google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 31, 2016

Misingi Mitano (5) Unayotakiwa Kuifahamu, Ili Kujihakikishia Kipato Cha Kudumu.

No comments :
Kati ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi katika hii dunia ni pesa. pesa hiyo imeanza kutafutwa toka enzi za mababu na mababu mpaka leo. Juhudi za kutafuta pesa hadi kuipata zimekuwa ni kubwa sana kila kukicha. Kutokana na matokeo ya juhudi hizo, hiyo yote imekuwa ikitudhirishia au kutuonyesha kwamba kumbe pesa ni sehemu ya maisha yetu, tena maisha ya kila siku.
Lakini pamoja na juhudi kubwa za kuitafuta pesa hiyo bado lipo kundi kubwa la watu ambao wamejikuta wakiikosa pesa hiyo. Harakati zote za kuamka asubuhi na mapema na hata kuchelewa kulala kwa sababu ya pesa zimekuwa ni kama kazi bure kwa sababu hawaipati. Watu hawa wamekuwa  wakipishana na pesa karibu kila siku,utafikiri wao wanalaana na pesa hiyo hadi washindwe kuipata.
Hebu jaribu kuangalia kwenye eneo unaloishi jinsi pilika pilika za kutafuta pesa zilivyo nyingi. Lakini cha kushangaza pamoja na juhudi na pilika pilika hizo bado ni wachache wanaoipata pesa na kuwahakikishia kipato cha kudumu. Wengi wamekuwa wakitafuta sana pesa na kuishia maumivu na mateso ya kutokuipata. Sina shaka hali hii unaijua vizuri ya wengi kuendelea kukosa pesa ingawa wanaitafuta sana.
Kutokana na mazingira haya wapo ambao huanza kuamini wamelogwa. Na wengine pia huanza kuamini wana mikosi au laana. Je, kitu cha kujiuliza hizo ndizo huwa sababu halisi za wao kukosa pesa? Ukifatilia kimsingi, hizo sio sababu halisi za wao kukosa pesa, bali sababu hizo hutumika kama kisingizio. Watu hao kitu wasichokijua mara nyingi hushindwa kuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya kukosa misingi ya kuwaongoza.
Ndio. Naona unashangaa, inawezekana hata wewe ukawa kwenye wimbi la kutokuwa na kipato cha kudumu kwa sabau ya kukosa misingi ya kukuwezesha kuwa na kipato hicho. Kama unafikiria natania, kwa nini huna kipato cha uhakika na kudumu mpaka sasa? Nafikiri sasa, utakubaliana nami kwa kile ninachosema. Je, unajua misingi hiyo ni ipi unayotakiwa kuwa nyo ili kujihakikishia kipato cha kudumu?
1. Bajeti.
Hatua ya kwanza itayokuhakikishia wewe uwe na kupata cha kudumu ni kujijengea utaratibu wa kuwa na bajeti yako. Bajeti hiyo itakuongoza kujua pesa yako inatoka wapi na pesa yako inaenda wapi. Lakini  si hivyo tu, unapokuwa na bajeti inakusaidia pia kujua ni lini na wapi uweze kuwekeza pesa yako. Hivyo ni njia mojawapo muhimu sana ya kukuhakishia kipato cha kudumu kwenye biashara na maisha yako kwa ujumla.

Pesa unayopata hata kama ni kidogo, wekeza.
2. Kuwekeza.
Njia nyingine bora ya kukupa kipato cha kudumu ni kuifanya pesa yako ikuzalishie. Hakuna namna nyingine ya kuweza kuifanya pesa yako ikuzalishie zaidi ya kuweza. Kama una kitega uchumi kimoja, ongeza na kingine cha pili, cha tatu na kuendelea. Watu wenye mafanikio wana vipato vya kudumu kwa sababu wamewekeza katika maeneo mengi. Halikadhlika, nawe unatakiwa kufanya hivyo ili kuwa na kipato cha kudumu.
3. Kuweka akiba.
Kati ya kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni kujiwekea akiba. Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata, jifunze kuweka akiba. Akiba hiyo itakusaidia katika kuwekeza kwenye miradi mingine mingi baadae, lakini si hivyo tu pia ni njia mojawapo ya kukutengenezea kipato cha kudumu. Kama inatokea umeishiwa ni rahisi kuweza kuchukua pesa kwenye akiba yako kuliko kukopa kopa hovyo.
4. Kulipa madeni mapema.
Ni vyema ukajua mapema ili kujiweka salama katika safari yako ya mafanikio, jifunze kulipa madeni mapema. Unapokuwa unalipa madeni mapema inakusaidia sana kutokukuvurugia mambo yako mengi. Kama una mkopo benk au sehemu nyingine, lipa mapema ili uanze kuwa huru kutafuta pesa zako mwenyewe ambazo zitakupa uhuru mkubwa  wa kimafanikio. Kama unadaiwa kila wakati si rahisi sana kuendelea na kuwa na kipato cha uhakika.
5. Kuwa mjasiriamali mpambanaji.
Hautaweza kuwa huru kipesa na kujijengea kipato cha kudumu, kama leo hii hutaweza kuamua kuwa mjasiriamali mpambanaji. Amua kuwa mjasiriamali mpambanji unayetaka kutengeneza matokeo na sio mjasiriamali wa kulalamika kila siku. Hakuna mafanikio yanayoweza kuja au kupatikaa kwa kulalamika. Kama kuna changamoto zitatue na utafika mbali kimafanikio kipesa.
Kabla ya kuweka kalamu yangu chini, naomba utambue kwamba kama hutojiwekea misingi hiyo imara ya kipesa, suala la kupata pesa na kuwa na kipato cha kudumu litakusumbua sana. Usishangae ukawa mtu wa kufukuza pesa siku zote za maisha yako bila mafanikio. Zingatia hili sana na chukua hatua.
Ansante kwa kunifatilia na pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,

May 30, 2016

Usipokuwa Makini Na Mambo Haya, Yatakuzuia Sana Kufanikiwa.

