google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 29, 2017

Ukiruka Mfumo Huu…Umeshindwa Tayari.

No comments :
Kama wewe ni msikilizaji mzuri wa muziki, utakubaliana nami kwamba CD nyingi zimetengenezwa kwa mfumo ambao kama hutaki kusikiliza wimbo unaochezwa basi una uwezo wa kurusha mbele na kusikiliza wimbo mwingine unaotaka.
Kwa hiyo utakuta CD moja yenye urefu wa saa moja , unaweza ukaisikiliza hata kwa dakika ishirini tu, hiyoni kutokana na kuruka ruka huko na pia kuchagua vile vipande muhimu ambavyo wewe unavitaka na unaviona vya muhimu kwako.
Kwa wengi wetu tumekuwa tukitaka kujaribu kuishi maisha yetu kwa mfumo kama huo. Tumekuwa ni watu wa kutaka kuruka vitu vingi au kuishi maisha yaliyopita na kusahau kuishi sasa na kufanya yanayotuhusu kwa sasa.
Unatakiwa kuishi maisha yako kama pumzi. Kwa mfano, huwezi ukasema ukavuta pumzi nyingi leo ili kesho usivute na eti ukabaki unaishi, hicho ni kitu ambacho hakiwezekani hata kidogo katika maisha yote, ni lazima utumie pumzi yako sasa. Hakuna pumzi ya akiba.

Na yale tunayofanya au kwa jinsi unavyoishi, inatakiwa tuishi sasa na si kuishi jana au kesho. Ukimua kuishi leo na kukazana kufanya ya leo basi uwe na uhakika utajijengea uwezo wa kutengeneza mafanikio yako moja kwa moja na unakuwa unaishi kwenye mfumo sahihi  jinsi maisha yanavyotaka.
Wengi wetu wana shindwa kwa sababu ya kuamua kuishi maisha yao kwa kuyarusha. Utakuta mtu yupo leo, lakini anaishi kesho. Kuishi maisha kwa namna hiyo huko ni kujipotezea maisha yako moja kwa moja. Kuruka mfumo unavyotaka, ni sawa na kuamua kushindwa kabisa.
Unatakiwa ukumbuke kila wakati, maisha yetu yametengenezwa kuishi kwa mfumo. Kuishi kwa mfumo sahihi pasipo kuuruka huko ndiko kunapokupa mafanikio. Ila kama utaishi kwa kuruka mfumo wa aina fulani huko ndiko kujitengenezea anguko kubwa la kushindwa kwenye maisha yako.
Leo ni siku yako ya kufanya mambo makubwa. Kesho itakuja kwa wakati wake, kikubwa kwako fanya mambo yako  leo kwa uhakika mkubwa. Ishi kwa mfumo kama unavyotaka hapo utakuwa unatengeneza mafanikio yako mwenyewe.
Unachotakiwa uelewe hapa, hutakiwi kuruka kitu. Fanya mambo kwa mpangilio kama yanavyotakiwa kufanyika. Usijadanganye kwa kuahirisha au kuacha vitu bila sababu ya msingi, ukifanya hivyo utakuwa unaishi nje ya mfumo na utashindwa tu.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



Nov 28, 2017

Ijue Siri Ya Kuondokana Na Ukata.

No comments :
Siku ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha hatari sana.
Kauli hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni  kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika ujumbe huo,  labda ujumbe huo upimwe na kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa.
Ujumbe huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa.
Binafsi nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho tunachokiita ni woga.

Woga ndio ambao umekua tatizo sugu lilojengeka machoni mwa watu wengi hata kuwapelekea watu hao kuweza kufa maskini huku watu hao wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa yenye kuleta mapinduzi ya kufikia kilele cha mafanikio yao.
Woga huu si mwingine ni ule woga wa kuthubutu kuweza kufanya mambo mbalimbali. Wapo watu ambao wanatamani kufanya biashara kubwa ila wakiwatazama watu ambao walifanya biashara hiyo na kuona ya kwamba walifeli basi nao hujikuta wanaogopa kufanya jambo hilo.
Achilia mbali biashara, wapo baadhi ya watu wanavipaji mbalimbali lakini watu hao wamekuwa ni waoga wa kuonesha vipaji hivyo machoni mwa watu wengine huku wakiamini ya kwamba watachekwa, watu wa aina hii mara nyingi hufa na ndoto zao.
Wapo baaadhi ya watu wanaogopa kujenga nyumba zao za kuishi huku wakisema, “kwa heshima niliyonayo nikijenga nyumba ya kawaida watu wengine wanatanishangaa” kwa kauli kama hizi basi hujikuta miaka inazidi kukatika bila watu hao kuweza kufanya kitu chochote cha maana.
Wapo baadhi ya wanafanzi wamekuwa wanaogopa kusoma masomo ya sayansi huku wakiamini masomo hayo ni magumu mwisho wa siku watu hao hujikuta wanafeli masomo hayo, kwa mtazamo wa aina hii ndipo ninapokubaliana na kauli ile ambayo nimesema hapo awali ya kwamba unachokiogopa ndicho kitakachokua.
Kabla sijamaliza kusema nawe siku ya leo nitakuwa ni mchoyo wa fadhira kama nitashindwa kutoa ufumbuzi wa tatizo hili, yawezekana ukawa na tatizo la aina hii ya kuogopa kufanya jambo fulani la maendeleo eti kwa sababu ya woga uliojengeke ndani mwako, unachotakiwa kukufanya ni kuhakakisha kila jambo ambalo unataka kulifanya, kabla hujaanza kulifanya jambo hilo hakikisha ya kwamba jambo hilo unalichunguza kwa makini  na sio kutanguliza woga mbele na ndiyo itakuwa siri ya kuondokana na ukata.
Mwisho nimalize kusema ya kwamba “kile unachokigopa kukifanya leo ndicho kitachokufanya uweze kuwa maskini”. Jambo lolote unalifanya hakikisha ya kwamba linakuwa jambo chanya ambalo halitavunja sheria na taratibu za sehemu ambayo unaishi.
Asante sana kwa kusoma Makala haya nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango; Benson  Chonya
0757-909942

