google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 31, 2018

Mawazo Yanayofanya Maisha Yako Yabadilike Ni Haya Hapa.

No comments :
Maisha uliyonayo mara nyingi sana ni matokeo ya yale mawazo ambayo unayo wewe. Uumbaji wa maisha yako yawe ya mafanikio au kushindwa, unaanza na mawazo.
Mawazo ndiyo chanzo cha uhalisia ambao unaona kwa nje. Kitu chochote unachokiona, kabla hakijawa hivyo, kilianza kama mawazo.
Mawazo yako yanapoanzia, hayaanzii sehemu nyingine zaidi kwenye akili. Hapa nikiwa na maana akili yako ndiyo inayotengenezea uhalisia wa matokeo ya nje.
Hiyo ikiwa na maana, chochote kile unachokiweka kwenye akili yako  kwa mda mrefu, ujue kitu hicho itafika muda utaona matokeo yake yakitokea kwa nje.
Hakuna namna ambavyo unaweza ukaficha, wewe ni matokeo ya vile unavyoviweka ndani yako na sio matokeo ya kitu kingine.

Ubora wa maisha yetu unategemea sana ni kwa namna gani, ambavyo tunajilisha mambo ya aina gani kwenye akili zetu.
Mawazo yanayofanya maisha yetu yabadilike iwe yawe mazuri au mabaya si mawazo mageni sana kwetu, ni mawazo yaleyale ambayo tunakuwa nayo kwa muda mrefu.
Inapotokea ukawa na mawazo ya aina fulani na kwa muda mrefu kwenye akili yako na yakijirudia tena na tena, mwisho wa siku hutokea kwa uhalisia.
Haupo muujiza katika hili hata kidogo, maisha yako yapo hivyo hapo kutokana na mawazo ambayo unayo wewe na umeyashikiria pengine kwa muda mrefu sana.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo unatakiwa kuwa na mawazo tulivu, mawazo ambayo yatakusaidia na si kuweza kukubomoa.
Haijalishi kiwango cha elimu ulichonacho, pesa ulizonazo au umri ulionao, lakini unao uwezo wa kufikiria mawazo yako kwa kwa ubora zaidi siku hadi siku.
Jiulize ni kitu gani ambacho unachagua kufikiri kwa kadri siku zinavyozidi kwenda? Je, unachagua kufikiri mawazo ya faida au ya mawazo yale ya kushindwa kwako?
Ruhusu ndani yako uwe na mawazo mazuri ya kukusaidia. Yale mawazo uliyo ndani, yana uwezo wa kutoka nje na kuleta matokeo uyatakayo.
Kitu ambacho unapaswa kuchukua hatua ili uweze kuleta mabadiliko ya maisha yako ni kwa wewe kuanza kuwa na mawazo ya thamani ndani mwako.
Kila siku hakikisha unaingiza mawazo ya thamani na ya kukusaidia kufanikiwa na si mawazo yale mabovu ya kukurudisha nyuma.
Mawazo haya unaweza kuyapata kwa kujisomea vitabu vizuri au hata kwa kujifunza kupitia watu chanya wenye mafanikio makubwa kukuzidi.
Hauwezi kushindwa katika hili, ni swala la kuamua tu wewe mwenyewe. Ikiwa lakini utashindwa kutengeneza thamani ndani mwako, nakuhakikishia utashindwa.
Hakuna bahati mbaya inayotokea au hakuna maisha ambayo unayapata ni ya bahati mbaya, yote yanatokana na wewe mwenyewe.
Kama nilivyosema uchaguzi ni wako, kuendelea kuingiza mawazo mabovu ambayo yatakupoteza au kuwa na mawazo chanya ya kukujenga.
Kumbuka, mawazo yanayoumba maisha yetu, mawazo yanayotengeneza kufanikiwa au kushindwa ni yale mawazo ambayo tunakuwa nayo kwa muda mrefu ndani mwetu.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Jan 30, 2018

Vitu Vya Kufanyia Kazi Sana Katika Maisha Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Yapo mambo mengi sana ya kufanyia kazi katika safari ya mafanikio ili uweze kupiga hatua. Kwa bahati nzuri sana mambo hayo tumekuwa tukijifunza hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila siku, naamini hilo unalijua vyema.

Leo hii kupitia makala haya, tumekuandalia vitu vingine vya msingi vya kufanyia kazi sana katika safari yako ya maisha ya mafanikio. Soma kwa makini na kutendea kazi, na maisha yako utayabadili ikiwa utachukua hatua.

