google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 31, 2017

Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo.

No comments :
Hapo zamani za kale kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alijulikana kwa jina la mhavila. Mfalme huyu alikuwa na utu sana kwa watu wake. Japo kutokana na majukumu yake ya hapa na pale ilikuwa ni ngumu sana kwake kuonana na watu wake  mara kwa mara.
Kila mwakijiji wa jamii ile alitamani sana kukutana uso kwa uso na mfalme mhavila, kwa kukuwa mfalme huyu alikuwa ni mtu mcheshi sana kwa watu wake. Siku moja mfalme mhavila aliandaa mkutano mkubwa sana ambapo kila raia wa eneo lile alihudhuria katika mkutano ule.
Watoto kwa wakubwa, vijana kwa wazee wote walimiminika katika mkutano ule. Mfalme mhavila aliwaeleza watu wake mambo mbalimbali ambayo kimsingi yalikuwa yana manufaa sana katika kufanikisha masuala ya  maendeleo ya jamii na maendeleo ya watu hao kwa ujumla.
Mara baada ya mkutano kuisha mfalme mhavila alikutana na mtu mmoja ambaye alikuwa ni mjane, mjane huyo alionekana kwa macho ni maskini wa kutupwa, tunaweza kusema hivyo hii ni kutokana na muonekano wake. Mjane yule alimtazama mfalme mhavila kwa macho yenye kutia unyonge sana, baada ya dakika chache ndipo mjane yule akafungua kinywa chache na kusema;
‘’samahani mfalme mhavila kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta nafasi ya kuzungumza na wewe ila kwa bahati mbaya nafsi hiyo sikuweza kuipata, ila kwa siku ya leo nina kila sababu ya kumshukuru Mungu wangu kwa sababu tumeweza kukutana.
Kabla ya mfalme hajainua kinywa chache mjane akandelea kusema ‘ nafahamu ya kwamba upo bize na shughuli za hapa na pale, na unafanya hii yote kwa sababu ya kusongesha kurudumu hili la maendeleo, kwa kufanya hivyo nikupongeze sana kwa sababu kila mwenye macho na maskio anakiona na kukishuhudia kwa kile ambacho anakifanya.
Mfalme mhavila baada ya kusikia vile moyo wake ulikwenda kasi kidogo, hii yote ilikuwa ni mshangao wa kile ambacho mjane alichokuwa amemueleza, mfalme mhavila aliwaza kidogo, kisha akatafakari ndani ya nafsi yake. kisha mfalme mhavila akajibu asante sana mama kwa kutambua mchango wangu kwa kile nikifacho, kwa kweli nakushukuru sana.
Wakati watu wengine wakishangaa na kujihoji mama mjane na mfalme walikuwa wanazungunza nini, hakuna aliyepata majibu.
Hivyo mara ya sekunde chache mama mjane akamwambia mfalme mhavila ‘’ samahani mfalme mhavila nafahahamu ya kwamba una majukumu mengi sana, ila naomba jioni ya leo uje tule   kwa pamoja chakula cha jioni nyumbani kwangu.
Mara baada ya mama mjane kuzungumza hayo, mfalme mhavila akainua kinywa chake na kusema “ nashukuru sana mama kwa maneno yako yenye kunitia nguvu za kiutendaji wa kimaendeleo, kwani ulichokisema kimenipa fikra mpya za kuleta mbadiliko mapya ya kimaendeleo, hivyo nakuahidi siku ya leo tutajumuika kwa pamoja katika kupata hicho chakula cha jioni kwa pamoja.
Baada ya mazungumzo hayo mfalme mhavila na mama mjane waliagana na kuahidiana kukutana hiyo jioni kama ilivyopangwa. Mama mjane  alielekea nyumbani kwake kwa ajili ya kuandaa chakula hicho. Baada ya dakika chache chakula hicho kilikuwa kipo tayari, hivyo mama mjane akaweka chakula hicho mezani kwa ajili ya kuliwa. Mama mjane alimsubiri mfalme kwa muda wa saa nzima, lakini cha ajabu ni kwamba mfalme mhavila hakufika .
Mama mjane hakuchoka kumsubiri mfalme mhavila kwani alimini atakuja kama ambavyo walivyokuwa wapenga, muda ilizidi kwenda laikini mfalme hakuonekana kufika. Hivyo mama mjane akaamua kufunga mlango wake  kwa kuwa muda ulikuwa umeshakwenda.
