google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 29, 2016

Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa.

No comments :
Kila kitu kilichopo dunia kinaongozwa na sheria zake. Sheria hizo zinapotumika ipasavyo mara nyingi sana huleta mafanikio makubwa. Na inapotokea sheria hizo zikavunjwa hakuna mafanikio yanayokuwepo zaidi ya kushindwa kwa wale wote waliovunja sheria hizo.
Haijalishi upo katika eneo gani sheria ni muhimu sana kuzingitiwa. Iwe katika afya, elimu, mchezo wa mpira wa miguu, au biashara sheria huwa zipo na zinafanya kazi. Sheria hizi ndizo zinazotupa mwongozo bila kujali uwe unazijua au huzijui lakini zipo, ukikosea unahukumiwa.
Katika makala hii tutajifunza sheria zitakazo kusaidia kufanya biashara yako kwa ushindi. Bila shaka umekuwa ukiona wengi wakifanya biashara zao kwa mazoea sana. Kutokana na mazoea hayo hupelekea biashara nyingi kugeuka kuwa kama ‘miradi bubu’ ambayo haina faida yoyote.
Sitaki hilo lizidi kukutokea sana la kufanya biashara ambayo haikupi faida kubwa unayoifikiri kwa muda mrefu. Inabidi ukubali umekosea na kaa chini ujifunze sheria za msingi kabisa ambazo zinaweza kukusaidia kukutoa hapo na kukupeleka katika hatua nyingine ya mafanikio kibiashara.
Zifuatazo Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa.
1. Toa huduma bora kwa wateja wako.
Toa huduma bora itakayowafanya wateja wako waweze kujisikia vizuri na kushawishika kuja kununua tena kwa wakati mwingine. Kwa kutoa huduma bora itakusaidia sana kutokuendesha biashara yako kimazoea. Ila ikiwa utajisahau au kusahau sheria hii basi elewa utajitengenezea mazingira ya kushindwa kiurahisi kwenye biashara unayoifanya.

TUNZA MTAJI WAKO.
2. Jijengee mazoea ya kuwa na lugha ya ukarimu.
Hili ni jambo litakalokusaidia sana kukuza biashara yako kwa sehemu kubwa. Kuna wakati unakutana na wateja ambao ni wakorofi hawaeleweki. Tambua hutakiwi kuwaonyesha chuki wala kuwasemesha kwa lugha ya ukali. Toa lugha ya ukarimu wakati wote unapokuwa kwenye biashara yako.
3. Jali sana muda wa wateja wako.
Kitu kizuri kabisa kitakachokufanya uweze kujijengea uaminifu na kukuza wateja wako ni uwezo wako wa kujaali muda wa wateja. Muda ni kitu cha muhimu sana kwa mteja wako. Kwa namna yoyote ile usimpotezee mteja wako muda wake. Jitahidi sana kumhudumia katika muda mwafaka ambao amefika na sio kumchelewesha bila sababu ya msingi.
4. Mazingira yako yawe safi.
Kila wakati na kila siku, hakikisha mazingira ya unapofanyia biashara yako yawe safi. Lakini si mazingira tu hayo yawe safi bali hata wewe na wahudumu wako lazima muwe wasafi ili kuhakikisha kumvutia wateja katika eneo watakalo kaa. Hii ni sheria nzuri sana ambayo inaweza kupelekea kukuza wateja wako siku hadi siku.
5. Weka matangazo ya biashara yako.
Ni vyema ukajitengenezea matangazo ya biashara yako. Hakuna biashara ambayo inaweza ikakua sana bila kuwa na matangazo. Matangazo ni muhimu sana kwa biashara yoyote. Matangazo yanaisadia biashara yako kuweza kujulikana katika maeneo mengi ambayo ilikuwa sio rahisi kuweza kujulikana na kwa muda mrefu.
6. Simamia kauli zako.
Unapokuwa kwenye biashara muda wako wote hakikisha unafanya kile unachokisema. Simamia kauli zako, bila kuyumbishwa. Kama uliwaambia wateja wako mzigo utaletwa wiki ijayo , hakikisha hilo linatekelezeka pia. Kwa kifupi hapa hutakiwi kuwa mwongo. Toa taarifa sahihi zitakusaidia kukuza wateja wako na kuwa wengi.
7. Kuwa mwangalifu na mtaji wako.
Pamoja na kwamba biashara yako inaweza ikawa imeanza kukupa ile faida inayotarajiwa, lakini ili kuikuza na kuifanya kwa ushindi zaidi ni vyema ukawa mwangalifu na mtaji wako. Acha kutumia pesa zako hovyo sana ambazo zipo kwenye biashara. Tunza mtaji wako ukusaidie kuweza kuwekeza pia katika maeneo mengine muhimu.
8. Jenga mazoea ya kujifunza siku zote.
Hapa nikiwa na maana jifunze kutoka kwa wenzako wanafanya nini? Jifunze kwako pia hasa kile kipindi unapotokea umekosea. Ukikosea acha kujibebesha hasira ambazo zinaweza kukubomoa na kukuharibu. Badala yake kaa chini, kisha jifunze kwa nini umekosea katika hili. Na baada ya hapo rekebisha na endelea na safari.
Kwa kuzijua sheria hizi zitakusaidia sana kuweza kuendesha biashara yako kwa ushindi na mafanikio makubwa.
Nikutakie siku njema na pia napenda kukumbusha endelea kuwakumbusha wengine kuendelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.

Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

Jan 28, 2016

Hawa Ndio Watu Ambao Hawadumu Sana Katika Ndoa Zao.

No comments :
Baada ya kusemwa kama hadithi, hivi sasa imethibitika kwamba, watu wanaooana kwa sababu ya kuvutana kimwili, kimtazamo, imani za dini zao na nasaba wanazotoka, hawawezi kudumu kwenye ndoa kama tabia zinatofautiana.
Kuna watu ambao huoana kwa sababu tu ni waumi wa dhehebu moja. Wengine huoana kwa sababu wazazi wao wanatoka kwenye familia za kiwango cha juu kimapato au kisomi, ama kiwango cha chini. Wengine huona kwa sababu wana mitazamo ya aina moja kwenye jambo fulani. Huku wengine wakiona kwa sababu ni kabila moja.
Imethibitika sasa kwamba, nusu ya ndoa zinazofungwa kwa sababu hizo, huwa hazidumu. Tafiti kadhaa zinaonesha kwamba, ndoa zinazodumu ni za wale watu ambao wameoana kwa sababu kila mmoja amezijua tabia za mwingine na kukubaliana nazo.
Lakini kikubwa kilichobainika ni kwamba, wanaooana  na kudumu kwenye ndoa, ni wale ambao wanalingana tabia kwa sehemu kubwa. Bila kujali kila mmoja anatoka na familia ya namna gani, dini au mitazamo, tabia zikikaribiana kulingana, uwezekano wa kuishi katika ndoa ya amani ni mkubwa sana.

TABIA NJEMA KWENYE NDOA NI MUHIMU SANA.
Kwa kuwa ni vigumu sana kwa watu kujua tabia zao, kuoana kwingi kumefungwa kwenye vigezo nilivyovitaja ambavyo ni muda. Baada ya muda fulani kwenye ndoa, wanandoa hugundua kwamba, vigezo vilivyotumika kuwaunganisha, havina uwezo wa kuwafanya wadumu tena kwenye ndoa hiyo.
Hii ina maana kwamba, wapenzi wanapokuwa na tabia zinazokaribiana, ndoa yao pia inaweza kuwa imara zaidi. Lakini wapenzi kuunganishwa na dini zao, hadhi yao katika jamii na mitazamo fulani, haiwezi kuwahakikishia wanandoa kuwa na ndoa imara.
Mitazamo fulani ya aina moja, imani ya dini au kiwango sawa cha kipato kifamilia, huwavuta watu awali wanapokutana na kuoana. Hii inatokana na ukweli kwamba, sifa hizi huonekana haraka na ni sifa muhimu kwa watu wengi katika kuendesha maisha yao, wakati tabia zimejificha.
Huchukua muda kwa mtu kugundua tabia halisi za mwingine. Bahati mbaya sana mtu anapohisi kwamba fulani amempenda, huweza kuficha udhaifu wake kitabia na hivyo kuwa ngumu zaidi tabia kuchukuliwa kama kigezo, wakati ndicho kigezo halisi kinachotakiwa kutazamwa kabla watu hawajaamua kuoana.
Lakini bahati mbaya ni kwamba, kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye ndoa, ndivyo tabia zinavyojitokeza na kuwa muhimu sana katika kuimarisha ndoa hiyo. Kwa hiyo, kama tabia hazifanani, ina maana kwamba, kadri siku zinavyoenda, ndivyo wanandoa wanavyozidi kushindana.
Uhusiano imara na wenye faraja unahitaji mawasiliano ya mara kwa mara kuhusiana na shughuli za wanandoa, masuala mbalimbali, matatizo na suluhu za mambo mengi ya kimaisha. Kama tabia za watu wawili haziwiani katika mambo, ni wazizi kutakuwa na tatizo.
Baadhi ya watafiti wanasisitiza kwamba watu wote ambao wanaingia kwenye ndoa huku wakijua kwamba kitabia hawakaribiani, ni sawa na kupiga mbizi baharini wakati mtu hajui kuogelea.
Pale ambapo watu wanataka kufunga ndoa, wanaona wazi wazi kuwa kitabia ni watu wawili tofauti sana, hawashauriwi kuendelea na zoezi hilo kwani litawaumiza vibaya sana hapo baadae.
Kama tabia zinalandana sana, bila kujali kama ni watu wadini moja, uwezo sawa wa kifamilia, kabila moja na mitazamo fulani ya aina moja, watu hao hao wanaweza kutabiriwa bila wasiwasi kwamba, ndoa yao itadumu.
Nikutakie siku njema na mafanikio bora katika ndoa yako. Endelea kujifunza kupitia DIRAYA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri uwe wa kibiashara/maisha, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com



Jan 27, 2016

Mambo Ambayo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kuyafanya Kwenye Maisha Yako Yote.

