazishambuliwi ovyo na magonjwa ukitofautisha na mbegu za kawaida hushambuliwa kirahisi na magonjwa.
Ubora wa bidhaa, mbegu chotara huwa na ubora zaidi baada ya kuvuna ukitofautisha na mbegu ya kawaida. Ndio maana wakulima wengi wenye mafanikio, hutumia sana mbegu hizi.
Mavuno ya mbegu chotara huwa zina mavuno mengi ukitofautisha na za kawaida. Mavuno haya mara nyingi huwa ni makubwa na kumfanya mkulima kunufaika na kipato atakachokipata.
Pia mbegu chotara hutoa mavuno mengi na yaliyo bora (High yield and quality) lakini za kawaida mavuno kidogo na siyo bora kama ya chotara(Low yield and not quality)
Kwa mfano mbegu ya nyanya FAIDA F1 3169 na FAIDA F1 3104 huweza kuvunwa zaidi ya miezi sita na huzaa matunda mengi sana. 
Hivyo hata katika soko huwezi pambana na mtu aliyelima mbegu za kawaida na aliye lima mbegu chotara, kwa mfano mtu atakaye lima nyanya mfano tanya hawezi fanana na mtu aliye lima FAIDA F1 NTH 3104 au FAIDA F1 NTH 3169.
Pia hata Yule aliye lima FAIDA F1 atauza bei ya juu (mara mbili au mara tatu zaidi) kuliko aliye lima nyanya ya kawaida, kwa kuwa zina ubora ulio tofauti. Kwa hilo hiyo mkulima hawezi kupata hasara kirahisi.
Naomba sana utambue hivi ili uweze kuingia katika kilimo na ukapata matokeo chanya, hutakiwi kukurupuka. Kaa chini, utulie, fanya uchunguzi wale wanaofanikiwa kwenye kilimo wanafanya nini cha ziada.
Kilimo cha manufaa hakiendeshwi kwa mihemuko au kwa whats app. Unataka kulima na umelenga kupata matokeo mazuri na hujui wapi pa kuanzia waone wataalamu wa kilimo.
Kazi kwako kwa wewe mkulima unaye taka mafanikio, tumia mbegu bora (Hybrid seeds) zikuletee mafanikio. Tukutane wiki ijayo kwa makala nyingine nzuri ya kilimo.
Wako mtaalamu wa kilimo,
Boniface L Pwele.                       
Kwa msaada zaidi wa kuendesha kilimo chenye  mafanikio, usisite kuwasiliana nasi. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0762567628 au tuma ujumbe kwa barua pepe blugahno95@gmail.com


Mar 16, 2017

Biashara Nzuri Ambayo Unaweza Ukaifanya Na Kupata Faida Kubwa Ni Hii Hapa.

No comments :
Habari za leo,  mpenzi msomaji wa safu hii ya biashara?  Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu ili tuweze kujifunza na elimu hii ya biashara. Andaa ubogo wako ili uweze kupokea mambo muhimu ya kukusaidi kufanikiwa.
Moja ya maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa sana na wasomaji wetu ni kwamba je, afisa mipango Ben, nifanye biashara gani ambayo itakuwa ina faida kubwa kwangu?
Kama ambavyo nimekuwa nikiulizwa mara kadha wa kadha na swali hilo tena limekuwa likijirudia. Hivyo kwa kutumia dakika chache naomba niweze kujibu swali hilo.
Jambo la msingi sana ambalo unatakiwa kulizingatia ni kwamba  kila biashara ambayo unaiona machoni mwako ina faida na hasara zake,  Nimeanza kwa kusema hivyo kwani watu wengi wamekuwa wakiaangalia upande mmoja tu wa kupata faida tu.

