google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 30, 2017

Njia Ya Mafanikio Yako Ipo Hapa...

No comments :
Mojawapo ya kosa kubwa linalofanywa na watu wengi katika safari ya mafanikio, ni kule kukata tamaa hasa wanapokutana na changamoto.
Kwa kukata tamaa huko kwa sababu tu ya kukutana na changamoto, naweza nikasema ni moja ya kosa ambalo linaweza kukufanya usifanikiwe.
Washindi katika maisha wanajua kwamba, changamoto au kushindwa kwa namna moja au nyingine sio ‘tiketi’ pekee ya kuanza kukata tamaa mapema.
Inapotokea kitu hakijaleta majibu unayoyataka, sio swala la kukimbilia kukata tamaa bali ni kubadilisha njia hadi uweze kufanikiwa.

Inawezekana kabisa njia unazotumia ni butu na hazifai, sasa hapo sio rahisi sana kuweza kufanikiwa, bali kufanikiwa kunakuja kutokana wewe kutumia njia mbadala.
Kama njia ya kwanza imekataa, jaribu ya pili na kama ya pili imekataa, jaribu ya tatu na nyingine na nyingine tena mpaka kuweza kufanikiwa.
Ipo njia ya kukufikiasha kwenye mafanikio yako, njia hiyo ipo. Ili uifikie njia hiyo, acha kukata tamaa mapema. Sumu kubwa sana ya kufanikiwa kwako ipo kwenye kukata tamaa.
Jifunze sana kutokana na matokeo yanayokatisha tamaa na kisha baada ya hapo tafuta njia mpya utakayoitumia kufanikiwa tena.
Kuendelea kufanya tena na tena hata kama unashindwa ni njia muhimu ya kukusaidia kufanikiwa. Kwani amini njia ya mafanikio yako ipo, huhitaji kukata tamaa.
Kama nilivyokudokezea watu waliofanikiwa wanatumia njia nying sana, ambazo njia hizo huwasidia kuweza kufikia mafanikio yao.
Hata wewe unaweza kutumia njia hizo pia. Lakini usiwe mtu wa kukimbilia tu kuacha kila kitu hasa unapokutana na changamoto.
Maisha ya watu wengi yapo hatarini na ni magumu kwa sabbu ni watu wa kuacha tu hasa wanapokutana na changamoto.
Watu hawa hawajafundishwa au hawajui kutumia njia mbadala, ila wao wanachojua ikitokea changamoto dawa ni moja tu ni kuacha.
Ukiwa hata wewe ni mtu wa kuishi maisha ya namna hii, itakuwia vigumu sana kuweza kufikia mafanikio yako makubwa.
Siri ya wewe kufanikiwa unatakiwa kujifunza kufanya jambo kwa namna nyingi sana, ambazo zitakupa mafanikio na sio kukata tamaa kila unapokuatana na changamoto.
Unachotakiwa kuelewa hapa kupitia makala hii ya leo ni kwamba, njia ya mafanikio yako ipo, acha kukimbia mapema kwa sababu ya changamoto. Changamoto zipo na ni za muda.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,                                        
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Sep 29, 2017

Maeneo Manne Ambayo Unatakiwa Kuwa Msikivu Sana Ili Kujenga Mafanikio Yako.

No comments :
Usikivu ni moja ya kitu muhimu sana katika safari yako ya mafanikio. Unapokuwa msikivu inakusaidia kujifunza mambo mengi sana tofauti na ambapo ungejifanya wewe ni mjuaji wa kila kitu hali ambayo ingekufanya ukose mengi.
Kitu cha kujiuliza ni watu wangapi ambao ni wasikivu, bila shaka ni watu wachache sana ambao wanajenga utulivu wa kusikiliza wengine wanasema nini au wao wenyewe ndani mwao wanasema nini hadi kuweza kufanikiwa.
Kwa kawaida tunapozungumzia usikivu, wengi wanajua ni usikivu wa kuwasikiliza tu watu wengine. Lakini jinsi ilivyo upo usiku wa aina nne ambao kila mtu anatakiwa kuwa nao makini ili kujenga mafanikio yake.

Jenga hali ya usikivu mkubwa ili kujifunza.
1. Usikivu kwa wengine.
Unatakiwa kujifunza kusikiliza wengine wanasema nini, nini maoni yao kwako bila kujali wanachokisema ni chanya au hasi. Kuna kitu cha msingi na cha kubadili maisha yako utakipata kama ni msikilizaji wa wengine kuliko ambavyo ungebaki wewe kama wewe ukawa unafuata yako bila kusikiliza mtu yeyote.
2. Usikivu kwako wewe mwenyewe.
Pia unatakiwa kujisikiliza mwenyewe na kuheshimu maoni yako. Pengine unajiuliza kivipi? Ndani yako kuna sauti ambayo huwa inasema na wewe. Sasa, kuwa makini kusikiliza sauti yako, maana hio ni muhimu sana kuliko hata sauti zinazotoka nje. Ukiwa msikivu kwako utapata uwezo wa kujenga pia mafanikio yako.
3. Usikivu kwa dunia.
Kwa jinsi tunavyoishi, dunia inatufundisha mambo mengi. Unapopata changamoto kuna vitu unajifunza na kwa namna hiyo unatakiwa kujua kujifunza jinsi dunia inavyosema na wewe. Utakuwa ni mtu wa ajabu kama hutaki kabisa kujifunza kutokana na dunia. Yapo mafundisho mengi sana unayoyapata  hata huhitaji kwenda shule.
4. Usikivu kupitia maarifa.
Vile vitu unavyojifunza vina sema bila kujali ni maandishi au kitabu. Sasa jifunze kusikiliza kile ambacho waandishi wanasema, kitabadilisha maisha yako kuliko jinsi ambavyo unang’ang’ana na kuwa mbishi bila kutaka kubadilika. Ukiweza kuyatumia maandishi vizuri yatakusaidia sana kuboresha maisha yako.
Hayo ndiyo maeneo muhimu ambayo unatakiwa kuwa msikivu sana ili yaweze kukusaidia kujenga mafanikio yako. Fanyia kazi maeneo hayo ili yawe msaada mkubwa kwako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Sep 27, 2017

