Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, December 29, 2015

Muda Sahihi Wa Mafanikio Yako Ni Huu Hapa.

No comments :
Bila shaka umewahi kuliona hili kuwa wengi wetu tumekuwa tukitafuta sana muda sahihi wa kuweza kufanikisha mipango au malengo yetu tuliyojiwekea. Muda huu ambao tumekuwa tukiutafuta, mara nyingi hupelekea  sisi kufanya maandalizi mengi sana ya kusubiri mambo mengi yakamilike ndio tuanze uwekezaji ule tunaouhitaji.
Lakini kitu kisichoeleweka kwa wengi ni kwamba siku zote hakuna wakati sahihi wa wewe kuanza jambo unalotaka kulifanya zaidi ya sasa. Kama kuna jambo unalotaka kulifanya au kulitimiza ni bora ukaanza kulifanya hivyohivyo sasa bila kuweka maandalizi mengi sana kama unavyofikiri. Tambua siku zote muda sio rafiki sana na wewe  hadi ukusubiri sana.
Kosa kubwa wanalolifanya watu wengi bila kujua ni kule kufikiri kuwa kuna vitu fulani hawana ambavyo ni lazima wavikamilishe kwanza ndipo waanze kufanya kile wanachokitaka kukifanya hadi kufikia mafanikio. Kama haya ndiyo mawazo yako kwa namna fulani utakuwa unachelewa.
Kwa sasa huhitaji kusubiri taarifa zaidi, huhitaji kusubiri muda zaidi ya ulionao wala huhitaji eti hadi uwe una mtaji wa kiasi fulani ndiyo uanze biashara. Unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza na kile ulichonacho. Mambo mengine unayofikiria sana hayajakaa sawa, yatakaa sawa wakati umeanza kufanya.

Utakuwa unajidanganya kama utakuwa unafikiri ukijiandaa sana hutakosea na utakuwa kamili kila eneo, makosa na kujifunza ni lazima. Kwa hiyo lilokubwa kwako ni kuwa tayari kufanya kile ambacho unaona kitakufanikisha tena kwa haraka kuliko ukasubiri sana.
Ukweli wa mambo ulivyo ni kwamba hakuna muda sahihi unaokusubiri wewe wa kuanza kufanya jambo unalolitaka kama ulionao sasa. Huu ndiyo muda sahihi kwako wa kufanya mambo yako. Jiulize kama hutafanya sasa utafanya lini? Je, hauoni kwamba utazidi kujichelewesha kufikia malengo yako makubwa kama utakuwa ni mtu wa kusubiri?
Kama umekuwa mtu wa kusubiri sana, leo tambua kitu kimoja hiyo imetosha. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua kwa kutumia kile kidogo ulichonacho kukufanikisha. Acha kudharau kile ulichonacho, hata kama ni kidogo vipi kinuwezo wa kukufanikisha. Tumia ulichonacho hadi kikupe mafanikio.
Weka mawazo pembeni ya kushindwa na anza kujiamini kwa kile unachokifanya kuwa ni lazima kikupe ushindi. Anza utekelezaji kwa kuchukua hatua kwa hatua kila siku hadi uyaone mafanikio. Hivi ndivyo mafanikio yako yatakavyokuja na hakuna muda wa kusubiri.
Kama utaendelea kusubiri elewa kabisa unajichelewesha kwenye mafanikio yako mwenyewe. Fanya mafanikio yako yaonekane sasa. Muda sahihi wa mafanikio yako ni sasa. Chukua hatua siku zote hata kama ni kidogo lakini mwisho wa siku ushindi utakuwa ni wako.
Tunakutakia ushindi katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuelimika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment