google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 31, 2017

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Usijitupe Kwenye Moto Kwa Sababu Ya Kuogopa Moshi.

No comments :
Ni wakati na siku njema tena , na kukaribisha katika siku ya leo katika jukwaaa letu la hekima za maisha na mafanikio. Kama siku zote ambavyo nimekuwa nikikukumbusha, hekima za maisha na mafanikio ni sehemu ya kujifunza busara na hekima za maisha.
Hilo linakujaje au kivipi? Ni rahisi tu, ni kupitia misemo au maneno ambayo yaliweza kuzungumzwa na babu zetu enzi za kale. Kwa kujifunza huko nasi tunatoka na vitu ambavyo ni adimu lakini, vinatukomaza na kutufanya tupige hatua.
Naomba nikukaribishe jamvini, vua viatu vyako hapo ulipo, karibu kwenye mkeka wangu hapa nilipo, ili nikukaribishe kwa moyo mkunjufu na tuweze kujiunga pamoja tufunzane juu ya hekima za maisha na mafanikio za siku hii ya leo.

Hekima ya 1; Anaye elewa vibaya ni yule anayesikiliza vibaya.
Kuna watu ambao unaweza ukasema jambo na ukarudia tena na tena huku wao kazi yao ikiwa ni kuitika tu mara mbilimbili. Katika hekima yetu hii, inatuonyesha kwamba anayelewa vibaya ni yule ambaye anasikiliza vibaya pia.
Hii ikiwa na maana kama wewe ni msikilizaji mzuri, ni lazima na kwako utaweza kulewa vizuri kile ambacho kimesemwa. Ikiwa lakini utaenda kinyume, basi ni lazima kwako utakuwa unaelewa vibaya kila wakati.
Hekima yetu inatukumbusha umuhimu wa kutega masikio vizuri pale jambo linaposemwa na mtu mwingine. Ni vyema kuachana karibu na kila kitu na kujenga usikivu mkuu ili kusikiliza vizuri ili kuepuka kulewa vibaya.
Hekima ya 2; Usijitupe kwenye moto kwa sababu ya kuogopa moshi.
Hii pia ni moja ya hekima ya maisha na mafanikio iliyotolewa na wahenga wa kale ambayo inakutaka sana na kukusihi usije ukajitupa kwenye moto kisa na sababu kubwa ni kwa wewe kuogopa moshi.
Hekima hii ukiiangalia ina chekesha kidogo, lakini ujiulize ina maana gani kwetu? au inafunzo gani kwetu ambalo ni kubwa? Hapa ukichunguza tunaonywa kwamba usije ukajiingiza kwenye matatizo makubwa sana kwa sababu ya kitu kidogo tu.
Hekima hii inawaonya watu wale ambao wakipata tatizo wanakimbilia kujidhuru, ambapo madhara yake yanakuwa makubwa kuliko hata ya tatizo lenyewe, hivyo inakuwa ni sawa na kujirusha kwenye moto kwa sababu ya kukwepa moshi.
3. Imara ya jembe kaingoje shamba.
Siku zote inaeleweka hivi, iwapo jembe ni imara hujulikana pale linapolima shambani. Hiyo ikiwa na maana, udhaifu wa mtu au kitu, huthibitika sana pale mtu au kitu hicho kinapokuwa kazini na si vinginevyo.
Hapa tahadhari kubwa tunayopewa na maneno haya ya hekima ni kwamba, tusikithamini sana kitu kwa sababu ya maneno au kujidai kwake, thamamini kitu au mtu kwa sababu ya kazi, au uwezo wake.
Kuna watu kwa sababu ya tabia au huluka zao, hujikuta ni watu wa kujidai sana na kutoa kila tambo za maneno kwamba wanaweza kitu fulani, lakini kumbe kiutendaji hakuna kitu. Hapa unatakiwa kuwa makini na kuangalia uimara wao kwenye kazi na si maneno peke yake.
4. Heri kupata mkate nusu kuliko kutokupata kabisa.
Funzo kubwa tunalolipata kupitia hekima hii ya maisha ya mafanikio ni kwamba, kile kidogo ulichonacho ni bora na ni nafuu sana kuliko kukosa kabisa. Huhitaji kukiona ni duni sana wakati unacho, unatakiwa kushukuru hata kwa hicho kwani kitakusaidia.
Wapo watu ambao wao ni kunung’unika tu, wakati ukiwaangalia kuna kitu ambacho wamekipata. Hapa maneno ya busara kutokana na hekima za maisha na mafanikio yanatuonya tuachane mara moja na tabia hii, inatuaangamiza.
Kama kuna kitu kidogo umepata basi kaa chini shukuru na kisha ongeza juhudi itakayokusaidia kuweza kupata kitu kingine zaidi na zaidi. Elewa nusu ya mkate uliyoipata ni bora zaidi kuliko kuikosa kabisa.
Nikutakie siku njema na kila la kheri katika kujifunza hekima hizi, kwa leo tunaishia hapa, naomba uwe na wakati mwema zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Dec 29, 2017

Vitu Vitano (5) Vya Muhimu Kuweka Kwenye Chakula Cha Kuku.

