google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 18, 2018

Faida Ya Kutoa Yale Mazuri Kwa wengine Ni haya.

No comments :
Siku zote katika maisha yako kabla hujatenda kitu chochote, kabla hujasema kitu chochote, jiulize kitu unachotaka kutenda au kitu unachotaka kusema je, kitaleta matokeo chanya kwako au hata kwa wengine?
Sio kwa sababu unayo nafasi nzuri ya kutenda au kusema hiyo ikawa na maana kwako ufanye au useme tu hata mambo yanayoumiza wengine. Unatakiwa kuwa makini na kuzingatia ni nini matokea ya kile ambacho unakwenda kutenda au kukizungumza. Kwani kila wakati tunakumbushwa ya kwamba ni heri kufikiri kabla ya kutenda.
Nisisitiza suala la kufikiri kabla ya kutenda kwa sababu wengi wetu hukurupuka katika kutenda mambo fulani, na kufanya hivyo kumekuwa chanzo cha kutotimiza jambo hilo. Hivyo kwa jambo lolote kabla ya kulitenda au kulisema ni heri kulitakari mara dufu zaidi.

Pia kufikiri kabla ya kutenda ni muhimu kwa sababu ni dhahiri wapo watu ambao moja kwa moja utawaumiza, kama utatenda au kusema maneno  hasi, hata kama hujui jinsi unavyowaumiza. Pia uelewe wapo watu utakaowaponya kama utaamua kusema au kutenda matendo chanya ambayo yana msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla.
Kila wakati, unayo nafasi nzuri sana ya kutoa mazuri katika dunia, ingawa uamuzi ni wako. Acha kutenda au kusema mara moja kile kinachokujia kichwani mwako, Jipe muda wa kukifikiri kitu hicho na kujua ni nini matokeo yake katika maisha yako na ya wengine.
Kuanzia leo jifunze kutoa yale mazuri katika hii dunia jenga utamaduni wa kutoa yale matendo au maneno mazuri iwe sehemu ya utamaduni wako. Ukifanya hivyo dunia itakupa mazuri pia na utafurahia  maisha yako kutokana na mazuri unayoyatoa.
Simama imara katika kuhakikisha  unalitenda hili vyema kila wakati. Simamia katika ukweli, ili kutengeneza amani ya moyo wako na mioyo ya watu wengine. Usiwe kichocheo katika kusababisha watu wengine wakose furaha, bali jitahidi kuwa katika kusimamia ukweli na haki daima. Kumbuka sana TOA YALE MAZURI KATIKA MAISHA YAKO,  GIVE GOODNESS TO LIFE, ukifanikisha hili furaha na mafanikio vitakuwa upande wako.
Mwisho tuweke nukta kwa kusema ya kwamba wewe ni matokeo ya mafanikio ya watu wengine kama utaamua kuwa mkweli kwa kutakari kabla ya kusema na kutenda utafanya vichocheo vya mafanikio kwa watu wengine.
Imeandaliwa na mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,

Sep 12, 2018

Nguvu Kubwa Tatu Za Kukusaidia Kufanikiwa.

No comments :
Sijui sana kama unajua una nguvu kubwa sana za kuweza kukusaidia kufanikisha jambo lolote unalo lihitaji katika maisha yako. Nguvu hizo unazo, bila kujali unajua kivipi au hujui lakini nguvu hizo zipo ndani mwako.
Ushahidi wa kutosha upo, unaonyesha nguvu hizo zipo, ndio maana, chochote unachokitaka ukiamua na ukapanga kweli, unaweza kukipata au maisha yako yapo hivyo yalivyo kutokana uwezo ama matumizi ya nguvu zako.
Mpaka hapa naona unashangaa na unajiuliza sasa nguvu zangu nitazijuaje au zipo kwenye nini? Sikiliza nguvu zako kubwa ulizonazo, zipo kwenye mambo makubwa matatu mabao yapo ndani ya uwezo wako mwenyewe.

