google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 6, 2018

Ifanye Hii… Iwe Sababu Ya Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Pale unapokuwa na kazi nyingi za kufanya na unaona kama hutaweza kukamilisha kazi hizo, hiyo sio sababu pekee ya kukufanya wewe ukate tamaa.
Pale unapoona njia ya kufikia mafanikio yako ni ndefu sana, na unaiona mafanikio yako kama yanachelewa vile, hiyo pia si sababu ya wewe kuweza kukata tamaa.
Kwa vyovyote vile unapoona ugumu wa kufanikiwa na kukatishwa tamaa na vitu kama hivyo, fanya sasa hiyo ndio iwe sababu ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Usitishwe na njia ya mafanikio yako ni ndefu au usitishwe kwa kuona kwamba una majukumu mengi, hapo ndipo unapotakiwa wewe kukaza mwendo kuelekea mafanikio yako.
Unapokuwa na vitu vingi zaid vya kufanya na vinakutaka wewe, hapo ndipo ipo fursa pia ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.

Unapoona njia ya mafanikio ni ndefu, hapo ndipo huo wakati wa wewe kuweza kutafuta njia nyingine za kuweza kukusaidia kukufanikisha.
Unapaswa kujua mafanikio makubwa yanakuja katikati ya changamoto nyingi zaidi, na changamoto hizo ndizo unazotakiwa kukabiliana nazo na kuzishinda.
Matajiri unaowaona, walifanikiwa katika njia hizi hizi ambazo hata wewe kuna wakati unaona kwa njia hii kufanikiwa ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa tena.
Unapokutana na magumu, unapokutana na hali ya kuona kama njia yako ya mafanikio ni ndefu sana na haiwezi kufika hiyo isiwe sababu ya kufanya ukashindwa.
Kila wakati jaribu kutafuta sababu ya kufanikiwa pale unapokutana na ugumu au kuna njia ya mafanikio ni ndefu kwako.
Unapaswa kujua hakuna maisha pasipo changamoto na changamoto zipo ili tuweze kuzishinda na kutupa sisi mafanikio.
Ndio maana kuanzia leo unatakiwa kujua kwa uwazi kabisa, fanya sababu yoyote ile inayokupa ugumu wa kuweza kufanikiwa kiwe ndio chanzo cha mafanikio yako.
Kikubwa unatakiwa uwe mvumilivu na usiwe mtu wa kuweza kukata tamaa mapema kwani hautaweza kufika mbali kama utakuwa ni mkata tamaa mapema.
Unapokutana na magumu na unapoona njia ya mafanikio ni ndefu kwako huo ndiio wakati wa kutafuta kwako kung’aa kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.