google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 30, 2016

Mbinu Za Kukuza Biashara Ndogo.

No comments :
Ni ukweli usiofichika zipo changamoto nyingi sana hasa pale unapukuwa unaanzisha biashara na kuitaka ifike mahali ikue na kujitegemea. Pamoja na changamoto nyingi kama za masoko au ushindani pia huwa ipo changamoto nyingine ya namna ya kukuza biashara yako.
Wafanyabiashara wengi wadogo inakuwa inafika mahali hujikuta wako palepale miaka nenda rudi bila kupiga hatua kubwa mbele. Hiyo yote hutokea hivyo kwa sababu wanakuwa wamekosa maarifa  ya kukuza biashara zao kwa namna moja au nyingine.
Kwa kusoma makala haya inakusaidia kujua mbinu zitakazo kusaidia kama wewe ni mfanyabiashara mdogo kuweza kukuza mtaji wako taratibu na kufika mahali na wewe ukawa na biashara yako kubwa kama wengine unavyowaona.  
Je, mbinu hizo ni zipi? Fuatana nami mwanzo hadi mwisho kuweza kuzijua mbinu hizo na kuzifanyia kazi.
1. Jitume sana.
Inawezekana biashara yako ikawa ni kuuza matunda. Pia inawezekana biashara yako ikawa ni ya uchuuzi yaani kutoa badhaa eneo moja na kuzipeleka eneo lingine kuziuza.
Sasa unapokuwa na biashara ndogo kama za namna hii, ili uweze kufanikiwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii sana na kujituma kwa nguvu zote bila kuchoka.

Kuwa mbunifu.
Ikiwa hautafanya hivyo ni lazima hautapiga hatua na biashara yako itakufa. Unajua ni kwa nini itakufa? Ni kwa sababu katika kipindi hiki biashara yako inapokuwa ndogo inataka uangalizi wa hali ya juu sana ili iweze kukua.
Hivyo, utalazimika kujituma sana na kufanya kila aina ya jitahada ambazo zitapelekea kuifanya biashara yako ikaweza kukua na kufika mahali ikajitegemea yenyewe.
2. Kuwa mbunifu.
Mbali na kujituma kapindi ambacho unakuwa una biashara ndogo, jitahidi uwe mbunifu. Unapokuwa mbunifu inakusidia sana kugundua ni kitu gani ambacho wateja wako wanataka au ni kipi ambacho hawataki. Hiyo ni njia bora sana itakayokusaidia kuboresha pale kwenye mapungufu na itakusaidia sana pia kuweza kuikuza biashara yako.
3. Sikiliza malalamiko ya wateja.
Ni vyema pia ukawa ni mtu wa busara kuweza kusikiliza kile ambacho wateja wako wanakisema katika kipindi hiki cha kukuza biashara yako. Hiyo itakusaidia kutimiza  matakwa yao na itakupelekea kuwa na wateja wengi ambao watasaidia kuifanya biashara yako ikue.
4. Tafuta msaada.
Katika kipindi cha kukuza bishara yako na kuifanya iwe kubwa, acha kujaribu kuishi kama kisiwa. Tafuta msaada wa ushauri kwa wale waliofanikiwa wakusaidie kimawazo wao walifanya nini hadi wakafikia huko waliko sasa.
5. Punguza utegemezi kwenye biashara yako.
Pia unapokuwa unaikuza biashara yako acha kutegemea sana pesa unayoipata kwenye biashara yako ndiyo iendeshee maisha yako. Jaribu kuwa na pesa nyingine, vinginevyo bila kufanya hivyo unaweza ukaua kila kitu bila kujijua.
6. Jifunze kukuza mtaji.
Kwa namna yoyote ili biashara yako ikue na ikafika mahali inajitegemea unalazimika sana  kujifunza mbinu za kukuza mataji wako. Hilo ni somo ambalo unatakiwa ulizingatie sanaa na kujiuliza kila wakati ni nini kifanyike ili mtaji uweze kukua.
kwa kifupi, hayo ndiyo baadhi ya mambo machache yanayoweza  kukusaidia kuweza kukuza bishara yako kama unaanzia chini.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.


Sep 29, 2016

Msingi Imara Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Ipo faida kubwa maishani mwako endapo utaamua leo kuchukua hatua mathubuti ya kutaka kufanikiwa. Tupo hivi tulivyo kwa sababu hututaki kuchua hatua sitahiki za kiutendaji kwa yale yalipo akilini mwetu na kuyaweka katika matendo. Watu wana maarifa lakini suala la kuyaweka maarifa hayo katika matendo.

Kuwepo kwa hali hii ndiyo ambayo inasababisha kuweza kuyatamani mafanikio na si kuyaishi. Hata hivyo moja ya siri nzito ya mafanikio yako husukumwa na kiu kubwa sana aliyonayo mtu  kutaka kufanikiwa, lakini kiu hiyohiyo huendana na msukumo na nia thabiti ya kuyaweka yale unayoyajua katika matendo.


Nasisitiza hili kwa sababu moja kubwa watu wengi wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wameamua hali hiyo kutokea, lakini ili kuondokana na hali hii huna budi leo hii kuacha kuishi kikawaida kwa sababu wewe sio mtu wa kawaida. 