1. Mawazo uliyonayo.
Nguvu zako nyingi ulizonazo na ambazo zinaweza kufanya kitu chochote ukitakacho, zinaanza kwenye mawazo yako kwanza. Mawazo yako  yana nguvu na kuumba kitu chochote unachokitaka na kikaonekana kwa nje.
Hebu jiulize ni kitu gani ambacho hakijianzia kwenye mawazo? Kila kitu unachokiaona kipo duniani kwanza ni matokeo ya mawazo. Unapoana gari au majumba  makubwa hayo ni mawazo ya watu. Ukizingatia matumizi ya mawazo vizuri, utafanikiwa sana.
2. Maamuzi uliyonayo.
Nguvu nyingine kubwa uliyonayo ndani mwako ambayo ukiitumia vizuri itakupa chochote ukitakacho ni maamuzi uliyonayo. Maamuzi yako ni ya muhimu sana katika kufikia mafanikio yako unayoyataka.
Angalia ni kitu gani unachokipata bila kuwa na maamuzi, utaona karibu kila kitu baada ya kuwa kwenye mawazo yako ni lazima kwanza ukifanyie maamuzi ambayo yatakupelekea ufanye kitu kile. Hakuna mafanikio utakayapata bila kuamua.
3. Hatua ulizonazo.
Umeona mawazo ulionayo na maamuzi uliyonayo ni mojawapo ya nguvu kubwa uzilizona ndani mwako za kimafanikio. Lakini hata hivyo nguvu hizo haziwezi kufanikiwa bila kuchukua hatua. Inabidi ifike mahali uamue kuchukua hatua ili kufanikiwa.
Hatua unazozichukua ndizo zitakazokufanya uweze kufanikiwa. Hata uwe na mawazo mazuri na maamuzi mazuri vipi lakini itakulazimu uweze kuchukua hatua ili hatua hizo zikuletee uhalisia wa kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Kumbuka, mawazo uliyonayo, uamuzi unaouchukua na hatua unazozichukua ni moja kati ya nguvu kubwa sana za kimafanikio ambazo unatakiwa uzitumie ili uweze kufanikiwa. Kwa kumiliki kwako nguvu hizo utakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



.



Sep 11, 2018

Njia Nne (4) Za Kuboresha Maisha Yako Sasa.

No comments :
Kwa jinsi unavyobadili mtazamo wako, ndivyo unavyozidi kujikuta ukibadilisha na maisha yako pia. Maisha yako ni lazima yabadilike kama una badili mtazamo wako kila wakati, hilo halina ubishi.
Kuna wakati katika maisha tunajirudisha nyuma sana kwa sababu ya kuwa na mitazamo finyu, mitazamo hasi ambayo haitusaidii. Ili kufanya maisha yako kuwa bora na ya mafanikio unalazimika kubadili mtazamo wako.
Katika makala haya, tutakupa njia muhimu ambazo ukizitumia, kwanza zitakusaidia kubadili mtazamo wako , na pia si hivyo tu zitakusaidia kubadili na kuboresha maisha yako;-
1. Fanya mambo yako kwa utofauti.
Mbinu bora ya kuboresha maisha yako sasa ni kufanya mambo yako kwa utofauti. Kama ni kazi fulani ifanye kwa utofauti. Kama ni kutembelea eneo fulani ulilolizoea hebu libadilishe na kwenda sehemu nyingine.
Hali zote zile za mazoea ambazo umekuwa ukiziishi naomba uzibadilishe na kuzifanya kwa utofauti. Ukifanya hivyo utashangaa kuona maisha yako yakibadilika na kuwa ya  tofauti na mafanikio.

Badili maisha yako kila siku.
2. Jitoe kwa ajili ya wengine.
Unaweza pia kuboresha maisha yako kwa kuamua kujitoa kwa ajili ya wengine. Unapojitoa kwa wengine hapa unamaansha usitegemee kupata kitu chochote kutoka kwao. Wewe jitoe kwa ajili yao.
Ni njia au mbinu ambayo itakuimarisha na kukufanya hata kazi zako mwenyewe utakuwa unazifanya kwa ukamilifu mkubwa sana. Ukikubali kujitoa basi utakuwa umeweza kuboresha maisha yako kwa sehemu kubwa sana.
3. Fanya mazoezi.
Upe mwili wako mazoezi. Unyumbue mwili wako huko na huko. Ni njia nzuri ya kuweza kuipa akili yako afya ya mwili, hali ambayo itakupelekea wewe uweze kufika mahali ukaboresha maisha yako kiafya pia.
Si rahisi sana kwa mtu ambaye anafanya mazoezi karibu kila siku kuweza kushambuliwa na vitu kama magonjwa ya hapa na pale. Unaweza ukaendelea kuboresha maisha yako kwa njia hii kwa utofati.
4. Furahi na marafiki zako.
Maisha mazuri na maisha yalioyoboreshwa ni pamoja na kuwa na rafiki zako, mkafurahi pamoja. Kama kuna rafiki wa zamani ambaye hujawasiliana nae muda mrefu mtafute na uongee nae.
Unapokuw na marafiki watakusaidia kuweza kubadilisha maisha yako kwa sehemu kubwa kutokana na mwazo yao ambayo wanakuwa wanakupa. Hivyo, marafiki pia wanawez kuboresha maisha yako.
Ukumbuke kuwa kufanya kazi kwa utofauti, kujitoa kwa wengine, kufanya mazoezi na kufurahia maisha na marafiki ni moja ya mambo machache ambayo yanaweza kukufanya ukaboresha maisha yako.
Fanyia kazi hayo na endelea kujifunza kupitia dirayamafnikio.blogspot.com kila siku na maisha yako yatabadilika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano;  +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com