No comments :
Habari za siku mpenzi msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Naamini umeianza siku yako ya leo ukiwa mzima wa afya na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako kwa kujifunza na kupata maarifa ya kukusaidia kwenye safari ya mafanikio.
Nakukaribisha kama kawaida yetu kuweza kujifunza tena. Katika makala yetu hapa leo, tutajifunza kuangalia yale mambo ambayo tunatakiwa kuwa wa kwanza kila siku kuyafanya katika maisha yetu. Kwa kadri tutakavyozidi kuwa wa kwanza kuyafanya mambo hayo yatasaidia sana kuboresha maisha yetu.
Yafutayo Ni Mambo Ya Msingi Ambayo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kuyafanya Kwenye Maisha Yako.
1. Siku zote katika maisha yako jifunze kuwa wa kwanza kunyanyuka hasa pale inapotokea umeshindwa kwa lile jambo unalolifanya. Acha kufanya kosa la kubakia hapo ikiwa umekosea nyanyuka haraka na endelea na safari.
2. Kuwa wa kwanza kuomba msamaha inapotokea umewakosea wengine. Ni kweli huwa tunawakosea wengi, lakini je wewe binafsi huwa ni wa kwanza kuwaomba msamaha, kama hufanyi hivyo anza sasa kusamehe mapema.
3. Kuwa wa kwanza siku zote kujifunza inapofika wakati unakosolewa. Jifunze kwanini wanakukosoa hivyo na kisha chukua kukosolewa huko kama somo au daraja la kukusaidia kuendelea mbele kimafanikio.

JIFUNZE HARAKA UNAPOKOSEA.
5. Kuwa wa kwanza siku zote kuonyesha ukarimu kwa watu wanaokuzunguka. Na inapotokea wengine wanata msaada wasaidie bila kinyongo, hiyo ni njia bora itakayokutengenezea maisha mazuri na jamii inayokuzunguka kwa ujumla wake.
6. Kuwa wa kwanza pia kutaka kuhoji pale unapoona mambo yako mengi hayaendi vizuri kwako. Inapotokea mipango imekwama jiulize kwa nini iko hivyo kwako. Kwa jinsi utakavyojiuliza hivyo utapata majibu mengi yakukusaidia.
7. Kuwa wa kwanza katika maisha yako kung’ang’ania mafanikio yako, mpaka yatokee. Usikatishwe wala usizuiliwe na kitu chochote. Jiwekee falsafa ya kuwa king’ang’anizi mpaka uone ndoto zako zote kubwa ulizojiwekea zinatimia.
8. Jifunze kuwa mtu wa kwanza kufurahia mafanikio unayoyapata hata kama ni kidogo. Unapofanikiwa ni vyema ukajijengea utamaduni wa kujipongeza kwa kile ulichokifanikisha. Hapo utavuta nguvu mpya za kutafuta mafanikio mengine tena.
9. Endelea kujifunza kuwa wa kwanza kufanya lile jambo ambalo unaliogopa sana kwenye maisha yako. Kwa kulifanya jambo hilo litakusababisha wewe ule woga uliokuwa nao kupotea kabisa.
10. Kuwa wa kwanza pia kuamini kwamba ipo nafasi nyingine ya kujaribu tena na tena, ikiwa umetokea umeshindwa kwa mara ya kwanza. Kushindwa kwako kusikufanye ukaamini huo ndio mwisho dunia. Jaribu tena kama umeshindwa mpaka utafanikiwa.
11. Kuwa wa kwanza kufanya yale mambo ambayo wengine wanayatolea sababu kuwa hawawezi kuyafanya. Mambo yanayochosha, yanayokatisha tamaa, ambayo yanaonekana kama hayana matumaini tena. Kuwa wa kwanza kuyafanya mambo hayo.
12. Kuwa wa kwanza kumsaidia yule ambaye hajiwezi, pengine amekosa mtu wa kumsaidia kabisa. Mtu huyo msaidie kimawazo, mpe moyo na nguvu kubwa ya kuona maisha kwa upya. Kuwa wa kwanza.
Kwanini unatakiwa kuwa wa kwanza katika mambo haya? Unapokuwa wa kwanza kwa mambo haya hii itakusaidia sana kukuweka tofauti kidogo na mazoea ya wanayofanya watu wengine na pia itakujengea kubadili sana maisha yako na ya wengine kimafanikio.
Nikutakie siku njema, kumbuka kuendelea kuwashirikisha wengine kuzidi kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com







Jan 26, 2016

Tabia 5 Unazotakiwa Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.

No comments :
Ili kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri ni safari inayohitaji kujituma na uwe mvumilivu hadi kufikia mafanikio hayo. Wengi hujikuta kushindwa kufikia mwisho wa safari hii kwa sababu mbalimbali zinazowakabili. Lakini moja ya sababu hizo ni tabia mbaya wanazokuwa nazo hasa pale wanapokuwa na pesa.
Unaweza ukashangaa kwa nini naziita tabia mbaya? Usipate tabu, hizi ni tabia mbaya kwa sababu ndizo zinazowakwamisha na kuwarudisha wengi nyuma kimafanikio zaidi. Sasa wengi wanakuwa ni watu wa kushikiria tabia hizi ambazo wanatakiwa kuziacha mara moja. Kwa kung’ang’ania huko huwarudisha nyuma sana kimafanikio.
Je, unajua ni tabia zipi unazotakiwa kuziacha mara moja hasa pale unapokuwa na Pesa?
Zifuatazo Ni Tabia 5 Unazotakiwa Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.
 1. Kutokupangilia matumizi.
Ili uweze kufanikiwa na kutunza pesa ulizonazo ni vyema sana ikiwa utapangalia matumizi yako kila siku. Unapokuwa unapangilia matumizi yako inakuwa inakusaidia sana kutokutumia pesa zako hovyo. Ni rahisi sana kutumia pesa zako hovyo kama hujaandika popote. Kutokupangilia matumizi ni moja ya tabia unayotakiwa kuiacha mara moja ili kufanikiwa.

