google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 28, 2018

Usiruhusu Sauti Hii Ikakufanya Ukashindwa Kufanikiwa.

No comments :
Ni rahisi sana kwenye maisha yako kusikia hasa pale tunapofatilia ndoto zako mtu akakwambia kwa uwazi kabisa kwamba ndoto na mipango yako hiyo huwezi kutimiza labda tafuta kitu kingine cha kufanya.
Wengi tumesikia sauti hizi sana na tumekuwa makini nazo na hata kulaani wale wte waliotuambia kwamba hatuwezi kufanya hivyo. Lakini je, ukijiuliza hizo ndizo sauti unazotakiwa kuwa makini nazo sana tu peke yake.
Ni kweli sauti hizo zina madhara kwetu, ingawa mbali na sauti za nje ambazo zinakwambia huwezi hili au lile lakini kiukweli ndani yako unayo sauti ambayo mara nyingi ni chanzo kikubwa cha wewe kushindwa kwa chochote kile.
Sina shaka yoyote na wewe, najua umeshawahi kujiambia kwa kujiamini kwamba naweza kufanya jambo hili na nitalifanikisha, wengi hujiambia sana hivi hasa linapokuja swala la kuelekea kwenye kutimiza ndoto zao muhimu.

Hata hivyo pamoja na kujiambia hivi huku wakiwa na uhakika kwamba watakwenda kufanya vile walivyojiambia na kwamba inawezekana, lakini ndani mwao utashangaa inajitokeza sauti inayokwambia huwezi.
Sauti hii karibu kila mtu inampata. Sauti hii kwa wengi imewaambia sana hawawezi hata kwa yale mambo ambayo walikuwa wanaweza. Inatokea sana hata kama umejiaminisha unaweza, lakini sauti hiyo inakusisitizia huwezi.
Kikawaida sauti hii mara nyingi ipo sana ndani mwako. Unachotakiwa kufanya ili kuishinda sauti hii ni kujiambia naweza nyingi sana hadi uweze kufanikiwa. Lakini ikiwa utairuhusu sauti hii uwe na uhakika itakukwamisha na hutaweza kufika popote.
Sauti hii wewe unayo na mwingine yoyote anayo ila kikubwa unachotakiwa kufanya ni kujenga ule uwezo wa kupambana nayo hadi uishinde. Hebu angalia ndoto zako umekuwa unazo nzuri kweli, lakini ukitaka kufanya kuna kitu kinakwambia huwezi.
Naamini umeshawahi kukutana na kitu kama hiki sana na umekuwa hujui uchukue hatua gani. Kwa vyovyote vile sauti hiyo inapotokea kwako ni lazima ujifunze kusema naweza hata kama inakwambia huwezi vipi.
Ikiwa hautaweza kuushinda sauti hii ni kweli usishangae hata yale malengo yako ambayo ulikuwa ukiaamini kabisa kwamba utaweza kutimiza unaona nayo hayatimii kwa sababu ya kuambiwa huwezi.
Kwa jinsi unavyoisikia sauti hiyo ndani inayokwambia huwezi, inatakiwa uwe mwepesi sana kusema naweza. Usije ukaambiwa huwezi na sauti inayotoka ndani mwako  halafu ukabaki kimya, hapo ndipo utakuwa unajipoteza.
Unatakiwa kujenga maisha yako kwa kujimini sana kwa kijiambia unaweza mara nyingi uwezavyo. Lakini usiishie kusema unaweza tu kwa mdomo huku hakikisha uwe unachukua hatua pia.
Kwa kuchukua hatua huku ukisema unaweza hakika amini utaweza kutimiza ile mipango uliojiwekea. Badilisha mwelekeo wa maisha yako kwa kuiushinda sauti inayokuja ndani yako ya kusema siwezi na kuwa naweza, hapo utafanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.