google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 31, 2017

Kama Unafikiri Mafanikio Utayapata Kwa Njia Hii, Sahau.

No comments :
Kujenga nidhamu binafsi na kuishi maisha unayoyataka wewe sio kitu rahisi kinachotokea tu mara moja.
Kujitoa na kufanya yale yanayotakiwa kufanyika ili kuweza kutimiza ndoto zako, halikadhalika hicho nacho si kitu rahisi.
Kuweza kutimiza ahadi zako na kuwa na mawazo zingativu juu ya ndoto zako pia nacho hicho si kitu rahisi kuweza kukufanikisha kama unavyofikiri.
Kupanga mipango yako na kufanyia kazi ili iweze kutoa mafanikio pia hicho sio kitu rahisi, kuna ugumu fulani unaojitokeza.

Ukiangalia katika maisha karibu kila kitu ambacho unataka kukifanya na kweli kikatoa mafanikio, kina ugumu wa aina fulani hivi.
Ukiona kuna jambo ukilifanya ni mteremko sana kwako na halihitaji wewe  kujibidiisha sana, ujue hapo kufanikiwa si rahisi sana pia.
Utaona mpaka hapo mafanikio yanahitaji nguvu na kujitoa sana kila wakati  na kila siku ili uweze kuyafikia.
Lakini ikiwa utaamua kuyaendea mafanikio kwa mkono wako mlegevu au kwa jinsi unavyotaka wewe kufanikiwa kwako itakuwa ni shida.
Hapa sina shaka unapata picha kamili kwamba hakuna kitu rahisi katika hii dunia. Kila kitu kina ugumu wake katika kukipata.
Ukiona mtu anakwambia mafanikio ni rahisi au wewe mwenyewe unaona mafanikio ya mwingine yamepatikana kama kwa urahisi vile, sio kweli.
Ipo namna yule mtu ambaye labda unamuona kafanikiwa kiurahisi kapigana na kuweza kufanikiwa kwa mafanikio yale.
Lakini ukiwa na ndoto za kufanikiwa huku umelala, na bila kijibiidisha vya kutosha andika utaumia hutaweza kufanikiwa popote.
Amua kwenye maisha yako kutenga muda wa kutafuta mafanikio yako, kubali kupigika kiakili, kimwili lakini usikubali ukashindwa kufanikiwa.
Unajua dunia tunayoishi ina kila kitu cha kukupa mafanikio. Kinachosababisha ukose mafanikio ni juhudi na nguvu zako tu na sio kitu kingine.
Kama unataka mali na pesa hizo zipo, lakini sio rahisi kuzipata, unatakiwa uweke juhudi na kufanya kazi kwa nguvu zote na kuachana na mchezo mchezo.
Kama utacheza na huku unasema unatafuta mafanikio makubwa, nikwambie tu ukweli huo ni uongo, ambao tena labda unajidanganya wewe na kuwadanganya na wengine pia.
Elewa hauna kitu ambacho cha kimafanikio ni rajisi katika maisha yako, ipo nguvu ambayo unatakiwa kuitumia ili kupata kitu chochote kile.
Chochote kile ambacho kinakupa mafanikio au chochote kile ambacho kinabadili tabia au hali yako na kuwa bora si rahisi sana kukipata.
Kama unafikiri mafanikio utayapata kwa njia ya urahisi, sahau. Unatakiwa kuweka juhudi kwa nguvu zako zote.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




Oct 30, 2017

Kama Utazingatia Hatua Na Mawazo Haya, Tayari Umefanikiwa.

No comments :
Siku zote ieleweke hivi, kama unarudia mawazo yako, kama unarudia hatua fulani hivi mara kwa mara ni wazi utakuwa bora sana kwa hicho unachokirudia kila wakati.
Haijalishi kitu gani unachokirudia sana kwenye mawazo yako yaani unakifikiria sana ila kitu hicho kitakuwa sehemu ya maisha yako kama utafanya hivyo sana.
Haijalishi ni hatua zipi utakuwa unazirudia sana kwenye maisha yako ila hatua hizo zitakua matokeo ya kitu fulani hivi kwenye maisha yako.
Ikiwa utatenga muda na masaa kadhaa kwa wiki kufikiria na kutenda jambo lolote lile katika maisha yako, uwe na uhakika jambo hilo utalivuna.

