google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 25, 2015

Mambo 5 Yatakayokusaidia Kutokuwa Na Mawazo Mengi Yaliyopitiliza.

No comments :
Kati ya tatizo ambalo huwa ni kubwa na linawakabili baadhi yetu bila kujua ni tatizo la kuwa na mawazo mengi. Wapo watu ambao huwa wanafikiria sana matatizo yao, shida zao au changamoto zao kiasi kwamba kwa wengine hupelekea kama kuchanganyikiwa. Natambua umeshawahi kukutana na watu wa namna hii mara kwa mara tu.
Kuna ambao ulipokutana nao walikuwa ni watu wa kuongea peke yao njiani. Pia kuna wengine ambao uliwahi kukutana nao wakiwa ni watu wa kujiinamia tu muda wote. Lakini watu hawa chanzo chao kikubwa ni nini kila ulipowafatilia, hakuna tatizo lingine, zaidi ya hili la kuwa na mawazo mengi ambayo yapo akili mwao muda mrefu.
Kitu kibaya kuliko vyote kwa binadamu ni kwamba, tatizo hili kwa bahati mbaya linapoanza kwa mtu kuisha kwake huwa sio rahisi sana. Tuchukulie kwa mfano umekuwa una mawazo mengi ya mara kwa mara yaliyokupelekea ukaanza kuongea mwenyewe. Tatizo kama hili likisha kuanza, kukuisha litachukua muda mwingi au linaweza lisiishe kabisa na ukawa ndiyo umechanganyikiwa. kwa hiyo ni lazima kuepuka kutokujiweka katika hali ya kuwa na mawazo mengi  hasa kutokana na ukubwa wa athari zake.
Sasa unawezaje kutoka kwenye tatizo hili la kuwa na mawazo mengi?
1. Ishi sasa.
Wengi wanapata tabu na kujikuta wakiwa na mawazo sana kutokana na wao kuamua kuishi jana au kesho. Hapa ili uweze kuondokana na mawazo yanayokutesa unatakiwa kusahau kila kitu kinachokusumbua kiwe kimetokea jana au kiwe kinakuja kesho. Kama kuna deni unalotakiwa ulilipe kesho lisahau mara na ishi sasa kesho hiyo ikifika itaeleweka hapo hapo.
Ruhusu mawazo yako yafikirie pale ulipo. Acha kujibebesha mizigo mingi ambayo huwezi kuibeba kwa pamoja. Acha kujibebesha matatizo ya jana na ya kesho halafu yote ukawa nayo leo. Kwa hilo hutaweza zaidi utazidi kuwa na mawazo kama uliyonayo sasa. Weka maisha yako yawe huru kwa kuamua kuishi sasa na sio kesho.

2. Jijengee mitazamo chanya.
Siri nyingine itayokufanya uishi kwa kutokuwa na mawazo mengi sana ambapo wakati mwingine unahisi hata kuchanganyikiwa ni kwa wewe kujijengea mtazamo chanya. Fikiria yale mambo yanayokufurahisha na kukupa matumaini. Acha kuweka fikira zako sana kwenye jambo linalokusumbua, hiyo itakuongezea mawazo zaidi.
Kwa jinsi utakavyoendelea kufikiria yale mambo yanayokupa furaha, ndivyo ambavyo utajikuta mawazo mengi ambayo ulikuwa nayo yanazidi kupungua kidogo kidogo. Kumbuka, unapata kile unachikzingatia. Kama unazingatia furaha basi basi utapata furaha. Kama unazingatia matatizo halikadhalika utapata hayo hayo matatizo kwenye maisha yako.
3. Kuwa makini na mawazo yako.
Katika kipindi ambacho unakuwa na mawazo mengi zaidi, jambo ambalo unatakiwa kuchunga sana ni mawazo uliyonayo. Ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini na jinsi unavyoruhusu mawazo yako yaingie akilini mwako. Wengi ukumbuke huwa tunapata mawazo hasi pengine kutokana na maneno ya watu ambayo huwa tumeambiw.  Sasa hayo ni moja ya mambo ambayo tunayotakiwa kuwa makini nayo sana.
Hata hivyo, kumbuka mara nyingi jamii tunayoishi ni hasi sana hivyo kuweza kuwa chanya wakati wote inaweza ikawa ni jambo gumu zaidi. Hivyo kitu cha kufanya ni kuhakikisha kila mara na kila wakati kama mtu akikuuzi achana naye na usipeleke hayo mawazo kichwani mwako moja kwa moja. Hiyo itakuwa njia rahisi sana ya kukufanya usiwe na mawazo mengi akili mwako.
4. Badilisha mazingira.
Inawezekana ukawa unazidi kuwa na mawazo zaidi kutokana na mazingira uliyopo. Kitu pekee cha kufanya kwako ni kuhakikisha unabadili mazingira hayo yanayokuplekea uwe na mawazo hayo. Unaweza ukaenda katika eneo tulivu kama baharini au ziwani kupata upepo mwanana. Kwa mazingira kama hayo ni lazima mawazo yako yabadilike.
Kwa hiyo ni lazima uendelee kutokung’ng’ania mazingira ambayo kwako siyo rafiki yanayokufya uendelee kuwaza mawazo yaleyale kila wakati. Kaa mbali na mazingira hayo hiyo itakusaidia sana katika hali ya kuweza kuondokana na mawazo hasi yanakusumbua. Ukitumia mbinu hii itakupa matokeao chanya na ya muda mfupi kuliko unavyofikiri.
5. Fanya tahajudi(Sala).
Ni jambo zuri sana pale unapokuwa na mawazo ikiwa utafanya tahajudi au sala. Hiyo itakusaidia kuyaweka mawazo yako katika hali tulivu zaidi. Unaweza ukafanya hili kwa kutafuta eneo ambalo ni tulivu na ukawa unafanya sala au tajudi angalau kwa muda mchache sana kwa siku. Hiyo itakusaidia kujenga kupunguza mawazo mengi uliyonayo.
Nakutakia siku njema na endelea kujifunza kila siku ila usikose  kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia matandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

