google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 31, 2021

Kitu Hiki Kinaweza Kubadili Sana Maisha Yako, Ukikitumia Vizuri.

No comments :
Kuna wakati katika maisha unakuwa unajiona hali yako ni mbaya, au anakuwa unaona huwezi kupiga hatua tena na kila kitu kwenye maisha unakuwa unakiona kimeharibika na huwezi kupiga hatua za kukuwezesha kusonga mbele kimafanikio.
Kutokana na mambo yako kwenda hovyo, hakuna ambacho unakuwa unaona kina mafanikio kwako, zaidi ya kuona kushindwa kwingi sana. Inafika mahali unakata tamaa na kuamua kuharibu maisha yako zaidi na zaidi.
Ninasema unaharibu maisha yako zaidi na zaidi nikiwa na maana gani? Ni kwamba unakuwa umekata tamaa na unakuwa huchukui hatua yoyote ya maana sana sana unakuwa ni mtu labda wa kulewa sana au kuendesha maisha yako hovyo tu.
Kila ukiangalia sababu ya wewe kuweza kufanya yote hayo ni kwa sababu huoni tena mwanga wa mafanikio yako, bali unachikiona ni kushindwa na ambako unakuwa hujui hata wewe ufanyaje ili uweze kutoka hapo na kufanikiwa tena.
Hali kama hii inawakuta watu wengi sana, ambao kimsingi wanakua wanashindwa kuelewa ni nini cha kufanya kwa sababu ya hali zao mbaya za kiuchumi na badala ya kutengeneza maisha yao hujikuta ndio wanaharibu kabisa.

Ninachotaka kukwambia wewe hapa ni hiki, wakati wote hata kama hali ya maisha yako ni mbaya sana na unaona kila kitu kimeharibika, lakini kipo kitu ambacho unaweza ukafanya kikaleta mchango wa mabadiliko ya maisha yako.
Kitu hicho kinaweza kikawa na mchango mdogo sana ambao hauonekani kabisa, lakini kipo kitu cha kuweza kubadilisha maisha yako hata kama ni kwa kidogo sana. Unatakiwa kuthamini na kuchukua hatua za kutenda bila kujali kitu hicho ni kidogo au hapana.
Kama ilivyo kipo kitu ambacho ukifanya kinapelekea kuharibu maisha yako pasipo wewe kujua, halikadhalika kipo kitu ambacho ukikifanya kinaweza kubadili maisha yako ya kimafanikio hatua kwa hatua hata kama hatua hizo wewe huzioni.
Huhitaji kuendelea kukata tamaa zaidi ya hapo ulipo, kama ulikuwa umekata tamaa, inatosha kwa sasa, fanya kitu cha kuweza kubadili maisha yako. Usikubali kubweteka na kuwa mtu yule yule fanya kitu cha kubadili maisha yako na kitu hicho elewa kipo.
Unaweza ukaanza leo kuchukua hatua kwa kujenga ndoto zako upya ambazo unaona zimeharibika kabisa kwa kufanya kitu kidogo kabisa. Kitu hicho usikidharau na kukiona hakifai, kina mchango wake katika kukusaidia kukufanikisha wewe.
Mafanikio makubwa mara nyingi yanajengwa pia hivyo, kwa kufanya vitu vidogo vidogo ambavyo vitu hivyo kwa baadae vinakuja kuwa vina mchango mkubwa wa kuweza kubadili maisha kwa sehemu kubwa.
Je, bado una sita sita kuchukua hatua, je, bado unajiona huwezi tena kufanikiwa? Tafadhari usiogope, wala usizuiliwe na chochote kile. Chukua hatua kwa kufanya kitu kidogo sana ambacho kitakusaidia bila hata wewe kujua.
Fanyia kazi kitu hicho na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,








Aug 30, 2021

Usiwe Mtumwa Wa Jambo Hili, Utakwama.

No comments :


Kuna yale mambo ambayo kwenye maisha huwa yanaonekana ni rahisi kabisa kufanyika na pengine kukupa mafanikio. Hata hivyo kitu cha kushangaza mambo hayo pamoja na urahisi wake wengi huwa hawayafanyi.