Ukiwa Makini Na Matokeo Haya…Utafanikiwa.

No comments :
Nafikiri na naamini pia, umeshawahi kufanya kitu ambacho haupo nacho makini nacho sana au hutegemei kupata matokeo makubwa kwenye kitu hicho.
Unajua nini kilichotokea wakati unafanya kitu ambacho hukuwa na matarajio nacho sana? ni wazi tu hukufanikinikisha jambo hilo, hicho ndicho kilichokutokea.
Na unajua ni kwa nini hukufanikisha? najua ulikuja na sababu na visingizio vingi sana kwamba umeshindwa kufanya jambo hilo kwa sababu ulizoziweka wewe.
Hata hivyo pia hukufanikisha jambo hilo kwa sababu nguvu ulizokuwa ukiweka hazikuwa nguvu kubwa sana, ulikuwa ukifanya tu kama unacheza na hutilii mkazo.

Kwa hiyo hata unapopata matokeo hayo, hayakukushangaaza sana kwa sababu ni kitu ambacho ulikitegemea kwa kiasi fulani.
Njia na siri ya pekee ambayo inaweza ikakusaidia wewe kutimiza lile lengo unalolitaka au mafanikio uyatakayo ni kuwa makini na matokeo kwanza unayoyahitaji.
Ni rahisi kushindwa kwa chochote kama haupo makini na matokeo unayotaka, kwa sababu kila kitu utafanya kizembe tu, kwa sababu matokeo kwako sio muhimu kivile.
Unapokuwa makini na matokeo unayoyataka,ni wazi utaweka kila aina ya nguvu mpaka kuhakikisha unakipata hicho unachokihitaji bila kuzuiliwa.
Ikiwa hujali sana kile unachokifanya, basi jiulize kwa nini unafanya kitu hicho? Maana hutaweza kuvuna matokeo unayoyahitaji hata kidogo.
Hiyo maanake nini? Unatakiwa uwe na sababu ya kile unachokifanya ili sababu hiyo ikupe nguvu ya kutaka matokeo unayoyahitaji.
Kuanzia leo jifunze kujali sana kile unachokifanya, kifanye kwa ukamilifu na kwa kujali huko utajikuta ukipata matokeo unayoyahitaji.
Hata juhudi unazokuwa unaziweka kwa sababu unajali, zitakuwa ni juhudi zinazokusaidia kwa sababu zinakupa matokeo unayoyahitaji kwenye maisha yako.
Utashindwa na utaendelea kushindwa ikiwa hujali na hauko makini na matokeo ambayo unayahitaji kwenye maisha yako.
Umakini unahitajika sana unatata matokeo yale unayoyahitaji ili uweze kufanikisha chochote kile unachokifanya, tofauti na hapo utakuwa ni mtu wa kushindwa sana.
Nini unachokitaka? Nini unachotaka kukifanikisha kwenye maisha yako? kwa chochote unachokitaka kumbuka, kuwa makini na matokeo, utavuna jinsi unavyopanda.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



Sep 26, 2017

Nguvu Ya Mtazamo Katika Kushindwa Au Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Mtazamo una nguvu ya kubadili hali mbaya inayoonekana na kuwa hali nzuri kabisa. Nguvu yote hiyo ya kubadili hayo inatoka kwenye mtazamo alionao mtu huyo.
Mtazamo unafanya maisha kuonekana ya maana, hata pale ambapo wengi wanaona maisha hayana maana tena na yanachosha.
Mtazamo una nguvu kubwa sana ya kulainisha kile kinachoitwa kigumu na kuonekana kirahisi, hiyo yote ni kazi ya mtazamo.
Unapokuwa upo kati kati ya matatizo, hakuna kitu kingine kinachoweza kukuokoa na kutoka hapo na kuwa na amani zaidi ya kubadilisha mtazamo wako.

