google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 23, 2022

Ushauri Kwa Kijana Aliye Mtaani, Hana Ajira, Haoni Cha Kufanya.

No comments :

Kuna watu hawajui cha kufanya, yaani ni watu ambao hawajui wafanye nini ili walau waingize kipato. Kwa bahati mbaya watu hawa huwa ni wahitimu wa chuo kikuu na wengine ni watu wa kawaida. 

Hebu fikiria, inakuwaje kwa mhitimu wa chuo kikuu anakuwa hajui cha kufanya? Lakini hali hiyo ndio huwa ipo mtaani na ndio uhalisia wenyewe unakuwa uko hivyo. 

Angalia kile unachopenda, unajua kuchora, kuimba, kuigiza, kuchekesha, fanya hivyo na kisha waonyeshe watu kile ulichonacho na uachane na kulala.

Jifunze kutengeneza tovuti, jifunze kuendesha mitandao ya kijamii kibiashara, jifunze graphics na vitu vingine vingi vitakavyokulipa baadae.

Tumia simu yako kuuza vitu vya watu wengine. Unaweza kuongea na mtu mwenye duka ukawa unauza vitu mtandaoni kisha unapata asilimia kadhaa.

Ukiweza fanya udalali wa viwanja, nyumba, vyumba, vyombo na bidhaa zingine ila fanya kwa weledi mkubwa.

Kama unapitia hali hiyo usipate shida sana, ndio maana dirayamafanikio.blogspot.com ipo kwa ajili yako kukupa mwelekeo wa maisha. Kwa kuwa huna kazi, usilale mpaka saa tatu, badala yake fanya haya:-

Kipindi ambacho huna ajira na huna labda smartphone, unaweza kujifunza ujuzi mpya utakaokulipa zaidi kwa baadae.

Jifunze ufundi, namna ya kutenengeneza simu zilizoharibika, kutengeneza friji, pasi, tv au redio. Unaweza ukajifunza vyote au kimoja unachopenda.

Ongea na wafanyabiashara wenye maduka, ili hata uweke pesa kidogo rehani, kama laki moja, ili uwe unachukua vitu dukani kwao na kuviuza kwa mali kauli, visiponunuliwa unawarudishia vitu vyao.

Nenda sokoni toa uvivu na aibu, tafuta kitu kimoja uza, iwe ni mboga za majani, dagaa na hii itakuondolea uvivu na kukuonyesha fursa mpya.

Fanya umachinga, uza bidhaa ndogo ndogo, kama chaji, cover, protector, hapa mtaji unaweza kuanza na laki moja tu.

Kumbuka watu ni mtaji, hakikisha unafahamiana na watu muhimu. Hawa watakusaidia kupata wazo, mtaji au kushirikiana na wewe.

Wakati mwingine katika makala zinazokuja tutaangalia biashara unazoweza kuzifanya kwa mtaji mdogo. Kitu kikubwa na cha msingi, endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza kwa kina.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.