google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 11, 2019

Tabia Muhimu Zitakazokusaidia Kukupa Mafanikio Kwa Kiasi Kikubwa.

No comments :
Moja ya sheria ya msingi na ya muhimu katika mafanikio yoyote yale ni kuwa na tabia nzuri. Tabia ni moja ya kitu ambacho ni cha msingi sana katika kukupa mafanikio yale uyatakayo. Ukiangalia wengi wanaoshindwa, chanzo kinaanzia kwenye tabia zao.
Tuchukulie kwa mtu anayataka mafanikio, kuwa na malengo tu peke yake na kuyafanyia kazi haitoshi, lazima mtu huyu awe na tabia zinazoendana na malengo hayo, kama kuwa na matumizi mazuri ya pesa au utunzaji wa muda mzuri.
Unapokuwa na tabia mbaya na huku ukitaka mafaniko, ni wazi hutaweza kufanikiwa na utahangaika sana kufikia mafanikio hayo. Mpaka hapo unaona tabia ni kitu cha msingi sana katika kukufanikisha wewe kwenye maisha yako.
Unaweza ukawa na mafanikio makubwa sana, ikiwa utajenga tabia bora za kukusaidia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kila wakati. Je, unataka kuzijua tabia hizi ni zipi za kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa?

1. Tabia ya kutafuta msaada.
Hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa akiwa peke yake. Kila mtu anahitaji msaada kwa mtu mwingine hata kama msaada huo ni kidogo sana lakini msaada huo unahitajika ili kuweza kujenga mafanikio ya kudumu.
Unapokuwa unawasiliana na wengine na wakajua changamoto zako, ni rahisi sana kwa wao kuweza kukusaidia wewe na kupiga hatua mbele za kimafanikio. Usijaribu kuishi kipeke yako yako, tafuta msaada kwa wengine na utafanikiwa pia.
2. Tabia ya kuchukua hatua.
Unayo nafasi kubwa sana ya kufikia mafanikio yoyote yale unayoyataka kwenye maisha, lakini kama huchukui hatua nikwambie tu, utakufa kwa msongo wa mawazo. Najua una mawazo mazuri lakini hayawezi kufanya kazi mpaka uchukue hatua.
Huhitaji kuwa na hamasa ili uchukue hatua, wewe chukua hatua kwa hali yoyote uliyonayo. Acha kuendelea kufikiria sana juu ya ndoto zako, chukua hatua. Soma vitu vya kukusaidia na kisha amua kuchukua hatua na ukijenga tabia hii itakusaidia sana.
3. Tabia ya kutokuishi kimazoea.
Maisha ya watu wengi yanakuwa mabaya kwa sababu ya kuishi sana kimazoea. Kuishi kimazoea ni sumu kubwa sana ya wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa. Unatakiwa ujue namna ya kuishi nje ya mazoea yako ili uweze kufanikiwa zaidi.
Kila wakati tafuta namna ambayo itakusaidia wewe kuweza kuishi nje ya mazoea yako. Ikiwa lakini kila wakati unaishi kwenye mazea hayo hayo itakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kusonga mbele na kupigia hatua hasa za kimafanikio.
4. Tabia ya kusema hapana.
Hii ni moja ya tabia nzuri sana kwako wewe kuindeleza ili kufikia mafamikio. Unatakiwa kujifunza kusema hapana kwa mambo mengi sana. Unatakiwa ujue kusema hapana kwa wanaokupotezea muda wako au kwa yale mambo usiyoyahitaji.
Ikiwa wewe utakuwa ni mtu wa kukubali kila kitu, kwamba kitu hiki kiwe hivi au vile ni ngumu sana kuweza kupiga hatua sahihi za kimafanikioo husika. Jifunze kusema hapana kwa kila kitu ambacho hakina manufaa kwako wewe.
5. Tabia ya kuchukua majukumu yako.
Unatakiwa ujue kila mtu ana changamoto zake za kimaisha, lakini kama unashindwa kuwajibika na majukumu hayo na kila wakati kutaka kulaumu tu watu wengine, hilo tu nikwambie utakuwa ni miongoni mwa watu ambao watashindwa sana.
Nikwambie tu, kubali kuwajibika kwa kila jambo linalokuhusu wewe. Wajibika kwenye ndoto zako, wajibika kwenye maisha yako ya kila siku. Kila wakati ujue jinsi ya kuwajibika na hapo utaweza kupiga hatua za mafanikio sahihi kwako.
Hivi ndivyo unavyoweza ukatumia tabia hizo vizuri na zikakusaidia wewe kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye maisha yako kama unavyotaka iwe. Ni jukumu lako wewe sasa kuchukua hatua na kuhakikisha unasonga mbele.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,






Mar 10, 2019

Ikiwa Unaishi Hivi, Maisha Yako Ni Mafupi Sana.