Ilipita nusu saaa tangu mama mjane afunge mlango wake lakini cha ajabu mfalme mhavila hakutokea, wakati mama mjane anatafakari ni nini ambacho kitakuwa kimemsibu mfalme mhavila ghafla akasikia mlango ukigongwa. Mama mjane aliinuka mahali alipokuwa ameketi na kuelekea mlangoni kwa ajili ya kufungua.
Kabla mama mjane haujaufungua mlango , mama mjane alifurahi sana kwani aliaamini aliyekuwa amegonga mlango alikwa ni mfalme mhavila. Taratibu mama mjane akashika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kuufungua mlango. Mara baada ya kufungua alistajabu kumbe aliyekuuwa akigongo mlango hakuwa mfalme mhavila bali alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anatokwa na jasho sana. Hivyo yule kijana hakupoteza muda, alimsabahi mama mjane kisha kueleza shinda yake moja kwa moja. Kijana yule akasema samahani mama nimetoka mbali sana sehemu ambayo ni jangwani , hivyo nimetembea muda mrefu bila kunywa maji, hivyo naomba unisaidie niweze kupata maji ya kunywa.
Mama mjane alipatwa na hasira kidogo kwa sababu alitegemea ambaye aligonga mlango huenda alikuwa ni mfalme mhavila. Basi mama mjane alimtazama yule kijana kisha akelekea ndani na kuchua maji ambayo alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na kumpa yule kijana.
Mara baada ya yule kijana kunywa yale maji alimshukuru mama mjane, kisha kijana yule akaondoka. Mama mjane alirudi ndani kwa ajili ya kumsubiri mfalme. Lakini cha ajabu mfalme hukuweza kufika. Mama mjane alitafakari na kusema haiwezekani ni kwanini mfalme hakuweza kutimiza ahadi?
Wakati akitafakari hayo mara akasikia tena sauti ikitokea mlangoni, mama mjane alifurahi  sana kusikia sauti ile ikibisha hodi kwani nafasi hii aliamini yule aliyekuwa akibisha hodi alikuwa ni mfalme mhavila. Hivyo pasipo kupoteza muda mama mjane alielekea mlangoni kwa ajili ya kumfungulia mfalme mhavila.
Mara baada ya kufungua mlango ailikutana na mtoto mdogo ambaye mama mjane hakuweza kumfahamu mtoto yule, mama mjane alijaribu kuvuta taswira ni wapi ambapo aliwahi kumuona mtoto yule, mama mjane alikosa majibu kwani mtoto yule alikuwa ni mgeni machoni pake.
Mtoto alimsabahi mama mjane kisha akasema “ samahani mama yangu  nimetoka nyumbani kwetu wazazi wangu wameniacha tangu asubuhi, sijaweza kula chochote, hivyo naomba unisaidie chakula niweze kula mama yangu, kwani naumwa na njaa sana mama.
Mama alimtazama mtoto kwa macho yenye huruma sana, hivyo kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana aliamini ya kwamba mfalme mhavila hawezi kufika kwake tena, hivyo alichukua chakula  ambacho alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na kumpa mtoto yule. Mtoto yule alikula na kumshukuru mama mjane.
Mama mjane alifunga mlango tena na kuamini ya kwamba mfalme mhavila asingeweza kuja tena. Wakati akiwa ameketi ndani mwake mama mjane alisikia watu wakija uelekeo wa nyumba yake wakiimba nyimbo nzuri na za kupendeza sana. Alitafakari kuna nini? Wakati anazidi kutafakari sauti zile zilikuwa zinazidi kusogea katika nyumba yake.
Mama mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme mhavila akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini mfalme mhavila kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme mhavila alifika kwa mama mjane na  kusema asante sana kwa kunijali.
Mama mjane aliwaza na kusema mfalme mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati sijamfanya chochote?
Je mfalme Mhafavila alimshukuru mama mjane kwa kipi hasa? Usikose itaendelea wiki ijayo siku kama ya leo,
Ndimi afisa mipango Benson Chonya
0757909942