Huenda ukawa unajiona wewe ni mnyonge katika maisha kwa sababu labda uliwahi kufeli kwenye jambo fulani ambalo ulitegemea ya kwamba litakupa matokeo chanya lakini matokeo yake yakawa kinyume chake. Lakini Amini usiamini ila ukweli ni kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa wao walikuwa ni watu ambao hawakutaka kuishi kikawaida. 

Hivyo hajalishi umefeli kwa kiwango gani ila lakini iambie nafsi yako ya kwamba wewe si mtu wa kukata tamaa bali ni mtu wa kusonga mbele kivitendo zaidi.

Tengeneza msingi bora wa mafanikio yako kwa kuamua kutokuwa wa kawaida.
Kuishi kikawaida ni sumu sana katika maisha yako. Wapo baadhi ya watu wamefeli kimaisha kwa sababu walikatishwa tamaa na watu wengine, huenda ukawa ni wewe ambaye unasoma makala haya ila ukweli ni kwamba maisha halisi ya kwako unayo wewe na si mtu mwingine haijalishi watasema nini ? Ila we songa mbele kivitendo ila pale unapofanikiwa wabaki midomo wazi.  Maana dunia hii imejaa wakatishaji tamaa.

Na kila mara tuzidi kuukumbuka ule usemi mtamu ambao unasema usiwambie watu ndoto yako, bali waosheshe ndoto hiyo kwa vitendo zaidi. Kwani kuwashirikisha watu juu ya ndoto yako, wapo baadhi ya watu endapo utawaambia jambo lako asilimia kubwa watakwambia haiwezekani.

Pia kwa kuwa maneno yana nguvu sana utajikuta kweli umeshindwa kuifanya hiyo ndoto yako . Simama imara kila mara kwa sababu wewe ni mshindi katika ulimwengu huu.

Kabla sijaweka nukta siku ya leo, nikandamizie maneno haya ya kwamba ili uweze kushinda vita vya umaskini, hautitaji uongozi imara kama ambavyo tumekalilishwa mashuleni, ila unahitaji kuwa bora kwa jambo lolote unalolifanya.

Kama ni biashara hakikisha unazalisha bidhaa yenye ubora kila mara, ukifanya hivi ni chachu kubwa sana ambayo itafanya wateja waongezeke wenyewe na si kuwa na kiongozi bora katika eneo lako unaloishi.


Nasema masuala haya ya uongozi  kwa sababu idadi kubwa wanahusisha masuala ya maisha yao kuwa magumu na masuala mazima ya uongozi, lakini ukweli ni kwamba ukifanya uchunguzi wa kutosha juu ya maisha yako utagundua ni nini ambacho nasema.

Maisha yako kuwa magumu usiyahusishe na masuala ya uongozi, bali tafakari katika kila kona ambayo unafanya kazi kwa kufikiri ni namna gani unaweza kuwa bora? Ukipata majawabu sahihi ya jinsi ya wewe kuwa bora hiyo siri kubwa ambayo ipo kwako ya wewe kufanikiwa.

Kama ni mwanafunzi fikiri jinsi ambavyo utakuwa bora katika taaluma yako, kama wewe ni msanii katika eneo lolote lile fikiri ambavyo utaweza kufanikiwa na sio kushirikisha imani potofu kutofanikiwa kwako na imani ambazo sio za msingi.

Dunia ni pana ila kwa maneno machache sana, kwa leo niishie hapo tukutane mara nyingine ambapo tutazidi kuelimishana masuala mazima ya mafanikio. Hivyo nikunong'oneze badili mfumo wa maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi.

Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.

Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.

TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.

Na; Afisa mipango Benson Chonya,

Sep 28, 2016

Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.

No comments :
Ili uweze kuishi maisha ya mafanikio makubwa kwako na kuwasaidia wengine ni lazima kwanza uwe huru kifedha. Unapokuwa upo huru kifedha ni hatua inayokufanya kuweza kutekeleza mahitaji yako yote ya kifedha, ikiwa pamoja na hata kusaidia wengine bila tatizo lolote lile.
Hivyo mpaka hapo unaona kwamba, ni lazima sana kuufikia uhuru wa kifedha ili kuishi maisha yenye manufaa kwetu na kwa wengine wanaotuzunguka. Sasa jambo la muhimu kuelewa hapa, tunawezaje kuufikia huo uhuru wa kifedha? Ni hatua zipi ambazo tunatakiwa tuzifuate?
Zifuatazo Ni Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.
1. Jiwekee malengo ya kifedha.
Tambua kwamba Ili kufikia uhuru wa kifedha, kabla ya kuanza kuwekeza, kuweka akiba, kutengeneza bajeti au kuweka pesa ya dharura, kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kujiwekea malengo ya kifedha. Hiki ni moja ya kitu muhimu sana katika kuufikia uhuru wa kifedha.