Nov 27, 2017

Maskini Na Tajiri Wanatofautiana Kwa Mambo Haya…

No comments :
Kila kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na mingine midogo ya kawaida.
Pia hata wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua. Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge wanyonge.
Halikadhalika linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu.

Kama mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe na matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo mambo mengi kidogo yanayosababisha wengine wawe matajiri na wengine kuwa maskini.
Lakini katika makala haya tutaongelea kipengele kidogo cha tabia na jinsi zinavyoleta utofauti kati ya maskini na tajiri. Ni kweli zipo tabia ambazo matajiri wanazo na huwafanya wao kuwa matajiri kila kukicha. Ni tabia ambazo huwatenga kabisa na maskini na kuwaacha matajiri waendelee kufanikiwa.
Ikiwa utaamua kujifunza na kuzifatilia tabia hizi kwa karibu, uwe na uhakika utajiri utakuwa mikononi mwako muda sio mrefu. Nasema hivyo nikiwa na maana hii, ukitaka kuwa tajiri fanya yale ambayo matajiri wanafanya nawe utafanikiwa.
Hebu kwa pamoja bila kupoteza muda, tuangazie nukta kadhaa, zinazoweza kutuonyesha tabia zinazowatenga kati ya  matajiri na maskini. 
 1. Kuwekeza.
Watu wenye sifa ya utajiri ndani mwao hata kama bado hawajafika huko kwenye utajiri halisi ni wawekezaji wazuri sana. Si watu wa kuridhika na chanzo kimoja cha mapato. Wana vitega uchumi vingi sana ambavyo vinawasaidia kuingiza mapato kwa wingi hata kama wamelala.
Kwa mfano uatakuta wamewekeza kwenye mashamba, mafuta, migodi na maeneo mengine mengi. Hii ni sifa mojawapo kubwa inawatenga maskini na matajiri. Ukiona una kitega uchumi kimoja ujue unajizibia nafasi mwenyewe ya kuelekea kwenye utajiri mkubwa.
2. Kuweka akiba.
Suala la kuweka akiba kwa watu matajiri sio suala la hiari, kwao ni lazima. Angalau huweka asilimia kumi ya kile wanachokipata. Wanajua vizuri akiba hizo ni msaada mkubwa kwa baadae katika suala zima la kuwekeza. Wao katika kuweka akiba ni lazima, na pia hawana mchezo katika hilo.
Kutona na tabia hii, huwafanya wazidi kufanikiwa kila siku na kuwaacha maskini wakibaki kuwa maskini. Ni kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuelewa kwamba, akiba ni jambo la msingi sana kujiwekea kama unataka kuwa tajiri. Vinginevyo acha kuweka akiba, uendelee kubaki kwenye umaskini.
3. Kutoa.
Tabia nyingine inayowatenga watu matajiri na maskini ni ile hali ya kutoa. Watu matajiri ni watoaji wazuri sana wa pesa na mali zao. Hufanya hivi si kwa sababu wanazo nyingi, bali kutoa ni moja ya kanuni kubwa ya mafanikio walioamua kuitumia. Huwezi kufanikiwa sana kama hutoi.
Ieleweke hivi, maskini wanaendelea kubaki kuwa  maskini kwa sababu ya uchoyo walionao. Hukumbatia sana walivyonavyo na kusahau kutoa. Kosa hilo huwafanya wazidi kuendelea kuwa maskini siku zote za maisha yao. Ili kuwa tajiri ni lazima kutoa.
Kumbuka, tabia ya kuwekeza, kuweka akiba na kutoa ni moja ya tabia kubwa zinazo watenga matajiri na maskini. Matajiri wanajikuta wakiwa ni watu wakuzifanyia kazi tabia hizo na kuwafanya kuwa matajiri na maskini hubaki na umaskini wao kwa sababu ya kutokuzifanyia kazi tabia hizo. Chukua hatua ya kutenda ili kubadili maisha yako.
Ansante kwa kunifatilia na pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,                             
Simu; 0713 04 80 35,




Nov 26, 2017

Hutakiwi Kukwepa Jambo Hili Kama Unataka Kufanikiwa Kwa Kishindo.