Sep 4, 2018

Hiki Ndicho Kitu Kiinachoongeza Thamani Yako Sana.

2 comments :
Kwa kawaida ipo hivi, ili uweze kutengeneza mafanikio ni lazima uweze kutoa thamani kwa uhakika. Kila mtu atakapoangalia kazi yako au kile unachokifanya ni lazima aone ubora na utofauti mkubwa juu ya kitu hicho ukifanyacho.
Inawezekana ukawa unajua thamani ni hali ya kuwa katika ubora, hadi kuwafanya wengine wakutamani wewe au watamani huduma yako unayoitoa.  Kitu cha kujiuliza je, unajua thamani ya kitu chochote inatengenezwa na nini?
Hapa kwenye swali hilo juu ndipo wengi wanaanza kushindwa, wanakuwa ni watu kweli ambao wanataka thamani kubwa katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hawajui hiyo thamani ambayo itawapa mafanikio inapatikana vipi na wapi.
Thamani yoyote unayoitafuta kwenye maisha yako uelewe, imejificha kwenye muda. Upo ulazima wa wewe kutumia muda wa kutosha ili kutengeneza thamani yako. Kama unakimbilia kutengeneza thamani ndani ya muda mfupi, huo ni uongo.

Waangalie watu ambao wana thamani kubwa sana na kwa maana hiyo pia watu hao wana mafanikio makubwa. Watu hao ukiwaangalia walitumia muda mwingi sana katika kutengeneza thamani hiyo ambayo imewapa mafanikio hayo mafanikio makubwa.
Ukiona mtu thamani yake inaonekana ni kubwa lakini imepatikana kwa muda mfupi, nikwambie tu thamani hiyo ni ya muda mfupi na wakati utafika thamani hiyo itatoka na yale mafanikio yataporomoka na ushindwe kuamini ni kitu gani kilitokea.
Kwa hiyo kama unaona maisha yako yameshuka au maisha yako hayasogei kama vile utakavyo wewe, amua kupandisha thamani yako. Kwa bahati mbaya sana thamani yako hiyo haiji kwa bahati mbaya bali ni kwa wewe kujituma na kujipa muda.
Kweli ukidhamiria kuongeza thamani yako na kuwa mtu wa tofauti hilo linawezekana. Anza leo kubadilisha thamani yako kwa kusoma vitabu sana vya mafanikio na hilo litaleta mabadiliko makubwa sana ya maisha yako na kwa kiasi kikubwa.
Ukumbuke thamani uliyonayo inabadili maisha yako sana.  Hakuna ambaye anashindwa kwenye maisha au atashindwa kupata pesa kama mtu huyo hana thamani kubwa ndani yake. Mafanikio ni lazima kama ndani yako una thamani ya kutosha.
Usikubaki kuishi kizembe, kila wakati jaribu kujiuliza ni kitu gani nifanye ili niongeze thamani yangu na kuwa bora na bora. Kwa kukijua kitu hicho na kukifanya, basi unakuwa upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa kwako.
Kitu kinachoongeza thamani yako zaidi ni matumizi ya muda. Weka hili akilini na fanyia kazi kila wakati. Kwa kufanya hivyo hapo utafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa ujumla.
Kama unataka mafanikio ya muda mrefu na wewe hakikisha unatengeneza au ndani mwako una thamani ya muda mrefu sana. Thamani hiyo kama nilivyosema haipatikani hivi hivi tu, ipo kwenye muda, ni lazima kujipa muda wa kutengeneza thamani hiyo.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035,

Sep 3, 2018

Mbinu Muhimu Itayokufanya Uondokane Na Msongo Wa Mawazo.

