google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 10, 2016

Mbinu Za Kupata Wafadhili Kutoka Nje Ya Nchi, Katika Kuitekeleza Fursa Yako.

70 comments :
Wiki moja iliyopita niliacha  ahadi yangu ya kuwa makala ijayo nitakueleza namna ya kupata wafadhili  katika fursa yako. Na nilipokea barua pepe nyingi  na ujumbe mfupi wa maandishi kwamba wanasubiri kwa hamu. Basi bila shaka siku uliyoingojea kwa hamu ndiyo hii. Kaa mkao wa kulisha ubongo kisha twende sawa ili niweze kukata kiu yako.
Enzi za utoto ndiko kulikonifanya niweze kujua ukweli juu ya jambo hili. Unajua ni kwanini? Wakati tupo wadogo pale kijini kwetu palikuwa na kanisa ambako watoto wengi tulikuwa tunapenda kwenda zaidi hasa pale walipokuwa wanakuja wazungu. Wengi tulikuwa tunapenda kwenda katika kipindi hicho wakija wageni hao kwa sababu walikuwa wanakuja na vitu vizuri kwa ajili yetu na kuweza kutugawia watoto wote ambao tulikuwepo siku hiyo. Walikuwa wanatugawia vitu kama saa, nguo, baiskeli na vitu vingine vingi ambavyo wakati huo vilikuwa vinatuvutia sana.

Nafikiri kwa kisa hicho kama utakuwa miongoni wa waliokuwa wanapata zawadi hizo nitakuwa nimekukumbusha mbali sana. Lakini kwa kipindi hicho hakuna aliyejali kwamba wale wazungu wamepajuaje kanisani petu pale kijijini zaidi ya kufurahia zawadi zao! na wakati hawajawai kufika hata siku moja katika bara letu hili! Kadri nilivyozidi kukua nikazidi kufanya uchunguzi ambao ulikata kiu yangu, naamini pia utakata kiu yako. Kumbe ukweli ni kwamba kuna njia ambazo huwa zinatumika mpaka kuweza kuwapata wafadhili ambao wapo nje ya nchi na wakaweza kukusaidia katika kutekeleza jambo lako.

Jambo ambalo huzingatiwa zaidi katika kupata wafadhili , wao huangalia mtu ambaye amekwisha kuanza kulitekeleza jambo lake kwa kiwango fulani. Kama nilivyokueleza  mfano wa kanisa hapo juu ili wawaze kukufadhili ni lazima uwe umeshalianzisha kanisa hilo. Usiwatafute wafadhili kwa kupiga ‘stori’ tu bila kuwa na kitu maana kuna usemi unasema mwenye nacho huongozewa. Je, unataka kufahamu ni njia zipi za kutumia ili kuwapata wafadhili?

Zifuatazo ndizo njia za kupata wafadhili katika mradi wako;

1. Intaneti/wavuti (website)

Hii ndio njia ya kwanza ambayo kiukweli itakufanya ambayo hata wewe ukiweza kuitumia leo utakwenda kunufaika zaidi. Ikumbukwe ya kwamba kuitumia intaneti  vizuri ni pesa mkononi ambayo itakufanya utengeneze pesa zaidi. Namna ya kutumia njia hii ni kwamba, ingia ‘google’ ile sehemu ya kuandika jambo ambalo unalihitaji, kisha andika jambo lako. Kwa mfano unacho kituo cha kulelea watoto yatima na unataka kupata hao wafadhiri.

Anza kwanza mradi wako kabla ya kutafuta wafadhili.
Unaweza kuandika hivi (Organization supporting orphan children) baada ya hapo, ‘google’ itafunguaka kurasa mbalimbali zenye matokea zaidi hata ya elfu tano. Tuliza akili yako na uanze kufungua moja baada ya nyingine. Ukifungua nenda sehemu ya ‘home ya page’ hiyo kisha tafuta sehemu ya ‘contact page’, baada ya kuipata sehemu hiyo zichukue namba zao za mawasiliano na uanze kuwasiliana nao watu hao. Huenda pia wakawa hawajaweka namba ya zao za simu au e-mail zao ila kukawa na sehemu ya wewe kujaza taarifa zao zijaze kisha utaona ni jinsi gani mtakavyoweza kuwasiliana nao.

