google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 31, 2016

Hii Ndio Sababu Kubwa Ya Kushindwa Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Mafanikio makubwa huja kwa watu waliojiandaa. Kitu hicho ni baadhi ya watu wachache sana ambao hutambua. Watu wengi tunafikiri ya kuwa mafanikio tunayoyahitaji msingi wake mkubwa ni mtaji kwa maana ya kuwa na pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara au jambo lolote.

Kuwa na wazo hilo la kuwa na mtaji sio tatizo sana. Ila tatizo linakuja pale ambapo tunasahau ya kuwa kuna tatizo kubwa ambalo linafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto zao.

Jambo hilo ni WOGA BINAFSI hili ndilo tatizo kubwa ambalo watu wengi linawafanya washindwe kufikia ndoto Zao. Kuna usemi husema maisha ya mwanadamu yamethiriwa kwa kiasi kikubwa na woga.

Watu wengi wana woga wa uthubutu katika jambo fulani, mfano mtu leo hii anawaza katika akili yake kwamba hawezi kufanya jambo fulani. Akili yake ndivyo inavyowaza hii ni kutokana na woga alio nao katika nafsi yake.

Woga binafsi mara nyingine hujenga na jamii ya watu ambao wanakuzunguka. Mfano leo hii unataka kuanzisha biashara fulani kuna baadhi ya watu watakwambia hautaweza na wewe unaamini kweli hautaweza, hii ni kutokana umeshajenga woga binafsi kwa kuwa mtu fulani alikwambia hautaweza kufanya jambo fulani.

PUNGUZA WOGA ILI KUFANIKIWA.
Wapo pia baadhi ya wazazi mara nyingi huwajengea picha mbaya watoto zao na watoto hao kuamini kuwa hawewezi. Mfano mtoto wako kila wakati anafeli katika masomo yake, badala ya mzazi kumuonesha njia za kuweza kufaulu ila wewe unamkatisha tamaa. Mwisho wa siku mtoto huyo anajenga woga binafsi, na kuamini yeye hawezi.

Ndugu Msomaji wa makala hii, inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa, hii ni kwa sababu kuna maneno ambayo uliambiwa na wazazi au ndugu wengine wanakuzunguka na leo hii bado unayakumbuka, mfano inawezekana uliambiwa wewe kichwa chako sio cha biashara na wewe ukayaamini maneno hayo.

Hivyo wakakwambia ujikite zaidi katika elimu yaani usome kwa bidii ili  uje kuwa mtu fulani hapo baadae.

Kwa kuwa uliamini kuwa huwezi kufanya biashara na ukajikita katika zaidi katika elimu. Umemaliza chuo, ajira hakuna kwa kuwa ulishaambiwa huna kichwa cha biashara leo hii unaona maisha yazidi kuwa magumu na huna njia nyingine za kujiongeza ili uweze kufanikiwa.

Huwa ni ukweli usiofichika wala hauhitaji mifano kutoka ulaya watu wengi tunashindwa kufanikiwa hii ni kutokana na woga binafsi tulionao. Wito wangu kwako ni kwamba ili uweze kufanikiwa unahitaji kujiamini, tumia akili, nguvu na kuwa na mawazo bora ya kufikiri yatakayokufanya wewe kutoka katika hali uliyonayo kusonga mbele kuyasaka Mafanikio. Naomba kwa Leo niishie hapo.

Usisite kumshirikisha mwenzako naye ajifunze kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.

Imeandikwa; Benson chonya


dirayamafanikio@gmail.com

Mar 30, 2016

Chanzo Kikubwa Kinachokufanya Usitimize Ndoto Zako.

