google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 31, 2016

Acha Kukata Tamaa, Mafanikio Yote Yanaanza Hivi…

No comments :
Kama upo kwenye safari ya mafanikio jifunze sana kutokuwa na dharau na kile kidogo ulichonacho. Kama una kitu ambacho ni kidogo iwe pesa au uwezo fulani au kitu chochote ambacho unaona ni kidogo kithamini sana kitu hicho.
Kitu nilichojifunza katika safari ya kutafuta mafanikio ni kwamba, mafanikio mara nyingi huweza kuanza kidogo kidogo sana mithili ya mbegu ya haladari. Kazi ya kukuza au kupapalia kile kidogo ulichopewa ili kiwe kikubwa sasa hapo ndiyo inakuwa  kazi yako.
Kwa mfano, kama ni pesa huwezi kuanza na kuwa na pesa nyingi mara moja, katika maisha yako unaweza ukaanza na pesa kidogo tu, lakini hizo pesa kidogo ukazifanya kama mbegu na kuwekeza huku na huko na baadae kuwa pesa nyingi.
Kama ni gari, nyumba, mtaji au maarifa fulani vyote hivyo huwa vinaanza kidogo kidogo na baadae kuwa vitu vikubwa vya kushangaza. Chochote ambacho unacho hata kama ni kidogo acha kukidharau hata kidogo zaidi kiheshimu.
Mafanikio yote makubwa, yanaanza kama mbegu.
Mafanikio yote makubwa yaliyopo duniani huwa yanaanza kwa kidogo sana. Hebu angalia miti mikubwa kama mibuyu ambayo inaishi zaidi ya miaka hata 500 nayo ilianza kama mchicha tena kukua kwake kukiwa kwa tabu.
Tambua Hakuna mafanikio ambayo yanaanza juu kabisa. Asili ya mafanikio yote makubwa yanaanza kwa kuanzia chini. Hizo ndizo hatua za mafanikio. Wakati wote mafanikio yapo kama hatua za mtoto mdogo ni lazima atambae kwanza kabla ya kutembea, na mafanikio yapo vivyo hivyo.
Kwa hiyo kwa kulijua hilo chochote ulichonacho hata kama ni kidogo vipi, mshukuru MUNGU kwa hicho na kisha kifanye kiwe mbegu kwako ya kukusaidia kufanikiwa. Acha kuwa na dharau na kidogo ulichonacho na kama ukiwa na dharau hutafika popote.
Kama una pesa kidogo zitunze. Kama unafanya kazi unayolipwa mshara mdogo iheshimu kwanza kazi hiyo, na halafu ile pesa kidogo unayoipata ifanye kuwa kama mbegu ya kukusaidia kufanikiwa katika maisha yako kwa kuiwekeza.
Hapo ulipo hata kidogo acha kuogopa kwa jinsi unavyoteseka na kusota kwa sababu ya kukosa pesa au maisha magumu, ninachotaka kukwambia huo ni mwazo tu wa mafanikio yako. Usikate tamaa endelea kupambana, Mungu yupo pamoja nawe.
Hakuna kitu ambacho hakibadiliki hata maisha yako yanakwenda kubadilika ikiwa hutakubali kushindwa na ukawa mtu wa kuchukua hatua. Siku zote kumbuka kuthamini kile kidogo ulichonacho.
Kama unakumbuka katika maandiko matakatifu wakati wana wa Israel wakiwa wamekosa tumaini na kuamini ni lazima wafie katika bahari ya shamu, lakini Mungu aliwaokoa kupitia fimbo aliyokuwa nayo mtumishi wake Mussa.
Hata wewe hapo ulipo kipo kitu  ambacho unacho hutakiwi kukidharau. Kama Mussa angeizarau fimbo yake na kusema kwamba isingeweza kufanya kitu basi wana wa Israel wangefia wote katika bahari ya shamu.
Kwa chochote ulichonacho, chukua hatua. Kiheshimu hicho ulichonacho na kifanyie kazi. Kama unaona unapata pesa kidogo sana, ziweke pesa hizo, acha kuzitumia hovyo na kusema haziwezi kunisaidia kitu.
Hivyo, ili kufanikiwa ni lazima utambue mafanikio yako huwa yanaanza kwa kidogo sana. Jukumu la kuyakuza na kuyafanya yawe makubwa lipo mikononi mwako. Kama ni mbegu ya mafanikio tayari unayo, acha kulaumu chochote zaidi, heshimu kidogo ulichonacho na utafanikiwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafikio.blogspot.com
Napenda pia kukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe. Hakuna gharama na karibu sana.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,

Oct 28, 2016

Jinsi Ya Kudumisha Afya Njema Na Kuishi Maisha Marefu.