Jiwekee malengo ya kifedha.
Jiwekee malengo ya kifedha yaliyowazi na yanayoeleweka. Kwa mfano, unaweza ukajiwekea malengo  kwamba baada ya miaka mitano ijayo nataka kumiliki milioni mia moja. Pengine unaweza ukajiwekea malengo ya kifedha kwamba ili kutimiza lengo hilo, kila mwaka ni lazima niingize milioni ishirini.
Unapokuwa na malengo ya wazi kama hivi ya kifedha, inakuwa ni rahisi kwako kuufikia uhuru wa kifedha. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu unakuwa unajua unakotaka kufika kifedha na pia inakuwa sio rahisi kwako kupoteza pesa zako kwa mambo yasiyokusaidia kuufikia uhuru huo unaotaka.
Kwa hiyo, ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha, jambo la kwanza la kuzingatia, jiwekee malengo ya kifedha. Tafuta daftari lako la kumbukumbu na andika unahitaji pesa ngapi kwa mwaka, unahitaji pesa kiasi gani baada ya miaka mitano. Kwa kufanya hivyo utaufikia uhuru wa kifedha kwa sababu juhudi zako zitakuwa kubwa sana kukusaidia kutimiza lengo lako.
2. Tengeneza bajeti.
Mara baada ya kujiwekea malengo ya kifedha, hatua inayofuata ni  kutengeneza bajeti yako. katika hiyo bajeti utakayoitengeneza ni lazima uifuate na kuitekeleza kila siku. Unapokuwa unaifuata bajeti yako inakusaidia zaidi kuwa karibu na lengo lako la kuufikia uhuru wa kifedha.
Ili kufanikisha hili vizuri, kabla hujapata pesa andaa orodha ya vitu utakavyokwenda kununua kabla. Kisha baada ya hapo fanya manunuzi kama orodha yako inavyosema na sio kinyume chake. Kwa hiyo unaona, Kila unapokuwa na bajeti yako na ukaitekeleza, inasaidia kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu na inakuwa ni chanzo cha kuufikia uhuru wa kifedha.
3. Weka akiba.
Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi, jifunze kuweka akiba angalau kwa sehemu. Watu wengi hili ni somo gumu sana kulielewa juu ya uwekaji wa akiba na ni kiwazo kikubwa cha kuufikia uhuru wao wa kifedha.
Sasa kwa lugha rahisi ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni lazima uweke akiba. Unapokuwa unaweka akiba inakuwa inakusaidia sana kutengeneza mtaji kidogo kidogo kama huna mtaji huo au unaazia chini kabisa kimaisha.
 4. Jiwekee pesa ya dharura.
Hata uwe unaingiza pesa nyingi vipi lakini moja ya jambo ambalo unatakiwa kulifanya ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni kutenga fedha ya dharura. Kiuhalisia binadamu tunachangamoto nyingi sana. Hivyo ni lazima pesa hii uwe nayo unapoelekea kwenye uhuru wa kipesa.
Hakuna sababu ya kusema sina mtaji au sijawekeza katika hili kwa sababu pengine niliumwa na nikatumia pesa zote. Ili kuepuka ‘majanga’ kama hayo unatakiwa kujiwekea pesa ya dharura. Pesa hiyo inakuwa mkombozi wako kwa lolote linatokea ambalo hukupanga.  
5. Wekeza.
Sasa baada ya hatua hizo ambazo tumetoka kuzijadili, ili kuufikia uhuru wa kifedha kiuhakika hatua inayofuata ni kuwekeza. Bila kuwekeza itakuwa ni kazi ngumu sana kuweza kuufika uhuru wa kifedha.
Hapa ni lazima ukae chini na kutafuta ni kitu gani ambacho unakiwa ufanye au uwekeze na kikakuletea pesa nyingi. Kwa kitu hicho utakachokichagua, anza kukitekeleza mara moja kwani kitakufanikisha na kukupa uhuru wa kifedha.
Kama kweli nia yako ni kuufikia uhuru wa kifedha, unalazimika sana kujiwekea malengo ya kifedha, kutengeneza bajeti yako, kutenga pesa za dharura, kuweka akiba na kuwekeza katika eneo ambalo litakupa faida kubwa. Hizo ndizo hatua muhimu za kutengeneza uhuru wa kifedha.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,





Sep 27, 2016

Jinsi Ya Kupata Mafanikio Makubwa Kwa Kuboresha Mambo Haya Matatu.

