google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 30, 2018

Kama Unataka Kuwa Tajiri, Anza Kufanya Biashara Hizi Kwanza.

No comments :
Katika dunia ya sasa zipo biashara nyingi ambazo mtu anaweza akachagua mojawapo na kuifanya, na kwa kuchagua huko biashara hiyo inaweza ikampa mtu huyo mafanikio makubwa na hadi kuweza kufikia utajiri mkubwa.
Hata hivyo pamoja na wingi huo wa biashara, kwa mujibu wa tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha zipo biashara ambazo ukizifanya zinaweza zikakufanya ukawa tajiri kwa haraka sana au zikakurahisishia njia ya wewe kwenda kwenye ubilionea wako.
Biashara hizi si mpya sana masikioni mwako unazijua, hapa nakukumbusha ili uweze kuzingatia kwa jicho la tofauti na pia kuzifanya kwa namna ya tofauti. Kwa kufanya biashara hizo kwa utofauti, utakuwa umemudu kuweza kupiga hatua ya kufikia mafanikio yako.
Biashara hizo ni zipi? Zifuatazo ni aina za biashara ambazo ukizifanya zitakupa mafanikio makubwa na yenye tija kwenye maisha yako.

1. Usafiri.
Moja ya biashara ambayo inaaminika hasa kwa bara la afrika ikiwa utaifanya kwa utulivu na ukafata misingi yake ni biashara ya usafiri. Hapa unaweza ukawa na kampuni yako ya kusafirishia abiria kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.
Kwa sasa hitaji la usafiri bado ni kubwa, kama si mjini hata kijijini. Watu wanataka kusafiri kila siku na kwa bahati mbaya wengi hawana uwezo huo wa kumiliki vyombo vya usafiri. Hii ni mojawapo ya biashara ya kuifikiria kuifanya kama unaweza, kwani itakupa mafanikio sana.
2. Afya.
Kama pia utajikita na kufanya biashara inayohususha mambo ya afya, basi upo uwezekano mkubwa zaidi wa wewe kufanikiwa sana. Huduma za afya katika maeneo mengi bado hazijafikiwa kisawasawa na zinahitajika kweli.
Hivyo kwa kufanya biashara hii, kama ukifungua hospitali au zahati au duka la dawa, utapata pesa na hapo pia utakuwa imeisaidia jamii. Kikubwa kubali kuzunguka kuangalia ni wapi ambapo ukifanya huduma au biashara hii wewe itakulipa.
3. Chakula.
Hakuna mtu asiyekula, hiyo ikiwa na maana ukianzisha biashara ya vyakula na ukaifanya kwa ufanisi mkubwa utafanikiwa. Hapa unaweza ukauza chakula, lakini si maanishi uje na picha ile ya mama ntilie ‘pasee.’
Ukiamua kuja na biashara ya kuuza chakula ifanye kwa ukisasa zaidi. Zipo sehemu bado nyingi zinazohitaji huduma hii ya chakula safi, mazingira safi, lakini hawaipati kwa uhakika kwahiyo unatakiwa ujue jinsi ya kuanza ili uanze kupiga pesa.
4. Viwanda vidogo vidogo.
Huwezi  kuendelelea sana kama utaendelea kuwa mlanguzi wa biashara za watu wengine. Changamsha akili na anza mchakato wa kuweka viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia wewe kuweza kukupa kipato kikubwa.
Uzuri wakuwa na kiwanda kidogo wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza kwa hiyo ni lazima utapata faida kubwa sana. Hapa unaweza ukatengeneza kiwanda chako cha kutengeneza juisi au unga wa sembe na lishe, uamuzi ni wako.
Kwa kuhitimisha, hizi ni baadhi ya biashara chache tu, ambazo unaweza ukazifanya na zikakupa mafanikio makubwa. Uamuzi ni wako uanze na biashara ipi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,


Nov 29, 2018

Kanuni Za Kujua Kusudio La Kuumbwa Kwako.

No comments :
Kila mwanadamu ameumbwa na kusudio lake hapa dunia. Pia itakuwa ni dhambi kubwa kama upo hapa dunia  pasipo kutambua hilo kusudio lako. Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika yale wayafanyayo hii ni kwa sababu watu hao wanafanya vitu ambavyo sio vyao bali ni  vya watu wengine.
Watu wengi tunaishi kwa kuigaiga mambo ya watu wengine, yaani utakuta mtu fulani anafanya jambo fulani kisha mtu mwingine naye anaanza kufanya jambo hilo , kitendo hiki ni kujipoteza wewe mwenyewe pasipo wewe kujua.
Hivyo zifuatazo ndizo kanuni za kujua kusudio la kuumbwa kwako;-