No comments :
Kuna baadhi ya watu wanazitambua njaa zao  na wengine hawazitambui njaa zao za mafanikio. Njaa hizo za mafanikio  zinatofautiana baana ya mtu mmoja na mwingine. Nimesema ni baadhi ya watu wachache ndio watu ambao wanajishughulisha usiku na mchana ili kuangalia ni mbinu zipi wanaweza kuzitumia ili waweze kufanikiwa.  Lakini watu hao wenye njaa ya mafanikio, mambo yao wakati wa kuyasaka mafanikio huwa ni mateso ya hapa na pale.
Watu hawa huzunguka huku na huko ili kupata maisha bora. Watu hawa naweza nikawaona ni watu ambao huwa wana sura za huzuni zaidi ila furaha huchukua kwa kiwango kidogo sana katika maisha yao. Wapo baadhi ya watu kutokana na njaa walinazo kila kazi yeyote yupo tayari kuifanya. Ila tatizo linakuja ni kwamba pindi apato fursa ya kufanya kazi wengi wao wanapweteka na kutoonesha njaa walizokuwa nazo mwanzo pindi wapatapo nafasi ya kufanya kazi. Hivyo katika makala ya leo nataka nikushirikishe kwa nini watu hao huwa hivyo.
Hii ndio sababu kubwa kwa nini watu wengi hawatumii nafasi walizozipata kwa asilimia mia moja;
Kuridhika na walichonacho.
Tafiti zinaonesha ya kwamba asilimia kubwa ya watu wakipata kile walichokuwa wanakihitaji hawakifanyi kwa asilimi mia moja. Hii ni kutokana mtu anaona kitu hicho ameshakipata hivyo hana haja tena na kuanza kuendelea kuongeza juhudi na ubunifu katika kitu au jambo fulani. Kimsingi ni kwamba binadamu ni watu wa kulalamika sana nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba leo hii ukikutana na mtu ambaye hana ajira au hafanyi biashara ni mtu wa kulalamika sana, na asilimia kubwa la kundi hili wengi wao husema nikija kupata kazi au nikija kufanya biashara nitafanya vizuri ili kutumiza ndoto zangu. Ila tazizo maneno hayo hugeuka dakika chache akilipata jambo hilo hafanyi kama alivyoahidi mwanzoni wakati wa akilitafuta jambo hilo.

USIRIDHIKE SANA NA KILE UNACHOKIFANYA.
Mfano leo hii tunaona baadhi ya wasanii wa nyimbo wanapotea katika sanaa,  hii mara tu baada ya kutoa wimbo mmoja ambao utapendwa na watu wengi.  Tatizo kubwa wengi wao huwa wanaridhika na mapokeo ya wimbo huo na kupweteka na kujiona tayari wameshafanikiwa  na mwisho wa siku hatuwasikii tena. Tatizo lao kubwa ni kuridhika na walichokipata mwanzo. Pia wengi wanasahau kujipanga upya na kuja kufanya vizuri katika kazi zake zote zinanazokuja.
Tupo baadhi ya wafanyabahara huwa tunaridhika na kuona kile tunachokipata kama ni faida kubwa. Jambo la msingi na la kuzingatia ni kwamba hicho ulichonanacho usiridhike nacho  na kujiona wewe ni mkamilifu na kinatosha, la hasha bali jione una mapungufu kwa kuzitambua njia mbalimbali za kuweza kuongeza thamani katika biashara na kazi zingine unazofanya.
Tukumbuke ya kwamba ili kuyaona mafanikio katika kila shughuli ambazo tunazifanya ni kwamba tujione ya kwamba vitu hivyo vinatudai kwa maana ya kwamba tusiridhike na kuona vinatosha hapo vilipo. Leo hii mtu aliyegundua ndege haridhiki na ndege amabayo ameigundua bali anafikiria kitu kingine ambacho atakiongeza katika ndege ili kuongeza ubora au anafikiria kitu kingine zaidi ya ndege.
Kama ndivyo hivyo hata wewe katika jambo lolote ambalo unalifanya lazima ufikirie hivyo.  Usiridhike na ulichonacho bali fikiria ni nini unakihitaji zaidi ili kuongeza thamani katika jambo ambalo unalifanya. Kuwa mtu ambaye ni mbunifu ambaye utatofautiana na wengine.  Endapo utayafanya hayo kwa njia tofauti na zile ambazo umezizoea utakuwa tofauti sana na watu wengine na ndoto zako zitazidi kung’ara mara dufu.
Daima tukumbuke ya kwamba wewe ndiye mmiliki wa mafanikio yako, hivyo una uwezo mkubwa wa kuyafanya mafanikio hayo yakuwe au yafe. Kitu cha msingi ili kukuza biashara  au jambo lolote  ni kuamua tu na kuvifanya mambo kwa njia na tofauti ulizozioa .
Makala imeandikwa na; Benson chonya
Simu; 0757-909942


Mar 29, 2016

Fursa Za Biashara Na Miradi Ambazo Unaweza Kuzifanya Kulingana Na Mtaji Ulionao.