Kwa mfano, ukiona una maisha mabovu au una maisha mazuri ujue ni mwendelezo wa mawazo fulani ambayo ulikuwa nayo kwa siku za nyuma.
Mawazo yapi uliyonayo kwa muda mrefu, ni hatua zipi ulizonazo kwa muda mrefu hizo ndio hatua zinazokupa matokeo ya kitu fulani kwenye maisha yako.
Hauhitaji sana kumtafuta mtu pengine anayefanya maisha yako mabaya, kama iko hivyo kweli, ila unachotakiwa kufanya ni kukagua hatua na mfumo wa mawazo yako ukoje.
Wakimbiaji wote duniani  wanaelewa vyema kabla hujawa mshindi katika mbio lazima ufanye mazoezi mengi sana yatakayokufanya uwe mshindi.
Kuna wakati itakutaka ukimbie mbio za muda mrefu zaidi ya mashindano unayochukua na tena mara kwa mara hadi uweze kushinda.
Kuwa mshindi katika mbio kwa wakiambiaji wanajua kabisa sio swala la mara moja bali ni swala linalochukua mazoezi karibu ya kila siku.
Halikadhalika, hata washindi katika maisha ni watu ambao wanajuhudi endelevu  za kila siku kwenye maisha yao. Kitu hiki leo kikikataa kuna kingine kitafanyika hadi kieleweke.
Hivyo hata kwako inatakiwa ieleweke mawazo yanayojirudia mara kwa mara akili mwako, hatua zinazojirudia hizo ndizo zinazokupa mafanikio yako.
Mafanikio yako yanajengwa hatua kwa hatua, unatakiwa kujua hata kama hatua unazo chukua ni kidogo lakini hatua hizo zipo na ipo siku zitakufanikisha.
Una uwezo wa kufanya maisha yako kuwa bora zaidi ikiwa utakuwa na mawazo na hatua bora zinajirudia akilini mwako kila wakati.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 29, 2017

Acha Kuendelea Kufanya Kosa Hili Tena Na Tena Unapotafuta Mafanikio Yako.

No comments :
Kati ya kosa ambalo hutakiwi kuendelea kulifanya kwenye maisha ni kufanya vitu au mambo yako kwa kuingia na mawazo ya kujaribu.
Hili ni kosa kubwa ambalo linawangusha wengi wanaposema wanataka kufanya kitu fulani halafu wanasema hebu ngoja ni jaribu.
Unajua unaposema najaribu maanake nini?  hiyo ina maana hicho kitu ambacho unakifanya kwanza huna uhakika nacho kama utakiweza.
Kwa hiyo unapojaribu, usitegemee kama kuna ushindi wowote unaweza ukatokea, maana wewe si unajaribu.

Wale wote wanaojaribu sio rahisi kuweza kufanikiwa kupata ushindi, kwa sababu akili na kila kitu kinakuwa kimekaa kwa kujaribu jaribu.
Unapotaka kufanya jambo halafu ukaingia na mawazo ya kujaribu, kwanza hata ukishindwa unakuwa hauna uchungu sana, kwa sababu utasema ulikuwa unajaribu.
Pia hata hivyo, utakuwa ni mtu ambaye una sababu hata  kama ukishindwa, lazima utasema tu si nilikuwa najribu tu sio nilikuwa nafanya kabisa.
Kwenye maisha hakuna uwanja wa majaribio hata siku moja. Kama unafanya kitu au vitu vyako kwa kujaribu unajipotezea muda wako bure na unajidanganya.
Ikiwa kama kuna vitu umeamua kuvifanya, jitoe kufanya vitu hivyo kwa ukamilifu wako wote lakini sio kufanya majaribio.
Wakati wewe utaendeleakuendeleza wimbo wa kujaribu, wapo watu ambao wamejitoa kufanya kweli kwenye maisha yao na hawajaribu.
Najua hili ni kosa ambao umekuwa ukilifanya sana na limekuwa likagharimu maisha yako lakini si wakati wa kuweza kurudia tena.
Kimefika kipindi cha kusimamia ndoto zako, kimefika kipindi cha kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia na kuwa kweli.
Jaribu kujiuliza utaendelea kujaribu mpaka lini? Jipe muda wa kufanya mambo yako, achana na habari ya kujaribu maisha hayakusubiri hata kidogo.
Washindi katika maisha ni watu wa kufanya na si watu wa majaribio. Chagua kufanya kitu hata kama ni kidogo sana lakini kifanye na usijaribu hata kidogo.
Kujaribu mara nyingi kunakuandalia mazingira ya wewe kuweza kushindwa moja kwa moja. Hakuna mafanikio utakayoweza kuyapata kwa kuishi maisha ya kujaribu.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




Oct 28, 2017

Huu Ndiyo Ujasiri Unaotakiwa Kuwa Nao Ili Kuzishinda Changamoto Zako Mara Moja.