Nov 24, 2015

Kama Utatumia Kanuni Hii, Mafanikio Ni Yako.

No comments :
Siku zote elewa ukweli huu, chochote unachokifanya katika maisha yako kinauwezo wa kukufanikisha. Hiyo haijalishi kitu unachokifanya ni kidogo au kikubwa kiasi gani. Kitu cha kuzingatia ili kupata mafanikio hayo ni kukifanya kwa juhudi zote huku ukitumia kanuni za mafanikio. Kanuni hizi za mafanikio zinapotumika ni lazima mafanikio hutokeo.
Bila shaka unajua hili na ni mara nyingi tumekuwa tukiongelea juu ya umuhimu wa kutumia mbinu na kanuni mbalimbali za mafanikio ili kutufanikisha. Sababu ya kubwa ya kufanya hivi ni kwa sababu kila zinapotumika matokeo chanya huweza kuonekana. Leo hii napenda nikukumbushe kanuni moja nyingine ya mafanikio ambayo ukiitumia ni lazima ibadili maisha yako kwa sehemu kubwa.
Kanuni hii inasema ‘fanya kama kila mtu anakuangalia’. Kwa kila jambo unalolifanya katika maisha yako lifanye kama vile mtu anakuangalia. Kama ni malengo panga malengo yako ukiamini kabisa pembeni yako kuna mtu anakutazama. Kama ni kupokea simu, pokea simu ukiamini kuna mtu anakutazama. Kwa kila tendo na mwenendo mzima fanya hivi kama unatazamwa na mtu mwingine.
Kwa kufanya hivi, itakusaidia sana kufanya mambo yako kwa umakini mkubwa na utakuwa bora zaidi siku zote. Hebu jaribu kufikiria wakati ambapo ulifanya kazi zako kwa kusimamiwa, hizo kazi zako ulizifanyaje? Bila shaka ulifanya kwa umakini sana. Na ulifanya hivi kwa sababu ya kuogopa kuharibu kile kitu ambacho ulikuwa ukisimamiwa na kuonekana wa ajabu.

FANYA KAMA KILA MTU ANAKUANGALIA
Hivi ndivyo kanuni hii inavyofaya kazi. Itumie kanuni hii, kwa kujijengea picha na kujitazama wewe kama vile unavyotazamwa na mtu mwingine ukifanya mambo yako. Kwa hili bila shaka hutaleta mchezo ni lazima uwe makini. Fikiria jambo hili pia, kama ingekuwa inatokea malengo yako ukayaweka hadharani ni nini kingetokea? Bila shaka ungekomaa sana mpaka yatimie. Unajua kwa nini? Kwa sababu usingekuwa tayari kukubali kuchwekwa kwa kushindwa kutimiza malengo yako.
Mara nyingi wengi wetu tunaharibu katika maisha yetu kwa sababu ya kujua kwamba eti hatufatiliwi. Jifunze kujisimamia mwenyewe kwenye maisha yako kama vile ambavyo unasimamiwa na mtu mwingine. Kumbuka siku zote hili katika maisha yako, ili kufikia mafanikio makubwa. FANYA KAMA VILE MTU ANAKUANGALIA.
Kwa umejua hili jipe ahadi mwenyewe ya kufanya kila jambo kama vile mtu mwingine anakuangalia. Sina shaka ukiweka picha hii vizuri kichwani mwako utajituma sana na itakusaidia sana kufanikisha mambo mengi ambayo ingekuwa siyo rahisi kwako kuyafanikisha kama usingekuwa na picha hii vizuri.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

Nov 23, 2015

Kama Utashindwa Kuyatawala Mambo Haya, Huwezi Kufanikiwa Tena.

