google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 1, 2018

Rafiki Sahihi wa Kukupa Mafanikio Ya Kweli Ni Huyu.

No comments :
Mara nyingi marafiki wanaokuzunguka  wanao mchango mkubwa sana wa kujenga au kubomoa kwa kile unachokifanya, hii inategemea na aina gani ya marafiki ulionao.
Pia marafiki hao ulionao wewe ndiye unayemua na  kuchagua ni yupi rafiki sahihi wa kushikirikiana, naye na yupi si wa kushirikiana naye? Nimesema hivyo kwa sababu wapo marafiki ambao wao kazi yao kukatisha tamaa wengine, lakini wapo wengine wao kazi kutoa ushauri maridhawa wakufanikiwa kwao  na hawa ndio wa kuwang`ang`ania.  
Hivyo mara nyingi katika maisha yako jifunze kuchagua marafiki sahihi wenye mchango sahihi katika mambo unayoyafanya. Na miongoni mwa rafiki muhimu unayepaswa kumng`ang`ania katika safari yako yote ya mafanikio hapa duniani ni yule rafiki ambaye mara nyingi anakueleza ukweli pasipo kukuonea aibu.

Rafiki huyu ndiye muhimu sana na kama unaye usimuache aende zake kwa sababu miongoni mwa tabia walionazo watu wa aina hii ni kwamba wao husema ukweli daima. Hata pale utakapokuwa umefanya jambo fulani ambalo wewe utaliona ni zuri, kwa kuwa yeye ni mkweli basi yeye hata ona haya kukosoa ili uweze kufanya vizuri zaidi na kwa ubora zaidi.
Mara nyingi wengi wetu tunakosa aina hii ya marafiki kwa sababu huwa tunahisi labda wanatuonea wivu kuendelea kusonga mbele kwa vitu ambavyo tunavifanya kumbe ukweli haupo hivyo, bali marafiki hawa kucheza sehemu kubwa ya maisha yetu kwa kuwa wao hutueleza ukweli ni jinsi gani tunakiwa kuishi na kufanya mambo yale ya msingi.
Lakini pia tunashauriwa ya kwamba kukaa na marafiki ambao wao kazi yao ni kusifia tu ya kile tukifacho, marafiki wa aina hii hawafai  kwa sababu hawana mchango wowote ule wa sisi kuendelea kusonga mbele bali kuturudisha nyuma hivyo hutuna budi kuwaepuka.
Marafiki wa aina hii huwa na  maneno  mafupi lakini yasiyoleta mabadiliko yeyote yale kwa kile ukifanyacho. Utawasikia wakisema aaah hongera sana, wengine utawasikia wakipaza sauti aaah ndugu yangu umepasua na maneno mengine kama hayo.
Maneno kama hayo siyo mabaya sana hasa pale yapenyezapo maskioni mwetu kwani hufariji sana mioyo yetu na kujihisi tupo sahihi kabisa .
Lakini mimi nafahamu hukuzaliwa kuja hapa duniani kufarijiwa moyo  na maneno ya watu pekee bali ulikuja hapa duniani kwa leo la kutimiza kusudio lako maaalum.
Hivyo ili uweze kutimiza kusudio hilo maalumu hauhitaji watu wenye kuufariji moyo wako tu pekee, bali unahitaji watu sahihi wenye kukufariji pamoja na kukupa ushauri wa kiutendaji kwa kile unachokifanya ili uweze kukufanya kwa ubora zaidi.
Lakini kabla sijaweka nukta kwa siku ya leo  nikuombe kitu kimoja kikubwa chukua walau dakika kadhaa kisha tafakari hivi katika maisha yako unazungukwa na marafiki  wangapi wasemao ukweli juu ya maisha yako ?
Mara baada ya kupata jawabu la swali hilo usiache kichwa chako kipoe bali zama tena katika dimbwi la fikra zako jiulize tena hivi kama hauna aina hii ya marafiki je, hatua gani utakazotumia kuwapata marafiki hawa?
Pia swali la mwisho je, na wale marafiki wasiokuwa na mchango wowote katika maisha yako je,  utawachukulia hatua gani?
Endapo Ukipata majawabu ya sahihi ya maswali hayo ni imani yangu kubwa utakuwa katika eneo sahihi ya kutengeneza njia ikupasayo kuyafikia mafaniko unayoyahitaji kwani utachagua ni mtu wa kuchagua marafiki sahihi kila nyakati.
Asante sana kwa kusoma makala haya, sina cha kukulipa zaidi ya kusema asante sana na nenda kayafanyie kazi yale yote niliyokueleza.
Ndimi: Benson Chonya

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.