No comments :
Haijalishi maisha yako uliyonayo yakoje, yaani ya mafanikio sana au ya kushindwa sana, lakini jambo ambalo ni lazima utakutana nalo kila wakati ni changamoto.
Changamoto katika maisha zipo kwa kila mtu, haziangalia hali ya kipato au kitu chochote, changamoto zipo na zinatofautiana.
Ujasiri unaotakiwa kuwa nao ni kuzishinda changamoto hizo na kuamua kuweza kusonga mbele bila kujali ukubwa wa changamoto hizo.
Lakini ikiwa kila wakati utaamua kutulia na kuchelewa kutatua changamoto zako mapema, ujue unaongeza changamoto zingine tena.

Kivipi, sikiliza, kila ukiona unachangamoto ya aina fulani, ujue kabisa nyuma yake ipo changamoto nyingine ambayo unatakiwa uivuke na kuifanikisha.
Ukiona unakutana na changamoto halafu unajipa muda kwamba utaitatua baadae, ujue basi kabisa unakaribisha changamoto zingine nyuma yako.
Kila unapokutana na changamoto, unatakiwa ujue nyuma yake ipo changamoto nyingine, hivyo unatakiwa kuitatua changamoto uliyonayo haraka maana nyingine zitakuja tu iwe unataka au hutaki.
Uwezo wako wa kutatua changamoto haraka ndiyo utakao kufanya uzidi kuwa mshindi. Hakuna anayeomba kukutana na chagamoto, lakini changamoto zipo na zinataka majibu.
Zipo changamoto katika fursa tunazokutana nazo na pia zipo changamoto tofauti tofauti tunazokutana nazo kwenye maisha, hizi zote tunatakiwa kuzitatua.
Ikiwa unakutana na changamoto, kisha unasema utakuja kuzitatua kwa wakati fulani, wewe elewa kabisa utakuwa unakaribisha changamoto zingine zaidi.
Kitu ninachotaka uelewe hapa ni kwamba kila unapokutana na changamoto, itatue haraka changamoto hiyo kabla changomoto nyingine haijakufikia.
Ujasiri unaotakiwa kuwa nao katika changamoto ni kuamua kuzikabili changamoto zako na si kuzipa nafasi ya baadae kwamba utazitatua kesho au siku nyingine.
Kujipa muda kwamba changamoto zako utazitatua wakati mwingine huko ni sawa kuamua sasa kwamba changamoto zako zikumalize.
Na kwa bahati mbaya sana unaweza ukaona ni kitu cha kawaida tu kwako kuahirisha changamoto, lakini changamoto hizo zikizidi ndio utajua umuhimu wa kutatua changamoto haraka sana.
Ukumbuke hata mafanikio yanakuja si kwa sababu hakuna changamoto, bali mafanikio yanapatikana kwa kutatua changamoto zako mapema sana.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 27, 2017

Kipe Kipaumbele Kitu Hichi Kikupe Mafanikio.

No comments :
Hivi umeshawahi kujiuliza au unajua ni kitu gani ambacho ni cha muhimu sana kwenye maisha yako? je, ni afya, familia, imani yako au ni kitu gani?
Iwe kwa kujua au kutokujua kwa kawaida kipo kitu cha muhimu sana karibu kwa kila mtu kwenye maisha yake. Kitu hicho ndicho kinacho ongoza maisha ya mtu huyo.
Hata hivyo pia, kila siku maisha yanatuuliza kitu cha muhimu kwetu, na kwa bahati nzuri tunajibu kupitia vitendo vyetu na si midomo.
Kwa mantiki hiyo, hata nikikuuliza kitu kipi cha muhimu kwako hata usiponijibu najua vitendo vyako vitanijibu vizuri sana kuliko maneno yako.