No comments :
Kimsingi, mafanikio yoyote unayoyatafuta yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizo ndizo huamua ufanikiwe au usifanikiwe kwa kiasi gani kulingana na jinsi unavyozitumia.
Bila kuzijua kanuni hizo na kuzifanyia kazi, ni kazi bure utahangaika sana kutafuta mafanikio na utaambulia patupu. Wengi wanaoingia kichwa kichwa kutafuta mafanikio bila kuzijua kanuni hizo, huwa si rahisi sana kufanikiwa.
Kama ambavyo umekuwa uijifunza mara kwa mara kupitia mtandao huu, zipo kanuni nyingi za mafanikio ambazo unatakiwa kuzitumia na kuziishi kila siku ili zikuletee manufaa makubwa kwako.
Moja ya kanuni hizo za mafanikio, ambayo leo kupitia makala haya nataka ujue ni kanuni ya kuboresha. Hii ni moja ya kanuni ambayo ni rahisi, ila itakupa mafanikio makubwa sana endapo utaamua kuifanya iwe sehemu ya maisha yako.
Kivipi? Ipo hivi. Kanuni hii inatueleza, kwa chochote unachokifanya, kadri siku zinavyokwenda lazima ukiboreshe na kuwa bora kuliko mwanzoni au ulivyokuwa ukianza. Ulazima wa kufanya hivyo upo kwa sababu ya mabadiliko yanayotokea kila siku.
Boresha mbinu na bidhaa zako, pesa utapata tu.
Na mabadiliko yanapotokea yakakuta hujaboresha mambo yako vizuri,  kwa vyovyote vile ni lazima utakwama. Hivyo ndio maana unatakiwa kuwa bora kila wakati.
Lakini hata hivyo ili kanuni hii iweze kufanya vizuri na kukupa matokeo ya haraka, yapo maeneo ya msingi amabayo unatakiwa kuyaboresha. Kwa kuboresha maeneo haya ni lazima ufanikiwe.
Hebu bila kupoteza muda, twende pamoja kuangalia maeneo ambayo unatakiwa kuyaboresgha ili kujitengenezea mafanikio makubwa maishani mwako.
Kwanza, boresha bidhaa zako. Kama wewe ni mzalishaji au muuzaji wa bidhaa za aina fulani, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kujua ni kuboresha hizo bidhaa zako kwa kiwango cha juu sana.
Hakuna mteja ambaye anapenda kuuziwa kitu ambacho si kizuri au ni feki. Hivyo ili umshawishi awe mteja wako wa kudumu katika kipindi hiki cha ushindani ni lazima ujifunze kwa kiasi kikubwa kuboresha bidhaa zako kwa viwango vya juu.
Hebu jaribu kuangalia kampuni nyingi kitu kikubwa ambacho zinafanya, utakuta karibu kila siku wanaboresha bidhaa zao. Kama ni kampuni ya usafirishaji, utawaona kila wakati wanajitahidi kama ni mabasi yao kuyafanya yawe bora zaidi.
Kila kitu chenye mafanikio makubwa katika hii dunia ili kifanikiwe ni lazima kwanza kiboreshwe. Bila kuboreshwa hakuna mafanikio ambayo yanaweza kupatikana ya maana.
Pili, boresha mbinu zako. Kama ilivyokuwa kwenye kuboresha bidhaa zako, pia unalazimika kutumia kanuni ya  kuboresha mbinu zako ili kupata kile unachokipata sasa kwa uhakika mkubwa.
Ili uweze kuboresha mbinu zako, kila wakati jaribu kuwa mbunifu na kujiuliza ni njia gani nyingine unaweza ukaitumia na ikakupa mafanikio makubwa. Ukishaipata njia hiyo itumie mara moja.
Kwa jinsi utakavyozidi kuwa mbunifu na kuwaza tena na kuwaza, namna ya kuboresha njia nyingine za mafanikio, ni uhakika mafanikio utaanza kuyaona bila tabu yoyote. Kikubwa boresha sana mbinu zako.
Tatu, chukua jukumu la kujiboresha wewe. Hakuna unachoweza kukibadili katika maisha yako, ikiwa kama wewe mwenyewe umegoma kuchukua hatua zitakazopelekea uwe bora katika maisha yako.
Oooh unajiuliza linawezekana vipi? Ni rahisi tu kwa kujifunza kwa wengine na kujisomea karibu kila siku, ndivyo unazidi kuwa bora na kupelekea mafanikio ya wazi kutokea kwenye maisha yako.
Kama kuna eneo unajiona ni mdhaifu au huwezi kwa namna moja au nyingine, lifanyie kazi eneo hilo mara moja. Kwa mfano, unataka kuwa mwimbaji bora, fanya mazoezi kila siku bila kuchoka.
Kumbuka, hakuna mafanikio ya kubahatisha hata siku moja. Kama unataka mafanikio ni rahisi tu, fuata kanuni za mafanikio kila siku na hakikisha unaboresha mbinu zako, unaboresha bidhaa zako bila kusahau ni lazima wewe ujiboreshe pia wakati wote.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


Sep 26, 2016

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.