2. Kujitolea na kujipendekeza.

Baada ya kutembelea hizo kurasa zao anza sasa na kujitolea na kujipendekeza kwa kutuma mawazo yako chanya, tuma picha mbalimbali za huku afrika ikiwemo vivutio tulivyonavyo, tuma shughuli unazofanya kama ni kilimo, biashara na vitu vingine baada ya hapo anza kutuma picha za jambo lako ambalo unalitaka ufadhili kama ni kituo cha kulelea watoto yatima tuma majengo yake kama tayari kimeanza kutoa huduma tuma picha mbalimbali.

Kufanya hivi kutawafanya wafadhili hao waweze kupenda kuja kukutembelea na kuona hivyo vitu vya utalii vilivyomo katika nchi yako. Hakikisha ya kwamba huwaombi fedha wafadhili hao mwanzoni tu mwa mawasiliano yenu maana watakuona wewe ni tapeli.

3. Jifunze kwa watu ambao tayari wana wafadhili.

Kwa kuwa kuna watu tayari wamekwisha wapata wafadhili ni muda wako muafaka wa kuwauliza waliwapata vipi wafadhili hao? Kufanya hivyo kutakufanya uweze kuwapa wafadhili katika jambo lako. Pia kama utakuwa hajaweza kuwapata wafadhili wa kutoka ya nje unaweza kujua namna ya kuwapata wafadhili wa ndani ya nchi ambao nao wana mchango mkubwa katika kukufanikisha jambo lako kwa muda sahihi. Kuwa ni mtu wa kutaka kujifunza zaidi kwa kufuatalia mwenyewe kwa ndani kuliko kusikia tu.

Asante sana kwa kusoma makala haya na pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.


DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Imeandikwa na Afisa mipango Benson Chonya.
E-mail;
bensonchonya23@ gmail.com

70 comments :

  1. naomba mtu atakae nisomesha form one hadi chuo namwahidi nitasoma kwa bidii

    ReplyDelete
    Replies
    1. naomba unitafute kupitia hi imail;jossemuyenjwa125@gmail.com

      Delete
    2. Mungu akubsriki kwa maelekezo mazuri

      Delete
  2. Natafuta ufadhili wa kunisomesha kozi ya Utangazaji 0714954609 sitamwangusha

    ReplyDelete
  3. Nipo Arusha na ni kijana mwaminifu nimekwama sababu ya ada.

    ReplyDelete
  4. Enter your comment...naomba mfadhili atakaye nisaidia ada yakusoma form five na six sita mwangusha kabisa

    ReplyDelete
  5. Msaada wa kusomeshwa chuo diploma kozi za sayansi namba 0679036768

    ReplyDelete
  6. Mimi Ni mtaalam wa saikolojia na mwalim wa watoto nataman kufungua shule ya watoto wadogo ushaur tafadhali pa kuanzia

    ReplyDelete
  7. Naomben msaada wa kunifadhili kuninunulia kinanda kikubwa aina ya YAMAHA ELECTONE HS-6 cha kupiga Hadi mguuni maana nmeamua kujiajiri nafundisha baadhi ya watu namna ya kupga kinanda lakn sio changu Ni cha kanisa. Mm Ni yatima ila mungu kanipa karama hii niendeshe maisha yangu.
    WhatsApp number
    +255762849143

    ReplyDelete
  8. kupata eliNimefurelimuphii mimi nahitaji kupatakdh mfadhiili nijiendelezekgazi kiengazi ya chetu au diploma cont.0752538837
    Whatsup no. 0752538837

    ReplyDelete
  9. Sisi ni wakina mama wenye ulemavu tunaomba kusaidiwa vitendea kazi tunahusika na ushonaji(Supporting local disability women)
    Email:Wakinamamatanzania@gmail.com
    Facebook:Wakinamama Tanzania
    Contact:0623106175

    ReplyDelete
  10. Naombeni msaada wa school fees ya no watoto nimekwama kuwaendeleza naombeni kwa mwenye Moyo wa kunisaidia jamani napatikana kwa no +255684800441/0679875776