Zipo namna nyingi amabazo zinaweza kukusaidia kujua kipi ni cha muhimu kwako au kwenye maisha yako na kipi si cha muhimu.
Unaweza kujua kitu cha muhimu kwako kwa kuangalia jinsi unavyotumia muda wako kufanya jambo fulani hivi.
Ikiwa muda wako umeutenga kufanya jambo fulani na kila siku na  jambo hilo unalifanya na huachi basi hicho ni kitu cha muhimu sana kwako na kina matokeo.
Chochote kile unachokipa muda wako mwingi hicho ndicho kitu cha muhimu bila kujali kitu hicho kina faida au hakina.
Inawezekana kabisa kitu cha muhimu kwako ikawa ni maongezi au kufatilia habari na inawezekana pia kitu cha muhimu kwako ikawa ni kufatilia ndoto zako.
Kitu kipi kitakachotufanya tujue kitu kipi cha muhimu kwako ni kwa jinsi wewe unavyotenga muda wako kwenye kitu hicho kila wakati.
Ukumbuke kitu cha muhimu kwako inaweza ikawa hata kuimba, kuangalia mpira ila kama kina kula muda wako basi hicho ndicho kitu cha muhimu kwako.
Maisha yako yako hivyo kutokana na kuna vitu ambavyo ulivipa umuhimu hivyo vitu ndivyo vimefanya uwe na maisha hayo.
Sasa ikiwa ulikuwa unatumia muda wako mwingi kwa vitu vya hovyo hovyo itakugharimu na kwa sababu havijakusaidia kitu.
Kuanzia leo, anza kufanya vitu vya muhimu kwako ili vikusaidie kukupa mafanikio bora leo na kesho kwenye maisha yako yote.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




Oct 26, 2017

Hatua Muhimu Za Matunzo Kwa Kuku Wanaokua.

No comments :
Katika matunzo ya kuku wanaokua, hapa tunaangalia mitemba au kuku wenye umri wa kuanzia miezi miwili hadi minne. Kuku hawa wenye umri huu wanatakiwa watunzwe vizuri ili wakusaidie kukupa mfugaji faida, vinginevyo ukishindwa hapa kutunza kuku wako vizuri basi usitegemee kupata faida kubwa.

1. Hatua ya 1, waweke kwenye banda kubwa.

Hatua hii inakuja kama walikua bado kwenye eneo la kulea vifaranga, wahamishe na uwapeleke kwenye banda kubwa. Kama banda ni hilo hilo moja, waondolee ‘hardboards’ ulizokuwa umetengea vifaranga, na waachie kwenye banda zima.

2. Hatua ya 2, wawekee bembea kwenye banda.

Ukumbuke kwamba kuku ni ndege, hivyo kuna wakati wanapenda kuwa juu. Hivyo ni muhimu kuwawekea bembea ili iwasaidie kufurahia maisha yao na kuwa huru zaidi. Hiyo itakuwa ni sehemu mojawapo ya kufanya zoezi.


 3. Hatua ya 3,  weka matandazo safi.
                                                                                                           
Hakikisha matandazo yasiwe na harufu kali au vumbi.  Hakikisha pia maji hayamwagiki bandani. Na Mara tu yakimwagika ondoa matandazo yaliyolowa na weka mapya. Pia ukumbuke kubadilisha matandazo mapema ili yasiweze kutoa halafu na kuleta magonjwa mengine yatakanayo na matandazo kurundikana.

4. Hatua ya 4, weka ratiba ya usafi.

Unaweza ukaweka ratiba ya usafi bandani na kwenye eneo la kuzunguka banda, angalau mara mbili kwa wiki. Tumia dawa ya V-RID kufanyia usafi na kupulizia dawa hewani. Hii itasaidia banda lako kubaki safi wakti wote na afya kwa kuku wako pia.

5. Hatua ya 5, wape kuku maji safi muda wote.

Pia unaweza kuwaongezea vitamin kwenye maji yao hasa kama wanafugwa ndani muda wote. unapowapa maji safi muda wote si rahisi sana kuweza kupata magonjwa yatokanayo na bakteria.

6. Hatua ya 6, wape chakula chenye virutubisho.

Usiwape kuku wako ilimradi tu chakula, wape kuku wako chakula chenye virutubisho vya kutosha. Unaweza ukaanza kuwapa ‘growers’ au aina nyingine ya chakula kizuri. Ukiwalisha kuku wako chakula duni, wanadumaa.

7. Hatua ya 7, rudia chanjo ya newcastle kwa wakati.

Hii unaweza kufanya yaani kila baada ya wiki 10 tangu walipochanjwa mara ya mwisho. Unaporudia chanjo inasaidia sana kuwafanya kuku wako wawe imara wakati wote na inakuwa ngumu kukutana na magonjwa.

8. Hatua ya 8, wape dawa ya minyoo.

Dawa ya minyoo unawapa kuku wakiwa na miezi miwili na rudia kila baada ya wiki 10. Ukishindwa kuwapa dawa hii basi tegemea kuokota kuku wengi ambao watakufa kutokana na kushambuliwa na minyoo.

