google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 18, 2018

Kama Utatumia Mambo Haya Hovyo, Utakwama Sana.

No comments :
Muda wako ulionao, nguvu zako ulizonazo na umakini wa mambo ulionao, ni moja ya mambo ambayo yana nguviu sana katika kubadili maisha yako au kuharibu maisha yako kwa namna ambayo hata wewe inaweza kukushangaza.
Jukumu lako kubwa ulilonalo, ni kufanya juu chini na kuyatumia mambo hayo kwa ukamilifu wake ili yakupe maisha unayoyahitaji, hapa nikiwa na maana maisha ya mafanikio. Kama ila utayatumia mambo hayo hovyo, hakuna ubishi utashindwa sana.
Pengine jiulize je, kuna kitu ambacho katika hali si ya kawaida kinakuingilia na kukupotezea muda wako, nguvu zako na umakini wako wa kuelekea kwenye ndoto zako? Kama kitu hiki kipo tafuta namna jinsi utakavyoweza kuachana nacho.
Kama utaendelea kung’ang’ana na kitu ambacho kinakupotezea muda, nguvu na umakini wako pasipo manufaa yoyote, nikwambie tu hapo unajitafutia balaa au njia ya kwenda kwenye shimo la kushindwa kwako vibaya kimaisha.

Tumia muda ulionao, nguvu ulizonazo na umakini wako kukusaidia kufanikiwa.
Waangalie watu wote wanaoshindwa kwa kitu chochote. Watu hao wanaoshindwa wanasifa moja kubwa sana ambayo ni kufanya mambo ambayo yanapoteza muda wao, nguvu zao na umakini wao katika kuelekea mafanikio wayatakayo.
Haya ni mambo yanaonekana kwa juu juu hayana athari kubwa katika maisha yako, lakini kiuhalisia mambo haya ndio yanaua ndoto za watu wengi na kujikuta ni kilio cha kuishi maisha yasiyo ya mafanikio sana karibu wakati wote.
Ukitaka kubadili hali hii na iwe ya manufaa kwako, kuanzia leo anza kutumia muda wako, nguvu zako  na umakini wako wote katika mambo ambayo unaamini yatakusaidia wewe kukubadilisha na kukupeleka sehemu nyingine ya mafanikio.
Ikiwa unachukua hatua, hakikisha unachuka hatua ambazo hazikupozei muda wako, nguvu zako na umakini ulionao katika kuelekea mafanikio yako. Ikitokea unachukua hatua ambazo zinakupotezea mambo hayo, basi kushindwa kunakuhusu sana wewe.
Ikiwa pia unawaza, una panga mikakati yako, hakikisha sana,  kuwaza kwako kusiwe unawaza tu kwa sababu wewe ni binadamu. Jitahidi kuwaza  kule ambako kunakuletea manufaa na si kukupotezea muda wako, nguvu zako na umakini.
Kitu ninachotaka unielewe hapa kwa umakini ni kwamba muda ulionao, nguvu ulizonazo na umakini ulionao, ndivyo vitu ambavyo vitakutambulisha wewe kama unafanikiwa au unashindwa na hiyo yote inatokana na jinsi unavyovitumia vitu hivyo.
Kila wakati, tumia vitu hivi viwe daraja la kukusaidia kufanikiwa kwako na si kukuangusha. Kama nilivyosema mwanzoni, kama utatumia vitu hivi hovyo kwenye maisha yako ya sasa, basi andika utashindwa sana na hautafanikiwa kwa sehemu kubwa maishani mwako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.