Hali hiyo huwa inatokea kwako kwa sababu ya kujikuta upo katika hali ya ‘rahisi kufanya…lakini pia sio rahisi kufanya,’ yaani urahisi kwa hali ya kawaida unauona, lakini ndani yake kuna ugumu fulani hivi ambao unakuzuia kufanikiwa. 

Ukweli wa mambo ulivyo kwenye maisha yako, iwe afya, furaha au utajiri unaweza kuvipata ikiwa utachukua hatua ndogo ndogo kila siku zile zinazowezekana ambazo zitakusogeza kwenye lengo lako bila kudharau hatua yoyote ile.

Kama ni rahisi hivyo, kwa nini watu wengi wanashindwa kufikia malengo yao? Hiyo yote ni kwa sababu ‘rahisi kufanya…lakini pia sio rahisi kufanya,’. Hatua ndogo ndogo zinakuwa ni ngumu sana kuweza kutekelezwa na wengi wetu.

Jiulize ni mambo mangapi katika maisha yako ulipoambiwa fanya kitu hiki, ulisema kwamba, ‘aaah kitu hiki ni rahisi, nitakifanya tu’. Lakini mwisho wa siku unajikuta unashindwa kuchukua hatua kabisa.

Kuanzia sasa, acha kuwa mtumwa wa ‘rahisi kufanya.’ Ukiwa mtumwa wa rahisi kufanya na halafu huchukui hatua utakwama. Hakuna kitu ambacho ni rahisi, kila kitu kichukulie kwa uzito wake mkubwa.

Chukua hatua ndogo ndogo bila kudharau udogo wa hatua hiyo. Kuwa siriaz na maisha yako haswaa. Ukifanya hivyo utaweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako kubwa. Hakuna kinachoshindikana, kila kitu kinawezekana.

Kila la kheri katika kufikia ndoto zako kubwa za kimafanikio.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 29, 2021

Tumia Mambo Haya Vizuri, Utafanikiwa.

No comments :

Kila wakati, unatakiwa kutumia kile ulichonacho kwa uhakika na vizuri kabisa. Acha kujidanganya kwamba unataka mafanikio makubwa wakati hata ile misingi ya kutengeneza mafanikio makubwa unaiharibu hovyo hovyo.

Haiwezekani eti unasema unataka mafanikio makubwa wakati unatumia muda, pesa na nguvu zako hovyo, ambapo vitu hivyo kwa pamoja vingekusaidia kufikia mafanikio makubwa kama ungevitumia vizuri na kwa busara. 

Pesa unazozipata hazijiamulii zenyewe kwamba ‘sasa mimi pesa ninakwenda kununua kitu hiki au kile.’ Wewe ndie mwenye jukumu la kupanga pesa zako zitumike wapi na kwa sababu ipi.

Sasa kama hiyo iko hivyo, kwa nini unafanya maamuzi mabovu ambayo yanakupotezea pesa nyingi na kwa kiasi kikubwa? Kuwa makini sana na matendo yako ili yasikupotezee pesa ambayo ni moja rasilimali muhimu kukusaidia kufanikiwa.

Hapo ulipo najua una pesa za kiasi fulani hata kama ni ndogo, najua una muda na nguvu fulani, sasa kwa nini hivi vitu usivitumie kwa uangalifu ili viweze kukusaidia kukupa mafanikio makubwa na badala ya kuvipoteza tu kiholela.

Watu matajiri, wanajua namna ya kutunza pesa zao vizuri, kwa nini wewe usiwe miongoni mwao? Huna pesa si kwa sababu pesa zinakukimbia bali ni kutokana na matendo yako yanayofukuza pesa.

Kitu cha kufanya jiulize, ni hatua zipi utaweza kuzichukua ili kuweza kulinda rasilimali zako za kukusaidia kufanikiwa ambazo ni pesa, muda na nguvu zako.  Kama hujui tafuta watu wenye mafanikio kisha wafatilie.

ukiwafatilia watu hao utajua ni kwa jinsi gani wanavyotunza pesa zao, muda wao na nguvu zao za kuwawezesha kufanikiwa. Kaa ukijua ukitumia mambo hayo vizuri, utake au usitake yatakusaidia kufanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 28, 2021

Makosa 28 Ambayo Hutakiwi Kufanya Kwenye Maisha.

