google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 4, 2021

Mawazo Kumi (10) Yatakayokupa Nguvu Kubwa Yakufikia Mafanikio Yako.

No comments :
Mafanikio siku zote yanaanza na mawazo. Kama hakuna wazo sahihi ieleweke pia hakuna mafanikio sahihi ambayo yataweza kuchipua kwa nje, sana sana  utakuwa ni mtu wa kushindwa kila wakati. Kupitia makala haya utajifunza mawazo muhimu yatakusaidia kuweza kufikia mafanikio yako. Karibu na twende tujifunze;-
1. Usifanye maamuzi kwa muhemko kwani utaahirisha tu, ni wachache wanaofanikiwa na maamuzi ya muhemko. Kwa mfano, utakuta mtu kasikia habari kwamba biashara ya aina fulani inalipa, mtu huyo utakuta anakurupuka na kujikuta kwenye wakati mgumu sana wa kuweza kushindwa. Kabla hujafanya maamuzi, tafakari kwanza.
2. Usitake mafanikio kama unavyotaka wewe. Mafanikio yana njia yake na misingi yake pia. Kama unataka mafanikio kwa jinsi unavyotaka wewe na unategemea utayapata huo ni uongo hutaweza kuyapata. Futa njia, kanuni na miiko ya mafanikio inasema nini utafanikiwa. Ulikilazimisha kufanikiwa kama unavyotaka wewe, haitawezekana.
3. Usikae tu na kusubiri mambo yatokee, utajichelewesha sana. Amua kupambana kufanya mambo yaweze kutokea na hiyo itakusaidia sana kuweza kufanikiwa. Kuwa mtu wa kulazimisha matokeo uyatakayo na uyapate. Kusubiri subiri tu mambo yajiendee, utajikuta unasubiri sana na mambo hayawi kama utakavyo, komaa.

4. Kama unaona maisha yako ni magumu sana, rudi kwenye mawazo yako, rudi na uende ukaanze kufikiri upya tena, maana ugumu wa kila kitu unaanzia kwenye akili na si kwingine tena. Inawezekana maisha yako ni magumu kwa sababu umeshindwa kuifikirisha akili yako vya kutosha, fikiri hili na chukua hatua.                                                                               
5. Kuwa tayari kwa wakati ufaao na wakati usiofaa kwenye maisha. Kuna wakati maisha yanakutaka uwe tayari hata wakati wewe unajiona hauko tayari iwe hivyo. Unatakiwqa uwe kama mwanajeshi kwa kuamua kufanya chochote kile na wakayi wowote ule ilimradi tu kuyafanya maisha yako yasogee mbele  na kuleta mafanikio yatakiwayo.
6. Fanya ufanyalo kwenye maisha yako, lakini hakikisha uwe una kitu cha watu kujifunza kwako. Usiishie kujifunza kwa wengine ila hakikisha watu nao wajifunze kwako kupitia wewe kama wewe. Fanya vitu ambavyo watu watakuiga na wakuone kwamba wewe ni mfano wa kuigwa na wakufate nakufanya maisha yao kuwa bora.
7. Ukiwa unafanya kazi, hakikisha uwe una kitu cha kuuza yaani una bidhaa ambayo unaweza ukawauzia watu na wakanunua kwako. Fanya ufanyalo lakini hakikisha uwe na pesa ya ziada, pesa hiyo ya ziada au akiba itakusaidia. Anza kuuza kitu ambacho kitakusaidia sana kuweza kukuza uchumi wako nje ya kazi uifanyao.
8. Kila mtu anaweza akawa na wasiwasi na wewe, lakini ukijitoa na kuamua basi kila kitu kinawezekana kwako na utafanya maajabu makubwa kwako. Jiamini kwamba unaweza ukafanya mambo makubwa maishani mwako hata kama hakuna mtu anayekuamini. Jiamini wewe kama wewe na utatoboa na kufikia mafanikio makubwa.
9. Weka juhudi sana kwa kila unachokifanya pasipo kuyumbishwa na wakati unaweka juhudi ili uweze kwenda mbele zaidi kubali kujifunza kwa kukosolewa. Bila ya juhudi, kukubali kukosolewa au kuelekezwa kwa usivyojua, hauwezi kwenda. Kukosolewa si dhambi, wewe kosolewa na kubali kujifunza na utafanikiwa pa kubwa.
10. Kila jambo lifanye kwa wakati wake. Kama kwako upo kwenye muda wa kuwekeza, nikwambie tu wekeza sana na mtu asikutanie katika hilo. Usipoteze muda mwingi sana kwa kuwaza kwamba muda upo pale pale au unakusubiri, utapotea. Utumie muda wako kufanya yale yaliyo ya msingi na yale ambayo yatakusaidia kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.