No comments :
Mafanikio siku zote hayaji kama ajali. Mafanikio ni safari ambayo huwa ipo hatua kwa hatua. Mafanikio kwa kawaida hayaji leo ghafla na kusema umefanikiwa, hapana. Mafanikio mara zote yanakuwa na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ili kufanikiwa.
Taratibu hizo au sheria hizo zinaposhindwa kufuatwa hakuna tena mafanikio yanayoweza kujitokeza zaidi ya kushindwa. Moja ya taratibu au sheria ambayo ni lazima uifate na ikupe mafanikio ni ‘sheria ya kutawala’. Ni lazima yawepo mambo ya kuyatawala kwenye maisha yako ili ufanikiwe. Bila kuyatawala mambo hayo itakuwa ngumu sana kufikia mafanikio makubwa.
Wengi hujikuta wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutaka kujaribu kutawala kila kitu au kushikiria kila jambo. Kwa maisha kama hayo inakuwa ni ngumu sana kuweza kufanikiwa. Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa ni lazima umudu kutawala mambo haya, ukishindwa kufanya hivyo sahau mafanikio.
1. Kutawala pesa.
Huwezi kupata mafanikio kama matumizi yako ya pesa hayako sawa. Hili ni jambo linalowatesa wengi na kuwasumbua. Lakini ili ufanikiwe ni lazima kutawala pesa na siyo pesa ikutawala wewe. Unapokuwa una mudu kuitawala pesa inakusaidia katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza. Unataka maisha yako yote uishi kiumaskini, acha pesa ikutawale.

TAWALA MUDA WAKO VIZURI.
2. Kutawala hamasa.
Nguvu kubwa ya mafanikio unaipata kutokana na wewe kuwa na hamasa kila siku. Hamasa tunaweza tukasema kama ni mafuta ya kukusaidia kusonga mele. Mara nyingi hamasa inapokosekana inakuwa siyo rahisi sana kuweza kufanikiwa. Kwani kazi kubwa ya hamasa ni kukupa nguvu na kichocheo cha kuendelea mbele zaidi ya ulipo.
3. Kutawala kasi ya mafanikio.
Ni uhimu kutawala kasi yako ya mafanikio yako. Unaweza ukajiuliza kivipi?sikiliza, kasi ya mafanikio unaitawala kwa kuhakikisha unafanya jambo linalokusogeza kwenye mafanikio kila siku. Kwa kufanya jambo hilo kila siku hata kama ni kidogo hapo utakuwa unaendana sawa na kasi ya mafanikio unayoitaka. Ila kama utashidwa kuitawala kasi hii na kushindwa kufanya jambo hata dogo ni lazima uachwe.
4. Kutawala tabia njema.
Ili uwe na mafanikio makubwa ni lazima uwe na tabia njema zinakusogeza kwenye mafanikio kila siku. Ukiwa na uwezo wa kutawala tabia hizi za kimafanikio uwe na uhakika ni lazima uweze kufanikiwa. Lakini kama utatawaliwa na mambo hayo basi tegemea anguko kubwa sana kwenye maisha yako.
5. Kutawala muda.
Muda ni kitu muhimu sana katika mafanikio yoyote. Pamoja na umuhimu wote huu wa muda, kwa bahati mbaya sana wengi wanatumia muda vibaya. Kwa tatizo kama hili la kutumia muda vibaya na kushindwa kutawala muda hupelekea maisha ya wengi kuharibika. Ukitaka kujua hili vizuri, cheza na muda wako sasa, baada ya miaka kumi utaniambia nini ambacho kitakutokea kwenye maisha yako.   
Haya ndiyo mambo unayotakiwa kuyatawala ili kufanikiwa kama ikatokea umeshindwa kutawala jambo mojawapo kati ya hayo basi utakuwa umejiweka kwenye wakati mgumu wa kuweza kufanikiwa.
Nikutakie siku njema, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waendelee kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

