google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 12, 2018

Inawezekana Kubadili Maisha Yako Sana…Ukiamua Kufanya Hivi.

No comments :
Kila wakati unapofikiria na kikiwaza kile kitu unachokita ili kikutokee, uwe na uhakika na ujue kabisa kitu hicho kitawezekana na kutokea.
Kila wakati unapojenga mategemeo chanya kwa kile ukifanyacho, tambua pia mategemeao hayo yatawezekana na kuwa kweli katika uhalisia.
Kila wakati unapoweka juhudi na kujitoa kikamilifu kwa kile ukifanyacho, uwe na uhakika inawezekana kufikia lile lengo lako ambalo umejiwekea.
Kila wakati unapokuwa upo tayari kuendelea kuchukua hatua na hata kama mbele yako kuna changamoto kubwa sana za kimaisha, tambua inawezekana kufanikiwa.

Kila wakati unapoamua kuwa king’ang’anizi na hadi kuhakikisha ndoto zako zinatimia, pia unatakiwa kujua kwamba hilo linawezeka na ndoto zako zitatimia.
Kila wakati unapojifunza kutokana na makosa unayofanya na ukachukua hatua za kujirekebisha kwenye makosa yako utafika wakati itawezekana kufanikiwa kwako.
Kila wakati unapoamua kuendelea mbele hata kama umekatishwa tamaa, itafika wakati pia ujue kufanikiwa kwako ni lazima utafanikiwa kwa sababu umeamua.
Kila wakati unapoamua kupambana na hali hatarishi, hali za kuogopesha zinakufanya uone ndoto zako hazitimii, ujue muda utafika itawezekana kufanikiwa kwako.
Unapaswa ujue kila hali unayotegemea, kila juhudi na kila kujitoa ambako unafanya kila siku, huko ndiko kutakapokupa mafanikio makubwa maishani mwako.
Hakuna ambaye anategemea kile kilichobora na halafu mwisho wa siku akabaki kama jinsi alivyokuwa mwanzoni.
Kitu cha kuzingatia ni kuwa mvumilivu na kujua kwamba mabadiliko katika maisha hayaji mara moja tu au ghafla, mabadiliko yanakuja wakati mwingine kidogo kidogo.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.