No comments :
Kuna vitu vitano muhimu vinavyotaijika kwa kuku ili awe na afya bora. Navyo ni kama vifuatavyo,
1. Protini.
2. Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.

1. PROTINI
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama ifuatavyo, Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya. Hivi vyote inategemeana na maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.
2. WANGA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo; mahindi yaliyo balazwa, pumba ya mahindi na pumba ya mpunga.
3. MAFUTA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo; mashudu ya alizeti na mashudu ya pamba.
4. MADINI
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu.
Pia yai la kuku ili liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo, mifupa, Chokaa ya kuku,  D.C.P hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia uimarisha maganda ya mayai, husaidia kuongeza mayai.
5. VITAMINI.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogamboga, lakini kazi yake kubwa ni kuimarisha mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi hili linavyakula kama vifuatavyo, mchicha, chainizi, spinachi na majani ya mpapai.
KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia.
  






Dec 25, 2017

KHERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA, MSOMAJI WA DIRA YA MAFANIKIO.

No comments :
Habari za muda huu mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima wa afya tele, na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
 Kwa upande  wetu sisi ni wazima wa afya tele, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya hilo.
Ikiwa na leo na tarehe 25 mwezi wa 12 uongozi wa mtandao huu, unapenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana wewe kwa mchango wako wa hali na mali katika kuhakikisha mtandao huu unaendelea kufanya kazi zake kila siku.
Kwani bila wewe, yale ambayo yanaandikwa katika mtandao huu yatakuwa hayana maana tena, lakini kwa sababu umekuwa unatenga muda wako ili uweze kujifunza mambo mbalimbali katika mtandao huu hivyo tunarudia kusema asante sana.

Hata hivyo kwa kuwa nasi ni binadamu, na hakuna binadamu ambaye huwa hakosei basi hivyo tunaomba tutumie wasaa huu kuomba msahama hasa pale tulipokukwaza na kukosea.
Lakini upo usemi usemao yule anayekosea naye zipo nyakati huwa unakosewa hivyo nasi pale ulipotukosea tumekusamehe na kuacha jua liendelee kuangaza na mambo mengine yaendelee pia.
Tunachokuhasa ili uweze kuwa bora katika maisha yako kwa mwaka ujao ni  lazima uhakisha unawekeza muda mwingi katika kujifunza vitu ambavyo vitakusaidia kuwa bora zaidi katika mambo mbalimbali ambayo unayafanya.
Kwa kila siku mpya jifunze na uhakikishe unakuwa bora zaidi katatika kutenda na kufikiri zaidi ya siku iliyopita, yaani jifunze kuwa bora zaidi ya jana.
Kwani endapo utaaamua kufanya hivyo nakuhakiishia ya kwamba yapo matokea makubwa sana ambayo utayaoona katika maisha yako na jamii kwa ujumla.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada tukutakie sikukuu njema na maandalizi mema ya kupokea mwaka mpya wenye mafanikio mengi kwa upande wako.
Muhimu Uongozi mzima wa uongozi wa Dira Ya Mafanikio umekuandalia mambo mengi mazuri ambayo yatakuapa hamasa kubwa ziaidi ya kuweza kufanikiwa katika mambo mbalimbali ambayo unayafanya.

Dec 23, 2017

MAMBO MUHIMU YAKUYAJUA KABLA YA KUINGIA KWENYE UFUGAJI.

No comments :
Habari za leo rafiki, karibu sana katika kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ufugaji bora wa kuku, lengo kuu la makala haya kukupa elimu iliyosahihi kuhusu ufugaji , Na mambo yote ninayoyaandika yanatoka kwenye uzoefu wangu mwenyewe katika ufugaji karibu sana katika somo letu la leo.

Moja ya changamoto kubwa kwa watu wengi tunajiwekea malengo makubwa kila mwaka kwamba nataka kufanya kile na kile ndani ya mwaka huu lakini kila siku bado unashindwa kuanza hii inatokana na changamoto mbalimbali za hapa na pale.

Pia wengi hushindwa kuanza kwa sababu kubwa ya kokosa hamasa ya ndani juu ya kile walichokiwejiwekea malengo na hii inapelekea kila mwaka kuwa na malengo yaleyale bila kupiga hatua na kwenye upande wa ufugaji mambo ni hayo hayo kila siku.

Utakuta tunajisemea natamani kufuga huku tukiendea kuimba wimbo usiokuwa na vitendo, nini ninachotaka kukwambia rafiki siku hii ya leo  unahitaji kuchukua hatua chukua hatua sasa nasiyo kusubili subili utachelewa sana kufanikisha ndoto yako.


Unapochelewa kuchukua hatua ukumbuke siku zinaenda na majukumu yanazidi kuongezeka huku umri nao unakimbia, ila rafiki yako nina jambo zuri ninalotaka kukwambia na unatakiwa uchukue mara moja.