1. Njia ya mafanikio ni njia ambayo ina changamoto nyingi sana katikati yake. Pale tu unapoanza safari yako ya mafanikio kwa chochote kile unachotaka kukifanya elewa mbele yako kuna changamoto tayari zinakusubiri. Huwezi kukwepa changamoto.
2. Ikiwa utakosa nidhamu kwenye maisha yako, basi dunia itakuonyesha jinsi nidhamu inavyotakiwa iwe. Utapewa adhabu kulingana na kukosa kwako huko nidhamu. Matokeo yoyote utakayoyapata maishani kwa sababu ya kukosa nidhamu usilaumu.
3. Jiruhusu mwenyewe katika siku hii ya leo uishi kwa kutoa thamani yote uliyonayo. Usiishi nusu nusu kwa kuwaza mambo ya jana au juzi. Usiishi nusu nusu kwa kufikiria kwamba kesho itakuwaje, ishi leo kwa siku nzima kama ilivyo ili kupata matokeo bora.

4. Kila mafanikio ambayo umeyapata, ni matokeo ya kwamba kuna vitu ambavyo ulivifanya na vikakupa mafanikio hayo. Kwa kujua hilo, endelea kufanya vitu hivyo, endelea kuchukua hatua ili upate mafanikio mengine zaidi na zaidi tena.
5. Maisha yako yanaishia wapi au yatafika wapi, inategemea sana na vitu viwili ambavyo ni mtazamo na jinsi unavyochukulia mambo. Mtazamo wako na jinsi unavyochukulia mambo ndivyo vinavyoamua maisha yako yaweje.
6. Chochote unachokizingatia kwenye maisha, kitu hicho kinakua. Kama unasahau kuzingatia kile kinachokupa matokeo ya kubadili maisha yako, hiyo itakuwa ni kazi bure hata kama ungekua unatunza muda vizuri sana. Anza leo kuzingatia sana kile kinachobadili matokeo ya maisha yako na utafika mbali kimafanikio.
8. Miaka kumi ijayo kuanzia leo ikifika, haitajali ulivaa kwa sasa kiatu cha aina gani au ulivaa nguo za mtindo upi zilizotoka au ulitembelea sana maeneo yapi au uliangalia ‘movie’ ipi nzuri kwako. Miaka hiyo kumi ijayo itajali na itakuja na matokeo ya ulichowekeza leo, bila kujali uliwekeza kitu cha aina gani.
9. Usijaribu kuangalia nyuma kwenye maisha yako na kuchunguza yale maeneo kila wakati uliyokwama na kujiona huwezi kitu. Ni vyema kuangalia maeneo uliyofanya vizuri na kuedelea kujiboresha na hadi kuweza kufanikiwa zaidi ya hapo.
10. Moja ya tabia ambayo unatakiwa kuiendeleza ndani mwako na katika maisha yako kwa ujumla, ni kwa wewe kutokuruhusu, kuwahukumu watu wengine. Usiumize kichwa chako sana kuwahukumu watu wengine, utapotea. Waache waishi maisha yao. Kuwahukumu watu mara kwa mara inaweza hata ikakuletea msongo wa mawazo.
11. Kila mtu unayekutana naye kuna vitu vitatu ambavyo anavyo ndani yake;-
 Kuna kitu anachokipenda.
 Kuna kitu anachokiogopa.
 Kuna kitu ambacho amekipoteza.
12. Watu wengi katika maisha hawasikilizi ili kuelewa, bali wanasikiliza ili kukimbilia kujibu. Kuwa msikivu mzuri unapoongea na watu wengine, hiyo itakusaidia sana kudumisha mawasiliano yako na kwa bora kabisa.
13. Katika hii dunia, hakuna kitu ambacho kinaitwa ulinzi bali kuna fursa. Kama unafanya kazi na kutegemea sana ulinzi au ‘security’ kama wengi wanavyodai unajipoteza. Tafuta fursa za kukusaidia kufanikiwa na si kutafuta ulinzi.
14. Siri ya kuweza kusonga mbele kwa chochote kile unachokifanya ni kuanza. Usijidanganye sana kama unapiga hatua mbele kama hujaanza. Ni muhimu sana kuanza, kwani unapoanza unajenga ‘momentum’ ya kukusaidia kuweza kusonga mbele zaidi kila siku kuliko usingeanza kabisa.
15. Kupata utajiri ni zaidi ya mawazo na mipango uliyonayo. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na akili ya kitajiri/rich mindset na sio mawazo na mipango peke yake. Mawazo mazuri na mipingo mizuri haiwezi kukusaidia kama una ‘poor mind set.’
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Jan 29, 2018

Sahau Kabisa Hali Hii, Ili Utimize Ndoto Zako.