9. Hatua ya 9, walishe majani na mboga mboga kwa wingi.

Unapowalisha kuku majani ya mboga mboga hiyo itawairishia miili yao kwa kuiongezea kinga dhidi ya magonjwa. Hata hivyo kama kuku wakilishwa majani ni rahisi pia kuweza kutaga vizuri inapofikia kipindi hicho.

10. Hatua ya 10, kama una eneo kubwa, wafungulie nje ili wazunguke zunguke.

Waache kuku wako wazunguke na waoge kwenye mchanga.  Kuzunguka zunguka na kuparua parua kunawafanya bize na kudonoana na kulana manyoya. Kuoga kwenye mchanga kunawafanya wawe safi na kama wana wadudu, wanaweza kuwaondoka.

11. Hatua ya 11, kuwa na mawasiliano ya karibu na daktari wa mifugo.

Mara tu uonapo dalili za ugonjwa, wasiliana na daktari wa mifugo kwa ushauri zaidi. Pia tafuta chanzo cha ugonjwa ili ukiondoe.

Mwisho wa somo letu la leo na tunaamini umejifunza kitu cha kukusaidia kuboresha ufugaji wako.

Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





Oct 25, 2017

Mbinu Bora Ya Kuishi Ndani Ya Bajeti Yako.

1 comment :
Hivi falsafa juu ya matumizi ya  bajeti ambayo ipo  ndani ya uwezo wako ikoje? Hili ni swali la muhimu sana ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kujiuliza kataka maisha yake ya kila siku. Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tabia ya watu wengi huwa wanaishi nje ya bajeti ambayo wanakuwa wamepanga.
Yote hii hutoka na sababu kubwa moja, sababu hiyo ni pale mtu ambapo amepata fedha nyingi kwa wakati mmoja. Kitendo hicho ndicho ambacho humfanya mtu kuweza kuishi nje ya bajeti yake ya kila siku.
Kwa mfano mtu akipokea mshahara hawezi kuishi maisha ambayo alikuwa ameyazoea ukifananisha na alipokuwa hana pesa, unakuta matumizi yanakuwa mengi kuliko pesa aliyonayo. Wapo wengine mara baada ya kutumia pesa yote hujikuta wanaingia kwenye madeni yasiyo ya msingi.

Achilia mbali madeni, wapo baadhi ya watu pindi wapatapo pesa utakuta wananua vitu vingi hata ambavyo hawakupanga kununua, tatizo hili lipo kwa watu wengi sana, siwezi ita tu ni tatizo bali ni ugonjwa wa matumizi ya pesa.
Niliwahi soma kitabu kimoja cha kanuni ya pesa, ndani ya kitabu hicho mwandishi anasema ya kwamba ukimpa mtu maskini pesa basi ndani ya sekunde kadhaa basi jiandae kujua tabia za mtu huyo, hii ni kwasababu ni mtu ambaye mara zote huongozwa na pesa, basi kila kilichopo mbele yake anataka kukimiliki yeye.
Lakini pesa hiyo ukimpa mtu ambaye anaelewa ni nini maana ya pesa,  basi  pesa hiyo huweza kufanya kitendo cha uwekezaji, ili pesa hiyo iweze kujizalisha yenyewe hapo baadae. Kwa nukta hiyo jaribu kutafakari  hivi pesa ambayo huwa unaipata mikononi mwako   unajiona upo kundi gani kati ya hayo niliyoyaeleza?
Kama utaona ya kwamba upo kundi ambalo umekuwa ni mtumiaji mzuri kuliko kuwa mwekezaji basi tambua lipo tatizo kubwa ndani yako, ambalo linakufanya uishi nje ya mstari wa bajeti yako, Hivyo unatakiwa kujua ni kwa namna gani unatakiwa kuishi ndani mstari bajeti yako kwa kuzingatia jambo hili.
Jambo Kwanza kabisa hakikisha pesa isikupelekeshe hasa pale unapoipata ila wewe ndiyo unatakiwa kuipelekesha pesa, kwa kuzingatia ya kwamba pindi utakapo ipa nafasi pesa ikuendeshe  basi tambua fika lolote linaweza kutokea ndani yako.
Lakini pia kwa  kuwa wanasema pesa ina makelele sana hasa pale unapoipata hivyo hakikisha pale unapoipata pesa unaishi kwenye pajeti yako ambayo umeizoa, kwani pindi utapopandisha bajeti yako eti kwa sababu umeipata pesa basi tambua ya kwamba  utaunganaa na wale wanaosema vyuma vimekaza.
Hivyo  pesa isiongeze matumizi yako ya kila siku eti kwa sababu umepata pesa, hivyo kila wakati jifunze kuishi ndani ya bajeti yako.
Ndimi; Benson Chonya

0757909942.

