google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 5, 2016

Hii Ndiyo Hasira Kubwa Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kufanikiwa.

No comments :
Naamini umzima wa afya mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO na unaendelea kujifunza kila siku ili kuboresha maisha yako. Katika makala yetu ya leo naomba nianze kwa kukuuliza swali hili, hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini simba anaua?
Unaweza ukawa unaashangaa au kwako ukaona ni swali la kawaida, lakini pamoja na hivyo je, umeshawahi kujiuliza kwa nini sImba anaua? Bila shaka wengi wetu tunatambua sifa alizonazo mnyama huyu kuwa ana nguvu, hasira na anauwezo mkubwa wa kuua vitu vingi sana. Sasa je, ni kwa nini huwa anaua?
Hivyo ni rahisi kusema anaua kwa sababu ana nguvu, hasira na pengine kutaka kujionyesa kwamba yeye ndiye mbabe wa wanyama wote ndiyo maana akikutana karibia na kila kitu ni halali yake. Lakini je, huu ndiyo ukweli ulio ndani ya simba anaua kwa sababu hizo tu?
Ukweli wa mambo ulivyo siku zote simba anaua siyo kwa sababu ana hasira sana au ana nguvu nyingi ameamua kuzitumia, hapana. Siku zote shauku ya simba kuua inaongozwa na njaa aliyonayo. Mara nyingi njaa aliyonayo ndiyo inayomwongoza kufanya chochote kile na kuhakikisha  mpaka anapata mawindo yake.

LAZIMA UWE NA HASIRA YA MAFANIKIO
Kila anapokuwa ana njaa anakuwa ana hasira, nguvu na uwezo mkubwa wa kuraua kitu chochote kinachojitokeza mbele yake bila kuogopa kitu chochote. Kwa hiyo utaona siyo ubavu au nguvu zake nyingi ndizo zinazomuongoza kuua bali ni njaa aliyonayo.
Kupitia maisha haya ya simba bila shaka moja ya jambo muhimu sana ambalo tunaweza kujifunza la kimafanikio ni lazima kuwa na hasira ya mafanikio ili kufanikiwa. Bila kuwa na hasira hii ni ngumu sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Watu wengi wana hulka au tabia ya kutafua mafanikio huku ndani yao wakiwa hawana ile hasira inayowaongoza kutafuta mafanikio hayo. Matokeo yake wamekuwa na hasira na vitu vidogo vidogo ambavyo haviwasaidii badala yake kuelekeza hasira zote kwenye kutafuta mafanikio.
Hebu jaribu kujiuliza je, una hasira, hamu na njaa ya kutosha kuhakikisha kuona ndoto zako zinatimia? Kama una hasira hii ya mafanikio hongera sana, upo kwenye njia sahihi ya kufikia mafanikio yako makubwa..
Mara nyingi unapokuwa na hasira ya mafanikio ndani yako unakuwa king’ang’anizi usiyekubali kushindwa kwa sababu unajua kuna kitu ambacho unakitafuta. Hata inapotokea umeshindwa utajaribu tena na ntena mpaka kufikia mipango na malengo yako.
Suala la kuahirisha au kujishusha linakuwa halipo kwako maana unacholenga kwako ni matokeo chanya. Hii ndiyo hasira kubwa unayotakiwa kuwa nayo ili kufanikiwa. Achana na hasira za kipuuzi ambazo zinakuumiza na kukurudisha nyuma, kuwa na hasira na maisha yako utafanikiwa.
Kama tulivyoona simba siku zote anaua kwa sababu ana hasira/njaa ya mafanikio. Hivi ndivyo unavyotakiwa kuwa na wewe. Leta matokeo chanya ya maisha yako kwa sababu una hasira au njaa au hamasa ya kufikia mafanikio yako. Ukiweza kufanya hivyo utafikia mafanikio yako makubwa unayoyahitaji.
Nakutakia siku njema sana rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO. Kikubwa kwako endelea kuwashirikisha wengine kuweza kujifunza.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.