Lakini ukweli ambao unatakiwa kuujua mapema ni kwamba kabla ya kuingia katika biashara tambua ya kwamba katika biashara hiyo kuna faida na hasara, hivyo uwe tayari kubeba mambo hayo mawili pindi yatakapojitokeza.
Biashara yenye faida huanza na wazo,  wazo ambalo limekuwa likitokana na mfanyabiashara kabla ya kuanza kufanya biashara husika. Wazo hilo hujengwa na misingi ya kina ya kufanya uchunguzi yakinifu juu ya biashara hiyo.
Usipofanya uchunguzi wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuifanya ipo siku utalalamika. Ila tunashauriwa ya kwamba katika kufanya uchunguzi wa kutosha ni lazima ujikite katika kuangalia eneo ambalo utaiendesha biashara hiyo.
Wakati unangalia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara, angalia eneo ambalo:-
Eneo linalofikika kwa urahisi.
Angalia eneo ambalo lina uwingi wa mkusanyiko mwingi wa watu tofauti tofauti.
Tafuta eneo ambalo kuna upatikaji wa huduma za kijamii, kama vile ukaribu wa benki, umeme, maji na mengineyo mengi yatakoyokusiadia kukua kibiashara.
Angalia eneo ambalo lipo karibu na wafanyabiashara wengine. Kwa mfano, kama unafanya biashara ya mashati  basi chagua eneo ambalo kuna mfanyabiashara anauza tai. Kufanya hivi kuna msaidia mteja kutopata tabu ya kuhangaika kupata bidhaa fulani.
Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba katika kufanya uchunguzi wa eneo la kufanyia biashara ni vyema unafanya uchunguzi kwa kuangalia hasa ni yapi mahitaji ya watu.  Kisha wewe uweze kuyasogeza mahitaji hayo karibu.
Mwisho naomba ujiulize hivi,  ni wapi ambapo imepanga kufanya biashara h?  Na watu wana changamoto zipi nawe umekuja suluhisho lipi? Ukipata majibu hayo huo ndio utakuwa mwanzo wa kujua  biashara gani italipa eneo hilo na hatimaye kupata faida.
Hivyo niseme hivi, biashara inayolipa na kutoa faida kubwa ni ile biashara ambayo umeshaifanyia uchunguzi wa kutosha na kujua soko lake liko wapi na lina ukubwa gani. Hiyo ndiyo biashara inayolipa.
Endelea kujifunza maisha, mafanikio na biashara kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku, usikose kumshirikisha na mwingine ili aweze kupata maarifa haya muhimu.
Afisa mipango Benson Chonya,

Mar 15, 2017

Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Umeanza Na Kidogo Ulichonacho.

No comments :
Yapo mambo ya lazima kuyajua na kuyafatilia kwa ukaribu sana kama unaanza na kidogo ulichonacho ili kuweza kufikia mafanikio. Bila kuzingatia mambo hayo uwezekano wa kufanikiwa utakuwa ni mgumu.
Kwa yeyote anayezingatia mambo haya haijalishi unaanza na kidogo kiasi gani, mafanikio yataanza kuonekana mara moja kama utachukua hatua. Mambo haya yanazingatiwa sana na kila anayeanza na kidogo hadi kufanikiwa.
Yafuatayo Ni Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Unaanza Na Kidogo Ulichonacho.
1. Kuwa kwenye mwendo.
Siri kubwa ya kuanza na kidogo ulichonacho hadi kufanikiwa ipo kwenye kukaa kwenye mwendo au ‘momentum’. Namaanisha nini ninaposema kukaa kwenye mwendo, yaani kuendelea kuchukua hatua kwa jambo ulilolichagua hata kama ni kwa kidogo sana.
Ni bora ukawa unafanya kitu kidogo kidogo, lakini mwisho wa siku utajikuta unasogea kuliko kutulia. Ni bora kuanza biashara hata ndogo kuliko kusubiri ile biashara iliyo kubwa ambayo hunayo. Anza na kidogo ulichonacho ili kikusaidie kuweza kukaa kwenye mwendo.