Oct 24, 2017

Kitu Hiki Ndicho Kitakachokufanya Ukue Sana Kimafanikio.

No comments :
Kitu chochote kinachokupa changamoto wewe, ni kitu hicho hicho ndicho kinachokufanya ukue na ujenge ukomavu kutokana na changamto unazopitia.
Unapokuwa unakutana na changamoto hizo, uwezo wako wa kutenda unaongezeka na unakuwa ni mtu mwingine hata mara baada ya kuvuka changamoto hizo.
Mara nyingi changamoto zinapoanza na kutokea kwenye maisha ya mtu ni mbaya sana, lakini kwa kiasi kikubwa zinasaidia kumpa mtu ukomavu.
Kwa mfano, kama unatembea kawaida huwezi kuwa sawa na yule anayepanda milima. Kwa vyovyote mpanda mlima ni rahisi kujenga misuli mikubwa ya mwili kuliko asiyepanda.

Changamoto ipi inayokukabili wewe? Changamoto hiyo kumbuka ndiyo inayokupa uzoefu na ukomavu mkubwa utakao kupa mafanikio yakutosha.
Watu wote wenye mafanikio makubwa, watu ambao ukiwaangalia wamefika mbali sana kimafanikio ni watu ambao wanapambana sana na changamoto kwenye maisha yao.
Huwezi kufanikiwa na kufika juu sana kwenye mafanikio yako kama wewe ni mtu wa kutoroka au kukimbia changamoto kila wakati.
Unatakiwa ufike wakati ujue ni kwa jinsi gani utakavyoweza kukabiliana na changamoto ili ziweze kukupa ushindi wa kimafanikio.
Changamoto kwenye mafanikio ni silaha au njia nzuri sana ya kuweza kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa au kufika mbali kimafanikio.
Ulimwengu una changamoto sana, ni changamoto hizo ndizo ambazo ukijua namna ya kukabiliana nazo zitakupa mafanikio makubwa sana.
Hakuna namna au hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuzikimbia changamoto. Uwe una pesa au huna, changamoto katika maisha zipo palepale.
Acha kuwaona watu wengine ni kama watu ambao maisha yao mazuri sana hayapitii kwenye changamoto zozote, changamoto kila mtu anazipitia na ndizo ziletazo mafanikio.
Kuwa miongoni miongoni mwa watu ambao wataamua kukua kutokana na changamoto wanazo kabiliana nazo kila siku.
Lakini ikiwa kila unapokutana na changamoto unalalamika sana au unaamua kukimbia kufanikiwa kwako itakuwa ni vigumu.
Washindi katika maisha wanakumbana na changamoto nyingi sana ambazo mwisho wa siku huwaacha wakiwa washindi kutokana na kuzishinda changamoto hizo.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 23, 2017

Jiandae Kwa Hiki Ili Kufanikiwa Katika Kila Jambo.

No comments :
Ili kuweza kufanikiwa katika jambo lolote kwenye maisha yako unahitaji kuwa na UJASIRI. Unahitaji kuwa na ujasiri wa kushinda hofu zako na pia unahitaji kuwa na ujasiri wa kushinda changamoto zozote zile zinazozojitokeza mbele yako.
Na ujasiri tunaouzungumza hapa hauji kwa bahati mbaya, ujasiri huo unakuja kutokana na maandalizi muhimu ambayo unatakiwa uyafanye. Hautaweza kuwa jasiri kama huna maandalizi ya muhimu kwako.
Inawezekana unaanza kujiuliza ujasiri huo utaujenga kwa vipi? Sikiliza, na twende kwa mfano. Mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa kusoma kabla ya mtihani, huyu anakuwa hana wasiwasi sana tofauti na  yule mwanafunzi ambaye hakusoma kabisa.
Halikadhalika wale wanaoongea mbele za watu alimaarufu ‘public speaker’ ambaye kabla ya kwenda kuongea usiku alifanya mazoezi, atakuwa ana ujasiri tofauti na yule ambaye hakuweza kufanya mazoezi na kuamua kwenda tu kuongea.