No comments :
Mara nyingi kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO  tumekuwa tukikushirikisha mbinu mbalimbali pamoja na fursa ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa. Lakini pamoja na mbinu hizo ambazo waandishi wetu wamekuwa wakizitoa bado tumekuwa tukipokea simu nyingi zinazouliza ‘Nifanye nini au nifanye biashara gani’.
Kwa kujua umuhimu wa hilo, leo katika makala yetu ya leo, DIRA YA MAFANIKIO itakushirikisha aina tofauti tofauti ya miradi ambayo unaweza kuifanya kulingana na eneo ulipo hasa kwa kuangalia urahisi wa utekelezaji unaona kwako unafaa. Kwa kupitia makala haya, tunaamini utakuwa umejifunza kitu na itakusaidia kukupa mwongozo wa kujua ni nini cha kufanya kitakachokupa mafanikio makubwa.
Bila kukupotezea muda, twende pamoja kujifunza aina mbalimbali ya miradi ambayo unaweza kuifanya kulingana na eneo ulipo.   
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya elektroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob,
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.

Fursa Za Biashara Na Miradi Ambazo Unaweza Kuzifanya Kulingana Na Mtaji Ulionao.
UFUGAJI WA NYUKI KWA KISASA.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51.Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo.
Chukua hatua na PIGA KAZI mpaka ufikie mafanikio makubwa lakini kama yote haya umeshindwa kupata la kufanya wewe utakuwa ushapotea, endelea na utaratibu wako wa kuilaumu serikali.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio mkubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Kwa maswali au ushauri unaweza kuwasilina nasi kwa dirayamafanikio@gmail.com au simu kwenda 0713 0480 35, karibu sana.


Mar 28, 2016

Mambo Mawili (2) Yanayotukwamisha Kufikia Malengo Yetu.

No comments :
Yapo mambo mengi ambayo umekuwa ukiyaona au kuyasikia ambayo yanakufanya usonge mbele au kurudi nyuma katika safari yako mafanikio.  Jambo la msingi ni jinsi gani ambavyo unachukulia mambo hayo  katika kuoziona fursa katika eneo lako unaloishi. Lakini  katika makala ya leo tunakwenda kujikita zaidi kwa kuangalia mambo ambayo yanatufanya tuzidi kuwa wanyonge na kuona mafanikio ni ya watu wachache.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayotukwamisha kufika malengo.
JAMBO LA KWANZA.
Kusemwa na  watu juu ya jambo lako. Tunashindwa kufika malengo makubwa kwa sababu , sisi wenyewe ni kikwazo katika baadhi ya mambo  ambayo hayana msaada wowote wa kimafanikio kwa watu wengine.  Wapo baadhi ya watu wapo  kwa ajili ya kuona watu  wengine hawasogei mbele kimafanikio .  Wao wamekuwa na maneno ya kuwakatisha watu wengine tamaa kwa kuwaambia wahusika maneno ambayo hayawajengi bali yanawarudisha nyuma. Mfano leo hii anamwambia mtu unataka kufanya biashara fulani, mtu huyo atakwambia hataweza kufanya jambo hilo kwa kuwa hufanani na kitu hicho unachotaka kufanya.
Wapo baadhi ya watu ukiwashirikisha mambo yako wao huchukua hatua ya kuwashirikisha watu wengine na kuwambia  fulani anataka kufunya jambo fulani. Lakini jambo la msingi la kuzingatia ili kuona unapata faida katika jambo lako unalofanya hakikisha maneno ya watu wanayokusema yanakupa hamasa za kiutendaji na kuongeza juhudi ili kupata faida kubwa.

JIAMINI KWA KILE UNACHOKIFANYA.
Mfano wewe ni mfanyabiashara watu wanakusema wewe unafanya biashara kwa njia za ushirikina au maneno mengine yanayofanana na hayo achana na maneno hayo bali songa mbele kwa kuziona fursa za jambo lolote ili kupata faida kubwa. Watu wanapozidi kukusema wewe unazidi kufanikiwa zaidi.
JAMBO LA PILI
Kusubiri kuambiwa ufanye jambo fulani. Hili ni jambo linalotukwamisha sana katika safari ya mafanikio. Watu wengine tunapenda kufanya mambo ya kimafanikio kwa kuambiwa na mtu mwingine. Wengi tunasubiri kuambiwa fanya hiki au fanya kile. Katika safari ya mafanikio  ukisubiri kuwaambiwa na mtu fanya hiki au fanya kile kwa upande wako mafanikio yatakuwa ni ndoto tu.
Mfano wewe ni mwanafunzi unasubiri mwalimu wako mpaka akuambie kasome kitu fulani au wewe ni mfanyabiashara unasubiri mtu akwambie boresha ofisi yako ili kuongeza wateja  ila wewe kwa akili yako hata siku moja hujawahi kujipa kazi za kufanya au kujiuliza ufanye nini ili kuboresha biashara. Kimsingi kufanya hivi ni sawa na kumfunika nyoka kwenye tenga ili asitoke.
Ewe msomaji wa makala haya ili kuona unafanikiwa kwa kiwango kikubwa hakikisha kwa kila jambo unalolifanya usisibiri mtu  fulani akwambie ufanye bali kuwa na akili ya kujiongeza. Kufanya hivi kutakufanya kuongeza ufanisi wa kiutendaji na kupata kile unachokihitaji.
Ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza zaidi.
Makala hii imeandikwa na afisa mipango na maendeleo; Benson chonya
Simu; 0757-909942

Email ; Bensonchonya23@gmail.com

Mar 25, 2016

Hizi Ndizo Fikra Chanya Za Kukusaidia Kufanikiwa.

