google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 20, 2023

Epuka Sana Kupoteza Muda Wako Wa Mafanikio Kwa Sababu Ya Kitu Hiki.

No comments :


Na Melisa Kawa, Dar es salaam, Tanzania.

Kabla hujaanza siku yako mpya, kuna namna ambavyo unakuwa unaipangilia siku yako jinsi itakavyokuwa. Kuna mipango ambayo unakuwa unajua kabisa kwamba utaifanya muda huu au ule, unachokuwa ukifanya ni kwenda na ratiba yako tu ya muda.


Sasa wakati umepangilia vitu vyote hivyo, na wakati huo huo mtu akakuuzi au ukakasirika kwa muda mrefu, je ulishajiuliza hasira hizo unazozibeba zinakupotezea muda kiasi gani? Maana ni hatari sana kukasirika kwa muda na kusahau kufanya majukumu mengine ya msingi.

Maana Unaweza ukakasirika wee, ukapoteza muda mwingi ukiwa na hasira, lakini yote hayo kumbuka hayakuwepo kwenye ratiba zako, kikubwa jua kabisa hapo utakuwa unapoteza muda wako bure kwa kujibebesha mzigo unaokuumiza lakini ambao hukutakiwa kuwa nao.

Kikubwa cha kujifunza hapa, jua namna ya kutumia muda wako vizuri, usipoteze muda wako kwa vitu kama hasira za muda mrefu na visasi visivyo na maana. Tumia muda wako kwa faida. Tumia muda wako kupanga mipango itakayokusaidia na si kukupotezea muda.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.