May 30, 2017

Fanyia Kazi Mambo Haya, Ili Kuendelea Kujenga Msingi Mkubwa Wa Mafanikio Yako.

No comments :
1. Zipo kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia kile. Usipokuwa makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya kuweza kujiokoa na kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele. Simamia na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na utafanikiwa.
2. Maisha na mafanikio ya kweli yanakuja kwa wewe kuweka thamani na kutoa mchango mkubwa kwa wengine. Mafanikio hayaji kwa bahati nasibu au chochote kile ambacho kipo kwenye njia ya mkato. Mafanikio ya kweli yanatengenezwa sana na kwa wewe kuendelea kuweka thamani na kutoa michango kwa wengine.
3. Kila wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya kile unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa. Kupenda kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni rahisi tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’ hasa kama unafanya kile unachokipenda.
Mara nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.

4. Wakati tukiwa vijana wadogo wengi wetu tulikuwa na ndoto nzuri sana kwamba nikikua nitafanya hiki au kile na ilikuwa rahisi kuweza kuona kama vile kila kitu kinawezekana na wala hakuna changamoto kubwa sana.
Lakini kwa kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda zile ndoto zetu zilianza kupotea hasa baada ya kukumbana na changamoto za kimaisha za hapa na pale. Kitu cha kujiuliza kwako kwa mfano je, ile ndoto yako ya utotoni unayo au imepotea?
Kwa vyovyote vile ilivyo ndoto yako ipo ila kikubwa ulichokifanya umeizika ndoto yako bila kujua.Umeshindwa kufanya namna nzuri ya kuweza kuifufua ndoto yako na kuiweka wazi hadi iweze kufanikiwa.
Sasa  jiulize hivi kama huna mpango na ndoto yako ambayo ulikuwa unapienda, kwa sasa unaishi maisha a aiana gani? Ni rahisi kukwama katika maisha na kupata ugumu fulani kama hufuati ndoto yako na hufanyi kile kitu unachokipenda maishani.
Kuanzia  sasa jipe muda wa kufikiri tena na anza kufatilia ndoto yako ile ambayo ulikuwa umeisahau. Kaa chini ujiulize una ndoto ipi ambayo unatakiwa kuifailia? Kisha anza kuifatilia ndoto yako na itakuwa kweli.
5. Kuna wakati tunajiambia sana ‘mwaka huu nahitaji kuongeza mtaji, mwaka huu nahitaji pia kufanya biashara ile, au mwaka huu nahitaji kufanya hiki au kile’. Hizi ni sentensi ambazo naamini umezisikia sana zikisemwa na kuna kipindi hata wewe umekuwa ukijisemea hivyo.
Katika ulimwengu wa mafanikio ipo hivi kile kinachokufanikisha si kile unachokihitaji, bali kile kinachokufanikisha ni kile unachokifanya au kukifanyia kazi, ndicho hicho kinachokufanikisha na kukupa mafanikio.
Hakuna atakayejali kwa kile unachohitaji au unakisema sana hata kiwe kizuri vipi, dunia inajali kile unachokichukulia hatua na kukifanya. Hicho unachokifanya kila siku, hicho ndicho kinachokusogeza kwenye mafanikio yako.
Unaweza ukahitaji mambo mengi sana lakini kama huchukui hatua uwe na uhakika huwezi kufanikisha kitu chochote katka maisha yako, zaidi yako utaishia kusema nahitaji hiki au kile na miaka inaenda na bado ukajikuta hupati kitu.
Kuna watu ambao ukiwachunguza karibu maisha yao yote ni watu wa kusema nitafanya hiki mwaka huu au kile na hawafanyi. Maisha ya mafanikio hayataki ‘blaa blaa’ yanataka ufanye kitu yaani uchukue hatua za kimafanikio.
Kumbuka unachokihitaji hakiwezi kukupa mafanikio unayoyataka kwa asilimia zote, acha kulinga na kujidai kwa kile tu unachokihitaji, badala yake uelewe kabisa kile unachokifanya hicho ndicho kitakachokupa maisha na mafanikio unayotaka.
6. Kipimo cha mafanikio yako  kipo kwako wewe mwenyewe na wala hakipo kwa mtu mwingine. Njia pekee itakayokufanya uweze kupima mafanikio yako ni kwa kwewe kuangalia hatua unazozipiga kulekea kwenye mafanikio hayo.
Mafanikio yako hayapimwi kwa kuangalia mafanikio ya mtu mwingine. Bali mafanikio yako yanakuja kwa sababu ya zile hatua zako mwenyewe unazotakiwa uzipige kila siku kuelekea kwenye mafanikio.
Unawezaje sasa kujua kama umefanikiwa ikiwa hujilinganisha sana na wengine? Hilo ni rahisi tu, ni kwa wewe kuangalia ni hatua gani umepiga ukijilinganisha na mwaka jana au wakati uliopita.
Kumbuka kila siku hili, chukua hatua kila siku za kuelekea kwenye kile unachokifanya. Usijali wala usiangalie ikiwa unachukua hatua kidogo, kitu cha msingi chukua hatua kwani hicho ni kipimo cha mafanikio yako.
7. Kuna wakati tunakutana na ugumu sana katika kufanya vile tunavyotaka kuvifanya. Kutokana na ugumu huo na kuna wakati huweza kujikuta hata tukitaka kuahirisha kufanya mambo yetu. Kwa hali yoyote unayokutana nayo hata kama ni ngumu vipi, hebu hicho unachotaka kukifanya kifanye.
Usiahirishe mambo yako kwa sababu ya ugumu, fanya hivyo hivyo, ‘just do it,’. Weka visingizio pembeni, usiwe kama mtoto mdogo ambaye kila kitu anasingizia. Tengeneza ukomavu wa kiakili kwa kuamua kufanya hata kama ipo shida na ugumu vipi wewe fanya kwa kusukuma na utaona mafanikio yakijitokeza kwako.
Nakutakia siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

May 29, 2017

Umuhimu Wa Kujiongeza Katika Maisha Ya Mafanikio.

No comments :
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini yetu mazima u mzima wa afya tele na unaendelea vyema katika harakati zako za kuweza kulisukuma gurudumu hili la maendeleo.  Ni siku nyingine tulivu ambayo sina budi nikukaribishe kwa moyo mkunjufu tuweze kujifunza kwa pamoja.
Siku ya leo nataka ttuzungumzie namna ambayo una uwezo mwingine wa kutenda jambo jingine ambalo linaweza kukupa mafanikio makubwa kwa upande wako tofati na hilo ulitendalo sasa. Unajua nataka tuzungumzie hili kwa sababu wetu wengi hawafahamu uwezo mwingine walionao, ambao unaweza kuutumia ili uweze kukamilisha jambo jingine ambalo Mwenyezi mungu kakujalia kulitenda.
Watu wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka mipaka katika kitu hicho pekee.

