google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 16, 2018

Aina Ya Watu Ambao Hawafanikiwi Katika Maisha.

No comments :
Katika maisha wapo watu ambao ninaweza sema kwa jinsi ya sifa zao au kwa jinsi ya tabia zao walizonazo sio rahisi kufanikiwa. Hawa ni wale watu ambao tunasema ni aina ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao.
Inawezekana ukawa huzijui sifa za watu hawa ambao hawafanikiwi katika maisha yao, lakini kupitia makala haya utajifunza sifa hizo za watu ambao kwa kiuhalisia huwa hawafanikiwi hata iweje, pengine wabadilike mara moja.
Najua hapo ulipo unataka kujua kwa hamasa kubwa watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao huwa wana sifa zipi. Nami bila choyo yoyote, nakukaribisha bila hiana na twende kwa pamoja kujifunza sifa za watu ambao hawafanikiwi katika maisha.
1. Watu ambao kazi yao ni kulaumu na kulalamika.
Mara nyingi watu ambao ni walalamikaji sana, kufanikiwa kwao katika maisha huwa sio rahisi. Hili hutokea kwa sababu, husau majukumu yao ya msingi juu ya maisha yao na kuwapa wengine mzigo huo kwamba ndio wamesababisha maisha yawe hivyo.
Hata wewe ukiwa mtu wa kulalamika na kulaumu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao hawataweza kufanikiwa katika dunia hii, hadi pengine ubadilike. Ukifatilia, utaelewa vyema aina hii ya watu jinsi walivyowengi na wanakwama kweli.

Wapo ambao hawabadiliki, hawafanikiwi.
2.Watu wanaojadili matatizo badala ya njia za kutatua matatizo.
Kama umekuwa ni mtu wa kujadili matatizo badala ya kutafuta njia za kutoka kwenye tatizo hilo, basi ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuja kufanikiwa katika maisha yao. Ili upate unachokitaka unatakiwa kujifunza kutatua changamoto na si kuzijadili. Kujadili changamo  zako sana ni kujikwamisha mwenyewe.
3. Watu ambao hawataki kubadilika hata kama wanafanya makosa.
Wapo watu ambao ni wabishi na ambao maishani mwao ni kama wamegoma kubadilika kabisa. Hata watu hawa wakikosea bado kubadilika kwao ni kugumu sana. Hiyo haitoshi si watu wa kujifunza hata kidogo iwe kwenye vitabu au kupitia wengine. Pia watu hawa ni miongoni mwa watu ambao sio rahisi kuweza kufanikiwa.
4. Watu ambao ni watumwa kwa mambo yasio ya msingi.
Kuna watu ambao ni watumwa wa mambo yasiyo ya msingi ambayo kiuhalisia yanawarudisha nyuma sana kwenye maisha yao. Unapokuwa mtumwa sana pengine pombe kwa sana au wanawake ka wingi, unajitengenezea shimo la kushindwa kwako. Kwa lugha nyingine hivyo ni vitu ambavyo vinapoteza pesa ukiviendekeza vibaya.
5. Watu wanaojilinganisha sana na wengine.
Acha kufanya kosa la kujilinganisha na wengine kwenye maisha yako. Unapojilinganisha na wengine utashindwa kuwa bora pasipo kujua na mwisho wa siku utashangaa unakwama. Itakuwa badala ya kufanya mambo yako, unakua unakazana tu uwe kama fulani, hapo utakwama.
Hawa ndio watu ambao wana sifa nyingi za kutokufanikiwa katika maisha yao. Kama una sifa miongoni mwa hizo unabidi uwe makini sana ili na wewe usije ikafika mahali ukakwama na kubaki hapo. Jenga maisha yako makubwa ya kimafanikio kwa kujitahidi kutoka kwenye sifa hizo kama unazo.
Endelea kujifunza kupitia diramafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kuhamasika na kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.