No comments :
Kila mtu anahitaji mafanikio ya aina fulani kwenye maisha yake, ikiwemo hata wewe unahitaji ufikie mafanikio ya aina fulani.
Pamoja na kwamba wengi wetu wana  kiu kubwa ya kuhitaji kufikia mafanikio ya aina fulani, lakini linapokuja swala la kufanya kazi hapo tena kuna shida.
Kuna wakati unapotakiwa kuweka kazi hasa ili uweze kufanikiwa, utajikuta mwili umechoka na hujisikii kufanya kazi kabisa na kuamua pengine  kutulia.
Hali kama hizo zinakuwa zinatokea sana, kwa hiyo utakuta mtu anajivuta sana katika utendaji wake kitu ambacho husababisha uzalishajji wake unakuwa mdogo.

Ili uweze kufanikiwa na kupata matokeo chanya ya kimafanikio ambayo utaridhika nayo, unahitaji kufanya kazi bila kujali hali yoyote inayotokea ndani mwako.
Unapokuwa na hali ya hisia ambayo unaona kabisa kwa jinsi ulivyo huwezi kufanya kazi, basi tambua hali hiyo inaweza ikakuzuia sana kufanikiwa kwako.
Maisha ya mafanikio hayaendeshwi kwa hisia za mwili wako hata siku moja, yanaendeshwa kwa zile hatua ambazo unazichukua kila siku.
Uwe unajisikia au hujisikii kufanya hicho unachokifanya, unatakiwa kukumbuka kwanza, kuchukua hatua hata kama ni kwa kidogo sana.
Watu wengi wanajiangusha kwenye maisha yao kwa sababu  ya kuongozwa na hisia kama hizi ambazo kila wakati zinasema nao kwamba usifanye saa hivi umechoka.
Unatakiwa uwe jasiri ili kuweza kuzishinda hisia zako ambazo zinaweza kukukwamishwa kwa namna yoyote ile na hapo utakuwa mshindi.
Usipofanya hivyo mwili wako utakuendesha sana na mwisho wa siku unajikuta unaanza kudondokea kwenye kundi la watu wavivu.
Kitu ambacho unachotakiwa kufanya kwa sasa, usikubali hata kidogo kuacha kuchukua hatua kwa sababu eti hujisikii kufanya kile unachokifanya.
Wewe unachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua, bila kujali unajisikia au hujisikii. Ukishachukua hatua basi, kama ni hamasa itakuja mbele kwa mbele.
Ukumbuke maisha ya mafanikio yanahitaji uvumilivu mwingi na hilo nalo unatakiwa kulivumulia, lakini usipofanya hivyo utashindwa.
Kumbuka, ndoto zako zitatimia tu, kama utachuka hatua na kutokujali hali hii ya hisia ambayo inatokea ndani mwako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








Jan 28, 2018

Unahitaji Sana Kuwa Na Jambo Hili, Ili Kupiga Hatua Endelevu Za Mafanikio.

No comments :
Kama kuna kitu fulani hukijui, kuwa na shukrani. Unatakiwa kuwa na shukrani kwa sababu, kwa kutokujua huko inakupa wewe sababu ya kujifunza.
Kama mambo yanakuwa magumu kwako sana, kuwa na shukrani pia. Ugumu huo utakusaidia kuwa jasiri na shujaa mkubwa kwenye maisha yako.
Kama umefika wakati umekimbia changamoto zako, kuwa na shukrani tena. Hapo ni wakati wa kutafuta wakati wa kuweza kujiboresha sana ili wakati mwingine usikimbie changamoto kama hizo.