1.    Muombe mwenyezi Mungu.
Kwa imani uliyonayo basi unashauriwa kutumia imani hiyo hiyo kuomba Mungu akujalie ili uweze kufahamu kusudio lako uwepo wako katika sayari hii. Kwani ukweli ni kwamba Mungu wetu ni mwema na ni muaminifu pia, hivyo tunaamini anatambua kila mmoja wetu lengo lake ni nini hapa duniani.
2.    Hakikisha unafanya kitu ambacho unakipenda.
Miongoni mwa mambo ambayo humsaidia mtu ili aweze kujua lengo lake na kuwepo hapa duniani ni pamoja na kufanya mambo ambayo anayapenda.
Wengi wetu tunashindwa kufanikiwa katika maisha hii ni kwa sababu tunafanya vitu tusivyovipenda. Hivyo kila wakati unatakiwa kuhahakisha kila unachokifanya unakipenda kutoka moyoni mwako.
Kama unafanya jambo ambao hulipendi unashauri uachane na jambo hilo mara moja kwani ni sawa na kupoteza muda tu, kwani unatakuwa unafanya ilimradi siku iendee tu.
3.    Jitafute/wewe ni nani?
Unashauriwa pia ili uweze kutambua uwezo ulionao ni pamoja na kuwekeza muda mwingi wa kujitafuta wewe ni nani. Ninapozungumzia wewe ni nani hapa ni maana ya kwamba ni lazima uwaze kuwa wewe upo vizuri katika kufanya jambo gani?
Mara baada ya kupata majibu ya kwamba wewe upo vizuri katika jambo gani ndipo unapotakiwa kuwekeza nguvu, muda, akili na pesa katika kulikeleza jambo hilo.
Kama wewe ni mwanamitindo, mfanyabiashara, fundi au jambo lolote lile basi ni vyema ukaweka mkazo wa kiutendaji katika mambo hayo na si vinginevyo.
Pia ni ili uweze kujitambua wewe ni nani zinahitajika akili za ziada za kuweza kujitambua madhaifu na uwezo ulionao katika utendaji wa jambo fulani.
Katika madhaifu uliyonayo basi yafanyie kazi madhaifu hiyo ili weze kuondokana nayo kabisa, ila katika uwezo ulionao basi unatakiwa kuongeza juhudi ili uweze kufanya bora zaidi ya uwezo wako.
Hayo ni baadhi ya ya mambo ya msingi unayopaswa kuzingatia katika kutambua kusudio lako hapa dunia ili uweze kuishi maisha yenye furaha hatimaye kupata mafanikio unayoyataraji.
Ndimi Afisa mipango: Benson Chonya.
bensonchonya23.gmail.com

Nov 28, 2018

Usiruhusu Sauti Hii Ikakufanya Ukashindwa Kufanikiwa.

No comments :
Ni rahisi sana kwenye maisha yako kusikia hasa pale tunapofatilia ndoto zako mtu akakwambia kwa uwazi kabisa kwamba ndoto na mipango yako hiyo huwezi kutimiza labda tafuta kitu kingine cha kufanya.
Wengi tumesikia sauti hizi sana na tumekuwa makini nazo na hata kulaani wale wte waliotuambia kwamba hatuwezi kufanya hivyo. Lakini je, ukijiuliza hizo ndizo sauti unazotakiwa kuwa makini nazo sana tu peke yake.
Ni kweli sauti hizo zina madhara kwetu, ingawa mbali na sauti za nje ambazo zinakwambia huwezi hili au lile lakini kiukweli ndani yako unayo sauti ambayo mara nyingi ni chanzo kikubwa cha wewe kushindwa kwa chochote kile.
Sina shaka yoyote na wewe, najua umeshawahi kujiambia kwa kujiamini kwamba naweza kufanya jambo hili na nitalifanikisha, wengi hujiambia sana hivi hasa linapokuja swala la kuelekea kwenye kutimiza ndoto zao muhimu.