Jambo hili ambalo nakwambie uchukue hatua sasa ni juu ya wazo la ufugaji.  Unajua kwanini nakwambia ni sasa, kwa sababu hakuna wakati mwingine mzuri wa kuanza zaidi ya sasa, anza kufanya na kuweka mipango yako mapema juu ya ufugaji wako.

Hapa  hapa nimekuandikia mambo ambayo unatakiwa kuyajuwa kwanza na kuyafanyia kazi unapotaka kufanya shughuli ya ufugaji za ufugaji ili uweze kufanikiwa katika ndoto yako ya ufugaji, najua unafahamu kuwa ufugaji kwasasa ni moja ya kazi yenye faida.


1. ELIMU NA MAARIFA SAHIHI KUHUSU UFUGAJI.

Hii imekuwa kama sehemu ya kujifichia kwa watu wengi wanaposhindwa kuanza jambo lllote hasa la ufugaji unakuta wanaibuka na sababu kuwa nashindwa kuanza kwasababu sina elimu sahihi juu ya ufugaji sasa sijui una subiri nini kuitafuta hiyo elimu na maarifa sahihi unajichelewesha rafiki, chukua hatua.

2. TAMBUA UNATAKA KUFUGA KUKU KWA MALENGO GANI. 

Nimuhimu kujua kwa nini unataka kufuga kuku kwa sababu ukijua kwanini unataka kufuga kuku itakupa picha halisi juu ya kuku unaotaka kufuga ili uweze kutafuta taarifa sahihi juu ya ufugaji wako  kwasababu kuna aina nyingi za kuku na kila kuku ana sifa zake na mahitaji yake hivyo ukijua malengo yako kuhusu ufugaji wako itakusaidia sana katika kufanya maamuzi na kutafuta taarifa sahihi kuhusu ufugaji wako.

3. ENEO UNALOTAKA KUFUGIA. 

Unapojua tayari malengo uliyonayo katika ufugaji na kujua aina ya kuku unaotaka kuwafuga sasa utakuwa na picha nzuri juu ya ufugaji wako, baada ya hapo unahitaji kujuwa ENEO GANI UNALOTAKA KUFANYIA UFUGAJI hii itakusaidia kujuwa mali ghafi ambayo itatumia katika banda lako, ni muhimu sana kuandaa eneo la kufugia mapema mara tu ya kuweka malengo yako ya ufugaji, jua eneo la kufugia mifugo yako.

4. GHARAMA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUFANYA UFUGAJI  WAKO.

Baada yakujuwa malengo eneo unalotaka kufanyia shughuli zako za ufugaji ni muhimu sana kuchanganua gharama zitakozotumika katika kuanza ufugaji gharama hizo ni pamoja na banda, chakula, chanjo na tiba, hii itakusaidia kuweka mipango yako sasa ili uweze kufanya ufugaji wako kwa ufanisi mzuri

5. ANZA NA ULICHONACHO.

Hii ni jambo la muhumu sana katika kutimiza malengo ya aina yeyote, ni muhimu kuanza na kile ulichonacho usisubiri hadi uweze kujipanga vizuri sana kwasababu unapoanza inakupa hamasa ya kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhusu ufugaji. Anza na kuku idadi yoyote, kama ni kumi, hamsini au hata mia mbili kulingana na uwezo ulionao, kikubwa anza na ulichonacho. 

Naomba niishie hapa kwa leo,

Endelea kunifatitia nina mengi mazuri yakukwambia kuhusu ufugaji naamini yatakusaidia sana.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni Mimi rafiki yako katika ufugaji,
Frank Mapunda, 
0758918243/0656918243
Karibu sana, 



Dec 19, 2017

Changomoto Kubwa Zinazojitokeza Katika Ufugaji Wa Kuku.

No comments :
Habari rafiki, karibu katika makala ya siku hii ya leo, makala ambayo itakuwa inakufikia mara kwa mara kwa lengo la kukupa elimu bora ya ufugaji wa kuku kutoka hatua y akwanza hadi ya mwisho karibu sana

Kwanini ufugaji wa kuku?                    
        
Ufugaji wa kuku ni sekta ambayo inakuwa kwa kasi sana hapa nchini na sasa imekuwa ni sehemu ya ajira kwa watu wengi, ufugaji kwa sasa umekuwa ukifanya vizuri sana kwa kuwa na soko zuri kwa ndani ya nchi yetu na hata nje ya nchi.

 Ufugaji umekuwa sehemu nzuri ya ajira kwa watu wengi na imekuwa kazi rasmi kwa watu wengi, ufugaji umekuwa ni sehemu nzuri ya uwekezaji unaompatia mtu kipato na kumtimizia malengo yake katika maisha.

Pia ufugaji umekuwa ni rahisi kufanya na unafanyika katika maeneo yeyote mjini au vijijini, licha ya kuwa ufugaji wa kuku kuwa na faida nyingi pia ufugaji wa kuku umekuwa na changamoto zake ambazo zinawafanya wafugaji wengi kukata tamaa katika Ufugaji huu wa kuku.


