google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 29, 2016

Unachokiamini Ndicho Unachopokea Na Kufanya.

No comments :
Mwanafalsafa mmoja aliwahi sema  “You cannot do beyond what you know and you cannot know beyond what you believe...therefore what you believe determines what you know and do”
Huwezi kufanya nje ya unavyojua na huwezi kujua nje ya unavyoamini...kwa hiyo unachoamini kinapelekea kujua kwako na kufanya kwako.
Hebu sisi tuchambue haya maneno muhimu matatu:-
Unachoamini.
Watu huamini tofautitofauti juu ya sababu za wao kuwa vile walivyo.Mwingine atakwambia yupo katika hali ya kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ya mtu fulani,au jambo fulani lililowahi kutokea maishani mwake.
Mwingine anaamini kuwa ni kwa sababu tu bado hajachukua hatua ya kubadili hali yake. Huyu wa pili ana kheri ingawa wote wawili wapo sahihi kufikiria hivyo kwa sababu ndivyo wanavyoamini.
Kwa mujibu wa mwandishi Orison Swett Marden "What we sincerely believe regarding ourselves is true for us". Tunachokiamini kuhusiana na sisi wenyewe ni sahihi kwetu.
Unachokijua.
Kwa kawaida mwanadamu yeyote hawezi kufanya jambo bila kutafuta maana(they search for meaning) bila kujali chanzo cha hiyo maana na kama maana hiyo ni sahihi au sio sahihi...hutaka tu kuona anachofanya kina msaidia kwa namna fulani.
Maana yangu hapa ni kwamba ni muhimu kutumia asili hiyohiyo kutanua uwezo wa kujua ZAIDI ili kupata maana kubwa zaidi kuliko kuishia kung'ang'ania maana moja uliyoipata juu ya jambo husika.Kusoma vitabu,kuuliza na kusikiliza wengine kwa makini huongeza uwezo wa mtu kujua zaidi.
Unachofanya.
Mtu yeyote timamu lazima afanye jambo kwa kuangalia maslahi yanayotokana na kuwekeza nguvu yake hapo.Vinginevyo ataachana nalo na kuangalia ustaarabu mwingine.

Kwa hiyo kwa mtu mwenye lengo la kufanya vizuri iwe katika masomo, biashara, kilimo, michezo, mahusiano, ufundi nk ni muhimu kuzingatia ngazi hizo tatu muhimu zinazotegemeana LAKINI mlango mkuu ni kubadilisha UNACHOKIJUA.
Jenga tabia ya kutamani kujua vitu vipya, mbinu mpya na mwelekeo mpya ili uweze kufika unapotamani kufika siku moja.
Imeandikwa na Moses Mkemwa
(Uncle Moses)
0757717572


Jul 28, 2016

Jinsi Ya Kutengeneza Chili Sauce.

2 comments :
Kama utakuwa ni mfutialiaji mzuri wa mtandao huu, siku chache zilizopita tuliweza kukulete makala ambayo ilikuwa inahusu ni jinsi gani unaweza kutengeneza tomato souce, namshukuru Mungu kuna watu wengi walichukua hatua na sasa wameanza kutengeneza pesa kupitia utalamu huo wa utengenezaji wa tomato souce.

Nakusihi hata wewe ambaye unasoma makala haya leo uweze kuchukua hatua mathubuti juu ya somo hili la leo na kuona ni wapi ambapo na wewe utatengeneza pesa kupitia somo hilo, maana somo hili si kwa ajili ya kukupa hamasa bali ni kwa ajili ya vitendo na kutengeneza pesa, nakuomba urudie kwa mara nyingine kusoma aya hii, maana kiukweli somo hili ni hili ni pesa mkononi. 

Afisa mipango kwa moyo wa ajasiri nimeamua kukuletea somo hili ili nikutoe katika kundi la watu ambao wanalalamika kwamba Maisha magumu, ajira hakuna, mara serikali ya awamu hii inabana na sababu nyinginezo kama hizo, ambazo kwa upande wangu huwa naziona ni stori nyoka tu.