No comments :
Ni matumaini ya tulio wengi ni kupata mafanikio kwa kila mambo ambayo tunayafanya, na ukichunguza kwa umakini  mara nyingi huwa hutapati kile ambacho tukitamani huku changamoto zikiwa nyingi kuliko mafanikio yenyewe. Huku wengine wakiamua hata kutumia njia zisizo rasmi katika kusaka mafanikio hayo na yote hufanyika kwa sababu ya tamaa iliyoko ndani ya mtu katika kutekeleza malengo yake. Na ukiendelea kufanya uchunguzi huo utakuja kugundua kuwa idadi kubwa ya watu hao huenda wasipate mafanikio hayo na kupoteza fedha nyingi zaidi ya kile wanachokitafuta.
Kwa kuwa mimi huwa naamini sana katika kufanya utafiti. Niliendelea kufanya utafiti ili kujua sababu zingine na vikwazo ambavyo mara kadhaa vimekuwa chanzo cha watu wengi kutokufanikiwa zaidi. Nakusihi ufuatane nami kwa kujifunza kupitia Makala haya mwanzo hadi mwisho.
Vifuatavyo ndivyo vikazo ambavyo vinasababisha watu wengi kutokufanikiwa.
1. Kutokujua pesa inafanya matumizi yapi.
Mara nyingi nimekuwa nikieleza kuhusu pesa, Pesa kwa sababu ndizo tunazozitafuta ili kupata mafanikio. Ila mambo yetu huwa hayawi kama tunavyotaka hii ni kutokana na kutokujua jinsi ya matumizi sahihi ya pesa kwa maneno mengine naweza sema kuwa hatuna nidhamu ya pesa. Kwa kuwa na maana hatujui pesa tunazopita zinatakiwa kutumika kwa utaratibu, ukitaka kubaini juu ya ukweli huu tofauti na daftari za kumbumbuku za biashara yako je una daftari inayohusu mapato na matumizi yanayohusu maisha yako binafsi na familia kwa ujumla?
Kama haupo katika misingi hiyo anza sasa kuwa na daftari ambalo utajaza kila kitu kinachohusiana na matumizi yako ya kifedha   na familia kwa ujumla. Pia kama una amini katika kujifunza kama mimi soma kitabu cha "rich dad, poor dad" kilichoandikwa na Robert Kayosaki ambacho kitakupa mwangaza zaidi juu matumizi sahihi ya kifedha.

Ipe thamani elmu yako itakufanikisha.
2. Kutoipa thamani elimu yako.
Hapa ndipo ambapo kunatufanya tuwe maskini zaidi. Mara nyingi mtu anashindwa kufanya kitu fulani kwa sababu hana elimu. Siwezi kulaumu sana maana tumeshakuta mifumo ambayo inatuambia msomi ni yule mwenye elimu ya chuo kikuu kwa maana shahada( degree) . Na kwa kuwa mifumo hiyo ndiyo ambayo tumeikuta na tumekuwa tukiamini hivyo. Na kwa kuwa imani ina nguvu basi tunajikuta wengi tunaamini hivyo. Na wale ambao kwa namna moja au nyingine hawana elimu hiyo ya chuo kikuu hujikuta wanafanya mambo ambayo siyo rasmi kama vile wizi, ukahaba na mengineyo mengi hii ni kwa sababu waliaminishwa ya kwamba elimu ni ufunguo wa maisha na kwa kuwa wao hawana elimu hiyo hujikuta wanafanya mambo ambayo sio ya kisomi.
Tatizo kubwa ambalo linasabisha yote hayo ni kutoipa thamani elimu iliyo nayo kwamba unaweza kufanya mapinduzi makubwa ya kimafanikio. Mtu anashindwa kufanya jambo fulani eti kwa kisingizio cha elimu aliyonayo. Mtu utamsikia si unajua niliishia darasa la saba au sikubahatika kumaliza elimu ya sekondari. Maneno hayo ni sumu kuliko ilivyo sumu ya panya katika swala zima la kimafanikio.
Hebu tuangalie watu wawili ambao ni uhakika unawafahamu sana. Yule tajiri ambaye ameamua kuilisha Tanzania kwa vyakula na vinywaji na kuuza ving'amuzi je elimu yake ni ipi?  Haya yule msanii anayetuwakilisha vizuri hasa katika kuitambulisha vizuri nchi yetu kimataifa je na yeye elimu yake ni kiasi gani? Usinipe majibu ila nikuombe uweze kufuatilia kwa umakini juu ya elimu zao ili kujua kwa undani ili kuipa thamani ya elimu uliyo nayo uone ni jinsi gani elimu hiyo uliyonayo inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimafanikio binafsi na jamii kwa ujumla.
Niweke nukta kwa kusema mafanikio makubwa yanakuja kama utaamini kile ulichonacho.
Nikutakie siku njema na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza.

Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
 E-mail; 
bensonchonya23@gmail.com

May 27, 2016

Aina Nne (4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako.

No comments :
Kila mmoja wetu bila shaka anaifahamu hofu aliyonayo. Zipo hofu zile ni za kawaida ambazo zipo ndani ya mtu na kila mmoja anayo. Kwa mfano mtoto akiwa peke yake mahali penye giza ni lazima aogope, pia ipo mifano mingine mingi kama hiyo. 
Lakini leo nataka tujadili aina zingine za hofu ambazo zinatengenezwa na watu wengine katika jamii zetu, pia zipo aina nyingine za hofu ambazo tunazitengeneza sisi wenyewe kutokana na vile tunavyoona mambo ambayo yanatuzunguka.
Hofu hizi ndizo zinazotuzuia kuwa na maisha mengine ya utofauti. Mwisho wa siku tunajikuta ni watu wa kuishi maisha ya vilevile kila wakati. Hata hivyo katika hali hiyo huenda ukawa unalaumu sana ukisema labda unashindwa kufanikiwa zaidi kwa sababu una changamoto ya pesa au sababu wewe ni yatima, mjane au umezaliwa katika familia maskini.
Inawezekana ya kwamba unaona ya kwamba Sababu hizo zina uzito sana na zimechangia wewe kuwa hapo ulipo. Ila ukweli ni kwamba moja ya chanzo kikubwa kilichosababisha wewe kuwa katika hali ya chini ni HOFU iliyopo ndani yako ambayo umeitengeza mwenyewe.
Zifuatazo ndizo aina za hofu zinazotufanya tushindwe kufikia malengo yetu.
1) Hofu ya kukoselewa.
Watu wengi wamebaki na maisha yale yale ya kila siku kwa sababu ya hofu hii ya kokosolewa. Watu wengi wamekata tamaa ya kuendelea kufanya jambo fulani kwa sababu ya kuna watu waliwakosoa kwa jambo ambalo walikuwa wanafanya. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wana kipaji cha kuimba na katika hilo wapo wengine hupeleka nyimbo zao stesheni mbalimbali za radio na pindi wanapoambiwa kuwa nyimbo zao ni mbaya huwa wanakata tamaa na hiyo ndiyo hofu ya kukosolewa.
Vivyo hivyo hata katika biashara watu wamekuwa wakiambiwa na watu wengine wamekuwa ya kwamba huwezi kufanya hivyo na kwa kuwa mtu anakuwa ana hofu hiyo ya kukosolewa ana amini na mwisho wa siku anaacha kufanya jambo fulani. Pia ikumbwe ya kwamba hii ndiyo sumu kubwa ambayo inaua ndoto za watu wengi sana. Ila kumbuka aina hii ya hofu ndiyo yenye mafanikio makubwa sana mbeleni.
Ondoa hofu ya kukosolewa, utafanikiwa.
2) Hofu ya kuzeeka na kufa.
Kuna baadhi ya watu wanataka mafanikio ya muda mfupi huku wakiwa na imani kubwa ndani yao kwamba Mafanikio ya muda wa kusaka mafanikio kwa muda mrefu haiwezekani kwa sababu inawezekana wakafariki au wakazeka. Mtu unamwambia matokeo ya jambo hili ni baada ya miaka ishirini kwa kuwa mtu huyo ana hofu atamsikia nikifa je? 
Mwingine anapoelezwa jambo hilo utamsikia anasema aaah nitakuwa nimezeeka. Kwa mifano hiyo utakuwa umegundua hofu hizo ni kwa jinsi gani umekuwa unahairisha kufanya mambo fulani ya kimafanikio huku ukihofia aina hizo za hofu. Ili kuondokana na hali hiyo daima kumbuka ishi kama utakufa kesho ila jifunze vitu vingi kama utaishi milele.
3) Hofu ya kushindwa.
Aina ya hofu hii imekuwa inatatesa wengi. Kimsingi ni kwamba kabla ya kuamua kufanya jambo fulani akili yako imekuwa inawaza juu ya jambo hilo. Ila kutokana na kuamua kwako kila ukiwaza juu ya utekelezaji wa jambo hilo unapata majibu mbalimbali ambayo yanakwambia hutaweza. Na kwakuwa unaona ya kwamba utekelezaji wake ni mgumu unaanza kuwaza kwamba jambo hilo ni gumu kwako.
Hivyo unaachana na kufanya  jambo hilo. Pia wapo baadhi ya watu wao huamini ya kwamba wao ni wa kushindwa tu kwa kuwa kila mara kadhaa wamekuwa wanafeli sana. Wito wangu kwako ni kwamba achana mara moja na hofu ya kushindwa amini wewe ni zaidi ya mshindi katika jambo lako.
 4) Hofu ya kuwasaidia wengine.
Tupo baadhi ya watu tumekuwa ni watu wa binafsi sana katika kuwasaidia wengine. Tumekuwa ni watu wakutofundisha watu wengine, huku tukiamini ya kwamba kufanya hivyo ni tutaibiwa mawazo yetu na sababu nyingine kama hizo, huku tukiamini kufanya hivyo ni kuwanufaisha wengine na kuzidi kuamini ya kwamba watatuzidi kiutalaamu. Ila nikwambie kumsaidia mwingine ni jambo jema sana pia kumbuka kuwa wewe ni origino hata akifanya hawezi kuwa kama wewe. Hivyo ni wakati wako muafaka wa kuua aina hiyo ya hofu na kuwasaidia wengine.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
Email;
 bensonchonya23@gmail.com