No comments :
Kuna wakati katika maisha unaweza ukajikuta una wazo la kufanya biashara au una wazo la kusoma kitabu au una wazo la kufanya kitu fulani kwa hamasa kubwa sana.
Lakini kitu cha kushangaza pale tu unapoanza kufanya jambo hilo, hamasa hiyo huanza kupungua kidogo kidogo na wakati mwingine hujikuta imeisha kabisa na wewe kujikuta huwezi tena kuendelea.
Wakati huo huo unakuwa unashangaa na kujiuliza sana, hamasa yote kubwa uliyokuwa nayo imekwenda wapi? Hapa kuna wakati unakuwa huelewi kabisa ni nini kilichopoteza hiyo hamasa?
Pia hata hivyo, unakuwa tena unashangaa kuwaona watu wengine wakifanya kitu hicho hicho, ambacho wewe umekishindwa. Tena unakuwa unajiuiza hamasa ya wao kufanya inatoka kwao wapi? Wakati wewe umeshindwa?
Kumbe, kitu usichokijua ni kwamba hamasa ni kitu ambacho huzaliwi nacho. Hakuna mtu ambaye anazaliwa akiwa na hamasa ya kufanya kila siku zaidi ya wewe kuamua kuitengeneza.
Inapofika mahali unajihisi kabisa umekosa hamasa, tambua kabisa ipo namna ambayo unaweza ukaiongeza hamasa hiyo. Lakini, kuongeza huko au kuchochea huko hamasa hakuji hivi hivi tu, mpaka uzingatie mambo muhimu ya kujenga hamasa.
Yafuatayo Ni Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.
1. Anza kwa kidogo.
Kwa chochote kile unachotaka kukifanya hata kama unahamasa nacho kubwa vipi, anza kidogo. Hiyo itakusaidia kutokuta tamaa au kukupunguza hamasa, endapo itatokea umepata matokeo ya tofauti.
Kwa jinsi unavyoanza kwa kidogo inakuwa sio rahisi kwako, kukosa hamasa kwa urahisi. Inatokea hivyo kwa sababu kila siku unavyofanya kwa kidogo, unakuwa unajitengenezea nguvu ya mwendelezo wa kusonga mbele.

Tafuta sababu ya kufanya.
2. Fanya jambo hilo kwa sababu.
Chochote unachokifanya ili kikujengee hamasa ya kudumu ni lazima uwe na sababu ya kufanya. Kosa wanalofanya watu wengi, sababu zinakuwa sio nzito sana au hazijitoshelezi.
Je, unaweza ukajiuliza binafsi, hilo jambo unalolifanya sasa, ni sababu ipi inayokuongoza hadi ukalifanya? Je, ni kwa sababu ya pesa au kwa sababu unalipenda au kwa sababu unataka kusaidia jamii? 

Ukishajua sababu inakuwa sio rahisi kwako kukata tamaa, hata pale yanapotokea mazingira ya kukatisha tamaa.
3. Kuwa na maono.
Wakati wengi wetu hamasa inapungua kwa sababu ya kushindwa kuwa na maono maalumu ya kule tunakokwenda na kile tunachokifanya. Lakini ikiwa maono yako wazi, ni rahisi kudumisha hamasa yako wakati wote.
Jaribu kujiuliza kama hicho unachokifanya kitakupa faida kubwa sana na pesa nyingi huko unakokwenda, je unaweza ukakiacha kwa urahisi? Ukiwa na picha ya namna hiyo itakusaidia sana wakati wote kujijengea hamasa ya kudumu maishani mwako.
4. Tengeneza tabia ya mwendelezo.
Kuna siku  tunajikuta kweli tumechoka na hatuwezi kufanya lile jambo tunalolifanya na akili inakuwa inatuambia tulia, utafanya kesho. Ukikubali kuisikiliza hiyo sauti, utapotea.
Kuwa na tabia ya kukifanya kile unachokifanya kila siku hata kama ni kwa dakika kumi tu inatosha. Haijalishi umejisikia au haujisikii wewe fanya.  Tengeneza mwendelezo wa kufanya kila siku(Consintence). Ikiwa utafanya hata pale ambapo hujisikii kufanya ni lazima utajenga hamasa yako sana.
5. Tumia kushindwa kama chanzo cha hamasa kubwa.
Hata inapotokea pale unaona kama umeshindwa, tumia kushindwa huko kama sababu kubwa ya kuelekea kwenye mafanikio yako. hakuna mtu ambaye hashindwi kwenye safari ya mafanikio.
Achana na habari ya kulalamika pale unashindwa zaidi ya kujifunza. Ukishalijua hilo, jifunze sana kutokana na makosa yako na chukua hatua ya kuweza kuendelea mbele hatua kwa hatua.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, hivyo ndivyo unavyoweza ukajikuta umejenga hamasa ya kudumu wakati wote katika maisha yako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

Sep 23, 2016

Fahamu Kwanini Kesho Si Rafiki Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Katika maisha yetu ya kila siku, neno "Kesho" linatumika sana kama njia pekee ya kuahirisha mambo mengi, ambayo kimsingi yalitakiwa yafanyike "leo" . 

Kesho ni miongoni mwa maneno yanayopendwa kutumiwa kama kinga ya kukataa kutimiza majukumu fulani ya leo. Badala ya mtu Kusema "HAPANA" Kitu hiki, utakuta mtu huyo anajibanza nyuma ya kesho, Huku akidhani Kuwa ataweza kufanya au kutimiza majukumu ya leo siku ya Kesho. 

Matokeo yake, kesho ikifika anasogeza tena mbele kwa sababu kuna kesho nyingi mbele yake. Kwa maneno mengine ni kwamba, tunahitaji kujiadhari sana na "kesho" kwani bila kufanya hivyo, tutajikuta kwenye hali ya umaskini mkubwa sana bila kujua.

Ni Ukweli usiopingika kuwa neno baya kuliko maneno mengine na linaloongoza kwa kuharibu maisha ya binadamu ni neno liitwalo "kesho". 

Watu wengi hasa maskini, watu ambao hawajafanikiwa, wasiokuwa na furaha, na wale wasiokuwa na afya njema ni kundi la watu ambao upendelea sana kutumia neno " Kesho" .


