google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 23, 2014

Linalokuhuzunisha Si Tatizo Kubwa Sana, Unajitesa Bure.

No comments :
Nafahamu kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina shaka kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika mapenzi, kudhurumiwa, kufilisika, kutotimiza malengo tuliyojiwekea na pengine kufutwa kazi ni mambo ambayo huzaa huzuni na machozi miongoni mwa watu wengi. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba tunalia au kuhuzunika kwa sababu matatizo yetu ni makubwa au ni kwa sababu yametuumiza sana na tumejikuta tukiwa ni watu ambao hatujui nini cha kufanya?

Hebu tujiulize ni wangapi tunahuzunikia mishahara midogo tunayolipwa makazini mwetu? Je katika huzuni hizo tulishawahi kuwaza kwamba kuna binadamu wengine hawana kazi na wanahangaika kutafuta shilingi mia tano kwa kuuza mihogo na karanga kwenye kona za mitaa huku wakiwa juani?. Kama hao wapo ukubwa wa tatizo la mshahara kidogo unaotuliza kila siku uko wapi? Uko wapi ukubwa wa tatizo la kutokuzaa wakati kuna waliozaa na watoto wote wakafa.

Kimsingi uwiano wa shida na uhimili wake unaopatikana baina ya mtu na mtu, kamwe sifa ya huzuni hailetwi na ukubwa wa tatizo, isipokuwa ni kukosekana kwa sanaa ya kuishi, yenye maono na hisia za kupunguza mambo makubwa kuwa madogo. Katika hisia, mwanadamu hawezi kuzuia machozi ya furaha au huzuni yasitoke, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Ifahamike kwamba kila mwanadamu ana uwezo wake wa kufanya, zaidi ya tatizo analokutana nalo.

Bila shaka umewahi kuona au kuwasikia watu wanalia kila siku kwa kuhitaji utajiri, lakini hawafikii malengo kwa sababu wanaona umasikini ni jambo kubwa na kuufikia utajiri ni jambo kubwa pia. Kitakachotokea hapo kama mambo yote ni magumu ni huzuni ndani mwao. Unaweza pia ukajiuliza mwenyewe ni kitu gani kinakuliza? Fahamu kwamba hulii au kuhuzunika kwa sababu matatizo ni makubwa, bali umekosa ufahamu wa maono.


Hebu chukua jukumu la kudharau shida zako kwa kujilinganisha na wengine ambao ambao wana matatizo makubwa kuliko yako. Fanya hivyo kila unapokabiliwa na tatizo, usilione tatizo ni kubwa kwa takwimu, lichukulie kuwa ni dogo kisha uanze kulishughulikia, utaona linamalizika kwa ushindi mkubwa. Kamwe usijaribu kulitatua kwa kulikuza sana, hutapata matokeo mazuri. Kuwa na mtizamo chanya kwenye tatizo lako, itakusaidia kukabiliana nalo vizuri.

Ya nini ulie na kuhuzunika kila siku? Ukiwa ni umasikini, kutokuzaa, kukosa kazi, kuteswa na mume na matatizo yote yatakayokukuta katika maisha yako yaone ni madogo kisha tumia nguvu zako zote kuyakabili nina hakika utayashinda kirahisi. Jaribu kupunguza matatizo, badala ya kuyakuza kwa kuona hayawezekani kutatuliwa, utaona majibu yake. Tambua kuwa tatizo lako si kubwa bali unalikuza katika mawazo yako, kwa kuwa wapo wenye matatizo makubwa zaidi yako na hawalii kama wewe.

Ili uweze kuwa mshindi na usihuzunike tena kumbuka hili siku zote ‘nyakati ngumu katika maisha hazitaisha, ni jukumu lako kukabiliana nazo tu.’ Jiulize tena mwenyewe, kama ni kulia utalia kwa mangapi? Dunia haina usawa, jifunze kuyakabili matatizo yako kwa mtazamo chanya hapo utakuwa mshindi. Acha kuwa na huzuni na simanzi kupitiliza linalokuhuzunisha siyo tatizo kubwa sana. Wapo watu ambao walishashavuka tatizo kama lako jifunze kwao, kisha songa mbele.

Nakutakia maisha mema yawe na amani na furaha, ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO endelea kujifunza na kuhamasika zaidi.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,

0713 048 0345/dirayamafanikio@gmail.com   



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.