google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 24, 2018

Kama Unapata Pesa Halafu Zinapotea Kwa Haraka Sana, Soma Hapa.

No comments :
Najua unawajua wale watu ambao wanaweka sana juhudi katika kile wakifanyacho, kama ni pesa wanapata kweli, lakini pamoja na kupata pesa hizo baada ya muda zile pesa na  mafanikio yao  halisi yanakuwa tena hayaonekani.
Hapa ndipo wengi huanza kuwaza na kutafuta ni mchawi yupi aliyewaloga. Watu hawa wanakuwa hawaamini kama kweli wanaweza wakapata pesa halafu  mafanikio hakuna. Kinakuwa ni kitu kigumu kutokuamini zile pesa zimekwenda wapi walizozipata.
Pamoja na hayo, kwa kawaida kunakuwa ipo sababu inayopelekea hali hii kutokea sana. Ikumbukwe hali  hiyo inakuwa inatokea si kwa bahati mbaya au si kwa sababu una mkosi wa aina fulani bali inatokea kwa sababu.
Sababu hii ni kwamba watu hawa wanakuwa hawana mafanikio ndani yao, basi. Ipo hivi, huwezi kufanikiwa kama ndani yako hujafanikiwa bado. Utaweka juhudi sana na kufanikiwa kwa muda, lakini utaanguka tena kwa sababu ndani hujafanikiwa.

Siri ya kuweza kuweka mafanikio ya kudumu kwenye maisha yako ni kwa wewe kuumba mafanikio ya kutosha ndani yako. Ukiona hujaweka mafanikio ya kutosha ndani yako kufanikiwa kwa nje ni ngumu pia kwako.
Ndio maana, kabla hujaanza kulaumu kwa nje kwa nini huna mafanikio, jiulize na kujitazama mwenyewe kwa ndani yako upya, je, yale mafanikio unayoyataka unayo na unayaona ndani yako jinsi yalivyoumbika.
Kama ndani yako huoni kitu halisia yaani kile unachokitaka na una malengo ya jumla, kufanikiwa kwa nje na ukaweza kudumisha mafanikio hayo inakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kutokea na ndio maana unatakiwa kulifahamu hili vyema.
Kwa kifupi, unatakiwa uwe na picha kamili ya kile unachokitaka ili ufanikiwe, na kama hauna picha hiyo wewe sahau kupata mafanikio hayo hata kama ukipata pesa nyinggi leo uwe na uhakika haziwezi kudumu sana, utazipoteza.
Elewa, kama unataka kujenga mafanikio ya nje ya kudumu, anza kufanikiwa ndani yako kwanza na huku nje utafanikiwa tu. Ukumbuke mafanikio yako ya nje yanategemea sana ndani yako umefanikiwa kwa kiasi gani, hakuna uchawi katika hili, tafakari.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia  wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.