Anza siku yako leo, kama hakuna kesho.
Ndiyo maana watu wa namna hii, mara nyingi hupendelea kusema maneno kama"nitaanza uwekezaji kesho au " nitaanza kutumia lishe bora kesho " au nitaanza mazoezi ya kupunguza uzito Kesho! Wengine husikika wakisema" nitaanza kusoma labda kesho.

Ukichunguza kwa undani unagundua kuwa neno "Kesho" linatumika sana kumaanisha kuwa jambo fulani litaanza kufanyika siku ambayo siyo ya leo. Ndiyo maana utasikia nitaanza hiki siku Ya kesho, wiki, mwezi, mwaka kesho au wakati ujao.

Kwanini Watu hupendelea Kusema Kesho?

Sababu ni moja tu kwamba tunayo HULKA ya kupenda kufanya Vitu vingi kwa mara moja na ambavyo haviko hata kwenye mpango maalum. 

Tunapenda sana kufanya kazi kwa kufuata kasi ya matukio yanayoendelea kutokea. Kwahiyo, mambo au shughuli za leo zinapozidi uwezo unaamua kuzipeleka siku ya kesho. 

Kwa mfano unaweza kukuta kwamba kufika saa sita mchana ya leo, Tayari umekwisha kuahirisha shughuli nyingi za leo na kuzipeleka kesho. Lakini uzoefu unaonyesha kuwa unapoona kitu hujakifanya leo, basi ujue siyo muhimu.

Kuhusu kitu gani muhimu ufanye leo, hakiji hivi hivi, ni lazima shughuli zako nyingi za kila siku zifanyike kwa kulenga ndoto yako ya maisha yaweza kuwa ni miaka mitano, kumi au na zaidi.

Bila kuwa na ndoto au maono juu ya maisha unayotaka kuyaishi, Lazima utaendelea kufanya kazi zako nyingi kwa kufuata matukio ya siku husika. 

Mwisho wake kila utakapofanya Tathmini ya miaka 5 au 10 iliyopita unajikuta umezidi kurudi nyuma, hapo ndipo utaanza kutafuta wa kumlaumu. Kuchanganyikiwa kwa Watu Wengi ambako huambatana na msongo mkubwa wa Mawazo, mara nyingi huja kwa njia hii.  

Kwahiyo, ni muhimu sana kwetu tunaotaka maisha huru ya mafanikio kutambua kuwa vitu vyote muhimu kwa maisha yetu ni inatakiwa vinavyofanyika leo. 

Maisha yako siyo kesho, wiki, mwezi, mwaka au miaka kumi ijayo bali maisha halisi, ambayo una fursa ya kufanya kazi itakayo kuletea mafanikio makubwa siku za mbeleni ni leo.

Ni muhimu tukafanya yale yote yaliyo muhimu leo. Ukishatambua hilo, utakuwa wa kwanza kuona umuhimu wa kuianza siku yako mapema Alfajiri. 

Kushindwa katika maisha yako hakuji siku moja bali ni matokeo ya kushindwa kidogo kidogo kila siku. Ukiona umeshindwa au unakabiliwa na umaskini usifikiri ni jambo ambalo limetokea leo bali ni kutokana Na wewe kuchezea yale masaa ya kuanzia unapoamka hadi unapolala.

Kwa hiyo kwa maneno au lugha rahisi "LEO Ndiyo Dili" kubwa ya kubadili maisha yako. Hii ikiwa na maana kwamba tukifanya kazi sana leo tutapata ushindi au mafanikio kidogo na kesho tukifanya kama au zaidi ya leo tutapata mafanikio Kidogo.

Yale mafanikio kidogo kidogo tunayovuna kila siku ndiyo kwa ujumla wake yatatufanya kuwa na mafanikio makubwa miaka 5 au 10 ijayo na hapo ndipo Wengi watakapoanza kukutambua kwamba na wewe huwa upo!

Jitahidi kuipenda na kuikumbatia leo na uachane kuwa na mpenzi wa kesho kwasababu, neno Hili linaharibu sana maisha ya watu wengi kuliko maneno mengine.

Achana na neno "Kesho" kwasababu haitatokea uione kesho. Kesho huwa haipo. Kesho huwa ipo tu kwenye akili za watu waota ndoto bila vitendo na washindwaji.

Nimalizie kwa Kusema Kuwa sijawahi kuiona "Kesho" Kitu tulichonacho Pekee ni "Leo". LEO ni neno la washindi na Kesho ni neno la washindwa.

Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.

Makala hii imeandikwa na  Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP.





Sep 22, 2016

Jinsi Ya Kukabiliana Na Changamoto Ili Kupata Mafanikio.

No comments :
Kila mmoja anahitaji mafanikio makubwa kwa kile anachokifanya siku zote, japo tatizo huwa ni namna ya kukabiliana na changamoto zinazomsonga ili asifike malengo.

Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia. Changamoto hizi zimekuwa zikijitokeza katika biashara, elimu, kazini hata mara nyingine kufiwa na mtu ambaye ulikuwa una mtegemea kwa namna moja ama nyingine pamoja na changamoto nyingine nyingi.