Hata katika maisha na mafanikio yako, unahitaji kuweka maandalizi ya nguvu ili kuwa na ujasiri na kufanikiwa. Maandalizi haya utayapata tu kwa wewe kuamua kufanya kazi kwa bidii na nguvu zote.
Kufanya kazi kwa juhudi na nguvu zote ndio kutakapokupa ujasiri wa kuweza kushinda hofu na kila aina ya woga ambao unakukabili.  Watu wote ambao hawana hofu sana katika maisha ukiwatazama vizuri  ni wachapakazi.
Ni wazi tu, hofu hiyo wanakuwa hawana na badala yake wanakuwa ni majasiri, unajua ni kwa sababu gani, ni kwa sababu wanakuwa wanajua hata mambo yagome vipi kwao hakuna kitu kitakachoweza kuharibika kwao.
Si jambo la kujiuliza sana unapokuwa unashindwa kuwajibika au kuchapa kazi kwa juhudi sana elewa tu kwa namna yoyote utaanza kukosa ujasiri na mwisho wa siku woga mwingi wa maisha yako utaanza kukuvaa.
Fanya wajibu wako. Fanya kazi kwa bidii sana bila kujali kazi unayoifanya ni ya aina gani na kwa kufanya kazi kwako huko utajikuta ukiwa ni mtu ambaye unavuta mafanikio kwa kiasi kikubwa sana kama sumaku.
Ujasiri ni kitu cha muhimu sana katika mafanikio yoyote yale. Kumbuka kama nilivyoanza kwa kusema bila kuwa na ujasiri huwezi kufanikiwa hata ufanyaje, zaidi utaendelea kubakia na maisha yako hayo.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 22, 2017

TANGAZO MAALUM; Mashine Za Kutotoleshea Mayai(Incubators) Zinazotumia Solar power au Betri, Zinapatikana Hapa.

5 comments :
Mashine itumiayo betri/solar power kwa ajili ya kutotoleshea mayai.


DM POULTRY FARM PROJECT kwa sasa mbali na mashine tulizonazo za kutotoleshea vifaranga, kwa sasa tunauza pia mashine za kutotoleshea mayai (incubator) zinazotumia SOLAR POWER AU BETRI YA GARI.
Mashine zetu hizi zina ubora wa kiwango cha hali ya juu na zinaweza kutumia umeme, solar power au betri ya gari. Kama umeamua kutumia umeme ni uamuzi wako ila umeme ukikatika unatumia betri yake maalum.
Vile vile mashine zetu hizi mpya  ni 'full automatic,' yaani zinafanya kazi kwa kujitegemea. Kwa maana hiyo zinafanya kazi katika mazingira yoyote yale iwe kijijini ambako hakuna umeme au mjini, kote ni sawa.
Karibu sana ujionee mashine zenye ubora na zenye viwango tofauti na ukubwa tofauti kutegemea na matumizi yako. Mashine hizi tunazo za mayai 45, 90, 180, 240, 300 na 500. 
Huhitaji kulalamika kwamba sina umeme, jibu la changamoto yako sasa limepatikana ikiwa utanunua mashine zetu.
Kwa maelezo zaidi au mawasiliano kuhusu oda yako, piga simu kwa namba 0767 04 80 35 na wote mnakaribishwa.
Mashine ikiwa ofisini kwetu tayari kwa kuuzwa.






Oct 21, 2017

Siri Ya Kupata Zaidi Kile Ukitakacho.

No comments :
Ni tabia au asili ya binadamu kila anachokipata kutaka kukipata zaidi na zaidi. Hapa yaani binadamu anakuwa ana shauku ya kupata kwa wingi zaidi.
Tabia au asili hii wewe unayo na mimi ninayo na kila aliye binadamu ili mradi anahema tu tabia hiyo anayo na anaitumia pia.
Kinachokuja kutofautisha ni matakwa ya utakaji wa vitu hivyo. Utakuta kila mtu anapenda kitu ambacho ni tofauti au hakifanani sana na mwingine ili kiwe kingi.
Kwa mfano, wapo wanaopenda wawe na mali au pesa kwa wingi, wapo pia wanaopenda wawe waimbaji wazuri na bora kabisa.
Pia wapo wale wanaopenda kupata idadi kubwa ya watu wanaowafatilia/ ‘followers’ hasa wasanii na wale watu ambao ni watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii.