Weka maandalizi yako mapema.
Pasipo kumung'unya maneno, wala kushika simu yangu kuangalia kama kuna meseji au kuna mtu kanipigia, wala bila ya wewe kukuchosha nadhani niende moja kwa moja kwenye maada amabayo siku majawabu tosha ya wewe kupata pesa. 

Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;

a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.

b) Nyanya kilo moja.

c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.

d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.

e) sukari vijiko viwili vya chai.

f)  maji ya moto kikombe kimoja cha chai.

g) vinega vijiko 3 vya chai.

Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce

HATUA YA KWANZA.

-Kata Pilipili kuondoa mbegu.

-menya nyanya kuondoa mbegu pia.

-menya vitunguu swaumu kisha
 vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.

Nb; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.

HATUA YA PILI.

Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;

*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.

*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.

*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.

* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.

* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.

Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza  chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.

Endelea kufuatilia mtandao huu Wa DIRA YA MAFANIKIO kwani uongozi wa mtandao huu umeandaa masomo mazuri kwa ajili yako, ambayo yatakufanya uweze kufanikiwa katika maisha yako. 

Ndimi; Afisa mipango; Benson chonya
0757909942

Jul 27, 2016

Je! Wajua Ni Kwa Nini Mpaka Leo Malengo Yako Hayajatimia?

No comments :
Moja yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake yanatimia.
Hata hivyo, kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo.
Ipo hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja ya mada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi gani unavyoweza kutimiza  malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhahiri anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha mafanikio.
Ndipo nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho anadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na njia ya kutimiza ndoto hizo.

Moja ya maajabu ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema nataka kuwa mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo hapo ndipo ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu wengi wana ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni wepesi sana wa kukuta tama.
Ndipo nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalitamani liwe kweli ni lazima ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo hususani kwa kujifunza na ikiwezekana kulipa gharama, lipa gharama kwa kuwa hakuna maisha ya kimafanikio ambayo hayana gharama.
Pia ikumbukwe ya kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto hizo hizo ndizo ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya  jambo hilo, na hawa ni watu ambao wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tunayafanya.
Wengi wetu tupo tayari kuahairisha mambo  na kuleta visingizio visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu anakwambia anataka kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni  mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Tuende mbele turudi nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini yapo vile vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya kuweza kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea kutafakari juu ya maisha yako.
Tafakari ni kwanini mpaka leo hii hujatimiza malengo yako? Kama umepata jibu, zama tena katika halmashauri yako ya kichwa tafakari tena je unahisi sababu ambazo umezipata ni za msingi au  sio za msingi? Kama umekwisha pata majibu inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara kisha tafakari tena na uje na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo yote uliyowaza? Usinibe majibu.
Mmmh, sawa labda nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha msingi ni kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za kiutendaji. Hata hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo usiishie kusema tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa mwelekeo tosha kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa nacho? Na baada ya muda gani!
Huenda bado ukawa haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo hilo. Maana tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia mafanikio hayo kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu wengine ambao kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa ni lazima uwe na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.
Nikushuru sana kwa kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika endapo utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya. Nikusihi ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya kwako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamfanikio.blogspot.com kila siku.
Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya
Blogu; dirayamafanikio.blogspot.com
Simu; 0757909942

Jul 26, 2016

Hatua Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.

