google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 13, 2018

Nyuma Ya Pazia La Mafanikio.

No comments :
Mafanikio yoyote unayoyaona  kwa nje mara nyingi yanatengenezwa sana na hatua au vitu visivyoonekana, kile unachoona ni matokeo yake tu.
Kazi fulani inapokamilika na mafanikio yake kuonekana kwa nje, ni wazi dunia nzima inakuwa makini kushangaa kwa kuyaona mafanikio yale yaliyotokea.
Lakini kuna kuwa hakuna mtu ambaye anakuwa yupo tayari kufatilia mchakato wa nyuma ya pazia ni nini kilifanyika hadi kuibua mafanikio hayo.
Na kwa sababu hiyo ya kuangalia mafaniko au matokeo ya nje, yote hiyo hupelekea kuwaona watu wenye mafanikio ni kama watu wenye bahati sana.

Ikiwa utang’ang’ania kuangalia mafanikio ya nje ya watu na kuchanganyikiwa nayo na kusahau kwamba kuna nyuma ya pazia la mafanikio, umepotea.
Mchezaji wa mpira anaonekana anafanya vizuri uwanjani, ujue nyuma yake kuna mazoezi mengi sana ameyafanya tayari.
Mpiganaji bora wa ngumi duniani unayemwona anang’ara na kuchukua ushindi wa kila aina ujue kabisa huyo kafanya mazoezi mengi ya kutosha yaliyompa ushindi huo.
Biashara yoyote inayoonekana ina mafanikio makubwa haikuanzia pale, nyuma ya pazia la mafanikio, ilianzia mbali sana na pengine na mtaji mdogo na wa kawaida sana.
Hiyo yote inaonesha mafanikio yanajengwa na vitu vidogo sana, vitu ambavyo kuna wakati kama havionekani, lakini baadae huleta matokeo makubwa.
Utakata tamaa na kujiona mshindwaji kama utakuwa unaangalia mafaniko kwa kuona tu matokeo yaliyopo sasa na kusahau, kuna vitu vinatengenezwa nyuma ya pazia.
Ushindi na mafanikio hauendi kwa watu wenye bahati kama unavyofikiri wakati mwingine kwamba ndivyo ulivyo.
Ushindi na mafanikio unakwenda kwa kila mtu ambae ameamua kujenga nidhamu, kujituma, kuwa king’ang’anizi na kuwa chanya wakati wote.
Angalia nyuma ya pazia la watu wenye mafanikio, utajua na wewe ufanye nini, ujitume vipi na uweke juhudi gani zinazotakiwa.
Lakini ukiwa utakuwa unaangalia matokeo yao na kushindwa kuangalia nyuma ya pazia hutaweza kujifunza kitu cha kukusaidia.
Mafanikio yote makubwa yanatengenezwa nyuma ya pazia la mafanikio, huko ndiko mafanikio yanakopikwa na kuandaliwa haswaa, mengine unayoyaona ni matokeo.
Usiendelee kusubiri, tengeneza mafanikio yako nyuma ya pazia na hayo matokeo yatakuja kuonekana huko mbeleni, kama huoni matokeo kwa sasa usijali.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.