Unapobadili mtazamo,  hata kama tatizo lako lilikuwa kubwa sana, tatizo hilo unaona linaanza kulainika na linakuwa linawezekana kutatuliwa.
Wengi wanaoshindwa katika maisha na kuamua kukata tamaa kabisa ni watu ambao mara nyingi wameshindwa kutawala mitazamo yao.
Kiuhalisia unaposhindwa kutawala mtazamo wako na ukajikuta una mtazamo hasi, elewa kabisa maisha yako yatakuwa magumu sana katika kila eneo.
Kwa hiyo unaona kabisa mtazamo una nguvu kubwa sana ya kubadili maisha yako, inategemea tu wewe unautumiaje huo mtazamo wako ulionao.
Ndio kila wakati unashauriwa kukaa na watu chanya, watu ambao wataweza kukusaidia kukujengea mtazamo mzuri wa kufanikiwa.
Kwa hiyo kuanzia sasa hutakiwi kushangaa, unapoona wengine wanafanikiwa na wengine wanashindwa hilo ni swala la mtazamo.
Kwa mfano, utakuta ni watu wanaokaa katika mji mmoja au nchi moja lakini wengine wamefanikiwa na wengine wameshindwa, hapo hakuna kingine zaidi ya mtazamo.
Anguko kubwa la watu linaanza na mitazamo yao. Kwa jinsi unavyokuwa na mtazamo mbovu ndivyo maisha yako yanazidi kuwa mabovu pia.
Lakini mtazamo mzuri una siri kubwa ya kugeuza chochote kuwa mafanikio. Mtazamo mzuri unaweza kugeuza hata maji kuwa almasi.
Mtu mwenye mtazamo mbovu mara nyingi hata apewe fursa nzuri vipi sio rahisi kufanikiwa, kinachomwangusha ni mtazamo wake tu.
Hiyo yote inaonyesha kushindwa kwa wengi kunasabbishwa na mtazamo wake sana, na hapo ndipo ulazima kwa kubadilisha mtazamo unahitajika kwa nguvu zote.
Leo kama unataka kufanikiwa, hebu anza kubadili mtazamo wako ili ukusaidie kwani una uwezo wa kubadili chochote na kuwa kizuri.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Sep 25, 2017

Ubora Wako Unatokana Sana Kufanya Hivi…

No comments :
Kwa jinsi unavyofanya kitu chochote kile kwenye maisha yako, ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi katika kitu hicho.
Kwa mfano, kama wewe ni mwimbaji kwa jinsi unavyoimba kila siku na kufanyia mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uimbaji wako.
Kama wewe ni mwandishi, kwa jinsi unavyoandika kila siku, hivyo ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uandishi wako.
Kama wewe ni mtu wa kujifunza vitu, kwa jinsi unavyojifunza, utashangaa unajikuta unakuwa ‘mlevi’ wa kutupwa wa kujifunza.
Kama wewe ni mtu wa kulalamika, kwa jinsi unavyoendelea kulalamika, hivyo ndivyo sasa utakuwa mlalamikaji mbobebezi, utalalamikia kila kitu.

Fanya kitu, uongeze ufanisi wako.
Kama wewe ni mtu mwenye tabia za kukopa kopa pesa kwa watu, utashangaa kwa jinsi siku zinavyokwenda unakuwa mkopaji kweli na una madeni kibao.
Kama wewe ni mtu wa kutoa sababu, basi hutafanya kitu cha maana, ni rahisi kuendelea kutoa sababu sana karibu kwa kila mtu.
Kama wewe ni mtu wa visasi, kuwa makini hapo, unaweza ukawa na mtu wa visasi kwa watu wengi sana kwa sababu ndio kitu unachokifanya.
Kama wewe ni mtu unayehakikisha jambo unalolianza lazima lifanikiwe, basi elewa utaendelea kufanikisha pia mambo mengine kwenye maisha yako.
Kwa chochote unachokifanya, bila kujali kitu hicho ni chanya au hasi utazidi kupta matokeo bora ynayoendana na kitu hicho unachokifanya kila siku.
Hebu jaribu kuangalia katika maisha yako ni kitu gani ambacho unakifanya sana? kwa kifanya kitu hicho utapata matokeo yake.
Hivyo basi kila wakati, chagua kufanya kwenye maisha yako mambo bora na fanya kila siku, baada ya muda utakuwa bora kwenye mambo hayo na kufanikiwa vikubwa.
Ni vigumu sana kuwa mshindi katika maisha yako kwa kufanya kitu mara moja na kutegemea mafanikio makubwa. Unatakiwa kufanya kila siku.
Kwa hiyo unaona mafanikio au kushindwa ni matokeo ya kufanya kitu fulani unachokifanya kila siku na kwa muda mrefu.
Kufanikiwa au kushindwa hakutokei mara moja kama wengi wanavofikiri, ni matokeo ya kuwekeza nguvu zako kila siku kwenye jambo hilo.
Anza leo kufanya mambo yatakayokusaidia kujenga ubora utakao kusaidia kufanikiwa sana na sio yatakayokuangusha.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





Sep 24, 2017

Kama Utaitumia Nguvu Hii… Ndiyo Itakayokufanya Ufanikiwe.

No comments :
Kwa nguvu ya ung’anga’nizi, ndiyo inayopelekea tone moja la maji linalodondoka kila siku ipo siku livunje jiwe hilo kabisa.
Kwa nguvu ya ung’ang’anizi, mbegu dogo kabisa inauwezo wa kukua kwenye tawi la mti mkubwa na hatimaye kuwa mti mkubwa sana pia.
Kwa nguvu ya ung’ang’anizi kila mtu ana uwezo wa kubadilisha maisha yake, hata kama mtu huyo yupo kwenye wakati mgumu sana.
Kwa nguvu ya ungang’anizi, ndiyo inayofanya maisha ya wengine yawe mazuri na maisha ya wengine kuwa mbaya kutokana na kung’ang’ania vibovu.