No comments :
Katika hali ya kawaida, hakuna mtu ambaye ana uhakika mkubwa wa maisha yake kwamba ni lazima afike kesho. Muda na dakika yoyote ile unaweza kuachana na mwili wako na ukafa. Swala la kufika kesho au kutofika huwa mara nyingi linabaki mikononi mwa Mungu mwenyewe.
Pamoja na kwamba binadamu huyo hana uwezo wa kujua kesho yupo au hayupo, lakini upo uwezo wa kutambua kama binadamu huyo ataishi maisha marefu au mafupi. Inawezekana unaanza kujiuliza maswali hilo linawezekana vipi? Tulia usiwe na wasiwasi nitakwambia.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya wanadai kwamba, ikiwa binadamu ataishi maisha yake ya kawaida bila kupata  changamoto nyingine za nje yake kama kugongwa na gari au  namna yoyote ile ya kukatisha uhai wake upo uwezo wa kujua maisha yake yataishia wapi.

Vyakula vyenye mafuta sana ni hatari kwa afya yako.
Wataalamu hao wanatuonyesha viashiria ambavyo vinaonyesha kama ukiishi hivyo ni lazima uishi maisha marefu. Mambo hayo au viashiria hivyo walivyotoa, ni matokeo ya utafiti yaliyofanywa hasa kwa watu walioishi miaka 100 na kuendelea.
Kwa mfano utafiti huo ulionyesha, watu wanaokula vyakula vyenye mafuta kidogo, watu hawa wao waliishi maisha ya muda mrefu. Mara nyingi ni kweli unapokula vyakula vya mafuta kidogo hiyo inakusaidia sana katika swala zima la mwili wako kutopata magonjwa  hovyo.
Pia utafiti huo uliendelea na kuonyesha kwamba, watu wanaokula vyakula vyenye wingi wa protini pia afya zao ziliimarika zaidi na kupelekea kuwa na maisha marefu. Vyakula hivyo ni kama  samaki, dagaa, maharage, nyama ana vinginevyo.
Hata hivyo pia watu wanaofanya mazoezi kila siku nao pia walionyeshwa kwamba wanauwezo wa kuishi maisha ya muda mrefu kutokana na mazoezi huweza kuimarisha afya na kupunguza baadhi ya magonjwa na hali za kunenepeana hovyo.
Hivyo utaona, vyakula visivyo na mafuta sana, vyakula vyenye protini na kufanya mazoezi ni mambo ambayo yametajwa na wataalamu yanaweza kuboresha afya yako na kupelekea kuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuishi maisha marefu.
Kumbuka siku zote, afya ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako na safari yako ya mafanikio kwa ujumla. Kama ukiwa huna afya njema hakuna utakachokifanikisha kwenye hii dunia. Ni muhimu sana kutunza afya yako kwa ajili ya mafanikio yako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Pia napenda kukukaribisha rafiki kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com  

Oct 27, 2016

Namna Ya Kutambua Shughuli Iliyokuleta Duniani.

No comments :
Watu wengi huwa ni watu wa kujiuliza na kutaka kujua hasa ni shughuli ipi iliyowaleta duniani.  Mara nyingi wengi huwaza ‘ Sasa nitajuaje kwamba, kazi hii ndiyo ambayo imenileta au nimekuja kuifanya hapa duniani’? Ni kweli kila mtu duniani ameletwa au amekuja kwa ajili ya shughuli ama kazi maalumu kwake ambayo ni lazima aitimize ili kuweza kufanikiwa kwa viwango vya juu zaidi.
Tatizo kubwa linalooonekana kwa wengi wetu ni kutokujua hasa shughuli iliyotuleta hapa duniani. Kwa kutokujua huko hupelekea wengi kuvamia kazi ambazo sio zao na matokeo yake kushusha kiwango cha ufanisi. Kama unataka kufikia kiwango kikubwa cha mafanikio ni muhimu kujua shughuli iliyokuleta duniani. Swali la kujiuliza hapa utajuaje hasa shughuli iliyokuleta hapa duniani?
 1.Tambua ni kipi kimeikalia akili yako sana.
Hatua ya awali itakayokuwezesha kujua shughuli au kazi uifanyayo ndiyo hasa unayotakiwa kuifanya, ambayo ndiyo itakayokupa ridhiko la moyo na mafanikio, ni kuangalia kiwango chako cha kuipenda na kuridhika nayo. Lakini pengine pia ni kupima au kujiuliza juu ya shughuli au kazi ambayo inaingia akilini mwako mara kwa mara. 

Siyo kuingia akilini kwa kufikiria kipato, hapana, bali kuingia akilini ukitamani kuifanya. Wakati mwingine hata kuona kama vile wale wanoifanya shughuli hiyo inayoitawala sana akili yako wamependelewa au kupata bahati. Shughuli hii inayotawala akili yako kwa muda mrefu, mara nyingi  huwa ndiyo shughuli iliyokuleta duniani.