 Jambo lililokuwa zuri ni kwamba changamoto nyingi zilizopo kwenye ufugaji ni aina changamoto ambazo inawezekana kabisa kuzipunguza ilimradi  tu tukiwa makini na kupata elimu bora na sahihi katika sekta hii ya ufugaji wa kuku.

Changamoto hizi zinatokana na  wafugaji wengi wanaingia kwenye Ufugaji bila kuwa na elimu sahihi ambayo itawapa mwongozo bora katika kufikia malengo waliyojiwekea katika ufugaji wa kuku kulingana na eneo husika.

Kwa kukosa huko kujua mambo muhimu yanayohusu ufugaji inawapelekea kupata hasara kubwa na kushindwa kutimiza malengo ambayo walikuwa wamejiwekea katika maisha yao ya kila siku.

Mimi kwa kuliona hili nimeona bora nikuletee elimu hii ili uweze kuwa na elimu sahihi katika uwekezaji wako katika sekta hii ya ufugaji. Mara baada ya utangulizi huo, naomba kwa leo tuanze somo letu moja kwa moja, linalohusu changomoto zinazojitokeza katika ufugaji wa kuku.

MAGONJWA.                                                    

Magonjwa yamekuwa ni changamoto kubwa kwa wafugaji wengi hasa wanaoanza kuingia katika ufugaji na hii inasababisha wafugaji wengi wakate tamaa ya kufuga na kuona kufuga hakuna faida yeyote kwasababu inawapa hasara kubwa sana.

Jambo lakuvutia nikuwa katika mfululizo huu wa makala zangu nitaeleza mbinu ambazo kama utatumia utaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa cha magonjwa ya kuku kwa kifupi nimekuja na majibu juu ya changamoto hii.

GHARAMA KUWA KUBWA ZA CHAKULA.

Hii ni moja ya changamoto kubwa kwa wafugaji wengi wa sasa kwa sababu wanapenda kufuga lakini wanajikuta wanashindwa kwasababu ya kukosa mitaji ambayo itaweza kuwa saidia katika kuwapa chakula mifugo yao. 

Kutokana na changamoto kuwa kubwa kwa upande wa chakula watu wengi wameshindwa kuendelea na ufugaji wa kuku kwa wingi na wamekuwa wakifuga kwa idadi ndogo sana au kuacha kabisa kwa sababu yakushindwa kupata chakula.

 WIZI.

Hii ni moja ya changamoto ambayo zinawakuta wafugaji wengi wa kuku hasa maaneo ya mijini, wezi wamekuwa wakibomoa mabanda na kuingia kuiba kuku wengi nakupelekea hasara kubwa kwa wafugaji.

Jibu la changamoto hii kama unafuga kuku wengi ni bora ukaweka mlinzi anaweza akawa mbwa au mlinzi kwa maana ya binadamu. Ukiweka mlinzi hapo itakuwa imekusaidia kwa kiasi kikubwa kutatua chagamoto hii.

Kwa leo naomba niishie hapa tutaendelea siku nyingine kwa llimu bora ya ufugaji wakuku. Endelea kutufatilia......

Kwa mahitaji ya vifaranga bora kabisa kwa ajiri ya ufugaji karibu sana vinapatikana, 
pia kwa mahitaji ya MASHINE  bora za kutotoleshea vifaranga zinapatika na
bila kusahau mayai kwa ajiri ya kutotoresha, kula yanapatika kwa bei nafuu sana yanasafirishwa popote pale. Mayai na vifaranga vinavyopatikana ni yakuku chotara aina ya kuroiler.
                                                
Karibu sana na wote mnakaribishwa. 

Kwa mawasiliano zaidi, 
0758918243/0656918243.
Ni mimi rafiki yako, 
FRANK MAPUNDA .
KARIBU KATIKA UFUGAJI BORA WAKUKU TUKUZE UCHUMI WA NCHI YETU.



Dec 18, 2017

Bila Kujali Kitu Gani Kinatokea, Taka Matokeo.

No comments :
Ugunduzi mkubwa duniani, ulianza au ulitokana na watu ambao walikuwa wana matatizo sana. Kwa mfano, kuna eneo fulani duniani ambapo watu walikuwa wakitembea kwa miguu, kutokana na kuchoka huko kutembea kwa miguu ndio utakaja ugunduzi wa magari na hata ndege ili kurahisha.
Ubunifu mkubwa duniani pia ulitokana na watu ambao walikuwa hawajaridhishwa na huduma zinazotolewa. Kwa mfano, watu baada ya kuchoshwa na mabasi yenye ‘keria’ juu hapo ndipo yakaja mabasi yenye ‘buti’ ili kuepusha hata upotevu wa mizigo na inakuwa salama wakati wote.
Mafanikio makubwa duniani pia yanazaliwa na watu ambao walikutana na changamoto nyingi sana. Kuna watu baada ya kuchoshwa na umaskini, basi waliamua kupigana usiku na mchana mpaka kuhakikisha wanaupa umaskini mkono wa kwaheri, hakuna umaskini uliotolewa kwa njia ya lelemama.