Anza na kidogo, hadi ufikie mafanikio makubwa.
Kaa kwenye mwendo. Hata kanuni za kisayansi zinatuambia kila kitu kilichoko kwenye mwendo kitazidi au kitaendelea kuwa kwenye mwendo, pengine itokee nguvu nje ya kuzuia. Sasa kwa nini usichukue hatua na kuamua kukaa kwenye mwendo kuliko kusubiri subiri.
Ili kufanikiwa kukaa kwenye mwendo, chagua kitu unachokitaka, kisha kitu hicho kifanye kila siku. Hiyo itakuwa ni njia nzuri sana ya kuweza kukuweka kwenye mwendo wa mafanikio yako. ukifanya kitu hicho kila siku utake, usitake ni lazima utasogea.
2. Maliza kila kitu unachokianza.
Ili uweze kuwa kwenye mwendo vizuri wa kufikia mafanikio yako, jifunze kumaliza kile ambacho unaanza nacho. Kama kila kitu ambacho unakianza hukimalizi, tambua unatengeneza nguvu kubwa ya kukufanya ushindwe kwa baadae.
Kwa vyovyote vile, kila siku jitahidi kumaliza kitu ambacho umejiwekea kufanya. Najua sio rahisi kuweza kumaliza kila kitu ambacho unakianza, kwa sababu vipo vinavyokwama pia bila kutarajia, lakini hiyo isiwe sababu, maliza kile unachokianza.
Kama kuna jambo umelianza, hata kwa macho ya kawaida kama linaonekana ni mlima lianze jambo hilo na kuhakikisha unalimaliza. Weka jitihada zitakazokuwezesha kulimaliza. Mafanikio yanajengwa na wewe jinsi unavyomaliza vitu na sio kuachilia kati.
3. Jenga tabia za kukusaidia kufanikiwa kila siku.
Kinachowangusha wengi kwenye safari ya mafanikio ni tabia zao. Tunapozungumzia tabia ni yale ,mambo ambayo kuna wakati tunayafanya hata bila kufikiria, unafanya tu kwa sababu ya mazoea ya kila siku. Hebu angalia ni mazoea gani yanakuzuia kufanikiwa.
Kwa mfano kuamka asubuhi na mapema ni tabia na pia kuchelewa kuamka ni tabia. Kulalamika ni tabia na hata pia kuwajibika ni tabia. Hiyo haitoshi kutumia pesa hovyo ni tabia na kuweka akiba nayo ni tabia. Ukichunguza zipo tabia nyingi ambazo tunazo.
Unaona mpaka hapo zipo tabia zinazokuangusha na zingine zinakusaidia kufikia mafanikio yako. Hivyo hapa unatakiwa ujue kabisa kwamba kumbe tabia ni lazima kuzijua ili kubadilisha maisha yako na kuwa ya mafanikio. Unapojenga tabia chanya zaidi unajitengenezea mazingira ya kufanikiwa.
4. Tafakari maisha yako.
Badala ya kuwa ‘busy’ muda wote katika kutwa nzima, kuna wakati unatakiwa utenge muda wako kwa ajili ya kutafakari siku yako imekwenda vipi. Ni muhimu kujua ni kitu gani umekifanya. Hapa ni lazima uwe na siku inayokupa faida kila siku.
Ni rahisi kujikuta kutwa nzima ukiwa uko ‘busy’ sana na shughuli hii mara ile nakushindwa kutambua kama kweli unaenda mbele au unarudi nyuma. Lakini kama utajenga tabia ya kutafakari nini ulichokifanya kutwa nzima na kimekusaidiaje itakusaidia kuelewa ni kipi uboreshe.
Unapotafakari juu ya maisha yako itakusaidia kuweza kujua ni maeneo yapi ambayo unatakiwa kuyaboresha zaidi na zaidi na mwisho wa siku utajikuta unazidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye mafanikio yako. Anza mara moja kutafakari juu ya maisha yako bila kuchelewa.
5. Tengeneza utamaduni wa kufurahia mafanikio yako.
Hatua ndogo ndogo unazozipiga kila siku inabidi uziweke wazi kwa kuziona na kisha baada ya hapo anza kusherekea hayo mafanikio ako. Jenga utamaduni wa kuweza kusherekea mafanikio yako. haina maana umefanikiwa halafu unashindwa kujipongeza hata wewe mwenyewe.
Unapokuwa unafurahia na kusherekea mafanikio yako inakusaidia kukupa nguvu na hamasa tena na tena ya kuweza kusonga mbele na kufanikiwa kwa hicho unachokifanya.   Watu wenye mafanikio wanafurahia mafanikio yao hata kama ni kidogo.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,