google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 1, 2018

UJUMBE WA PASAKA; Tenda Wema Kwa Faida Hizi Kwako.

No comments :

Habari za muda mpenzi mzomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
Ikiwa leo ni tarehe 1/4/2018 ambapo wakristo wote duniani wanasherekea siku za kufufuka kwa bwana wetu Yesu Kristo yaani ni sikukuu ya pasaka.
Siku hii huenda sambamba na kipindi chenye tafakari kubwa yenye kuwataka wakristo wote duniani kote waweze kutafakari uwepo na uweza wa matendo makuu ya mwenyezi Mungu.

Kwa Misingi hiyo Uongozi mzima wa Mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO inapenda kukutakia sikukuu njema ya Pasaka, huku ujumbe wetu mkubwa kwako ikiwa ni  kwamba  hakikisha unaitumia siku hii katika kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kuhakikisha unakuwa ni mtu Mwema na si kutenda dhambi.
Tunasiitiza juu ya hilo kwa sababu watu wengi hutumia siku hii katika kufanya maovu ambayo ni chukizo mbele ya Mungu wetu, yamkini yawezekana vipo vishawishi mbalimbali ambavyo vitajitokeza katika siku ya leo, unachopaswa kukifanya ni kujitenga mbali na vitu hivyo. Hata maandiko yanasema ya kwamba jicho lako likikukosea ling'oe.

Hivyo katika siku hii epuka sana marafiki ambao watakusababisha uingie katika kutenda maovu, kwani maovu ni dhambi na pia ni chukizo mbele za mwenyezi Mungu.
Tukutakie sikukuu njema ya Pasaka.
Imeandaliwa na uongozi mzima wa Blog hii ya dira ya mafanikio na kuletwa kwako nami Afisa Mipango Benson Chonya.



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.