No comments :
Msongo wa mawazo ni ile hali ambayo humpata mtu kisha kumpelekea mtu huyo kuwa na mawazo mengi kupita kiasi. Mawazo haya yanaweza kuwa chanzo chake mahusiano, kazi,elimu, magonjwa, biashara, fedha na mengineyo mengi.

Pamoja na kuweko kwa vyanzo hivyo au visababishi hivyo vya msongo wa mawazo inaelezwa kuwa msongo wa mawazo mara nyingi husababishwa na mahusiano, usigune huo ndio ukweli, pia leo sipo kwa ajili ya kuzungumzia msongo wa mawazo utakanao na mahusiano bali nipo hapa kuzungumzia namna ambavyo utaweza kuondokana na msongo wa mawazo.

Nataka kuzungumzia namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kwani athari ya kuwa na msongo wa mawazo ni kubwa mno. Tumekuwa tukiwaona watu wakishindwa kufanya kazi wazifanyazo kwa ufanisi eti tu kwa sababu watu hao wana msongo wa mawazo.


Lakini athari iliyo kubwa kupita zote wapo baadhi ya watu ambao huchukua hata maamuzi ya kujaribu kujiua kwa sababu tu mawazo  waliyonayo yamewazidi  akilini mwao.  Lakini athari nyingine ya msongo wa mawazo ni kwamba ni chanzo cha magonjwa mbalimbali. 

Swali ambao huwa najiuliza hivi ni kwa nini watu hao hufikia uamuzi huo wa kutaka kujiua? Hivi ni kweli watu hao hawajui namna ya kuweza kuondokana na hali hiyo ya msongo wa mawazo? . Kwa majibu yangu ya haraka haraka nikagundua yawezekana ni kweli watu wengi hawajui namna ya kuondokana na msongo wa mawazo.

Kwa kuwa hawajui basi naomba niwape mbinu hii maridhawa ambayo itawafanya watu hao waweze kujifunza hapa namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kama ifuatavyo: 

·  Unatakiwa kutafuta majibu ya changamoto iliyokufanya uwe katika msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo sababu yake kubwa hutokana na changamoto fulani iliyokukabili katika eneo lako fulani. Hivyo kila wakati usiwe ni mtu wa kunung'unika, au kuamua kuchukua uamuzi fulani ambao ni mbaya utakaokufanya kuyagharimu maisha yako kwa namna moja ama nyingine, bali jifunze kutafuta majibu chanya yatakayokufanya uondokane katika hali  hiyo ya msongo wa mawazo.

Kutafuta majawabu ya changamoto zinazomkabili mtu, humsadia mtu huyo kwa namna moja ama nyingine kutengeneza amani ya moyo, na mtu anapokuwa na amani ya moyo huwa ni mtu chanya kwa kuwa mara nyingi hujiwekeza katika mawazo mazuri yatakayomsadia kufanya mambo yenye tija na si vinginevyo.

Mwisho naomba nitamatishe kwa kusema mara zote epuka msongo wa mawazo kwa kuzingatia njia hii ambayo nimeieleza hapa kwani msongo wa mawazo huwa una athari kubwa sana katika maisha ya kila siku kimwili na kifkra pia.

Kwa leo naomba niishie hapa tukutane tena panapo majaliwa,

Ndimi: Benson Chonya.

Sep 2, 2018

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuondokana Na Majuto Uliyonayo Na Kuishi Maisha Ya Amani Na Furaha.

No comments :
Wengi wetu huwa tunajuta sana. Mara nyingi tunapokumbana na kushindwa kwetu au mambo yetu kukataa kwenda kama tulivyotarajia, huwa tunajuta sana. Nini yaweza kuwa hasa sababu ya kujuta kwako sana na pengine huweza kupelekea wewe mwenyewe kuanza kujiona kama hufai vile.
 
Kujuta huweza kujitokeza pale ambapo hukutenda itakiwavyo kwa kile ulichokuwa ukikifanya. Kujuta sio kubaya kama ni kwa ajili ya kurekebisha makosa. Kuyajua makosa hayo ina faida kwa maana kwamba sasa unaweza kubadilika na kuwa tayari kwa ajili ya maendeleo au kufanya vizuri zaidi. 