PANGILIA MATUMIZI YAKO VIZURI.
2. Kutumia kila pesa unayoipata.
Mara nyingi watu walio wengi hutumia pesa zao zote walizonazo bila ya kuweka akiba hata tone. Haya ni maisha ambayo wengi wamekuwa nayo na wanayaishi kila siku. Kila wanapoulizwa kwa nini iko hivyo, sababu yao ni moja tu kwamba pesa haiwekekiki. Na kwa imani hiyo hujikuta hakuna akiba wanayoiweka na kubaki kuishi maisha magumu. Kama nia yako kubwa ni kufanikiwa achana na tabia hii mara moja.
3. Kufanya matumizi yasiyo ya lazima.
Kuna watu wanapokuwa na pesa huwa zinawasumbua sana. huwa ni watu wasiotulia kwa kutaka kununua karibu kila kitu wanachokiona mbele yao. Unapokuwa na tabia hii kwa uhakika unakuwa sio rahisi kuweza kufanikiwa. Kitu ambacho kinakuwa kinakufanya ushindwe kufanikiwa ni kwa sababu pesa zote unakuwa unazitumia hovyo na kushindwa kuweka hata akiba ya kukusaidia
4. Kutokuweza.
Utakuwa upo kwenye hatari sana kwenye maisha haya kama utakuwa unaishi maisha bila ya kuwekeza. Kuwekeza ni jambo la msingi sana ambalo unatakiwa ulitilie mkazo kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi. Ili uweze kufanikiwa unalazimika kuwekeza pesa zako na sio suala kutumia tu. Kutokuwekeza ni moja ya tabia unayoitakiwa kuicha ili kujenga mafanikio ya kudumu.
5. Kushindwa kulipa madeni yako mapema.
Yapo madeni ambayo wengi hutakiwa kulipa mapema, lakini hata hivyo wengi pia hujikuta wanashindwa kulipa madeni hayo kwa muda mwafaka. Kitu cha msingi hapa kama kuna madeni unadaiwa kwa mfano ada za watoto, kodi mbalimbali ni vyema ukalipia mapema na kwa utaratibu ili kujiepusha na usumbufu ambao unaweza ukjitokeza kwako kwa baadae.
Kama utachukua hatua na kuamua kuachana na tabia hizo utajijengea mazingira ya kufikia mafanikio makubwa kwako kwa kadri siku zinavyokwenda kwenye maisha yako.
Nakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe upande wako. Kumbuka endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu, 
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com





Jan 25, 2016

Anza Na Ulichonacho Kupata Mafanikio.

No comments :
Kisaikolojia na kimaumbile binadamu wote ni sawa ila tunatofautiana jinsia na matumizi ya vitu tulivyopewa na mwenyezi Mungu. Na hii ndio hupelekea tofauti kubwa kati ya walichonacho (Matajiri) na wasionacho (maskini).

Katika kuanza na ulichonacho leo tunaangalia vitu sita ambavyo tumepewa kama zawadi na Mungu. Na kila mtu amepewa sawasawa na mwenzie ila tofauti ni matumizi yetu katika kutupatia kile tunachokitaka katika maisha yetu ambacho ni Mafanikio.

Ili kufanikiwa haijalishi upo katika hali gani, kitu kikubwa kwako ANZA NA ULICHONACHO KUPATA MAFANIKIO. Unaweza ukajiuliza kivipi? Usipate tabu. Ungana nami mzee wa Nyundo nikuhabarishe na kukupa nyundo za kukuzindua katika usingizi ili upate mafanikio ya kweli.

1. Akili.
Ni ukweli kwamba kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanazitumia kwa faida na malengo na kupata mafanikio ila wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha shida hadi wanakufa.

Katika kuitumia akili ndipo huonekana tofauti ya wanaojua na wasiojua kitu. Wanaofuata mkumbo na wanatumia akili zao kufikiri na kuamua ni nini wafanye, kivipi na wakati gani. Ili kuonyesha matumizi sahihi ya akili kila binadamu anatakiwa kufikiri na kuwaza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote katika maisha yake.

Ni vyema tusiwe watu wa kuamini kirahisi tunayoona na kusikia kwa watu na kuyafanya bila tafakari. Tuzitumie akili zetu katika kujituma na kufikiri kwa utofauti na wanavyofiki wengine . Tuwe tayari kujifunza kwa wenye elimu juu ya kile tunataka kufanya na sio kuiga wanavyofanya watu wengine. 