May 26, 2016

Tunaposhindwa Kulinda Tunachokipenda Huvuna Maumivu.

No comments :
Wazazi wana nafasi gani kwenye kutuamulia maisha yetu ya uhusiano? Jibu la swali hilo linategemea mambo mengi. Mojawapo ya mambo hayo ni malezi yetu, na namna tulivyopata nafasi ya kukua kiufahamu nje ya malezi. Lakini ukweli ni kwamba, wazazi wana nafasi ya ushauri tu, kuhusu maisha yetu ya uhusiano. Lakini kwa bahati mbaya, wazazi wengi hujipa nafasi kubwa na mamlaka zaidi na watoto wengi huwaruhusu wazazi wao kuchukua nafasi hiyo.
Hebu tuchukulie kwa mfano mzazi ambaye anamkatalia mtoto wake wa kiume asimuoe binti aliye nyumba ya tatu kwa sababu ya kuona tu binti yule ni mfanyakazi wa ndani. Kwa tafsiri ya haraka haraka mzazi huyu anakuwa amemwona binti yule kama nusu mtu na asiyefaa kitu. Naye mtoto wa kiume pengine kwa kusikiliza ushauri wa mzazi anaweza kukubali lakini baadae inaweza ikawa majuto kwake ikiwa ataoa mwanamke ambaye atamtesa ingawa kiuhalisia anakuwa ametoka familia tajiri.
Lakini pia huwa inatokea sana kwa wazazi wanapoona mtoto wao awe wa kike au kiume akiwa amependana na mtu ‘choka mbaya kimaisha’ kwa wengi huwa sio rahisi kukubali mahusiano hayo na kujikuta kuweka vizuizi vingi sana kwa watoto ili wasiweze kuoana. Hapa watoto wasipokuwa makini hujikuta wamekubali walichoelezwa na wazazi wao na matokeo yake hujikuta kwa pande zote mbili kujuta kutokana na kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo sahihi.

Linda unachokipenda, kisipotee.
Hali kama hizi zipo sana katika jamii zetu. Kuna wengi ambao ndoa zao zinaingiliwa sana na wazazi au hata ndugu zetu na pengine tu hata marafiki zetu na kujikuta hata kukosa uhuru. Hali kama hii inapokutokea na ukajikuta umekosa uhuru wa kuonyesha ukakamavu wa kuonyesha kile unachotaka kwenye mahusiano au ndoa yako utaumia sana. Utahisi dunia sio sehemu salama kwako kwa sababu ya kuhisi kama ndugu wanakuonea kila wakati. Kama hili limewahi kukutokea pole sana.
Naamini umeshawahi kusikia mikasa kama hii ya kuingiliwa kwenye mahusiano. Wengi wetu mara nyingi tunafundishwa namna ya kuishi na wake au waume zetu, kama tuendelee kuwa nao au tuwaache. Huwa tunawasikiliza wazazi, ndugu au marafiki na kuvunja uhusiano. Baadaye, kwa maumivu makubwa tunakuja kubaini makosa tuliyoyafanya. Tunajaribu kuunga palipokatika. Huwa inawezekana, ingawa mara nyingi haiwezekani tena.
Unaweza ukasambaratishwa kwenye mahusiano au ndoa yako na ndugu zako pasipo kujua na matokeo yake kuleta majuto makubwa sana. Na majuto hayo unaweza ukaendelea kuamini pengine ungedumu kwenye uhusiano wako wa mwanzo ungekuwa upo salama kimafanikio na kindoa pia. Lakini ulipo ‘moto’ umewaka kutokana na kwamba upo sehemu ambayo siyo sahihi. Ni kitu ambacho kina uwezo wa kukuuma sana siku zote na ukajikuta umeharibu kila kitu ikiwa pamoja na mafanikio sababu ya uhusiano.
Kumbuka kwamba, wewe ndiye unayetakiwa kusema na kuamini kwamba, umempenda fulani. Wewe ndiye unayetakiwa kulinda uhusiano wako kwa msimamo wa hali ya juu. Wengine wanakuwa wana uhuru wa kutoa maoni kuhusu penzi au mpenzi wako, lakini hawana ruhusa au nafasi ya kuamua kuhusu hatma ya penzi lako. Ikiwa kwa namna moja au nyingine utashindwa kulinda kikamilifu kile unachokipenda, elewa utavuna maumivu tena makubwa sana.
Tunakutakia mafanikio mema katika ndoa na maisha. Pia endelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,


May 25, 2016

Tabia Tatu (3) Muhimu Unazotakiwa Kuziendeleza, Ili Kufanikiwa.