Huku ni kujuta kwenye kujenga na kwa hali hiyo hatupaswi kuita hali hii kujuta. Kama tutajilaumu kwa kushindwa, bila kujali kama ni kosa letu au hapana, hapo ndipo tunapoita kujuta. Kujuta siyo kule kujua kwamba, tumekosea na pengine ni uzembe, lakini tukawa tayari kujifunza.

Kihoro cha mawazo kina uhusiano na mambo yaliyopita. Ili mawazo hayo yaweze kudumu hayana budi kubaki ndani ya moyo wako. Kila siku unayoishi, yaani leo, ndiyo siku yako kubwa ya kujisahihisha. Ukiruhusu mawazo yako yakutawale, basi utakuwa umejilimbikizia kikwazo kikubwa dhidi ya maendeleo yako.

Kwa kadiri utakavyoendelea kujuta sana bila kujifunza kitu, ndivyo utakavyojikuta maisha yako unazidi kuyaharibu. Hii inatokea kwa sababu unakuwa hufanyi kitu kipya, unakuwa umeganda kwenye kujuta tu. Unawezaje kupambana na majuto haya unayokutana nayo mara kwa mara katika maisha yako na ili yasikuumize tena? 

1. Kuwa na muda wa maamuzi

Kufikia sasa utakuwa umeshajielewa wewe ni nani na unataka kuzoea nini badala ya kile ulichokuwa umekizoea. Ukishajua unachokitaka fanya kile ambacho unapaswa kufanya kama vile, kubadilisha imani. Njia yenye nguvu ni kuvifanya vitu ambavyo una uwezo wa kuvifanya. Unachokifanya leo kinaathiri maisha yako ya baadae na kitakusaidia usijute baadae.



2. Jiulize sana maswali.
 
Kile ukifanyacho ni kupambana kwa ajili ya kubadili unavyojisikia. Unataka kujisikia vizuri kwa nini uhisi majuto ndani yako na kufadhaika. Kama una utashi wa kweli wa kutaka kuondokana na kujilaumu, lazima upitie zoezi zima la kujiuliza maswali mazito.

Hii ni aina mojawapo ya kubadili mwelekeo wa ubongo wako. Kwa yale yote unayoyajua unaweza kuwa unayaalewa mambo pengine kimakosa. Endelea kujiuliza maswali ili kuweza kugundua mambo ambayo ulikuwa hujayaona na ambayo yanakufanya uumie na kujuta.

3. Badilisha picha katika mawazo yako.

Mawazo kuhusu mwenendo wako mbaya au upumbavu wako husababishwa na picha ambazo uliziunda ndani ya akili yako.  Unaendelea kujiadhibu, kwa kila wakati kwa kuziona taswira na kukurudisha nyuma ulikotoka. Unavyozidi kukumbuka ya kale, ndivyo unavyozidi kuleta majuto.
Una udhibiti juu ya yale tu yanayojionyesha kwenye fikira zako. Unaweza kufanya hivyo kwa kupandikiza mawazo mapya na mazito juu ya yale ya zamani, ambayo umeyagandisha kwenye ubongo wako. Inahitaji nidhamu na kujitoa mhanga, tena ni jambo la maana ili kujiondoa kutokana na uozo uliopita.

4. Geuka na fanya mabadiliko

Kama ulichokuwa umekifanya kilikuwa kibaya achana nacho. Badilisha mwelekeo. Jipe ahadi mwenyewe kwamba hutarudia tena. Jisamehe kwa ujinga wako. Kama umewakosea wengine au umewaumiza waombe msamaha, kisha songa mbele.

Fanya kazi na fanya vitu ambavyo vitakufanya ujisikie vizuri na kurudisha kujiamini kulikokuwa kumepotea. Hujacheleweshwa kuanza upya wala usijali kuhusu umri wako. Daima kuna kitu ambacho unaweza kukifanya ili kuyaweka maisha yako na ya wengine sawa.

Kumbuka, ni lazima wote tuathiriwe na aina mbili za maumivu, maumivu ya nidhamu na maumivu ya kujuta. Tofauti ni kwamba nidhamu ina uzito kidogo na majuto yana uzito mkubwa. Hivyo, ndivyo unavyoweza kuondokana na majuto uliyonayo na kuishi maisha ya amani na furaha.

Nakutakia mafanikio mema katika maisha yako, karibu sana na endelea kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza mambo mazuri yatakayokuwa yanakujia.

TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

Sep 1, 2018

Rafiki Sahihi wa Kukupa Mafanikio Ya Kweli Ni Huyu.