TUMIA AKILI YAKO VIZURI KUKUFANIKISHA.
2. Muda.
Kila binadamu awaye ana muda na amepewa muda wa kuishi na kufanya mambo yake kwa  uhuru na amani . Lakini si watu wote wanaoutumia muda wao vizuri katika kujipatia mafanikio. Wengi hutumia ujana wao katika starehe, ulevi na kujirusha. Wengine wanatumia muda wao katika kufuatilia maisha ya watu umbea na majivuno.

Pamoja na kutumia muda hovyo lakini kumbuka, huo ndio muda wako wa kujitafutia maisha na mafanikio. Muda ndio rasilimali muhimu kuliko zote ukiutumia vizuri hakika mafanikio utafanikiwa. Embu jiulize kuna tofauti gani kati ya tajiri na masikini katika muda? Kila mtu ana masaa  24 tofauti ni matumizi tu .

Ukafatilia utagundua, tajiri ana panga malengo na mipangilio yake katika siku wakati maskini hana mipangilio na muda wake anaweza kushinda asubuhi hadi jioni anaangalia  Televisheni au movie ambazo hazimsaidii kitu katika maisha yake. Jiangalie vizuri unatumiaje muda wako ili kuyafikia mafanikio yako?


3. Watu.
Kila mtu iwe  kwa kutaka au kutotaka amezungukwa na jamii ya watu. Na kimsingi umepewa watu hao na Mungu ili uweze kuwatumia na kupata kile unachotaka. Kuna wale wa hiyari na ambao unalazimika kuwatafuta mwenyewe ili wakusaidie kupata kile unataka katika maisha yako.

Kwa  mfano mwalimu inabidi umtafute ili akupe elimu, wataalamu wa afya inakulazimu uwafuate ili wakutibu. Lakini kuna watu ambao umepewa bila kutaka au kupanga wewe kama wazazi, ndugu, wajomba na mashangazi. Hakuna aliyepanga kuzaliwa na wazazi fulani au kuzaliwa tumbo moja na mtu fulani bila kujali ni masikini au tajiri.

Lakini kutokana na watu hawa unaweza na unapaswa uwatumie katika ushauri na maarifa waliyonayo ili kupata kile unachotaka ambacho si kingine ni mafanikio. Kushindwa kwako kuwatumia watu hawa hili litakuwa ni tatizo lingine ambapo ukishindwa kufanikiwa usimlaumu mtu.

4. Kipawa / kipaji.
Huu ni uwezo wa ndani alionao kila binadamu bila kujali kabila lake au rangi yake ana kile anachoweza kukifanya tofauti na wenzake. Hicho ndicho kipaji na mtu akikigundua na kukitumia vizuri hupata mafanikio kwa haraka.Tena ndio wale ambao muda mfupi hupata utajiri wa ghafla na watu kusema kajiunga na Freemason huyo au amemuua mama yake ili apate utajiri na maneno mengineyo.

Siku zote tafuta ukijue kipaji chako na kitumie upate utajiri na mafanikio katika maisha yako. Unapokuwa na kipaji na ukikitumia ipasavyo mafanikio makubwa yanakuwa upande wako. Jaribu kuangalia watu wote ambao walimudu kutumia vipaji vyao kwa namna moja au nyingine maisha yao yako vipi, bila shaka ni ya mafanikio makubwa sana.


5. Nguvu.
Kila mtu amepewa nguvu na uwezo wa kufanya jambo fulani.Tunaweza kuzitumia nguvu zetu katika kilimo, biashara na hata kazi yeyote halali na kujipatie kile tunataka katika maisha. Tatizo watu wengi tumebweteka tunataka maisha simple/rahisi  tulale tuamke kesho matajiri bila kufanya kazi.

Vijana wengi utakuta wanataka kufanya kazi rahisi na kupata faida kubwa. Wanacheza mchezo wa kubeti wakiamini watatoka kimaisha, wanacheza bahati nasibu wakiamini watapata utajiri, wengine  wanauza miili yao wakiamini ndio njia pekee ya kupata maisha mazuri na bora kumbe wanapotea na kuharibikiwa kabisa. 

6. Afya.
Kila binadamu amepewa afya ya mwili kabla ya kufikwa na maradhi. Tunapaswa tujue uzima na afya ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu hivyo tuzitumie vizuri afya zetu katika kupata kile tunataka katika maisha yetu. Afya ni kitu cha muhimu kukilinda na kukitumia vilivyo kwa faida ya maisha yetu.

Ili tufurahie maisha yetu lazima tujali afya zetu kwa kula vyakula bora na vinywaji bora. Na sio kula ilimradi chakula.  Na kunywa ilimradi tu au kwa kuwa watu wanakula nasi tule. Tujitahidi kuzilinda na kuzitumia vizuri afya zetu ili tuweze kutimiza malengo yetu tuliyojipangia katika maisha. Bila afya nzuri hakuna Mafanikio. Kila mtu na azingatie mbinu hizi katika mafanikio yake zitamsaidia na kumwongoza.


Kabla ya kuhitimisha makala hii ni vyema ukajiuliza je, unatumia vizuri akili, watu, muda, nguvu, afya na kipawa ulichonacho kukusaidia kufikia mafanikio yako? Tafakari juu ya hili na chukua hatua.