Wakati mwingine changamoto zikitokea, wengi hukata tamaa na muda mwingine kujiona hufai kuendelea kuishi. Wapo wanaofikia hatua ya kukufuru kwa kutoa kauli kama vile Mungu anapendelea, dunia haina usawa na maneno mengine mengi yanayofanana na hayo.

Lakini wasichokielewa watu ni kwamba changamoto ni njia ya kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto huja ili kupima imani na uwezo wako kama kweli unaweza kupambana vitani.

Kabiliana na changamoto mpaka uzishinde.
Zifuatazo ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabiliana na changamoto katika maisha ya kila Siku;

Kwanza, zikubali changamoto; Kama nilivyoeleza hapo awali, changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo hakikisha na kisha utafute mbinu zakuweza kupambana nazo. 

Unaweza kuanzisha biashara, lakini katikati ya safari ukakimbiwa na wateja, jambo la msingi ni kufanya uchunguzi ni nini kimesababisha hali hiyo, ili uweze kuchukua hatua badala ya kulalamika na kuwanyoshea vidole wengine kwa kuona wao ndio chanzo.

Epuka kukimbilia kwenye imani za kishirikina au mitazamo potofu kama vile chuma ulete, nguvu za giza na mengineyo mengi kwani kufanya kinyume chake kwa kuamini imani hizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo.

Pili, tafuta washauri. Nafahamu ya kwamba baadhi yetu tuna watu wa karibu ambao huwa tunawaeleza shida zetu. Mfano wazazi, ndugu, marafiki na wengineo. 

Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linao kutatiza, kwani ni watu ambao wana nguvu sana katika jamii hususani suala zima la masuala ya ushauri hasa katika mambo yanayotutiza katika kufikia malengo yetu. Pia unaweza kujifunza kupitia mafunzo mbalimbali kama vile semina kwani kufanya hivyo utaweza kupata majibu ya changamoto zinazokukabili.

Vile vile katika utatuzi wa changamoto, watu wengi huwa tunakosea sana. Huwa tunaanza kuangalia matokeo ya jambo, badala ya kuangalia vyanzo ya matokeo hayo.

Nitaomba kukupa ufafanunuzi wa nukta hii kwa kuangalia mfano mdogo wa ugonjwa wa mlipuko maarafu kama kipindupindu ambao umekuwa ukizuka sana maeneo kadha wa kadha ikiwepo na jiji la Dar-es-salaam, ambapo kila kipindi cha muda fulani huzuka na kuwaathiri watu wengi.

Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuwa siku zote tunatibu  matokeo, yaani unapotikea viongozi serikalini wanajihimu kuandaa mazingira ya kuwapatia wagonjwa tiba.

Kufanya hivo ni kushughulika na matokeo ya tatizo na kuacha chanzo cha tatizo ambacho kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni wananchi kuendelea kuishi kwenye mazingira machafu yanayotoa mwanya watu kula vinyesi kitendo kinachosababisha with kuugua ugonjwa huo.

Tukifuata kanuni hii ya kuangalia chanzo kisha tuangalie matokeo, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda changamoto zinazotukabili katika shughuli zetu za kila siku iwe kwenye biashara, kazini, masomoni na maeneo mengine. 

Pia naomba usemi huu kila mara "usizibe ufa uktani kabla ya kujua chanzo cha ufa huo"

Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku. Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.

Ndimi: Benson chonya

Sep 21, 2016

Mambo Ya Kujifunza Pale Unapokosa Tumaini La Kufanikiwa.

No comments :
Kipo kipindi katika safari yako ya mafanikio kutokana pengine na changamoto za kimaisha, unajikuta unakata tamaa na matumaini yote yanapotea.
Katika kipindi hiki, kila unachokifanya kinakuwa hakileti matokeo na mbele yako unakuwa unaona giza na hakuna hata njia wala mwanga wa matumaini. Je, kwa hali  kama hii inapokutokea unafanyaje?
Kwa mfano, tuchukulie umeanzisha mradi fulani, lakini umejitahidi sana ili ukuletee angalau faida imeshindikana, hapo inapokuwa hivyo unawaza nini au unachukua hatua gani?
Najua kuna mambo mengi yanakuwa yanapita kichwani mwako, ikiwa nia pamoja na kuachana kabisa na kitu hicho ambacho sasa unaona hakifai tena na hakina manufaa kwako.
Lakini leo hapa kwa kupitia makala haya, naomba nikushirikishe mambo ya msingi ya kujifunza hasa inapotokea pale umekata tamaa na kukosa matumaini  kwa kile unachokifanya.