Ongeza thamani ya biashara yako kila iitwapo leo.
Ukweli haipo hivyo hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa  na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi kutengeneza ‘six park’ kwa kufanya mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali unaweza kutengeza ‘six park’ kwa kufanya mazoezi ya aina tofauti tofauti.
Kwa  muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate wako wa kila siku.
Hata mwandishi mmoja aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get what you always gotten” hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale ambayo umekuwa  ukifanya siku zote, utapata yale yele ambayo siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena aya hii ili uielewe vizuri.
Kwani aya hiyo ipo wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi matokeo yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya aina tofauti  na uliyoyazoea, unachotakiwa kufanya ni kubomoa uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda mambo yako ya msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako  kwani binafsi naamini una kitu kingine cha kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.
Mwisho nimalizie makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako ya msingi acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa nyingine,  bali unachotakiwa kufanya ni kubomoa uzio huo ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani pindi unavyoacha ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na mwisho wa siku kuelekea jehenamu ya umasikini. 
Narudia kwa kusema tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya umaskini. Usiogope na kusema afisa mipango anakutisha hapana,  ila kazi yangu ni  kukwambia ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni kuwaza ni namna gani utaweza kufika mbali zaidi.
Kwani umuhimu wa kujiongeza kunamsaidia mtu kuweza kuwa milango mingi ya kuweza kufanikiwa zaidi. Pia faida nyingine ya kujiongeza humsaidia mtu kuweza kuwa mbunifu zaidi kwa kile akifanyacho. Na ubunifu humsaidia mtu aweze kujilikana na ukijulikana ndo mwanzo wa mafaniko yenyewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba kazi ibaki kuwa kwako kwa kuamua kwenda kuyatekeleza hayo ambayo nimekwambia. Asante.
Ni wako katika ujenzi wa mafaniko; afisa mipango, Benson Chonya.
0757909942.

May 27, 2017

Mambo Muhimu Ya Kufanya Ili Kuitawala Biashara Yako Kwa Mafanikio.

No comments :
Mafanikio katika biashara ni kitu ambacho karibu kila mafanyabishara anataka kitokee kwake. Wafanyabiashara na wajasiriamalia karibu wote, wana kiu na shauku kubwa ya kutaka kuona biashara zao zikifanikiwa.
Hata hivyo pamoja na kiu hiyo, lakini ukweli unabaki pale pale, kwamba suala la kutawala biashara na ikakupa mafanikio si jambo la kubahatisha bali yapo mambo ya muhimu ambayo wewe binafsi unatakiwa uyafanye ili biashara yako iweze kufanikiwa.
Bila kupoteza muda, fuatana nami katika makala haya ili nikuonyeshe mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyafanya katika biashara yako na kuifanya biashara hiyo ikawa ya mafanikio makubwa.
1. Kubali kuwa mwanafunzi wakati wote.
Tafuta maarifa kila siku ya kukusaidia katika biashara. Jifunze kuhusu washindi katika biashara zao ni kipi wanachokifanya na hata wale wanaoshindwa ni kwa nini pia wanashindwa. Kila unapojifunza hiyo inakupa nguvu ya kujiamini  na kufanikiwa. Kama ulikuwa hufanyi hivyo hebu anza sasa kujifunza zaidi juu ya biashara yako.

2. Chukua tahadhari kubwa kwenye biashara yako.
Ili biashara yako iweze kufanikiwa, unatakiwa kujua namna ya kuchukua tahadhari kubwa kwenye hiyo biashara. Unatakiwa kuchukua tahadhari ya nidhamu binafsi katika matumizi ya pesa na mambo mengi chungu nzima ya lazima ili kukuza biashara yako. Ikitokea ukakosa tahadhari hizo si rahisi sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara.
3. Unahitaji kutengeneza mtandao mzuri wa kibiashara.
Mara nyingi biashara inakuwa na kustawi vizuri sana hasa pale kunapokua na mtandao mzuri wa kibiashara. Hivyo ni vyema kujenga mtandao mzuri wa kibiashara na wafanya biashara wenzako, hali ambayo itakupelekea kuweza kukua kimafanikio katika biashara. Huhitaji kukaa kama kisiwa, jenga mtandao wa mafanikio ya biashara yako.
4. Unahitaji kuchukua tafahadhari ya afya yako.
Huwezi kufanikiwa kwenye biashara au katika maisha kwa ujumla kama afya yako ni mbovu. Unatakiwa kila wakati kuhakikisha afya yako inakuwa imara ili ikuwezeshe kufanya mambo mengi yakayoweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara kila wakati na kusiwe na kipangimizi.
Kumbuka haya ni mambo ya msingi sana ambayo unatikiwa uyazingatie kila wakati na kuyafanya  ii kuweza kuifanya biashara yako ikawa ya mafanikio makubwa. Chukua hatua na fanyia kazi mambo haya.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri katiika kufikia mafanikio yako makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0628 92 9816,

May 26, 2017

Ijue Kanuni Halisi Ya Ubongo Wako.

No comments :
Watalamu mbalimbali wa masuala ya mafanikio wanasema ya kwamba kanuni ya akili yako inatokana na ubongo wako, na katika ubongo wako inatokana na mawazo yako ambayo kila siku unakuwa unayawaza. Swali dogo la kujihoji ni je kila siku huwa unawaza nini?
    Je mawazo yako huwa ni chanya? Au mawazo yako huwa ni hasi?
Kama mawazo yako ni chanya ni hatua gani ambazo umekwisha kuzichukua mpaka sasa ambazo kimsingi umekuwa ukijivunia? Majibu naomba ubaki nayo maana wewe ndiye ujuaye.
Nawe ndugu yangu ambaye kimsingi kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukiwaza mawazo hasi, swali dogo ambalo unatakiwa kujiuliza kwanini umewekeza nguvu na akili zako katika kufikiri vitu hasi ? naomba nawe mwenye tabia hii naomba majibu usinipe.