No comments :





 
Yapo makosa ambayo pengine kwa kutokujua, uliyafanya na yamekufanya unashindwa kufikia viwango vile vikubwa vya mafanikio ulivyokusudia.

Na makosa hayo hutaki yajirudie kwako, na hutaki mwingine akutane nayo. Katika makala hii inakuonyesha makosa hayo kwa wazi.

1. Kutokuthubutu, wakati una uwezo wa kuthubutu kufanya hicho unachotakiwa kukifanya na kikakupa mafanikio makubwa.

2. Kutokujifunza elimu sahihi ya fedha na mafanikio mapema, ni kosa ambalo ukilifanya utalijutia sana maishani baadae.

 3. Kufanya biashara ambayo una hadithiwa inalipa na wakati wewe huijui na hujawahi kuifanya na unaingiza pesa za kutosha.

 4. Kuharibu mahusiano ya watu, eidha yawe ya kibiashara au kimapenzi.

5. Kuwa na marafiki ambao sio SAHIHI kwenye maisha yako.

6. Kufanya maamuzi yasiyo sahihi kabla hujafikiria vya kutosha.

 7. Kuwaamini watu ambao hukustahili kuwaamini na ukaamua kuwaelezea kila kitu. Kujiachia sana kwa watu sio kuzuri.

8. Kutokujua kwamba mtaji si pesa tu, hata uaminifu nao ni mtaji mzuri sana, kama ukiutumia kwa uaminifu na uhakika mkubwa.

 9. Kuacha ulichokuwa ukikifanya, na kuamua kukimbilia kwenye kitu kingine kipya. Huko ni kupoteza nguvu bure, ulichokuwa ukikifanya, hakitafanikiwa na hicho kipya hakitafanikiwa pia.

10. Kuanzisha biashara mpya na kuacha watu wasimamie na wewe ukiwa mbali, ni kosa kubwa sana kibiashara. 

11. Kuanzisha mahusiano na mtu usiyemjua vizuri, halafu mwisho wa siku yule mtu anakuja kukupotezea muda na pesa zako bure.

 12. Kutumia pesa hovyo na kujikuta ukiwa kwenye madeni makubwa sana.

13. Kughairisha mambo kila wakati kwa kuamini muda upo, kumbe muda haupo.

14. Kumwamini mtu kirahisi rahisi tu ambae humjui iwe kwa kuwasiliana nae au kuishi nae kwa ukaribu.

15. Kuitumia pesa hovyo bila ya kuifanyia mpangilio maalumu. Kabla pesa yoyote haijatumika, ni lazima ipangiliwe na kuwekewa bajeti.

16. Kuamini hutoweza kitu bila kuwa na 'connection' au mtu kati. Unaweza ukaweza hata kama huna mtu mwingine.

17. Kuogopa kuanza upya, mara baada ya kila kitu kuwa kimekwenda hivyo.

18. Kutokuanza na kidogo ulichonacho kwenye maisha yako.

19. Kuchanganya ujasiriamali mchanga na anasa.

20. Kutokuwa mtu wa kutafuta maarifa, unafanya kazi kubwa, lakini unakosea padogo tu, maarifa huna.

21. Kununua vitu bila mpangilio na matokeo yake kuviona tena havikufai vitu hivyo.

22. Kufanya vitu vingi kwa mara moja na kukosa usimamizi.

23. Kutokujikubali kuwa unaweza, na kumbe uwezo wa kuweza unao tu na tena mkubwa.

24. Kuogopa kufanya kitu kwa sababu ya kuogopa kukataliwa au kukosea.

25. Kutokusema hapana, ni kitu kidogo lakini kinakupotezea sana.

26. Kuacha kufanya unachokipenda na kufanya mambo mengine eti ili kuwaridhisha watu.

27. Kuoa au kuolewa na mtu asiye na hofu ya Mungu. Kila ukimwambia hiki, ni mbishi hatari.

28. Kuanza na biashara na kitu kikubwa sana, wakati kwenye biashara kuna kujifunza mengi na kukosea ni lazima.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 27, 2021

Jifunze Kuiona Dunia Katika Jicho Hili, Utafanikiwa.

No comments :

 

Watu wengi wamekuwa wakiingalia dunia na mazingira yanayowazunguka kwa mtazamo mdogo na hafifu zaidi, ambao husabisha kushindwa kufikia ndoto zao.

