google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 25, 2021

Ukijiambia Hivi, Kila Kitu Utaweza.

No comments :

Inawezekana umejiambia huwezi kufanya biashara, huwezi kuongea mbele za watu, huwezi kuchora au hata umejiambia huwezi kutoka hapo ulipo kimafanikio na umeamua kubaki katika eneo ulilo zoea kimaisha.

Kama umejiambia hivyo mara nyingi, nataka nikwambie hiyo sio sababu ya wewe kubaki hapo. Unaweza ukaweza hicho unachojiambia kila wakati huwezi, na ukapiga hatua kubwa za mafanikio yako uyatakayo.

Nini unachojiambia huwezi leo, kitu hicho unaweza ukakiweza ikiwa utaamua. Hamna haja ya kubaki pale pale ulipo na kujiambia ooh huwezi huwezi, unaweza kufanikiwa na kuweza hicho unachosema huwezi.

Amua kutoka kwenye hali ya mazoea yako ya kila siku, na utaweza hicho unachosema kila wakati kwamba huwezi. Kwa nini usiweze, inawezekana ukaweza, jambo la kuzingatia jiambie "naweza" na utaweza kweli.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.