Watu wanaofanya shughuli zilizowaleta duniani huwa wana mafanikio mkubwa sana, hata kama shughuli hizo zinaonekana ni za watu duni, wasio na kipato wala heshima katika jamii, lakini huweza kustawi kimapato na kuweza kuishi kwa utulivu wa nafsi. Mtu anapofanya kile ambacho ndicho kilichomleta duniani, kufanikiwa kwake ni lazima.

2. Tambua ‘hobi’ yako ni ipi.
Kuna wakati shughuli zilizotuleta hapa duniani ni yale mambo ambayo sisi huwa tuyachukulia kirahisi na kuyafanya kwa urahisi kwa sababu ya kujifurahisha. Utafiti mwingi kuhusiana na malengo yetu maishani, unaonyesha kuwa, yale mambo tunayoyaita ‘hobi’ zinaweza zisiwe ‘hobi’ bali ndiyo shughuli zetu za kutupa mafanikio ya kweli maishani.

Kwa mfano unaweza ukaona mtu ana kipaji kikubwa sana cha kuchora na akawa anakitumia katika kujifurahisha tu, mwenyewe anaita ‘hobi’ wakati ukweli ni kwamba, angeamua kuingia kwenye uchoraji kama shughuli kamili, angefanikiwa sana. Wakati mwingine hata zile tunazoziona kama ‘hobi’ zisizo na maana sana, wengine ni shughuli maalumu kwao na kubwa.

Kama unayo shughuli au jambo ambalo unalipenda sana na unalifanya kama ‘hobi’, jaribu kulikagua. Inawezekana kabisa isiwe ‘hobi’ kama unavyofikiri bali ndilo limefanya ukaletwa hapa duniani. Kumbuka hakuna shughuli ndogo, ya kijinga au haina faida, bali inategemea wewe unayeifanya unaifanya kwa sababu gani?

3. Kama haina umuhimu wa nje.
Kama mtu anaipenda shughuli ambayo ni wazi haijulikani wala kufahamika kwa nje nap engine hata iikfahamika ni kwa kudharauliwa sana nab ado mtu huyo akajivunia kuifanya shughuli hiyo, hii ni dalili nzuri ya mtu kuwa kwenye shughuli iliyomleta hapa duniani.

Kuna watu ambao huficha shughuli zao, hawataki wengine wakajua wanafanya shughuli gani. Huficha kwa sababu wanahisi aibu kwa kuamini kwamba hizo shughuli zao ni zenye pengine kudhalilisha. Hawaoni kama wanastahili kuzifanya, kwani kwao hizo ni shughuli za watu wa aina Fulani wa kiwango cha chini.

Mtu anapogundua kuwa, anahisi aibu kutaja shughuli yake kwa sababu anadhani ni shughuli duni, ni vizuri akaacha kufanya shughuli hiyo, kwani anapoteza muda wake wa bure. Kudhani shughuli mtu aifanyayo ni dhalilisho, ni dalili kubwa ya kwamba mtu huyoanafanya shughuli ambayo hakutakiwa kuigusa maishani mwake.

4. Kutambua matatizo siyo hoja.
Kama kweli shughuli ambayo unaifanya ndiyo imekuleta hapa duniani,ndiyo shughuli ambayo unatakiwa kuifanya, haeiwezi kuwa na matatizo. Siyo kwamba ukifanya shughuli hiyo, huwezi au shughuli yenyewe haiwezi kukumbwa na vikwazo, hapana. Bali yanapotokea matatizo hutakata tamaa na kusema ‘basi’. Badala yake matatizo hayo yatakusukuma kusonga mbele na kukusaidia kujikita zaidi kwenye shughuli hiyo.

Bila shaka umeshawahi kuona au kusikia juu ya watu ambao shughuli fulani wazifanyazo zinakumbwa na matatizo, wengine wote wakajitoa, lakini wao wakabaki peke yao na kuendelea nazo, kama kwamba hayo matatizo ndiyo waliokuwa wanayasubiri. Biashara inakumbwa na matatizo ya aina fulani ambapo kuendelea kwake ni kwa kubahatisha sana na wengi wazifunga biashara zao, lakini mwingine anaendelea kama vile hakijatokea kitu. Kazini na mahali pengine hali kama hiyo huweza kujitokeza pia.

Kama kweli shughuli unayoifanya ni yako kabisa haiwezi kutokea hata mara moja ukaiacha kwa sababu ya matatizo. Hata kama utaiacha ni kwa muda tu, kwani utajikuta unatafuta njia au mbinu ya kupata ufumbuzi wa matatizo hayo. Matatizo hayawezi kukukatisha tamaa kama ambavyo yanaweza kumkatisha tamaa mtu ambaye anaifanya shughuli hiyo kwa sababu za nje, ikiwemo kipato. Huyu anayeifanya kwa sababu ya kipato, umaarufu au madaraka na sababu nyingine, ndiye ambaye tatizo likitokea ni mwepesi kughairi na kubadili shughuli.

