google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 17, 2018

Hivi Ndivyo Jinsi Unavyopanga Kuwa Maskini.

No comments :
Katika hali ya kawaida, kila binadamu anaishi kwa kupanga vitu vya kufanya. Katika zoezi zima la mpango, kuna makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza ni watu waliopanga kutokuwa na mpango wowote wa maisha yao na kundi la pili ni watu waliopanga kuwa na mpango wa maisha yao.

Kundi la watu waliopanga kutokuwa na mpango, maisha yao yanategemea zaidi imani na matumaini. Kwa kawaida watu hawa wanaamini mambo yote yanapangwa na Mungu, na kwa hiyo, wao ni kufanya yale tu yanayowajia vichwani mwao kila waamkapo asubuhi.

Imekuwa ni kitu cha kawaida kusikia wengi wa kundi hili wakinena “Hata ufanyeje, Mungu kama hajapanga unajisumbua bure! huwezi kufanikiwa”. Kauli za namna hii ni za kukata tamaa ya maisha na pia yule anayeambiwa anakatishwa tamaa pia—anza kukaa mbali na wenye kutoa kauli hizi ni hatari kwa mafanikio yako.

Tabia hii ya kutokupanga aina ya matokeo unayoyataka ndiyo inayopelekea watu kuishi maisha ya kufuata upepo kama siyo mkumbo. Pia ni tabia hii inayowafanya watu kuwa na mipango ya muda mfupi na kupenda matokeo ya haraka.



Kwanini tunasema ni lazima kuwa na mpango? Kwasababu kuna vitu vikubwa viwili ambavyo vina nguvu sana katika maisha yako; navyo ni MUDA na MABADILIKO. Muda una nguvu kwasababu, utake usitake lazima muda uende na mabadiliko ni hivyo hivyo, lazima yaje utake usitake .

Njia pekee ya kuweza kuwa na mamlaka juu ya muda na mabadiliko ni wewe kuwa na mpango. Binadamu wote tumepewa uwezo wa kuweza kupanga nini cha kufanya hata kama hakijatokea.

Tofauti na wanyama wengine, wao huweza kuishi kwa kufuata matukio au hali ya wakati huo. Wanyama hawana kabisa mpango unaoweza kuwaongoza kwenda kwenye mwelekeo wa maisha wanayoyataka.

Ikitokea malisho yameisha wao uhamia sehemu nyingine na hiyo sehemu nyingine wakikuta wanyama wanaowawinda watarudi huko ambako walihama mwanzoni.

Ajabu na kweli ni kwamba watu wengi wanaishi kwa kufuata mabadiliko yanayojitokeza kwenye mazingira yao. Kikubwa hapa ni wewe kubadilika na siyo kubadilishwa na mabadiliko. Ukisubili kubadilishwa na mabadiliko maana yake mabadiliko yatakubadilisha jinsi yanavyotaka.

Yawezekana wewe unajiona uko sawa na mambo yako yanaenda vizuri, lakini ujue kuwa ukiwa na maisha ambayo huna mpango ulio katika maadishi, hapo ujue kuwa lazima ufuate kile ambacho mabadiliko yatakuletea na siyo wewe unavyotaka mabadiliko yawe. Ndiyo maana tunaambiwa kwamba ufunguo pekee wa mtu kuweza kudhibiti MUDA na MABADILIKO ni kuandika “mpango”.

Mpango maana yake ni kwamba wewe mwenyewe unapanga aina ya mafanikio unayoyataka kabla ya kuanza kuyatafuta. Mafanikio yoyote makubwa lazima upange kuyapata. Kwahiyo, tuseme kuwa mafanikio yako yapo tayari, kinachosubiliwa sasa hivi ni mpango kazi wako. Kama umepanga kutokuwa na mpango—tambua kuwa “Usipopanga kupata mafanikio, basi ujue unapanga kimya kimya kuwa masikini”.

Mpango ndio unakupa mwelekeo mzuri wa unakotakiwa kwenda. Kama wewe ndiye unayeshika upinde na mshale basi “Mpango” ndio unasaidia kuelekeza wapi mshale uende—wewe unachagua upande gani mshale upige. Athari za kutokuwa na mpango ambao unatuongoza juu ya nini cha kufanya ni pale tunapojikuta tunadhibitiwa na maisha badala ya sisi kuyadhibiti maisha.

Mpango unakupa nguvu na uwezo wa kuuamrisha muda ukufanyie nini. Ikiwa umepanga kutokuwa na mpango, basi ujue muda ndio utakupangia nini cha kufanya. Inafika kipindi fulani muda wenyewe unakulazimisha kufanya vitu ambavyo hupendi kuvifanya. Ulikuwa na nafasi ya kuamrisha muda, lakini hukuitumia, sasa ni zamu ya muda wenyewe kukuamrisha cha kufanya.

Ukiwa huna mpango unakuwa ni mtu wa kuishi kwa matumaini. Lakini kumbuka kuwa watu wengi wanaoishi kwa matumaini mara nyingi ni maskini. Kwahiyo, unahitaji mpango ambao ndio utakujengea imani ya kufanikiwa.