Tumia kanuni halisi ya ubongo wako kufanikiwa.
Nimeanza kwa tafakari  hiyo fupi ili tuone kwa pamoja akili zetu tumezielekeza wapi? Na akili hizo hizo zinatupa matokeo gani ambayo yapo maisha yetu ya kila siku?
Kwa kuwa kama nilivyowahi kueleza hapo awali ni kwamba kanuni ya akili inasema ya kwamba wewe ni matokeo ya mawazo yako, hii ikiwa na maana kila ambacho unakiwaza katika mawazo yako ndicho ambacho kinachotokea katika hali halisi.
Hivyo kama mawazo yako ni hasi, basi hata kile utakochokifanya basi matokeo yake yatakuwa ni hasi, kama unawaza kutajirika kwa kuwa jambazi basi matokea yake ni jiandae kufungwa. Maana akiwazacho mtu ndicho kitakochomtokea.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba kama kweli umechoka hali uliyonayo hususani masuala ya umaskini, jitahidi ufuate mfumo wa kufikiria chanya kila wakati, maana matokeo ya mawazo chanya ni mafanikio ya kweli.
Asante kwa kusoma makala hii naomba uweze kuwa bora kwa kuwa na mawazo chanya kila wakati, kwani ukiwa hivyo mafaniko makubwa yanakuja kwa upande wako.
Ndimi afisa mipango; Benson chonya,
0757909942.

May 25, 2017

Sababu Sita (6) Ni Kwanini Unatakiwa Kuacha Kutumia Sukari Kwa Wingi.

No comments :
Kwa sasa vipo vyakula vingi sana ambavyo vimekuwa na sukari na tunavitumia karibu kila siku. Kwa bahati mbaya au nzuri vyakula hivi vya sukari vimekuwa vikipendwa na wengi bila ya kujali madhara yake kiafya yakoje.
Wengi wetu hatujui sana kiundani hasa pale tunapotumia vyakula vingi vya sukari, ni madhara gani ambao yanaweza kukutokea zaidi, tumekuwa tukijua juu juu tu kwamba ukila vyakula vya sukari vinaweza kukuletea shida hii au ile bila kuwa na uhakika sana.
Kwa sababu hiyo ndani ya makala haya ya afya, tutakueleza kinagaubaga sababu ya msingi ni kwa nini unatakiwa uache kutumia sukari kwa wingi mwilini mwako na ikiwezekana kuacha kabisa baadhi ya matumizi ya vitu vyenye sukari nyingi sana.
1. Sukari nyingi mwilini ni kisababishi cha magonjwa.
Matumizi ya sukari kwa wingi ni chanzo kimojawapo cha kuongezeka kwa uzito, lakini si hivyo tu sukari inapokuwa nyingi mwilini inaweza kukupelekea kupata magonjwa kama vile magonyjwa ya moyo na kuongezeka kwa shinikizo la damu jambo ambalo ni hatari kwa afya yako kwa kiasi kikubwa.
2. Sukari nyingi mwilini inapunguza uwezo wa kuona.
Mara nyingi wanaoutumia sukari kwa wingi sana au wale amabao viwango vya sukari vimeongezeka mwilini mwao,  moja ya madhara yake kwa baadae ni kutokuona vizuri. Hilo hutokea kwa sababu,  sukari inapokuwa nyingi hupelekea lensi ya jicho kuongezeka na matokeo yake matatizo ya macho huanza kujitokeza kwa mhusika.

Punguza matumizi ya sukari.
3. Sukari nyingi huozesha meno.
Bila shaka hili umeshawahi kulisikia au kuliona. Na mara nyingi hutokea sana kwa watoto, meno huweza kuoza baada ya matumizi ya sukari kwa wingi. Kinachotokea sukari huzalisha bakteria wenye sumu ambapo hao huweza kuharibu meno na kupelekea kuweza kuoza kabisa.
4. Sukari nyingi inapoteza uwezo wa mwili kukabiliana na magonjwa.
Wale wote ambao sukari inakuwa imeongezeka miili yao inakuwa haina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Unajua ni kwa nini? iko hivi,.. unapokuwa na sukari nyingi mwilini inatabia ya kuua seli nyeupe ambazo husaidia kupambana na magonjwa. Kwa hali hiyo ndio maana watu wenye visukari hawaponi vidonda kwa sababu kama hii.
 5. Sukari nyingi mwilini zinasababisha mwili kuonekana umeezeka.
Kila sukari inapokuwa nyingi mwilini, inazalisha kemikali ambazo baadae kemikali hizo hupelekea mwili wako kuanza kuoneana kama vile umezeeka. Hapa njia pekee ya kuondokana na hali hiyo ni kupunguza matumizi ya sukari. Vinginevyo utaanza kuonekana kikongwe.
6. Sukari nyingi husababisha viungo vya mwili kulegea.
Zipo ‘joints’ kama vile za miguu hasa pale unapokuwa unatembea zinakuwa zinachoka upesi na kulegea kama mwili wako una sukari nyingi. Hali hii hutokea sana hasa kwa wagonjwa wenye kisukari. Hii ninhali ambayo huwakuta wengi wagonjwa wa kisukari na inakuwa ni hali inayosumbua.
Mwisho kabisa hapa sina shaka mpaka unafika mwisho wa makala haya utakuwa umeelewa hatua za kuchukua na hiyo haitoshi ni vyema ukamshirikisha na mwingine makala haya ili aweze kujifunza na kundokana na matatizo ambayo pengine yangemkuta.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0628 92 98 16,




May 23, 2017

Mbinu Sita Za Ufugaji Bora Wa Kuku.