Watu hawa wanakuwa na mtazamo huo kwa sababu ya mambo ambayo wameyapitia siku za nyuma, kama vile kushindwa, hivyo wanaona kila kitu hakiwezekani tena.

Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu hao, kitu cha kufanya ili kufanikiwa unatakiwa kupanua mtazamo wako. Hutakiwi kuyaona mambo katika jicho la kutowezekana.

Unatakiwa kuyaona mambo katika upana wake mkubwa, unatakiwa kuona mafanikio yapo katika dunia, unatakiwa kuona kila mtu ni wa muhimu katika maisha yako. 

Kwa hiyo, katika kila mazingira au kila mtu unayekutana nae, jiulize huyu mtu nitafanya nini cha kubadilisha maisha yake, nami pia nitajifunza nini kutoka kwake mtu huyu. 

Kwa kuwa na mtazamo huo, yaani mtazamo ambao hauoni kushindwa, yaani kuwa na mtazamo ambao una ona mbele kuna mafanikio, basi utaweza kufanikiwa na kufika mbali zaidi.

Jifunze, kuwa na mtazamo wa kuona dunia katika jicho chanya, katika jicho la mafanikio makubwa na acha kuona dunia, watu wake na mazingira katika jicho hafifu, utajikosesha mengi.


Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Aug 26, 2021

Hizi Ndizo Biashara Kubwa Tatu, Ambazo Ukizifanya Lazima Uwe BILIONEA.

No comments :

Zipo biashara kubwa tatu, ambazo ukizifanya lazima uwe BILIONEA ikiwa utajipa muda. Hizi ni biashara ambazo hazijawahi kumtupa yeyote.

Kwa nini nimekwambia hivyo, kwa sababu hizo ndio biashara ambazo zimetengeneza mabilionea wengi barani Afrika na duniani kote. 

Moja, biashara ya viwanda vidogo na vikubwa.

Ikiwa kweli umejikuta kwenye biashara za viwanda, lazima uwe tajiri. Hiyo iko hivyo kwa sababu, wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza, faida kupata kwako ni lazima na huwezi kukwepa.

Tunaposema viwanda hatumaanishi lazima uwe na mabilioni ya pesa ndio uanze, vipo viwanda vidogo, ambavyo hata havihitaji mtaji mkubwa sana na unaweza ukaanza navyo. 

Kwa mfano, mashine ya kutengeneza sabuni ya unga, gharama zake hazizidi MILIONI tatu. Zipo mashine nyingi za kutengeneza bidhaa ambazo gharama zake ziko chini sana.

Kama una wazo la kutaka kuuza bidhaa fulani hivi, acha kuwaza tu kuwa mlanguzi, waza utawezaje kutengeneza bidhaa hizo nakupata mauzo makubwa ya kujaza pesa mfuko.

Mbili, biashara ya kuagiza bidhaa nje ya nchi. 

Kama utaweza kumudu kuagiza bidhaa nje ya nchi kama China, Dubai, Uturuki na kwingineko, basi ipo fursa kubwa sana ya kupata pesa nje nje na za kutisha kuliko unavyofikiria.

Matajiri wengi Tanzania, wamejipatia pesa kwenye fursa hii ya kuagiza. Siri iliyopo unapoagiza bidhaa nje unapata bidhaa kwa bei nafuu sana ambapo ikiletwa huku lazima upige faida iliyosimama.

Huhitaji kulaza damu ni kuamua kuchangamkia fursa, na kujifunza juu ya kuagiza, eidha iwe kwa njia ya mtandao au kuamua kwenda kabisa kama China ikiwa pesa mfukoni ipo.

Nakuhakikishia ukifanya kazi hii tu peke yake ya kuagiza bidhaa nje kwa muda wa miaka mitano mfululizo na ukawa 'siriaz, haswa, kama usipokuwa tajiri basi utakuwa umelogwa sana.

Tatu, biashara ya kilimo biashara.

Ikiwa kama kweli utajikuta kwenye kilimo biashara, iwe kilimo wazi au kilimo Cha hema, uhakika mkubwa wa kufanikiwa na kuwa tajiri upo na tena kwa uhakika wote mkubwa.