No comments :
Mafanikio ni matokeo ya tabia nzuri ambazo unaziendeleza katika maisha yako karibu kila siku. Tabia hizi chanya ama unazoziendeleza na kuzifanya kuwa zako,  ndizo zinazokupa mafanikio. Hivyo, kwa mtu yeyote anayesaka mafanikio ni lazima kwake kuendeleza tabia bora za kimafanikio ili kufanikiwa.
Watu wenye mafanikio wanatambua ukweli huu kuwa mafanikio ni tabia. Na kutokana na kuujua ukweli huu unaowapa mafanikio, huamua kufanyia kazi ukweli huu karibu kila siku. Lakini kwa kusoma makala haya, utajua tabia tatu muhimu unazotakiwa kuziendeleza ili kufanikiwa. Ni tabia ambazo watu wenye mafanikio huzitumia pia kufanikiwa.
1. Tabia ya utendaji.
Haijalishi una mipango au malengo mazuri vipi, kama hakuna utendaji hiyo itakuwa ni sawa na kazi bure. Kuwa mtendaji wa jambo ulilolipanga, ni njia mojawapo bora ya kukupeleka kwenye mafanikio. Mara nyingi wengi huwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kuwa waongeaji sana kwenye mambo yao.
Mbinu nzuri ya kufanikiwa kwenye mambo yako ni kujifunnza kuwa mtendaji. Wakati wengine wanapiga mdomo kwamba watafanya jambo hili kesho au mwezi ujao, wewe tafuta namna ya kulifanya hata kwa kidogo. Watu wote wenye mafanikio ni watendaji. Ukijifunza kuiendeleza tabia hii, uwe na uhakika utafanikiwa.


2. Tabia ya kuanza na kidogo ulichonacho.
Mbali na kuwa mtendaji pia, unatakiwa kujifunza kuanza na kile kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu kikamilike, anza na kile ulichonacho. Hata kama kitu hicho unakiona ni kidogo anza nacho hicho, baada ya muda fulani kitakuwa kikubwa. Jambo la kuzingatia hapa unapoaza na kidogo ni kuhakikisha unanidhamu ya kutosha na kukitunza.
Kwa mfano inawezekana ukawa unataka kuanza biashara ya mtaji wa milioni tano na wewe una milioni moja mkononi, acha kusubiri sana. Unaweza ukaanza na pesa yako hiyo kwa kufanya biashara ndogo ndogo na ukajikuta unakuza mtaji wako hadi pale unapotaka kufika. Kuanza na kidogo ulichonacho ni mbinu mojawapo nzuri ya kukufanikisha.
3. Tabia ya uzingativu.
Ili uweze kufanikiwa ni muhimu sana kuweka nguvu za uzingativu kwa kile unachofanya. Kama nguvu zako utakuwa unazipeleka na kuamua kuzingatia kila jambo ni wazi hutaweza kufanikiwa. Siri ya mafanikio yako ipo kwenye kuzingatia mambo machache, ikiwezekana jambo moja  lenye kukupa mafanikio makubwa.
Katika maisha yako, unaweza ukajikuta upo kwenye wakati mgumu pengine hufanikiwi kwa sababu ya kukosa uzingativu. Wengi huwa wanajikuta hawafanikiwi kwenye maisha kwa sababu hii. Utakuta ni watu wa kujaribu kutaka karibu kila kitu, matokeo yake kunakuwa hakuna kitu kikubwa walichokifanikisha.
Kwa kumalizia makala haya, nifupishe kwa kusema hivi, tabia ya utendaji, kuanza na kidogo ulichonacho na uzingativu ni moja ya tabia muhimu ambazo unatakiwa kuzizingatia kila wakati ili uweze kufanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio yako na endelea kuweka nguvu katika kujifunza kupia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,


May 24, 2016

Athari Za Kuwa Na Mipango Mingi Kwa Wakati Mmoja.

No comments :
Moja ya changamoto kubwa ya kushindwa kufanikiwa ni kutokujua unataka nini katika Maisha yako. Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikueleweshe, ni hivi unakuta mtu anaona maisha hayaendi vizuri mwisho wa siku ukimuuliza mtu huyo anataka kufanya nini, bila shaka kwa kuwa mtu huyo hajui kile anachokitaka atakwambia kazi yeyote ile mimi nafanya. 
Ukiangalia juu ya kauli hiyo ni sawa, mtu huyo huenda akawa sawa hii ni kutokana na hali yake aliyonayo. Lakini katika kununi ya kimafanikio hakuna majibu ya kusema unataka kufanya chochote kile. Ila ni lazima ujue unataka kufanya nini. Moja ya majonzi ya watu waliofeli kimaisha ni kwamba walichanganya vitu vingi kwa wakati mmoja.
Tujifunze kitu kupitia hadithi ifuatavyo.
Hapo zamani za kale kulikuwepo na mfugaji fulani katika kijiji fulani. Na mfugaji huyo alijipatia umaarufu mkubwa sana kijinini hapo hii ni  kutokana alivyobobea katika shughuli hiyo, na kutokana na umaarufu huo aliweza kulinda heshima ya jina lake na kuongeza idadi kubwa ya mifugo. 

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na mifugo ilivyozidi kuongezeka miaka na miaka, hata hivyo kama ilivyo kwa jongoo kuwa na miguu mingi bila macho ni sawa na bure hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mfugaji huyo kutokana na ufugaji hakutaka hata siku moja kumuuza hata mnyama mmoja kwa sababu aliweka malengo yake ya muda mrefu na kuamini ipo siku atakuja kuwa na pesa nyingi na kuwa tajiri mkubwa zaidi kijijini hapo.

Acha kuwa na tamaa na mipango mingi, itakukwamisha.
Hata hivyo kutokana imani hiyo aliyokuwa nayo furaha na umarufu uligeuka kilio na majonzi hasa pale ulipo ingia ugonjwa wa bonde la ufa (Rift valley) kijijini hapo. Ugonjwa huo uliweza kuangamiza idadi kubwa ya wanyama aliowamiliki mpaka akabakiwa na ng'ombe mmoja.
Mfugaji alinung'unika sana lakini alimbidi akubaline na hali hiyo ambayo imetokea. Hivyo akaamua kumuhudumia yule ng'ombe kama mtoto wake kwani kila alichokihitaji ng'ombe yule alikipata kutoka kwa mfugaji huyo. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya mfugaji na ng'ombe yalivyokuwa.
Siku moja alfajiri mfugaji aliamua kwenda na ng'ombe wake sehemu ambayo ng'ombe yule alikunywa maji kama ilivyokuwa ratiba ya mfugaji yule kila siku. Wakati wanaelekea katika eneo hilo ghafla mbele aliona kiatu, kiatu ambacho kilikuwa ni kizuri sana, aliamua kukichukua kiatu kile na kukiangalia na kuona kinamtosha vizuri baadae ilishangaa mbona kiatu kizuri kiasi kilikuwepo pale barabarani wakati anajiuliza hayo aling'aza macho yake huku na huko lakini hakuona kiatu kingine cha mguu mwingine. 