    ReplyDelete
  11. Natafuta wafadhili Wa green house

    ReplyDelete
  12. Natafuta wafadhili wa kunifadhiria ktk kituo changu cha malezi ya watoto wadogo,atupe vifaa vya michezo,lishe,na kuniboreshea kituo zaidi

    ReplyDelete
  13. Nashukuru kwa maelezo mazuri Mimi naomba anwani/ email za wafadhiri sielewi namna ya kuwapata pamoja na maelezo naomba anwani zao

    ReplyDelete
  14. Ntapataje ufadhili ya kusoma shahada ya urubani

    ReplyDelete
  15. Mimi nikijana ambae niko na elimu ya mifugo na nimfugaji pia naomba mfadhiri ambae twaweza weka mradi uhusuo ufugaji ili tuweze tengeneza pesa. napatikana kwa namba 0674074170

    ReplyDelete
  16. Mimi ni mchungaji. Naomba kwa yeyote anayewajua wafadhili wa kujenga makanisa na kununua vyombo vya muziki vya kanisa anisaidie email zao na namba za simu. Ahsanteeni sana.

    ReplyDelete
  17. Mimi ni mchungaji. Naomba kwa yeyote anayewajua wafadhili wa kujenga makanisa na kununua vyombo vya muziki vya kanisa anisaidie email zao na namba za simu. Ahsanteeni sana.

    ReplyDelete
  18. Mimi ni mchungaji. Naomba kwa yeyote anayewajua wafadhili wa kujenga makanisa na kununua vyombo vya muziki vya kanisa anisaidie email zao na namba za simu. Ahsanteeni sana. Namba zangu za simu 0714-257594/ 0784-774134.

    ReplyDelete
  19. Nina ndoto ya kufungua chuo cha ufundi veta ila tatizo ni uchumi msaada tafadhal 0766499018 au michaelmzwisa@gmail.com

    ReplyDelete
  20. Mimi ni kijana ninayetamani kutimiza ndoto yangu ya kusomea Udaktari wa binadamu ngazi ya Shahada.Naomba msaada wa ufadhili masomo yangu/au mawasiliano ya wadau nimechaguliwa kujiunga chuo kikuu.
    0759320490-Whatsapp na email:gilbertpius08@gmail.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi ni mchungaji peter mwachula.nipo mafinga Mkoani IRINGA naomba mfadhiri wa kununua vyombo na kujenga kanisa kuwa namba zangu.0746110081 /0716006021.natumia email ya mtoto wangu.danielmwachula@gmail.com

      Delete
  21. Naitwa Sesilia Anthony Myonga wa Morogoro Tanzania ni mtunzi wa vitabu vya tamthilia,nina vitabu sita 6 ambavyo ni 1.KIUMBEJINI,2.KIPAJI CHANGU,3.SIWEZIKUAMINI AHADI YAKO,4.NANI ADUI YANGU WA PILI IKIWA WA KWANZA NI MIMI MWENYEWE,5.HUU NI MTIHANI WANGU NA CHA 6.MIMI NI NANI KATIKA JAMII?. Ambacho kinazungumzia unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa wanawake na ubaguzi wa rangi kwa watu wenye ualbino, ambacho kilihaririwa na chuo kikuu Sua Morogoro Tanzania.Naomba msaada wa kupata wafadhili wa kuniendeza kipaji changu kwa kusaidiwa kutoa kitabu namba 6.MIMI NI NANI KATIKA JAMII?,pamoja na kupata wanunuzi au masoko.+255719832483

    ReplyDelete
  22. Naitwa diana naomba msaada wa kusomeshwa form five na six nitafanya vizur sana. hata mimi nije kuwasaidia wengine baadae namba yangu 0786465964

    ReplyDelete
  23. Nina ndoto za kuwa famasia lakin uwezo wa kifedha umekuwa mgumu kuendelea basis naomba ambaye yuko tayar kunisaidia anitafute kwa naomba 0685526946 au jacksonmussa12@gmail.com Nina elimu ya kidato cha sita na Nina matokeo mazur sana