Uzuri wa Tanzania ardhi bado kubwa na pia kuna maeneo ambayo mvua inanyesha mara mbili na kilimo kinakubali kama Tanga, pwani na mikoa ya kusini, pia kuna mito mingi sana ya maji.

Lakini hata hivyo hata mwenye maeneo ambayo hayana mvua ukifanya kilimo kama cha bustani kwa kumwagilia pia uwezekano wa kufaulu upo sana. Kikubwa kwako ni kujiwekea mikakati.

Jifunze kwa waliofanikiwa kupitia kilimo biashara watakupa Siri zitakazoweza kukutoa kwenye umaskini wako. Acha kuwa mbishi eti kilimo hakifai kumbe ulilima mara moja na kukimbia.

Hizi, ndio biashara ambazo ukizifanya kaa ukijua utajiri hauwezi kuukwepa. Ni jukumu lako kuchukua hatua na kufanyia kazi yote ukiyojifunza kwenye makala haya. 

Kwa mahitaji ya mashine yoyote au bidhaa yoyote ya kuagiza nje ya nchi, kwa mahitaji ya msaada wowote wa kimawazo usisite kuwasiliana nasi kwa 0687449428.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.


Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.


 

Aug 25, 2021

Kila Mtu Anakiu Na Hamu Kubwa Ya Kupendwa Ila Jukumu Letu Si Kupendwa Bali Ni Kupenda.

No comments :
Katika maisha watu wengi hupenda kupendwa nasii wao kuwa wakwanza Kupenda.

Muda mwingine unapokuwa umempenda mtu na ukaamua kumwambia,Na akakataa huwa mala nyingi wengi wanajikuta katika hali ngumu sana.


Ila sikiliza Rafiki,neno Sikupendi alimaanishi ya kwamba anakuchukia.

Tazama Video Katika Ukurasa wetu wa Youtube hapo chini ili uweze kujifunza kuhusiana na swala hili.

Usisahau Ku Subscribe na kubonyeza alama ya kikengere kwani Mafanikio ni yetu sote.




WAKO KATIKA MAFANIKIO:

IMANI NGWANGWALU



Aug 24, 2021

Hili Ndilo Tatizo Kubwa Ulilonalo Linalokukosesha Furaha Na Mafanikio.

No comments :
Unaweza ukawa unakosa sana furaha yako na pia hata kukosa mafanikio kwa sababu moja tu ya wewe kushindwa kuweka utulivu kwenye eneo moja. Watu wengi si wazuri sana katika kuweka akili zao eneo moja. Hawa ni watu wanaoishi jana, au ni watu wanaoishi kesho na kusahau leo yao iliyo ya msingi.
Kwa sababu hiyo hapa ndipo linapoibuka tatizo linawakosesha watu wengi furaha na mafanikio, tatizo hilo si lingine bali  ni la kutokuishi sasa. Watu wengi hawaishi sasa, ni watu wanaotaka kuishi jana au kesho zaidi. Wakati nguvu kubwa ya mafanikio inatengenezwa sasa na kila tukio linatokea sasa.
Ukiwafatilia watu wengi kwa sasa hawako tayari kuweka mawazo yako kwa kile wanachokifanya kwa asilimia mia moja. Utakuta mtu anafanya jambo la aina fulani sasa, lakini mawazo yake yapo kwenye jambo lingine la kesho au jambo la jana pengine ambalo lilimuuza, lakini utakuta mtu huyu analiwaza jambo hilo.

Inapotokea ukahamisha mawazo yako sasa na kuwaza jana au kesho na kushindwa kuitumia sasa yako kwa vizuri, ni wazi si rahisi mtu wa namna hii kuwa na furaha wala mafanikio makubwa sana. Kuwa na mawazo ya nyuma kama kuna vitu ulifanya vibaya yanaweza yakakuhuzinisha na mawazo ya mbele pia yanaweza yakakutia hofu kubwa.