No comments :
Mafanikio siku zote mbali na kufanya kazi kwa bidii yanahitaji uwe na fikra au imani chanya ili uweze kufanikiwa. Kwa kuendelea kuwa na fikra au imani sahihi inakupelekea kufikia mafanikio makubwa. Baadhi ya imani unazotakiwa kuwa nazo ili kujijengea mafanikio ni kama hizi zifuatazo:-
1. Amini kwamba pamoja na kushindwa kwako sana lakini una uwezo mkubwa wa kufanikiwa lakini ikiwa utajaribu tena na tena kile unachokitaka kwenye maisha yako.
2. Amini kwamba unatakiwa kufanya mambo yako kwa utofauti kama unataka kufika hatua fulani kimaisha. Acha kuishi kimazoea sana utakwama.
3. Amini ndani yako unao uwezo wa kufanya kitu chochote cha kukupa mafanikio ikiwa lakini utaamua iwe hivyo. Ukichukua hatua hali yoyote utaibadilisha.
4. Amini kufanya kazi kwa bidii ni njia pekee ya kukutoa kwenye umaskini. Kama unafikri natania angalia watu wengi ambao wanafanya kazi sana lakini huku wakikubali kujifunza. Maisha yao ni ya mafanikio makubwa.
5. Amini muda ulionao ndio unaouwezo wa kukufanya ukawa maskini au tajiri. Itatokea hivyo kwako kwa kupanga matumizi mazuri ya muda wako.

KUWA NA MAWAZO CHANYA.
6. Amini kuwa mbali na watu hasi ni njia mojawapo ya kukusaidia kufikia malengo yako.
7. Amini kwamba wewe ndiye unayeyajibika kwa maisha yako. Kwa vyovyote vile maisha yako yalivyo wewe ndiyo chanzo kikubwa cha kwanza hakuna wa kumlaumu.
8. Amini kuwa mshindani mkubwa wa kwanza wa maisha yako ni wewe. Unatakiwa kuwa bora kuliko jana kila siku.
9. Amini una uwezo mkubwa wa kujifunza kitu chochote na ukaweza. Unaweza kujifunza mafanikio, biashara au chochote kile unachokitaka.
10. Amini una uhuru wa kuchagua maisha yako yawe vipi. Kama unataka maisha yako yawe ya mafanikio makubwa huo ni uchaguzi wako au kama unataka maisha yako yawe ya kawaida pia huo ni uamuzi wako.
Ansante kwa kujifunza na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,

Simu; 0713 04 80 35,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

Mar 24, 2016

Vipindi Muhimu Anavyopitia Mwanadamu Katika Maisha.

No comments :
Katalamu binadamu katika safari ya ukuaji hupitia vipindi mbalimabali. Katika vipindi hivyo binadamu kwa muda mwingine huwa na furaha,huzuni,wasiwasi na hofu pia. Pia ni hivi ndivyo vipindi ambavyo humsaidia kujifunza mambo mabalimbali ikiwa pamoja na tabia na mafanikio.
Hebu twende pamoja kujua na kujifunza Vipindi hivyo ni;
Umri wa mwaka (0-18).
Katika kipindi hiki binadamu huwa mtoto na anayependwa sana na wazazi wake, katika kipindi hiki mwanadamu anakua katika kipindi cha  kufundishwa vitu kutoka kwa watu mbalimbali. Mfano mtoto mdogo katika hali kwa kila anachokifanya kwake huona ni sawa eidha ni jema au baya.
Mzazi huchukua jukumu la kemkekemea kama anafanya jambo baya na humpongeza pale anapofanya vizuri. Mfano mtoto  hupongezwa  kumsaidia mzazi kufanya kazi, kuwaheshimu watu wote, kufaulu katika masomo yake na mengineyo mengi. Kiujumla katika kipindi hiki binadamu huwa ni tegemezi kwa jamii inayomzunguka.
Kipindi cha umri kati miaka (19-35).
Katika kipindi hiki binadamu huanza kujitambua yeye ni nani.Vilevile katika kipindi hiki ni kipindi ambacho binadamu anaanza kupanga mipango mingi. Mfano katika kipindi hiki mtu huanza kupanga mambo mbalimbali nataka katika maisha yangu kitu cha kwanza kuwa nacho ni gari, mwingine utamsikia mimi nataka nianze kuwa na nyumba, wengine utasikia nataka kuolewa na mtu mwenye pesa, wapo wengine utawasika nataka kuoa mwanamke mzuri na mipango mingine mingi.
Katika kipindi hiki utawasikia  wanasema ndio kipindi cha kula ujana wakiwa na maana ya kwamba ni kipindi cha kwenda kumbi mbalimbali za burudani, pia ni kipindi cha kupendeza, pia ni kipindi cha vijana wengi kujiingiza katika kuiga mikumbo kutoka kwa watu mbalimbali hatimaye kujiingiza kwenye wizi,kuvuta bangi,umalaya na mengineyo mengi. Utawasikia wengine wanakiita kipindi cha tumia pesa ukuzoee.