“Imani ni bora zaidi kuliko matumaini” jitahidi kuwa na imani juu ya mpango wako, huku ukizidi kuutekeleza kwa nguvu zako zote—hakika mafanikio uliyolenga kupata lazima yatokee tu!

Habari njema ni kwamba Mungu yupo anasubiri mpango wako ili aubariki. Mafanikio yako makubwa yapo, lakini utayapata tu endapo utaandika leo mpango wako. Ukishindwa kupanga unapanga kuwa maskini—habari ndio hiyo!.

Kuendelea kupata maarifa mengi jiunge na kundi la Whats app kwa ajili ya kujifunza zaidi. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 04 80 35 ili kuunganishwa.



Oct 16, 2018

Aina Ya Watu Ambao Hawafanikiwi Katika Maisha.

No comments :
Katika maisha wapo watu ambao ninaweza sema kwa jinsi ya sifa zao au kwa jinsi ya tabia zao walizonazo sio rahisi kufanikiwa. Hawa ni wale watu ambao tunasema ni aina ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao.
Inawezekana ukawa huzijui sifa za watu hawa ambao hawafanikiwi katika maisha yao, lakini kupitia makala haya utajifunza sifa hizo za watu ambao kwa kiuhalisia huwa hawafanikiwi hata iweje, pengine wabadilike mara moja.
Najua hapo ulipo unataka kujua kwa hamasa kubwa watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao huwa wana sifa zipi. Nami bila choyo yoyote, nakukaribisha bila hiana na twende kwa pamoja kujifunza sifa za watu ambao hawafanikiwi katika maisha.
1. Watu ambao kazi yao ni kulaumu na kulalamika.
Mara nyingi watu ambao ni walalamikaji sana, kufanikiwa kwao katika maisha huwa sio rahisi. Hili hutokea kwa sababu, husau majukumu yao ya msingi juu ya maisha yao na kuwapa wengine mzigo huo kwamba ndio wamesababisha maisha yawe hivyo.
Hata wewe ukiwa mtu wa kulalamika na kulaumu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao hawataweza kufanikiwa katika dunia hii, hadi pengine ubadilike. Ukifatilia, utaelewa vyema aina hii ya watu jinsi walivyowengi na wanakwama kweli.

Wapo ambao hawabadiliki, hawafanikiwi.
2.Watu wanaojadili matatizo badala ya njia za kutatua matatizo.
Kama umekuwa ni mtu wa kujadili matatizo badala ya kutafuta njia za kutoka kwenye tatizo hilo, basi ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuja kufanikiwa katika maisha yao. Ili upate unachokitaka unatakiwa kujifunza kutatua changamoto na si kuzijadili. Kujadili changamo  zako sana ni kujikwamisha mwenyewe.
3. Watu ambao hawataki kubadilika hata kama wanafanya makosa.
Wapo watu ambao ni wabishi na ambao maishani mwao ni kama wamegoma kubadilika kabisa. Hata watu hawa wakikosea bado kubadilika kwao ni kugumu sana. Hiyo haitoshi si watu wa kujifunza hata kidogo iwe kwenye vitabu au kupitia wengine. Pia watu hawa ni miongoni mwa watu ambao sio rahisi kuweza kufanikiwa.
4. Watu ambao ni watumwa kwa mambo yasio ya msingi.
Kuna watu ambao ni watumwa wa mambo yasiyo ya msingi ambayo kiuhalisia yanawarudisha nyuma sana kwenye maisha yao. Unapokuwa mtumwa sana pengine pombe kwa sana au wanawake ka wingi, unajitengenezea shimo la kushindwa kwako. Kwa lugha nyingine hivyo ni vitu ambavyo vinapoteza pesa ukiviendekeza vibaya.
5. Watu wanaojilinganisha sana na wengine.
Acha kufanya kosa la kujilinganisha na wengine kwenye maisha yako. Unapojilinganisha na wengine utashindwa kuwa bora pasipo kujua na mwisho wa siku utashangaa unakwama. Itakuwa badala ya kufanya mambo yako, unakua unakazana tu uwe kama fulani, hapo utakwama.
Hawa ndio watu ambao wana sifa nyingi za kutokufanikiwa katika maisha yao. Kama una sifa miongoni mwa hizo unabidi uwe makini sana ili na wewe usije ikafika mahali ukakwama na kubaki hapo. Jenga maisha yako makubwa ya kimafanikio kwa kujitahidi kutoka kwenye sifa hizo kama unazo.
Endelea kujifunza kupitia diramafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kuhamasika na kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Oct 15, 2018

Hii Ndiyo Mbegu Muhimu Sana Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.

No comments :
Kila mtu ana uwezo mkubwa sana ndani yake wa kufikia mafanikio makubwa, lakini kwa bahati mbaya ni wachache sana wanaojua kwamba uwezo huo wanao na waliobaki hawaamini kabisa hata kwamba uwezo huo mkubwa wanao ndani mwao.
Kitu ama hali hii inatokea kwa watu hawa kushindwa kuamini wana uwezo mkubwa ni kwa sababu moja tu, watu hawa hawajaambiwa na mtu kwa msisitizo au hawajatiwa moyo sana hadi kuweza kuamini uwezo mkubwa ulio ndani mwao.
Ni kweli watu hawa uwezo wa kufanikiwa wanao lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa mbegu muhimu ya kupewa matumaini kwamba uwezo huo wa kufanikiwa wanao kama wanavyowaona watu wengine wakifanikiwa pia.