Unapokosa tumaini, panga mipango yako upya.
Jambo la kwanza unalotakiwa kujifunza na kulitambua  ni kwamba hakuna mafanikio ya mara moja. Hapa hii yote inatuonyesha ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tujaribu tena na tena hadi kufikia mafanikio.
Inapotokea unaona kama umekosa tumaini unaonyeshwa kwamba sasa huu sio wakati wa kutulia na kujiona mnyonge uliyopoteza karibu kila kitu, bali ni wakati wa kunyanyuka tena na kujaribu njia zingine za kukupa mafanikio yako.
Jambo la pili unalotakiwa kujifunza ni kwamba katika maisha hakuna kukata tamaa. Ni kweli, unakuwa unajiona umekosa matumaini na huna chako tena, lakini ni wakati wako wa kijiamini tena na kushikiria ndoto zako upya mpaka kufanikiwa.
Hata kama unaona dunia na kila hali kama imekutenga, jifunze hapo ulipo sio ndio mwisho wa mafanikio yako ipo nafasi ya kufanya tena na ukafanikiwa sana kuliko unavyofikiri.  
Jambo la tatu la kujifunza hasa pale unapokosa matumaini tena ni panga mipango yako upya. Hiki hasa ndicho kitu ambacho unachokuwa unaambiwa na maisha.
Badala ya kukaa chini na kulia na kuanza kulalamika kwa kushindwa kwako kufanikiwa, lakini unachoambiwa na maisha panga mipango yako upya, tafuta njia nyingine na tumia akili yako vizuri hadi ufanikiwe.
Tambua, ili kufanikiwa inatakiwa ujue hakuna mafanikio ya mara moja, hakuna kukata tamaa na inabidi kila wakati kupanga mipango upya.  Hayo ndiyo mambo ya msingi  unayotakiwa ujifunze hasa pale unapokata tamaa na kukosa.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.


Sep 20, 2016

Faida Kubwa Za Kujijengea Mtazamo Chanya.

No comments :
Kuna jambo kubwa sana ambalo linaweza kubadili maisha yako ndani ya muda mfupi, ambalo siku ya leo ni vyema kulifahamu, na si kulifahamu tu bali kuamua kulichukua jambo hili na kulifanya libadili maisha na jambo lenyewe si jingine bali ni mtazamo ulionao.

Mtazamo ni vile ambavyo unaamini huenda ikawa ni katika fikra chanya au fikra hasi. Lakini katika makala haya nitazungumzia umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, kwani mitazamo ya watu ndio ambayo humueleza kwa undani zaidi ni kwa njisi gani mtu alivyo kutokana na vitu ambavyo anavyovifanya na asivyovifanya.

Na jambo hilo huleta tofauti uliyopo kati ya walinacho na wasionacho, na tofauti hiyo ni kwamba waliofanikiwa wao wanaamini ya kwamba katika dunia hii hakuna kisichowezekana ila watu ambao hawajafanikiwa wao huamini ya kwamba mambo  mengine hayawezekani hii ni kutokana wao hukata tamaa mapema zaidi kabla ya kuanza kufanya, hali hii hutokea kwa sababu watu wengi ambao maisha yao duni huishi kwa kuogopa sana wakati ujao.

Jenga mtazamo chanya, ukusaidie.
Pia akili za mwanadamu zimetawaliwa kwa kiwango kikubwa na vitu ambavyo havionekani, hapa ndipo lile somo la kujipa majibu hasi linapofanya kazi, kwa vitu ambavyo anaviwaza ambavyo kimsingi bado havijawekwa katika utekelezaji.

Kwa mfano unakuta mtu ana mawazo mengi ambayo ukiyatazama kwa "jicho la tofauti" mawazo hayo yatawezwa kubadilishwa na kuwa katika matendo yana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha maisha ya mhusika huyo kwa asilimia mia moja, ila changamoto kubwa pindi mtu awazapo huanza kuja na vikwazo ambavyo kimsingi huwa na vitu ambavyo havimpi nguvu ya kuthubutu kutenda jambo hilo.

Hii huwa ni ishara mawazo yetu huwa ni chanya mara nyingi lakini suala zima la utekelezaji wa suala hilo huwa ni kikwazo kikubwa, lakini nikwambie neno moja ya kwamba kuanza sasa unahitaji ubongo wa ziada.

Unaweza ukajiuliza ubongo wa ziada labda ni kuwa na ubongo mwingine, la hasha sina maana hiyo ila ukweli ni kwamba uanze kufikiria katika akili nyingine ambayo itakufanya uwe mpya, katika fikra mpya hususani suala zima la kuwa na mtazamo chanya.

Inawezekana ukajiuliza unawezaje kuwa mtazamo chanya?

Suala zima kuwa mtazamo chanya huwa linatokana na kujiuliza katika mambo ambayo unayofanya, je mambo hayo yana matokeo gani katika maisha yako na watu wengine?

Watu ambao wanakuzungua huwa wanatazamo gani juu yako? Na mara zote ikumbukwe ya kwamba maisha yako yanatazamwa kwa asilimia kubwa na watu wengine, watu wanaokuzunguka wakikutazama katika jicho chanya hata kile kitu ambacho unakifanya kinaweza katika kuwa bora zaidi. 

Ifike pahala jamii ambayo inakutazama wakufikirie kwamba ni mtu chanya, kufanya hivi kutakufanya uweze kujitangaza jina na kujiongezea thamani.

Amua sasa kutenga muda wa kujiuliza mambo ya msingi ambayo yatakusaidia kuwa na mtazamo chanya kwa kila jambo amabalo unakiwaza au ambalo unalitenda. Pia ikumbukwe ya kwamba ni vyema ukaamua kubadili maisha yako kwa kuwa na mtazamo sahihi.

Afisa mipango Benson Chonya.
0757909942