No comments :
Ni jambo ambalo watu hulisema  mara nyingi bila kujua maana yake. Unaweza kukuta mtu akisema, ‘ndio maana amekauka, ana roho mbaya sana’. Ukimuuliza ni kwa nini anahusisha kukauka au afya mbaya na roho mbaya au kukosa upendo alikonako mtu, hataweza kukupa jibu sahihi. Lakini, anajua kwamba, kukauka huwapata wenye roho mbaya. Kauli hiyo ina ukweli mkubwa wa kutosha. Watu wengi ambao wanatengeneza nguvu nyingi hasi, hatimaye nguvu hizo huwarudia na kuwadhuru.

Kwa sehemu kubwa, madhara ya nguvu  hizo huja kujitokeza kwenye miili yao. Mtu ambaye anaumwa mara kwa mara, anaweza kuwa anaumwa tu kwa sababu nyingine, lakini pia anaweza kuwa anaumwa kutokana na nguvu hasi anazotengeneza. Nikisema nguvu hasi, nina maana ya kufikiri na matendo ambayo yanamuumiza mwenye mawazo na matendo hayo, pia wale wanaomzunguka. Kwa mfano, mtu asiyeweza kusamehe, mwenye visasi, mwenye kijicho, mpenda makuu, mshindani na mengine ya aina hiyo.

 Kuna watu ambao hutengeneza sana nguvu hasi kwa kufikiri kwao na tabia zao. Kwa kawaida, nguvu hasi huwa zinadhuru hisia na mwili wa mhusika. Kwa vipi? Hebu tutazame kushindwa kusamehe na kijicho. Mtu ambaye hawezi kusamehe, anajiweka mahali ambapo muda wote anakuwa kwenye hasira, hisia chungu na mikakati ya kulipa kisasi. Hii ni sawa na mtu ambaye ana kijicho, kwa mfano. Huyu naye, muda mwingi wa maisha yake, atakuwa akiumia kwani, kila wengine wakifanikiwa kwa chochote, atajihisi vibaya tu. kwa hiyo, hisia zake zitakuwa zinachokozeka karibu muda wote.

Kwa kawaida, hisia zetu zinapochokozeka, tunaiiingiza miili yetu kwenye kuzalisha kemikali au homoni ambazo wakati huo hazihitajiwi. Kwa uzalishwaji huo wa kemikali zisizohitajika mwilini, tunaiumiza miili yetu kwa njia mbalimbali. Kemikali hizo, hatimaye huanza kutuumiza kwa kuteleta maradhi mvalimbali miilini mwetu. Hili ni jamba ambalo limethibitishwa kitaalamu.


Kuna maradhi zaidi ya kumi ambayo chanzo chake ni mihemko yetu, maradhi ambayo kitaalamu hufahamika kama Emotionally Induced Diseases. Haya ni pamoja na maumivu ya mwili, tumbo, kufunga choo na mengine. Ndiyo maana, wale watu wote wanaokwenda hospitalini wakiwa wanaumwa, ambao wanaambiwa vipimo havioneshi maradhi yoyote, ukiwachunguza, utagundua kwamba, wanakabiliwa na hofu, mashaka, visasi  na matatizo mengine ya kihisia.

Sisemi kwamba, wote wanaopimwa na kuonekana hawana maradhi ndivyo walivyo, hapana. Lakini wengi kati yao ndivyo walivyo. Hata wale wanaodaiwa kuwa na mapepo pia, utakuta baadhi ni wale wenye hisia chungu. Kwa sababu ya maumivu ya kimwili na yale ya kiakili, unakuta watu hawa wakiwa dhaifu. Kama walivyo wagonjwa wengine, suala la udhaifu wa kimwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa mara kwa mara.

Ni rahisi kwa hali hiyo, watu wenye roho mbaya kukauka au kukosa afya imara. Ingawa siyo kweli hata hivyo kuwa watu wote wenye afya mbovu, inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini, kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu hasi, ni rahisi zaidi kwao kukosa afya bora kama tulivyoona. Ndiyo maana tunasema hivi, kama unaishi maisha haya kuwa na roho mbaya tu, maisha yako ni mafupi kwa sababu utakuwa ni wa afya mbovu kitu ambacho ni hatari sana kwako.