Nov 20, 2015

Jinsi Ya Kutambua Kipaji Cha Mtoto Wako Na Kukiendeleza

No comments :
Hujambo mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO na karibu sana katika siku ya leo kwa ajili ya kujifunza. Leo katika makala yetu tutajifunza namna unavyoweza kutambua kipaji cha mtoto wako na kukiendeleza. Na tunapozungumzia kipaji  huu ni uwezo anaokuwa nao mtu wa kufanya jambo fulani bila hata kwenda kujifunza shuleni. Najua unaelewa hili vizuri.
Mara nyingi mtu huzaliwa na uwezo huo na anapokwenda shule inakuwa ni rahisi kuweza kuuendeleza kipaji hicho na kufanya jambo hilo kwa ufanisi sana. Sasa wewe kama mzazi unawezaje kutambua kipaji cha mwanao na kukiendeleza? Ili kupata majibu hayo ya nini unachotakiwa kufanya fuatilia yafuatayo katika makala hii;-
Kama mtoto wako anaongea kupita kiasi; Kuna watoto ambao huongea kwa spidi sana na huwa hawachoki kuongea. Watoto hawa huongea mpaka anapokwenda kulala na wengine huwa wanaongea mpaka usingizini. Huwa na tabia ya kusimulia visa mbalimbali au kukueleza mzazi yote yaliyotokea mchana pengine wakati wewe umeenda kazini au kwenye shughuli zako.

KUZA KIPAJI CHA MTOTO WAKO.
Kwa mfano unapokutana na mtoto wa aina hii, hiyo hapo ni dalili nzuri sana kwa watoto hawa kama kipaji chao kitaendelezwa vizuri na kutokana na mwenendo huo wanaweza kuwa  wanasheria, waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na Mc wa majukwaani.
 Jinsi ya kuwasaidia watoto wa aina hii;
1. Epuka kuwakatisha tamaa kwa yale wanayoongea na kama yanakera mfundishe kuongea yanayofurahisha.
2. Unaweza kumwambia akusimulie visa mbalimbali wakati wewe ukimrekodi na baada usikilize pamoja nae. Hii humjengea kujiamini na kuona kuwa anachofanya kinathaminiwa.
3. Msaidie pia aweze kuwa msikilizaji mzuri kwa wewe kumsimulia wakati yeye akikusikiliza ana kumwambia arudie ulichosema.
4. Mtengenezee tabia ya kujiamini kwa kuepuka kumfokea au kumpiga mara kwa mara hususani kutokana na kosa la yeye kuongea sana.
Asante sana mpenzi msomaji wakati mwingine tutaangalia kipaji cha mtoto ambae kila jambo anataka kulifanya yeye mwenyewe.
Makala hii imeandikwa na Deo Mukebezi Unaweza kuwasilina naye kwa 0654627227



Nov 19, 2015

Nguvu Kubwa Ya Mafanikio Inapatikana Kwa Kufanya Jambo Hili Kwanza.

No comments :
Habari za siku rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka umzima wa afya na unaendelea vyema kujifunza ili kuboresha maisha yako. Leo katika makala yetu napenda kukushirikisha namna unavyoweza kuipata nguvu kubwa ya mafanikio utakayoweza kuitumia kuweza kutimiza malengo yako makubwa.
Je, umeshawahi kujiuliza nguvu kubwa ya mafanikio inapatikana wapi? Hili ni swali muhimu sana kwako kwa sababu kuna wakati katika maisha, kwa sababu ya changamoto mbalimbali huwa tunajikuta tunakosa nguvu na mwelekeo wa kusonga mbele na kushindwa kujua tufanye nini? Inapofika hali hii, wengi hukata tamaa na kusahau kuitumia nguvu kubwa ya mafanikio waliyonayo kuwafanikisha.
Kama hali hii imekukuta huna haja ya kukata tamaa tena, unaweza kutumia nguvu hii kubwa uliyonayo kukufanikisha. Je, unajajua nguvu hii inapatikanaje hadi kukufanikisha? Sikiliza, mafanikio yoyote unayoyatafuta yapo Kwenye Kuanza. Kama kuna jambo unataka kulifanikisha ni lazima ulianze na sio kulisubiria. Nguvu kubwa ya kuendelea na kusonga mbele inapatikana kwa kuanza. Unapokuwa unaanza jambo, sio tu unakuwa na nguvu ya kuweza kulifanya bali nguvu hiyo inakuwa inaongozeka siku hadi siku.