Kama kuna wakati umechoka kwa kushindwa kendelea kwa sababu huoni mafanikio tena, pia kuwa na shukrani kwani huo ni wakati wa kuwa wa tofauti.
Kama kuna wakati umekosea sana si wakati wa kujuta kupitiliza, kuwa na shukrani kwani makosa hayo hutaweza kuyafanya tena.
Kama kuna wakati umekula hasara kwenye biashara yako, kuwa na shukrani. Kupata kwako hasara kutakusaidia sana kuongeza umakini mkubwa.
Ni rahisi sana kushukuru katika mambo mazuri, lakini si rahisi kuweza kushukutru katika yale mambo ambayo tunaona mabaya kwetu hata kama yana mafundisho tusiyoyaona.
Unatakiwa kuzingatia mabadiliko chanya kwenye kila unachokutana nacho, hata kama kitu hicho kinaonekana hakifai, elewa kuna fundisho la kujifunza.
Shukrani zako ni muhimu sana katika kuweza kubadili mtazamo ule wa kushindwa ulionao na kuleta mafanikio kwa yale utarajiayo.
Ni jukumu lako kuweza kujifunza na kukua kutokana na shukrani ulizonazo. Wewe utakuwa ni watofauti sana ikiwa maisha yako yakiwa amejaa shukrani.
Zipo fursa nyingi ambazo utaziona kupitia shukrani na hata ushirika na ikiwezekana misaada ya watu utapata kulingana na shukrani zako.
Waangalie watu ambao wana shukrani kwenye maisha na wale watu ambao hawana, utakuja kuona watu hawa maisha yao ni tofauti kabisa.
Maisha ya watu wenye shukrani utakuja kugundua yamejawa na utele wakati maisha ya watu ambao hayana shukrani yamajawa na utupu.
Kila siku ianzapo, kumbuka kuanza kumshukuru Mungu, shukuru upo kwenye siku ya kipekee ambayo unaenda kufanya mabadiliko makubwa.
Hiyo haitoshi shukuru pia juu ya kila unachokipata hata kama ni kidogo. Usipokuwa na shukrani hata hicho kidogo unaweza kukikosa.

Msingi wa maisha yako pia unatakiwa kujenga kwenye shukrani hapo pia utakuwa umefanya jambo la maana sana la kuweza kukusaidia.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





KIPAJI CHAKO; Wosia Wa Mafanikio Kutoka Kwa Mama, Sehemu Ya 02

No comments :
Ilipoishia wiki iliyopita
“Mama Ester mke wangu kwa kweli mimi hali yangu siku ya leo naona haipo sawa kabisa hivyo sidhani kama nitapona mke wangu ” sauti ile ya baba yenye kila aina zote  upole na ukarimu zilinifanya niamini ya kwamba baba alikuwa amezidiwa sana usiku ule.
Sasa endelea nayo………
Kwanini unasema hivyo Baba ester? Mama naye alihoji.
“Kwa kweli mke wangu hali yangu ni mbaya sana, najisikia joto sana harafu na kifua changu kinawaka moto hivyo nakuomba uchukue japo nguo unipepee mke wangu”