Asanteni kwa kunifuatilia na kuwa pamoja nami. Pia naamini umepata mwanga na kitu cha kukusaidia kutoka hapo ulipo. 

Nakutakia siku njema na endelea kujifunza mambo mengine matamu ya kimafanikio hapa kwenye mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.

Shukrani za pekee zimwendee SHARIFF H. KISUDA a.k.a MZEE WA NYUNDO kwa kutushirikisha makala hii nzuri. Unaweza ukawasilina naye kwa simu namba 0715 079993 kwa msaada zaidi wa Saikolojia ya mafanikio.



Jan 22, 2016

Misingi 5 Ya Kuifahamu Kabla Hujaanza Biashara.

No comments :
Karibu tena mpenzi msomaji wa makala hii ya DIRAYA MAFANIKIO, ni wakati mwingine  tunakutana tena katika safu hii ili kuweza kukumbushana baadhi ya mambo msingi katika biashara zetu, ili kuweza kufanya biashara yenye faida kubwa.
 Mara nyingi baadhi yetu huwa tunaanza biashara kwa kusikia kwa watu faida ya biashara hiyo, bila kuwa na msingi halisi wa kuifahamu biashara husika.  Lakini katika makala yetu hii ya leo tutaangalia misingi muhimu ya kuielewa mapema kabla ya kuanza biashara yoyote.
Mambo hayo ya msingi tutakayojifunza hapa ni maalumu kwa ajili ya wote wanaotaka kuwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia. Kwa yeyote anahitaji kupata faida kubwa na kuepuka kupata hasara zisizo za lazima katika biashara yake, misingi hii ni muhimu sana kwake kuijua.
1. Eneo la kufanyia biashara.
Kwa kuwa ndio kwanza unaanza kufanya biashara lazima ufanye uchunguzi wa kutosha juu ya kile unatochotaka kukifanya. Eneo hili lakufanyia biashara  ni lazima ulichunguze kwa kuangalia uhitaji wa  wa wateja wa eneo husika.
Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza vifaa vya shule (stationery) lazima ujiulize ni wapi ambako unahisi ukiweka biashara yako kuna wateja wengi. Baada ya kufikiri unaweza ukaangalia kwenye maeneo ya shule,vyuo , kanisani na maeneo mengine.
Lakini hiyo haitoshi nenda sehemu husika jaribu kufanya uchunguzi ni vitu gani wanavifanya wafanyabiashara wengine ambao wana biashara kama yako? Angalia ni changamoto gani wanazozipata ili pindi ukianza kufanya biashara hiyo ujue mbinu za kupambana na changamoto hizo kirahisi.

CHAGUA ENEO ZURI LA KUFANYIA BIASHARA.
2. Wateja.
Baada ya kuona ni eneo gani linafaa kufanya biashara jambo la pili la kujiuliza je wateja wako watakuwa ni wakina nani? Hili ni swali la msingi sana kujiuliza kwa sababu lengo la kufanya biashara ni kupata wateja wengi, hata hivyo katika kuangalia hili pia fanya uchunguzi wa kina juu mahitaji ya wateja.
Hii utakusadia wewe pindi unapofikiri ni biashara gani ya kufanya.Tukiangalia tena mfano wa kuanziasha biashara ya vifaa vya shule yaani (stationery) tunaona ya kuwa wateja wako watakuwa ni wanafunzi na baadhi ya watu wengine kama eneo ambalo ulilifikiri la kufanyia biashara itakuwa kwenye taasisi yeyote mfano shule au kanisani.

TAZAMA ENEO LENYE WATEJA WA KUTOSHA.
3. Bidhaa.
Ewe msomaji wa makala hii unayependa kufanya biashara yeyote eidha ni ndogo au kubwa lazima ufikiri kwa kina je bidhaa gani ambazo utaziuza? Swali hili la bidhaa utajiuliza baada ya kufanya uchunguzi juu ya eneo husika la kufanyia biashara? na pia kwa kuangalia je ni mahitaji gani ya wateja ?
Pia jifunze kuangalia bidhaa ambazo baada yakufanya  uchunguzi na ukagundua ni bidhaa gani adimu pia zina uhitaji mkubwa chukua kama changamoto na lifanye kama fursa. Ukishapata majibu fanya utaratibu wote mpaka upate bidhaa hizo.

BIDHAA ZAKO ZIWE NA UBORA
4. Matangazo.
Kuna usemi husema biashara matangazo. Hii ni kweli kabisa ili biashara iweze kuwa nzuri ni lazima wateja wako waipate kupitia matangangazo. Matangazo haya yanaweza kuwa kuwajulisha wateja wako juu ya ujio wa bidhaa mpya, mabadiliko ya bei na vitu vinginevyo vihusuvyo biashara.
Matangazo haya unaweza kuyasambaza kupitia mitandao ya jamii na vyombo vya habari pia kwa mfanyabiashara mdogo unaweza ukaandika bango  la biashara nje ya eneo lako la biashara unayoifanyia ili kuwajulisha wateja wako.
Tunakutakia kila la kheri katika mafanikio ya biashara yako.
Makala hii imeandaliwa na:-
Afisa mipango na mendeleo,
Mr. Benson .O. Chonya,
Mawasiliano,
Instragram; Benson Chonya,
Facebook; Benson Chonya,
Tel; +255 757 909 42.