No comments :
Ili biashara yako iweze kukua na kukupa mafanikio ni lazima ipitie katika hatua nne muhimu. Hizi ni hatua ambazo biashara yoyote ile, ili iweze kuleta mafanikio, ni lazima ipitie hapo bila kuruka hata hatua moja.
Kama ulivyo umuhimu wa hatua za malezi kwa mtoto kuanzia kutambaa hadi kukimbia na pia hatua hizi ni muhimu katika mafanikio ya biashara hivyohivyo. Ikiwa ikatokea hatua moja imerukwa  ni rahisi kwa biashara husika kupoteza mwelekeo au kufa kabisa.
Mpaka hapo bila shaka utakuwa umeona ni kwa jinsi gani hatua hizi zilivyo za muhimu katika kukua kwa biashara. Ni hatua ambazo zinampa mfanyabiashara uzoefu wa kukua siku hadi siku na kupelekea biashara kuleta mafanikio mkubwa.
Je, hatua hizo ni zipi?
Zifutazo  Ni  Hatua Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.
1. Hatua ya mbegu (Seed stage).
Katika hatua hii, mara nyingi mjasiriamali anakuwa yupo katika hatua ya kujaribu wazo la biashara yake kama linafanya kazi au la. Ni hatua ambayo humfanya mjasiriamali ajaribu mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya kuchunguza soko jinsi lilivyo.
Pia hii ni hatua ambayo biashara kwa namna yoyote ile huhitaji pesa ili iweze kusonga mbele. Kwa kifupi hii ni hatua inayohitaji umakini sana kwa sababu ndio msingi na mwanzo wa mafanikio wa hatua zingine zinazofuata. Ikiwa umakini utapotea hapa ni lazima biashara ife.

2. Hatua ya kuchipua ( Start-up stage).
Baada ya kujaribu wazo lako na kuona wazo linafanya kazi, hatua inayofuata baada ya hapo ni hatua ya kuchipua kwa biashara. Hii ni hatua ambayo sasa unaanza utekelezaji wa wazo lako. Ni hatua ambayo unakuwa unatafuta wateja wako mwenyewe sasa.
Katika hatua hii pia mjasiriamali, ni lazima ujifunze jinsi ya kupata mrejesho kwa wateja wako. Ni lazima ufahamu wateja wako wanataka  nini au hawataki nini ili kufanya maboresho. Unapozidi kuwa makini katika hatua hii ni lazima idadi ya wateja wako itaongezeka na biashara itakua pia.

3. Hatua ya kukua ( Growth stage).
Mara baada ya bidhaa zako kuwa sokoni, ikiwa utaona bidhaa zako zinatakiwa kwa wingi, elewa kabisa hapo biashara yako hiyo ina dalili tosha ya mafanikio kwa kukua.
Sasa kaika hatua hii, hiki ndicho kipindi ambacho mjasiriamali anatakiwa kuanza kuangalia ushindani na wafanyabiashara wengine. Ikiwa ikatokea umeweza kumudu vizuri katika hatua hii, basi ni wazi mafanikio kwenye biashara yako ni lazima yaonekane.

4. Hatua ya kukomaa ( Maturity stage).
Hapa katika hatua hii, biashara yako inakuwa imemudu kuweza kukabiliana na ushindani wa kila aina. Hiki ni kipindi ambacho biashara yako inakuwa inajitatanua na kutengeneza matawi katika sehemu zingine tofauti.

Kwa kifupi, hii ni hatua ambayo mjasiriamali anayaona mafanikio yake kwa sehemu kubwa. Lakini hata hivyo ni hatua ambayo mjasiriamali pia hatakiwi kulewa zaidi ya kuendelea kuweka juhudi hadi kufanikiwa zaidi na zaidi.
Kumbuka, hizo ni hatua muhimu nne ambazo biashara yako ni lazima ipitie ili iweze kukua na kukuletea mafanikio. Hata hivyo, hizi ni hatua ambazo zinategemeana sana. Kushindwa kwa hatua moja, ni dalili tosha inayoonyesha  pia na hatua zingine zitashindikana kufanikiwa.
Kitu cha kujiuliza wewe upo katika hatua ipi? Kwa hatua yoyote uliyopo itakusaidia kujua kama utafanikiwa au la!
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,






Jul 25, 2016

Sheria Tatu (3) Za Mafanikio (3 Laws Of Success).