5. Kuwa na ridhiko la ubunifu au ugunduzi.
Kama kweli shughuli unayoifanya ndiyo ambayo ‘umeandikiwa’ kuifanya, utajikuta mara nyingi unakuwa mtundu nayo na kuvumbua au kugundua mambo mapya. Hata kama mambo hayo mapya hayakupi faida inayogusika au ya moja kwa moja kama ya kipato, bado uvumbuzi au ugunduzi huo utakufanya kuridhika zaidi kuliko yule ambaye angepata pesa na kufurahia kuridhika tu kwa sababu ya pesa.

Wengi wanapobuni au kuvumbua vitu kwenye shughuli zao hukata tamaa, kuvunjwa moyo, kuvunjwa nguvu na pengine kubadilisha shughuli zao hasa wanapoona kwamba hakuna mtu aliyeonyesha kutambua ugunduzi wao na pengine kuwapa zawadi au fedha. Ukiwa hivyo jua kabisa unafanya shughuli ambayo siyo yako na ambayo haijakuleta duniani.

Kugundua na kuvumbua kinachozungumzwa hapa kunaweza kuonekana kuwahusu watu wachache, wasomi au wenye taaluma maalumu, hapana. Mtu yoyote, katika shughuli yoyote anaweza kugundua au kuvumbua jambo jipya na la manufaa kwa shughuli yake, kwake mwenyewe na kwa wengine pia.

6. Nguvu ya wito.
Kuna wakati huwa tunajiuliza ni kwa nini baadhi ya watu ambao wanauwezo mkubwa  wa kubadili shughuli, bado wanang’ang’ania shughuli ambazo zinaonekana kuwa hazina hata matumaini kidogo ya baadaye? Kwa hapa ilifika mahali Fulani ambapo ualimu ulionekana kama vile kuufanya ni kujitafutia umaskini na balaa kubwa kimaisha.

Lakini ni jambo linaloweza kuonekana kama la kushangaa kugundua kuwa, kuna baadhi ya watu ambao wangeweza kufanya shughuli nyingine na kufanikiwa sana kimapato, lakini wameamua kuwa walimu kwa furaha kubwa, wewe mwenyewe ni shahidi umeshawahi kukutana na watu wa namna hiyo.

Hapa ndipo ambapo tunasema, mtu anafanya shughuli fulani kwa sababu ya wito, siyo kwa sababu ya kitu kingine. Mtu anajua wazi kwamba, shughuli aifanyayo inadharauliwa nap engine haina maslahi ya fedha, lakini yeye anajisikia vizuri, anaona fahari na anafurahia kuifanya. Wito maana yake ni mtu kufanya kile ambacho ndicho alichotakiwa kuja kukifanya hapa duniani, ambacho kwa hali hiyo kimemkaa moyoni na akilini.

Kumbuka, hakuna aliyekuja hapa duniani kufanya tu shughuli ambayo haimhusu, kila mtu ameletwa na shughuli yake. Kaa chini tafakari na utafute shughuli iliyokuleta hapa duniani itakupa mafanikio makubwa sana.

Ni wako rafiki,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Oct 26, 2016

Kipindi Muhimu Sana Cha Mafanikio Yako.

No comments :
Njia mojawapo kubwa ya uhakika ambayo ukiitumia ni lazima itakupa mafanikio ni kusubiri. Hakuna kitu au mafanikio ambayo utashindwa kuyapata katika maisha yako ,ikiwa utakuwa ni mtu wa kufanya kazi na kusubiri.
Wataalamu mbalimbali wa mafanikio, akiwemo mwandishi wa vitabu wa kimarekani ndugu J.G Holland amewahi kuthibitisha hili pia kwa kusema“Hakuna mafanikio makubwa duniani ambayo utayapata bila kufanya kazi kwa bidii na kusubiri”.
Hiyo ikiwa inaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa sana kati ya kile unachokitaka na swala zima la uvumilivu wakati unasubiri kufanikisha jambo lako. Ni lazima ufanye kazi na usubiri mchakato wa kufanikisha jambo lako hilo.
Hakuna mafanikio  ambayo unaweza kuyapata ‘chapuchapu’ na kuamua kukwepa njia hii. Mchakato wa kusubiri na kuwa mvumulivu kwa kile unachokitaka, upo palepale. Watu wote wenye mafanikio wanapitia njia hii kufanikiwa na sio kinyume cha hapo.