Pamoja hali ya baridi iliyokuwepo usiku ule, nilishangaa kwanini baba alikuwa anahisi joto?
Huku nikiwa nimesimamisha masikio yangu yalikuwa yamesimama dede kama mnala wa baberi kusikiliza kile kilichojili chumbani kwa wazazi wangu,
Kwa wakati huo waoga ndio uliokuwa umetawala akili mwangu……..
Nikiwa nikiendelea kusikiliza kile kilichokuwa kikijili chumbani kwa wazazi wangu, nilimsikia mama akinyanyuka na kwenda kufanya kile baba alichomuagiza, japo na yeye mama yangu alikuwa ni mjamzito si ujauzito tu, bali ulikuwa ni ujauzito wa miezi saba na nusu.
Wakati maongezi ya baba na mama yakiendelea chumbani, nami huku nilikuwa nasali kwa kasi zaidi ya 4G ili mwenyezi Mungu aweze kumponya baba yangu, kwani yeye ndiye aliyekuwa msaada mkubwa sana katika familia yetu na masomo yangu kwa ujumla.
Wakati nikiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kumsaidia baba yangu aweze kupona haraka, nilimsikia baba akisema;
“mke wangu naomba unisamehe sana!” mama alihoji kwa sauti ya chini
“nikusamehe kwa lipi tena mume wangu?
Naomba unisamehe kwa sababu enzi za uzima wangu sikutaka kabisa kukufundisha kufanya biashara yeyote, zaidi ya kukufundisha kulima, japo ilikuwa ni kwa asilimia chache sana  na kama unavyojua ya kwamba kwa hapa kijini kwetu kitu pekee ambacho hutufanya sisi kupeleka mkono kinywani ni kilimo pamoja na biashara ambayo nilikuwa naifanya mimi pekee yangu pasipo kukufundisha wewe.
Na siku ya leo kifo kinanikabiri na nikikutazama nagundua nakuacha katika mateso makali sana, kwani nakucha pasipo kukuachia ujuzi wowote ambao utakusaidia katika kufanya biashara, lakini pia nasononeka kwani najua familia yangu itaishi maisha magumu sana.
Lakini jambo la mwisho nawaza juu ya ujauzito ulionao kwani nafahamu fika mwanagu atakua bila kujua sura ya mimi baba yake......
Wakati baba anaendelea kusema maneno yale nilijawa na simanzi mayoni....... Niliwaza ndani ya nafsi yangu, ni kwanini baba alisema maneno yale? Wakati baba akiendelea kuzungumza na mama, nilimsikia baba sauti ikizidi kufifia huku akizidi kuongea kwa tabu.
Mmmmmke wangu, nananaku.......pe........nda sana, nakuomba nawe umpende mwaaaaanangu Ester pamoja na huyo Mmm____mmtoto wetu mwingine ambaye atazaliwa.
Mara baada ya baba kusema maneno hayo sikuisikia tena sauti ya baba zaidi ya kuisikia sauti ya mama, ikisema;
Baba Ester........ Bababa ester........
Mume wangu baba ester.......amka mume wangu...........
Baba Ester tafadhari nakuomba uamke mume wangu
Niliendelea kumsikia mama akimuita baba pasipo mafanikio. Wakati kule chumbani kwangu nikiwa katika hali ya ulutivu, nilimsikia mama akiniita kwa sauti ya juu,Ester mwanangu njooooo.
Sauti ile ya mama ilinifanya niogope, kwani ilikuwa si sauti ya kawaida ambayo mimi binafsi nilikuwa nimeizoea, nilikaa kimya kidogo pasipo kuitika, mama alirudia kunita tena kwa sauti nyingine.
Ester mwanagu njooo, baba ako anaku……..
Nilitoka mbio chumbani kwangu hadi chumbani kwa kina mama ambapo sauti ya mama ilinita huko. Nilifika mlangoni wa chumba cha wazazi wangu na kubisha hodi,,,,,,, hooo kabla sijamalizia kusema hodi, mama aliniamulu nipite.
Je ni nini ester alikikuta huko chumbani, usikose muendelezo wa hadithi hii nzuri ya kusimumua sehemu ya tatu siku ya jumamosi ijayo.
Mtunzi: Benson chonya
0757909942



Jan 27, 2018

Utengenezaji Wa Chakula Cha Kuku Kwa Kutumia Mchwa.

No comments :
Rafiki, mchwa na funza ni chakula bora sana kwa  kuku. Chakula hiki kina protini kwa wingi sana kwa mifugo yetu, ili kuku aweze kukua vizuri na kuwa na uzito mzuri anahitaji vyakula vyenye protein kwa wingi.

Wadudu jamii ya funza na mchwa ni jamii ya wadudu ambao wana protin nyingi, iwapo kuku wako utawapa chakula hiki basi kuku wako watakuwa kwa haraka na watakuwa na uzito mkubwa ambao itakua ni faida kwako.  

Pia chakula hiki cha mchwa na funza kinapunguza changamoto ya magonjwa kwa kiasi fulani hasa yale magonjwa yanayotokana na lishe. Mpaka hapo unaona faidaya wazi itokanayo na chakula hiki cha mchwa na funza.


 1. UTENGENEZAJI WA FUNZA.

Ili uweze kutengeneza funza unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo; Nailon, samadi, maji na jembe na eneo la kutengenezea.

Jinsi ya kutengeneza funza;

Tengeneza tuta.

Weka nailoni katika tuta lako.

Weka samadi yako (samadi mbichi ya Ng'ombe)

Weka udongo kwa mbali kwa juu katika samadi yako.

Mwagia mwagia maji, ninaposema mwagia mwagia maji namaanisha nyunyuzia maji katika tuta lako kwa kiasi kidogo.

Funika juu kwa nailoni katika eneo ambalo umetengeneza tuta lako hakikisha kusiwe na jua kali.

Katika tuta lako hakikisha kunakuwa na unyevu unyevu.

Baada ya siku kumi funua nailoni lako utakuta kunafunza wengi waache kuku wako wale hadi watakapomaliza.

Baada ya kumaliza kula funika tena na nailoni baada ya siku mbili utakuta tena kuna funza wakutosha hivyo unatakiwa utengeneze matuta mawili au zaidi kwa ajili ya chakula kwa mifugo yako, 


2. UTENGENEZAJI WA MCHWA.

Ili kutengeneza mchwa unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo;

Samadi ya ng'ombe, maranda ya mbao au majani makavu au mabua mahindi,
Mabox au chungu.

Jinsi ya kutengeneza mchwa.