2 comments :
Uhali gani mpenzi wa makala haya, ni matumaini yangu makubwa umzima wa afya kabisa, katika makala hii natakaka tujikite zaidi katika kujua  sheria ambazo zitatufanya tuweze kutimiza ndoto zetu.

Mara kadhaa umekuwa ukizoea kuona ya kwamba mahali palipo na sheria lazima pawe chombo au mtu wa kuzisimamia ili sheria hizo ziweze kutekelezeka kirahisi.

Lakini katika sheria za ya mafaniko huwa ni kinyume kwa sababu haina haja ya kuwepo chombo au mtu wa kukuongoza isipo kuwa wewe mwenyewe ndiye nahodha wa Maisha yako.

Maana tunaambiwa ya kwamba hatima ya maisha yetu tunayo wenyewe. Hiyo ina maanisha kwamba sheria za mafanikio zipo, uwe unajua au hujui, ila unapovunja sheria hizo lazima uadhibiwe na ulimwengu.

Leo katika makala haya, Afisa mipango nataka nikushirikishe na wewe sheria tatu tu za mafanikio. Ikiwa ikatokea ukazitumia sheria hizo uwe na uhakika utafanikiwa.

Zifuatazo Ndizo Sheria Tatu Za Mafanikio.

1. Fikiri (think).

Kila mwanadamu ana uwezo binafsi ambao amezaliwa nao kwa ajili ya kufiri, lakini fikra hizo hizo hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine, hata siku moja hakuna mtu ambaye atafanana uwezo wa kufikiri na mtu mwingine.

Hata hivyo kila kitu chochote ambacho unakiona leo hii  yupo mwazilishi wa kitu hicho. Hapa ina maana ya kwanza yupo yule mwanzilishi wa kitu na yupo yule ambaye ni mtaalamu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya kitu hicho andapo kitukuwa hakipo sawa.  

Vilevile katika kufanya vitu ambavyo tunaviona leo vinazidi kuwa katika ubora huohuo hutuna budi kutazama vitu hivyo katika jicho la tofauti sana, inawezekana bado hujanielewa ila ukweli ni huu upo utofauti mkubwa kati ya kufikiri na kuwaza.


Mara kadhaa endapo utamsikia mtu anasema nilitaka kufanya hiki na kile lakini hakijaenda kama alivyokuwa amepaga ujue fika mtu huyo ni alikuwa anawaza tu. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufika kilele cha mafanikio yako huna budi kuweza kufikiri mambo kwa hali juu sana na sio kuishia kuwaza tu.

Unajua ipo hivi hapa ulimwenguni hakuna kazi ngumu kama ya kufikiri vitu vipya, na kama nilivyosema hapo awali ya kwamba kila binadamu ana uwezo wake binafsi ambao amezakiwa nao kwa ajili ya kufikiri, hapo sasa inategemeana ya kwamba unafikiria nini ?

Je ni mawazo chanya au mawazo hasi? Tafakari kidogo kisha ugundue juu ya jambo hili .Hata hivyo wapo baadhi ambao wamefanikiwa kimtazamo hata kimaisha watu hawa wao walifikiri mambo ya msingi katika mtazamo chanya, ndivyo hivyo ambavyo leo inatupasa mimi na wewe kuweza kutazama katika mtazamo huo huo ili tuweze kufanikiwa zaidi.

Kwa kuongezea pasipo kumung'unya mdomo wala kuharibu silabi za matamshi, kila kitu ambacho unakifijiria ambacho kipo katika mtazamo chanya huna budi kukiandika katika sehemu ambayo mara kadhaa utakuwa unakiona, kufanya hivi kutakufanya uweze kufikiri kwa kina zaidi ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza ukakitekeleza kitu hicho. Mara kadhaa ukitaka kufanikiwa zaidi kumbuka kufikiri tofauti.

