google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 16, 2018

Maisha Yatakuwa Bora Na Mazuri Sana Kwako Kama Utafanya Mambo Haya…

No comments :
Maisha yatakuwa mazuri kwako, kama utajiruhusu kuishi maisha mazuri kwa kufanya yale yaliyo ya msingi na yanayoweza kujenga maisha yako yakawa mazuri.
Maisha yatakuwa mazuri kwako, kama nguvu zako nyingi za uzingativu unaziweka kwenye mambo chanya na ambayo yanaleta mabadiliko kwako na kwa wengine.
Maisha yatakuwa mazuri kwako kama unaweka nguvu zako za uzingativu pia katika kutoa matokeo chanya, ambayo yanakubadilisha wewe na yanawabadiisha watu wengine pia.
Maisha yatakuwa mazuri kwako kama utaondoa mitazamo yako potofu uliyonayo, pamoja na kinyongo kwa wengine na kuanza kuuona usawa kwa wote.
Maisha yatakuwa mazuri kwako, kwa sababu, leo hii unayo tena nafasi na fursa ya kuishi na kufanya chochote ukitakacho pasipo kuzuiliwa na kitu cha aina yoyote.

Maisha yatakuwa mazuri kwako, kwa kuona mazuri kwa wengine na kubali kujifunza kutokana na mazuri hayo na si kubaki wewe kama wewe.
Maisha yatakuwa mazuri kwako, ikiwa utakubali kujifunza kutokana na makosa na kukubali kujirekebisha na kisha kusonga mbele kwa mafanikio.
Maisha yatakuwa mazuri kwako, kwa wewe kukubali kuwasaidia watu wengine kuweza kufikia ndoto zao na kwa kufanikiwa kwao na wewe utajikuta ukipiga hatua.
Maisha yatakuwa mazuri kwako na ya Baraka, kama utaamua kuwa mtu wa shukrani na sio mtu wa kunung’unika kila wakati kama ilivyo mazoea ya wengi.
Ruhusu siku ya leo iwe maalumu kwa ajili ya kutengeneza maisha yako ya kesho na yakawa bora na ya mafanikio makubwa.
Hata siku moja usikubali kubaki hapo ulivyo kwa kuwa king’ang’anizi kwa mambo yanayoharibu maisha yako ya leo na kesho.
Nguvu ya kuumba maisha yako na kuwa bora unayo. Kikubwa kwako ni kuweka juhudi na kujiruhusu ili uwe na maisha ya namna hiyo kwako.
Ikiwa utajiruhusu kufanya maisha yako yawe bora na huku ukichukua hatua, ndivyo itakavyokuwa na maisha yako yatakuwa bora vivyo hivyo siku zote.
Boresha maisha yako, kwa kuruhusu yale yaliyo mema yatokee kwako, na amini hilo unaweza na hakuna shaka, anza sasa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia  wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.