Hata hivyo pamoja na kujiambia hivi huku wakiwa na uhakika kwamba watakwenda kufanya vile walivyojiambia na kwamba inawezekana, lakini ndani mwao utashangaa inajitokeza sauti inayokwambia huwezi.
Sauti hii karibu kila mtu inampata. Sauti hii kwa wengi imewaambia sana hawawezi hata kwa yale mambo ambayo walikuwa wanaweza. Inatokea sana hata kama umejiaminisha unaweza, lakini sauti hiyo inakusisitizia huwezi.
Kikawaida sauti hii mara nyingi ipo sana ndani mwako. Unachotakiwa kufanya ili kuishinda sauti hii ni kujiambia naweza nyingi sana hadi uweze kufanikiwa. Lakini ikiwa utairuhusu sauti hii uwe na uhakika itakukwamisha na hutaweza kufika popote.
Sauti hii wewe unayo na mwingine yoyote anayo ila kikubwa unachotakiwa kufanya ni kujenga ule uwezo wa kupambana nayo hadi uishinde. Hebu angalia ndoto zako umekuwa unazo nzuri kweli, lakini ukitaka kufanya kuna kitu kinakwambia huwezi.
Naamini umeshawahi kukutana na kitu kama hiki sana na umekuwa hujui uchukue hatua gani. Kwa vyovyote vile sauti hiyo inapotokea kwako ni lazima ujifunze kusema naweza hata kama inakwambia huwezi vipi.
Ikiwa hautaweza kuushinda sauti hii ni kweli usishangae hata yale malengo yako ambayo ulikuwa ukiaamini kabisa kwamba utaweza kutimiza unaona nayo hayatimii kwa sababu ya kuambiwa huwezi.
Kwa jinsi unavyoisikia sauti hiyo ndani inayokwambia huwezi, inatakiwa uwe mwepesi sana kusema naweza. Usije ukaambiwa huwezi na sauti inayotoka ndani mwako  halafu ukabaki kimya, hapo ndipo utakuwa unajipoteza.
Unatakiwa kujenga maisha yako kwa kujimini sana kwa kijiambia unaweza mara nyingi uwezavyo. Lakini usiishie kusema unaweza tu kwa mdomo huku hakikisha uwe unachukua hatua pia.
Kwa kuchukua hatua huku ukisema unaweza hakika amini utaweza kutimiza ile mipango uliojiwekea. Badilisha mwelekeo wa maisha yako kwa kuiushinda sauti inayokuja ndani yako ya kusema siwezi na kuwa naweza, hapo utafanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Nov 27, 2018

Kipato Kikubwa Kinatengenezwa Kwa Kufuata Hatua Hizi.

No comments :
Katika nyakati za sasa, wakati ambapo dunia inakwenda kwa kasi na hali ya uchumi ikibadilika sana, ipo haja ya kila mtu kuweza kujifunza namna ya kuweza kutengeneza kipato kikubwa na cha kudumu.
Hiyo iko hivyo kwa sababu, bila kufanya hivyo, utaachwa nyuma sana kimafanikio na utajikuta ukiwa ni mtu wa pale pale, miaka na miaka. Una anzaje kujitengenezea kipato kikubwa wakati pengine mtaji wako ni mdogo?

  1. Anza na kidogo.
Katika harakati za kutengeneza kipato cha kikubwa na cha kudumu ni vyema ukajifunza kuanza na kidogo. Anzia pale ulipo ili kutafuta mafanikio yako. Chochote ambacho unaona kinakufaa kifanye, hata bila kuona haya.
Watu waliofanikiwa si kwamba walianza na mambo makubwa sana, hapana. Mara nyingi ni watu waliomua kukubali kukaa chini na kuanza na kidogo kile walichonacho ili kufikia mafanikio yao.
Ni jukumu hilo hilo ambalo unaweza hata wewe ukalichukua na kuanza na kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu kikamilike ndio uanze kufanya. Ukifanya hivyo, yaani kuendelea kusubiri utakuwa unajichelewesha mwenyewe kufanikiwa.
2. Jenga fikra chanya.
Hautaweza kutengeneza kipato kikubwa na  kufanikiwa kama kila wakati fikra zako zipo hasi, hasa linapokuja suala linalohusiana na mambo ya fedha. Ni lazima fikra zako ziwe chanya na kuamini kwamba una uwezo wa kutengeneza  pesa.
Acha kuendelea kung’ang’ania fikra mgando ambazo hata hazikusadii kitu, zaidi zinakukwamisha sana kufanikiwa. Watu waliofanikiwa kipesa na kutengeneza pesa nyingi, kila wakati huamini sana wao ni watu wa pesa.
Kwa kuamini kila siku na kuendelea kufanyia kazi yale wanayoyafanya bila kuchoka hujikuta wakiwa na pesa nyingi sana katika maisha yao. Kama leo hii unataka kutengeneza kipato kikubwa, jenga fikra chanya juu ya pesa na utafanikiwa.
3. Weka mipango imara.
Silaha pekee ya kuweza kufanikisha kujenga kipato kikubwa na cha uhakika ni kwa wewe kuhakikisha unakuwa na mipango ya kutengeneza kipato hicho. Ni muhimu sana kujiwekea mipango imara ili ikusaidie kutimiza lengo lako.
Kwa mfano, unaweza ukaweka mipango ya kuwekeza vitega uchumi vya aina tofauti tofauti ambavyo vitakusaidia katika kutengeneza kipato kikubwa. Ukishaweka mipango hiyo unaiweka kwenye utekelezaji.
Watu wenye mafanikio makubwa ndvyo ambavyo hujiwekea mipango yao kwa staili hiyo karibu kila siku. Lakini hawaishii kuweka mipango hiyo bali huchukua jukumu la kuifatilia kial siku. Hicho ndicho kitu unachotakiwa kukifanya ili ufanikiwe pia.
4. Kuwa mvumilivu.
Kila mafanikio yanahitaji uvumulivu wa aina fulani ili uweze kuyapata. Hakuna mafaniko ambayo unaweza eti ukayapata bila kuvumilia. Kipo kipindi ambacho kwa vyovyote vile ni lazima usibiri.
Hivyo wakati umejiwekea mipango na mikakati yako ya kukuwezesha kufanikiwa, tambua unatakiwa kuwa mpole kwa kukaa chini na kusubiri mchakato wa mafanikio yako kuwezekana.
Kila mtu aliye na mafanikio leo hii ukimuuliza ni lazima atakwamba alivumilia kwa namna fulani hivi na hakuyapata mafanikio hayo mara moja. Ili nawe uweze kujenga kipato kikubwa unahitaji uvumilivu wa kutosha. Jipe muda wa kuvumilia.
Kitu unachotakiwa ukijue mapema ili uweze kutengeneza kipato kikubwa ni kwamba, kipato hicho huwa hakitengenezwi kwa bahati mbaya. Mara nyingi huwa ipo misingi au hatua unazotakiwa  uzifuate kama ambavyo tulivyojadili kujadili.
Kumbuka zaidi ili uweze kutengeneza kipato kikubwa, unahitaji kuanza na kidogo, kujenga fikra chanya juu ya pesa, kuweka mipango imara na wewe kuwa mvumilivu. Ukiweza kuzingata mambo hayo. Hilo halina shaka, tayari utakuwa na uhakika wa kutengeneza kipato kikubwa.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com  kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,