CHUKUA HATUA MARA MOJA ILI KUFANIKIWA.
Moja kati ya wanasayansi waliopata kuwepo katika hii dunia, Isack Newton aliwahi kulieleza hili vizuri katika sheria yake ya mwendo kwamba kitu chochote kikiwa kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo huo na kitu chochote ambacho kipo katika hali ya kutulia au utulivu, kitaendelea kutulia siku zote mpaka itokee nguvu nje ya hapo ya kubadili hali hizo.
Tafsiri au maana yake ni nini hapa? Ni kwamba kama utaamua kuchukua hatua juu ya maisha yako, utazidi kupata nguvu ya kukufanikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji. Chochote unachotaka kukifanya kwenye maisha yako hata kiwe kikubwa vipi, siri kubwa ya kukifanikisha ipo kwenye kuanza.
Mafanikio yote makubwa chini ya jua yalianza kwa kufanya kwanza na sio kusubiri. Kumbuka ”DO THE THINGS YOU WILL HAVE THE POWER TO ACCOMPLISH IT. Kama kuna jambo unataka kulifanya, wewe lifanye tu acha kujiandaa sana, wala kusubiri sana kwani nguvu ya kufanikisha jambo hilo itapatikana wakati unafanya. Kama ni uzoefu mkubwa utaupata kwa kuanza. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyopatikana kwa kuchukua hatua za utekelezaji.
Tumia kanuni hii bora ikusaidie kufanikiwa kwa viwango vya juu, kumbuka siku zote unalo jukumu la kuhakikisha unakuwa bora kila siku.
Tunakutakia mafanikio mema, endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku, TUPO PAMOJA.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,



Nov 18, 2015

Kanuni 6 Za Mafanikio, Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.

No comments :
Wengi wetu bila shaka umeshawahi kumuona au kumsikia mcheza sinema maarufu duniani kwa kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Gavana wa jimbo la calfornia, Anord Shwarzenegger. Enzi zake alicheza sinema nyingi ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana. Leo hii akiwa kama Gavana, Anorld anatushirikisha baadhi ya kanuni za mafanikio alizozitumia hadi kufikia viwango vya juu vya mafanikio.
Zifuatazo Ni Kanuni 6 Mafanikio Za Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.
1. Jiamini wewe mwenyewe.
Watu wengi mara nyingi hutafuta ushauri wamafanikio kwa watu mbalimbali ili kuwafanikisha. Ni jambo zuri. Lakini kitu cha cha muhimu hapa kwako ni kujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Tafuta ni kipi unachokipenda, unataka kuwa nani na kisha tekeleza kwa kujiamini kabisa, UTAFANIKIWA.
VUNJA SHERIA ZINAZOKUZUIA KUFANIKIWA.
2. Vunja sheria zinazokuzuia kufanikiwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambao unasheria nyingi nyingi za uasili zinazoweza kutuzuia kufanikiwa. Sasa hizi ni sheria ambazo kwa vyovyote vile ni lazima zivunjwe. Sheria hizi zinaweza zikawa ni uvuvi au mazoea fulani mabaya tuliyojijengea. Kwa kung’ang’ania sheria hizi hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.
3. Acha kuogopa kushindwa.
Siri kubwa ya mafanikio  ni kujifunza kutokuogopa kujaribu. Kama kuna fursa imejitokeza jaribu kufanya kwa ujasiri mkubwa na acha kukaa katika mkao wa kuogopa hiyo haitakusaidia sana. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaa tu. Jitoe mhanga na hakikisha mpaka mipango na malengo yako makubwa yatimia.
4. Acha kusikiliza maneno ya wanao kukatisha tamaa.
Yatasemwa mengi kwamba huwezi kufanya hili wala lile. Wasikilize kisha achana nao. Lililo kubwa kwako jiamini mwenyewe kuwa utafika kule unakotaka kufika na kisha endelea mbele. Najua ni mara nyingi umewahi kusikia kauli hizi zikija kwako. Jambo la kufanya zipuuze kauli hizo, halafu fanya kile unachoamini kitakupa mafanikio.
5. Fanya kazi kwa bidii sana.
Hiyo ni nguzo kubwa ya mafanikio yako. Fanya kazi kwa bidii kwa kuamua kujituma na kulipia gharama zote za mafanikio. Hakuna mafanikio ambayo yatakuja kwako bure zaidi ya wewe kuwekeza nguvu na uwezo wako wote mkubwa kwenye kufanya kazi kwa bidii na maarifa makubwa siku zote. Hapa ndipo mafanikio makubwa yanapopatikana.
6. Kumbuka kutoa.
Mafanikio yoyote utakayokuwa umeyapata , hakikisha unatoa kwa jamii yako kiasi fulani  kama sehemu ya shukrani. Hii ni sheria au kanuni ya asili ambayo itakusidia kufikia mafanikio makubwa siku zote.
Hizo ndizo kanuni za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa, kama zilivyotolewa na Arnold Shwarzenegger, Gavana wa jimbo la Calfornia marekani.
Nikutakie siku njema, ansante kwa kupitia makala hii na endelea kuashirikisha wengine kwa ajili ya kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,




Nov 17, 2015

Vifungo Ambavyo Jamii Inakufunga.