Vumilia mpaka utimize ndoto zako.
Kwa kawaida ile tu kujua kusubiri kitu ambacho una mhemko nacho au mchecheto mkubwa kukipata ni siri au hatua kubwa sana ya kuweza kukusaidia kufanikiwa. Utulivu utakao utengeneza wakati unasubiri, ndio utakusaidia ukae sana na kitu hicho tofauti na ungekipata kwa upesi.
Elewa zipo namna nyingi za kusubiri kile unachokitaka kwenye maisha yako ili ukipate. Kwa mfano, kipo kipindi cha kusubiri wateja kuongezeka pale unapoanza biashara yako. Kipo kipindi cha kusubiri miezi tisa mtoto, pale mama anapopata ujauzito.  Kipo kipindi cha kusubiri kujibiwa majibu yako pale unapoomba kazi.
Kuwa na subira, ni kipindi muhimu sana cha mafanikio yako  na pia ni kanuni ya asili. Kanuni hii inaweza ikajitokeza katika yai. Kwa kawaida yai haliwezi kutoa kifaranga mpaka zifike siku 21.
Si hivyo pia tunaona kanuni hii inajitokeza pale unapoumia na kupata kidonda. Kwa mfano tunaona, ukipata kidonda huwa hakiponi mara moja, upo muda wa kusubiri hadi kidonda chako kipone. Na ndivyo kanuni hii inafanya kazi kwa misingi kama hiyo kwa mambo mbalimbali.
Kwa hiyo inapotokea umejiwekea malengo yako na kuanza kuyafanyia kazi, jifunze kuwa na subira. Acha kuwa na haraka zisizo na msingi kuharakisha matokeo. Kama kila wakati wewe ni mtu wa haraka haraka hutafika popote. Maisha yanakutaka sana uwe mvumilivu na mtulivu ili kufanikisha makubwa.
Kipo kipindi ambacho kinakulazimisha uwe na subira ili mambo yako yatimie. Hiki ni kipindi au muda ambao unakujenga na kukufanya uweze kufanikiwa. Hichi ndicho kipindi au wakati muhimu sana wa mafanikio yako. Ukishindwa kuvumilia hapa basi utaharibu kila kitu.
Hebu jaribu kufikiria ni wangapi ambao huwa hawana uvumilivu wa kusubiri mafanikio yao, bila shaka ni wengi tu. Huwa kuna ugumu kwa watu wengi kuvumila kile wanachokitaka, zaidi ya wengi hutafuta njia za mkato sana ambazo pia huwaangusha.
Kutokana na kukosa subira, wengi hutaka mipango yao iende upesi sana. kwa mfano, vijana wa miaka 22 wao hutamani kwa umri huo wawe wana gari, nyumba nzuri, mke mzuri, miradi ya kutosha na watoto. Haa! Haa! Haa! kama hizo ni ndoto zako umepotea.
Huwezi kufanikisha maisha yako kwa kwenda kinyume na kanuni za asili au kanuni za mafanikio. Maisha yanakutaka ufuate kanuni ndogo ndogo ambazo zitakusaida kupiga hatua kila siku. Mojawapo ya kanuni hizo ni kuwa na subira.
Kama huna subira ya kutosha unataka mambo kwa upesi sana huwezi kufanikiwa. Anza leo kwa kujenga msingi wa maisha yako kidogo kidogo. Anza leo kwa kuchapa kazi huku ukiwa na subira na ndoto zako. Kumbuka ile kusubiria ndoto yako itimie, ni kipindi muhimu sana cha mafanikio yako.
Endelea kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Pia napenda kuchukua fursa hii kukaribisha wewe rafiki yangu, kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza pamoja nami kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,






Oct 25, 2016

Sheria Ya Mafanikio; Nguvu Ya Umakini.

No comments :
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua, kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.

UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa pamoja. 

 Mwalimu mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa “Umakini ni kama mwanga wa jua, unauona ni wa kawaida lakini ukiweka lensi mbinuko unaukusanya mwanga ule na kuwasha moto.”


Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona tamaduni za Ki-Asia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo nguvu hiyo huamka.

Kile unachokizingatia sana, ndicho Unachokipata.
Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni pale unapoamua kujifunza kitu kama Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza kutengeneza. 

Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo. Sheria hii kiini chake kipo hivi.  POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani, utaona ufahamu huo unakua.

Buddha aliwahi kusema hivi,”Chochote unachokiwekea umakini ni lazima kikue
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana, halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri.


Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au ‘Nature’ imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya asili, na hata akili ni asili hivyo ipo mpaka kwenye fikra, mawazo au misimamo.

Mfano unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe ‘reality’ yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu kuwa kuna sheria kama hii duniani.

Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini. Je ni kweli ‘reality’ yako imetokana na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona hivyo au ni reality?

Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu. Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi, ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu.

Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe.

Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe. Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu unaohukumu hali na sio hali yenyewe. 


Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu unaumba ulimwengu wa nje.

Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine. Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO. 

Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona. 

Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa na akili. Kuna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza kuona dalili. 

MAKALA HII IMEANDIKWA NA APOLINARY MACHA WA JITAMBUE SASA.

Oct 24, 2016

Unachotakiwa Kufanya Pale Unapoiona Fursa.

No comments :
Siku kadhaa zilizopita nieleza namna ambavyo utaweza kuzitambua fursa mahali ambapo unapoishi, na siku ya leo nitaeleza kitu cha kuzingatia pale uonapo fursa.

Jifunze kupitia hadithi hii;

Ilikuwa ni majira ya asubuhi, ambapo hali ya hewa haikuwa shwari, mawingu mazito yaliyoambatana na radi pamoja na ngurumo ndizo ambazo zilikuwa zimetawala siku hiyo.

Wanyama wengi walishukuru sana kwani walidhani mvua kubwa ingenyesha siku hiyo kwani ni siku nyingi zilipita bila mvua kunyesha na kupelekea baadhi ya mazao yaliyokuwako shambani kuendelea kunyauka.

Hata hivyo cha ajabu pamoja na kuwako kwa hali hiyo yenye ishara ya kunyesha mvua kubwa itanyesha, lakini mvua haikuweza kunyesha. Kila Mnyama alisikitika sana kutokea kwa hali hiyo. Kadri siku zinavyozidi kwenda njaa kali ilitawala mahala pale hata kupelekea kwa idadi kubwa ya wanyama wengi kufa.

Chunguza kwa makini fursa mpya.
Kati ya wanyama walioathiriwa na hali hiyo ni fisi, kwani  ndiye alikuwa mnyama mwenye watoto ambao walikuwa ni bado wadogo hivyo hawakuwa na uwezo wa kujitafutia chakula hivyo ilimpasa fisi huyo kila wakati kwenda kutafuta chakula kwa ajili ya wanae.

Fisi huyo pamoja na kuwako kwa hali ngumu ambayo iliwatala mahali pale, kila alipojaribu kuwinda alikuwa anapata kitoweo kidogo sana ambacho kutokana na idadi kubwa ya watoto ambao alikuwa akiwamiliki kitoweo hicho kilikuwa hakiwatoshi watoto wake.

Kuna wakati zilipita siku tatu mvululizo bila ya kupata kitu chochote, hata kupelekea watoto wake kudhoofu sana. Kutokea kwa hali ile kulimchanganya sana mama fisi.

Siku moja mnamo usiku wa maneno watoto wa fisi kutokana na njaa ambayo walikuwa nayo waliweza kulalamika kwa mama yao ya kwamba njaa kali inawasumbua sana hivyo ingefaa kwa mama yao aende mawindoni angepata chochote ambacho kiwafaa kwa siku ile.

Pasipo kupoteza muda mama fisi alifanya kama ambavyo wanawe walimtaka afanye japo ilikuwa ni majira ya usiku. Mama fisi aliaamka na kuanza harakati za kutafuta chakula usiku ule, japo usiku ule haukuwa na giza kubwa kwa sababu kulikuwa na mbalamwezi ambayo ilimsaidia kumpa mwanga wakati wa mawindo yake.

Mama fisi alizunguka sana usiku ule pasipo kupata chochote. Lakini kadri alivyozidi kutembea kwa mbali aliona kama maji. Baada ya dakika chache kufika mahali pale cha ajabu alikutana na kisima ambacho kilikuwa kimejaa maji.


Mama fisi alimshukuru sana Mungu kwa kuyaona maji yale kwani alikuwa amebanwa sana na kiu pamoja na njaa isiyoelezeka. Hata hivyo wakati mama fisi akitaka kunywa maji yale aliona kitu ambacho kinaelea juu ya maji.

Mama fisi alijaribu kufanya uchunguzi juu ya kile kitu ambacho kilikuwa kinaelea, kadri alivyozidi kufanya uchunguzi aligundua kwamba ulikuwa ni mfupa. Mmmh si unajua tena fisi na mfupa.

Mama fisi pasipo kupoteza muda alijitupa ndani ya maji kwa ajili ya kuuchukua mfupa ule. Lakini pamoja na kufanya uchunguzi wake wa kina ukweli ni kwamba kilichokuwa kikielea juu ya maji haukuwa mfupa bali ilikuwa ni mbalamwezi.

Baada ya kuingia kwenye kisima kile mama fisi alishangaa kuona hakuna mfupa ambao aliuona wakati yupo nje ya maji. Na kwa kuwa kisima kilikuwa ni kirefu sana mama fisi hakuweza kutoka hivyo alikufa ndani ya kisima kile.