VIPINDI VYOTE NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA.
Dah yaani ni kipindi hiki kina mambo mengi sana. Katika kipindi hiki tupo baadhi ya watu huwa bado wapo katika kipindi cha utegemezi. Mfano mzuri ni wanafunzi wanasoma elimu za juu yaani vyuo wao huamini ya kwamba hawawezi wenyewe kusimama na kujitengeneze njia sahihi ya kujipatia kipato.Pia wanafunzi hawa kwa walio wengi huwa wanafikiri maisha baada ya elimu zao ni kuajiriwa.
Lakini ndugu msomaji wa makala hii lazima ufikiri zaidi kuajiriwa peke yake ili uweze kuona mafanikio makubwa ndani yako. kitu kikubwa ni kuwa mbunifu.Wito wangu kwako ni kwamba endapo utatumia vizuri kipindi hiki ukiwa na mtazamo chanya utapata mafanikio makubwa sana.
Umri kati miaka (36-45).
Ni aina nyingine ya vipindi ambayo hupitia mwanadamu. katika kipindi hiki ni kipindi cha utekelezaji wa   yale uliyoyapanga katika kipindi ulichopita yaani cha miaka( 19-35). Katika kipindi hiki  ni kipindi ambacho kina majukumu mengi ambayo yanamfanya mtu akose hata usingizi. Katika kipindi hiki mtu huwa na majukumu mengi sana kwa mfano kujenga, kusomesha watoto,huenda ukawa tegemeo katika familia yako.
Kwa kuwa katika kipindi hiki kina mambo mengi ya utekelezaji ni vema kile unachokipanga katika kipindi cha mipango yaani miaka (19-35) na utekelezaji uanza katika kipindi hicho. Nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba katika kipindi hiki  cha miaka 36-45 watu wengi hujikuta wana mipango mingi lakini ugumu unakuja katika utekelezaji.
Umri kati ya miaka 46-na kuendelea
Hiki ni kipindi cha uzee ambacho mara nyingi huiitwa ni kipindi cha masahihisho. Katika kipindi hiki baadhi ya watu hupungua uwezo wa kufikiri hatimaye kuwa kama watoto. Pia Watu wengi hapa hupatwa na magonjwa mbalimbali kama pressure,figo kufeli, kisukari na mengineyo. Katika kipindi hiki watu hustaafu kazi zao. Katika kipindi hichi watu wengi hupatwa na pressure kutokana na walishindwa kupanga na kutekeleza mambo yao katika vipindi vya umri kati (19-35).
Mfano mtu alikuwa ni mfanyakazi wa serikali na hajawahi kujenga nyumba yake ya kuishi wala  hana usafiri vyote alivyokuwa anatumia vilikuwa ni mali za ofisi. Inafika wakati wa kustafu anapata mafao yake ndo pale anaanza kupanga mipango yake na kujikuta hela aliyopewa katika kiunua mgongo imeisha kwa sababu mtu huyu anakuwa ana mipango mingi katika kipindi cha uzee matokeo  haelewi aanze na kipi katika utekelezaji. Je, aanze na kununua gari? Je aanze na kufungua biashara? Je aanze na kujenga nyumba? Matokeo yako mipango inakuwa mingi kuliko utekelezaji hatimaye anapata pressure.
Wito wangu kwako kumbuka siku zote  kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua. Katika safari ya mafanikio kila linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe kijana tambua ya kwamba muda wa kupanga na kutekeleza mambo yako ni sasa achana na usemi eti kijana ni taifa la kesho kwa kuwa  ukiushika usemi  huo utakuwa unachelewa katika  safari yako mafanikio.
DIRA YA MAFANIKIO inakutakia kila jema katika safari yako ya mafanikio. Pia endelea kutembelea  ukurasa huu kila siku ili ujifunze zaidi kuhusu mbinu mbalimbali za mafanikio.
Imeandaliwa na;
Afisa mipango na maendeleo:Benson .O. Chonya,
Mawasiliano;
Simu;0757-909942/0652-015024
E-mail;bensonchonya23@gmail.com

Mar 23, 2016

Siri 15 Za Kukabiliana Na Changamoto Za Soko Katika Biashara.