Nov 24, 2018

Kwa Nini Hutakiwi Kuonyesha Udhaifu Wako Kwa Wengine?

No comments :
Kila mmoja wetu ana udhaifu wa aina fulani. Kwa mfano, kuna wengine wana hasira, kuna wengine wana huruma, na kuna wengine hawawezi kuficha siri. Kila mmoja ukiangalia ana udhaifu wa aina fulani, hata wewe upo udhaifu ambao unao.
Pamoja na kila mtu ana udhaiafu wake, lakini kitaalamu unashauriwa usijaribu kuuweka udhaifu wako huo kwa watu wengine kwa sababu, ipo siku watu hao watakaojua udhaifu wako watautumia udhaifu huo huo kuumiza wewe.
Hata ikitokea mtu huyu ni wa karibu sana, usimwambie udhaifu wako wewe kaa nao. Ndio maana hata kwenye biashara wengine wanashinda na kufanikiwa kwa sababu ya kujua udhaifu wa upande wa pili uko wapi na kuufanyia kazi.
Si kwenye biashara tu, hata kwenye vita, au kwenye mpira, wale wanaojua udhaifu wa wengine vizuri hao ndio wanaoshinda. Kwa hiyo kuweka udhaifu wako nje ni sawa na kuanza kujitangazia kwamba ni lazima utashindwa katika eneo fulani la maisha yako.



Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.

Katika mfano huo, ingawa wengi tunajua lakini unaonyesha Samsoni siri ya nguvu zake nyingi ambazo alitumia kuulia Simba na kupiga maadui zake zilikuwa kwenye nywele. Alikuwa hatakiwi kukata nywele kwa namna yoyote ile na hiyo ilikuwa ni siri kwake ambayo hakutakiwa kusema kwa mtu.
Lakini alipoulizwa na kubembelezwa sana ataje siri ya nguvu zake na mkewe, mwisho akajikuta akiisema, aliamua kuweka udhaifu wake nje, na matokeo yake wakati amelala aliweza kukatwa nywele na kukosa nguvu hizo alizokuwa nazo na matokeo mabaya yalimkuta kwa sababu ya kuonyesha udhaifu wake nje.
Unatakiwa kujua ni kitu kibaya na hatari kwako ni kujaribu kuuweka udhaifu wako nje na kila mtu auone. Huko ni kujitakia hatari kubwa sana ambayo inaweza kukupoteza wewe. Kama una udhaifu wa aina fulani kaa kimya, sio lazima useme.
Kikubwa kwako na kitu cha kufanya ni kuufanyia kazi udhaifu wako na kuhakikisha unakuwa bora. Lakini usijaribu kuweka udhaifu wako nje hata kwa rafiki, watoto au mtu wa karibu unayemwamini kama mkeo. Ni kosa kubwa kama kweli ukiamua kuanika udhaifu wako.

Amini usiamini ipo siku utaumizwa tu kwa wewe kuuweka udhaifu wako nje kama utafanya hivyo. Kwa hiyo dawa pekee ya kuweza kukwepa kuumizwa huko ni kukaa kimya na udhaifu wako na si kusema kwa kila mtu.
Achana na tabia ile ya watu utakuta anasema aah, mimi nina hasira ujue. Watu ipo siku watatumia hasira hizo hizo kukufanyia kitu ambacho wewe hujaamini. Kitu cha msingi hapa ni kuhakikisha unafunga mdomo wako na kuweka moyoni mwako udhaifu wako.
Neno la mwisho kwangu nikukumbushe, usijaribu hata siku moja kuonyesha udhaifu wako kwa wengine, watu hao watatumia udhaifu huo kama fursa ya kuweza kukuumiza wewe. Tafakari hili na utagundua ukweli hasa wa hiki nikisemacho.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,

Nov 23, 2018

Mbinu Za Kujitofautisha Kibiashara Hatimaye kupata Faida.