No comments :
Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu: Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu sana, na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja Tshs 10,000 mpaka 15,000, kuku wakubwa wanaanzia Tshs 15,000 mpaka 30,000).

Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi, kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote. Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio:

1. Aina ya kuku.

Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai.
Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti za mazingira.

Pia wanauwezo wa kutaga mayai mengi (Wastani wa mayai matano kwa wiki) karibu sawa na kuku wa kizungu. Aina ya kuku hawa ni kama vile, Chotara wekundu (Rhode Island Red), Black Australorp (Weusi/Malawi), Barred Plymouth Rocks (Madoa), New Hamshire Red, Kuroila wanapatikana sana Uganda, na Kari kutoka Kenya. Hizi ni aina ya kuku zinazo patikana Tanzania.

Chagua kuku waliobora
2. Chanjo.

Kama nilivyosema mwanzo, kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa lakini si kwamba hawayapati, kuna magonjwa ambayo ni hatari pia kwa kuku wa kienyeji. Chanjo ni muhimu kuwaepusha na hatari ya kuyapata magonjwa haya.

Chanjo muhimu kwa kuku wa kienyeji ni; New Castle, Gumboro, Marek’s na Ndui ya kuku. Fuata utaratibu wa chanjo kutokana na ushauri wa daktari. Hivi karibuni pia makala ya magonjwa na chanjo itakujia.

Jipatie vifaranga bora na incubators toka DM farm project

3. Chakula.

Kuku wa kienyeji pia wanahitaji mchanganyiko sahihi wa chakula, ili waweze kukupatia mazao mengi na bora, na kuwaepusha na magonjwa. Zipo fomula mbalimbali za chakula kutokana na umri wa kuku, na aina ya kuku.

Kuku wote wanahitaji chakula chenye mchanganyiko sahihi wa Madini, Vitamini, Protini, Fats, Wanga, Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi, na Maji safi. Muhimu kuwapatia kuku majani kama ziada ya chakula, hii hupunguza gharama za chakula na kuwafanya kuku waonekane wenye afya bora.

Ni vizuri kuwapatia vifaranga chakula spesheli cha dukani kama huna ujuzi wa kutengeneza mwenyewe. Kwani vifaranga wengi hufa kutokana na kutokupata chakula chenye mchanganyiko sahihi kwao. Kuku wa mayai pia wanahitaji mchanganyiko sahihi ili waweze kutaga mayai kwa wingi.

Wape kuku wako chakula bora.

4. Banda.

Kuku wa kienyeji pia, wanahitaji banda au nyumba ya kuku imara ili kuweza kuwakinga na baridi kali, wanyama hatari, na wizi. Banda pia liwe na semu nzuri za kutagia na sehemu za kulala ziwe juu , kwani kuku hupendelea kulala juu. Ni muhimu banda liwe katika hali ya usafi muda wote.

Kwa hivyo ni vizuri linyanyuliwe juu kidogo ili kuruhusu uchafu kuanguka chini na lijengwe ka kutumia mbao, mabanzi, milunda, nyavu, na mabati. Vifaranga wanahitaji kutenganishwa na kuku wakubwa. Banda si lazima liwe la gharama kubwa, kwani mafanikio ya ufugaji wa kuku ni vile unavyo waangalia na si banda. Mada inayohusu mabanda bora ya kuku itakuja hivi karibuni.

Tengeneza banda bora.
5. Majogoo kwa majike.

Ili mayai mengi yaweze kutotolewa, ni vizuri jogoo mmoja aweze kuwahudumia majike wasio zidi 7. Kwani kuku wanaweza kutaga bila ya jogoo, lakini mayai hayatoweza kuleta kifaranga. Ili mayai yalete vifaranga ni lazima yawe yamerutubishwa (Fertilized eggs) na jogoo.

Kwa hivyo ni vizuri kuweka Jogoo 1 kwa majike 7, hivyohivyo Jogoo 2 majike 14, Jogoo 3 majike 21, n.k. Pia hakikisha kuku wanao tumika kuendeleza kizazi ni wale wenye afya bora. 

Pata pia  majike na madume bora.
6. Vyombo vya chakula.

Hakikisha vyombo vya chakula ni visafi na vinawatosheleza kuku wote. Vyombo hivi ni vizuri vifanyiwe usafi wa mara kwa mara, ili kuwaepusha kuku na magonjwa. Maji machafu huwa ni chanzo kikuu cha magonjwa hasa ya kuhara. Hakikisha kuku wako wanabadilishiwa maji angalau mara mbili kwa siku.

Kuku wapewe chakula kwenye vyombo safi muda wote.
Kama msaada wa ufugaji wa kuku au kama unahitaji vifaranga na mashine za kutotoleshea vifaranga( Incubators) wasiliana nasi kwa 0767 04 80 35. Karibu sana.

May 22, 2017

Utajiri Wako Unacheleweshwa Hivi...

