google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 8, 2021

Fanya Zoezi Hili Kila Siku La Kuboresha Maisha Yako.

No comments :

Lipo zoezi moja la muhimu unalotakiwa ufanye kila siku, ni zoezi unalotakiwa kulifanya kila siku, ina maana zoezi hilo linakutaka wewe ufanye jambo mojawapo  kila siku, ili kuboresha maisha yako yawe safi na salama..

1. Kulala masaa nane.

2. Kula milo, miwili badala ya mitatu.

3. Kutokusema sema hovyo, kutunza kinywa chako kwa faida.

4. Hakuna kuangalia Tv kabisa.

5. Kutokulalamika kabisa.

6. Kutokula vyakula vitamu vitamu.


7. Kumwambia rafiki yako ansante kwa kile alichokufanyia.

8. Kuangalia movie za kufurahisha au kusoma kitabu kama riwaya za kufurahisha.

9. Kuandika mawazo kumi ya msingi ambayo unaweza ukayageuza na yakawa pesa.

10.  Kusoma ujumbe wa neno la Mungu kila siku.

11. Kila unapoamka unatakiwa kujiambia kwamba, leo ni siku ambayo unakwenda kuikoa dunia.

12. Mshangaze mtu mmoja kwa siku.

13. Fanya kitu cha hobi, kitu ambacho kitakwenda kukutoa katika ulimwengu wa kawaida na kukupeleka katika ulimwengu mwingine wa tofauti.

14. Wafikirie watu kumi, ambao watu hao utakwenda kuwashukuru.

15. Wasamehe wote  wale wanaokuudhi.

16. Tenga muda kidogo kuwaombea watu waliojirani na wewe na hata maadui zako wakubwa kimaisha.

17. Tembea kwa miguu, badala ya kutumia usafiri kama gari au pikipiki.

18. Sema hapana kwa kile unachotaka kusema  hapana, na sema ndio kwa kile unachotaka kusema NDIO.

19. Fanya zoezi la kumwambia mtu mmoja kila siku na kwa mwaka mzima kwamba unampenda.

20. Acha kufanya mapenzi na mtu usiyempenda.

21. Fanya mpango wa kuwa na muda na marafiki zako, muda wa kuongea pamoja na kufanya mipango ya kimaisha.