Kwa kuwa hakuona kiatu kingine aliamua kuachana na kiatu kile na kuondoka na ng'ombe wake. Mfugaji aliendelea na safari yake kwa mwendo mrefu sana lakini kadri alivyozidi kwenda ghafla alikutana na kiatu kingine cha mguu mwingine ambacho kinafanana na kile alichokiacha awali. Mfugaji alifurahi sana hivyo alimua akiache kiatu kile cha pili pamoja na ng'ombe mahali pale na kurudi kwa kasi sana kwenda kuchukua kiatu kingine.
Lakini cha ajabu kilichomkuta ni kwamba baada ya kwenda mahali pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukiona kiatu kile, alijaribu kukitafuta sana kiatu kile lakini hakukipata hivyo aliamua kurudi mwanzo ambako aliamuacha ng'ombe na kiatu cha pili lakini cha kushanganza ni kwamba hata huko hakumkuta ng'ombe wala kiatu kile. Mfugaji alilia sana kwa sababu alimpoteza ng'ombe wake ambaye alibaki mmoja na aliyempenda sana. Mwisho wa siku alikosa vyote.
TAFSIRI YA HADITHI HII NI NINI?
Tafsiri ya hadithi hii ni kwamba watu wengi ni wazuri wa kimawazo na kuchangamkia fursa mbalimbali ila changamoto kubwa inakuja hasa pale ambapo unataka mafanikio ya haraka hivyo unajikuta unaingia katika sakata la kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja. Mwisho wa siku unajikuta unafanya kitu hiki unaacha mara unafanya kitu kingene kama alivyofanya mfugaji na mwisho wa siku akajikuta anakosa yote. Hivyo ni wakati muafaka leo wa kujua unataka kufanya nini na kukimalisha na sio kuwa na maisha yakutaka mambo mengi kwa pupa pupa na mwisho kukosa vyote. Kuwa mtu chanya ili kupata mafanikio ya kweli.
Nukuu ya Leo inasema; Ukijua kilichomo ndani yako wewe ni tajiri.
Mwandishi ni afisa mipango ;Benson chonya.
Facebook; Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail: 
bensonchonya23@gmail.com

May 23, 2016

Mambo Ya Msingi Kuhusu Mafanikio Unayotakiwa Kuyajua.

No comments :
Ili uweze kufanikiwa kwa jambo lolote, ni lazima uwe na msingi imara wa jambo hilo kwanza. Pasipo kuwa na misingi imara utasumbuka sana katika kufikia mafanikio kwa kile unachokifanya. Lakini hiyo haitoshi unatakiwa pia kulielewa kwa mapana zaidi jambo unalolifanya ili likufanikishe. Hata kwenye maisha yako binafsi, huwezi kufanikiwa kama hujui mafanikio ni nini kwako au yanataka nini.
Wengi kwa sababu ya kutokujua hili hujikuta wakisaka mafanikio kwa muda mrefu na kuambulia patupu. Kama unataka kufanikiwa kweli, kuanzia leo anza safari yako ya mafanikio kwa kuyapata mtazamo chanya wa kitofauti. Ni lazima ujue mambo ya msingi yanayohusu mafanikio ili uweze kufaniwa na kuwa mtu wa tofauti. Acha kun’gang’ania kukaa kwenye umaskini, toka hapo na uufuate utajiri.
Karibu sana na twende pamoja kujifunza mambo ya msingi yanayohusu mafanikio.
Mafanikio ni hatua.
Hakuna ambaye amewahi kulala na kuamka asubuhi akiwa tajiri. Hakuna ambaye aliyeweka juhudi kubwa kwa muda mfupi halafu akawa tajiri. Hakuna mafanikio ambayo yanapatikana kwa muda mfupi. mafanikio yote unayoyajua wewe yanatengenezwa kwa hatua. Ndio, mafanikio ni matokeo ya kupiga hatua kwa hatua kila siku.
Usitishike na kuona mafanikio makubwa ya watu ukafikiri walianzia hapo walipo. Kama unawaza hivyo, unajidanganya. Mafanikio yao yalijengwa kidogo kidogo, siku kwa siku na hata miaka. Ikiwa unataka kufika huko waliko acha kukurupuka. Jipange na anza kuelekea kwenye mafanikio yako hatua kwa hatua. Baada ya miaka michache utakuwa mbali sana.

Mafanikio ni hatua kwa hatua, usikate tamaa.
Mafanikio ni kujitoa.
Siku zote mafanikio ni kujitoa tena kwa moyo wote. Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata kama haupo tayari kujitoa. Iwe unataka au hutaki ni lazima ujitoe na kukubali kupoteza baadhi ya vitu ili uweze kufanikiwa. Upo wakati ambapo ni lazima utapoteza marafiki, muda wako, pesa kwa ajili ya mafanikio.
Yanapotokea hayo yote usijali sana, kwani kumbuka kama nilivyosema mafanikio yanahitaji kujitoa. Kwa wale rafiki zangu ambao wanataka mafanikio lakini wakati huo huo hawako tayari kupoteza baadhi ya vitu ili kufanikiwa, huwa  sio rahisi kwao kufanikiwa. Ili kufanikiwa unahitaji kujitoa mhanga kwa mambo mengi sana ikiwemo pamoja na kuwa mgumu kwenye mambo yako. Bila kujitoa kikamilifu mafanikio utayasikia kwa wengine.