Mpaka hapo unaona siri ya wewe kuwa na furaha na mafanikio mazuri kwako, ni kwa wewe kuishi sasa. Kama nilivyosema, ipo nguvu kubwa sana ya kuishi sasa kwani hapo ndipo nguvu kubwa ya  kimafanikio inapozaliswa. Jaribu kujiuliza kama kuna kitu kinazalishwa nje ya sasa, utagundua kila kitu au kila jambo ni lazima liweze kuanzia sasa.
Hata majibu ya changamoto zetu tunazozipitia unatakiwa kukumbuka zinapatikana sasa. Huwezi kupata majibu ya changamoto hizo kwa kesho au kesho kutwa, bila kuanza kuishughulisha akili yako sasa. Kila majibu ya changamoto yanaanza kupatikana kwanza sasa. Unatakiwa kuishi sasa, kwa kuweka mawazo yako eneo moja na utashangaa ukiona mafanikio makubwa sana yakitokea kwako.
Ikiwa kila wakati unawaza sana kesho inayokuumiza au kuwaza mambo yaliyopita, na kusahau sasa uliyonayo hapo ujue akili yako inakuwa inakutawala na wewe huitawali akili. Ili uweze kuitawala akili yako vizuri, hutakiwi kuyumba hata kidogo, akili yako unatakiwa kuielekeza kwenye sasa yako kwa usahihi sana.
Kuna wakati kuendelea kuwaza vitu vya kesho vinavyokupa hofu au jana ni kutengeneza matatizo yetu wenyewe. Kitu cha msingi kwa wewe ni kutuliza akili yako na kuhakikisha kila wakati unashughulika na sasa yako kwa uhakika sana. Acha kuyumbishwa mawazo yako, waza sasa kwa manufaa ya maisha yako.
Kabla sijaweka kalamu chini nikukumbushe, ukiitumia sasa yako vizuri, ukiishi sasa vizuri, utafanikiwa. Tambua, kila mmoja anaweza kufikia mafanikio yake ikiwa mtu huyo atahitaji mafanikio hayo. Na ikumbukwe hatma ya maisha yetu tunayo sisi, maisha yetu yawe ya namna gani uchaguzi ni wetu. Kwa nini basi tusichagua maisha ya mafanikio ya kweli? Ishi sasa na ufanikiwe zaidi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,



Aug 23, 2021

Wakimbie Watu Hawa.

No comments :

Kuna watu ambao wao wana asili ya ugumu tu. Ni watu ambao hawataki vyao vitumike, ila ni watu wanaopenda kutumia vya wengine. Hawa ni watu ambao kama wanyonyaji wa wengine.

Watu hawa ni wazuri sana katika kufurahi, na kucheka na vitu vya watu. Lakini inapofika vya kwao kutumiwa au kuliwa wanakuwa wagumu sana na hawataki hata kidogo kuguswa. 

Unapokuwa na watu kama hawa, jihadhari. Achana na marafiki kama hawa, ambao wao urafiki wao, unapokuwa na kitu, ukikosa kitu wanakutupa. Rafiki wa kweli ni yule akufaae kwa dhiki.

Kwa nini uwe na marafiki wanaotaka kukutumia tu na kukutupa unapokuwa huna kitu. Kataa hili, chagua rafiki bora ambao mnaendana. Achana na marafiki wanafiki maishani.


Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 22, 2021

Ukiacha Jambo Hili, Utaanza Kupata Pesa Na Mafanikio.

No comments :

Hata siku moja, hakuna aliye tayari kulipa gharama kubwa kupata kitu feki wakati anaweza kupata kilicho halisi kwa gharama hiyo hiyo. Hakuna wa kufanya hivyo kila mtu anataka kitu halisi na chenye ubora. 

Kama unataka kulipwa zaidi au kupata fedha zaidi, acha kuiga wengine na anza kuwa wewe. Unapoanza kuiga watu utajipoteza maana watu wakijua kule unakoiga watakimbilia huko na kukuacha ukiwa mtupu.

Kuwa wewe halisi, na watu watakuja kwako wakiwa tayari kukulipa zaidi, kwa sababu unawapa kile ambacho hawawezi kukipata pengine. Ukiwa mtu wa kuiga iga, jua wakati utafika utakimbiwa.

Je, uko tayari kukimbiwa kwa sababu ya kuiga? Kama hutaki iwe hivyo kuwa kama wewe. Jitengeneze kama unavyotaka uwe, na utavuta wengi kuja kwako kwa sababu upo orijino na huigi sehemu yoyote.

