google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 15, 2022

Usitishwe Na Watu Wa Aina Hii...

No comments :

Katika maisha yako unatakiwa usitishwe na watu wa aina mbili, wakosoaji na watu wasio na shukrani. Hawa watu inatakiwa wasikutishe kwa lolote lile, maana ni watu ambao wapo na hawawezi kuisha. 

Wewe jiruhusu kufanya mambo yako kama kuna ambao watakukosoa acha wakukosoe kwa jinsi wanavyotaka, kama kuna utakaowasaidia kisha wakashindwa kuwa na shukrani achana nao pia.

Inatakiwa ujue wakosoaji na watu wasio shukrani ndio watu pekee wanaweza wakakufanya uhisi huwezi kufanikiwa tena. Lakini elewa, hakuna mtu atakayekufanya ujihisi wa kawaida au kuacha ndoto zako bila ya ruhusa yako. 

Watu wanaweza kusema sana kuwa huwezi hicho unachokifanya, lakini hiyo sio sababu ya wewe kujiona hutaweza. Mpaka ifike mahali ya kuwa huwezi inakutaka wewe ujiruhusu kuwa kweli sasa huwezi.

Unaweza kukosolewa sana, lakini hicho kisikutishe. Kama kile unachokifanya kipo kwa ajili ya kusudi la Mungu, acha wanaoendelea kusema waseme mpaka kesho, ila utafanikiwa. 

Acha kuweka nguvu zako kwenye kukosolewa, zingatia kile unachofanya. Wakosoaji juu ya maisha yako hawawezi kuisha, ni wapo tu, leo watasema hiki na kesho watasema kile.

Si wakosoaji tu pia unaweza ukawa na watu wasio na shukrani lakini usipigwe na mshangao hata wakati wa Yesu katika wale wakoma kumi walioponywa ni mkoma mmoja aliyerudi na kushukuru.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Endelea kujifunza kupitia MafanikioApp na dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya mafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2022 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rukhsa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.