Watoto wa mama fisi walisubiri kwa siku kadhaa bila mafanikio ya mama yao kurudi, hivyo na wao waliliwa na wanyama wengine. Na historia ya mama fisi pamoja na wanawe ikaishia pale.

Tafsiri ya hadithi hii ni nini?

Ukweli ni kwamba watu wengi hulalamika katika mambo ambayo huwa wanayaanzisha, na mwishowe wanajikuta wanashindwa katika mambo hayo. Lakini moja ya tatizo kubwa ambalo hufanya kutokea kwa hali hiyo ni; 
Kutofanya uchunguzi wa fursa ambazo unazoziona, hili ndilo tatizo kubwa sana ambalo huwakumba watu wengi sana.

Unakuta mtu anaiona fursa fulani na fursa hiyo ana uhakika kwa kiwango kikubwa kuweza kibadili maisha yake kwa kiwango cha hali ya juu lakini cha ajabu unakuta mtu anashindwa sana katika fursa hiyo kwa sababu hakufanya uchunguzi wa kutosha juu ya fursa hiyo.

Huenda ukawa unataka kufanya jambo fulani la msingi sana katika maisha yako, lakini nikwambie jambo moja ya kwamba usikurupuke bali tafakari kwa kina kuhusu faida na changamoto ya jambo hilo.

Hivyo jambo la msingi ambalo ni vyema kulizingatia ili uweze kufanikiwa unahitaji kufanya uchunguzi wa kutosha kwa kila fursa ambayo unaiona. Kwani endapo hautafanya hivyo ipo siku utalalamika tu , pia utayaathiri maisha yako na watu wengine kama tulivyoona kwa fisi.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada, tukutane siku nyingine.

Pia napenda kukukaribisha rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.

Ndimi;afisa mipango Benson Chonya.

Oct 21, 2016

Usiruhusu Makosa Haya Yawe Sehemu Ya Maisha Yako.

No comments :
Yapo makosa ambayo hutakiwi kuyaruhusu mara kwa mara kutokea katika maisha yako. Ni muhimu kuzingatia hilo kwa sababu maisha tuliyonayo ni mafupi na kila hatua inatakiwa tuifanye kwa uhakika ili tusipoteze muda sana.
Kumbuka hata hivyo wengi wetu kuna wakati tunashindwa kufanikiwa sana kutokana na kuruhusu makosa ya aina fulani yatokee sana katika maisha yetu. Makosa haya ndio yamekuwa yakipelekea mipango mingine kuweza kukwama.
Je, ni makosa gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu katika maisha yako mara kwa mara ili uweze kufanikiwa?
1. Usiruhusu  kutawaliwa na watu hasi.
Hata kidogo usiruhusu kuweza kutawaliwa na watu hasi. Usiwape nafasi kubwa ya kuweza kuwasikiliza. Ikiwa utafanya hivyo kuwaruhusu watu hasi, watakuharibia maisha yako sana kwa kukupa ushauri wa kukatisha tamaa na mwisho utaona maisha hayawezekani tena.

Acha kuruhusu woga utawale maisha yako.
2. Usiruhusu woga ukutawale.
Woga ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Acha kuruhusu woga ukatawale sana. Kwa wale ambao huruhusu woga uwatawale kwa kiasi kikubwa hawafanikiwi. Hiyo hutokea hivyo kwa sababu hata hushindwa kuchukua hatua za kujaribu kufanya jambo jipya kwa sababu ya woga.
3. Usiruhusu kuiga sana.
Inapotokea ukawa unaiga sana kwa kawaida unaua ule ubunifu wako wa ndani. Hivyo kama unaiga kitu uwe na mipaka, lakini lilokubwa kwako unatakiwa kuwa mbunifu sana ili iweze kukusaidia kutengeneza mafanikio makubwa.
4. Usiruhusu kufanya jambo usiloweza.
Kama kuna kitu hukiwezi ni vyema usikifanye. Kukifanya kitu hicho huku ukiwa huwezi au huna hakuna na matokeo chanya hiyo itakuharibia sana sifa na maisha yako. Kila unapotaka kulifanya jambo fulani, hakikisha unalijua vizuri kwa undani ili likupe mafanikio.
Hivyo ni vyema ukatambua kwamba hayo ndiyo makosa ambayo hutakiwi  kutokuyaruhusu sana yatokee ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kama itatokea unaruhusu makosa hayo sana maishani mwako, basi utakuwa unajitengenezea mazingira ya kushindwa mwenyewe.
Nikutakie siku njema na ansante sana kwa kutembelea  DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Kitu cha kufanya kwako, washirikishe na wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


Oct 20, 2016

Mfumo Unaotengeneza Maisha Yako.

