google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 23, 2021

Umechagua Kuwa Mshindi Au Mshindwaji Katika Maisha Yako?

No comments :

Washindwaji katika maisha husema, "niko bize sana sina muda". Washindi katika maisha wao wanasema " nitatafuta muda na nitaweza kufanya".

Washindwaji kila wakati wao wanatafuta visingizio vya kufanya jambo. Washindi katika mafanikio wao hutafuta njia ya kufikia mafanikio yao makubwa.

Washindwaji katika maisha hulalamika sana juu ya maisha yao jinsi yalivyo, washindi katika maisha wao huchukua hatua na kuamua kuwajibika.

Washindwaji katika maisha hulaani kwa ajili mambo au matukio waliyokutana nayo jana, washindi wao huandaa kesho yao kwa ubora zaidi. 

Washindwaji hutafuta majibu mepesi sana ya maisha yao, wakati washindi wao hutumia muda wa kutosha kutafuta majibu na suluhu ya maisha yao.

Washindwaji katika maisha hawataki kubeba jukumu lote la maisha yao, wakati washindi wao wanaamua kubeba jukumu lote la maisha yao, upo?

Kwa kila siku unayoipata, una nafasi ya kukaa upande wa washindi au washindwaji. Uamuzi unabaki ni kwako, unataka uwe upande upi wewe, basi.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki © 2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.