2. Panga (plan).

Jambo la pili ndugu msomaji wa mada hii, ni kwamba baada ya kufanya tafakari juu ya jambo lako huna budi kukaa chini na kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo. Katika kupanga mpango kazi wa kile ambacho umekifikiria kitakupa picha kamili juu ya kile ambacho unatamani kukifanya, hii ikiwa na maana ya kwamba kitakuwa na matokeo chanya au matokeo hasi.


Kwa mfano labda unataka kufanya biashara, ni lazima uwe na mpango wa kibiashara (business plan) ambayo itakupa picha kamali ya jinsi ya biashara yako itakavyokuwa, kufanya hivi ni chachu ya kufika mahali ambapo unatamani kufika.

Pia yamkini unatamani kufanya jambo fulani kwa hapo mbeleni hivyo tumia muda huu kupanga mambo ya msingi yatayokwenda kukufanikishia jambo lako. Maana kuna usemi ambao unasema ukikosea kupanga mambo ya msingi umekwisha kufeli mambo yako.

3. Fanya (do).

Baada ya kufanya tafakari ya kina, pia baada ya kupanga namna ya kutekeza, jambo la tatu huna budi kuanza kutenda jambo hilo, si kutenda tu! Bali kutenda kwa njia tofauti na ulivyozoea kutenda au watendavyo watu wengine.

Pia kwa jambo lolote ambalo unataka kulifanya, au umekwisha kuanza kulifanya ili uone ya kwamba jambo hilo lina matokeo kiasi gani ni lazima ukipende jambo hilo haijalishi lina changamoto kiasi gani. 

Kwa mfano  unafanya biashara  haina haja ya kutumia nguvu katika kutafuta wateja bali unachotakiwa ni kuongeza thamani katika bidhaa au huduma, kufanya hivi wateja watakuja wao wenyewe, kwa sababu moja ya tabia ya wateja wengi wana tabia ya kuambiana hasa ni wapi ambapo hutolewa huduma nzuri. Narudia kusema tena penda kutoka ndani ya dhamira yako kwa jambo lolote ambalo unalifanya, maana hapa ndipo mzizi wa mafanikio yako ulipo.

Ni matumaini yangu makubwa ya bila shaka tumeelewana vizuri, na nikuhakikishe tu kwamba endapo ulichokisoma hapo juu utakwenda kukiweka katika matendo basi mafanikio yanakuja kwako kwa asilimia zote.

"Naamini katika kujifunza" kama na wewe unaamini hilo tukutane tena siku nyingine katika makala ijayo.

Ndimi; Afisa Mipango; Benson Chonya.
Phone no; 0757909942


Jul 22, 2016

Mambo Ya Msingi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ujasiriamali, Kabla Hujaacha Kazi.

No comments :
Inawezekana umechoshwa sana na kazi unayoifanya na una hamasa kubwa ya kutaka kuwa mjasiriamali kwa kujiajiri. Kama hayo ndiyo mawazo yako, kwanza hongera sana, kwani unachagua njia sahihi itakayokufikisha kwenye ndoto zako za kweli.
Nasema hivyo kwa sababu, watu wenye mafanikio makubwa duniani ni wajasiriamali na si vinginevyo. Lakini pamoja na kwamba umekuwa umechagua njia sahihi ya kukufikisha kwenye ndoto zako, ipo haja ya wewe kujua mambo ya msingi kwenye ujasiriamali kabla hujaingia huko.
Kwa kujua mambo hayo itakusaidia wewe kujiwekea misingi imara itakayokufanya usitetereke. Naamini kwa kusoma makala haya, itakusaidia usiwe na maamuzi ya kukurupuka ikiwa upo kazini na unataka kuachana na kazi yako na kuingia kwenye ujasiriamali moja kwa moja.
Sasa bila kupoteza muda, twende pamoja kujua mambo ya msingi unayotakiwa kujua kuhusu ujasiriamali, kabla   hujaacha kazi.
 1. Ujasiriamali unataka kujituma sana.
Hakuna ubishi katika hili kama umemua kuwa mjasiriamali wa kweli ni lazima kujituma sana kila siku. Bila kufanya hivyo hutafika kilele cha mafanikio. Kuna wakati unatakiwa kufanya kazi kuliko kawaida ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio yako.
Kama upo kazini na unataka kuingia kwenye ujasiriamali huku ukiamini utakuja kujiachia sana utakuwa unajipoteza. Hivyo, unachotakiwa kujua kama una mpango wa kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali, elewa unaingia kwenye kambi inayokutaka kujituma sana ili kuweza kufanikiwa.