No comments :
Babu yangu aliwahi kunisihi ya kwamba kufanya biashara na hatimaye kufanikiwa katika biashara hiyo kunahitaji juhudi za maksudi kutoka kwa mfanyabishara husika. Hii ni kwa sababu kufanya biashara ni kumsubiri mteja ambaye huna imani ya kwamba atakuja ama la.

Pia ulimwengu wa sasa kila kitu kinachonekana kwa macho  kimekuwa ni biashara na biashara hizi asilimia 99.9 ni biashara ambazo zinafanana, hivyo ili uweze kuona unafanikiwa katika biashara hiyo ni lazima uwaze juu ya kujitofautisha kibiashara hatimaye upate faida.

Swali linaweza kuja ni je najitofautishaje kibiashara? Wala usipate tabu nipo hapa kwa ajili ya kukata kiu ya maswali yako kama ifutavyo:-


Ili uweze kuwa ni mtu wa tofauti katika biashara unayoifanya unatakiwa kuhakikisha unajikita zaidi katika kuhakikisha unatangaza biashara yako kwa kiwango cha hali ya juu na ya kipekee, kwani ukweli ulio bayana na usiopingwa ni kwamba biashara nzuri na yenye kuleta faida kubwa chanzo chake ni matangazo.

Jambo jingine linakalokusaidia kuwa ni mtu wa kitofauti katika biashara yako ni kuhakikisha ya kwamba unaboresha zaidi katika kitengo cha huduma kwa wateja. Mfanye mteja wako asikuchoke yaani kuanzia anapokuja mpaka anapoondoka, awe ni mtu ambaye anajisikia furaha na amani muda wote na hii yote itatokana na vile ambavyo utakavyompokea na kumuhudumia.

Pia jifunze kuweka mazingira ya ofisi yako katika muonekana nadhifu na wenye kuvutia kila mteja anayepita au anayekuja, hii ni kuanzia mapambo yako, upangaji wa vitu vyako vya kuuza na vile visivyo vya kuuza pia.

Mwisho kabisa kila wakati unatakiwa kukumbuka hakuna mteja anayependa kucheleweshewa kupata huduma, hivyo jifunze kutoa huduma yako kwa haraka na kwa wakati muafaka.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada, kazi ibaki kuwa kwako katika utekelezaji wa hayo niliyoyaeleza. Nikutakie siku njema na mafanikio ,ema, na Mwenyezi Mungu akawe pamoja nawe katika utekelezaji wa majukumu Yako.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942


Nov 21, 2018

Ongeza Umakini Sana Kwenye Maamuzi Haya Na Utafanikiwa.

No comments :
Tafiti nyingi zinaonyesha binadamu anafanya maamuzi  madogo madogo zaidi ya 300 kwa siku moja tu. Maamuzi anayoyafanya ikiwa ni pamoja na ale nini, avae nini, aende wapi, aongee na nani, aamke saa ngapi, afanye biashara gani, ni maamuzi madogo madogo lakini hadi yanafikia zaidi ya 300 kwa siku moja peke yake.
Inaweza ikakushangaza kidogo, lakini ukweli ndio huo hapo kwamba kwa siku unafanya maamuzi zaidi ya 300. Hivyo na kwa sababu hiyo, unatakiwa kujiuliza maamuzi hayo unayofanya ingawa wakati mwingine unaweza usiyaelewe sana ni ya aina gani? yanakusaidia au yanakuharibu? ni muhimu sana kujiuliza swali hilo.
Kwa mfano, kama kila siku unafanya maamuzi ya kula vyakula vya hovyo kama vile vyenye mafuta, kiafya unategemea nini? Au kama kila siku unafanya maamuzi yasiyo ya msingi kwa kutumia pesa zako hovyo unategemea kweli itafika wakati utafikia ule  uhuru wa kifedha? Maamuzi mabovu kama hayo ni rahisi tu kukudondosha.
Ukiangalia tokea muda una amka asubuhi hapo ndipo maamuzi yako yanapoanzia, najua utaamua uamke unafuraha au huzuni, au  utaamua siku hiyo ufanye kazi kwa bidii sana au kwa ulegevu. Yapo mambo mengi sana ambayo utaamua lakini yote yana matokeo kwenye maisha yetu bila kujali matokeo hayo ni hasi au chanya.