No comments :
Vipo vitu vingi katika safari yako ya mafanikio ambavyo hutakiwi kivikwepa hata kidogo kama unataka kufika juu sana kwenye mafanikio. Ila kama unataka kufika kwenye mafanikio ya kawaida tu, unaweza ukavikwepa tu hakuna hata shida.
Leo sitataka kuzungumzia sana vitu vingi, naomba nikudokezee jambo moja tu ambalo  unatakiwa kutolikwepa ila unatakiwa ujue namna ya kukabiliana nalo ili uweze kufanikiwa kwa kishindo kikubwa.
Jambo hili si lingine bali ni kubeba hali hatarishi au kukabiliana na hali yoyote hatarishi ili kuweza kufanikiwa. Unaweza ukawa hujanielewa vizuri lakini ninachomaanisha hapa ni kuchukua ‘risk’ ili uweze kufanikiwa. Mpaka hapo sina shaka tupo pamoja.

Ukumbuke maisha yamejaa kila aina ya hali hatarishi. Huwezi kukwepa kukutana na hali yoyote hatarishi katika maisha yako. Ukikwepa hali hii ni lazima utakutana na hali nyingine hatarishi ambayo unatakiwa kupambana nayo mpaka kuweza kuishinda.
Kama kila wakati unaogopa kujitoa mhanga kwa sababu ya kuogopa kujihatarisha, basi tambua hapo ni sawa na kuchagua umeshindwa. Hutaweza kufika popote kama hauko tayari kuchukua ‘risk’ yoyote inayokupeleka kwenye ndoto yako.
Inatakiwa ujitoe mhanga kweli, haijalishi unajitoa mhanga kwenye kitu gani, kwenye malengo yako uliyojiwekea au kwenye kitu kingine chochote. Swala la kujitoa mhanga nakukubali kupoteza baadhi ya vitu ili ufanikiwe unatakiwa kulijua kwa ufasaha sana.
Maarifa uliyonayo unayatakiwa kuyatumia ili kukabiliana na kila aina ya changamoto na si kukimbia changamoto yoyote ile. Kukimbia changamoto na kuogopa kujihatarisha hiyo inaweza ikawa ni sawa na ujinga kwako ambao utakunyima mafanikio.
Unaweza ukajiuliza ni kitu gani ambacho utakipata hapa dunia pasipo wewe kuweza kujihatarisha. Ukisema biashara ni lazima uweke muda na pesa zako ili upate kile unachokitaka. Ukiangalia karibu kila kitu kwanza lazima uhatarishe ndio upate.
Kwa mfano hata wewe, umezaliwa kwa kujihatarisha pia. Uhai ulionao vilevile wewe kama wewe hauna uhakika nao, hiyo yote bado unaishi katika hali hatarishi. Hiyo kama iko hivyo kwa nini usiamue ukubali kujihatarisha kwa chochote ili ufanikiwe.?
Mara nyingi kuchukua ‘risk’ kwa kile unachotaka kukifanya, mwisho wa siku huweza kukupa wewe unayechukua ‘risk’ hiyo zawadi kubwa ya mafanikio. Ukumbuke tu mafanikio yote yanaanza kupatikana kwa wewe kuchukua ‘risk’ na sio kinyume chake.
Kwa hiyo badala ya kukimbia hali hatarishi yoyote kwako, unatakiwa kujua namna ya kuweza kukabilina nayo ili uweze kufanikiwa. Kama hautafanya hivyo utashindwa tu hata ufanyaje, hutaweza kukwepa kushindwa.
Ukumbuke kama nilivyokwambia mafanikio yanapatikana kwa wale watu ambao wanajitoa mhanga sana yaani kwa watu wanaochukua ‘risk’ kama wewe si miongoni mwao sahau kidogo kuhusu kufanikiwa, waache wachukua ‘risk’ wafanikiwe.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Nov 24, 2017

Mambo Ambayo Unatakiwa Kuyakumbuka Kila Wakati.

No comments :
U hali gani mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO naamini siku yako imekwenda poa na unaendelea kuweka juhudi za kweli katika kubadilisha maisha yako. Kwa harakati hizo tu nakupa hongera na endelea kupambana mpaka kieleweke.
Naomba pia nitumie wasaha huu kuweza kukaribisha katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza juu ya mafanikio. Naamini unajua kujifunza hakuna mwisho, hivyo unatakiwa kila siku kuweka maarifa ya kukusaidia, ukishindwa kufanya hivyo utakwama.
Katika makala yetu ya leo nitaomba tu nikukumbushe mambo ambayo unatakiwa uyakumbuke kila wakati kwenye  maisha yako . Ni mambo ya msingi kwani yatakusaidia kuweza kuwa na mtazamo chanya na kubadili mambo mengi sana kwako.