    ReplyDelete
  24. Ninandoto za kuwa shelia tafazalii nakuomba 0788431935

    ReplyDelete
  25. Ninandoto za kuwa shelia tafazalii nakuomba 0788431935

    ReplyDelete
  26. Mimi Nina kituo cha taasisi ya elimu ya watu wazima kwa wale wote waliokomea LA saba au waliokomea kidato cha 1,2 au 3,ila wanaitaji kuendelea na elimu ya ya sec ba hatimaye chuo,Nina vijana 25 wanaitaji watu wa kuwasomesha kufikia malengo yao,tupo kisesa kwanza wilaya ya magu,kituo kimesajiliwa na taasisi ya elimu watu wazima,kwa yeyote atakaye pendezwa kusaidia vijana hao kuwasomesha,mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atambariki sana,mawasiliano 0769370814 au 0620322267,mbarikiwe

    ReplyDelete
  27. Asante Sana kwa makala hii mkuu mungu akubarik,, Maana Sisi Tuna NGO yetu ambayo tunaitaji mfadhili

    ReplyDelete
  28. Nahitaji mfadhili nataka kufungua kiwanda

    ReplyDelete
  29. Mimi ni kijana ambaye nina fani ya udeleva nina resen na chet cha veta nina uzoef wa udeleva natafuta kazi kwa mwenye uwezo wa kuniajir anisaidie napatikana kwa namba 0756867510

    ReplyDelete
  30. Habar kwa jina naitwa George Sanga mim tayari nishafungua kampuni ya uuzaji na usambazaji wa chakula kwa sasa naitaji pesa kwa ajili ya kuendesha kampuni yang ili iwe na mafanikio makubwa

    ReplyDelete
  31. asante kwa maelezo mazuri naomba kwa wanaosoma comment na wanauwezo wa kusupport please niasidie nimefaulu vizuri kidato cha nne na sita ila nimekosa ada kujiunga na chuo mwaka wa pili sasa pleasa kwa atakaeguswa number yangu 0621607147 email judyj8189@gmail.com

    ReplyDelete
  32. Naitwa YOHANA mamasita nina kipaji cha kuimba ila Pesa sina nimeshatoa nyimbo mbili zipo YouTube ila nimerekodia studio za chini kwa sababu ya uwezo nikipata mfadhili hakika nitafanya mambo makubwa sana. 0739506150 na 0744763101 au yohanamamasita6 @gmail.com

    ReplyDelete
  33. Tunashukuru sana. Tunaomba uwe unatoa elimu kama hizi mara kwa mara ili tujifunze zaidi. Kwa upande wangu nimejifunza kitu na nitawasiliana nawe ili nijifunze mengi zaidi. Asante sana.

    ReplyDelete
  34. My name's justine ammany I need a sponser I have great talent contact 255 0623241408

    ReplyDelete
  35. Naitwa LUCAS CHAMBIKA ni mwanafunzi wa chuo pia na mjasiliamali najihusisha na kilimo cha mpunga kwa sasa nina hekari tatu lakin lengo langu n kuwa na hekali hamsini ili niweze kuajiri na vijana wenzangu pamoja na kufungua taasisi mbalimbali kama shule..naomba ushauri wa jinsi gani naweza kupata masoko na pia kufikia malengo yangu .

    0753210031

    ReplyDelete
  36. My name is LUCAS CHAMBIKA I am also a college student and an entrepreneur I am currently involved in rice farming but I have three hectares but my goal is to have fifty temples so that I can employ my fellow youths as well as open various institutions like schools..I am asking for advice on how I can get marketing and also achieving my goals.

    0753210031
    lucaschambika@gmail.com

    ReplyDelete
  37. طالب جامعي ورائد أعمال أعمل حاليًا في زراعة الأرز ولكن لدي ثلاثة هكتارات ولكن هدفي هو الحصول على خمسين معبدًا حتى أتمكن من توظيف زملائي الشباب وكذلك فتح مؤسسات مختلفة مثل المدارس .. أنا أطلب النصيحة حول كيفية الحصول على التسويق وكذلك تحقيق أهدافي.