No comments :
 Leo napenda kusema msemo mmoja, "JARIBU KUJIFUNZA KUTOKA NJE YA PULIZO". Pulizo ni kama vile puto au Bubble kwa kingereza. Ukilitazama pulizo, hewa ikiwa ndani yake haitoki tena nje. Hivyo kuwa ndani ya pulizo au puto kunamaanisha kuwa kifungoni. Hivyo kauli hiyo inamaanisha jifunze kutoka kifungoni katika kutafuta dhumuni lako la maisha. 

Kifungoni ni wapi? Je ni kama mahabusu? Hapana, nikisema kifungo ninakuwa ninamaanisha pale ambapo panakunyima uhuru au unapokosa nafasi ya kuwa wewe kama wewe. Pulizo ni kama vile kifungo cha kidunia ambacho kila mmoja wetu anakuwa ndani yake. Mfano kifungo hicho kinaweza kuwa ni:-

·         Wasiwasi wa wakati ujao,
·         Dhana unayoifahamu juu ya mafanikio katika maisha,
·         Kulazimisha kupendwa na kila mtu,
·         Kulazimisha kumfurahisha kila mtu,
·         Kulazimisha kuwa mkamilifu,
·         Maneno ya watu,
·         au Imani ambayo hauna uhuru au uhakika nayo.

TOKA KWENYE KIFUNGO HIKI.
Kila mmoja wetu katika jamii ambayo amekulia, kuna mengi ambayo jamii imemfundisha na kumuambia kuwa ndio jamii inavyopaswa. Mfano 

·         Jinsi ya kuishi,
·         Jinsi ya kuvaa,
·         Jinsi ya kula,
·         Kipi cha kula na kipi cha kutupa, 
·         Dini/Imani gani ipo sahihi,
·         Wewe ni nani na kwanini upo hapa,
·         Miziki, Television na vyombo vingine vya habari visemavyo,
·         Matangazo yakikuambia kipi cha kununua au cha muhimu na bora kuliko vingine,
·         Maana ya mafanikio ni nini,
·         Kazi gani ni ya maana kuliko nyingine na mengi ambayo jamii imeona ni mazuri kwao basi nao hupenda yawe mazuri kwako.

Ni jambo zuri sana kwani ni jamii inajitahidi kukujali na kukufundisha kile ambacho inaona ni haki. Lakini je wewe utajuaje kama jamii ipo sawa? Je kama ni kutokana na kutofahamu kwao ndio kunapelekea mitazamo hiyo? Ni vyema kuisikiliza jamii inasema nini lakini pia nawe ni vyema kuutafuta ukweli wewe kama wewe, na ndio maana upo hapa ulimwenguni. Kama hakuna umuhimu wa wewe kuwepo ni kwanini upo? Lazima kuna sababu ya msingi. 

Jamii inatuweka kwenye pulizo, hivyo ni vyema kutoka nje ya pulizo ili kuufahamu ukweli. Ukweli hauwezi kuufahamu kwa kuambiwa tu bali nawe unapaswa uuthibitishe. Je aliyeanzisha ukweli huo aliambiwa na nani? Kwanini na wewe usiutafute? Kwa kuacha kulazimisha mambo unaweza ukajikuta unajifunza mengi sana kuhusiana na maisha kwa ujumla, na ikakusaidia kutafuta dhumuni lako la maisha.
 

Kama unatafuta dhumuni lako la maisha kwa kutegemea jamii ikuchagulie dhumuni la kuishi utamaliza maisha yako hujaishi maisha yako bali unaishi maisha ya wenzako. Ili kuijua safari yako ina malengo gani toka nje ya pulizo na chunguza ndani mwako unapenda nini na jamii inakuambia nini. Mfano kuna anayependa kuwa daktari lakini wazazi wanamwambia awe fulani. Sio kwamba wazazi wamekosea, nao wapo sahihi. Jitahidi uwaelewe kwani kuna wakati mtu hukuchagulia maamuzi kwa kukulinda na kwa kutumia akili aliyonayo yeye, hivyo nawe unapaswa kutambua ni kwanini mtu anakupa mtazamo fulani na kisha amua mtazamo wako kiusahihi na bila kubishana au kumdharau mtu. Heshimu kila mtu na tambua mchango wa kila mtu katika maisha yako.