Hii yote inadhihirisha kuwa, mafanikio makubwa hayaendi kwa watu ambao wanasema siku nikipata muda au siku nikipata pesa za kutosha basi nitawekeza kwenye mradi wa aina fulani, bali mafanikio makubwa yanaenda kwa watu wote ambao wako tayari kuchukua hatua hata kama rasilimali zao kwa akili na macho zinaonekana ni kidogo sana.
Hebu jiulize aliyegundua ndege au aliyegundua meli ni pesa au rasilimali gani za kutosha alikuwa nazo? Ukiangalia elimu, hawakuwa nazo za kutosha, ukiangalia ni pesa hawakunazo za kutosha, kila kitu kilikuwa hakitoshi kwao, lakini kilichowasukuma ni kutaka matokeo wanayoyataka bila kujali wana rasililmali chache kiasi gani.
Lakini tunaona mwisho wa siku, kutokana na ung’ang’anizi wao huo wakaja na kitu kikubwa, endapo kama wangekaa na kuanza kulia lia kama wewe unavyolia kwamba ‘ooh sina mtaji na siwezi kufanya biashara,’ basi inawezekana kabisa leo hii tungekuwa labda tunatembea kwa miguu.
Maisha ya mafanikio yanataka utayari. Upo tayari kutoa nini? Kwa chochote kile ulichonacho mkononi mwako hata kiwe kidogo sana kina uwezo wa kukufanikisha ikiwa kitu hicho utakilea na kukitunza vizuri. Haijalishi iwe ni kazi ya mshahara kidogo au una biashara ndogo lakini unaweza kupiga hatua na kufika mbali sana kimafanikio.
Kwa nini uendelee kuteseka na kuamini kwamba huwezi kufanikiwa, wakati uwezo huo unao. Kipi kinachokurudisha nyuma, je umeamua kukwama kwa sababu unaamini kwamba wewe si kitu na hutaweza kipiga hatua kwa sababu ya rasilimali ulizonazo ni chache sana, hiyo tu ni kwambie si kweli hata kidogo.
Kuanzia leo, acha kabisa kusubiri kuwa kamili, fanya kila ufanyalo kuhakikisha unapata matokeo unayoyataka. Kama unataka kwekeza kwenye mradi wa aina fulani, wekeza pasipo kutafuta sababu yoyote ile. Sababu hazina nafasi kwenye mafanikio yako, unatakiwa kufanikiwa tu.
Vizuizi au vikwazo vipo tu katika maisha yako. ukitafuta sababu kwamba ipo siku utavikimbia vizuizi hivyo hapo utakuwa unajidanganya sana. Tafuta njia ya kuweza kuondokana na vizuizi hivo ili uweze kuwa mshindi wa maisha yako.  Kwa namna yoyote ile, bila kujali nini kitatokea, taka matokeo ya mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






Dec 17, 2017

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Hakuna Mkate, Pasipo Kazi.

No comments :
Naamini leo yako iko poa na unaendelea kuimalizia wikiendi yako kabla ya kesho hujatua kazini kuanza kukamilisha majukumu ya Juma zima. Kama iko hivyo, shukrani za pekee zimwendee Mola wetu.
Ni wakati na jumapili njema kabisa nami na kualika katika jamvi letu la Hekima za maisha na mafanikio. Kumbuka hizi ni hekima ambazo zilitolewa kitambo na babu zetu au wahenga, sasa pia nasi ni muhimu tujifunze.
Na kwa nini tunajifunza misemo au maneno ya wahenga wetu ni kwa sababu, wengi wetu enzi hizo kwanza hatukuwepo, kwa hiyo kwa kujifunza hapa kupitia ukurasa huu, vipo vitu vizuri vya maisha na kimafanikio ambavyo vitatusaidia sote kutujenga kifikra na kimaisha.
Kwa kuwa na mimi si mchoyo, na sipendi kukunyima kitu, naomba nikukaribishe moja kwa moja na twende tujifunze hekima na mafanikio ambazo nimekuandalia siku ya leo. Kikubwa kaa mkao wa darasa na karibu sana.