Tambua, ikiwa asilimia 90 ya maamuzi haya madogo madogo unayoyafanya kila siku hayapo sahihi, basi hakuna ubishi lazima ushindwe kwenye maisha. Pia ikiwa maamuzi haya madogo madogo unayoyafanya yapo sahihi kwa asilimia 90, ujue unao uhakika wa mafanikio kabisa na hakuna ubishi.
Kazi kubwa inabaki kwako maamuzi unayoyafanya ni ya aina gani? Ndio maana unatakiwa usikurupuke, kichwa chako kinatakiwa kutulia na kujua maamuzi unayoyafanya yanakupoteza kwenye njia ya mafanikio au yanakuweka kwenye njia halisi ya kufanikiwa kwako.
Kama nilivyotangulia kusema, huwezi kuwa na maamuzi ya hovyo ukategemea kufanikiwa. Mafanikio yako yanategemea sana na maamuzi yako ya kila siku. Kwa lugha nyingine kipimo sahihi cha mafanikio yako ya kesho kinatokana na maamuzi yako ya kila siku unayoyafanya.
Kama kila siku ukiwa makini na maamuzi yako, ni rahisi sana kujua wewe kama kweli utafanikiwa au hautafanikiwa. Ukiongeza umakini kidogo na kujua sawasawa maamuzi unayoyachukua kila siku, basi utaelewa nisemacho hapo, juu ya umuhimu wa kuyaangalia maamuzi yako kila siku.
Mwisho kabisa elewa hivi, kila maamuzi unayoyafanya yana matokeo kwenye maisha yako, eidha matokeo mazuri au mabaya,  inategemea tu ni maamuzi gani ambayo umeyafanya. Hivyo kila siku ongeza umakini kwenye maamuzi yako na  hakikisha unafanya maamuzi sahihi ili ujenge maisha yako ya mafanikio kwa usahihi  pia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,






Nov 20, 2018

Sababu Tano (5) Kwa Nini Unaogopa Sana Kushindwa.

No comments :
Kati ya kitu ambacho watu wengi sana wanakiogopa ni kule kushindwa. Ukiwauliza watu hao kwa nini wanaogopa sana kushindwa kwenye kile kitu wanachataka kufanya, sana sana watakwambia sababu moja tu kwamba wanaogopa kupata hasara.
Watu hawa wanakuwa hawana sababu zingine makini za kwa nini wao wanaogopa kushindwa, na hali ambayo inawasababishia wao hata washindwe kuchukua hatua. Suala la kuogopa kushindwa lipo kwa watu wengi sana, na unaweza ukawa miongoni mwao.
Hebu tuulizane mimi na wewe, au nikuulize je, unajua hasa kwa nini watu wanaogopa sana kushindwa, iwe kuogopa kushindwa kwenye mradi, kwenye masomo, au kwenye usaili, lakini woga huo upo tena kwa sehemu kubwa tu, naamini unalijua hilo.
Sina shaka unafikiri na kujiuliza aisee ni kweli watu tunaogopa kushindwa na una hamu ya kutaka kujua sababu zake ni zipi hasa zinazofanya watu waogope sana kushindwa. Tulia hapo hapo, nikupe sababu yakinifu  za kwa nini watu wengi wanaogopa kushindwa.