Kwa nguvu ya ung’ang’anizi, ndio inayompa mtu mafanikio hata kama anatokea chini kabisa bila kuwa na kitu.
Hakuna kinachoshindikana, hakuna mafanikio ambayo utashindwa kuyapata kama kweli leo, utaamua kung’ang’ania kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Nguvu unayotumia kung’ang’ania mambo, hata kama nguvu hiyo ni kidogo itakusaidia sana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa sana, kwa sababu ya kushindwa kutumia nguvu ya ung’ang’anizi kwenye yale mambo wanayoyafanya.
Sio ajabu sana kumkuta mtu kaanzisha jambo leo, lakini kesho mtu huyo akikutana na changamoto anaacha kila kitu.
Huwezi kufanikiwa kwa viwango vikubwa kama wewe si king’ang’anizi. Kama mafanikio kweli  utayapata, lakini utapata mafanikio ya rasharasha.
Unatakiwa utambue hata ukutane na changamoto, unatakiwa kukomaa mpaka kieleweke. Hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi.
Ikiwa kuna kitu unakifanya hata sasa na unaona hakikupi matokeo ya upesi kama unavyotaka, jipe muda kwanza na usikimbilie kukata tamaa.
Kama utakuwa ni mtu wa kukata tamaa mapema na kushindwa kuwa king’ang’anizi basi elewa utashindwa kwenye mambo mengi sana.
Ifike mahali ujiulize ni wapi unapotaka kufika kimaisha, ni wapi unapotaka kwenda na ukishajua hivyo amua kabisa kung’ang’ania mpaka kieleweke.
Usikubali kitokee kitu eti ambacho kitakuzuia kufanikiwa kwako. amua kwamba iwe itakavyokuwa bila kujali utatumia muda gani mafanikio yako ni lazima.
Ukijivusha ujasiri huo wa kuwa king’anganizi mafanikio yeyewe yatakupisha na kutakuwa hakuna namna nyingine ya kukuzuia.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






Sep 23, 2017

Ongeza Uwezo Wako Wa Kufikia Mafanikio Yako Hivi…

No comments :
Haijalishi maisha yako ni mazuri  kiasi gani, lakini unayo nafasi ya kuyafanya maisha yako yakazidi kuwa bora kuliko ya hapo ulipo
Haijalishi una hali ngumu vipi za kimaisha, lakini unaweza kuboresha maisha yako kidogo kidogo na mpaka kuwa bora kabisa.
Haijalishi ni kwa jinsi gani unajua mambo mengi sana, lakini kwako ipo nafasi ya kujifunza na kuendeleza kupata maarifa yatakayokusaidia.
Chochote unachokifanya leo jiulize, kina uwezo wa kukua kesho na kuendelea kukupa mafanikio makubwa?

Ongeza uwezo wa mafanikio yako.
Ni kitu gani ambacho utakifanya leo na kikaendelea kukuweka juu tena na tena kwenye maisha yako ya kimafanikio?
Ukikaa na ukatulia, utagundua zipo njia ambazo zina uwezo wa kukufanya ukakua na kuongeza nafasi ya mafanikio yako sana.
Huhitaji kujilinganisha na wengine ili kuwa bora, unatakiwa kujilinganisha wewe tu mwenyewe na kuongeza ubora ulionao kila wakati.
Usikubali kuyafanya maisha yako yakaonekana mabovu kwa sababu ya kusimama au kuridhika kwa namna fulani.
Mashujaa katika maisha ni watu ambao wanajipa changamoto sana za kukua kila siku kwenye maisha yao.
Hicho ndicho kitu ambacho unatkiwa ujipe au ukifanye ili kufanikiwa. Unatakiwa ujipe changamoto ambazo zitakusaidia kukua.
Kwa mfano, kama umeamua kusoma, soma idadi kubwa sana ya vitabu ambayo itakufanya uwe mkomavu kiakili.
Kama umeamua kuwekeza, wekeza sana na isifike mahali ukatikisa kichwa na kusema kama ni kuwekeza sasa imetosha.
Unatakiwa kukua, unatakiwa kuongeza misuli ya kile ukifanyacho na kuwa kikubwa sna zaidi ya hapo ulipo kwa sasa.
Ukumbuke hakuna mtu ambaye ataweza kukuzuia katika hilo, zaidi yako wewe. Unao uwezo mkubwa wa kuongeza mafanikio yako.
Hautakiwi kusimama sasa, unachotakiwa kufanya sasa ni kuweka nguvu zako za uzingativu eneo unalotaka ukue.
Ukishaweka nguvu zako za uzingativu eneo hilo, anza kufanyia kazi huku ukiweka kila aina ya juhudi inayotakiwa ili kufanikiwa.
Nuia kubadilisha maisha yako tena, nuia kubadilisha matokeo ya maisha yako tena, nuia kubadilisha chochote maishani mwako.
Usikubali kukaa kama jiwe, mwanza wa mabadiliko katika maisha yako ni sasa kwa wewe kukubali kuuongeza uwezo wa mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



Sep 22, 2017

Sifa Moja Ya Muhimu Sana Katika Kukupa Mafanikio.