Makala hii imeandikwa wa Apolinary Protas wa JITAMBUE SASA BLOG. Kama una maoni au ushauri wasiliana na Waandishi wa makala hii kwa email jitambuesasa@gmail.com

Nov 16, 2015

Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.

No comments :
Kwa kila safari yoyote ya mafanikio duniani ni lazima iwe na changamoto zake. Hakuna mafanikio ambayo yanakuwa yanakuja moja kwa moja bila kukutana na changamoto. Mara nyingi changamoto hizi zinapotokea kwa wengine hupelekea kushindwa kufanikiwa kwa kile kitu ambacho wanakifanya.
Inapotokea ukashindwa kufanikiwa kwa kile unachokifanya kutokana na changamoto yoyote, ni nini ambacho huwa unafanya? Hapa ndipo ule umuhimu wa kujifunza kutokana na makosa huwa unakuja. Najua umewahi kusikia sana juu ya kujifunza kutokana na makosa pale unapokosea. Lakini je, umeshawahi kujiuliza ni mambo gani unayotakiwa kujifunza?
Yafuatayo Ni  Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
 1. Mafanikio hayaji mara moja.
Kwa lugha rahisi naweza nikasema kwamba mafanikio yote yanakuja hatua kwa hatua. Hakuna mafanikio yanayokuja mara moja. Kwa hiyo kushindwa kwa lile jambo unalolifanya ni ishara inayo onyesha kwamba ili kufanikiwa ni lazima kujaribu tena na tena mpaka kufanikiwa, ikiwa lakini umefanya kwa mara ya kwanza na kushindwa.
Itakuwa haina maana kwako na utakuwa hupo makini na mafanikio ikiwa utaka tamaa mara moja baada ya kushindwa. Ukishindwa jambo tambua huo siyo mwisho wako, bali ndio mwanzo wa mafanikio kwa sababu mafanikio hayaji mara moja. Ukijua hivyo mafanikio hayaji mara moja hutakaa ukisikitika pale unaposhindwa, zaidi utaongeza juhudi na uzoefu.

JIFUNZE KITU KUTOKANA NA MAKOSA YAKO.
2. Kujenga mafanikio inahitaji muda.
Pia unaposhindwa kufanikiwa katika jambo unalolifanya kwa mara ya kwanza, hiyo inatuonyesha kwamba mafanikio yanahitaji muda kuyajenga. Mafanikio sio kitu cha kutokea tu mara moja kama wengi wanavyofikiri. Unatakiwa ujipe muda wa kujaribu tena na tena mpaka matokeo chanya yatokee.
Watu wote wenye mafanikio, walitumia muda mwingi kuwekeza kwenye mafanikio yao. Hakuna mkato juu ya hilo, inabidi ujitume na kuwekeza muda wako vya kutosha ili ufanikiwe. Kama kuna jambo unalifanya usihisi kama vile unapoteza muda kama hupati matokeo ya haraka. Kumbuka siku zote kujenga mafanikio inahitaji muda.
3. Siyo rahisi kufanikiwa kama jambo unalolifanya hulipendi.
Kama kuna jambo unalifanya halafu ukawa hulipendi sana, elewa ukishindwa huo ndio utakuwa mwisho wako. Kanuni au sheria za mafanikio zinatufundisha kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima ulipende lile jambo unalolifanya kwa moyo wote.
Unapofanya jambo unalolipenda hata unapokosea inakupa nguvu ya kusonga mbele kwa kuweza kujaribu tena na tena. Hili ni jambo ambalo unatakiwa kulielewa kuwa utajifunza kutokana na makosa yako kama jambo hilo unalipenda kweli kutoka moyoni. Kinyume cha hapo haitawezekana kwako.
4. Kushindwa kwako ni ishara ya kwamba umechukua hatua.
Ni sawa umeshindwa kwa kile unachokifanya, lakini yote hiyo inakuonyesha kwamba umechukua hatua. Kama usingechukua hatua ya kufikia mafanikio yako, basi ni wazi ungebaki kama ulivyo. Kwa kuwa umelijua hilo endelea kuchukua hatua kwa kusonga mbele. Usihofie kukosea kwako, huo pia ni msingi wa mafanikio yako.
Ansante kwa kusoma makala hii, kumbuka kushindwa kwa kile unachokifanya ni njia mojawapo ya kukupeleka kwenye mafanikio ikiwa utajifunza. Usifanye kushindwa kwako kukakurudisha nyuma.
Ni kipi unachojifunza wewe pale unaposhindwa kwa mara ya kwanza kwa jambo unalolifanya? Unaweza ukanishirikisha machache hapo chini kwenye maoni, tukajifunza kwa pamoja.
Nikutakie ushindi katika safari yako ya mafanikio, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waweze kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika.
Tupo pamoja katika safari ya kuyafikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,


Nov 13, 2015

Kama Unaona Maisha Ni Magumu Utawezaje Kushinda?