Hekima ya 1; Hakuna mkate, pasipo kazi.
Hekima hii inajipambanua na iko wazi ikiwa na maana kwamba pasipo kazi, usitegemee mafanikio. Kama utakuwa umekaa tu na huweki juhudi za makusudi za kukusaidia kuweza kupata mafanikio yako, sahau kuhusu mafanikio. Mafanikio yanakuja kwa kazi, na kazi ndio inatupatia mkate au ridhiki ya kila siku.
Hata vitabu vya dini vimeweza kuandika hili ‘asiyefanya kazi na asile’ na hicho ndicho kitu unachopaswa kuzingatia. Kama unataka mavuno ya aina fulani, jiulize ni kazi ipi ambayo umeifanya. Kumbuka wahenga wetu kutokana na hekima zao  wanasema wazi, hakuna mkate, pasipo kazi na hio ndio kweli halisi huwezi kupinga.
Hekima ya 2; Unapokwenda kununua kitu, tumia macho na usitumie masikio tu.
Ni mara nyingi sana wengi wetu tunapokwenda kununua vitu iwe dukani au sokoni, huwa tuna tabia ya kuwasikiliza sana wale wanaotuuzia na kusahau kabisa kuangalia ubora wa kitu. Matokeo yake sasa, tunajikuta ni watu wa kuingia hasara kwa kuchukua vitu vibovu. Utakuta mtu anasikiliza sana maelezo bila hata na yeye kuangalia ukweli uko wapi.
Tabia hii wanayo wengi sana, miongoni mwao inaweza ikawa ni hata wewe, lakini hapa leo hekima hii inatukumbusha hivi, unapokwenda kununua kitu, tumia macho pia na usitumie masikio peke yake. Hiyo ikiwa inaonyesha kwamba ni vyema kujiridhisha kwa macho yako na si kusikiliza peke yako. Kusikiliza peke yake ni sawa na kuamua kuingia hasara.
Hekima ya 3;  Ushauri mzuri, ni bora kuliko dhahabu.
Hii ni hekima  ambayo msingi wake umejikita katika kuonyesha kwamba ushauri mzuri siku zote ni bora kuliko dhahabu. Unaweza ukapata dhahabu leo au mafanikio makubwa leo, lakini kama huna ushauri mzuri hiyo ni sawa na bure, kwani ni rahisi hata kuweza kuipoteza hiyo dhahabu au kitu cha thamani ulichokipata kama huna ushauri wa maana.
Kwa hiyo hapa tunaonywa kuwa ni bora kupata ushauri mzuri kwanza, na kisha ushauri huo mzuri utakusaidia kuweza kutumika katika kupata mafanikio makubwa ambayo yanafananishwa na dhahabu. Mifano hai tunayo, waangalie watu wote ambao walipata ushauri mbovu na maisha yao pia yapo hovyo pia.
Hekima ya 4; Usijilinde sana kwa kutumia fensi, jilinde kwa kutumia marafiki.
Wapo watu ambao katika maisha wanaamua kujilinda sana kwa kutumia kuta za nyumba, wanajilinda sana kwa kutumia fensi na vitu vingine kama hivyo, na kusahau kuwa kujilinda huko kunaweza kukawa kwa bure kama usipojua kwamba hata marafiki ulionao pia nao ni walinzi wazuri tu.
Katika hekima hii inatuonyesha kwamba ulinzi mzuri na wa maana upo kwa marafiki zetu pia. Marafiki zetu ndio watakaotuambia kipi kizuri na kipi kibaya. Pia marafiki zetu ni rahisi wao kutuonyesha  marafiki wengine wabaya na wepi ni wazuri. Kupitia hekima hii ya maisha na mafanikio ni wajibu wetu kutafuta marafiki bora ili wawe walinzi kwetu.
Naamini mpaka hapo kutokana na hekima ulizojifunza kuna kitu cha kipekee ambacho umejifunza. Nikutakie wakati mwema na tukutane wiki ijayo kwa hekima zingine kama hizi za maisha na mafanikio. Kila la kheri.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,









Dec 16, 2017

Kataa Sana Kujibebesha Mzigo Huu Unapotafuta Mafanikio Yako.

No comments :
Visingizio ni moja ya njia kubwa ambayo inakufanya ushindwe moja kwa moja kwa kile kitu ambacho unakifanya. Haijalishi visingizo hivyo unavitafuta wewe mwenyewe ama unavikubali tu kutokana na hali unayokutana nayo kimaisha.
Lakini unachopaswa kujua ni kwamba visingizio ni kama bendera ya ishara inayokuonyesha sasa kushindwa kwako wewe kunakujia wakati wowote. Ndio maana unatakiwa uwe makini sana hasa pale unapoanza kutoa visingizio ujue kushindwa kunakujia.
Ili kutokana na visingizio unatakiwa kuchukua hatua. Ikumbukwe pia kuchukua hatua kila wakati ni njia ya kuondokana na visingizo, lakini pale unapochelewa kuchukua hatua kwa jambo lolote lile au kutokuchukua kabisa hapo ujue ndio chanzo kinakuja cha kukalibisha visingio ambayo haviwezi kukusaidia.
Katika maisha yako ya mafanikio kwa namna yoyote ile visingizo havina maana na havikubaliki hata iweje. Unapokubali visingizio hata viwe vizuri namna gani kwako huko ndiko kushindwa kwako kunakuja pia.