Soma; Tabia Zinazoua Ndoto Na Mafanikio Ya Wengi.
Mafanikio ni uchaguzi.
Kila siku katika maisha yetu huwa tuna chaguzi nyingi ambazo tunazifanya. Kwa mfano huwa ni watu wa kuchagua chakula tunachokula. Huwa ni watu wa kuchagua mavazi, njia na mambo chungu nzima yanayofanana na hayo. Halikadhalika, na mafanikio unayoyatafuta nayo ni uchaguzi. Ni lazima uchague kufanikiwa ili ufanikiwe bila kufanya hivyo, hutafanikiwa.
Kwa bahati mbaya wengi huwa hatuna uchaguzi na maisha ya kimafanikio tunayoyataka. Kwa mfano nikuulize wewe, umeshawahi kujiuliza unataka kufanikiwa kwa viwango vipi? Usitoe macho tu, ulishawahi kujiuliza hivyo? Kama huwa unajiambia nataka tu kufanikiwa, lakini hujui kwa viwango vipi ni sawa na kama hujafanya uchaguzi kabisa. Fanya uchaguzi sahihi wa kufanikiwa kwako na ujue unataka kufika wapi na kwa muda upi?
Mafanikio ni kuona fursa.
Ili ufanikiwe ni lazima utumie kila aina ya fursa inayokuja mikononi mwako vizuri. Lakini hiyo haitoshi, kama huna uwezo wa kuona fursa za kukusaidia kufanikiwa pia hutaweza kufanikiwa. Ni muhimu sana kuzijua fursa ambazo unatakiwa uzitumie ili kufanikiwa. Bila kufanya hivyo utahangaika sana kutafuta mafanikio bila kuambulia kitu.
Watu wanaopata mafanikio mazuri kwenye maisha yao, siku zote wanatumia fursa. Ni jambo ambalo kwa sasa unatakiwa kulijua na kulizingatia vizuri sana kichwani mwako kwamba mafanikio pia huwa yanakuja kwa kuona na kutumia  fursa vizuri. Ikiwa utakuwa unaona na kutumia fursa vizuri kila wakati, uwe na uhakika hakuna wa kukuzuia kufanikiwa.

Soma; Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Bilionea Bill Gates.
Mafanikio ni kutatua matatizo.
Katika safari ya mafanikio wakati mwingine inakuwa ni safari yenye kila aina ya vizuizi. Na wakati mwingine kutokana na vizuizi hivi hutufanya tuumie na hata kulia. Sasa ili uweze kufanikiwa unapaswa kutambua pia mafanikio wakati mwingine ni ule uwezo wa kutatua matatizo. Kwa kadri unavyotatua matatizo ndivyo ambavyo unajikuta unazidi kufanikiwa.
Kama unafikiri natania mafanikio sio kutatua fursa, kuanzia leo anza kutatatua matatizo yaliyo katika kijiji chako au eneo unaloishi. Kwa kutatua matatizo hayo utajikuta ukijipatia pesa kwa wingi sana. Hiyo yote inadhihirisha kwamba mafanikio ni kutatua matatizo. Jifunze juu ya hili na tatua matatizo muhimu kwenye jamii na hakika utafanikiwa.
Mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii.
Hakuna ubishi wowote ili uweze kufanikiwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii. Kama ulikuwa huna mtazamo huu mwanzoni unalazimika kuwa nao na kujua kwamba mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii zote. Hakuna lelemama katika kutafuta mafanikio. Unatakiwa kujituma sana tena sana kila siku ili ufanikiwe. Vinginevyo usipozingatia hili hutaweza kufanikiwa.
Kwa kuhitimisha makala hii, nifupishe kwa kusema mafanikio ni hatua, mafanikio ni kujitoa, mafanikio ni uchaguzi, mafanikio ni fursa, mafanikio ni kutatua matatizo ya jamii na mafanikio pia ni kufanya kazi kwa bidii. Kwa kujua mambo haya yatakusaidia sana kujiwekea mtazamo tofauti juu ya mafanikio ambao utakupa msukumo mkubwa wa kuweza kusonga mbele na kufanikiwa.
Ansante kwa kuwa nami na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,

May 20, 2016

Mfumo Bora Utakao Badili Maisha na Biashara Yako.

No comments :
Kila utayekutana leo endapo utamuuliza unapenda nini katika maisha yako? Jibu ambalo atakupa bila shaka litakuwa linahusiana na masuala ya mafanikio na endapo utakutana na mtu ambaye majibu yake yatakuwa ni  kinyume na  mafanikio ni lazima utabaki unamshangaa huyu mwenzangu vipi? .
Bila shaka idadi ya watu wengi ni kuona kila mmoja anapata mafanikio ila tatizo ni pale linapokuja suala zima unapataje Mafanikio hayo. Tulio wengi ni wazuri wa kunuia (kusema ) kuliko kujua tunapaje Mafanikio hayo.

Leo niamua kuwaza kwa sauti hata wewe mwenzangu usikie nilichokiwaza ili uweze kupata mafanikio hayo na sio kuishia kusema nataka kile bila hata kujua utakipata vipi.

Zifuatazo ndizo mbinu zitakazobadili mfumo wa Maisha yako;


1. Usijadili vitu kwa macho.

Katika safari ya kuelekea au kupata mafanikio hakuhitaji kuvitazama tu vitu bali ni lazima ufanye uchunguzi wa kutosha. Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule hasa somo la hesabu wengi wetu tulikuwa tukiyatazama maswali tulikuwa tunasema haya yameisha kwa maana ya kwamba uhakika wa kupata majibu ya maswali hayo upo wazi, lakini kinyume chache baada ya kusema hivyo tulikuwa tunakosa na kufeli somo hilo kwa sababu tulikuwa wazuri sana wakuona na kusema kuliko kutenda.

Jaza kichwa chako mawazo chanya.
Mfano huu ndivyo unavyoendelea mpaka leo hii kwa watu wanaotaka kupata mafanikio. Wengi wao hutumia macho tu na kujipa majibu kwamba watafanikiwa. Kwa mfano mtu anataka kufungua biashara mahali fulani kwa kuwa anatumia macho peke yake katika kuona, anaona wafanyabiahara wengine wanafanikiwa na yeye kwa kutumia uzoefu wake wa kuona tu hujikuta na yeye kaanza biashara mara moja.

Lakini inapotokea pale mtu huyo ambapo biashara hiyo haitakwenda vizuri utamsikia mtu huyo anasema karogwa ila ukweli hakuna atakayekuwa amekuroga zaidi ya kujiroga mwenyewe. Pia daima kumbuka kuona peke yake haitoshi bali uchunguzi wa kina huhitajika kwa jambo ambalo unataka kulifanya.

2. Kujaza kichwa chako mawazo chanya.

Mawazo chanya ni mawazo yatakayokufanya uweze kutoka hatua moja hadi nyingine ya kimafanikio. Swali dogo la kujiuliza kabla siku mpya haijaisha, je huwa unajiuliza ni mawazo gani chanya ambayo umewaza kutwa nzima? Na umeyachukulia hatua kwa kiasi gani? Na kama umechukulia hatua yana uwezo gani wa kubadili maisha na kinyume chake ni vipi.


Nikumbushe tu ya kwamba moja ya sifa ya watu wenye mawazo chanya kwa kile ambacho anakiwaza hukiandika katika kumbukumbu huku utekelezaji ukisubiri kuanza mara moja. Mawazo chanya ndiyo ambayo humbadilisha mtu siku zote na mawazo hasi ndiyo ambayo yamekuwa yakiwafanya watu waishi mawazo ya umaskini kila siku.


