google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 20, 2021

Chukua Hatua Hizi, Utafanikiwa.

No comments :

Kwa kadri unavyochukua hatua chanya kuelekea kwenye ndoto zako, hapo unakuwa unapiga HATUA. Hata kama kuna kuna wakati unaonekana unarudi nyuma, unakata tamaa au una msongo wa mawazo na unaona mambo hayaendi, lakini kwa kuwa unachukua hatua chanya, weka akilini unapiga HATUA.

Kadri unavyochukua hatua chanya, utajua mafanikio unayoyataka ni mchakato wala si tukio la mara moja. Kuna mambo mengi ya kujifunza kabla hujafikia mafanikio yako, kama vile kujua kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi kazi. Unatakiwa kujua vizuizi si kitu ni muhimu kukupa fundisho la mafanikio.

Chukua Hatua Za Kuelekea Ndoto Yako

Kitu cha kuzingatia, endelea kuchukua hatua za kuelekea ndoto yako. Endelea tu kuweka juhudi na kupiga kazi, utakaribia mafanikio yako. Hata kama unapata matokeo hovyo kwa sasa, lakini kwa kila juhudi unayoiweka inakusaidia kupiga HATUA. Ni nini au kipi unasubiria, chukua hatua, UTAFANIKIWA.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki © 2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.