Najua kila kushindwa kwenye maisha yako kuna sababu au kisingizio. Na kila kukosea kwa kile unachokifanya pia kuna sababu zake, lakini usikubali sababu au visingizo hivyo ukavitumia. Kama kuna jambo umeshindwa kubali umeshindwa, hakuna haja ya kutoa sababu au visingizio vyovyote vile.
Kila kisingizio unachotoa ujue kabisa kinatoa mwanya wa wewe kushindwa kwa kile unachokifanya kwa sehemu fulani. Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kukataa kutoa visingizo kwa nguvu zote.
Wewe kama ni kazi, chapa kazi yako kwa uhakika mkubwa sana, lakini inapotokea umeshindwa usitumie visingizio kama silaha ya kujihami na kueleza jinsi wewe ulivyoshidwa huko, hapo utakuwa unajiangusha wewe mwenyewe.
Wapo watu ambao katika maisha yao ni kama wameathirika na visingizo. Kikitokea kitu kidogo watu hawa wanakuwa na sababu nzuri sana ambazo wanatumia kama ngao ya kuhalalisha kushindwa kwao.
Ukiwaangalia watu ambao mara nyingi maisha yao yamejaa visingizio kwa asilimia kubwa, mara nyingi watu hawa hawafanikiwi sana katika maisha. Na huo ndio ukweli huwezi kufanikiwa kama wewe ni mtu wa visingizio.
Ndio maana kati ya jambo ambalo unatakiwa kulikataa sana katika maisha yako unapotafuta mafanikio ni kujibebesha mzigo wa visingizio. Ukiona unajibebesha mzigo huo ujue kushindwa kunakuhusu.
Kama ulikuwa hujui au ulikuwa hujaanza, hebu leo chukua hatua kwa kuanza kuishi maisha yako bila visingizio. Kama ulikuwa mtu wa visingizio sana, jaribu leo tu peke yake kuishi bila visingizo vyovyote tuone nini kitatokea kwako.
Ukiona leo umeshinda kuishi bila visingizio, kesho ishi hivyo, utashangaa wiki nzima umemaliza mara mwezi na yanakuwa ndio maisha yako ambayo sasa unakuwa unayaishi pasipo kuwa na visingizo vyovyote vile.
Naamini utaanza kujenga maisha bora sana ukiamua kuishi bila visingzio. Kumbuka unawajibika kwenye maisha yako kwa asilimia zote. Ukileta visingizo kwa namna yoyote ile ni sawa na kuchagua kuamua kujiangusha wewe mwenyewe.
Kwa nini ukubali kujiangusha kwa sababu ya visingizio? Ni wakati wa kukataa kujibebesha mzigo huu wa visingizio, ukiendelea kujibebebsha utashindwa vibaya katika maisha yako bila kutarajia.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,



Dec 15, 2017

Tabia Hii Haifai Kwenye Biashara Na Uwekezaji Wowote.

No comments :
Kuonekana umefanya makosa mbele za watu ni kitu kinachotishia utambulisho wa mtu, ndiyo maana watu wengi wanachukulia kufanya makosa kama jambo la kurudi nyuma. Mtazamo wa waliowengi ni kwamba kwenda mbele ni pale tu wenzako wanapokuona uko sahihi kwa mtazamo wao binafsi. Kutaka kuonekana sahihi mbele ya macho ya wenzako ndiyo usababisha hali ya kupenda kila mara kujihami, kujilinda, kulaumu watu wengine au kusingizia kitu kingine, hasa pale inapotokea mambo yemekwenda ndivyo sivyo. 

Watu walio na shauku ya kuonekana sahihi, mara nyingi ukazana sana kufanya kazi au shughuli zile zinazowathibitisha kwa watu wengine kuwa wao wana uwezo. Ukiwa mtu mwenye shauku ya kuonekana sahihi kila wakati, mara nyingi utapendelea kufanya kazi zako kwa kufuata maoni ya watu wengine. 

Matokeo yake na bila kujua unajikuta unakuwa mtumwa wa watu wengine—wanageuka kuwa mabosi wako. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila jambo inabidi uwasikilize wao wanasemaje—unapata ruhusa kutoka kwao.


 Endapo ukifanya jambo la lenye manufaa kwako na kwa watu wengine lakini wale watu wako wa karibu wakasema siyo sahihi, basi wewe utaliacha “eti kwasababu watu wanasema siyo zuri”. 

Unapokuwa mtu wa kuongozwa na maoni kutoka kwa watu wengine, ujue kuwa muda si mrefu utaanza kupoteza ubunifu wako. Kwa sababu, kila wakati unafanya kazi zako kwa tahadhari sana, ukilenga kutoonekana mbaya. Hofu ya kufanya kazi kwa kuogopa kuonekana mbaya ikizidi, kinachofuata ni kuziba kwa mfereji wa ubunifu kutoka kwenye akili yako. 

Kuziba kwa mfereji maana yake ni kwamba, juhudi na akili zako hazijikiti tena kwenye kutafuta suluhisho kwa changamoto na matatizo yaliyopo, bali kwa kiwango kikubwa utatumia akili nyingi katika kufanya vitu ambavyo unadhani watu wako wa karibu watakupongeza au kukusifu.

Mtu anayependa kuonekana sahihi pia ni mtu asiyeamini kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya vizuri zaidi ya yeye. Huyu ni mtu asiyeamini vipaji vya watu wengine. Siku zote anaamini asipofanya yeye hakutakuwepo na matokeo mazuri. Kila mara anakuwa ni mtu wa kujisemea rohoni ya kwamba“bila mimi kuwepo mambo hayawezi kwenda". 