Kujituma ni muhimu sana kwa mafanikio ya mjasiriamali yeyote.
2.Ujasiriamali hautakupa uhuru wote.
Kama ilivyo kwa mwajiri wako kuna wakati anaweza kukubana, halikadhalika nao ujasiriamali uko hivyohivyo. Hata kama unafanya kazi ya kwako kuna mambo ambayo huwezi kuwa huru kwa asilimia zote, kwani ukifanya hivyo utapoteza mengi.
Kuna kipindi ambacho utatakiwa kuamka asubuhi na mapema. Pia kuna wakati itatakiwa kujinyima baadhi ya mambo ili kufikia mafanikio yako. Hiyo yote hutokea, kwani bila kufanya hivyo, utakaa sana kwa muda mrefu eneo moja bila kufanikiwa, kwa sababu utakuwa kama unazunguka tu.
3. Ujasiriamali unataka juhudi ya kujifunza kila siku.
Ili uweze kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio ni lazima ukubali kujifunza kila siku. Kila wakati ubongo wako ni lazima upokee vitu vitakavyokusaidia kukubadilisha wewe ili ukubaliane na hali yoyote ya shindani.
Mjasiriamali wa kweli ni yule anayekubali kujifunza na kurekebisha udhaifu wake pale unapohitajika. Kujifunza huko hakuishii kwenye maandishi peke yake ila mpaka kwenye vitendo. Binafsi jiulize upo tayarii kujifunza kila siku? Kama ni ndiyo endelea na safari yako ya ujasiriamali bila kuchoka.
4. Hutakiwi kukata tamaa mapema.
Unapoamua kuwa mjasirimali na kuchagua njia yako mwenyewe, kitu cha kimojawapo cha cha kukijua, ni kwamba hutakiwi kukata tamaa mapema. Kuna wakati mambo na mipango yako inakuwa inakwenda hovyo sana lakini unatakiwa kuvumilia bila kuchoka.
Ukiingia kwenye ujasiriamali halafu huku ukawa una roho ile ya kukata tamaa mapema hutafika popote. Kwa hiyo ingia kwenye ujasiriamali ukiwa tayari kwa lolote. Ikitokea hasara vumilia na kisha chukua jukumu la kuweza kusonga mbele bila kukata tamaa.
Hayo ndiyo mambo ya msingi unayaotakiwa kujifunza kabla hujaingia kwenye ujasiriamali. Chukua hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,


Jul 21, 2016

Kitu Unachotakiwa Kuanza Nacho Ili Kujitengenezea Utajiri.

No comments :
Watu Wengi wanatafuta utajiri kwa udi na uvumba, japo wengine wachache wanapata na walio wengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo ambalo ni dhahiri kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya kutafuta utajiri kwa kutumia vituo tofauti fofauti na mbavyo vingi havitufikishi kwenye huo utajiri. Kwahiyo, kitu cha kujiuliza je? Safari Yetu ya kutafuta utajiri inapaswa kuanzia wapi?

Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kwamba, UTAJIRI unaanzia kwenye Fikra.Na "Fikra ni Nguvu Pekee inayoweza kuzalisha utajiri wa kuonekana kutoka kwenye vitu visivyoonekana. Fikra, hichi ndicho kitu unachotakiwa kuanza nacho ili kujitengenezea utajiri.  