Jan 21, 2016

Mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.

No comments :
Sasa baada ya utafiti wa muda mrefu imegundulika kwamba macho yetu yana uwezo wa kutufundisha mengi sana ikiwa tutakuwa tunayachunguza kwa umakini. Wataalamu hao wamegundua macho yetu yana uwezo wa kutuonyesha mambo mbalimbali  kama tunasema uongo au ukweli,  kutuonyesha jinsi tunavyofikiri na hata kutoa mustakabali wa afya zetu.
Kwa  mujibu wa wataalamu hawa wanadai kwamba yapo mambo mengi yaliyofichika kwenye macho yetu bila hata sisi wenyewe kuelewa. Hii ni sayansi ambayo inaweza ikawa ya kustaabisha kidogo kwako, ingawa ukweli wa mambo ndivyo ulivyo na utabaki hivyo. Ni vyema sana kama ukafahamu vizuri mambo yaliyofichika kwenye macho yako.
Yafutayo Ni mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.
1. Magonjwa uliyonayo.
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika zinaonyesha kwamba rangi za macho yetu zinauhusiano mkubwa wa moja kwa moja na baadhi ya magonjwa yanayotupata. Kwa mfano watu wengi wenye macho yanayoonyesha rangi ya ‘bluu’ hawa hupatwa sana na magonjwa ya kisukari, mabaka mabaka mwilini na kansa ya ngozi.
Lakini hata hivyo kuna wengine wanakuwa wana macho yana rangi za aina mbili kwa mfano labda ‘bluu’ na ‘brown’. Kwa watu kama hawa magonjwa yanayowakumba ni kama vile ngozi kukakamaa maeneo ya usoni. Kwa hali hiyo ukichunguza watu wenye macho ya rangi ya ‘bluu’ wengi wanasumbuliwa sana na magonjwa hayo.

MACHO RANGI YA 'BLUU'
2. Haiba yako.
Macho yako pia yana uwezo mkubwa wa kuonyesha haiba uliyonayo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Australia na  jopo la waataalamu lililoshirikisha watu 366,  utafiti huo unaonyesha kwamba watu wenye macho hasa ya mng’ao (bright eyes) mara nyingi hawa wana mvuto mkubwa sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na kwenye masuala ya kimapenzi.
Na wakati huo watu wenye macho meusi (dark eyes) utafiti huu unaonyesha hawa ni watu ambao hawana mvuto sana katika jamii, mara nyingi huwa ni wa kimya na mambo yao kwa ujumla usipowachunguza hata kidogo huwa yanayoonekana ni kama vile hayaeleweki na ni ngumu kuwatambua kirahisi.

UGONJWA WA MABAKA MABAKA (VITILIGO)
3. Maumivu unayobeba.
Pia utafiti unaonyesha macho yana uwezo wa kuonyesha kwamba wewe ni mtu mwenye uwezo wa kubeba maumivu ya aina gani. Kwa mfano wanawake wenye macho ya mng’ao (bright eyes) utafiti unawaonyesha kwamba hawa hupata maumivu kidogo pale wanapojifungua tofati na wanawake wenye macho ya ‘dark blue’.
Wanawake hawa wenye macho ya mng’ao ( bright eyes)  si tu kwamba wanakuwa wana maumivu madogo wakati wanajifungua lakini pia ni watu wenye hofu kiasi, hawana msongo wa mawazo mkubwa na pia si watu wa kuwaza hasi sana. Pia hiyo haitoshi inapotokea wakanywa pombe kwao huwa sio rahisi sana kulewa.

MACHO RANGI YA 'BROWN'
4. Maumbile yako.
Ni ukweli ulio halisi pia macho yako yana uwezo wa kututambulisha maumbile (Genetics) ulizonazo. Kwa mfano mwaka 2008 wanasayansi waliweza kugundua kwamba watu wote wenye macho ya ‘bluu’ wamerithi maumbile au genetics moja kwa moja kutoka kwa baba zao. Kwa hiyo ni watu wanaofanana na baba zao.
Pia si hivyo tu, watu hawa wenye macho ya ‘bluu’ wamerithi pia mambo mengi kutoka kwa babu zao. Wana vitu vinavyofanana na babu zao na pia kutoka kwa baba zao. Kwa msingi huo utagundua watu hawa wenye macho ya ‘bluu’ mambo mengi warithi sana kutoka kwa baba au babu zao. 

MACHO RANGI YA MNG'AO (BRIGHT EYES)
5. Namna gani unavyoaminika.
Macho ulionayo yana uwezo wa kutuonyesha jinsi unavyoamika. Utafiti unaoyesha watu wengi wenye macho ya ‘brown’ ni watu wa kuaminika sana katika jamii kuliko watu wenye macho tofauti na hayo.
Hivyo basi, macho yako yanauwezo wa kubeba haiba, maumbile, uaminifu, maumivu na hata magonjwa. Hayo ndiyo mambo yanakuwa yamefichka mara kwa mara kwenye macho yetu.
Nikutakie siku njema sana na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio, 
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com





Jan 20, 2016

Mambo Ambayo Wengi Hujutia Katika Dakika Za Mwisho Za Maisha.

