google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 1, 2018

Kama Unataka Kufanya Jambo Lolote Ili Ufanye Kwa Urahisi Na Mafanikio, Tumia Kanuni Hii.

No comments :
Katika ulimwengu wa mafanikio, zipo kanuni nyingi sana ambazo kama ukizitumia zinatenda kazi na zinakupa matokeo makubwa sana kwako. Moja ya kanuni ambayo kama ukiitumia inaleta matokeo makubwa ya kimafanikio ni kanuni ya kutenda kwa kidogo. Hii ni kanuni ambayo  ina matokeo makubwa sana kwako kama ukiielewa.

Kanuni hii inasema, kabla hujaamua kufanya kitu chochote, jiulize unawezaje kufanya kitu hicho kwa kutumia nguvu kidogo. Kila wakati epuka kufanya mambo yako kwa kutumia nguvu nyingi sana. Kwa mujibu wa kanuni hii, unatakiwa kujifunza namna ya kutumia nguvu kidogo tu ili uweze kufanikiwa.

Naomba usinielewe vibaya, hapa sizungumzii swala la wewe kuwa mvivu bali kutumia nguvu kidogo ila unafanya mambo makubwa. Tambua ipo namna ya wewe kutenda mambo makubwa tu kwa kutumia nguvu kidogo. Naona hapa unaanza kunishangaa na kujiuliza hili linawezekana, kivipi? Usipate tabu juu hilo ila naomba nikupe mifano.


Inachukua nguvu kidogo sana kuweka akiba ambayo itakusaidia kuliko kujikalia tu huku ukiwa huna akiba yoyote.Kama unaweka pesa kidogo kidogo ni rahisi kukuza pesa zako hata kama ni kwa kidogo kuliko kizisubiri zikawa nyingi kwa pamoja.

Inachukua nguvu kidogo sana kutatua tatizo mapema kuliko ukaaliacha tatizo na likawa kubwa, hilo litakushinda. Watu wengi wanajikuta wanashindwa kwa sababu ya kutumia nguvu zao nyingi kutatua tatizo badala wangetumiaz nguvu hizo kulizuia.

Inachukua nguvu kidogo sana kula kwa afya kuliko ukajilia kila aina ya chakula na mwisho wa siku ukaanza kujitibu kwa shida. Ukiangalia kula kwa faya hakutakugharimu kitu, lakini kutibu tatizo la kiafya itakusumbua sana hiyo kwako.

Inachukua nguvu kidogo sana kufanya sasa, kuliko ukaairisha jambo hilo na kusema utalifanya kesho. Nguvu itakayoitumia kesho itakuwa kubwa sana. Hapa unatakiwa kujua kuahirisha airisha kila wakati, kutakufanya wakati siku unaanza utumie nguvu nyingi sana.

Inachukua nguvu kidogo kubadili ‘oil’ ya gari lako mara kwa mara, kuliko nguvu kubwa utakayotumia kubadilisha injini ya gari zima. Uzembe mdogo wa kushindwa kubadilisha mafuta ya kwenye gari yako inaweza ikapelekea wewe ukaua injini kabisa.

Inatumia nguvu kidogo sana kuanza kujenga nyumba yako kama utaanza kidogo kidogo, kuliko ambavyo ungekaa na kusema ningeanza mwakani au siku  nyingine. Kuanza kwa kidogo ujenzi wako itakuwa ni bora sana kwako.

Hivi ndivyo unavyoweza kutumia nguvu kidogo kufanya mambo yako makubwa au tunasema jinsi unavyoweza kufanya mambo makubwa kwa kutumia kanuni ya LESS IS MORE. Kanuni hii ni muhimu sana kukupa mafanikio.

Kwa chochote kile unachotaka kukifanya tafuta namna ya kukifanya kitu hicho kwa kutumia nguvu kidogo sana na ambazo hazitakusumbua. Fanya hivi kila siku na kila wakati na utafika mbali.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.