Kila Kitu unachokifanya sasa hivi kimeanza kama wazo kutoka ndani yako. Hakuna matendo utakayotenda bila kuanzia kwenye fikra (Mawazo). Kwahiyo, ukiwaza kwa namna fulani, basi ujue kwamba utapata utajiri wa namna fulani sawa na ulivyowaza mwanzoni kabla ya kupata utajiri huo. 

Fikra au mawazo, ndio kitu pekee ambacho huweza kukusukuma kufanya vitu fulani fulani ambavyo ndivyo huweza kukuletea utajiri. Utajiri sio dhambi, bali ni sehemu ya Maisha, tumeletwa hapa duniani kuweza kutawala vilivyopo na kama ukiweza kuvitawala vizuri ni lazima utakuwa tajiri.


Unachohitaji ni kuweza kugeuza ndoto yako kuwa kweli. Wakati ukifanya yote hayo, kumbuka Kuwa, wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana isiyokuwa na mwisho. Hata kama wewe unajiona sio mtu mbunifu, hata kama ulishashindwa huko nyuma, hata kama unafikiri umeshajaribu kila Kitu ila ukashindwa, jua kwamba bado una nafasi Kubwa ya kupata Chochote unachotaka. 

Huwezi kuishi maisha unayoyataka, huwezi kuishi maisha yenye uhuru kama huna utajiri. Huwezi kuinuka na kufikia juu kwenye chochote unachofanya kama Kweli huna uhuru wa kipato. Ndio Maana ni muhimu sana Kwako Kuwa tajiri.

Kwa Kawaida binadamu tunazo nia tatu ambazo nazo tunaishi, yaani mwili, akili Na roho. Njia hizi ndizo utengeneza maeneo muhimu ambayo utuongoza Kuishi ama maisha ya utajiri au maisha ya umaskini. Maeneo hayo yote matatu ni muhimu sana katika kuishi maisha yenye mafanikio na furaha. Ni Lazima mwili Uwe na utajiri, akili iwe ya utajiri Na Roho pia iwe na utajiri, hapo ndipo itawezekana wewe kuifikia ndoto yako ya utajiri. 

Lengo la maisha yetu ni maendeleo yaletwayo na utajiri na wala si Kitu kingine. Msingi mkuu wa maisha ni kuendelea kupiga Hatua za kusonga mbele.  

Kama kila Kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa, iweje wewe leo uendelee kuwa hivyo miaka na miaka yote?
 Mti unakazana kukua zaidi ya ulivyo sasa.  

Na Wewe Binadamu pia ni Lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa kwa maeneo yote muhimu ya maisha yako. Katika harakati zako za kutafuta utajiri, Lazima kuhakikisha Kuwa fikra zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako kuzuia akili yako isilishwe mambo ya Umasikini, na ifanye akili yako ibaki imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au kuumba. 

Kamwe usizungumze: Jitahidi usizungumzie kuhusu matatizo yako ya ya zamani kifedha kama Ulikuwa nayo; usiyafikirie kabisa. Usizungumze kuhusu umaskini wa wazazi wako au ugumu wa maisha yako ya huko nyuma. Kufanya lolote Kati ya hayo ni kujiweka katika umaskini kwa wakati Huu ulionao sasa.

Weka umakini na mambo yote yanayohusiana nao kado au nyuma yako kabisa. Linda mazungumzo yako: Kamwe usizungumze kuhusu masuala yako au chochote kile kwa namna ya kuvunja moyo au kukatisha tamaa. Kamwe usikubali uwezekano wa kushindwa au kuzungumza kwa namna inayoashiria kushindwa. 

Unatakiwa kutozungumza Kuhusu nyakati kuwa ngumu au mazingira ya Baza Kama Vile una mashaka. Nyakati zinaonekana kuwa ngumu kwa wale walio na usawa wakushindana na wenzao. Lakini, wewe unayetafuta utajiri wako hunabudi kuanza kujifunza maisha yale ambayo unashindana na malengo yako au ndoto zako basi. 