No comments :
Mafanikio yako yanakuja kutokana na wewe kuwa wa muhimu. Mafanikio yako ya kweli hayaji kwa sababu ya bahati nasibu wala hayaji kwa sababu ya kuwanyonya watu wengine sana, mafanikio yako ya kweli na ya kudumu yanakuja kwa sababu ya wewe kuwa wa muhimu katika maisha yako.
Kwa jinsi yoyote ile unavyotafuta mafanikio unatakiwa kuwa wa muhimu na kutoa thamani inayohitajika ili kufikia mafanikio yako. Hutakiwi kuwepo kuwepo tu kwenye maisha yako, unatakiwa uwe na machango wa kimafanikio kila siku iitwayo leo.
Jiulize kitu gani ambacho utakifanya sasa kitakuwa na mchango na umuhimu kwenye maisha yako? Jiulize tena ni juhudi gani kubwa ambazo unaendelea kuweka mwenye kazi na hata kwenye maisha yako kwa ujumla?

Kuwa mtu wa thamani utafanikiwa.
Ni rahisi kuweza kuiba na kufanya kitu chochote ambacho sio haki ili ujipatie mafanikio. Lakini ukumbuke kwa njia hizo sio rahisi kabisa kupata mafanikio ya kweli yatakayokufanya ung’are na uwe miongoni mwa watu waliofanikiwa.
Kupata mafanikio ya kweli kunaanza ndani mwako kwanza, kutokana na thamani unayoitoa, ambapo thamani hiyo ndiyo itakayo kufanya kila kona uwe wa muhimu na kupelekea kila mtu akikutamani uwe nae karibu kwake.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona ili kufanikiwa, unahitaji kuwa wa tofauti, unahitaji kuwa wa thamani, unahitaji kuwa wa pekee ili kutengeneza thamani ambayo ukiipata ni lazima uweze kufanikiwa hata kama mazingira yanakataa.
Kama unatilia shaka hilo la umuhimu wako kwenye maisha ya wengine, ngoja tu nikwambie wewe ni wa pekee sana na mchango wako mkubwa unahitajika katika maisha ya wengine pia ili uweze kuyabadilisha.
Kama una umuhimu mkubwa hivyo kwa wengine, jifunze kuweka juhudi kubwa sana kila siku ili kutengeneza umuhimu na thamani yako zaidi. Umuhimu wako hauji kwa kukaa tu, umuhimu wako unakuja kutokana na kujituma na kuweka juhudi hadi kufanikiwa.
Anza kuwa wa muhimu leo kwa kubadilisha maisha ya wengine, kwa jinsi unavyobadilisha maisha ya wengine unazidi kuwa baraka kwa wengine , nawe pia maisha yako yanakuwa yanabadilika vivyo hivyo.
Ni kipi unachosubiri kuwa wa muhimu? Kuwa wa muhimu, ni sifa mojawapo kubwa sana ya kukupa mafanikio yako.  Anza sasa na chukua hatua katika kuelekea kufikia mafanikio yako makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



Sep 21, 2017

Mara Ngapi Umeshindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Hizi?…

No comments :
Ni mara ngapi umekuwa ukitaka kubadilisha hali fulani hivi kwenye maisha yako, lakini cha ajabu tena umekuwa ukikata tamaa kwa mara ya kwanza hasa pale unapokutana  na changamoto kwenye maisha yako?
Ni mara ngapi umekuwa ukijiwekea malengo yako na kusema lazima nitatimiza lengo hili, lakini kitu cha ajabu umekuwa ukiyasahau malengo hayo mara moja na tena umekuwa huyakumbuki kama vile hukuweka malengo kabisa?
Ni mara ngapi umekuwa ukitoka nje ya mstari wa malengo yako uliyojiwekea hasa kutokana na maoni au malengo ya watu waliokwambia kwamba huwezi kitu hiki na wewe kutokana na kuwasikiliza ukaacha kweli?

Usikatishwe tamaa na chochote
Ni mara ngapi umekuwa ukisema utaweka akiba, ambayo itakusaidia baadae kuwekeza kwenye maisha yako, lakini umekuwa hufanyi hivyo kutokana na sababu zako ambazo unazijua wewe?
Ni mara ngapi umekuwa ukitoa sana visingizio badala ya kutoa matokeo yanayotakiwa kutolewa? Umeshawahi kujiuliza hili? Kila kitu unakuwa umejipanga kama vile unataka kutoa sababu badala ya kutoa matokeo yanatakayokusaidia kwenye maisha?
Ni mara ngapi umekuwa ukiishi maisha chini ya kiwango, maisha ya kuhuzunika na kuacha kuchukua hatua sahihi ambazo hatua hizo zinaweza kukupeleka kwenye mafanikio yako makubwa uyatakayo?
Muda huu na wakati huu ulionao una mahusiano moja kwa moja na kesho yako ya mafanikio. Hivyo, jinsi ambavyo umekuwa ukiahirisha mambo na kusema utafanya hili na hufanyi, elewa kabisa ndivyo umekuwa ukijiangusha mwenyewe kwenye maisha yako.
Unatakiwa kuishi kwa nia moja na hamu kubwa ya kujitoa hadi kufikia mafanikio. Lakini kama kila mara unasema unafanya hili halafu hufanyi, utakuwa unajenga tabia ambayo moja kwa moja msingi wake mkubwa ni kukuangusha na si kufanikiwa.
Najua changamoto kweli zipo katika maisha, lakini changamoto hizo isiwe sababu kubwa ya wewe kuacha mipango yako kila mara na kutoka nje ya mstari. Wakati wa kufanya na kutimiza ndoto zako ni sasa, fanya kitu.
Usikubali kushindwa kwenye maisha yako kwa sababu ya kutokufanya, usikubali kushindwa eti kwa sababu kila mara unaahirisha. Chukua hatua sahihi za kubadili maisha yako ili ufikie mafanikio makubwa.
Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




Sep 20, 2017

Jinsi Unavyoweza Kujifunza Kuweka Nguvu Za Uzingativu Eneo Moja.