1. Mambo yaliyopita hayawezi kubadilishwa tena.
Unatakiwa kuelewa kama kuna mambo ambayo yameshapita huwezi kuyabadilisha tena hata kama yalikuumiza au ulifanya makosa kiasi gani. Kwa sasa unatakiwa kuganga yajayo, habari ya mambo yaliyopita yatumie kama fundisho tu kwako, lakini ndio yameshapita, usiumize kichwa na kujilaumu sana.
2. Maoni ya watu hayaamui hatima ya maisha yako.
Hata siku moja usije ukakaa ukafikiri kwamba maoni ya watu wengine wanayosema juu ya wewe ndiyo yanaamua maisha yako yawe vipi. Maisha yako yanabaki hivyo yalivyo kwa sababu wewe umeamua yawe hivyo. Lakini usikubali hata siku moja maoni ya watu yakurudishe nyuma na usiyatumie kama kisingizio.
3. Maisha yako yatakuwa mazuri tu ukijipa muda.
Ukiamua siku zote kubadilisha maisha yako unaweza. Kikubwa jipe muda wa kutosha kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadalika. Haijalishi unaona maisha yako ni magumu kiasi gani, lakini muda ndio kila kitu. Muda unaweza kusawazisha mambo mabaya na yakawa mazuri kabisa. Tumia muda wako vizuri.
4. Utashindwa tu, kama utakata tamaa.
Ndoto yoyote ile uliyonayo au ambayo unatamani kuifikia una uwezo mkubwa wa kuifikia. Ila hautaweza kuifikia ndoto yako hiyo ikiwa utafika mahali wewe mwenyewe utaamua kukata tamaa. Moja ya sumu kubwa ya kimafanikio ni kukata tamaa, ukikata tamaa ujue kila kitu kwako kimeishia hapo na hutaweza kusogea tena.
5. Furaha ya kweli inapatikana ndani mwako.
Ukweli huu hautakaa ubadilike kamwe kwamba furaha ya kweli inapatikana ndani mwako na wala si nje yako. Unaweza ukakazana sana kutafuta furaha nje kwa kufanya vitu ambavyo unaamini vitakupa furaha, lakini ukivipata vitu hivyo unashangaa ile furaha tena bado huna. Hivyo jifunze kutafuta furaha ya kweli ndani mwako.
6. Mawazo chanya, ni njia ya mabadiliko chanya pia.
Mbinu mojawapo ya kuwa na maisha bora. Ni kwa wewe kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa na mawazo chanya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kuleta mabadiliko chanya pia. Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kuwa na mlundikano wa mawazo mengi ambayo kwao ni hasi. Kuwa na mawazo chanya ubadili maisha yako.
Yapo mambo mengi ya kukumbuka kila unapoelekea kwenye mafanikio yako. Kwa leo hii nimekukumbusha mambo haya machache. Kwa kuyafanyia kazi itakuwa sehemu kubwa ya mabadiliko kwenye maisha yako.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


Nov 23, 2017

Ukitaka Kufanikiwa Zaidi, Hakikisha Unashughulika Na Jambo Hili.

No comments :
Habari za muda huu mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima na unaendelea na pilikapilika zako za kila siku. Hivyo nichukue wasaa huu nikukaribishe katika kujifunza kwa pamoja, ambapo siku ya leo nataka tujifunze jambo ambalo inakupasa kushughulika nalo kwanza ili uweze kufanikiwa.
Kabla sijajikita katika kiini cha somo letu la leo, nataka tujiulize, hivi ili uweze kufanikiwa katika maisha yatu inatupasa tushughulike na nini hasa? nini ambacho huwa kinakuja katika kichwa chako hasa pale ukiambiwa kuhusu mafanikio?
Binafsi niliwahi kufanya uchunguzi usio rasmi kuhusu mafanikio, nikagundua ya kwamba fikra na mtazamo ya watu wengi juu ya neno mafanikio unaegemea zaidi katika mitazamo hasi.

Wapo baadhi ya watu wengi wao huamini ya kwamba, kufanikiwa ni bahati ya mtu mwenyewe, lakini wapo baadhi ya watu wengine wao  huamini ya kwamba mafanikio ni uchawi, huku wakiamaini ya kwamba huwezi kufanikiwa bila kujihusisha na masuala ya kishirikina. Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba mafanikio yana mitazamo mingi sana katika vichwa vya watu.
Lakini ukweli ni kwamba neno mafanikio ni Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, ambapo Baraka hizo hujengeka katika kuamini ya kwamba mafanikio yako yanakuja kwa kuaamini njia sahihi za kuleta mafanikio hayo na si vinginevyo.
Hivyo ili uweze kuyapata mafanikio hayo inakupasa ushughulike na fikra. Fikra ndio kitu cha kwanza ambacho unapaswa kushughulika nacho katika kuyasaka mafanikio hayo. Tuposema neno fikra, tunamaanisha fikra chanya.
Au kwa maneno mengine ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uweze kushughulika na mtazamo wako juu ya maisha yako. Swali la kujiuliza ni kwamba ni nini mtazamo wako juu ya mafanikio?
Endapo majibu ya swali hilo ni mtazamo hasi, basi jifunze kila wakati kuwa na mtazamo chanya, kwani endapo utajifunza kuwa na mtazamo chanya kutakufanya uweze kupiga hatua za kimafanikio.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba ukitaka kufanikiwa katika maisha yako hakikisha unashulika na fikra, kwani fikra sahihi ndio kiwanda cha kutengeneza maisha yako.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson chonya,

0757-909942

Nov 22, 2017

Hiki Ndicho Kitu Cha Muhimu Sana Kuzingatia Katika Mafanikio.