No comments :
Kwa jinsi binadamu tulivyo, tunaweza kuona vitu vyote ambavyo havionekani mbele ya macho yetu. Ukifuatilia kwa undani unagundua kuwa vitu ambavyo tunaambiwa na kuamini kuwa havionekani, kiuhalisia vitu vyote vyaweza kuonekana endapo ukiamua. Kwa mazoea, wengi tunafikiri kwamba kama kitu hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, basi tunasema...
hakipo. 

Ajabu na kweli ni kwamba, mtu asipoona kitu kwa macho yake ya kawaida, basi udhani kwamba kitu hicho hakionekani na wengine ufikiri kwamba kitu hicho hakipo kabisa duniani. Kumbuka kuwa kuendelea kufikiri na kuamini kwamba kitu fulani hakionekani au hakipo haina maana kwamba hakionekani kwa wengine! Wewe usipoona wengine wanaona.

Tunapodhani kwamba kitu fulani hakipo duniani, wakati kipo, moja kwa moja tunapoteza uwezo wetu wa ndani na nje wa kukifanya kile kisichoonekana kionekane mbele ya macho ya wengi.

Kwa binadamu ni akiri yake pekee iliyo na uwezo wa kuona vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Unapofikiri kwa kutumia akiri (ubongo), hapo tunasema kuwa umeona kwa macho ya akiri au ubongo. Pia, kile uonacho kupitia fikra zako, ndicho ambacho ukusukuma wewe kutumia rasilimali zilizopo, ili kukiweka katika uhalisia.


Kitu kikishakuwa kwenye uhalisia, basi hapo tutasema “umefanya kwa vitendo au umetenda”. Ukisha tenda, maana yake ni kwamba, unakifanya kile ambacho kilikuwa hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, kionekane sasa machoni mwa wengi. Endapo watu wataona kile ulichotenda, wasijidanganye kuwa “wameona BALI wajue wametazama”.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya “kuona” na “kutazama”. Kutazama siyo kuona, na kuona ni zaidi ya kutazama. Dhana nzima ya “KUONA” ni pale tunapoweza kutumia akiri kuota ndoto, halafu tukapiga picha, halafu tukapanga, tukaamini, na kisha tukatenda. 

Kwa maana nyingine ni kwamba, akiri (ubongo) ni kiwanda na karakana ya kuzalisha mambo mapya. Lakini pale tuonapo picha ya kitu kutokea nje (kwa macho ya kawaida), basi huko siyo “kuona” bali ni “KUTAZAMA”.

Binadamu wengi tunao uwezo wa kuona kila kitu endapo tunataka kufanya hivyo. Pamoja na uwezo mkubwa tuliopewa, bado hatuutumii katika kuona fursa za kujiondoa kwenye majanga ya umaskini. 

Watu waliofanikiwa mara nyingi wanatwambia kila siku kuwa popote tulipo Tanzania tumezungukwa na fursa nyingi. Kwanini sasa watu wengi ni maskini katika nchi iliyo na fursa nyingi? Jibu ni moja tu nalo ni watu wengi hawaoni fursa bali wanatazama fursa”.

Utajiri wa uhakika hautapatikana kutokana na watu wengi kutazama fursa BALI ni pale tu watu watakapoweza kutumia akiri zao kuona fursa na kisha kuanza kuchukua hatua za maksudi ili kuzifikia fursa hizo. 

Kumbe watu wengi tumekuwa ni watu wa “kutazama” fursa na siyo“kuona” fursa. Unapoona fursa unakuwa na ujasiri, nguvu na shauku ya kutenda ili kufaidi fursa husika. Lakini unapotazama fursa, mara nyingi unajawa sana na uoga, hofu inayotokana na wewe kukosa majibu muhafaka ya maswali unayojiuliza baada ya kuona kwa macho yako kile kilichofanywa na wenzako.

Unapotazama kitu kilicho mbele ya macho yako, mara nyingi utajiuliza maswali mengi bila majibu juu ya jinsi kilivyotengenezwa. Unapokosa majibu sahihi ya mswali yako, mara nyingi utapata hitimisho moja tu! Nalo ni “HAIWEZEKANI”. 

Ukishajiridhisha kuwa haiwezekani, basi unaamua kwenda kutazama fursa nyingine ambayo nayo utapata hofu na woga wa kuifanyia kazi. Mwisho wake unaishia kuwa ni mtu wa kutazama na kuongea tu! Huku ukizidi kuandamwa na maisha ya taabu na umaskini.

Watu wenye kuona fursa ndio wenye “maono”. Maono ni ndoto kujumlisha na ukweli wa mambo. Ukiwa na maono yafanyie kazi. Tumia macho ya akiri au ubongo kuona fursa. 

Ukitumia macho ya ubongo au akiri, utaweza kuona vinavyoonekana na visivyooekana. Fursa za uhakika hazionekani kwa macho ya kawaida. 

Usipoona fursa machoni mwako haina maana kwamba fursa hizo hazipo! ni uhamuzi wako tu! ukiamua zionekane na ziwepo basi, itakuwa hivyo. 