Kama vile ulivyo udongo hata uwe mzuri vipi na una rutuba ya kila aina, lakini udongo huo ukikosa mbegu au usipopanda chochote hakiwezi kuota kitu, na vivyo hivyo hata uwe na uwezo mkubwa vipi lakini usipopanda mbegu ya kutiwa moyo ni kazi bure.
Hamasa na kumpa mtu moyo na kumwaminisha kwamba anaweza ni kitu ambacho kinahitajika sana katika kila maisha ya mwanadamu. Hii ndio mbegu ya msingi sana katika mafanikio ambayo wengi hawaijui.
Ndio maana kama unaipa akili yako hamasa kila wakati ni rahisi sana kuweza kufanikiwa. Wengi wanashindwa kwa sababu ya kuzipa akili zao ‘matango pori’ kwa kulisha mambo yasiyofaa ambayo yamejaa hofu.
Unatakiwa kuelewa unatakiwa kupewa mbegu ya hamasa, mbegu ya kutiwa moyo  ili kuweza kufanikiwa na kufika juu kabisa kimafanikio. Ukiwa na msingi mzuri wa mbegu hii utafanikiwa tu kwenye maisha yako.
Kama unafikiri natanaia waangalie watu ambao wamelelewa katika mazingira ya kupewa sana moyo kwamba mafanikio yanawezekana. Utakuta ni kweli na wao wamefanikiwa kwa sababu wanalishwa vitu kama hivyo hivyo kila siku.
Yapo mabadiliko makubwa sana yanayotokea kwa wengine na ndani mwako hasa pale unapoamua kujipa moyo na kuwapa moyo wengine. Hakuna kinachoshindikana unapojipa moyo, kwa vyovyote tu utasogea hata iwe kwa kutambaa.
Kujipa moyo na kuwapa moyo watu wengine ni mojawapo ya mbegu ya mafanikio ambayo unatakiwa kuitumia kila wakati. Acha mizizi ya mbegu ya kutia moyo ikue na hakikisha imekuwa vya kutosha na hapo utaona matunda ya mafanikio yako.
Endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
 DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


Oct 2, 2018

Sababu Kubwa Inayokufanya Usianze Kuchukua Hatua Ni Hii…

No comments :
Moja ya sababu kubwa inayopelekea watu wengi kuahirisha mambo na kushindwa kuchukua hatua ni kule kufikiri  kuna vitu havijakamilika katika kulifanikisha jambo hilo. Mtu anakuwa anaahirisha kwa sababu anakuwa anaona bado hajawa tayari kufanya jambo hilo kabisa.
Uelewe hivi, ni jambo zuri kufanya kitu chako ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja. Hata hivyo hiyo isiwe sababu ya wewe kutokuanza, unaweza ukaanza kwa hali yoyote uliyonayo hata kama unajiona hujakamilika sawa sawa.
Usiwe na wasiwasi juu ya kuanza jambo fulani huku ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja, kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni juu ya wewe kuanza. Fanya ufanyalo na uhakikishe umeanza kufanya jambo lako na usisite hata kidogo kuanza.

Kwa muda ulionao, kwa chochote kile ulichonacho, anza. Usisubiri ukamili wa jambo lolote ule ndio uanze. Usijiweke kwenye mtego wa kuahirisha kwa sababu ya kuanza. Kikubwa anza na kile ulichonacho na hapo ulipo na usisubiri kitu.`
Kama ukitaka uwe kamili kila kitu ndio uanze kufanya hicho unachotaka kufanya, hebu jiulize utajifunza nini kwenye safari ya mafanikio yako? Endelea kufanya huku ukiwa unajifunza na utafika muda utayafikia imafanikio yako kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi ikiwa pamoja na wasomi mambo yao yanashindwa kukamilika au kufanyika kikamilifu kwa sababu tu ya wao wenyewe kutaka kufanya mambo yao wakiwa kamili kwa kila kitu, nikiwa na maana ni watu wa kutafuta ukamili sana.
Naomba labda nikwambie hivi, hata wale watu unawaona wamefanikiwa sana, hawakuanza wakiwa na kila kitu, walianza kidogo na vile walivyonavyo, ila kilichowafanya wakawa hivyo ni kwa sababu ya wao wenyewe kujifunza na kukua.
Ukikubali kuendelea kufanya huku ukijifunza na kukua, itafika muda hata kama ulianza na kidogo sana lakini nakupa uhakika utaweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio, kwa nini, kwa sababu umeamua kufanya pasipo kujali ukamili.
Ili uweze kuondokana na hali ya kuahirisha mambo, acha kabisa kusubiri uwe kamili kwa asilimia zote, wewe fanya hivyo hivyo na utafika muda utaweza kufanikiwa katika hilo na ndoto zako zitatimia na kuwa kweli.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,