No comments :
Upo ushauri mwingi sana ambao umekuwa ukitolewa juu ya namna gani mtu afanye ili aweze kufanikiwa. Waandishi na vitabu vingi vya mafanikio vimekuwa vikiandika sana na kutoa ushauri wa kipi kifanyike ili mtu kuweza kufanikiwa.
Pamoja na ushauri wote huo mzuri ambao umekuwa ukitolewa, lakini kipo kitu kimoja cha muhimu sana ambacho mtu akiamua kukifatilia na kukifanyia kazi hicho ndicho naweza kusema ndio mafanikio yote yaanzia hapo.
Kitu hicho si kingine bali ni kujitoa/‘commitment.’ Mafanikio yote yanaanza kwa wewe kuamua kujitoa na kuamua kweli kufikia mafanikio yako. Hakuna unachoweza kukifanikisha usipojitoa kikamilifu.

Kuwa na malengo, shauku ya kufikia malengo yako na hamasa hivyo kweli ni vitu muhimu, lakini huwezi kufanikiwa hata kama una vitu hivyo ikiwa hautaweza kujitoa. Kujitoa kwako ndio kila kitu katika kufikia mafanikio uyatakayo.
Ni kweli ili kufanikiwa unahitaji kufanya kazi kwa juhudi, unahitaji kuwa na nidhamu, unahitaji kuwa na shauku ya mafanikio yako, lakini lililo muhimu kwako ambalo unatakiwa ulizingatie sana ni kwa wewe kujitoa kwako.
Angalia maisha ya watu waliofanikiwa au angalia vile vitu ambavyo umewahi kuvifanikisha katika maisha, sina shaka utapata jibu kwamba kwenye vitu hivyo ulijitoa sana na ndio maana ukaweza kufanikiwa.
Kujitoa kunakuja kwa wewe kuamua kufanya kila linalowezekana hadi kuweza kutimiza ndoto zako. Hata kitokee kitu gani au kizuizi kipi kwa kuwa umeshaumua kujitoa utaamua kwa chochote kile utafanya hadi uweze kufanikiwa.
Wataalamu wote waliobobea katika fani mbalimbali duniani wametokana kwa sababu ya kujitoa. Ugunduzi wowote duniani umetokeaa kwa sababu ya kujitoa. Kuna watu walikuwa hawalali hadi wakawa wa wataalamu au wagunduzi wa kitu fulani.
Unapoona mafanikio ya aina fulani yametokea pia hayo ni matokeo ya kujitoa. Kuna vitu lazima vilipotea au vilitolewa sadaka ili mafanikio hayo yaonekane. Pasipo kujitoa kwa nguvu zote ni rahisi tu kusikia mafanikio yakionekana kwa wengine lakini sio kwako.
Kwa hiyo huhitaji kukwepa kiujitoa unapotafuta mafanikio. Kama ni kazi unatakiwa kazi ufanye haswa. Swala la kujionea huruma huko ni sawa na kuamua kuyapa mafanikio mkono wa kwaheri kwamba hutaki tena.
Hata kila mtu mwenye mafanikio ukimwona ujue kabisa kuna vitu ambavyo aliamua kujitoa hadi akaweza kufanikiwa. Kwa namna yoyote ile kama unataka kufanikiwa angalia unajitoa kwenye vitu gani.
Kujitioa ni kitu pekee ambacho kitakuhakikishia mafanikio yako wakati wote. kwa sababu utakapoanza kujitoa basi juhudi, kufanya kazi kwa moyo, kuwa na nidhamu hivyo ni vitu ambavyo vitakuja vyenyewe kwenye safari yako ya mafanikio.
Kuanzia leo, amua kujitoa kwa chochote kile unachokifanya kwenye maisha yako. hiyo itakusaidia sana kuweza kufika katika kilele cha mafanikio makubwa uyatakayo katika maisha yako kwa sehemu kubwa.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 14. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





Nov 20, 2017

Mambo Ya Kukumbuka Sana Wakati Unatafuta Mafanikio.

No comments :
Yapo mambo ya msingi ambayo kila wakati unatakiwa uyakumbuke unapotafuta mafanikio yako. Kwa nini unatakiwa kuyakumbuka mambo hayo, hiyo yote ni kwa sababu ndio kama msingi na nguzo ya kufikia mafanikio yako.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutoyajua au kutoyakumbuka kabisa mambo hayo na mwisho wa siku hujikuta wakipotea na kushindwa kufikia mafanikio yatakawayo kimaisha.
Kupitia makala haya nataka nikukumbushe mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuyakumbuka wakati unatafuta mafanikio. Naamini utajifunza na itakusaidia kuchukua hatua ya kufanikiwa kwa kuyajua mambo haya tena.
1. Jipe muda wa kufanikiwa.
Mafanikio ni kitu ambacho hakitokei mara moja tu. Mafanikio yanaenda hatua kwa hatua. Si kwa sababu eti kuna jambo umepanga kulifanikisha basi ulifanikishe leo leo, kama ni hivyo basi huo utakuwa ni uongo mkubwa sana.
Unatakiwa ujipe muda wa kufikia mafanikio yako. Acha kuangalia njia za kutaka kujipatia utajiri wa haraka. Unatakiwa kuweka juhudi kila siku. Hata Roma kumbuka haikujengwa kwa siku moja na mafanikio pia yanataka mchakato vivyo hivyo.
Wakati mwingine inaweza ikakuchukua miaka 5, 10, 17 na hata 20 ili kuweza kufikia mafanikio makubwa uyatakayo. Usishangae huo ndio ukweli,  ila kama wewe wa kutaka mafanikio makubwa na ya haraka, jiandae mafanikio hayo yatakupoteza rafiki.