Kumbuka siku zote Mafanikio ni mchakato siyo tukio . Kwahiyo, Kama Wewe umeweza kujifunza Kitu Chochote kipya na cha Thamani kutoka kwenye makala hii ni Wazi kwamba Tayari umeanza mchakato wa kuelekea mafanikio.

Makala hii imeandikwa na Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP.  

Jul 20, 2016

Mambo Ya Msingi Kuzingatia Katika Kilimo Cha Alizeti.

No comments :
Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Kuchagua aina bora ya mbegu. Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.

KUWEKA MBOLEA
Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.

KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA; 
UKAGUZI 
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu. 


DALILI ZA ALIZETI ILIYOKOMAA
Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi. Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia. 

UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI 
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka shambani
 Kisu, Vikapu,  Magunia, Matenga Vifaa vya kukaushia, Maturubai, Mikeka, Kichanja bora, Vyombo vya usafiri kutoka shambani, Matoroli, Matela ya matrekta, Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama, Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu.

Pia mashine (combine harvester) hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shamba. Kisha alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa kukausha. 

KUKAUSHA 
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti; kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti. Kukausha masuke . Masuke hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze kukauka vizuri. Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au sakafu safi. Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha upuraji.

KUPURA Upuraji hufanyika baada ya kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu kutumia mti. Ni muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu. Pura kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka. 

KUKAUSHA MBEGU 
Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi. Tandaza mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
 Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho ni asilimia 8. 

JINSI YA KUTAMBUA MBEGU ZILIZOKAUKA VIZURI 
Kufikicha mbegu 
 Mbegu zilizokauka maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwa. Kumimina kwenye chombo kama debe, Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo hivyo. Mbegu zilizokauka hung’ara Kutumia kipima unyevu. Mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha asilimia 8.

KUPEPETA NA KUPEMBUA 
 Kupepeta na kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu zilizooza au kupasuka. Mbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umeme. Mashine hizi zina uwezo wa kupepeta na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa mashine yenyewe

KUHIFADHI
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au bini. Alizeti ya kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye chaga kwa kupishanisha. Ili kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya mita moja kutoka kwenye ukuta. Ziba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya kuingia.

Panya hupenda sana kula punje za alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhi. Asilimia ya upotevu inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula vingine kwa wakati huo. Matumizi ya Mbegu za Alizeti Mbegu za alizeti hasa zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwa. Pia zinatumika katika utengenezaji wa mikate. Mbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya mafuta. 

KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI KUPATA MAFUTA
Vifaa

Mashine ya kukamua mafuta

Chujio safi 

Ndoo 

Vifungashio

Sufuria

Mizani Malighafi 

Mbegu za alizeti 

Maji 

Chumvi 

NJIA YA KUKAMUA MAFUTA 

Chagua mbegu bora za alizeti

Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1 hadi 2

W eka kwenye mashine ya kukamulia ya daraja au Ram

Kamua mafuta

Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio safi 

Pima mafuta yaliyokamuliwa. 

Ongeza maji na chumvi. Katika lita 10 za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi.

Weka mafuta kwenye chombo cha kuchemshia (sufuria)

Chemsha hadi maji yote yaishe 

Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili kuwa maji yamekwisha.

Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa kitambaa safi au chujio 

Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu na vyenye mifuniko 

W eka lakiri na lebo

Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na yenye mwanga hafifu. 

MATUMIZI 
 Mafuta hutumika katika mapishi mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori 900

WASTANI WA MAVUNO YA ALIZETI KWA EKARI MOJA.

Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba lako ulivyolihudumia.

Kwa maswali na majibu kuhusu kilimo bora cha kisasa kitakachokutoa kwenye umaskini pamoja na ufungaji wa hema(Green House) na Drop irrigation, unaweza ukawasiliana na mtaalamu wetu wa kilimo Ndugu John Mabalaga kwa mawasiliano 0754 282 448.