No comments :
Watu wengi wanafanya biashara, kulima au kuzalisha mali kwa lengo la kutafuta pesa na maisha mazuri. Lakini je, mteja wetu tunaemzalishia ni nani? Na kile tunachokizalisha kinatupa soko la uhakika? Mara nyingi soko ni tatizo kubwa sana kwa wazalishaji iwe wadogo au wakubwa. Na hili ndilo tatizo kubwa linalosababisha kutokufanikiwa katika biashara au shughuli zetu.

Soko ndio kila kitu katika biashara yeyote ile. Bila soko hakuna biashara na bila biashara hakuna soko. Kama nilivyosema hapo awali tatizo au  changamoto kubwa aliyonayo mkulima, mfugaji,mjasiriamali,mfanyabiashara mdogo na mfanya biashara mkubwa ni soko. Kwa nini tatizo ni soko? Tulia mzee wa nyundo nikupe uhondo leo.

Mara nyingi soko linakuwa ndio tatizo na changamoto  kubwa   kwa watu wote wanaofanya biashara kwa sababu kuu zifuatazo:

1.Kutegemea  wateja wale wale kwa wafanyabiashara wote.

2.Kuzalisha bidhaa zinazofanana kwa wazalishaji wote kama ni mchele ni huo huo wa  mbeya na morogoro unafanana tofauti tunaitengeneza walaji tu ila bidhaa ni ileile.

3. Kutumia mbinu zilezile za kizamani katika kuuza bidhaa hakuna uboreshwaji katika ufungaji au upangaji.

4. Soko ni tatizo kwa sababu watu wengi hawana elimu ya biashara hukurupuka tu kwa kuambiwa na rafiki au kusikia biashara fulani inalipa.

5.Watu wengi hawafanyi utafiti wa soko la bidhaa wanazozalisha huamini nitawapata tu wateja madamu mzigo au mali ninayo na hivyo kujikuta wakipata hasara na kufilisika.

Siri 15 Za Kukabiliana Na Changamoto Za Soko Katika Biashara.
FANYA UTAFITI WA SOKO KABLA HUJAFANYA BIASHARA
6. Watu wengi hufuata mkumbo kwa kufanya biashara kwa kuona jirani au rafiki yake kafanikiwa naye hujidumbukiza bila kutafiti alianzaje? Hizo ndizo sababu za kwa nini soko ni changamoto au tatizo katika biashara.

Ni kwa namna gani tunaweza kutatua hizi changamoto za Soko?
Sasa twende pamoja nikupe siri 15 za kukabiliana na changamoto au tatizo la soko katika bidhaa, huduma na mali unazozalisha.

1. Lazima ufanye utafiti wa kutosha juu ya uhakika wa soko la bidhaa  zako au biashara  nje na ndani kabla ya kuanza kuifanya biashara hiyo.

2. Ni lazima ujue uhitaji wa bidhaa au huduma ya biashara yako ni ya msimu au ya muda wote.

3. Ni lazima ujue wateja wako ni wa aina gani katika kipato chao, kipato cha juu, cha kati au cha chini kabisa ili ikupe uhuru wa kupanga bei.

4. Ni lazima ujue ni muda gani wanahitaji huduma yako.

5. Ni lazima ujue gharama za uzalishaji, usafiri, na faida ama posho yako kabla ya kufanya biashara yako vinginevyo utaambulia hasara.

6. Ni lazima uwe na taarifa sahihi muda wote kuhusu soko kushuka au kupanda.

 7. Ni lazima ujue uwezo wa washindani wako kibiashara ili ujue namna ya kukabiliana nao kiushindani katika soko.

8. Ni lazima uwe na lugha nzuri kwa wateja wako

9. Ni lazima uwe mbunifu kwenye biashara yako ili kuwavutia wateja wapya na wa zamani.

10. Ni lazima utengeneze network ya watu wazuri wa kushirikiana nao katika biashara yako.

11. Ni lazima uzalishe bidhaa na uuze bidhaa zenye ubora na sio bora bidhaa.

12. Ni lazima wakati mwingine uzalishe bidhaa zako kwa ‘order’ usizalishe ilimradi tu unaweza kuzalisha na kwenda kuweka sokoni ukimsubiri mteja ambaye huna maagano naye kama atakuja ama laa.