Lakini, ukiamua zisiwepo basi, hazitakuwepo wala hazitaonekana mbele ya macho yetu ya kawaida. Jambo hili aliwahi kulisisitiza mwanafalsafa wa Kifaransa aliyejulikana kama Henri Bergson kuwa “Jicho linaona kile ambacho akiri iko tayari kukiona au kuelewa”

Kutokana na maneno hayo ya Bwana “Henri Bergson”, tunajifunza kwamba fursa ambazo hazionekani machoni mwako, ni lazima uziite wewe mwenyewe ndipo zitakuja kwako na usipofanya hivyo watu wengine watafanya hivyo, mwisho wake fursa ulizotakiwa kuzifaidi wewe, utabakia KUZITAZAMA kwa jirani. Endapo jirani au watu wengine wasipoziita fursa hizo, basi zitaendelea kubakia katika hali yake hiyo ya kutoonekana, mpaka zitakapoitwa na vizazi vijavyo.

Leo hii Tanzania kama taifa tunaishi maisha duni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanaanzisha miradi ya biashara baada ya kutazamia kwa wengine. Ni bora ukaona mradi anaoufanya mwingine kuliko kuutazama. 

Watu wengi hasa Tanzania, huwa hawaoni miradi bali uitazama tu basi. Kwa maana nyingine ni kwamba, unapoona mwenzako akijishughulisha na mradi fulani wa kibiashara na wewe ukafanya kama anavyofanya bila kuongeza kitu chochote kipya, basi ujue kuwa mradi huo “haujauona”BADALA yake “umeutazama” tu!.

Ni nini faida za kufanya mradi ambao umeuona?
Kimsingi nchi inapokuwa na watu wengi ambao tunafanya miradi tunayoiona kwa macho ya ubongo au akiri zetu, ni wazi kwamba tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto na kero nyingi ambazo zinasababisha maisha magumu kwa jamii tunayoishi nayo. 

Pili, tutaweza kutengeneza bidhaa na huduma za thamani kubwa kwa watu wa Tanzania na dunia kwa ujumla. Tatu, tutasaidia katika kuharakisha ukuaji wa uchumi wetu binafsi na taifa letu kwa ujumla.

Watu wengi tukiona na siyo kutazama miradi ya maendeleo, tutaweza kutegeneza bidhaa nyingi ambazo ni tofauti tofauti. Tukiwa na bidhaa nyingi zenye ubora wa hali ya juu, ni wazi kwamba tutaweza kuvuta pesa nyingi kutoka kwa watu wengine hasa nje ya nchi. Watu wenye pesa zao, watapenda watume pesa zao kwetu, ili kupata bidaa na huduma na hivyo kutufanya sote tuwe na pesa nyingi. 

Kwa ngazi ya kitaifa ni kwamba watu kutoka mataifa ya nje watapendelea kutuma pesa zao Tanzania ili kununua suruhisho tulizonazo juu ya changamoto walizonazo kwao – hali hii ndiyo itachangia uwepo wa ajira na hatimaye nchi kuwa na uchumi mkubwa.

Hili tuwe na uwezo wa kuona miradi tufanye nini?
Katika hili hakuna namna na hakuna njia muhafaka ZAIDI ya kuzidi kuwekeza sana kwenye fikra. Ninaposema kuwekeza kwenye fikra ni zaidi ya watu kusoma hadi vyuo vikuu au kubobea kwenye taaluma fulani.

Uwekezaji mzuri kwenye fikra ni ule ambao unajifunza kila siku kwa kutumia njia mbalimbali, kama vile kujenga tabia ya kuwa mdadisi wa kila jambo/kitu na hasa yale yanayohusu kile ambacho unakifanya au unatarajia kukifanya.

Kabla ya kuanzisha mradi wako hakikisha unafanya utafiti wa kero na changamoto zinazowakabili watu waliokuzunguka au wengine wa mbali --- kwa kawaida kero inayo wapata watu waliokuzunguka mara nyingi huwa inawapata pia watu wengi walioko mbali na wewe.

Uzuri wa uwekezaji katika fikra hauna usumbufu na wala hauitaji gharama kubwa. Kinachohitajika ni nidhamu ya kufanya kile ulichopanga kukifanya hata kama ni kigumu. Kwa hiyo, huu ni uwekezaji ambao unaweza kufanywa na karibu wa aina yoyote, ilimradi mtu awe anajua kusoma na kuandika.

May 20, 2017

Jiongeze...Hauhitaji Elimu Kubwa Sana Ili Kufanikiwa.

No comments :
Hauhitaji elimu kubwa sana ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu bora ambayo unaihitaji au  unatakiwa uipate ni elimu ya kubadilisha maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu inayotoa thamani ya maisha yako na sio vinginevyo.


Kwa hiyo kama kwa namna moja au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika mahali unajilaumu kwamba ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea, huu sio wakati wa kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani itakayobadilisha maisha yako. na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani darasani, inatafutwa mtaani kwa watu sahihi.

Ni mzigo mkubwa sana kwako na kwa jamii kwa ujumla kuwa umesoma halafu hauna mafanikio makubwa. Kama iko hivyo kwako, jiongeze kidogo tu, anza kuisaka elimu sahihi, elimu ambayo itakupa thamani sahihi ya maisha yako na kukubadilisha na kuwa mtu wa mafanikio. Maisha ya mafanikio hayaji kwa kusoma saana, bali ni kwa kujifunza vitu sahihi ambavyo vina uwezo wa kubadilisha maisha yako.

Endelea kuipata elimu hii sahihi ya mafanikio yako kwa kuendelea kusoma dirayamafanikio.blogspot.com kila siku. 

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,