Chukua samadi ya ng'ombe  changanya na maranda ya mbao vizuri mwagia maji michanganyiko wako ulowane vizuri.

Weka kwenye  chungu au box michanganyiko wako.

Chukua chungu/box lako weka katika njia ya mchwa kwa maana sehemu yenye asili ya mchuguu ambapo mchwa wanapatikana.

Baada ya siku tatu utaona box lako linamejaa mchwa chukua ka wape kuku wako wale.

Hapa ndipo mwisho wa somo letu la leo natumaini umejifunza mengi katika somo la leo nenda kayafanyie kazi haya uliyojifujifunza ili kuboresha mifugo yako.

MUHIMU;-  Chakula hiki kitumike kama  chakula cha ziada.

Nikutakie utekelezaji mwema na tutaonana wakati ujao, usipange kukosa mfululizo wa makala hizi.

NI MIMI RAFIKI YAKO,
FRANK MAPUNDA,
0758918243/0656918243.

Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.

Jan 26, 2018

Hata Kama Unaona Unashindwa Sana, Ipo Sehemu Hii Yenye Ushindi Wako.

No comments :
Pamoja na kwamba maisha yana changamoto nyingi sana, lakini kipo kitu cha kijifunza kupitia changamoto hizo hata kama zinakukatisha tamaa sana.
Pamoja na kwamba unaweza kudondoka au ukashindwa kwa namna fulani kwenye maisha yako, lakini upo uwezekano wa kuamka na ukawa mshindi tena.
Pamoja na kwamba unaweza ukapata hasara sana kwenye biashara au chochote kile ukifanyacho, lakini upo uwezekano wa kupata faida iliyo kubwa tena.
Pamoja na kwamba kuna kukakatishwa sana tamaa kwenye maisha yako, lakini tambua tumaini la kukuwezesha kusonga mbele kwenye mafanikio uyatakayo lipo.

Ushindi wa mafanikio yako upo, ukiamua.
Pamoja na kwamba umekuwa ukikosea na kufanya mambo mengi kwa njia ambayo si sahihi, lakini upo wakati ambao utaweza kufanya mambo yako kwa usahihi pia.
Unachopaswa kuelewa hapa ni kwamba, kwa sura yoyote ile ambayo maisha yanakujia, hata kama ni kwa sura mbaya, tambua ushindi upo.
Huhitaji kulia, huhitaji kulalamika sana kwamba maisha yako ni hovyo sana, upo upande wa pili ambako kuna ushindi wako pia.
Hata inapotokea hali unaona kama umekandamizwa na maisha, huwezi kunyanyuka, nikwambie tu uwezekano wa kunyanyuka tena upo, unatakiwa kulijua hilo akilini mwako.
Kitu kikubwa unachotakiwa kuelewa, kama upo kwenye upande wa kushindwa, unatakiwa kufanya jitihada za kuwa kwenye upande wa ushindi kimafanikio.
Maisha hayapo kwenye upande wa ubaya tu, maisha yana pande mbili, upande wa hasi na upande wa chanya ambao ni ushindi.
Kwa hiyo kila unapoona kama dunia inakuonea au unajiona kuna vitu umekosa kabisa, unatakiwa kukumbuka upo wakati utakuwa huru na hautaweza kuonewa.
Unatakiwa uondokane na fikra za kufikiri sana ubaya katika maisha yako, mambo yakija kinyume na ulivyotarajia, ujue ushindi pia upo.
Upo upande wa ushindi, upo upande ambao unatakiwa uufanyie kazi na uweze kushinda kwenye safari ya mafanikio.
Upande wa mafanikio upo, hilo unatakiwa kulijua kila wakati, nakukumbusha tena hutakiwi kukata tamaa au kujiona huwezi tena, mafanikio yako yapo.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Jan 25, 2018

Mbinu Itakayokufanya Ukue Kibiashara Ili Upate Faida Ni Hii...

No comments :
U hali gani mpenzi msomaji wa  mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima na unaendela vyema na majukumu yako ya kila siku, naomba nichukue wasaa huu  nikukaribishe siku ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja mbinu moja ya muhimu ambayo itakufanya ujiongee thamani na wateja kwa ujumla katika biashara unayofanya.

Nimekuletea mbinu hii  moja muhimu kwa sababu nimegundua  ya kwamba ni mbinu ambayo imekuwa ikiwasaidia wafanyabiashara wengi wakubwa kwa wadogo, ambao wamekuwa wakiiitumia mbinu hiyo.