Mara nyingi mtu huanza kuwaza maamuzi mazuri ila namna ya kutekeza ndiyo huja mawazo hasi ya utekelezaji, Kwa mfano mtu anawaza kuwa mfanyabiashara mkubwa wa maduka ya nguo ndio hayo ni mawazo chanya lakini mawazo ya utekelezaji jambo hilo yanakuja mawazo mabaya kama vile tumia njia za kishirikiana hapo utafanikiwa. Baada ya hapo kwa kuwa mtu huyo baadala ya yeye kuiongoza akili yake ila yeye anaongozwa na akili yake mwisho wa siku anaingia katika kutekeza jambo lake kwa njia zisiso rasmi na mwisho wa siku anakuwa maskini maisha yake . Badili mtazamo na waza chanya ama hakika utafanikiwa.

Nukuu  ya leo inasema ; Hakuna Binadamu aliyeletwa duniani kuzurura.

Imeandikwa na Afisa Mipango; Benson Chonya.
Simu ;0757-909942
E-mail:
bensonchonya23@gmail com

May 19, 2016

Kupinduana Kwenye Ndoa Hutokea Sana.

No comments :
Unapoishi nyumbani na ndugu yako, jamaa yako na hata mtumishi wa kike, ni vizuri ukajitahidi kulinda ndoa yako. Kumbuka kwamba, wanaume hawajali sana hisia, bali hujali zaidi mwili. Kama ukimwachia jamaa yako, ndugu yako au rafiki yako kumzoea sana mumeo, jua tu kwamba, inawezekana unajitengenezea maumivu makubwa sana hapo baadae.
Tafiti zinathibitisha sasa kwamba, mwanamume anapohisi kuwa mwanamke fulani anamwonesha kwamba, yeye ni mwanaume kwelikweli, anapoonesha kwamba, anatambua uwepo wake na mchango wake katika familia, mwanaume huanza kumpenda, bila kujali sura au hadhi.
Kama ndugu yako ni mjuaji wa mambo haya, anaweza kumwonyesha mumeo kwamba, anaamini kuwa ni mwanamume kwelikweli. Hii hufanyika kwa kumsifu, kutokupingana naye, kumpongeza mara kwa mara na kumwosha kwamba, anaamini katika yeye.
Hata wale watumishi wa ndani, wanaochukuliwa na wanaume za watu hawafanyi hivyo kwa sababu, ati hao watumishi ni wazuri sana wa sura au wanajua sana mapenzi, hapana.

Kuwa makini na ndoa yako.
Wanaume huwachukua kwa sababu, wake au wapenzi wa wanaume hao, wameshindwa wajibu wao, wameshindwa kujua kwamba, wanaume hutazama uhusiano kwa jicho tofauti.
Lakini, iwe ndugu zetu au jamaa zetu na hata watumishi majumbani mwetu, bado na wao ni binadamu, wana udhaifu. Kwa udhaifu wao, pamoja na udhaifu wa wanaume au wapenzi wetu, wanaweza kutusaliti. Kwa hiyo ni juu yetu kulinda ndoa zetu, ili udhaifu huo usiwe chanzo cha kuvunjika kwa matumaini na matarajio yetu ya kujenga familia.
Kuna mambo mawili makubwa hapa. Kwanza, inawezekana tumejiachia sana kama wanawake na kusahau kuwa wanaume huvutiwa na mambo gani. Kwa hali hiyo, tunawaacha wale waliokaribu nao kuwafanyia yale wanayohitaji na kuchukua nafasi zetu..
Lakini pili, ni udhaifu wa kibinadamu na zaidi kwa wanaume, linapokuja suala la mwili. Kwa udhaifu huo, inabidi tuwasaidie kuwalinda ili wasishawishiwe kiurahisi. Lakini, ndugu zetu wa kike au watumishi tunaoishi nao, inabidi tuwakague vizuri na kuacha kuwaamini kupita kiasi kwa wanaume au wapenzi wetu.
Ni hatari sana kwa mwanamke kwa mfano, kumwambia au kumruhusu mumewe aende sehemu za starehe na rafiki yake wa kike au na ndugu yake wa kike, ati kwa sababu anamwamini rafiki huyo au mumewe. Kumbuka, suala hapa siyo kuaminika, bali ukweli wa kiimaumbile pia. Chunga ndoa yako, ilinde sana, kwani siyo dhambi kufanya hivyo.
Nakutakia siku njema na Baraka katika ndoa yako.
Makala hii imeandaliwa na Devotha Kauki. Unaweza kuwasiliana na mwandishi kwa dvkauki@gmail.com




May 18, 2016

Kweli Nne (4) Kuhusu Mafanikio, Ambazo Hutakiwi Kuzisahau.

No comments :
Ili uweze kufanikiwa ni lazima uzijue kweli zenye uwezo wa kukupa mafanikio. Haijalishi unafanya nini, ukizijua kweli, kanuni au mbinu zinazotoa mafanikio ni lazima ufanikiwe. Hivyo haitajalisha una historia gani au unatoka katika taifa ama familia gani kufanikiwa kwako kutakuwa ni lazima ukielewa kweli au kanuni hizo. Mara nyingi watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kushindwa kuzijua kweli hizo.
Sipendi uwe miongoni mwao ukashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutokujua mafanikio yanataka nini. Kwa kusoma makala haya, nitakushirikisha kweli ambazo unatakiwa kuzijua ili uweze kufanikiwa. Ni kweli ambazo zinatumiwa na wengi ikiwemo mpaka na watu wenye mafanikio makubwa. Hakuna ubishi ukijua kweli hizi na kuzifanyia kazi, nafasi ya kufanikiwa kwako itakuwa ni kubwa. Je, kweli hizo ni zipi?
1. Maisha yako yanakutegemea kwa asilimia zote.
Ukitaka kufanikiwa kwa viwango vikubwa, elewa kabisa kwamba maisha yako yanakutegemea wewe kwa asilimia zote. Acha kutegemea kitu au chochote kilicho nje ya maisha yako, wewe ndiye unayewajibika katika maisha yako kwa asilimia zote. Hata inapotokea pengine umekosea acha kusukumia makosa hayo kwa wengine, jifunze kutambua wewe ndiye chanzo.
Kwa kuwa umeshajua maisha yako yanakutegemea wewe, acha kubeba visingizio vinavyokuzuia kufanikiwa. Sahau juu ya habari ya wazazi wako eti kwamba ooh hawakuweza kukusomesha, sahau kila kitu. Wajibu wa maisha yako, unao wewe. Tenda kazi zako kwa nguvu zote huku ukiamini mtu pekee wa kubadilisha maisha yako ni wewe. Huu ni ukweli ambao kamwe hupaswi kuusahau kwenye maisha ya mafanikio.