No comments :
Ni kama kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona mtu akiwa anakula huku macho yake yote yakiwa kwenye simu, tv au kitu kingine tofauti. Hiki si kitu cha ajabu kwa siku hizi, japo naweza kusema limekua kama tatizo ambalo linawasumbua watu wengi.
Watu wengi kwa nyakati hizi wamekosa sana utulivu, wamekuwa ni watu wakutaka kufanya mambo mengi sana na kwa mkupuo. Kutokana na hili, ufanisi wa kazi umekuwa ukipungua na hakuna cha maana ambacho kimekuwa kikifanyika.
Kutokana na ujio wa teknolojia hasa ingizo la simu janja/ ‘smart phone’ hili limechangia sana kwa kiasi kikubwa kwa kuelekeza watu nguvu zao nyingi kwenye simu na kusahau majukumu ya msingi. Kwa mfano, ukiingia kwenye gari, ofisini au nyumbani ni rahisi kumkuta karibu kila mtu anatazama simu yake.
Lakini ukichunguza hata kile anachokitazama kinaweza kisiwe na maana sana, lakini ni hali ambayo ipo na inapelekea badala ya kufanya majukumu ya msingi, muda mwingi unakuwa unapotea kwenye simu na bila faida yoyote.

Weka nguvu zako za uzingativu eneo moja.
Nimekupa mfano kidogo ili upate picha ya kile ambacho nataka kusema. Simaanishi tu kwamba simu peke yake ndio imekuwa chanzo cha watu kufanya mambo kwa undumila kuwili, la hasha, bali watu wamekuwa na mambo mengi sana wao kama wao kutokana na kuibua tabia hii mpya.
Kwa sasa haishangazi tena kama mtu akianza jambo hili kabla hajamaliza anataka tena kurukia jambo lingine. Unaweza ukajiuliza kama akili haitulii sehemu moja, ukishika hiki unaacha na unakimbilia kitu kingine, sasa kwa mwendo huo ni kitu gani ambacho utaweza kweli kukifanikisha kwenye maisha yako?
Kwa kifupi hili ni tatizo na kwa wengi imekuwa ngumu sana kuweza kuvunja tabia hii kwa sababu ya mazoea, ingawa zipo mbinu au njia za kufanya hivyo. Kitendo cha kushindwa kuishinda hali hii, ni sawa na kuamua kuendelea kuharibu maisha yako.
Kwa vyovyote vile iwavyo, unatakiwa kujua jinsi utakavyoweza kuweka nguvu zako za uzingativu katika eneo moja ili uweze kutenda mambo yako kwa ufanisi na mafanikio. Itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa ikiwa utashindwa kuvunja tabia hii. Je, unawezaje hili;-
Hivi ndivyo jinsi unavyoweza kujifunza kuweka nguvu za uzingativu eneo moja.
1. Chagua jukumu moja la muhimu kutekeleza.
Asubuhi unapoamka mara baada ya kusali na kufanya ‘meditation,’ kabla hujawasha simu yako anza kutekeleza jukumu lako la muhimu. Najua unaweza ukawa una vitu vingi vya kufanya, lakini chagua kitu kiomoja tu cha kuanza nacho na vingine vyote visahau kwa muda mpaka ukamilishe jukumu lako moja la muhimu kwa wakati huo.
2. Jukumu ulilichagua lifanye kwa dakika 15 bila kuacha.
Katika dakika hizi usikubali kuingiliane na kitu chochote, tumia dakika hizo vizuri nguvu zako zote zihamishie hapo. Usichague dakika nyingi sana za kuanza kuweka nguvu za uzingativu kwa pamoja, anza kwanza na dakika chache, ikitokea umeshindwa dakika 15, punguza ziwe hata 10 au 5 lakini lazima uibuke mshindi.
3. Fanya kila siku na kwa kila kitu.
Ili tabia hii iweze kukaa na iwe yako, fanya kila siku na kwa kila kitu kiwekee nguvu ya uzingativu. Unapoamua kufanya kitu fulani mawazo yako yote hamishia hapo na bila shaka hapo utakuwa na ufanisi mwema wa kazi yako. Lakini ikiwa utashindwa zoezi hilo hiyo itakuwa ngumu kwa wewe kuweza kufanikiwa.
Inabidi ieleweke kwamba, kuweka nguvu za uzingativu katika eneo moja kwa masaa kadhaa, kwa siku kadhaa na kwa muda fulani maalumu kuna leta mabadiliko ya maisha yako bila kipangamizi chochote.
Ni jukumu lako leo kuanza kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kila ukifanyacho ili kikuletee mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




Sep 19, 2017

Ukiweza Kutumia Muda Huu Vizuri, Utafanikiwa.