2. Fanya kile unachokiamini kitakupa mafanikio.
Usifanye hata siku moja kosa kwa kuamua kufanya kitu ambacho moyoni mwako unaona hakikupi mafanikio. Fanya kile ambacho unaamini kinakupa mafanikio, hata kama kitu hicho kinadharaulika sana kwa wengi.
Kwa kufanya kile kitu ambacho unaamini kitakupa mafanikio, naamini utaweka juhudi sana hadi kuweza kufikia mafanikio yako makubwa. Ila kama unataka kushindwa kabisa fanya kitu ambacho unaamini hakikupi mafanikio, utajuta.
3. Fanya kile unachokipenda.
Hakuna mafanikio makubwa utakayoweza kuyapata kwa wewe kufanya kile kitu usichokipenda. Najua hili tumeliongelea sana hapa, lakini nakukumbusha ili kufanikiwa unatakiwa kufanya jambo unalolipenda kwanza.
Ukiwaangalia watu wote wenye mafanikio wanafanya vitu wanavyovipenda kwani huko ndiko mafanikio makubwa yanapopatikana yaani inapotokea chanagamoto ni rahisi kuweza kupambana nayo mpaka kieleweke.
4. Boresha kile ukifanyacho kila siku.
Haijalishi kile unachokifanya ni bora kiasi gani, lakini maboresho kwa kile ukifanyacho ni muhimu sana, kama hautaweza kuboresha kile unachokifanya itafika mahali utakwama na hautaweza kusonga mbele sana.
Boresha kuanzia leo biashara yako, uandishi wako, akili yako kwa kujisomea kila siku ili uweze kusonga mbele. Kitu chochote ambacho hakina maboresho mafanikio yake ni ya muda mfupi sana na itafika wakati mafanikio hayo hupotea.
5. Jifunze kutokana na makosa yako.
Kwenye maisha hakuna kitu kinachoitwa ushindi wa moja kwa moja. Inabidi ifike mahali ukubali kujifunza kutokana na makosa pale unaposhindwa. Ukijifunza tu kutokana na makosa hiyo itakuwa ni fursa bora kwako ya kukusaidia kuweza kusonga mbele.
Naamini kwa kujifunza mambo hayo kuna kitu ambacho umetoka nacho na kimekusaidia kuweza kuchukua hatua ya kuweza kusonga mbele. Fanyia kazi hayo na ukumbuke kila unapotafuta mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







Nov 18, 2017

Ijue Msingi Ya Kuwa Mbunifu.

No comments :
Katika maisha yako yote ambayo unayaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu basi  utaendelea kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati  katika maisha yako ni lazima uwe mbunifu.
Ubunifu ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo tayakuwa ni ya kawaida tu.
Kwa sababu  katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu ambacho  unakifanya wewe kwa asilimia kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa mfanano wa vitu unazidi kuongezeka swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni, hivi natajitofautishaje na wenzangu?

Majibu ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha na wengine unachotakiwa kufanya ni kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja kifua mbele akaniuliza sasa afisa mipango huo ubunifu ni nini?
Pasipo kuona haya endapo niutaulizwa swali kama hilo jibu ambalo nitampa nitamwambia, ubunifu ni kuongeza thamani kwa kitu ambacho unakifanya, aidha kama  utashindwa kuongeza thamani basi utakiwa kuunda kitu kipya.
Katika swala kuunda kitu kipya hapa ndipo pamekuwapo na tatizo fulani kwa sababu watu wengi wanapenda sana ganda la ndizi kuteleza, kwa maneno mengine tunaweza kusema akili zao zimeganda hasa katika suala la kufikiria wao wamekuwa wanapenda sana kufanya ‘copy & paste.’ Kufanya hivyo ni kujipoteza mwenyewe hivyo unachotakiwa kufanya ni kwamba lazima uwe na misingi ya kubuni kitu cha kwako.
Pasipo kupoteza kusudio la mada yangu ya siku ya leo, niliona ni vyema niianze na utangulizi huo ili uelewe maana ya ubunifu. Mara baada ya kufahamua maana ya ubunifu basi naomba japo kwa dakika chache tuangalie misingi ya ubunifu  kama ifuatavyo.
1. Fanya kitu Unachokipenda.
Ukitaka kuwa mbunifu katika eneo lolote lile , kwanza ni lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho unakipenda. Ukifanya kitu ambacho unakipenda kwa asilimia zote, upo uhakika wa asilimia zote kwamba ni lazima utakuwa mbunifu ili kuwashinda washindani wako wanakuzunguka.
 2. Wekeza muda katika kuwaza na kutenda jambo hilo.
Ili uweze kuwa mbunifu katika jambo ambalo unalifanya jambo jingine ambalo unatakiwa kulizingatia ni kwamba ipo haja kubwa sana ya kuwekeza muda mwingi katika kuliwaza na kulitenda jambo hilo. Hivyo kwa kuwa umeamua kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba huku ukiamini ya kwamba ubunifu ndiyo ambao utakusaidia kuwa hivyo basi hakikisha ya kwamba unajipanga kikamilifu kuweza kujitoka kwa kuwekeza muda wako mwingi ili kuweza kulitimiza jambo hilo.
3. Jifunze vitu vipya vinavyoendana na jambo lako.
Jambo jingine ambalo litakufanya wewe uweze kuwa mbunifu ni kwamba ni lazima uhakikishe ya kwamba kila wakati huchoki kujifunza vitu vipya ambavyo vinaendana na jambo hilo. Sambamba na hilo kwa kuwa binadamu kwa asilimia kubwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kile alichojifunza kuweza kusahau, hivyo kwa kile ambacho unajifunza ni lazima uhakikishe ya kwamba unakiandika na uwe unakipitia mara kwa mara ili usikishau.
4. Jiulize maswali mara kwa mara.
Jambo la mwisho kati ya mengi yahusuyo somo hili ni kwamba kila wakati ni lazima uwe ni mtu wa kujiuliza maswali ya mara kwa mara. Moja kati ya swali muhimu ambalo unapaswa kujiuliza wewe katika misingi hii ya ubunifu ni, Je hivi nikifanya jambo hili nitapata faida gani?
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie ubunifu mwema na siku njema.
Ndimi: Afisa Mipango ; Benson Chonya
0757-909942