Zingatia, kila mtu anataka kitu orijino na kitu halisi. Vitu orijino haviji kwa kuiga, vinatengezwa. Acha kuiga, kuwa wewe, kuwa orijino. Ukiacha ubabaishaji wa kuiga, utaweza kufanikiwa sana kwa chochote ukifanyacho.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 21, 2021

Unahitaji Mambo Haya Matatu, Ili Kushinda Changamoto Inayokusumbua.

No comments :

Kati ya kitu ambacho huwezi kukwepa katika safari ya mafanikio yako ni changamoto. Kwa namna yoyote ile ni lazima utaweza kukutana na changamoto, uwe unataka au hautaki, utakutana nazo.

Na ili kushinda changamoto yoyote ile, unahitajika uwe na ufahamu au uelewe mambo matatu ya msingi sana kwako. Kama hautaelewa hayo mambo matatu haiwezekani kushinda hiyo changamoto.

Jambo la kwanza, muda. 

Ili uweze kuishinda changamoto yako, lazima ujipe muda. Haiwezekani changamoto imetokea sasa hivi, na unataka kuishinda muda huu huu, hicho kitakuwa ni kitu kigumu na sio rahisi. Muda unatakiwa ili kushinda changamoto. 

Jambo la pili, juhudi.

Pia mbali na muda inahitajika, juhudi. Ni lazima uweke juhudi sana ili kushinda changamoto yako. Ikiwa utaiendea changamoto yako huku ukiwa unacheka cheka, basi ni ngumu kuishinda changamoto yako. Unatakiwa uweke juhudi haswa ili kushinda.

Jambo la tatu, nguvu.

Unatakiwa uelewe, kuna changamoto ambazo ili kuzitatua, zinahitaji uwekeze nguvu pia. Inawezekana kuna kazi unatakiwa uifanye, sasa kwa kufanya hivyo utaishinda changamoto yako.

Hayo ndio mambo unatakiwa kuyajua na kuyazingatia ili uweze kuishinda changamoto yoyote. Kama usipoyajua mambo hayo huwezi kufanikiwa katika kushinda changamoto yako.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 20, 2021

Kila Unapokutana Na Changamoto, Anza Kufanya Jambo Hili,...

No comments :

Kila unapoingia kwenye kwenye changamoto yoyote ile, kitu cha kwanza akili yako inachowaza, ni mawazo hasi ya kujuta, kujilaumu pengine kulaumu wengine na kujiuliza, kwa nini hii changamoto imetokea.

Hata hivyo, kila inapotokea changamoto, eneo sahihi la kuanzia, badala ya kuwa na hayo mawazo hasi, anza kuanza kwa kushukuru. Hapo ndipo unapoweza kuanzia kupambana na changamoto yako.

Unaweza usielewe sana, lakini unaposhukuru kwa mara ya kwanza kwa sababu ya hiyo changamoto uliyonayo, kunakuwa kunakusaidia akili yako kutafuta njia ya haraka ya kutatua changamoto yako.

Kutokana na imani yako kila unapokutana na changamoto, shukuru kwa kilichotokea, kubali ndio hivyo uko kwenye changamoto, kisha anza kutafuta suluhisho la changamoto hiyo ambayo unayo bila kusita.

Jaribu kitu hiki ninachokwambia, kila unapokutana na changamoto yako anza na kushukuru kabla hujafanya chochote, nakwambia utapata uvumbuzi wa changamoto yako kuliko unavyofikiria.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 19, 2021

Tengeneza Sababu, Utapata Kila Kitu.

No comments :

Je, unatafuta wateja wengi kuweza kununua katika biashara yako? Wape sababu wateja wako kwa nini wanunue kwako na si kwa mtu mwingine. Ni muhimu kuwa na sababu ya maana.

Je, unatafuta kuheshimiwa na watu wengine? Wape watu sababu ya kwa nini waweze kukuheshimu wewe na wasimheshimu mtu mwingine yeyote aliye kama wewe.

Mafanikio yanaweza kuja kwako, kama utakuwa na sababu kwa nini, unatakiwa kufanikiwa. Ukijipa sababu hayo mafanikio utayapata na sio jambo la kubahatisha bahatisha.

Hakuna matokeo yanayopatikana bila sababu yoyote. Wateja wananunua kwako kwa sababu, biashara inakua kwa sababu na hakuna kitu chochote cha kubahatisha.