Ukweli ni kwamba bidhaa au huduma yoyote ile tunayoiona sokoni haiwezi kamwe kutolewa na mtu mmoja, kwa sababu hakuna binadamu anayeweza kuwa na vipaji vyote.

Tabia ya kupenda kuonekana sahihi kwa watu, kwenye biashara na uwekezaji haifai. Hii ni kwa sababu, kwenye biashara na uwekezaji tunaamini sana katika kuunganisha vipaji vya watu mbalimbali (timu) kwa lengo la kuzalisha suluhisho kwa changamoto na matatizo yaliyopo kwenye jamii. Tunafanya hivyo kwasababu, bidhaa na huduma unazotumia leo hii, ni matokeo ya vipaji mbalimbali vilivyounganishwa pamoja na mfanyabiashara au mwekezaji.

Katika nyanja nyingine za maisha, kuongezeka kwa watu ambao wanakupongeza na kukusifu hakuleti faida ya moja kwa moja kwako, kama ipo. Na mara nyingi ukifanikiwa kupata faida, inakuwa siyo ya kudumu. Wakati huohuo, hali ya nyanja za maisha ya biashara na uwekezaji ni tofauti kidogo na uko kwingine. Kwenye biashara, mpango mzima ni kuelekeza juhudi na akili kwenye kuzalisha, kuongeza, na kutoa thamani kubwa kwa watu wengine. 

Kwenye biashara hasa kubwa, wateja ndio rafiki zetu wa karibu na ndio kipimo cha usahihi wa kile tukifanyacho. Jukumu kubwa ni pamoja na kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa mpaka pale wateja wanaporidhika. Uzuri wa kufanya kazi kwa lengo la kuridhisha wateja wako ni kwamba, wale wateja wanaoridhika na kazi unayoifanya wanavyozidi kuongezeka, ndivyo kipato chako kinavyozidi kuongezeka pia.

Kama unataka kuwa mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa, anza leo kujiwekea mazingira ya kufuta tabia hii ya kupenda kila wakati kuwafurahisha watu. Kamwe usitake kuwa sahihi kwa ajili ya watu wengine, bali kuwa sahihi kwa ajili ya wewe mwenyewe binafsi, pia kufanya yale unayotakiwa kufanya. Usipoacha tabia hii ya kila wakati kutaka kufanya vitu vinavyokuthibitisha kwao kuwa wewe una uwezo mkubwa, nakuhakikishia kuwa haitatokea hata siku moja ukafanikiwa kwenye biashara.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA Cypridion Mushongi WA MAARIFA SHOP BLOG.

Dec 13, 2017

Fanya Maisha Yako Yawe Bora Kwa Kujipa Changamoto Hii…

No comments :
Ipo njia au namna ya kuyapa maisha yako nguvu na ikakupelekea wewe kupambana na changamoto yoyote pasipo ya hofu. Njia hii si nyingine bali kuamua kujipa changamoto wewe mwenyewe na sio kuzisubiri.
Hakuna namna unavyoweza ukafanya maisha yako yakabadilika sana kama huna changamoto. Ukumbuke changamoto ninazozingumzia hapa ni  zile za kujiwekea yaani hapa wewe unaamua sasa najipa changamoto hii halafu unasikilizia matokeo.
Kwa mfano, unaona kabisa kipato chako imefika wakati unaona kidogo kwa kifupi,  hakitoshelezi. Hapa unaweza ukajipa changamoto na kusema sasa ndani ya miezi minne nitahakikisha naongeza kipato changu kikue kwa laki moja kila mwezi.

Pengine labda una mradi unaotaka kuuanzisha, na ambao pia unahitaji pesa, hapa pia unaweza ukajipa changamoto na kusema kila mwezi lazima nipate kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya mradi wangu huu.
Pia unaweza ukawa ni mwanariadha, kila wakati unakimbiakia kilomita kumi yaani hapo ndio mwisho wako. Unaweza ukajipa changamoto kwa kuongeza kilomita zingine tano za kukimbia wewe mwenyewe bila shuruti ya mtu.
Na kweli kutokana na changamoto hizo unazojiwekea utashangaa unatimiza malengo yako, ingawa mwanzo inaweza ikawa ni shida, lakini mwisho wa siku malengo yako yanatimia na kufika kule unakotaka kufika.
Kujipa changamoto kwa namna hiyo ni njia mojawapo ya kuweza kukua na kufanya wewe kuwa na uwezo wa kukabaliana na changamoto yoyote bila tabu. Hatua unayotakiwa kuanza nayo wewe  ni kujipa changamoto.
Hapa unachotakiwa kuangalia ni eneo lipi ambalo hufanyi vizuri, kisha jipe changamoto ya kuweza kuboresha eneo hilo. Huhitaji kujiwekea changamoto kubwa sana unaweka kidogo, ukiivuka, unaongeze tena.
Hivyo ndivyo unavyoweza kujipa changamoto na kuzishinda na hatimaye lakini utakuwa umetengeneza maisha unayotaka wewe yawe hivyo. Kitu cha kufanya kwako leo ni kutafuta wapi ambapo unakwama na kisha jipe changamoto zaidi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,