13.Tengeneza utaratibu wa kumsogezea huduma mteja wako ikiwezekana mpelekee hadi nyumbani kwake ili kumteka akili yake na kumtoza gharama ya usumbufu kijanja bila yeye kujua.

14.Tengeneza utaratibu wa kuwa na mawasiliano na wateja wako na kuwapigia simu kwa lengo la kuchukua ‘order’ za siku inayofuata.

15. Wape motisha wateja wako ili kuwavutia wadumu kwako na kukuletea wateja wengine.

Asante kwa kunifuatilia ubarikiwe sana ni mimi mshirika wako katika mafanikio na siri za mafanikio Shariff H.Kisuda alimaarufu mzee wa nyundo kali.

Karibu na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.


Mar 22, 2016

Fursa Anazoweza Kuzitumia Kijana Wa Kitanzania Kufanikiwa.

2 comments :
Kimazingira Tanzania, ni moja ya nchi ambayo imejaliwa sana hapa duniani kuwa na fursa nyingi za wazi ambazo ukizitumia ni lazima ufanikiwe. Lakini pamoja na wingi wa fursa hizo ambazo zinaweza kutumiwa na kuleta mafanikio kwa taifa lakini bado kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao hawana ajira.
Kutoka na ukosefu wa ajira vijana wengi wamekuwa wakihaha kutafuta ajira huku na huko bila matumaini. Ni tatizo ambalo limekuwa likisumbua sana si kwa wazazi tu pekee ambao ni wahanga watoto hao, bali hata taifa kwa ujumla. Lakini yote hayo yamekuwa yakitokea na kusahau kwamba tupo kwenye nchi mbayo ina utitiri ama wingi  wa fursa za kutosha.
Kwa kuwa fursa hizi zipo ni matumaini yetu kwamba, badala ya vijana wetu hawa waliomaliza vyuo vikuu kukimbilia ajira ambazo tena kwa sasa ni finyu, ni vyema wakazitumia fursa zinazowazunguka kuwafanikisha. Kwa kusoma makala haya, utajifunza fursa ambazo zinaweza kumsaidia kijana wa kitanzania  popote alipo kujiajiri na kutengeneza mafanikio makubwa kuliko kubweteka peke yake kwa kusubiri ajira.
1. Kilimo cha kisasa kwa kutumia hema.
Hiki ni kilimo kigeni kwa wengi ambacho kinatumia teknolojia ya kisasa ya hema. Lakini pamoja na ugeni wake hiki ni kilimo ambacho pia kinaweza kutatua tatizo la ajira kwa uhakika. Kwa nini iko hivyo? Hiyo ni kwa sababu pato lake linakuwa kubwa na la uhakika ingawa eneo la kulima linakuwa dogo.
Kwa kutumia kilimo hiki kijana anaweza kuchangamkia fursa hii na kuajiri.  Hapa kijana anaweza kujiajiri kwa kujihusisha na kilimo hiki kuliko kukaa na kutegemea ajira peke yake. Kwa mfano, wataalamu wanatuambia katika eneo dogo lenye urefu wa mita kumi na tano na upana wa mita nane lina uwezo wa kutoa tani za nyanya zisizopungua kumi ikiwa litasimamiwa vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa hiyo utaona kwamba kwa kijana ambaye yupo makini na ameamua kuwekeza akitoa nguvu zake nyingi kujihusisha na kilimo hiki basi atakuwa yupo sahihi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine. Kitu kikubwa cha kuzingatia ni  kuwa tayari kutoa gharama zinazohusika hadi kilimo hiki kikafanikiwa na kuwa chenye manufaa makubwa kwa kila kijana mwenye uthubutu.

