google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 22, 2018

Mawazo Yakinifu Ya Mafanikio Endelevu Kwako.

No comments :
Mafanikio yoyote yanaanza na mawazo. Hakuna mafanikio yanazaliwa nje ya mawazo. Kwa jinsi unavyokuwa na mawazo bora ndivyo unavyozidi kuwa na mafanikio bora kwako. Mawazo bora unayapata vipi, unayapata kwa kujifunza.
Kupitia makala haya, nakukaribisha tujifunze pamoja mawazo yakinifu ya mafanikio yako endelevu. Naamini kupitia mawazo haya, utajifunza kitu ambacho kitakutoa hatua moja na kwenda hatua nyingine, karibu tujifunze.
1.Unaweza ukaendelea kuteseka kila siku na maisha na kuteseka kila na kila aina ya ugonjwa, lakini hiyo yote inaweza ikasababishwa na ujinga ambao  umeushikilia. Ujinga ni adui mkubwa sana wa mafanikio yako.
Fanya ufanyalo, futilia mbali ujinga wote ambao upo kwako. Ukifuta ujinga utakuweka huru na utaishi maisha ya mafanikio. Wajinga ndio waliwao na ujinga haumfanikishi mtu, tadhari usiwe kichaka cha ujinga, UTAKWAMA.
2. Kwa mawazo uliyonayo ujue kabisa yanatengeza dunia yako, yanatengeneza maisha yako au yanaumba maisha yako. Swala la kuwa makini sana kwako ni nini ambacho unakiwaza kila wakati.
Kama unawaza upuuzi mwingi, ujue kabisa ndio maisha yako unayabomoa na kuyaharibu kabisa. Kuwa makini na kile ukiwazacho maana hicho kitaleta matokeo ya maisha yako hata kama matokeo hayo huyapendi.
3. Kama unaona matokeo ya nje yanaathiri maisha yako kwa namna moja au nyingine, basi huhitaji sana kulalamikia matokeo hayo ya nje, bali unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi za kutawala mawazo yako.
Msingi wa maisha yako unaanza na mawazo yako, ukianza kutawaka mawazo yako kwa uhakika na vitu vingine vya nje utavitawala kwa uhakika. Anza kutawala mawazo yako kikamilifu ili ufanikiwe.

4. Kila kitu kinaanzia kwenye mawazo, uzuri au ubaya wa kitu unaanzia kwenye mawazo yako. Kama unaona kitu fulani ni kibaya kwako, kuna mwingine anaonaona kitu hicho ni kizuri kabisa.
Akili yako inaona kutokana na wewe jinsi unavyoamua akili hiyo iweze kuona. Kama unaiona bahari ni sehemu mbaya, wengine wanaona bahari sehemu nzuri ya kuvua samaki, ni suala  la mtazamo wako tu.
5. Furaha ni kitu ambacho unakipata kwanza ndani yako. Furaha kwa lugha nyingine ni uchaguzi ambao wewe unaamua kwamba sasa nataka kuwa na furaha ya namna hii. Furaha si kitu ambacho kinatoka nje yako. Furaha ni wewe unayoiumba ndani yako.
Kama unasubiri hadi ukamilishe mambo fulani hivi, halafu ndio uwe na furaha,  hapo utakuwa ni sawa na kujidanganya. Kwa nini ninasema hivyo ni kwa sababu, furaha ni kitu ambacho ni matokeo ya wewe na si nje yako, fikiri hili na tengeneza furaha yako.
6. Pamoja na kwamba maisha  yanaonekana ni magumu, lakini kipo kitu ambacho unaweza  ukafanya na kitu hicho kikabadili maisha yako na kuwa bora kabisa. Acha kuendelea kukazana kusema maisha ni magumu, fanya kitu.
Kuendelea kukaa tu na kujiimbia wimbo wa maisha ni magumu, hiyo haitakusaidia sana. Amka kutoka kwenye usingizi, amua kuchukua hatua kwa kufanya kitu ambacho kitakutoa kwenye ugumu wa maisha uliopo.
7. Mara nyingi mafanikio makubwa yoyote yale yanakuja kutokana na kufanya mambo ambayo watu wengi hawawezi kufanya. Kama jambo unalolifanya kila mtu analifanya, kufanikiwa kwake inakuwa ni ngumu kwa sababu ya ushindani wake unakuwa mkubwa pia.
Kuwa mtu ambaye unathubutu, kuwa mtu ambaye utajitoa mhanga kufanikisha jambo lile ambalo kila mtu anasema hawezi. Huhitaji maarifa ya ziada au kitu kingine tofauti, ni wewe tu kuamua kujitoa na kusema moyoni mwako kwamba nafanya na naweza pia, DO WHAT CAN’T BE DONE.
8.. Mara nyingi mategemeo bora ya maisha yako ya kesho yanatokana na uzoefu ulionao. Kama kwa siku za hivi karibuni umekuwa na uzoefu mbaya wa kupitia katika hali ngumu ni wazi na lazima utategemea mabaya tu katika maisha yako. Ikiwa lakini umekuwa ukipitia mambo chanya , mategemeo yako yatakuwa pia yapo vizuri.
Dawa pekee itakayoweza kukusaidia wewe uwe na mategemeo mazuri ni kuamua kujilisha dozi kubwa sana ya mambo chanya kwenye maisha kila siku. Kwa kadri unavyozidi kuwa chanya ndivyo mategemeo yako yanazidi kuwa bora. Hakuna mtu ambaye anaweza kuwa na mategemeo bora kama hayuko chanya.
Fanyia kazi mawazo haya yakinifu na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.