No comments :
Kama unavyojua dakika moja si muda mrefu sana. Hata hivyo pamoja na kwamba muda huo ni mfupi sana ila kila kitu kilichofanyika duniani na kikaleta mafanikio, kilianza kufanywa kwa kuanza na dakika moja tu na sio vinginevyo.
Kipi ambacho unataka kukifanya, hakitaanza kufanywa kwa dakika moja ya kwanza, bila shaka hakuna. Kama una kitu unataka kukifanya na unaona uvivu fulani jipe muda wa dakika moja tu kwanza, dakika hiyo itakupa nguvu ya kuendelea zaidi.
Kama unaweza kufanya kitu chochote kwa dakika moja, kama unaweza kuvumulia kwa dakika moja, basi unaweza kuendelea zaidi ya hapo kwa kutumia muda wako vizuri sana ikiwa pamoja na kila dakika unayoipata kwenye maisha yako.
Ukimudu kuweza kuitumia dakika moja yako vizuri, itakusaidia kuokoa muda wako mwingi ambao ulikuwa unaupoteza bila manufaa yoyote kwako. Dakika moja ukiitumia vizuri na ukaendelea kutumia zingine vivyo hivyo, ni msingi mkubwa wa mafanikio yako.

Sep 18, 2017

Jinsi Watu Wanavyoweza Kukurudisha Nyuma Kwenye Maisha Yako, Ikiwa Utawaruhusu.

No comments :
Wapo watu katika safari ya maisha ambao wapo tayari kukusaidia kukua kimafanikio na kukuona wewe ukifanikiwa na pia wapo watu katika safari ya maisha ambao wao wapo tayari kukuona wewe ukikamwa na hawapendi sana ufanikiwe.
Unapokuwa na kundi kubwa la watu hasa hili la pili ambalo halitaki kukuona wewe ukifanikiwa kwenye maisha yako, uelewe kabisa unakuwa upo katika hatari kubwa sana ya kutokufanikiwa kwa kile ukifanyacho.
Nasema hivyo kwa sababu, watu hawa wanakuwa wanatumia njia au mbinu zao kuhakikisha unakwama au husogei kabisa, yaani wanataka uwe kama wao. Je, watu hawa wanakurudisha vipi nyuma kwenye maisha yako?

Kuwa makini na watu wanaotaka kukurudisha nyuma.
1. Kukukosoa sana.
Watu wenye lengo la kukurudisha nyuma, moja ya njia au mbinu wanayoitumia ni kukosoa sana. kila wakati watajaribu kukuonyesha kwamba wewe ni mtu wa kukosea na hadi ujione hufai. Kwa mbinu hii ukiikubali hutafanya kitu, zaidi utatulia usifanye kitu  kwa kuogopa kukosolewa.
2. Kutokuthamini mchango wako.
Njia nyingine ambayo watu wenye lengo la kukurudisha nyuma kwenye maisha huitumia sana ni kutokujali mchango wako kabisa. Kila utakachokifanya kitaonekana kwao hakuna kitu. Sasa kwa kuwa umejua hili usijisikie vibaya, kama kuna kitu umekifanya wewe endelea kukifanya kwa moyo wote kwa sababu unajua ni nini ukifanyacho.
3. Kukufanya ujitilie shaka.
Kati ya kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu kwenye maisha yako ni kumruhusu mtu mwingine akushushe au akutilie shaka ule uwezo wako mkubwa ulionao. Watu wanaotaka kukurudisha nyuma mara nyingi hutumia mbinu ya kutaka kukufanya ujione huwezi kitu yaani wewe ni mtu wa kawaida tu. Ukiruhusu hali hii utakwama.
4. Kutaka kukufanya ujione maisha yako yamekwama kabisa.
Mbali na kukukosoa sana, kutokukuthamini mchango wako na kukufanya ujitilie shaka, pia watu wanaokurudisha nyuma wanataka wakuonyeshe maisha yako yamekwama kabisa na hakuna njia mbadala ya kuweza kutoka hapo. Hapo watakuonyesha kwamba wewe huwezi kitu.
Hivi ndivyo watu wanavyoweza kukurudisha nyuma kwenye maisha yako ikiwa utawaruhusu kufanya hivyo. Kitu cha msingi ni kuwa makini na njia zao hizo na kuepuka kuendana kama wao wanavyotaka iwe.
Chukua hatua na kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Sep 17, 2017

Sababu Zinazofanya Watu Wengi Kufanya Maamuzi Mabovu.

No comments :
Kati ya kitu kimojawapo kinachofanya watu washindwe sana kwenye maisha ya mafanikio ni kile kitendo cha kufanya maamuzi mabovu. Maamuzi mabovu yanaharibu na yanapoteza maisha ya mafanikio ya watu wengi sana.
Ni vyema kujua maamuzi mabovu ni chanzo cha kushindwa kwa watu wengi sana na maamuzi hayo mabovu yanafanywa karibu kila siku na wengi. Kitu cha kujiuliza, je, ni kwanini watu wengi wanafanya maamuzi mabovu ambayo yanapelekea kuharibu maisha yao?
1.  Mitazamo mibovu waliyonayo.
Kitu ambacho kinasemwa na wataalamu wengi wa mafanikio kwamba kinapelekea kwa watu wengi kuwa na mamuuzi mabovu mitazamo mibovu au ‘poor mindset’ walizonazo, hiki ndicho kitu kinachofanya watu wengi wanakuwa na maamuzi mabovu sana.
Hivyo ili kuwa na maamuzi sahihi, unatakiwa kuwa na mtazamo sahihi. Na mtazamo sahihi hauji hivi hivi tu bali ni matokeo ya kujifunza kila siku kupitia vitabu na kujua mawazo ya wengine. Ukijifunza hiyo ni njia itayokusaidia kuwa na mtazamo sahihi utakao kufanya uwe na maamuzi sahihi pia.

