google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 31, 2018

Fursa Na Mipango Peke Yake Sio ‘Tiketi’ Ya Kukupa Mafanikio.

No comments :
Kuna watu wanaofikiria, kwa kuwa wana mipango mizuri na kwa kuwa wana fursa nzuri basi hapo mafanikio ndio tayari. Kama una ndoto za namna hiyo hata wewe, nikwambie unajidanganya na bado haitoshi hiyo, ila unahitaji kitu cha ziada ili kufanikiwa.
Najua unao uwezo wa kufanya kile unachokitaka, lakini uwezo huo bado hautoshi. Najua unayo fursa ya kuweza kufanikiwa lakini fursa hiyo bado pia haitoshi. Pia najua unayo mipango mizuri sana  ya kukusaidia kufanikiwa, lakini mipango hio pia haitoshi.
Ni nini kinachotosha au nini sasa unachotakiwa kufanya ikiwa unayo mipango, uwezo na fursa lakini tu haitoshi? Kinachotosha kwako ni wewe kuamua kuchukua hatua. Hata kama una kila kitu kizuri cha kukufanikisha sana kama huchukui hatua ni sawa na bure.
Hatua zinatakiwa ili uwezo ulionao ufanye kazi vizuri. Hatua zinatakiwa ili uweze kutumia fursa zako vizuri na pia hatua zinatakiwa ili uweze kufanya mipango yako vizuri. Kujidanganya kwako wewe una mipango halafu huchukui hatua ni kazi bure.

Hatua ndogo ambazo utakazoamua kuchukua ni za maana kwako sana kuliko mipango mikubwa uliyonayo ambayo huifanyii kazi. Kipi ambacho unasubiri, unatakiwa kuanza kuchukua hatua sasa za kukupeleka kwenye ndoto zako hata kama ni kidogo sana.
Leo ni siku ambayo unaweza ukaamua kutumia kila aina ya fursa iliyopo mbele yako kubadili maisha yako. Leo ni siku ambayo unaweza ukaitumia mipango yako na uwezo wako wote kukusaidia kufanikiwa.
Chochote ulichonacho hakina maana, chochote ulichonacho hakiwezi kutosha kama hutaweza kuchukua hatua. Kitu cha msingi kabisa ni kuchukua hatua za kubadilisha ndoto zako. Hatua ndizo zitakazokupa kile ukitakacho.
Lakini kitendo cha kuringa au kujidai eti kwa sababu wewe una mipango mizuri na ukaishia kwenye mipango hiyo, nakwambia hiyo itakupelekea kwako itakuwa ni ngumu sana kuweza kuchukua hatua za kimafanikio.
Washindi katika mafanikio wanajua vizuri mafanikio makubwa yanakuja kwa wewe kuchukua hatua. Hizo zote zingine zinaweza zikawa ni kelele, lakini kufanikiwa kwako kunatengenzwa sana na wewe kuweza kuchukua hatua.
Huhitaji kuendelea kuwa na matamanio ya ndoto zako wakati wote, unachotakiwa kukifanya sasa ni kubadili matamanio hayo na kuwa ya kweli. Hiyo ukumbuke lakini haiwezi kutokea mpaka uchukue hatua.
Yajaze maisha yako hatua na itafika mahali utaona matunda ya kile unachokifanya, hata kama kitu hicho ni kidogo sana. Hakuna kinachoshindikana kwenye kuchukua hatua. Mafaniko na mabadiliko katika maisha ni lazima yaonekane.
Hatua ndio kitu cha kitakachokufanya ufanikiwe. Kuwa na wazo, mipango na fursa hiyo haitoshi kwamba ndio ‘tiketi’ ya mafanikio. Unatakiwa kuchukua hatua, unatakiwa kufanya kazi ili uweze kufanikiwa, lakini sio kusema umefanikiwa na kumbe bado.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.