No comments :
Hebu kaa chini na jaribu kujiuliza maswali haya kwa muda kidogo? Maisha yako ni nini? Una mtazamo gani unapofikiria juu ya maisha yako? Je, maisha yako yanakupa kile unachokihitaji? Haya ni maswali ambayo unapaswa kujiuliza ili yakupe dira,mwelekeo na picha ya maisha yako unavyotaka yawe.
Namna unavyoyaona maisha yako ndivyo unavyoyatengeneza. Namna ambavyo unaishi na malengo ndiyo yanaeleza maana ya maisha yako. Watu husema vitu tofauti kuhusu maisha kama vile maisha ni safari, maisha ni kitendawili kigumu, maisha ni kama duara, maisha ni kama foleni au maisha ni mchezo mchafu.
Lakini kila unapojiuliza wewe mwenyewe maisha ni nini! Unapata picha gani? Watu wengi wanaelewa maisha kupitia mavazi, vitu vya thamani, magari, mtindo na pesa au kwa namna nyingine kwa kadri jinsi wanavyoyatafsiri.
Picha uliyonayo juu ya maisha inakuhamasisha kwa hayo uliyonayo. Kama una picha ya maisha ni kama riadha utafanya mambo yako harakaharaka na kukazana. Kama una picha ya maisha ni mapambano utafanya chochote kupigania maisha yako. Ila kila siku upo katika mtihani au mchezo unaopaswa kushinda wala si kushindwa. Maisha ni jaribio la muda mfupi. Kwenda ngazi nyingine unahitaji kushinda mtihani kila siku.

KAMA UNAONA MAISHA NI MAGUMU UTAWEZAJE KUSHINDA?
WEWE NI MSHINDI WA MAISHA YAKO.
Maisha yamegawanyika katika ngazi tunazopaswa kuzivuka na kushinda. Huu ni ushindi wa lazima kwako, ambao ni lazima uushinde kama vile ulivyo mchezo wa mpira wa miguu. Sote tunapaswa kushinda maisha katika ngazi mbalimbali kama vile, ngazi ya makundi(Utoto), Robo fainali( Kijana),Nusu fainali(Mtu mzima) na fainali( Uzee).
Ili ushinde lazima uwe na kanuni, mbinu na mipango madhubuti ya kushinda. Kama vile kilivyo kikosi cha mpira wa miguu, tumia kikosi cha mambo yafuatayo kushinda katika maisha yako.
Kikosi cha kwanza cha mambo yako kitakachokupeleka kwenye mafanikio kiwe hiki:-
1. Kweli.
2. Utu wema.
3. Uvumilivu.
4. Uwajibikaji.
5. Imani.
6. Msamaha.
7. Elimu.
8. Furaha.
9. Umoja.
10. Kiasi
11. Upendo.

KAMA UNAONA MAISHA NI MAGUMU UTAWEZAJE KUSHINDA?
UKIWEKA JITIHADA NA KUVUMILIA UTASHINDA.
Kikosi cha ziada weka au fanya mambo haya:-
1. Uadilifu.
2. Haki na heshima.
3. Uaminifu.
4. Ndoto.
5. Fadhili.
6. Upole.
7. Uelewa.
Tambua wewe ndiye kiongozi na kocha wa maisha yako unatakiwa kuyasimamia na kuhakikisha unafanya mambo hayo ili kufanikiwa.
Unapokuwa na kikosi imara kama hicho ni rahisi kupambana na kikosi angamizi cha maisha yako kama magonjwa, umaskini, kufeli, marafiki wabaya, tamaa na kujidharau. TAMBUA USHINDI KWAKO NI LAZIMA kama utayaona maisha yako kwa mtazamo chanya.
Nikutakie siku njema, yafanyie kazi mambo hayo na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamsika.
Makala hii imeandikwa na Noel Ngowi wa Moshi- Tanzania. Kama una maoni au ushauri wasiliana na mwandishi wa makala hii kwa email truesuccess89@gmail.com