1. Ufinyu wa mawazo.
Watu wanaogopa kushindwa kwa sababu ya ufinyu wa mawazo au akili zao zinakuwa  kama vile zimefikia ukomo. Kivipi? Mtu anakuwa anaogopa kushindwa kwa kuamini kwamba akishindwa ndio hana nafasi tena ya kujaribu, kwa hiyo hawezi kufanikiwa hata iweje.
Ukiwa una mawazo haya yanayoamini nafasi pekee ya hicho ukifanyacho ni moja tu na haitajirudia kwako tena, basi utaogopa sana kushindwa. Hutaweza kufanya biashara kwa usahihi au chochote kwa sababu utaogopa kama ukishindwa ndio umepoteza na kupotea.
Maisha hayana nafasi moja kama unavyofikiri. Ukishindwa leo, kuna nafasi ya kujaribu tena na tena mpaka utafanikiwa. Ukiondoa ufinyu wa mawazo au ‘limited mind’ ya kuamini kwamba ukishindwa ndio basi, hutaogopa kushindwa tena, upo?
2. Kutaka kuonekana sahihi wakati wote.
Leo kila mtu akifikiria kufanya jambo anataka kuwa sahihi sana mbele ya watu. Anataka kufanya jambo lake huku akiwa amekamilika kwa asilimia mia moja. Mtu huyu anasahau kabisa kwamba hata wale anaowaona wamekamilika walianza wakiwa hawajakamilika.
Kwa mawazo hayo ni lazima, piga ua garagaza, mtu huyu ataogopa kushindwa. Kila wakati akitaka kufanya jambo anakuwa anajiuliza je, nikishindwa itakuwaje, si nitachekwa na watu na nitaonekana sifai.
Kwa hiyo hapa na kwa kifupi, kinachowapoteza watu wengi na kuogopa kushindwa ni kwa sababu ya kutaka kuanza kwa ukamili, ukiwa sawa kila kitu. Kwa sababu hiyo kuogopa kushindwa huwezi kukwepa hata iweje, umeidaka hiyo?
3. Athari mbaya tulizofundishwa shuleni.
Tokea tukiwa shule au tukiwa wadogo tumefundishwa na kukaririshwa na kwa bahati mbaya na sisi tukameza kama kasuku na kujua kwamba kushindwa ni kitu kibaya. Hakuna ambaye kafundishwa kushindwa ni kitu kizuri.
Ili kukuhakikishia kushindwa ni kitu kibaya, tena tukawekewa na viboko, ukizingua  tu kwa kushindwa unacharazwa bakora zako ili kesho usishindwe. Kwa hiyo kila wakati ulikuwa ukiwaza mmh nikishindwa tu, kimenuka.
Sasa nikuulize, je, uliyepitia mazingira kama haya utakwepa kuogopa kushindwa? Hapa ni lazima utaogopa kushindwa tu na utakuwa unaona kushindwa ni kosa kubwa sana. Hivyo utafanya kila linawezekana usishindwe, kumbe ndio umepotea, umeiona hiyo?
4. Kuhofia kuchekwa.
Eti unaogopa kushindwa kwa sababu ya kuogopa kuchekwa, unasema daah, hivi nikishindwa watu watasema nini, si watanicheka sana na itakuwaje. Kwa sababu hii tu, aloo, lazima uogope kushindwa na hutaweza kuchukua hatua.
Unajua kila mtu anataka kuonekana simba, anataka kuonekana anafanikiwa kwenye jamii, sasa kwa mawazo hayo mtu anataka mambo yake yaonekane yamewaka hakuna kushindwa, hapo ndipo hofu inapoanza kuzalishwa sasa.
Kwa mtu mwenye mawazo kama hayo ya kuogopa kuchekwa, wee, utamwambia nini, badala ya kuweka nguvu zake kwenye kuchukua hatua, yeye anakomaa na kuogopa kushindwa kwa kile anachotaka kukifanya, hatari hiyo umeisoma eeh?
5. Kutokujiamini.
Sababu  nyingine ya kiufundi ya kuogopa kwetu kushindwa ni kwa sababu hatujiamini. Hauamini kwamba eti unaweza ukatoka kwenye kushindwa hadi kufanikiwa. Haumini kama ndani yako unao uwezo mkubwa wa kukusaidia kufanikiwa.
Kama hujiamini kuogopa kushindwa kunakuhusu sana tu na tena sana. Kama huamini uwezo wako, basi hiyo kwako itakuwa ni sababu ya msingi sana itakayokufanya uogope sana kushindwa kwa chochote kile, unachotaka kukifanya.
Kwa kujifunza sababu hizi zinakufanya uogope kushindwa naamini zimekuondolea hofu kwa kiasi, lakini elewa hivi, huwezi kufanikiwa pasipo kushindwa, kwani kushindwa ni sehemu ya mafanikio. Hivyo usiogope sana kushindwa, bali kushindwa huko kufanye kuwa ngazi ya mafanikio yako. Na piga marufuku kuogopa kushindwa maishani mwako kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,


Nov 18, 2018

Mambo Kumi Utakayofaidika Nayo Kupitia Kujifunza Kila Siku …

No comments :
Watu wanao anguka sana kwenye maisha na hawafiki mbali ni wale watu ambao hawajifunzi iwe kwa kusoma vitabu au kujifunza kwa wengine. Ipo faida kubwa sana ya kujifunza ambayo wengi hawaijui na kuchukulia mambo kwa kawaida tu.
Labda nikwambie hivi, ikiwa husomi vitabu ni kweli unaweza ukafanikiwa, lakini hutaweza kufikia mafanikio yale ya juu sana. Utaishia tu kwenye haya mafanikio ya kawaida. Sasa je, faida za kusoma vitabu ni zipi?
Hapa kwenye makala haya nimekuwekea faida kumi na kwa kifupi tu ambazo unaweza ukazipitia na kuchukua hatua.