No comments :
Mara nyingi marafiki wanaokuzunguka  wanao mchango mkubwa sana wa kujenga au kubomoa kwa kile unachokifanya, hii inategemea na aina gani ya marafiki ulionao.
Pia marafiki hao ulionao wewe ndiye unayemua na  kuchagua ni yupi rafiki sahihi wa kushikirikiana, naye na yupi si wa kushirikiana naye? Nimesema hivyo kwa sababu wapo marafiki ambao wao kazi yao kukatisha tamaa wengine, lakini wapo wengine wao kazi kutoa ushauri maridhawa wakufanikiwa kwao  na hawa ndio wa kuwang`ang`ania.  
Hivyo mara nyingi katika maisha yako jifunze kuchagua marafiki sahihi wenye mchango sahihi katika mambo unayoyafanya. Na miongoni mwa rafiki muhimu unayepaswa kumng`ang`ania katika safari yako yote ya mafanikio hapa duniani ni yule rafiki ambaye mara nyingi anakueleza ukweli pasipo kukuonea aibu.

Rafiki huyu ndiye muhimu sana na kama unaye usimuache aende zake kwa sababu miongoni mwa tabia walionazo watu wa aina hii ni kwamba wao husema ukweli daima. Hata pale utakapokuwa umefanya jambo fulani ambalo wewe utaliona ni zuri, kwa kuwa yeye ni mkweli basi yeye hata ona haya kukosoa ili uweze kufanya vizuri zaidi na kwa ubora zaidi.
Mara nyingi wengi wetu tunakosa aina hii ya marafiki kwa sababu huwa tunahisi labda wanatuonea wivu kuendelea kusonga mbele kwa vitu ambavyo tunavifanya kumbe ukweli haupo hivyo, bali marafiki hawa kucheza sehemu kubwa ya maisha yetu kwa kuwa wao hutueleza ukweli ni jinsi gani tunakiwa kuishi na kufanya mambo yale ya msingi.
Lakini pia tunashauriwa ya kwamba kukaa na marafiki ambao wao kazi yao ni kusifia tu ya kile tukifacho, marafiki wa aina hii hawafai  kwa sababu hawana mchango wowote ule wa sisi kuendelea kusonga mbele bali kuturudisha nyuma hivyo hutuna budi kuwaepuka.
Marafiki wa aina hii huwa na  maneno  mafupi lakini yasiyoleta mabadiliko yeyote yale kwa kile ukifanyacho. Utawasikia wakisema aaah hongera sana, wengine utawasikia wakipaza sauti aaah ndugu yangu umepasua na maneno mengine kama hayo.
Maneno kama hayo siyo mabaya sana hasa pale yapenyezapo maskioni mwetu kwani hufariji sana mioyo yetu na kujihisi tupo sahihi kabisa .
Lakini mimi nafahamu hukuzaliwa kuja hapa duniani kufarijiwa moyo  na maneno ya watu pekee bali ulikuja hapa duniani kwa leo la kutimiza kusudio lako maaalum.
Hivyo ili uweze kutimiza kusudio hilo maalumu hauhitaji watu wenye kuufariji moyo wako tu pekee, bali unahitaji watu sahihi wenye kukufariji pamoja na kukupa ushauri wa kiutendaji kwa kile unachokifanya ili uweze kukufanya kwa ubora zaidi.
Lakini kabla sijaweka nukta kwa siku ya leo  nikuombe kitu kimoja kikubwa chukua walau dakika kadhaa kisha tafakari hivi katika maisha yako unazungukwa na marafiki  wangapi wasemao ukweli juu ya maisha yako ?
Mara baada ya kupata jawabu la swali hilo usiache kichwa chako kipoe bali zama tena katika dimbwi la fikra zako jiulize tena hivi kama hauna aina hii ya marafiki je, hatua gani utakazotumia kuwapata marafiki hawa?
Pia swali la mwisho je, na wale marafiki wasiokuwa na mchango wowote katika maisha yako je,  utawachukulia hatua gani?
Endapo Ukipata majawabu ya sahihi ya maswali hayo ni imani yangu kubwa utakuwa katika eneo sahihi ya kutengeneza njia ikupasayo kuyafikia mafaniko unayoyahitaji kwani utachagua ni mtu wa kuchagua marafiki sahihi kila nyakati.
Asante sana kwa kusoma makala haya, sina cha kukulipa zaidi ya kusema asante sana na nenda kayafanyie kazi yale yote niliyokueleza.
Ndimi: Benson Chonya