Kila mtu kama nilivyosema kipo kitu ambacho anataka kiongezeke na kuwa kingi kabisa na kutokana na hilo, hufanya kila linawezekana kukiongeza kitu hicho.
Kutaka kile ulichonacho kiendelee kuongezeka sio jambo baya ni jambo zuri, lakini badala ya kuwa na shauku hiyo tu peke yake, unachotakiwa kufanya, ongeza juhudi.
Unajiuliza uongeze juhudi wapi? Ongeza juhudi ya kufanya zaidi kwa kile kitu ulichonacho au unachokifaya ili kikusaidie kupata mambo mengine zaidi.
Najua vizuri sana kuna kitu fulani unakifanya, kitu hicho kinaweza kikawa kidogo na kisikupe hamasa sana, lakini unatakiwa kuongeza juhudi ili kujenga mafanikio zaidi.
Hakuna kitachoweza kukusaidia kupata kitu unachokitaka kwa wingi zaidi kama hutaweka juhudi kwa unachokifanya. Juhudi yako itakupa matunda.
Ila kama unafikiri kila wakati unataka zaidi, kiuhalisia utaanza kujiona huna kitu kabisa, utaanza kuona maisha yako yapo tupu na huna kitu kabisa.
Ndio maana nasema unataka kupata kitu zaidi weka juhudi kwa unachokifanya ili kikusaidie kupata zaidi na zaidi.
Kuendelea kufikiri makubwa unayotaka bila kuweka juhudi utakuwa unatengeneza nguvu za kukufanya wewe mwenyewe ukashindwa kufikia malengo yako.
Acha kuendelea kuweka nguvu za mawazo yako kwa yale mambo ambayo hauna, weka juhudi kwa kile ukifanyacho, nguvu hizo zitakupa mambo makubwa.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na PURE KIENYEJI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 20, 2017

Usifanye Kosa La Kuwekeza Nguvu Hizi Tu Basi Kwenye Mafanikio Yako.

No comments :
Ili kufanikiwa kwa chochote kile unalazima kwa wewe kuanza kwanza jambo hilo. Hakuna kitu au mafanikio ambayo utayapata kama utabaki tu kuongelea mafanikio mdomoni. Kuanza ni lazima uanze bila kujali unaanza kwa namna gani.
Lakini hata hivyo kuanza peke yake hiyo haitoshi na wala hiyo siyo 'gerentii' ya mafanikio, unahitajika kuendelea kuongeza juhudi zaidi za kuweza kufanikiwa kwa kufanya kazi kila siku. Juhudi endelevu ni muhimu kwa mafanikio yako.
Watu wengi wanaanguka sana kwenye vile vitu wanavyofanya kwa sababu wanakuwa ni watu ambao wakati wanataka kuanza walikuwa ni watu wa juhudi sana, lakini mara tu wanapoanza, hujikuta wanajisahau na juhudii zile kuziacha mara moja.

Sasa inapotokea ukafanya hivi yaani ukaweka juhudi kubwa mwanzoni na mbeleni ukajisahau, kupiga kwako hatua inakuwa ni ngumu. Mafanikio yako ni rahisi yakaonekana kwenye hatua za mwanzoni huko mbele hakitaonekana kitu tena kama hutaendeleza juhudi.
Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa unatakiwa kukumbuka kila mara kuweka juhudi mwanzoni lakini na kuendelea kuweka juhudi hizo hizo kwenye kila hatua unayopitia. Hiki ni kitu muhimu sana na msingi sana kwa mafanikio yako.
Ndio maana siku zote huwa tunasisistiza unapotaka kuanzisha jambo acha kujiandaa sana, unapokuwa unajiandaa sana hiyo itakupelekea wewe kutumia nguvu nyingi mwanzoni na kujisahau kufanya majukumu ya msingi mbeleni.
Watu wengi wamejikuta katika mtego huu wa kushindwa kufanikiwa sana kwenye kila wanachokifanya kwa sasa kwa sababu tu ya kujivunia nguvu kubwa walizoweka mwanzoni na kusahau kuweka juhudi hizo mbeleni tena.
Ili kuelewa hili vizuri, angalia mfano mzuri wa miti mikubwa. Miti hii huwa inaanza kama kitu kidogo tu. Lakini katika kuendelea kukua hurefuka na mwisho wa siku kuwa mti mkubwa sana ambao kuukata inahitajika nguvu nyingi sana.
Halikadhalika, hata mto huwa unaanza kidogo kidogo lakini kwa jinsi unavyozidi kwenda mbele unakuwa una nguvu kubwa ya kuweza kusomba chochote kile kinachoweza kukatisha mbele.
Vivyo hivyo na wewe ndio unatakiwa kuwa hivyo. Anza na nguvu fulani hata kama sio kubwa sana, lakini nguvu hiyo endelea kuiwekeza ili iwe kubwa zaidi na zaidi. Kama hautafanya hivyo mafanikio yako yatakuwa ya muda tu na kutoweka mara moja.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,