Naomba pia niwe muwazi kwako kama endapo  mbinu hiyo haitukusaidia endapo utaamua katika biashara yako naomba tuwasiliane nipo  tayari kurudisha kiwango cha Mega bites(Mb) zako ambazo utatumia kusoma makala hii.


Pasipo kupoteza muda mbinu hiyo ni kutoa ofa kwa wateja wako au ‘promotion’ kama wengi wanavyopenda kuita.

Kanuni hii kwa mfanyabishara mdogo anaweza akasema labda kanuni hii hamhusu ila ukweli ni kwamba kanuni hii ni nzuri sana kwa mfanyabishara mdogo na mfanyabishara mkubwa pia, hii ni kwa sababu mbinu hii ina mashiko sana katika kuikuza biashara yako.

Hata ukifanya uchunguzi wako usio rasmi utagundua makampuni yaliyo mengi yana ushindani mkubwa katika jambo hili  la utoaji wa ofa, yaani wengi wao wamekuwa wakiishinda kuleta ofa mbalimbali mpya  zitakazowavutia wateja wa zamani na wateja wapya.

Na katika ofa hizo huendana na maneno mazuri yenye kuleta hamasa za kumvutia mteja, wapo ambao utawasikia wanasema ya kwamba jaza ujazwe, wapo wengine ambao husema onja msimumuko, wapo wengine husema jipimie, wapo wengine husema usipoelewa utarudishiwa ada yako na maneno mengine kama hayo.

Yupo mfanyabishara mwingine nimewahi kukumbana na bango dukani kwake lenye maneno yanasomeka hivi “ ofa ofa piga picha mbili kwa bei ya moja” mwisho wa kunukuu. Kwa maneno kama haya unadhani mteja hawezi kwenda kweli? Naomba majibu ya swali hilo uyaweke ‘password.’

Hivyo haijalishi ni biashara ndogo au kubwa ni vyema kuna wakati  uweze kutoa ofa kwa wateja wako na katika kutoa ofa hii ni lazima uzingatie ya kwamba ni lazima iwe ofa ambayo haitakuletea maumivu makubwa katika biashara yako, bali iwe ni ofa ambayo itakuongezea faida kwani siku zote ikumbukwe  utoaji wa ofa katika biashara huleta faida.

Mwisho nisikuchoshe kwa maneno mengi, kwani maneno mengi hayavunji mfupa bali nikwambie ya kwamba biashara ili iweze kwenda vizuri inahitaji pia ni ofa na ofa huleta faida na wateja kemkem. Hivyo walau kwa mwaka ukiweka ofa moja katika biashara yako basi itapendeza zaidi.

Ndimi: Benson chonya
0757909942

Jan 24, 2018

Hukuna Kinachoshindikana Kwenye Maisha Yako Ukiamua Hivi…

No comments :
Upo uwezekano mkubwa sana kwa kile unachokifanya pengine unakiona kama hakiwezekani na hauna nafasi tena ya kufanikiwa kwa hicho na hata kwa maisha yako kwa ujumla. Hali hiyo inaweza ikawa inakutokea sana na kujiona wewe si kitu.
Lakini kabla hujakata tamaa naomba nikwambie hivi, kwa vyovyote vile iwavyo mtu pekee ambaye ana uwezo wa kubadilisha maisha yako ni wewe mwenyewe. Kukata tamaa hakuwezi kukusaidia kwa namna yoyote ile zaidi ya wewe kuamua kuchukua hatua.
Maisha ya mafanikio ni matokeo ya kuthubutu sana kuchukua hatua hadi kuweza kufanikiwa kwako. Ikiwa lakini utakuwa unachukua hatua za kukata tamaa hutaweza kufika popote zaidi utaweza kukwama.
Ukiweza kuthubu kila siku na kila wakati hakuna maisha ambayo hutaweza kuyapata. Ngazi ya mafanikio fulani utaifikia tu kama wewe ni mchukuaji wa hatua na hakuna kinachoshindikana juu ya hilo hata siku moja.