2. Kufuata sana maamuzi ya watu wengine.
Kuna wakati maamuzi mabovu yanakuja kwa sababu tu ya kufuata maamuzi na taratibu za jamii. Hapa unajikuta mtu unaamua jambo fulani kwa sababu jamii yako inafanya hivyo au inaishi hivyo na wewe unaamua kuamua  hivyo.
Mfano wa athari za maamuzi haya zinajitokeza kwa watu hasa wanapokuwa wanataka pengine kujiunga na masomo ya aina fulani, mathalani, utakuta kozi fulani inasemekana inalipa sana ukiisoma, kwa sababu hiyo utashangaa na mtu mwingine anaifuata, pengine kumbe kwa maamuzi hayo ni mabovu na kozi hiyo inaweza isimsaidie.
3. Kutokujielewa.
Mbali na maamuzi mabovu na kufuata maamuzi ya watu wengine kitu kingine kinachopelekea maamuzi mabovu ni kutokujielewa. Watu wengi wanachelewa sana kujielewa bila kujijua na matokeo yake hufanya maamuzi mabovu sana kila wakati.
Ili kuepuka kuendlea kufanya maamuzi mabovu elimu ya utambuzi inahitajika karibu kwa kila mtu ambayo itasaidia kufanya maamuzi yaliyobora. Bila kupata elimu ya utambuzi itakuwa ni kazi bure tu maamuzi mabovu yataendeea kufanikiwa na kuharibu maisha.
Kama tulivyoeleza kila wakati unapoona maamuzi mabovu yamefanikiwa sehemu yoyote ujue kabisa sababu kubwa zinazochangia ni pamoja na kutokujielewa, mitazamo mibovu na kufuata mitazamo ya watu wengine.
Chukua hatua na endelea kutembelea dirayamafaniko.blogspot.com kujifunza kila siku..
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Sep 16, 2017

Ili Ufanikiwe, Ishi Kwa Sababu Hii…

No comments :
Kipo kitu kwenye maisha yako ambacho kinakufanya uamke asubuhi na mapema. Kipo kitu ambacho kinakufanya uongeze juhudi zako hata kama unakutana na changamoto za kila aina. Kitu hicho kinaweza kuwa ni ndoto au yale malengo unayotaka kuyakamilisha kwenye maisha yako.
Hiyo yote inaonyesha unaamka asubuhi na unaweka juhudi bila kukata tamaa kwa sababu ipo sababu inayokufanya ufanye hivyo, sababu yenyewe si nyingine bali ni kukamilisha malengo yako. Hiyo hasa ndiyo sababu kubwa inayokufanya ufanye kila linawezekana mpaka kuona mipango yako yote inatimia.
Kwa hiyo unachotakiwa kuelewa ipo sababu, katika kila kitu ambacho unatakiwa kukifanya. Unatakiwa kuielewa sababu hiyo vizuri ili ikusaidie kuchochea moto mkubwa wa mafanikio ulio ndani mwako. Ukiwa huna sababu ya hicho unachokifanya utashindwa kuweka juhudi kubwa na mwisho wa siku utashindwa tu.

Ishi kwa sababu maalumu.
Anza leo kuishi kwa sababu, jiulize kitu hicho unachokifanya sasa, kwa nini unakifanya, chanzo cha msukumo wake ambao unatoka ndani mwake ni nini hasa? Ukishaijua hiyo sababu itakufanya usikate tamaa na kila wakati utatamani sana kukifanya kitu hicho ili utimize sababu ya kufanya kitu hicho.
Watu wengi katika maisha wanajikuta hawasogei sana au ni watu wanaotaka kusukumwa sukumwa tu, hiyo yote ni kwa sababu ni watu ambao hawajui hasa sababu ya kufanya hivyo wanavyotakiwa kufanya. Ukiwa hujui hasa sababu inayokusukuma kufanya jambo unalolifanya sio rahisi kufanikiwa.
Hata safari yoyote unapoianza asubuhi, sina shaka unakuwa una sababu kwa nini unaenda safari hiyo. Sijawahi kuona mtu anasafiri tu ilimradi asafiri, lazima awe na sababu huko anakoenda anaenda kufuata nini? Bila ya kuwa na sababu ya hiyo safari basi itakuwa safari hiyo ni kazi bure.
Halikadhalika, maisha yetu hasa kwa yale mambo tunayoyafanya yanatakiwa yawe na sababu haswaa, sababu ndio msingi wa kwanza wa kukusaidia kuweza kupiga hatua za kufanya hicho unachotakiwa kukifanya. Hatua zako zitakuwa imara na utafika mbali sana ikiwa unajua sababu ya kile hasa unachokifanya.
Chukua hatua leo na anza kuishi kwa sababu, hapo utafika mbali kimafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,