google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 15, 2018

Hii Ndiyo Mbegu Muhimu Sana Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.

No comments :
Kila mtu ana uwezo mkubwa sana ndani yake wa kufikia mafanikio makubwa, lakini kwa bahati mbaya ni wachache sana wanaojua kwamba uwezo huo wanao na waliobaki hawaamini kabisa hata kwamba uwezo huo mkubwa wanao ndani mwao.
Kitu ama hali hii inatokea kwa watu hawa kushindwa kuamini wana uwezo mkubwa ni kwa sababu moja tu, watu hawa hawajaambiwa na mtu kwa msisitizo au hawajatiwa moyo sana hadi kuweza kuamini uwezo mkubwa ulio ndani mwao.
Ni kweli watu hawa uwezo wa kufanikiwa wanao lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa mbegu muhimu ya kupewa matumaini kwamba uwezo huo wa kufanikiwa wanao kama wanavyowaona watu wengine wakifanikiwa pia.

Kama vile ulivyo udongo hata uwe mzuri vipi na una rutuba ya kila aina, lakini udongo huo ukikosa mbegu au usipopanda chochote hakiwezi kuota kitu, na vivyo hivyo hata uwe na uwezo mkubwa vipi lakini usipopanda mbegu ya kutiwa moyo ni kazi bure.
Hamasa na kumpa mtu moyo na kumwaminisha kwamba anaweza ni kitu ambacho kinahitajika sana katika kila maisha ya mwanadamu. Hii ndio mbegu ya msingi sana katika mafanikio ambayo wengi hawaijui.
Ndio maana kama unaipa akili yako hamasa kila wakati ni rahisi sana kuweza kufanikiwa. Wengi wanashindwa kwa sababu ya kuzipa akili zao ‘matango pori’ kwa kulisha mambo yasiyofaa ambayo yamejaa hofu.
Unatakiwa kuelewa unatakiwa kupewa mbegu ya hamasa, mbegu ya kutiwa moyo  ili kuweza kufanikiwa na kufika juu kabisa kimafanikio. Ukiwa na msingi mzuri wa mbegu hii utafanikiwa tu kwenye maisha yako.
Kama unafikiri natanaia waangalie watu ambao wamelelewa katika mazingira ya kupewa sana moyo kwamba mafanikio yanawezekana. Utakuta ni kweli na wao wamefanikiwa kwa sababu wanalishwa vitu kama hivyo hivyo kila siku.
Yapo mabadiliko makubwa sana yanayotokea kwa wengine na ndani mwako hasa pale unapoamua kujipa moyo na kuwapa moyo wengine. Hakuna kinachoshindikana unapojipa moyo, kwa vyovyote tu utasogea hata iwe kwa kutambaa.
Kujipa moyo na kuwapa moyo watu wengine ni mojawapo ya mbegu ya mafanikio ambayo unatakiwa kuitumia kila wakati. Acha mizizi ya mbegu ya kutia moyo ikue na hakikisha imekuwa vya kutosha na hapo utaona matunda ya mafanikio yako.
Endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
 DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.