Nakutakia kheri ya mwaka mpya, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,




Mar 9, 2019

Kama Mambo Yako Yako Hovyo, Yaweke Sawa Kwa Kufanya Hivi.

No comments :
Ikiwa kuna wakati unaona maisha yanakuchanganya hasa kutokana na changamoto unazokutana nazo, usije ukakubali ukafanya kosa la kuchanganywa huko, badala yake tuliza akili yako na tafuta mwelekeo sahihi wa maisha yako kwa kuweka mambo sawa.
Ikiwa unaona pia unaweka juhudi nyingi sana na juhudi hizo hazikupi matunda sahihi, hapa tena usikatishwe tamaa, endelea kuweka juhudi, lakini tafuta kuelewa kwa nini juhudi zako hazikufanikishi na anza kutafuta njia nyingine itakayokupa matokeo makubwa kwako na kuweka mambo sawa.
Upo wakati katika maisha yako ambapo kuna mtu au watu  watakurudisha nyuma hata bila ya wewe kutegemea. Inapotokea wakati kama huu, sio swala la kutupa lawana na kusikitika, bali ni kuuvaa ujasiri na ushujaa na kutafuta mwelekeo upya kwa kuweka mambo yako sawa.
Kuna wakati katika  maisha yako unajiona upo njia panda, huelewi hata ufanye nini, inapofika wakati huu , jifunze kuweka nguvu za uzingativu katika kitu kimoja na kutafuta mwelekeo sahihi utakaokusaidia kuweka mambo yako sawa na yakae katika mkao wa mafanikio.
Zipo nguvu nyingi na kubwa sana katika maisha yako, ambapo nguvu hizo zinauwezo wa kubali hali yoyote ambayo unayo na unaona ni  mbaya na nguvu hizo hadi kukupa mafanikio halisi kama vile unavyotaka iwe.
Ndio maana, badala ya kulalamika na kutoa kila aina ya visingizio, jitahidi sana kuweka mambo yako sawa, kila unapoweka juhudi ya kuweka mambo yako sawa, utajifunza na kugundua kwamba kumbe unaweza ukatawala maisha yako kwa jinsi unavyotaka.
Je, katika maisha yako kuna kipi ambacho unakiona ndio tena basi kimeharibika na hakiwezi kukusaidia hata kufanikiwa. Kama kipo kitu cha namna hiyo, anza kikiweka sawa na kutafuta njia ya itakayofanya kitu hicho kikupe matunda uyatakayo.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Mar 8, 2019

Kama Utaruhusu Kelele Hizi…Utashindwa Kufanikiwa.

No comments :

Usisikilize kila kitu
Zipo kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia kile, ilimradi kukicha tu zipo habari na taarifa nyingi ambazo zinatolewa ambazo lengo lake wewe uzisikie na pengine kuzifanyia kazi.
Usipokuwa makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya kuweza kujiokoa na kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele.
Simamia na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na utafanikiwa. Kuendelea kusikiliza kelele au kila linalosemwa utakuwa ni sawa na mtu ambaye ameamua kujipoteza yeye mwenyewe.
Katika dunia ya sasa, ni rahisi sana kusikia fursa hii au ile, lakini kwa ukweli uliowazi wewe kama wewe huwezi kufanya kila kitu. Kama ni fursa ni lazima utafanya chache na si kila fursa itakuwa yako.
Hivyo unatakiwa kuwa makini na taarifa unazozipokea. Unatakiwa kuwa mtulivu na usiwe mtu ambaye unaendeshwa na mihemiko isiyo ya maana. Kelele za dunia zisikuyumbishe hata kidogo, fuata malengo yako.
Ikitokea umekubali kuyumbishwa na dunia au na kelele za dunia, basi utaishi kama bendera fuata upepo maana hutafika popote. Utagusa hiki mara kile na kila kitu utakuwa unakianza na kukiacha kila ukisikia kuna kingine kizuri kinalipa.
Kuanzia leo jifunze kuweka masikio yako pamba, jifunze kuweka nguvu zako za uzingativu eneo moja, mahali ambapo utafanya kitu na kitaonekana cha thamani. Ukiziba masikio usisikie kitu, utajenga uwezo mkubwa wa kufanikiwa.
Chukua hatua kwa kufanyia kazi hicho ulichojifunza na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza na kuhamasika zaidi kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

Mar 7, 2019

Sehemu Sahihi Ya Kuanzia Mafanikio Yako Ni Hii Hapa.

No comments :
Bila kujali upo mbali kimafanikio kwa kiasi gani, lakini bado unayo nafasi ya kuchagua kuendelea mbele kwenye safari ya mafanikio yako.
Si kitu cha ajabu sana kwako na kwa wengine pia wanapoona wako mbali kimafanikio, hasa kwa kuwalinganisha na wengine wanaanza kukata tamaa.
Kitu ambacho watu hawa wanakuwa hawajui ni kwamba, mafanikio hayategemei sana au hayajali eti upo umbali gani, bali kinachojalisha ni mwelekeo wako.
Mwelekeo ndio kitu cha msingi sana katika safari yako ya mafanikio. Hiyo ikiwa na maana pale ulipo kwa sasa unaelekea wapi kimafanikio.
Kama mwelekeo wako ni sahihi, basi hakuna shaka hata kama mwendo wako ni kidogo kama wa kinyonga lakini wakati upo utafanikiwa.

Kikubwa ambacho hutakiwi kukipoteza kwenye maisha yako ni ule mwelekeo wa kule unakoenda kwenye maisha yako. Ukipoteza mwelekeo ndio basi huwezi kufanikiwa.
Watu wengi hawafanikiwi katika maisha sio kwa sababu ya kwamba wapo mbali kwa hiyo ni ngumu kufanikiwa. Hawafanikiwi kwa sababu hawana mwelekeo.
Hata katika mazingira ya kawaida kitu chochote kikikosa mwelekeo hakiwezi kufika kule kinakotakiwa kufika, lazima kitapotea hapa katikati.
Kwa mfano, ukiangalia ndenge inaporuka hewani inakuwa na mwelekeo fulani unaongozwa na rubani. Inapotokea mwelekeo huo haupo, basi ndege haiwezi kufika.
Na maisha yako hayana tofauti sana na hivyo. Maisha yako yanahitajji mwelekeo kwanza na sio wapi ulipo kimaisha ndio hatma yako iamulie.
Kama umekuwa bado unasingizia kwamba eti uko mbali kimaisha na ndio maana hufanikiwi, huo sio ukweli ni uongo.
Wewe sehemu ya kuanzia kwenye safari yako ya mafanikio ni kutafuta mwelekeo. Ukiupata mwelekeo basi njia kuu ya mafanikio umeiona.
Inatakiwa sasa kujiuliza karibu kila siku, mwelekeo wa maisha yako uko wapi. Kitu gani utakachofanya ambacho kitakupa mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Hutakiwi kulaumu hata siku moja pale ulipo, unatakiwa ushukuru kwanza, kwani sehemu ulipo hapo ndipo unatakiwa kuanza kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Hutaweza kufanikiwa kama hautataka  kuanza kutafuta mwelekeo wako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio kama nilivyosema ni kujua mwelekeo wako pale ulipo.
Hakuna kitu ambacho kitaweza kushindikaa kwako, kwa sababu utakuwa umeamua kutafuta kwa dhati sehemu ya kuanza kutafuta mfanikio yako.
Amua leo iwe siku ya kuanza kutafuta sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako kwa kutafuta mwelekeo wa wapi uende.
Usiruhusu mtu akwambie huwezi kufika kule unakotaka kufika kimafanikio, wakati una uwezo wa kuanza kutafuta mwelekeo wako na kusonga mbele unao.
Usiruhusu mtu akakukatisha tamaa iwe kwa vitendo au kwa chochote kile kwamba wewe upo mbali sana na hautaweza kufanikiwa.
Usiruhusu tena wewe mwenyewe ndani yako ukajiambia kwamba, kwa maisha haya niliyonayo ndio basi tena siwezi kufanikiwa.
Hautakiwi kuruhusu chochote kile ndio kiwe kikwazo chanzo cha wewe kushindwa kuwa na mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Kila wakati unatakiwa kujua ule uwezo wa kufanikiwa na kufika ngazi ya juu kimafanikio unao,  kwa sababu sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako umeshaiona.
Kama kuna watu wao wanaendelea kukubeza, waache waendelea kukubeza na hiyo itakula kwao, wewe endelea kuchanja mbuga kutafuta mwelekeo wako kimafanikio.
Hutakiwi tena kujiuliza uliza au kumuuuliza mtu kwamba ni wapi mafanikio yako  yanaweza kuanzia au ni sehemu gani.
Kitu cha kukumbuka ulichojifunza hapa ni kwamba, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako ni kwa wewe kuchukua hatua za kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,











\