    0753210031
    lucaschambika@gmail.com

    ReplyDelete
  38. Samahani mim mkulima kwa Mara ya kwanza lakini nimepungukiwa fedha kidogo ili nimalizie mazao yangu napatikana katika namba hii 0655720401

    ReplyDelete
  39. Natafuta mfadhili wa kuniwezesha kuendeleza shughuli zangu za kilimo biashara, namba zangu ni 0623706254 nipo MBEYA

    ReplyDelete
  40. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  41. Mimi naitwa khalfan bahati naomba kufadhiliwa ili nitimize malengo,Nina kituo chs tuition lakini lengo langu ni kuwa na shule,Sina uwezo wa kununua eneo kujenga na pia kusajili shule,atayeguswa namba zangu 0769035519 au 0717202292

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama unaitaji mwalimu wa geography na English nipo Moshi boma ngo'mbe 0692996739

      Delete
  42. Mimi naitwa namanya Stanley Bashagi nimemaliza elimu ya chuo kwa shaada ya walimu wa secondary masomo ya geography and English language anae itaji mwalimu day care na kadharika nipo tayari, 0692996739

    ReplyDelete
  43. Hello, habar ya kazi naitwa Samira nyange nipo dodoma , Ninatamani kuanzisha kituo Cha watoto walemavu ,, Sina pa kuanzia,, Yani eneo pamoja na vifaa,, watoto walemavu wamekua wakitengwa saana mashuleni hata kwenye jamii naongea haya kwa uzoefu mkubwa coz Nina mtoto wangu mwenye shida hii naelewa chàngàmoto,,,, I wish nipate mfadhili nifungue shule yao

    ReplyDelete
  44. Hellow naitwa Helena b bundala natafuta wafadhil.nimeandika andika mrad inayohusu ukeketaji kwa wanawakr nipo Mara naomba mnipe mwongizo nitume andiko hiil kwa wafafhil namba yangu mi 0766535512

    ReplyDelete
  45. Hello naitwa Eva mdoe Mimi ninaeneo langu napenda kufungua shule ya nursery naomba msaada kwa wafadhiri wa kujegewa shule mi 0692321044

    ReplyDelete
  46. Hello
    Naitwa swabrudin Nuru nipo
    Mimi ni fundi mziefu wa computer ila sikuwahi kupita shule lakini nina uzoefu toka mwaka 2010 ila nakutana na changamoto katika shughuli yangu kwa sababu Sina cheti cha shule yoyote lakini najiweza ktk kazi naomba msaada nifanye nini ili niweze kupata kazi ktk makampuni na taasisi mbalimbali?? Naombeni msaada
    Namba yangu 0684279099 Ahsante

    ReplyDelete
  47. So good advice
    Nami yule ambaye yupo tayari kuwasaidia watoto wenye ulemavu tuwasiliane Mimi ninaorodha ya watoto zaidi ya 15 katika tarafa yangu lakini nikiunganisha Na tarafa jirani wanafika zaidi ya 40.
    My
    Contact
    0716461086
    Email. evaristhm20@gmail.com
    Nipo Tanga Tanzania

    ReplyDelete
  48. Ndugu zangu nipo chuo cha afya kairuki nipo mwaka wa pili nasomea nursing hila wazazi wangu hawana uwezo mama mlezi amekuwa akiniambia hana hela yaan nadaiwa ada mpaka sasa ya nusu mwaka sina hela ya matumizi naomba anayeweza kunisaidia kunilipia ada plse anisaidie naomba

    ReplyDelete
  49. Namba yangu ya simu ni 0718464348

    ReplyDelete
  50. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta udereva

    ReplyDelete
  51. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta ud

    ReplyDelete
  52. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta ud

    ReplyDelete
  53. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta udereva veta, 0752025034,suchmimi@gmail.com

    ReplyDelete

  54. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta udereva veta, 0752025034,suchmimi@gmail.com

    ReplyDelete

  55. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta udereva veta, 0752025034,suchmimi@gmail.com

    ReplyDelete

  56. Naitwa James Andrew John, Niko mwanza, naomba ufadhili wa chuo cha veta udereva veta, 0752025034,suchmimi@gmail.com

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.