No comments :
Kwa waliofanya au wanaofanya kazi katika hospitali kwenye vitengo ambavyo wanaweza kuongea na kuonana na wagonjwa ambao wapo katika hali ya kukaribia kifo au walizidiwa na kushindikana kupona hivyo wanangojea kifo, wamejifunza mengi. Au kama umewahi kuwa karibu na mzee anayesubiri siku zake za mwisho kufika au mgonjwa ambaye anaumwa ugonjwa usiopona. Katika mahospitali au kwenye watu wazee wanaosubiria siku zipite, kuna mengi sana wanaweza kutufundisha kuhusiana na maisha. 
Leo tutaangalia mambo matano ambayo wengi hujutia katika dakika za mwisho kabla ya kifo. 
1. Natamani ningeishi maisha yangu kwa jinsi ninavyopenda mimi mwenyewe na sio kama watu wanavyonilazimisha niishi.
Hii ni mojawapo kati ya kauli ambayo wengi wanaokaribia kufa huzungumza. Ni kauli inayotamkwa na wengi. Katika maisha ya ujana kuelekea utu uzima wengi huishi maisha ambayo wanakuwa wamelazimishwa na marafiki, ndugu au wazazi. Wengine huishi maisha kuwafurahisha watu bila wao kupenda maisha hayo. Wengine huona raha kudanganya maisha wanayoyaishi na ikifika safari ya mwisho wa maisha hujutia sana kwa walipoteza muda wao kuishi maisha kwa jinsi watu wanavyotaka na sio kama wao wanavyotaka.

Kama unapenda kuwa daktrari kuwa daktari na sio uwe mtu wa aina nyingine wakati ndoto zako hazipo huko. Ishi katika ndoto zako na malengo yako. 

FURAHIA MAISHA NA FAMILIA YAKO.

2. Natamani nisingefanya majukumu na kazi nyingi kwa kujitesa sana na kukosa muda.
 Wengine hutumia muda mwingi katika maisha yao kufanya kazi na kuwa busy sana muda wote. Wengine husahau familia, marafiki na ndugu. Mwisho wa maisha ukifika unajutia kutumia maisha yako kuwa busy kila saa na kusahau kuyafurahia maisha kwa wakati mwingine na sio kujitesa katika majukumu tu.
Maisha yanahitaji usawa (balance). Kila kitu kina nafasi yake na umuhimu wake. Kimoja kuzidi sana huleta madhara. Ni vyema kuwa mtu wa kupangilia muda wako vyema katika kila jambo. 
3. Natamani ningekuwa na nafasi ya kuonyesha hisia zangu. 
Kuna watu wanajisahau kuonyesha au kuelezea hisia zao kwa ndugu, watu, familia na marafiki. Na inapofika dakika za mwisho za maisha mtu anaumia sana na anajuta ni kwanini hakutumia muda wake vyema kujali watu, kuonyesha upendo kwa maneno na vitendo.

Wakati ni kitu cha umuhimu sana katika maisha, hivyo inatufundisha ni vyema kujitahidi kutumia muda tulio nao kuonyesha hisia zetu kwa tunaowapenda na wanaotupenda. Kama kuna matatizo omba msamaha au toa maamuzi mazuri yatakayo saidia kusuluhisha matatizo na mwisho uweze kuishi kwa amani. 
4. Natamani ningekuwa karibu na familia na marafiki zangu. 
Wengi huonyesha kujali mtu pale akifariki. Marafiki wa zamani watakuja kukuaga, ndugu na watu wanaokufahamu. Lakini hivi sasa hakuna anayefanya hivyo. Kila mmoja ana shughuli zake, lakini katika dakika za mwisho au baada ya maisha kuisha wengi watajitokeza kuwa wanakujua na kukupendi, hivyo ndivyo wanadamu tulivyo. Wajali marafiki na ndugu zako. Tumia wakati huu vyema.

5. Natamani ningekuwa nimeipata furaha yangu ya Kweli. 
Wengi wanajisahau sana. Wengine wanaitafuta furaha kwa tamaa, mali, raha n.k. Mwisho ukifika wanajuta na kutamani wangeweza kuipata furaha ya daima. Furaha isiyoshikiliwa na mali, raha, thamani na anasa. Mpaka mwisho wa maisha ukifika unaanza kutambua kuwa kumbe furaha sio mali, raha, anasa, na tamaa. Bali furaha inatoka ndani mwako ukiweza kuishi kiusahihi na kuridhika na maisha na kushukuru kwa kila jambo.
Maisha ni YAKO. Hakuna mwingine anayeweza kukuchagulia maisha ya kuishi. Maamuzi unayoweka katika maisha yana adhari kwako na kwa watu wanaokuzunguka kwa kiasi fulani. Fanya maamuzi sahihi ya kimaisha, kuwa mkweli na nafsi yako. Amua kuwa na furaha hivi sasa.
 Makala hii imeandikwa na Apolinary Protas wa JITAMBUE SASA.