Nov 17, 2017

Sababu Tano Kwanini Watu Wengi Hawafanyi Kazi Zao Kwa Ufanisi Mkubwa.

No comments :
Si kitu cha ajabu, mara nyingi kumekuwa na malalamiko mengi kwa ‘mabosi,’ kulalamikia watu walio chini yao kwamba wanafanya kazi chini ya viwango, lakini si hivyo tu bali wanafanya pia kwa ufanisi mdogo sana, yaani hakuna ubora.
Ni tatizo ambalo limekuwa likiongelewa sana na kuhusishwa na uvivu, kwamba vijana wa siku hizi ni wavivu na hawataki kufanya kazi sana na tatizo hili limekua likikua siku hadi siku katika maeneo mengi makazini.
Je, kwa wewe binafsi, unafikiri chanzo cha tatizo hili ni nini? Kwa nini watu wanakwenda kazini karibu kila siku, lakini utendaji na ufanisi wao ni kidogo sana na hata hauridhishi kwa kiasi kikubwa kuweza kuleta mabadiliko.
Kiuhalisia zipo sababu kadhaa, ambazo moja kwa moja zinakuwa zinapelekea utendaji wa kazi kuweza kushuka sana kazini. Sitaki kukutajia sababu nyingi sana, katika somo hili nakutajia sababu tatu tu, kwa nini watu wengi hawafanyi kazi zao kwa ufanisi.
1. Mwingiliano wa mambo yasiyo ya msingi.
Ufanisi wa kazi kuna wakati unapungua sana kutokana na kuingiliana kwa mambo yasiyo ya msingi. Kwa mfano, utakuta mtu anafana kazi moja lakini wakati huo huo akili yake ipo kwenye kitu kingine kama simu au Tv au kuongea na watu wakati wa kazi.
Ufanisi katika kazi na kufanya kazi katika ubora hakuwezi kuja kwa namna hii. Ndio maana unatakiwa kila aina ya mwingiliano uweze kuutoa ili ufanisi uweze kuonekana kwa uwazi kabisa kwenye kila unachokifanya.
Sababu hii peke yake, ni chanzo kikubwa sana cha watu wengi kutokufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Matokeo ya hili ni kuendeleza kushindwa kwenye maisha. Kama unataka kufanya kazi kwa ufanisi na kufanikiwa, punguza mwingiliano wa mambo yasiyo ya msingi kwako.

2. Kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Pia kuna wakati ufanisi katika kazi unakufa kwa sababu ya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Inapofika kipindi wewe ni mtu mmoja halafu ukawa na kazi nyingi kwa wakati mmoja ni ngumu sana kuweza kuleta ufanisi.
Kitu cha muhimu kuzingatia hapa, ni kufanya kazi zako kwa utaratibu. Usijipe kazi nyingi kwa wakati mmoja, huko kutakuwa ni kujichosha na utapoteza ufanisi sana na usishangae hutaweza kupiga hatua kwa jambo hata moja.
Siri kubwa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele, chagua jambo moja na kisha jambo hiilo lifanye kwa uhakika sana. Nguvu na mawazo yako yote yaweke hapo mpaka jambo lako lilete matokeo na ufanisi mkubwa sana.
3. Kukosa hamasa kutoka kwa wanaowaongoza.
Kuna wakati kama unafanya kazi kwenye kampuni yaani uko chini ya mtu, unaweza ukakosa ufanisi kwa sababu ya kukosa hamasa kutoka kwa wanaokuongoza. Ni muhimu sana kwa watu wanaokuongoza au viongiozi wakatoa hamasa kubwa.
Pengine unajiuliza hamasa hii ni ipi? Ni muhimu na kwa viongozi pia nao kuweza kujitoa kufanya kazi ili kuonyesha mfano. Kinyume cha hapo unaweza ukakatishwa tamaa kwa kujiona kama hiyo kazi unayoifanya ni kazi yako tu peke yako.
Lakini kwa kushirikiana pamoja kuanzia viongozi hadi wafanyakazi wa kawaida ingawa kila mtu anakuwa anafanya kazi kwa sehemu yake hiyo itasaidia kukupa motisha na mwisho wa siku kuleta ufanisi mkubwa katika kazi.
Kimsingi, hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanapelekea moja kwa moja watu kuweza kufanya kazi chini ya ufanisi mkubwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