No comments :
Upo mfumo unaotengeneza maisha yako na kuyafanya yawe hivyo kama yalivyo. Hapo ulipo upo hivyo kimaisha si kwa bahati mbaya, mkosi au laana kama ambavyo unajifikiria kila wakati, bali upo hivyo ni kwa sababu ya mfumo.
Kwa  bahati mbaya au nzuri mfumo huu mara nyingi unautengeneza wewe iwe kwa kujua au kutokujua. Habari njema kubwa kwako ni kwamba, kwa vyovyote vile iwavyo, mfumo huo unao uwezo wa kuutawala hata kama umejitengenezea mfumo mbovu.
Mfumo huu ambao ninauzungumzia hapa na ambao unatengeneza maisha yako upo kwenye mawazo yako. Mawazo yako ni kila kitu ikiwa utajua namna ya kuyatawala na kuyatumia vizuri ili yakupe mafanikio.
Tatizo kubwa la sasa ni kwamba, ulimwengu umejazwa na watu wengi ambao hawajui jinsi ya  kutawala mawazo yao. Kwa sababu hiyo hujikuta ni watu wa kuishi tu kwa kupoteza muda bila ya kuwa na mafanikio makubwa.

Kila wakati fikiria kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Na kitendo cha kutokutawala mawazo yao kinasababishwa na watu wengi kushindwa kuelewa kile kinachoweza kutawala maisha yao. Nikiwa na maana ule mfumo ambao unaweza ukatawala maisha ya mtu.
Mfumo huu unaotengeneza maisha yako umefundishwa tokea miaka mingi sana na umefundishwa pia karibu  na dini zote. Kwa mfano tukisoma bibilia mithali 23;07 inatuambia “maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo…”
Andiko hilo linatuthibitishia na kutuonyesha kwamba mfumo unaoendesha maisha ya binadamu upo kwanza kwenye mawazo yake. Kipi unachokifikiri? Kipi unachoendelea kukiwaza kila wakati hicho ndicho kinaunda maisha yako.
Wanasaikolojia pia wanatufundisha kwamba kila mtu ana kitu anachokiwaza au kile anachokiweka akilini kwa muda mrefu.  Kitu hicho ambacho kinakuwa kipo akilini au picha ambazo unaziweka ndizo zinazo tengeneza maisha yako.
Ukichunguza utaelewa hicho kinachozungumzwa kipo na tunakiishi. Hiyo ikiwa na maana mfumo unaoendesha maisha ya mwanadamu upo kwenye kile anachokifikira kia wakati. Hakuna ubishi juu ya hili, ushahidi upo karibu kila kona.
Kwa mfano tunaona, watu maskini wanaendelea kuwa maskini zaidi kwa sababu ya mawazo au picha zile wanazoziweka kwenye akili zao. Kila wanachokiwaza au kikiona ni umaskini na mwisho wa siku huushia kuupata huo umaskini.
Pia watu matajiri wanaendelea kuwa matajii zaidi, lakini hiyo yote inatokana na kile wanachokiwaza kwa muda mrefu. Watu hawa kila wakati huwaza mafanikio, hivyo kwa sababu hiyo huvuta mafanikio na utajiri maishani mwao.
Kama kila wakati unaona umaskini, ni wazi utakuwa maskini. Kama kila wakati unawaza utajiri na kuweka picha za utajirii nalo hilo utalifanikisha bila shida yoyote. Mfumo unaotengeneza maisha yako yawe ya kushindwa au mafanikio haudanganyi, unakupa kile unachokizingatia akilini mwako.
Kwa kuwa mfumo huu upo, kila mmoja wetu anatakiwa kujua namna ya kujifunza kutumia na katawala mawazo yake kwa ufasaha ili yaweze kumpa mafanikio makubwa.
Lakini ikiwa endapo utaacha mawazo yako yakutawale, hutaweza kufanikiwa zaidi utabaki na utaendelea kuishi maisha ya kuwasindikiza wengine kwenye maisha na utashangaa huoni mafanikio yoyote yale.
Ili sasa uanze kuufaidi mfumo unaoutengeneza maisha yako na ukafikia mafanikio makubwa kama wengine, kila wakati unatakiwa kuwaza kile unachokitaka. Acha kuwaza na kinyume unachokitaka.
Jaza picha za kule unakokwenda. Jaza picha za kile unachotaka kukifanikisha. Jaza picha za kiwango cha pesa unachokitaka mwaka huu. Ukifanya hivyo kila wakati huku ukichukua hatua za utendaji UTAFANIKIWA.
Kwa kifupi hivyo, ndivyo ambavyo mfumo unaotengeneza maisha yako jinsi unavyofanya kazi. Kumbuka kila wakati hakuna bahati, muujiza wala mkosi katika maisha bali upo mfumo unaotengeneza maisha yako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kuchukua fursa hii kukukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,