Sep 18, 2018
Faida Ya Kutoa Yale Mazuri Kwa wengine Ni haya.
Siku zote katika maisha yako kabla hujatenda kitu
chochote, kabla hujasema kitu chochote, jiulize kitu unachotaka kutenda au kitu
unachotaka kusema je, kitaleta matokeo chanya kwako au hata kwa wengine?
Sio kwa sababu unayo nafasi nzuri ya kutenda au kusema
hiyo ikawa na maana kwako ufanye au useme tu hata mambo yanayoumiza wengine.
Unatakiwa kuwa makini na kuzingatia ni nini matokea ya kile ambacho unakwenda
kutenda au kukizungumza. Kwani kila wakati tunakumbushwa ya kwamba ni heri
kufikiri kabla ya kutenda.
Nisisitiza
suala la kufikiri kabla ya kutenda kwa sababu wengi wetu hukurupuka katika
kutenda mambo fulani, na kufanya hivyo kumekuwa chanzo cha kutotimiza jambo
hilo. Hivyo kwa jambo lolote kabla ya kulitenda au kulisema ni heri kulitakari
mara dufu zaidi.
Pia kufikiri kabla ya kutenda ni muhimu kwa sababu ni
dhahiri wapo watu ambao moja kwa moja utawaumiza, kama utatenda au kusema
maneno hasi, hata kama hujui jinsi
unavyowaumiza. Pia uelewe wapo watu utakaowaponya kama utaamua kusema au
kutenda matendo chanya ambayo yana msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla.
Kila wakati, unayo nafasi nzuri sana ya kutoa mazuri
katika dunia, ingawa uamuzi ni wako. Acha kutenda au kusema mara moja kile
kinachokujia kichwani mwako, Jipe muda wa kukifikiri kitu hicho na kujua ni
nini matokeo yake katika maisha yako na ya wengine.
Kuanzia leo jifunze kutoa yale mazuri katika hii dunia
jenga utamaduni wa kutoa yale matendo au maneno mazuri iwe sehemu ya utamaduni
wako. Ukifanya hivyo dunia itakupa mazuri pia na utafurahia maisha yako kutokana na mazuri unayoyatoa.
Simama imara katika kuhakikisha unalitenda hili vyema kila wakati. Simamia
katika ukweli, ili kutengeneza amani ya moyo wako na mioyo ya watu wengine.
Usiwe kichocheo katika kusababisha watu wengine wakose furaha, bali jitahidi
kuwa katika kusimamia ukweli na haki daima. Kumbuka sana TOA YALE MAZURI
KATIKA MAISHA YAKO, GIVE GOODNESS TO
LIFE, ukifanikisha hili furaha na mafanikio vitakuwa upande wako.
Mwisho
tuweke nukta kwa kusema ya kwamba wewe ni matokeo ya mafanikio ya watu wengine
kama utaamua kuwa mkweli kwa kutakari kabla ya kusema na kutenda utafanya
vichocheo vya mafanikio kwa watu wengine.
Imeandaliwa
na mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani
Ngwangwalu & Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.