Nov 16, 2017

Maisha Yako Yanajengwa Sana Na Mambo Haya Matatu.

No comments :
Yapo mambo mengi ambayo yanajenga maisha yako au yanafanya maisha yako yawe kama hivyo yalivyo. Lakini hata hivyo pamoja na mambo hayo mengi, yapo mambo matatu ya msingi ambayo yanajenga maisha yako au ndio msingi wa maisha yako.
Kama utapuuzia ama hautaweza kujali mambo hayo matatu tu, basi kufanikiwa kwako kutakuwa ni kitu ambacho hakiwezekani. Mimi na wewe tunatengeneza mafanikio au kushindwa kwetu kupitia mambo hayo.
Sina shaka, una hamu ya kutaka kujua ni mambo gani ambayo yanapelekea maisha yako kujengwa. Sasa kamata kalamu na karatasi, kisha twende pamoja kwenye darasa kuweza kujifunza somo letu la leo.
Jambo la kwanza, mawazo yako.
Kila kitu unachokitaka kinaanzia kwenye mawazo yako. Hakuna jambo ambalo lipo duniani limeanzia nje ya mawazo. Mawazo yana mchango mkubwa katika kukupa chochote ukitakacho kwenye maisha yako.
Ukishindwa katika mawazo yako, na nje utashindwa pia. Ndio maana ili kufanikiwa unatakiwa kila wakati uwe na mawazo chanya sana, mawazo yakujenga, mawazo ambayo yatakutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine.
Na mawazo haya hayawezi kuja kwa bahati mabya tu, mawazo haya yanakuja kwa wewe kujilisha vitu chanya karibu kila siku. Unatakiwa ujifunze vitu chanya, unatakiwa uwe na marafiki chanya ambao watakusaidia kuwa na mawazo bora.
Kuendelea kuwa na mawazo yale yale ambayo yamekuweka hapo ulipo, ni sawa na kuchagua kupotea kwenye maisha yako. Kila siku hakikisha una mawazo bora yatakayoweza kukusaidia wewe kufanikiwa na si kukuangusha.

Jambo la pili, vitendo vyako.
Mawazo bora peke yake hata yawe mazuri vipi hayawezi kukusaidia kitu au hayawezi kukufikisha mbali. Kitu kingine ambacho kinajenga maisha yako kwa sehemu kubwa ni hatua unazozichukua kila siku.
Inatakiwa ujiulize hatua unazochukua kila siku hata kama ni kidogo sana lakini katika kuelekea ndoto zako ni zipi? Kama hakuna hatua unazochukua basi ujue sio unajenga maisha yako bali ndio unayaharibu kabisa na kuwa maisha ya hovyo.
Hakuna mafanikio ya kukaa tu, hakuna mafanikio ya kuyaongelea mdomoni, mafanikio yanajengwa kwa kuchukua hatua. Ukiona hakuna hatua unazochukua usijidanganye kwamba unatafuta na wewe mafanikio, maana wewe utakwama hata iweje.
Watu wanaochukua hatua karibu kila siku, watu hao ndio wanaofanikiwa na kujenga bahati kubwa katika maisha yao. Kwa hiyo unaona, vitendo ni kitu kimojawapo ambacho kina mchango mkubwa sana pia katika kujenga maisha yako.
Jambo la tatu, maneno yako.
Pamoja na kwamba una mawazo mawazo mazuri na una vitendo vizuri, lakini unatakiwa kukumbuka maneno yako pia yanamchango mkubwa sana katika kujenga maisha yako na yakaonekana kama hivyo yalivyo hapo.
Maisha ya wengi yamejengwa au kuharibiwa kutokana na maneno yao waliojinenea siku za nyuma. Ndio maana kabla hujaongea inabidi ujiulize unaongea kitu gani na je kitu hicho kinamchango upi katika kuelekea ndoto zako.
Unaweza ukawa mtabiri wa maisha yako, eidha kwa kwa kubomoa au kuyaumba. Maneno yako yanaumba sana maisha yako kwa sehemu kubwa. Ukijinenea vibaya, uelewe kabisa ndivyo maisha yako yataharibika kabisa.
Hivyo ni muhimu kuwa na uchaguzi wa maneno bora ili ikusaidie kuweza kufanikia. Usiwe mtabiri wa kuharibu maisha yako kila wakati. Jifunze kuwa mtabiri wa kuweza kukusaidia kujenga maisha yako.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanajenga maisha yako sana, ingawa ukienda kinyume na hapo ndivyo unaharibu maisha yako kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,