Wewe ni mshindi.
2. Mawazo yako ni kila kitu.
Mawazo uliyonayo ndiyo yanayaoamua maisha yako yawe vipi. Upo hapo kimaisha ni kwa sababu ya mawazo ambayo ulikuwa nayo siku za nyuma. Kwa hiyo, sisi ni matokeo ya fikra au mawazo tuliyonayo. Mawazo yetu ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio kitu kingine. Hivyo kwa kujua hili ni muhimu sana kuwa makini na kile unachokiwaza kwa sababu utakivuna, haijalishi kiwe kibaya au kizuri.
Kila siku jifunze kufikiri mawazo chanya. Fikiria yale mambo ambayo unataka yakutokee. Acha kufikiria yale usiyataka utayapata. Mawazo yako hayatakudanganya, utavuna kile unachofikiria. Kumbuka kama nilivyoanza kwa kusema, upo hivyo kwa sababu ya mawazo uliyonayo. Kwa kulijua hili, itakusaidia kuwa makini na kile unachokiwaza.
3. Una uwezo mkubwa wa kupata chochote, ukiamua.
Kweli nyingine ambayo hutakiwi kuisahau katika maisha yako ni kwamba, una uwezo wa kupata chochote ikiwa utaamua. Kama utaamua kuwa na mafanikio makubwa, utayapata. Kama utaamua kuwa mwanamziki, mwandishi au kitu kingine chochote, unauwezo wa kukipata pia. Kitu cha msingi ili kukipata hicho unachokitaka ni lazima ujitoe kwanza.
Hakuna ajali kwenye mafanikio. Upo hivyo pia kwa sababu ya maamuzi yako uliyoyafanya. Kama kuna kitu chochote unachokitaka, fanya maamuzi  na kisha chukua hatua. Uwezo wa kufanikisha chochote katika maisha yako, unao.
4. Una nguvu kubwa zilizo ndani yako.
Fanya kazi kwa ubora na juhudi zako zote huku ukiamini nguvu kubwa ambazo unazo ndani yako. Unao uwezo mkubwa wa kufanikisha jambo lolote ulio ndani yako. Lakini kwa bahati wengi wetu ni watu wa kutumia nguvu zilizo chini ya viwango vyetu. Ukijua uwezo ulionao na ukaamua kuutumia, utafanikiwa sana. Huu ni moja ya ukweli unaotakiwa kuujua kuhusu mafanikio na kukubali kutumia.
Utafika kwenye mafanikio makubwa ikiwa utaamua kuzitumia kweli hizo, kukusaidia kufanikiwa.
Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki,

Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,



May 17, 2016

Njia Tano (5) Bora Za Kukuza Biashara Yako.

No comments :
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wafanyabiashara walio wengi ni kutokujua kiundani juu ya biashara zao. Kutokana na changamoto hiyo ya kutokujua kiundani biashara zao, wafanyabiashara hao walio wengi hujikuta biashara zao huwa haziwi za muda mrefu na hata pale zinapokuwa za muda mrefu huwa hazikui.

Naamini kwa kuwa lengo lako ni kukuza biashara, ni vyema kwa kupitia makala haya, ukafahamu pia baadhi ya mambo muhimu yatakayokusaidia kukuza hata biashara yako. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na maisha marefu na yenye kukua siku hadi siku.

1.  Ongeza maarifa kwa kujifunza.

Kama kweli unahitaji mafanikio zaidi ya kiabiashara ni vyema ukawa ni mtu wa kujifunza kuhusiana na biashara yako. Ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wafanyabiashara wengine kufanikiwa. Kujifunza huku kukupe muda muafaka wakugundua pale ambapo wafanyabiashara wengine wanashndwa. Baada ya kujua wanashindwa wapi kwako ifanye kama fursa ya kuboresha biashara yako. Kufanya hivyo kutakufanya uongeze wateja kwani utakuwa mbunifu zaidi.

Acha kuridhika na hali uliyonayo.
2. Badili tabia zako.

Moja ya chachu nzuri ya kukufanya ukue kibiashara ni lazima uweze kujua vizuri tabia yako. Inawezekana wewe unajiona upo sawa ila kumbe sivyo unavyofikiri. Hata hivyo ili kuweza kujua ni ipi tabia yako ni vyema ukafanya uchunguzi ili kujua watu wanakuzungumziaje wewe? Kufanya hivyo kutasaidia kwa sababu watu wengine ndio wana picha kamili juu ya wewe na biashara kwa ujumla. Pia ili kuweza kufanikiwa ni lazima uweze kubadili tabia uliyonayo ya uvivu na ongeze juhudi za kiutendaji katika kufanya kazi.

3. Tenga muda wa kufikiri kuhusu biashahara yako.

Moja ya mbinu ya kuweza kukuza biashara yako ni kuweka muda kwa ajiri ya kujua biashara yako inakwenda vipi. Biashara zilizo nyingi huwa hazina maisha marefu kwa sababu wahusika hawa na muda wa kutosha kuhusu kufikiri jinsi gani biashara inakwenda bali walio wengi hutazama faida tu. Kufanya hivyo tambua biashara yako hatakuwa na Maisha marefu ni vema ukawa mzuri kujua utendaji wako wa kibiashara na changamoto zake na jinsi ya kutatua.


4. Tambua mchango wako wa watu wengine.

Ukitaka kufanikiwa zaidi ni vyema ukajua ni kwa jinsi unavyojenga mahusiano mazuri pamoja na wafanyabiashara wengine  na wateja wako pia. Mchango mzuri uliona nao utakufanya uongeze wateja wengine. Kwa mfano unauza biashara fulani ghafla ukaishwa bidhaa fulani harafu mteja akaja kuuliza bidhaa hiyo, usimwambia mteja huyo kwamba kama huna bidhaa hiyo mwambie ngoja nikakuchukulie kwenye stoo. Na kwa kuwa wewe huna bidhaa hiyo nenda kwa jirani yako nenda ukanunue na uje kumpa mteja huyo. Kufanya hiyo kutakufanya uweze kujenga mahusino na wafanyabiashara nyingine pia njia ya kuongeza wateja na kufanikiwa zaidi.

5. Usiridhike na hali uliyonayo.

Kuwa mfanyabiashara mkubwà ni lazima kuwa katika imani ambayo inatamani kufanikiwa zaidi. Maana yangu hata kama wewe unajiona tayari umefanikiwa wewe jione bado una kiu ya kufanikiwa zaidi. Kama wasemavyo kwamba pesa haitoshi basi hata wewe una deni la kufanikiwa zaidi. Moja ya kufeli kwa biashara ni pale mtu anapoona amepata mafanikio na yeye anaridhika . Kuridika ni adui wa mafanikio. Kuridhika ndiko kunako turudisha nyuma watu wengi sana. Pia nikumbushe ya kwamba kufeli sio kushindwa ni sehemu ya mafanikio
.

Haya ndiyo mambo kadhaa unayoweza kuzingatia ili kuweza kukuza biashara yako. Chukua hatua mapema za kubadili maisha yako.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Mwandishi: Afisa Mipango Benson chonya .
Simu; 0757-909942
E-mail;
 bensonchojya23@gmail.com