Tatizo walilonalo watu wengi ni kule kukaa na kufikiri kwamba maisha yao ya leo jinsi yalivyo na ndivyo jinsi yatakavyokuwepo vivyo hivyo hata kwa miaka ijayo. Hicho unachokifikiri sio sahihi na kinakupoteza kabisa.
Leo unaweza ukawa na maisha mabaya sana, lakini kesho ukumbuke hayawezi kuwa hivyo kama unachukua hatua. Kila siku mpya inakuja na fursa zake, kwa nini ugande na fikra potofu kwa kukariri kwamba maisha yako ya leo ni sawa na ya kesho?
Hutakiwi kuwaza hivyo hata siku moja, chukua hatua za kubadilisha maisha yako, hata kama maisha yako unaona hayabadiliki mara moja, lakini elewa kuna wakati itafika maisha yako hayo yatabadilka hata kama yana hali ngumu sana.
Ndio maana nakwambia hakuna kinachoweza kushindikana kwenye maisha yako kama ukiamua kuchukua hatua za kuthubutu. Watu wote wenye mafanikio wanathubutu, kama itatokea huwezi kuthubu ni ngumu sana kuweza kufanikiwa.
Anza leo kufanya jambo ambalo umekuwa ukilitamani sana kulifanya. Huwezi kulifanya lote zima zima anza kulifanya kwa kidogo kidogo hata kwa mithili ya nukta lakini anza. Kwa kuanza kwako unakuwa ndio unathubutu na kubadilisha maisha yako.
Kile utakachokifanya leo hata kama ni kidogo sana lakini ina nafasi kubwa ya kuweza kubadilisha maisha yako na kuwa bora hata kama huoni matokeo ya ghafla yakitokea. Kikubwa thubutu na chukua hatua.
Unapaswa kuelewa kwamba hakuna kitakachoweza kushindikana kwenye maisha yako kama wewe hautaweza kuchukua hatua za kuthubutu na kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia. KILA KITU KINAWEZEKANA.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Jan 23, 2018

Fanya Jambo Hili Tu, Pale Unapoona Maisha Yako Hayaeleweki.

No comments :
Inapotokea pale unaona maisha yako yanakuwa magumu sana na unaona kama ulimwengu wote unakusaliti kitu pekee ambacho unatakiwa ukifanye kwa wakati huo jiweke bize, fanya kitu kitakacho kushughulisha sana kwa siku nzima.
Inapotokea tena  unaona huna kitu mfukoni mwako na unajiona wewe ndio maskini wa kutupwa, amua kujiweka bize kwa kwa kufanya kazi kwa bidii sana, tafuta kitu kitakachokupa changamoto na kukutoa hapo ulipo.
Inapotokea wewe unajiona ni mtu wa kuonewa na kutaka kulalamika sana, futa kwenye akili yako kuonewa huko. Kitu cha kufanya anza kujiweka bize kwa mambo yako na kuonewa huko ambako unafikiri hautakuona tena zaidi utaona amani tu kwako.

Inapotokea kwenye maisha yako umejawa na woga na hofu hadi kufika mahali huoni tumaini lolote mbele yako, tena kitu cha kufanya hapo ni kujishughulisha na kuwa bize zaidi kila wakati kwenye maisha yako.
Zipo nyakati nyingi ngumu ambazo zinakuwa zinatutokea kama hizi ambazo nyakati hizo hufungua milango ya kutaka kutufanya sisi tuyaone maisha yetu ni magumu na tumechelewa sana. Unatakiwa kujua inapotokea hali kama hii kumbuka kuwa bize.
Unapokuwa bize ni dawa pekee ambayo inakusaidia wewe kusahau kila kitu na mwisho wa siku unajikuta ndoto zako zimetimia mapema sana kuliko unavyoweza kufikiria hapo awali. Hivyo kujishughulisha ni kitu cha msingi sana kwako.
Pale unapokuwa bize na kufanya mambo yako, pia inakusaidia kuweza kuona fursa nyingine zaidi. Kwa tahadhari hapo,  kuwa bize kwa yale mambo ya msingi tu, usiwe bize kwa mambo ambayo hayawezi kukupa faida kwako.
Ukweli na uhalisia ambao naweza kukupa katika maisha ndio huo. Unajiwekea mikakati ya kushughulisha hata kama inatokea hali gani kwako, wewe jiweke bize hiyo ni dawa kubwa sana kwako ya kuweza kukufanya uweze kusonga mbele kwenye maisha yako.
Kuanzia sasa amua kujishughulisha sana kwenye mambo yako. Usikubali muda upite hivi. Kama utajishulisha kila wakati kwanza hiyo itakupa mafanikio, pia si hivyo tu inakusaidia kuweza kupata fursa na mafanikio mengine kwako.
Ndio maana tumekwambia pale unapoona maisha hayaeleweki, yamekuwa kama ya hovyo sana, ni jukumu lako kuwa bize ili usiweze kukaribisha msongo wa mawazo na mawazo yasiyo na maana kwako tena.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,