MKOMBOZI KWA MKULIMA
2. Ufugaji wa nyuki.
Kati ya miradi ambayo naweza kusema ni rahisi kwa kijana yeyote yule wa kitanzania ni ufugaji wa nyuki. Ni moja ya mradi ambao unaweza ukafanywa katika mazingira tuliyonayo bila kuhusisha gharama kubwa sana na ikawa ni chanzo kimojawapo cha kujiajiri na kuingiza kipato kikubwa. Ufugaji huu hauhitaji gharama kubwa sana mara nyingi unafanywa kulingana na pato alinalo mwenye nia ya kuwekeza.
Tuchukulie kwa mfano kwa kijana ambaye hana mtaji anataka kufuga nyuki ili wamzalishie asali hapa anafanyaje? Kitu ambacho anaweza akafanya si lazima awe na mizinga ya kisasa. Anaweza akatengeneza vibuyu au magome ya miti na kuweka mizinga yake kwa ajili ya ufugaji rasmi. Baada ya kuweka mizinga inatakiwa aweke mazingira rafiki ya kuvutia nyuki kama maji na nta.
Kwa kijana amabaye atafanikiwa kujihusisha na ufugaji huu na akasimamia vizuri, ni ushahidi tosha hata hiyo ajira hatoitaka tena kutokana na pesa atakayoingiza. Hii ni moja ya fursa kubwa sana ambayo inatoa ajira isipokuwa vijana wengi wanakuwa kama wamefungwa macho kwa kushindwa kuona ni nini cha kufanya na kujikuta kukimbilia mjini ambako ajira zenyewe zimekuwa ni kwa uchache.

WEKA MIZINGA BORA.
3. Kilimo cha mazao ya biashara.
Mbali na ufugaji wa nyuki na kilimo cha hema, kijana anaweza kuchangamkia fursa ya kufanya kilimo cha mazao ya biashara. Mazao haya yanaweza yakawa kama karanga,  choroko, kunde, alizeti au hata pamba lakini hiyo yote inategemea sana na eneo ambalo upo urahisi wa kipi kwako cha kufanya.
Kitu kikubwa ni kule kufuta mitazamo hasi kwamba kilimo ni cha watu duni hiyo siyo kweli. Watu wengi wanaoendesha maisha yao vizuri sana kwa kutegemea kilimo hiki cha kisasa. Anza kwa kujifunza kwa wale wakulima waliofanikiwa na kisha changamkia fursa ya kilimo hiki ambacho kinaweza kikawa mwanzo wa ajira kubwa kwako kuliko unavyofikiri.
Kwa kijana ambaye ataingia kwenye kilimo hiki kikamilifu na akasimamia masoko vizuri, njia ya mafanikio itaonekana kwake. Uzuri wa kujihusisha na kilimo hiki cha mazao ya biashara hata soko lake mara nyingi linakuwa kubwa hali ambaye hupelekea kupata faida kubwa kwa mkulima. Hivyo ni wito wetu kuhakikisha vijana wengi wanaolia ajira hakuna kulizingatia hili sana na kuamua kuchukua hatua.

IKILIMWA VIZURI, PATO NI KUBWA.
4.  Ufugaji wa samaki.
Pia ufugaji wa samaki unaweza ukawa ni chanzo kizuri cha kipato kwa vijana wengine ambao hawana kazi hasa katika yale maeneo ambayo ni shida kupatikana kwa samaki. Ufugaji huu unaweza  ukafanywa kwa kuchimba bwawa dogo la samaki na kuanza kutengeneza pesa. Bwawa si lazima liwe kubwa sana linaweza likawa  dogo hata la mita 'square' mia nne.
Uzuri wa kufuga samaki ni kwamba kwanza wanachukua muda mfupi,  pia inachukua miezi minne kukua. Lakini hiyo haitoshi upatikaji wa vifaranga wa samaki pia sio mgumu na vinapatikaana kwa bei rahisi. Lakini uzuri mwingine si kupatikana kwa vifaranga tu,  bali hata pato lake linakuwa ni kubwa kulingana  na kile ulichowekeza kwa muda mfupi.

BWAWA LA KUCHIMBWA LA SAMAKI.
Wataalamu wanatuambia hivi, kwa mfano kama umeweka samaki kwenye bwawa dogo la mita square mia nne. Kwanza bwawa hilo linauwezo wakuchukua samaki elfu nne. Sasa kama eneo hilo linachukua samaki hao na kila samaki akawa na nusu kilogramu, basi kwa bwawa hilo ndani ya miezi minne utapa milioni nane hata kama kilo moja hapo utauza kwa shilingi elfu nne.
Hizi ni baadhi ya fursa chache ambazo kijana wa kitanzania anaweza kuzitumia kufanikiwa. Ingawa hata hivyo kijana anaweza kujihusisha na mambo mengine zaidi ya kumuingizia kipato kama ufugaji wa kuku kwa kisasa au hata kilimo cha matunda.
Chukua hatua kufikia mafanikio makubwa na acha kuendelea kulia eti ajira hakuna, yapo mambo mengi ya kufanya.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwau,
Simu; 0713 048035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com