Chochote unachokitafuta kwenye maisha yako, uwe na sababu kwa nini unakitafuta hicho kitu. Kila unapojipa sababu ya kwa nini unataka hicho ukitakacho, utafanikiwa.

Je, wewe sababu yako ni ipi inayokufanya utafute hicho unachokitafuta? Je, sababu hiyo unayo? Kama sababu hiyo unayo basi, utafanikiwa. Kuwa na sababu ya mafanikio yako, UTAYAPATA.


Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi. 

Aug 18, 2021

Unatakiwa Kujua Kitu Hiki, Ili Kufanikiwa.

No comments :

Jaribu kufikiria jinsi ambavyo ingekuwa inachanganya kwa kiasi kikubwa, kama mchezo wa riadha ungekuwa hauna ule mstari unao onyesha mwisho wake ulipo, yaani mwisho wa kukimbia kwa kila mtu.

Unafikiria ni kivipi wana riadha wangejua wameshinda? Kama ingekuwa hivyo hakuna mstari, basi ungekuwa ni moja ya mchezo usio na maana, kwa sababu mshindi wa haki asingeweza kupatikana.

Kukimbia mbio inakutaka lazima uwe unajua ni wapi unakofika, mstari lazima uone ndio uweke juhudi zako. Kama ingekuwa hakuna mstari basi inawezekana na mashindano hayo yasingekuwepo. 

Ukweli huo uko sawa sawa na kwenye mafanikio. Ikiwa kweli unataka kufika kule unakotaka kufika, lazima ujue mwisho. Mbio za mafanikio zinataka ujue lengo lako linaishia wapi ili ushinde mbio za mafanikio yako.

Unapokuwa unaona kule unakotaka kufika, juhudi zako zinakuwa zinakazana kuutafuta huo mwisho.  Hutakiwi kuzunguka zunguka, unatakiwa kuujua lengo lako vizuri ili kufikia mafanikio yako.

Kwa kifupi, unahitaji kujua kile unachotaka ili kufanikiwa. Unatakiwa kujua mstari wa mwisho wa mafanikio yako ni upi. Kama hujui unachokitaka, utaishia kuishi maisha ya kawaida sana na yasiyo na maana kwako.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Aug 17, 2021

Dunia Inapoamua Kukufundisha...

No comments :

Dunia inapoamua kukufundisha jambo haisemi kwa sauti na wewe, inakufundisha kimya kimya, lakini utaelewa ina maanisha nini, hata kama unajifanya kiziwi, ila utaelewa. 

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uishi kwa NIDHAMU, haisemi na wewe kwa sauti, matokeo ya kutokuishi na NIDHAMU utayaona, kama kweli hutaishi kwa NIDHAMU.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uishi kwa UADILIFU, haisemi na wewe kwa sauti, matokeo ya kutokuishi kwa UADILIFU utayaona wewe na jinsi yatakavyokugharimu.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa UJITUME, haisemi na wewe pia kwa sauti hata kidogo, bali matokeo ya kutokujituma utayapata na kutakuwa hakuna wa kumlaumu hata mmoja. 

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uwe na matumizi mazuri ya pesa, haisemi na wewe kwa sauti, kama unaamua kutumia pesa hovyo, we tumia, siku ukija kuzikosa utajuta sana. 

Dunia inapokufundisha kwa chochote, haisemi kwa sauti, haigombani na wewe, ni wewe tu unatakiwa uwe makini na lugha ambayo dunia inasema na ufuate maelekezo hayo.

Kama usipoweza kuisikiliza dunia inasema nini na wewe kwenye maisha yako, basi utaharibu sana maisha yako. Mambo mengi utayavuruga kwa sababu huisikilizi dunia. 

Dunia inasema na wewe, unatakiwa kuweka masikio yako kuisikiliza. Kama utaisikiliza vizuri na kwa umakini, basi utaweza kufanikiwa. Kama usipoweza, utapotea. 

Ukikosea katika kuisikiliza dunia, basi utaharibu sana maisha yako na utakuwa na maisha ya hovyo. Jambo la muhimu kwako, ni kuwa makini na kuisikiliza dunia, hapo utafanikiwa sana.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.