1. Ukisoma vitabu, utakuwa unakua kila siku kimafanikio angalau kwa asilimia moja tu, kuliko ambavyo ungekaa  bila kujifunza kupitia vitabu.
2. Ukiamua kusoma vitabu, itakusaidia kuvunja baadhi ya tabia zako mbaya na zinakupeleka wewe ushindwe, na kutengeneza tabia zaidi za kimafanikio.
3. Vitabu vinakuepusha na kukwepa kufanya makosa , ambayo watu wengi wanayafanya karibu kila siku kwenye safari zao za mafanikio.
4. Kupitia kusoma vitabu, vinakupa hamasa na nguvu ya kusonga mbele zaidi hata pale ambapo kuna wakati unajiona unakosa hamasa, vitabu vinakupa nguvu hiyo.
5. Pia faida nyingine ya vitabu, vinakupa uwezo zaidi wa wewe kuweza kujiamini na kuona kwamba kumbe unaweza kufanya kitu kwenye maisha yako .
6. Vitabu vinasaidia kukutengenezea mfumo mpya wa maisha na ambao hata hukuwa nao, yaani unakuwa unajishangaa unakuwa mpya kila siku iitwapo leo.
7. Kujisomea vitabu pia inasaidia wewe kuweza kutengeneza mazingira ya wazi ambayo yatakusaidia sana kuweza kufanikiwa tofauti na ambavyo kama hujisomei kabisa.
8. Vitabu vinakusaidia wewe kuweza kufanya mabadiliko madogo madogo na kila siku, ambapo mwisho wa siku unashangaa unafika mbali sana kimafanikio.
9. Vitabu vinakupa msukumo wa kurudi kwenye njia kuu hasa pale unapokuwa umetoka kwenye njia kuu hii ni mojawapo ya faida kubwa sana kuijua.
10. Na muhimu zaidi, vitabu vinakufanya wewe unakuwa mtu wa kuchukua hatua zaidi kila siku. Kama ulikiwa unashindwa kuchukua hatua vitabu vinakusukuma kufanya hivyo.
Kwa uchache hizi ni faida ambazo wewe utakazopata kupitia kujisomea, unasubiri nini tena? Washa moto zaidi wa kujisomea.…
.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Nov 17, 2018

Kila Wakati Zitumie Kanuni Hizi Muhimu Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.

No comments :
Leo nitaomba nichukue walau dakika chache ili niweze kukumbusha kanuni sita za kukupa mafanikio unayoyahitaji. Hizi ni kanuni ambazo ukizitumia na kuzifanyia kazi ni lazima zikupe matokeo makubwa kwa ajili ya mafanikio yako.

Wengi wanaozitumia kanuni hizo zinawasaidia sana kupiga hatua na kuwafanikisha. Kila wakati jaribu kuzitumia kanuni hizi kwa ajili ya manufaa yako na ya wengine pia. Usitoke hapo ulipo twende pamoja katika somo letu la leo tujifunze kanuni hizi;-

1. Kanuni ya 1; Chukua hatua stahiki.

Miongoni mwa vitu vitakuvyofanya uzidi kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa ni pamoja na kuendelea kuchukua hatua stahiki kwa hicho unachokifanya au kile unachotaka kufanya. Kushindwa kuchukua hatua huko ni kuchagua kujiangusha wewe mwenyewe.

2. Kanuni ya 2;Tumia siku yako vizuri na kwa uhakika.

Mafanikio siku zote ni matokeo ya vile unavyoitumia siku yako vyema, hivyo ulivyo leo ni matokeo ya hatua ulizozichukua siku ya jana. Hivyo jifunze kuitumia leo yako vyema ili uishe kesho yako yenye mafanikio na furaha tele.


 3. Kanuni ya 3; Jenga mtazamo sahihi kila wakati.

Hivyo ulivyo leo katika suala la mafanikio ni matokeo ya mawazo yako. Kama mawazo yako ni hasi basi hata maisha yake yatakuwa vivyo hivyo. Kama unataka unataka kubadili maisha yako, basi badili na mawazo yako na kuwa chanya.

4. Kanuni ya 4; Tafuta njia ya mafanikio yako.

Kama tutaamua kutafuta mafanikio ya kweli ni lazima tutafuta njia ya kuyapata mafanikio hayo, ila kama hatuhitaji mafanikio ni lazima tutafuta visingizio. Hivyo ili tuweze kufika katika kilele cha mafanikio tunatakiwa kutafuta njia ya kupata mafanikio hayo.

5. Kanuni ya 5; Jenga uwezo wa kutatua changamoto;

Katika maisha haya kila kitu kinawezekana, kama kuna jambo unaliona ni changamoto na haliwezekani basi mahala hapo ndipo palipo na fursa lukuki zilizojificha, hivyo jifinze kushughulika na kila changamoto zilipo katika jamii yako kwani hapo ndipo palipo na fursa.

6.  Kanuni ya 6; Toa hofu zako.

Siraha hatari zaidi duniani si bunduki wala mabomu ya nyuklia kama wengi wadhanivyo, bali siraha hatari zaidi duniani ni hofu. Hofu ndio chanzo kikubwa cha kuua ndoto za walio wengi, wengi wetu tunashindwa kuthubutu kufanya jambo fulani eti kwa sababu ya kwamba tunaogopa kitu fulani.

Hivyo kama kweli unataka kupiga hatua za kusonga mbele tunatakiwa kuhakikisha ya kwamba tunaondokana na hofu, kwani hofu ni adui nambari moja wa mafanikio.

Asante sana kwa kusoma makala haya kupitia mtandao huu wa Dira Ya Mafanikio, nikutakie siku njema na mafanikio mema.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com