Sep 3, 2018
Mbinu Muhimu Itayokufanya Uondokane Na Msongo Wa Mawazo.
Msongo wa mawazo ni
ile hali ambayo humpata mtu kisha kumpelekea mtu huyo kuwa na mawazo mengi
kupita kiasi. Mawazo haya yanaweza kuwa chanzo chake mahusiano, kazi,elimu,
magonjwa, biashara, fedha na mengineyo mengi.
Pamoja
na kuweko kwa vyanzo hivyo au visababishi hivyo vya msongo wa mawazo inaelezwa
kuwa msongo wa mawazo mara nyingi husababishwa na mahusiano, usigune huo ndio
ukweli, pia leo sipo kwa ajili ya kuzungumzia msongo wa mawazo utakanao na
mahusiano bali nipo hapa kuzungumzia namna ambavyo utaweza kuondokana na msongo
wa mawazo.
Nataka
kuzungumzia namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kwani athari ya kuwa na
msongo wa mawazo ni kubwa mno. Tumekuwa tukiwaona watu wakishindwa kufanya kazi
wazifanyazo kwa ufanisi eti tu kwa sababu watu hao wana msongo wa mawazo.
Lakini
athari iliyo kubwa kupita zote wapo baadhi ya watu ambao huchukua hata maamuzi
ya kujaribu kujiua kwa sababu tu mawazo waliyonayo yamewazidi akilini
mwao. Lakini athari nyingine ya msongo wa mawazo ni kwamba ni chanzo cha
magonjwa mbalimbali.
Swali
ambao huwa najiuliza hivi ni kwa nini watu hao hufikia uamuzi huo wa kutaka
kujiua? Hivi ni kweli watu hao hawajui namna ya kuweza kuondokana na hali hiyo
ya msongo wa mawazo? . Kwa majibu yangu ya haraka haraka nikagundua yawezekana
ni kweli watu wengi hawajui namna ya kuondokana na msongo wa mawazo.
Kwa kuwa hawajui basi naomba niwape
mbinu hii maridhawa ambayo itawafanya watu hao waweze kujifunza hapa namna ya
kuondokana na msongo wa mawazo kama ifuatavyo:
· Unatakiwa kutafuta majibu ya changamoto iliyokufanya uwe
katika msongo wa mawazo.
Msongo
wa mawazo sababu yake kubwa hutokana na changamoto fulani iliyokukabili katika eneo lako fulani. Hivyo kila wakati
usiwe ni mtu wa kunung'unika, au kuamua kuchukua uamuzi fulani ambao ni mbaya
utakaokufanya kuyagharimu maisha yako kwa namna moja ama nyingine, bali jifunze
kutafuta majibu chanya yatakayokufanya uondokane katika hali hiyo ya msongo wa mawazo.
Kutafuta
majawabu ya changamoto zinazomkabili mtu, humsadia mtu huyo kwa namna moja ama
nyingine kutengeneza amani ya moyo, na mtu anapokuwa na amani ya moyo huwa ni
mtu chanya kwa kuwa mara nyingi hujiwekeza katika mawazo mazuri yatakayomsadia
kufanya mambo yenye tija na si vinginevyo.
Mwisho
naomba nitamatishe kwa kusema mara zote epuka msongo wa mawazo kwa kuzingatia
njia hii ambayo nimeieleza hapa kwani msongo wa mawazo huwa una athari kubwa
sana katika maisha ya kila siku kimwili na kifkra pia.
Kwa
leo naomba niishie hapa tukutane tena panapo majaliwa,
Ndimi: Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.